AIDS

 _____________________

UKIMWI
AIDS

_____________________

UKIMWI

MAJIBU YA BIBLIA KWA MASWALI YA LEO

Upungufu wa kinga ya mwili (UKIMWI) yameitwa ni maradhi yenye tatizo kubwa zaidi kiafya katika jamii kwenye karne hii. Huu unaweza kuwa ni mtazamo usioweza kubadilika. UKIMWI unaweza ukawa ni moja wapo kati ya maradhi yenye kuambukiza
sana katika historia ya mwanadamu. Lakini kitu cha kushangaza zaidi kuhusu UKIMWI ni kwamba hauenezwi kwa njia ambazo magonja mengine mabaya huenezwa. Kwa mfano, ndui na mafua makali haya huenezwa kutoka kwa aliye na ugonjwa, kwa kuwa na uhusiano wa karibu moja kwa moja na asiye na ugonjwa, kipindupindu huenezwa na chakula au maji yenye vidudu vya kipindupindu, tauni huenezwa kwa njia ya viroboro vya panya na hewa; homa ya malaria, taifodi (homa ya matumbo) na homa ya manjano huenezwa na wadudu wafyonzao damu. Bali ukimwi ni tofauti. Huu ni ugonjwa unaoenea haraka sana duniani hasa kwa njia ya zinaa. Ukimwi ulifahamika kwa mara ya kwanza Marekani mwaka 1981. Kufikia tarehe 30 Septemba 1987, nchi 124 zilitoa taarifa za ugonjwa kwa shirika la Afya duniani. Miongoni mwa wagonjwa 60, 653, wagonjwa 41, 825 walikuwa ni wagonjwa wa kutoka Marekani, 1,000 kutoka Kanada, 935 kutoka Uingereza na 583 kutoka Australia. Katika Marekani peke yake ilikisiwa peke yake ilikisiwa kuwa si chini ya watu 1,500,000 walikuwa wameambukizwa ukimi. Kufikia mwaka 1991 ni kwamba ilitarajiwa kuwa na wagonjwa wapya wa ukimwi 75,000 kwa mwaka. Katika Afrika, inaaminiwa kuwa kuna mamilioni ya watu wenye viini vya ugonjwa wa ukimwi.

Ukimwi husababishwa na viini ambavyo hushambulia chebechembe fulani ambazo ni muhimu sana kwa kinga ya mwili. Matokeo ya upungufu wa kinga ya mwili huwezasha vijidudu vingi visivyo sababisha maradhi ya kawaida kushambulia mwili na kusababisha matokeo yenye athari kubwa. Wagonjwa walio wengi hufa katika kipindi cha miaka miwili baada ya kupatikana na ugonjwa huo wa ukimwi. Hata hivyo UKIMWI wenyewe sio mwisho wa mambo. Kiini kinachosabisha UKIMWI pia hushambulia ubongo moja kwa moja kwa mojanna kusababisha wazimu. Magonjwa mengine pia yaweza kusababishwa na hali hii. Haijajulikana bado ni msururu wa magonjwa gani ambayo huambatana na huu UKIMWI. Kinachojulikana tu, ni kuwa theluthi moja ya wanaoambukizwa au hata wote wataathirika na maradhi ya muda mrefu yasiyoponyeka na ya kukondesha sana na hatimaye kifo.

Kiini cha UKIMWI huambukizwa kutoka kwa mtu hadi mwingine kutokana tu na vitu majimaji vya mwilini vikiwa na viini vya |UKIMWI, vitu majimaji hivi hutekwa kutoka kwa mgonjwa wa UKIMWI na kumwingia mtu mwingine.

Linatokeaje jambo hili? Zipo njia kuu tat:-

-    Zinaa
-    Kutoa damu aidha kwa njia ya kuchanjwa sindano ambazo zimetapakaa damu yenye viini hivyo au kuongezewa damu au vitu majimaji ambavyo vinatokana na damu yenye viini vya UKIMWI.
-    Mama kwa mtoto katika tumbo la uzazi au wakati wa kujifungua.

UKIMWI uligunduliwa kwa mara ya kwanza miongoni mwa vijana walawiti huko Marekani na mpaka sasa idadi kubwa ya wagonjwa wa UKIMWI katika Marekani ni walawiti. Asilimia themanini na tano ya wagonjwa wa UKIMWI katika Uingereza ni walawiti. Kuna sabbu mbili za kuelezea jambo hili. Kwanza, walawiti wa kiume hujionyesha wanazo nguvu nyingi zaidi kwa kuwa na mamia ya wapenzi wa zinaa. Uwezekano wa kuambukizana ni mkubwa sana. Uchunguzi uliofanywa kwa walawiti unaonyesha kuwa zaidi ya 5% katika baadhi ya miji mikubwa wameambukizwa viini vya UKIMWI. Pili, yumkini viini vya UKIMWI hupita kwa urahisi zaidi kati ya mwanaume na mwingine kuliko mwanamke na mwanaume.

Kulawiti hakuambatani na maumbile asili, mwili wa binadamu haukuumbwa kwa ajili ya mambo na kusababisha mikwaruzo yenye kutoa damu, mikwaruzo ambayo itavirahisishia viini vya UKIMWI kuuingia mwili kwa kupitia sehemu za mwili zilizo athirika na michubuo.

Katika nchi za magharibi kundi la pili kubwa la wagonjwa wa UKIMWI ni watumiaji wa madawa ya kulevya kwa njia ya sindano. Kuna wimbi sugu la uenezaji wa matumizi mabaya ya madawa ya kulevya katika nchi za Magharibi kwa njia ya kutumia kwa pamoja sindano zitumikazo kudunga madawa ya kulevya kupitia mishipa ya damu na hatimaye kuambukizwa kwa njia hii.

Katika Afrika, mahali palipofikiriwa kuwa ndipo chimbuko la UKIMWI kwa kumwambukiza binadamu kwa mara ya kwanza katikati ya miaka ya sabini sasa mtazamo ni tofauti. Njia kuu ya kuambukiza zinaa asilia (ya kawaida). Nusu ya wagonjwa ni wanawake na watoto wengi wameambukizwa. Lakini matumizi ya sindano zisizo chemshwa vizuri na kupewa damu yenye viini katika harakati za tiba, yawezekana yahusika zaidi. Zaidi ya hayo akina mama wenye viini vya UKIMWI, huweza kuwaambukiza watoto wachanga kabla ya kuzaliwa. Kwa nini uambukizaji wa

UKIMWI
kwa njia ya zinaas asilia (kawaida) ni mkubwa zaidi katika Afrika, lakini bado haujawa mkubwa katika nchi za Magharibi si dhahiri lakini sababu mbili zimetolewa.

Watu walioathiriwa na UKIMWI katika Afrika huelekea kuenea sana kama walawiti wa nchi za Magharibi. Pia ile hali ya kudumu ya maradhi ya zinaa katika Afrika huenda inasaidia uenezaji wa UKIMWI kwa kuwezesha viini vya Ukimwi kuingia kwa urashisi zaidi katika mwili kupitia kwenye sehemu za mwili zilizo athirika.

Biblia na Ulawiti

UKIMWI umewaweka wazi wazi mbele za watu wanaume walawiti na tabia zao za kupenda zinaa. Watu wengi wamelazimika kujifunza kile ambacho hawakutaka kujua kamwe. Biblia inaeleza jambo hili wazi wazi. Ulawiti ni dhambi, sheria ambayo Mungu alimpa Musa inasema:-

Usilale na mwanaume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. (m/Walawi 18:22)

Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume,kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao. (M/Walawi 20:13)

Vile vile katika Agano Jipya ujumbe ni ule ule:-

Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyangaeyi. (1 Wakorintho 6:9,10)

Baadhi ya watu wamebisha kuwa hukumu ya kibiblia kuhusu kulawiti sio halali kwa kuwa walawiti hawawezi kujizuia jinsi wajisikiavyo na hii ni nyongeza tu ya ubaguzi na mateso makali yanayowapata wengine kubisha kuwa hukumu kama hii ni kinyume cha Ukristo. Wanatupilia mabali maneno dhahiri ya Biblia wakati huo huo wanajisai ni Wakristo. Baadhi yao wameisha hata kutoa rai kuwa kuna hisia ya kuwa wapo walawiti miongoni mwa watu wa Biblia. Katika kujibu mabishano haya maelezo yafuatayo yametolewa:

1.     Katika Biblia Mungu anakataza vitendo vya ulawiti na sio mielekeo yake. Kuta watu ambao wana hulka ya kiasili ya kujitamani wenyewe. Hulka kama hizi zitasababisha majaribu ambayo wengine hawayapati, lakini yafaa wafikiriwe sawa na wale wanaopata majaribu asilia. Mielekeo na majaribu sio dhambi labda yakiendekezwa. Isipokuwa hapo tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi (Yakobo 1:15). Majaribu ni lazima yazuiliwe, nayo Maandiko yanatufunza jinsi ya kufanya.

2.    Hapana shaka kwamba hukumu ya kulawiti Maandiko Matakatifu ni ile ile iliyo katika Agano la Kale na ile illiyo katika Agano Jipya na ni mamlaka wazi aliteuliwa na Bwana Yesu Kristo mwenyewe kuushuhudia ukweli wa Yesu Kristo kokote kwa watu wa mataifa. Paulo mtume alizungumza na kuandika kwa miujiza ya uwezo wa Roho Mtakatifu. Ikiwa sisi tutazikataa Nyaraka zake, basi tutakuwa tunakataa sehemu zingine za Biblia.

3.    Kuna mifano ya upendo na mapenzi yaliyoonyeshwa kati ya watu katika Maandiko Matakatifu, lakini hakuna mifano ya ulawiti ambayo inakubalika. Makabila mengi ya Waingereza asilia (Anglo-Saxons) huweza kuchanganya kati ya upendo na mapenzi kutokana na sababu za kimila. Lakini katika Ufaransa, Urausi na nchi zinginezo ni kawaida kwa wanaume kusalimiana kwa busu. Katika Biblia hali hii ni kweli pia. Mtume Paulo anawashauri wafuasi wa Kristo wasalimiane kwa busu takatifu (Warumi 16:16 n.k). Bwana Yesu alionyesha mapenzi kwa wafuasi wake (Yohana 15:13). Urafiki kati ya Daudi na Yonathani unafafanuliwa kwa maneno haya: Roho ya Yonathani ikaambatana na roho ya Daudi, na Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe (1 Samueli 18: 1). Kwa hiyo basi, urafiki na mapenzi ya kweli kati ya watu wa Mungu katika Maandiko Matakatifu ni kamili. Ni mawazo potofu tu yanaweza kugeuzwa toka urafiki na mapenzi ya kuunga mkono ulawiti. Waraka wa Tito 1:15 unasomeka:

Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi, lakini hakuna kilicho safi kwao walio najisi na wasioamini, bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.

4.    Hakuna msingi wa Maandiko Matakatifu kuhusu kuwatesa au kuwakandamiza walawiti kwa njia yoyote ile. Ingawa walawiti wamebezwa hata kidini, Biblia inaeleza wazi:

  • Mtumwa wa Bwana haimpasi kuwa mgonvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote (2 Timotheo 2:24).
  • Wasimtukane mtu yeyote a. Wasiwe wagonvi, bali wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote (Tito 3:2).

5.    Ulawiti ni dhambi inayosameheka. Wakati mturme Paulo aliuelezea ulawiti kama mojawapo ya dhambi katika orodha ya madhambi ambayo kama ikifuatwa, basi itamzuia mtu kuingia Ufalme wa Mungu, aliendelea kusema.

Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii, lakini mliosha mkatakaswa, na kuhesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo kwa Roho wa Mungu wetu. (1 Wakorintho 6:11).

Ujumbe wa Injili ni huria na wazi kwa aina zote na madhambi. Kutubu kunahitajiwa na Mungu kutoka kwa kila mmoja ambaye ataokoka, na kwa njia ya ubatizo wote watapata msamaha wa dhambi kwa kufuata mtindo mpya wa maisha mapya.

Biblia na Ngono zisizo na utaratibu Katika Maandiko Matakatifu yaliyonukuliwa hapo juu na ambayo yanalaani ulawiti inapaswa kueleweka kuwa ulawiti ni mojawapo ya dhambi nyingi zilizo orodheshwa. Tafakari tena maneno ya mtume Paulo:

Msidanganyike; waasherati hawaurithi Ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala walawiti, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watukanaji, wala wanyang?anyi. (1 Wakorintho 6:9,10).

Dhambi za uasherati na uzinzi ndizo hurejewa zaidi katika Maandiko nazo zinalaaniwa zaidi kuliko ulawiti. Mahali pekee panapo stahili kwa ngono ni kwa walioowana kikweli na ndivyo Maandiko yanaruhusu. Kwa mwanaume na mwanamke wa kisasa, watu wa Magharibi jambo hili kamili halikubaliki kidofo. Mbali ya mikasa ya magonjwa ya zinaa, mimba zisizo takiwa, kutoa mimbam kuvunjika kwa ndoa na matatizo ya kusongwa akili na sasa tunaweza kuongeza UKIMWI kwa orodha ya matokeo ya kutokuiangalia njia nyembamba. Katika Afrika, tamaa ya kufanya ngono za ovyo ndiyo njia kubwa ya uenezaji UKIMWI. Bado katika nchi za Magharibi tamaa ya kufanya ngono sio sababu kubwa, lakini yawezekana ueneaji wa aina hii utakuwa mkubwa sana. Tangu mapenzi huria yamekuwa ni mtindo unaokubalika kwa miaka ya sitini, ngono za ovyo zimekuwa za kawaida. Magonjwa ya kuambukiza ya zinaa yaliyo wapata wanasimulia. Maambukizo ya kaswende na kisonono yanatoa ushahidi mkubwa. Mwaka 1985 Uingereza na Wales pekee kulikuwa na zaidi ya wagonjwa wapya 650,000 wa maradhi yaenezwayo kwa njia ya zinaa na waliweza kutibiwa kutibiwa kwenye Kliniki za huduma ya afya za kitaifa.

Je! UKIMWI ni adhabu kutoka kwa Mungu?

Kutokana na mafundisho ya Biblia kuhusu ulawiti, baadhi ya watu wamedai kwamba
UKIMWI ni hasira ya Mungu dhidi ya ulawiti. Ni kweli kuwa katika nyakati za Biblia BWANA wakati mwingine aliingilia katika masuala ambayo yawahusu binasamu pindi walipokithiri katika maovu, nayo Biblia inakumbukumbu kuwa Mungu aliwaadhibu watu au mataifa kwa njia ya magonjwa. Hata hivyo hatuna mamlaka ya Maandiko Matakatifu kusema kwamba Mungu ameingilia kati kimiujiza kuleta UKIMWI kwa walawiti, na sasa hivi kuna watu chungu nzima wenye UKIMWI ambao wameupata ugonjwa huu bila makosa yao, kwa njia kama vile kuongezewa damu au tu kwa kuzaliwa na mama ambaye ameambukizwa UKIMWI. Lakini kuna fundisho la Maandiko ya moja kwa moja ya kuvunja amri zake.

Katika Warake kwa Warumi, mtume Paulo anaeleza jinsi binadamu alivyoacha kumwabudu Mungu wa kweli na kugeukia kuabudu sanamu. Likihusishwa na jambo hili. Kulikuwa na hali ya kupungua katika maadili ya kiroho kuelekea huo ulawiti. Mara tatu katika taarifa hii, mtume anasema kwamba Mungu awaacha watu hao ili wavune matokeo ya matendo yao:

Kwa jinsi hiyo Mungu aliwaacha katika tamaa za yao waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya muumba wao aliyeahidiwa milele. Amina. Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aidbu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili. Wanaume nao vivyo wakayaacha matumizi ya mke ya asili wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa hivyo wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Mungu akawaacha wafuate akili zao zisizo faa (Warumi 1:24-28).

Katika fungu hili la maneno matokeo ya mwili kwa walawiti yameelezewa. Walipokea nafsini mwao malipo ya upotevu wa yaliyo haki yao. Ni hakika maelezo haya yafaa kwa kuwa ni matokeo ya moja kwa tabia ya kulawiti. Sio kwamba Mungu anawaletea UKIMWI papo hapo walawiti, bali ni hapo wanapo ivunjia hadhi miili yao kwa kuitumia kinyme na asili, wanateseka kwa matokeo ya kwanza.

Mungu kwa kuwaacha ameruhusu mfuatano wa viumbe uende kwa mpango wa asili. Kwa jibu la hili, watu wengine wamesema kwamba UKIMWI pia unaweza kueneza tamaa ya kupenda kufanya ngono. Hii ni kweli, na ngono nje ya ndoa pia ni uvunjaji wa sheria ya Mungu na yanawafichua wapenzi kwa magonjwa yatokanayo na kitendo cha kukutana kimwili. Lakini hakuna shaka kwambu uovu wa kutoheshimu matumizi ya mwili ya asili kwa njia ya kulawiti katika nchi za Magharibi kwa miaka ya karibuni, pamja na vitendo vyao zaidi vya kulawiti ovyo na matendo yasiyo ya asili, yamesababisha UKIMWI kusambass kwa haraka sana. Ingawa walawiti au kulawiti hakusababishi UKIMWI, lakini fungu kubwa la hao walawiti ndilo linaathirika, pengine ndilo limesasbabisha maambukizo katika Amerika na Uingereza. Tokana na hao wamepelekea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na kisha kuwakiana tamaa, hali kadhalika kwa njia ya mchango wa damu na mazao yatokanayo na damu.

Katika Waraka kwa Warumi kulawiti hasa ni njia moja ya kuacha mwongozo wa Mungu ambako kumesisitizwa sana ambako wanadamu wamevubua. Walianza kwa kukengeuka kumwamini Muumba na kisha wakazidharau sheria za maumbile, na hatimaye wakavuna matokeo. Ili mtu asije jihesabia haki kwa kiburi kwa kuto heshimu kwa njia hii, fungu lile lile la maneno ya Maneno ya Maandiko yanaendelea kulaani dhambi zingine ambazo zimejumuishwa uasherati, tamaa, husuda, choyo, ugonvi, majivuno, kiburi, na hata kutowatii wazazi, kama mtindo wa maisha wa wenye akili mbaya. Kwa kweli, kama tukisoma sura za mwanzo za Waraka kwa Warumi tutatambua kwamba maana yote ya Mtume ni kuthibitisha kuwa kila mtu bila ubaguzi, ni mwenye dhambi kwa asili:

Hakuna mwenye haki, la, hata mmoja a Maana wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Warumi 3:10, 23).

Ni jambo la msingi kukubali ukweli huu kama tutathamini haja ya ukombozi kwa njia ya Yesu Kristo. Yesu aliwaambia viongozi waliojihesabia haki wa dini katika siku zake:

Wale ambao ni kamili, hawahitaji mgananga, bali wenye dhambi watubu (Mathayo 9:12, 13).

Kuna jambo moja maarufu ambalo li katika Maandiko Matakatifu ambapo Mungu aliingilia kuwaangamiza watu, jina la mji wao umekuwa ni kurejea kwa ulawiti. Dhambi ya Sodoma ya jirani yake Gomora imesemwa na Mungu kuwa imeongezeka sana (Mwanzo 18:20). Wakati wajumbe wawili walipokuja kumuokoa Loti na jamaa yake, watu wote wa Sodoma wazee kwa vijana, watu wote kutoka kila mahali walimjia Loti na kumpigia kelele: Walete hao watu kwetu ili tuwajue (Mwanzo19:4, 5). Hapana shaka kwamba huo mkutano ulitaka kuwalawiti wajumbe kutokana na maelezo ya maneno. Waliharibika akili kabisa hata walipopigwa kwa upofu bado walijichosha kwa kuutafuta mlango wa nyumba ya Loti.

Mfano wa Sodoma ni onyo la Leo

Kwa sababu ya uovu wao wa kupindukia Sodoma na jirani yake waliteketezwa ghafla kwa mlipuko wa moto wa volkano na mawe yaliyoyeyuka na kuwaangamiza kabisa kutoweka kwenye uso wa ardhi. Mtume Petro katika Agano Jipya anasema walifanywa wawe ishara kwa wasiomcha Mungu (2 Petro 2:6). Na mtume Yuda anasema kwamba wamekwa kuwa dalili wakiadhibiwa kwa moto wa milili (Yuda7). Hivyo, kwa msiba wa Sodoma na Gomora umewekwa kwetu kuwa mfano wa hukumu ambayo mwisho ataileta kwa ulimwengu usiomcha Mungu, kwa kuwaangamiza waovu kabisa wasiwepo tena. Huu ni mwelekeo wa mafunzo ya Biblia ambao mara nyingi umedharauliwa na wakati mwingine haujaeleweka vema. Kurudi kwa Bwana Yesu kutaleta amani na haki kwa dunia hii hapo Ufalme wa Mungu utakaposimamishwa; lakini katika kuiweka haki hapata epukika wale waliozikataa njia ya Mungu. 2 Wathesalonike 1:7-10 unasema:

Bwana Yesu atafunuliwa kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake katika mwali wa moto huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; na wataadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile.

Basi bhambi ya Sodoma ilikuwa ni ya kuchukiza hata kuangamia kwake kumekuwa ni onyo kwa vizazi vyote. Pima basi maneno na uzito wake ya Bwana Yesu aliyo sema kwa miji hiyo ya Israeli ya waliokataa kuikubali Injili:

Amini nawaambia itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu kuliko mji ule (Mathayo 10:15). Siku ya hukumu kwa ile miji iilikuja baada ya miaka arobaini hivi wakati Rumi ilipoiangamiza Israeli kwa kisasi kikali ajabu, balaa mbaya zaidi kuliko maangamizi ya ghafla ya Sodoma. Hukumu ile ilikuwa ni mbaya zaidi kwa sababu madaraka yao yalikuwa makubwa zaidi baada ya kumwona na kusikia Mwana wa Mungu, waliukataa ujumbe wake na walimsulubisha.

Onyo hili linatuhusu sisi siku hizi. Bwana Yesu aliizungumzia Sodoma kuhusiana kwake na kuja mara ya pili. Wakati ule alielezea jinsi ya kuja kwake tena hapa duniani kuanzisha Ufalme wa Mungu kwa namna hii:

Kama ilivyokuwa siku za Lutu walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kujenga. Lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulikunya moto na kibiriti kutoka mbinguni wakaangamia wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu. (Luka 17:28-30).

Labda inashangaza kuona kwamba hakuna liliotajwa kuhusiana na uovu wa zinaa iliyopotoka ya Sodoma. Badala yake Sodoma inalezewa kama mji uliojawa na ulimwengu wa leo upo katika hali hii ukijishughulisha na maendeleo ya vitu na kuachilia mbali mambo mema ya kiroho. Neno la Mungu ni aidha linafanyiwa mzaha au linaachiliwa mbali, lakini bado ni Neno lile ambalo linatuonya sisi tujiandae kwa ujio wa Kristo.

Ingawa Bwana hakuweka dhahiri uovu wa Sodoma katika onyo lake, alikidhihirisha kiini chake cha maovu ya Sodoma. Unabii wa Ezekieli 16 unaeleza:

Tazama uovu wa umbu lako, Sodoma ulikuwa huu kiburi na kushiba chakula na kufanikiwa hayo yalikuwa ndani yake na binti zake, tena hakuutia nguvu mkono wa masikini na mhitaji. Nao walijivuna, wakafanya machukizo mbele zangu na kwasababu hiyo naliwaondoa hapo nilipoyaona. (Ezekieli 16:49-50).

Jamii yao ilikuwa imejawa na matajiri waliwanyoya maskini. Ustawi mkubwa wa matajiri ulisababisha kuwa na starehe muda mwingi, hata vishawishi vya mwili hawakuweza kuvizuia. Hapa kuna mwelekeo uliowazi wa dunia yetu ya sasa na katika hali hii ya nyakati ili kutuonyesha mambo yanayofanana kati ya sasa na ya wakati ule wa Sodoma.

Kuzuiakuenea kwa UKIMWI

Mamilioni ya fedha yanatumika sasa kwa kuuwaelimisha wakazi wa dunia hii jinsi ya kuzuia kuenea kwa UKIMWI. Inatumainiwa kuwa watu watabadili tabia zao ikiwa watapata taarifa ihusuyo ugonjwa wenyewe. Ujumbe wa Serikali katika Uingereza unakubaliana dhahiri na ushauri wa Maandiko Matakatifu. Kisiasa haukubaliki wala hauwezi kufanya kazi kufanya kazi kwa kwa kutoa ushauri kwa watu kuwa wazingatie ndoa ya halali na yenye uaminifu. Ushauri unaotolewa ni ule wa kupunguza idadi ya wapenzi na njia za kuzuia za kuzuia mimba ambazo zitazuia kuambukizwa. Uamuzi wa kuchukua hatua za kijamii badala ya njia za kiroho imewafanya watu wenye imani kubwa ya dini kuusakama uamuzi huo.

Serikali imeamua kuwa jamii ndiyo yenye kutoa mwanya mkubwa kwa mtindo wa zamani kwa uadilifu wa nguvu ya wazi. Lakini vyovyote Serikali itakavyo ona kuwa uamuzi wake watumika kwa wakati, wafuasi wa Bwana Yesu Kristo inawapasa, kwa wao wenyewe na watoto wao, wajihadhari kwa kuusikiliza ujumbe wa Maandiko. Ngono nje ya ndoa ni kosa. Kulawiti ni kosa. Na kujaribia madawa ya kulevya ni kosa. Magonjwa kama UKIMWI yangeweza kuwa yameenea zamani katikanchi ya Kanaani wakati ule Israeli walipotoka Misri. Wakanaani walipotoka sana kiasi kwamba hawakuweza kufaa kuishiriki pamoja nchi ya Israeli. Kwa hiyo tofauti Israeli walipewa sheria ambayo kama ikifuatwa vema itawalinda dhidi ya magonjwa kama UKIMWI. Pasingekuwa na hatari kama jamii wangekuwa waaminifu kwa ndoa kutoka magonjwa yatokanayo na zinaa. Vitendo vinavyohusiana na desturi za kidini zilipigwa marufuku.

Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu mimi ndimi BWANA. (M/Walawi 19:28).

Siku hizi katika Afrika vitendo kama hivi vinaweza kuchangia sana kuenea kwa UKIMWI na magonjwa mengine yaenezwayo kwa njia ya damu.

Sheria ya Musa ni maarufu kwa manufaa ya jamii kutokana na sheria za kiroho. Busara hii kubwa ambayo ni ya kisasa ikitazamwa kwa undani inatoa ushuhuda wa kweli kwmba ile sheria kweli Musa alipewa na Mungu. Na wakati sherehe zote za tambiko na kanuni ya sheria vikioanishwa kwa wafuasi wa Kristo, misingi ya utakatifu iliyomo ndani yake itakuwa imeidhinishwa na Kristo mwenyewe. Wafuasi wa kweli wa Kristo kwa mujibu wa wito wao watapukana na tabia ambayo itawaeka katika hatari sana ya kupata UKIMWI. Katika kutii Maandiko Matakatifu watauona ukeli wa maneno ya Mtume Paulo:

Utaua unafaa kuliko mambo yote, yaani, unao ahadi ya uzima wa sasa, na ule utakao kuwepo baadaye" (1 Timotheo 4:8).

Ushauri umepuuzwa

Jamii yetu ambayo haimjui Mungu kabisa haitishwi na Maandiko Matakatifu na wengi wanaonekana kutotiishwa hata na ushauri wa Serikali. Vijana wengi hasa wanaofanya zinaa ya kawaida (MUME NA MKE) wanaona ni kama ndoto, hatari ziletwazo na uovu huu. Mtu mmoja wa miaka 25 aliandika katika gazeti la Sunday Times: Haitamzuia mmoja wetu, uwezekano ni kwamba hakuna kitakachotokea. Wakati tukiwa katika hatari ya kifo, tutachukua bahati zetu wote jinsi nyingine haifai kufikiria abasani.

Watu wa jinsi hii huweka imani kubwa katika dawa za kisasa, hutafuta dawa za kuponya au kuzuia. Lakini kwa muda mfupi yote haya mawili huonekana bure. Njia pekee iliyobaki ni kuzuia. Hata hivyo, kwa wengi hilo linahusa kujinyima anasa za uovu ambazo wanaonekana hawana nia ya kuziacha pamoja na kwamba zina matokeo sana. Imani hii haiwahusu vijana peke yao au kizazi hiki tu. Idadi kubwa ya watu imekuwa ikikataa kila mara kuzingatia maonyo ya Biblia. Katika unabii wa Isaya kuna maelezo ya mji ambao ulikuwa unazingirwa na kutaka kuangamizwa na adui mwenye mguvu kwa sababu ya uovu wao. Lakini badala ya kutubu na kumrudia Mungu ili awakomboe, hivi ndivyo nabii alivyogundua:-

Siku hiyo BWANA wa majeshi akawaita watu walie na kuvaa nguo za magunia, na kumbe furaha na kuchekelea na kuchelea na kuchinja ng'?mbe na kuchnja Kondoo na kula nyama na kunywa mvinyo, tule tunywe, kwa maana kesho tutakufa" (Isaya 22:12, 13).

Je! Hii haiwahusu pia wale zaidi kupata fursa ya anasa na kujirahisisha kuliko kujinusurisha? Na je, hili halihusu pia dunia nzima ambayo inajihusisha zaidi na vitu kutafuta utajiri hata kama inahatarisha uzima wa milele?

Kulenga kwenye Habari Njema
Ikiwa UKIMWI utafaulu au kumaliza uzuri hakika itakuwa kwamba kwa kufunua haki ya jinsi gani mwanadamu alivyokwenda upande kutoka kwenye njia ya Mungu, wengine wanaweza kuacha kupima tena njia ya maisha yao. Katika Biblia njia iliyo bora imetolewa: njia ambayo inafaida katika maisha haya na pia na muhimu zaidi italeta uzima wa milele kwenye Ufalme wa Mungu ambao Bwana Yesu atausimamisha katika dunia hii akirudi.

Yesu atakapokuja atawahukumu walimwengu, na kuwazawadia wafuasi wake waaminifu maisha ya milele, na kuweka haki katika dunia yote (Zab. 72). Kwa kipindi cha miaka 1000 ya utawala wa Kristo duniani patakuwa na mabadiliko makubwa na maeo ya jangwa yatachanua (Isaya 35). Maisha ya kuishi wakati huo yatarefushwa kwa umma utakao kuwepo katika Ufalme. Magonjwa yataondolewa, kuonewa na kunyanyaswa hakutakuwepo, wenye njaa watashibishwa, masikini na wahitaji watapata kuhurumiwa, na dhambi yenyewe itafungwa kwa uweza Mungu. UKIMWI utakuwa ni jambo la zamani.

Kwenye mwisho wa kazi yake Bwana Yesu hatimaye ataziondoa dhambi kabisa, hivyo ni kusema kuwa mauti yenyewe yataharibiwa (1 Wakorintho 15). Hizi ni Habari Njema za Ufalme wa Mungu.

KIMERUDIWA OKTOBA : 1987.

Na Dr. Stephen Palmer.

KIMETAFSIRIWA

Na Mosses S. Komanya (1990)

                               

 

Swahili Title: 
Ukimwi
Web file: 
Text file: 
Swahili Word file: 
PDF file: 
Status: 
Printed
African text: 
Carl Hinton
Translator 1: 
Mosses S. Komanya