376. MWANZO - UTANGULIZI

376. MWANZO - UTANGULIZI

"Hapo mwanzo Mungu"

MAZINGIRA YAKE NA MWANDISHI

Biblia inaanza na kundi la vitabu vitano, vinavyoitwa kwa ujumla The Pentateuch, kutoka kwa nahau ya Kigiriki "kitabu cha miongo mitano." Maudhui ya vitabu hivi ni pamoja na historia (Mwanzo), Amri (Kutoka), sheria ya ibada (Mambo ya Walawi), serikali (Hesabu), na maonyo (Kumbukumbu la Torati). Uandishi wa vitabu hivi kwa ujumla unahusishwa na Musa (tazama Kut. 24:4; 34:28; Hes. 33:2; Kum. 1:1; 4:44; 33:1; Mk. 12:19, 26; Yoh. 1:45, nk.), na kidesturi, jambo hili limekubaliwa bila swali. Hata hivyo, falsafa ya upinzani wa juu imepinga kauli hii, ikidai eti vitabu hivi ni vya Ki-Musa wala si vya Musa. Inasisitiza kuwa vitabu hivi ni mchanganyiko wa waandishi mabalimbali, na ikavipa herufi za kustaajabisha, kama vile, J ama E au P, kulingana na maneno yaliyotumika, kwa kuwa waandishi halisi hawajulikani. Msingi wa kauli yake upo katika matumizi ya maneno, mpangilio wa sarufi katika kifungu, na kadhalika; kana kwamba waandishi daima hutumia mtindo mmoja wa lugha, ama kuwa hujipimia fungu moja la msamiati kutumika katika uandishi wao wote

Kauli hizi zimebatilishwa kikamilifu na wanafunzi wa jadi. Wanatambua mwandishi mmoja tu mwendelevu: Musa

Hata hivyo, kuna matatizo yanayohusiana na uandishi wa vitabu vya kale vya Biblia. Kwa mfano, Kutoka 14:14 inapeana jina "Dani" kama mahali ambapo (Abramu ) Ibrahimu aliyafuata majeshi ya Kedorlaoma; Ilhali hudaiwa, jina hili halikupeanwa hadi wakati wa Wafalme (Waamuzi 18:29).

Tena, Mwanzo 36:31 yaongea juu ya wafalme wa Edomu kutawala kabla ya "kumiliki mfalme ye yote juu ya wana wa Israeli"; taarifa inayoashiria wakati wa uandishi kabla ya utawazwaji wa Sauli (1 Sam. 8:5). Zaidi ya hayo, kazi ya Musa wakati mwingine imeelezwa katika nafsi ya tatu, kama kwamba imeandikwa na mtu mwingine bali na yeye. Kwa mfano, twasoma katika Kutoka 11:3 na Hesabu 12:3 kuwa "Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri" na "huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi." Katika Kutoka16:35; Hesabu 32: 34-42; Kumbukubu la Torati 2:10-12, 20-23 and 34:1-12, matukio yametajawa yaliyofanyika baada ya kifo cha Musa.

Kuna maoni kuwa marekebisho haya duni yaliongezwa baadaye ili kukamilisha rekodi ya Musa. Hii yaweza kuwa kweli kwa sababu mwandishi halisi wa vitabu hivi ni Mungu wala sio Musa. Musa alikuwa mkono ambao kuupitia, ufunuo wa Mungu ulijulikana kwa binadamu na kama Mungu alidhamiria nyongeza hizi zifanywe, Mungu angesababisha yatimizwe hayo.

Hata hivyo, yawezekana kuwa Musa aliviandika. Sio vigumu kuwa Ibrahimu alipaita mahali pale Dani, alikomwaga hukumu ya uungu kwa Kedorlaoma, kwa kuwa Dani inamaanisha hukumu, na kwa hivo jina hilo lilikuwa mwafaka katika mazingira yote mawili. Kuhusu taarifa ya of Mwanzo 36:31, lazima ikumbukwe kuwa Waisraeli walikuwa wameahidiwa wafalme (Mwa. 35:11), na Esau pia alikuwa ameahidiwa mamlaka (Mwa. 27:40), hivi kwamba taarifa hiyo iliambatana na ujuzi na matarajio ya Musa. Hisia zinazopatikana katika Kutoka 11:13 na Hesabu 12:13 huenda ziliandikwa na Musa, kwa msukumo wa Mungu, na kunakiliwa katika nafsi ya tatu kuepuka shutuma za ubinafsi. Maelezo sambamba yaweza kuelekezwa kwenye pingamizi zingine juu ya uandishi wa Musa. Alikuwa nabii. Yehova alikuwa Amembainia nia Zake; na lugha ya unabii ni dhahiri katika maelezo ya wazi yanayohusiana na adhabu ya Israeli, utawanyikaji na marejesho kama inavyodhihirika katika Kumbukumbu la Torati 28:64-68; 29:20-29; 30:4-8, na kwingineko. Taarifa ya kifo cha Musa, na tathmini ya thamani yake, iliyomo katika Kumbukumbu la Torati 34, yaweza kuwa iliongezwa na Yoshua; lakini yaweza kuwa iliandikwa na Musa kwa mwongozo wa Mungu.

 

MPANGILIO WA KITABU

Vigingi Viwili Ambavyo ni Daraja ya Ufunuo wa Mungu kwa Binadamu

Mwanzo ni kitabu cha kipekee cha mianzo, kinachoweka msingi wa kusudio la Mungu kwa binadamu. Kinafafanua jinsi Mungu alivyoumba dunia mwanzo, vile binadamu alivyoasi, vile kifo kilivyolazimishwa kwa binadamu, vile Ibrahimu alijitenganisha na watu wake, vile Yakobo aliwazaa wana kumi na wawili waliokuwa makabila kumi na mawili ya Israeli

Mwanzo kina uhusiano wa karibu na Ufunuo: kitabu cha kwanza na kitabu cha mwisho. Vitabu hivi viwili ni kama nguzo mbili zinazotekeleza ufunuo wa Mungu kwa binadamu; cha kwanza kikieleza vile yote yalivyoanza, cha pili kikieleza vile yote yatakavyoishia.

Mwanzo kinaongea juu ya uumbaji wa asili (ml. 1); Ufunuo juu ya uumbaji wa kiroho (Ufu. 3:14); katika Mwanzo, nyoka anena; katika Ufunuo, azuiwa (Ufu. 20:2). Katika Mwanzo, laana yawekwa (Mwa. 3:16-19); katika Ufunuo yaondolewa (Ufu. 21:14). Katika Mwanzo, kukaribia mti wa uzima ilikuwa marufuku (Mwa. 3:24); katika Ufunuo, ruhusa imepatikana (Ufu. 2:7). Katika Mwanzo, paradiso ya kwanza imefungwa kwa mwanadamu (Mwanzo 3:23); katika Ufunuo, amefunguliwa (Ufu. 21:25).

Na kadhalika. Uhusiano baina ya vitabu hivi viwili waweza kuongezwa, kwa sababu katika Mwanzo kunaonekana mianzo ya yote ambayo Ufunuo kinatabiri kuwa ukamilifu wa nia ya Mungu duniani.

Mwanzo na Ufunuo vimepata mashambulizi kuliko kitabu kingine chochote katika Biblia; Mwanzo na wakosoaji wanaodai eti matukio kinayonakili (uumbaji, uchafuzi wa semi, gharika, na matukio mengine ya kipekee) hayawezekani; Ufunuo na wale wanaosizitiza kuwa maono yake ya utukufu ujao hayawezekani pia. Mwanzo inakataliwa kwa misingi kuwa ni vigumu kuamini matukio ya aina hiyo; Ufunuo kwa misingi kuwa ni vigumu kufafanua!

 

Methali ya Torati

Kila kitabu cha Biblia kinawakilisha lengo la Mungu katika Kristo kwa jinsi fulani. Aidha, vitabu mbalimbali vya Biblia vikichukuliwa katika makundi vimeweka kwa mpangilio lengo lile lile la Mungu. Uhamasisho huu waonekana kutoelekeza tu maneno ya Biblia , bali pia mazingira ya vitabu vyake.

Kwa mfano, angalia jinsi Mwanzo kinavyoanza na kinavyokoma. Kinaanza na Mungu akiangalia vyote Alivyoumba, na kutamka "ni vyema". Kianaishia na maneno manne ya mafumbo: "Jeneza nchini Misri", kikiongea juu ya kifo uhamishoni. Katika mwanzo na mwisho wa kiajabu wa kitabu hiki cha kwanza cha Biblia, kuna maelezo ya mapema ya binadamu kushuka kutoka neema. Haya hakika ndio maudhui ya kitabu hiki kizima.

Tafakari maneno mawili muhimu ambayo yanatamatisha Agano la Kale: "laana". Si hiyo inaashiria yote yanoyopatikana katika Agano la Kale kupitia utovu wa kuweka Sheria wa binadamu? Na Agano Jipya linaanzaje? Bila shaka na maelezo ya kuzaliwa kwa yule aliyeteuliwa kuondoa laana! Na kwa hivyo, uwiano na tofauti zinaendelea.

Angalia sasa methali ya Torati - "Pentateuch" ( pente - tano; na teuchos - kitabu), vitabu vitano vya Musa, kwingineko vikiitwa Sheria.

Tano ni nambari ya neema, na vitabu vya Musa vyasimulia hadithi endelevu ya neema. Hadithi hii yaweza kuchukuliwa kutoka kwa mtizamo wa Mungu, ama kutoka kwa mtizamo wa binadamu. Hakika maudhui ya vitabu hivi vitano kutoka kwa mtizamo wa Mungu yamepanga kwa utaratibu maendeleo maenevu ya neema.

 Mwanzo:

chaongea juu ya Mamlaka na Nguvu za Mungu — katika kuumba, kuadhibu na kuchagua.

Kutoka:

chaongea juu ya Huruma ya Mungu — katika kuchagua na kutoa.

Mambo ya Alawi:

chaongea juu ya Utukufu wa Mungu — katika kutenganisha na kutakasa

Hesabu:

chaongea juu ya Wema wa Mungu na Ukali — katika ugavi na hukumu

Kumbukumbu la Torati:

chaongea juu ya Uaminifu wa Mungu — katika kutoa nidhamu na ugavi.

 

Sasa, tafakari, havifanyi hatua tano ambazo ni lazima tuchukue ili tupate wokovu? Si ni lazima kwanza tutambue mamlaka na nguvu zake Mungu kabla tufurahie huruma Yake na kadhalika? Na si uaminifu Wake utadhihirika katika kuja kwake Bwana wakati tutajua maana ya nidhamu Yake katika maisha yetu, na kupata ukombozi katika Kristo?

Sasa tafakari juu ya vitabu vivyo hivyo kutoka kwa mtizamo wa binadamu, na tena uone jinsi vinavyoongea juu ya hatua tano kwelekea kwenye neema ya Mungu:

 Mwanzo:

chaongea juu ya Uharibifu na Uchaguzi wa Mungu.

Kutoka:

chaongea juu ya Ukombozi.

Mambo ya Alawi:

chaongea juu ya Ushirika na Mungu.

Hesabu:

chaongea juu ya Mwongozo wa Mungu.

Kumbukumbu la Torati:

chaongea juu ya Upataji wa Tumaini.

 

Tena, yote haya yaonyesha hatua tano ambazo sharti tuzichukue ili tupate wokovu. Mwanadamu sharti atambue hali ya kuanguka ya asili ya binadamu, na umuhimu wa ukombozi kutoka humo, na kwa hivyo kuitikia Mwito wa Mungu kupitia maji ya ubatizo. Wanadamu sharti watafute ushirika wa kweli na Yehova. Lazima wawe chini ya mwongozo wa ushawisi Wake, kama, hatimaye watapata matumaini yao.

Na kwa sababu hivi vitabu vitano vinaeleza wazi kanuni za Neema ya Mungu, kuna maswala muhimu ya kibinafsi ya kujifunza kutoka kwa maelezo na mafunzo ambayo kila kitabu kinafichua.

 

Kugawanya Neno

Zingatio la makini la kitabu kizima — kupiga darubini kwa mtazamo — lafichua kuwa kimegawanywa kwa sehemu mbili:HISTORIA YA AWALI KABISA

Sura ya 1 hadi 11

HISTORIA YA UBABA

Sura ya 12 hadi 50

 

Gawanyiko la kwanza lanakili matukio manne muhimu:1. Uumbaji

Utukufu wa Mungu katika maisha ya kawaida.

2. Kuanguka kwa binadamu

Mamlaka ya Mungu katika kutoa adhabu.

3. Gharika

Adhabu ya Mungu katika dhihirisho la uzuri na ukali.

4. Chafuo la Usemi

Hekima ya Mungu katika utekelezaji wa mapenzi Yake.

 

Utukufu wa Mungu, mamlaka, hukumu na hekima, vyapanga ujumla wa ufunuo wa Mungu.

 

Historia ya Ubaba yahusu watu wanne mashuhuri:1. Ibrahimu

Akiwakilisha wito wa Mungu.

2. Isaka

Akiwakilisha uzazi kwa uungu.

3. Yakobo

Akiwakilisha utunzaji wa uungu.

4. Yusufu

Akiwakilisha cheo kwa uungu.

 

Tazama jinsi wanaume hawa wanne walivyopanga malengo ya hatua nne za ukombozi; kwanza, mwito; halafu, uzazi; hatimaye, mwongozo; na mwisho, kupandishwa cheo.

Mwanzo kimejaa vielelezo vya kawaida vya matukio ya baadaye, na mafunzo ya kibinafsi kwa mwanafunzi.

 

Vizazi Kumi na Kimoja vya Mwanzo

Kwa kutoa uchambuzi wa kitabu cha Mwanzo, litakuwa kosa kubwa kama mgawanyiko wa asili wa kitabu hiki utapuuzwa. Mgawanyiko huo unaonyeshwa katika marudio ya kirai: "Kizazi cha ..." Kirai hiki kinajiri mara kumi na moja katika kitabu, hivi kwamba, pamoja na sehemu ya utangulizi, Mwanzo kimegawanywa katika sehemu kumi na mbili. Neno la Kiyahudi lililotafsiriwa "Vizazi" ni toledot ambalo wasomi wa Kiyahudi husema inamaanisha "historia", "hadithi" ama "taarifa", badala ya nasaba tu. Hivyo, kitabu hiki kinaporejelea "vizazi vya mbingu na nchi" (Mwa. 2:4) ni hadithi, ama taarifa, ya uumbaji wa dunia na nchi, na zilizoleta, ambayo yastahili kuangaziwa.

Katika marejeo hapa chini, kumeorodheshwa mahali kadhaa ambapo kirai hiki kimetumiwa; na itabainika kwamba sehemu kumi na mbili ambazo hii imegawanya Mwanzo kwazo, tena inaonyesha maendeleo ya kiroho. Hivi:

1. Uumbaji — Utambulisho.

Msingi wawekwa - Mwa. 1:1-2:3

2. Vizazi vya bingu na nchi (Mwa. 2:4).

Udhihirisho wa Sheria, Dhambi na Mauti, na ahadi ya Ukombozi - Mwa. 2:4-4:26

3. Kitabu cha Vizazi vya Adamu (Mwa. 5:1).

Maendeleo ya jamii ya binadamu - Mwa. 5:1-6:8

4. Vizazi vya Nuhu, mtu wa haki (Mwa. 6:9).

Gharika; hukumu ya ulimwengu wa zamani, utunzaji wa aliyenusurika - Mwa. 6:9-9:29

5. Vizazi vya wana wa Nuhu (Mwa. 10:1).

Maendeleo ya mataifa - Mwa. 10:1-11:9

6. Vizazi vya Shemu (Mwa. 11:10).

Utengano wa watu kwa ajili ya Jina - Mwa. 11:10-26

7. Vizazi vya Tera (Mwa. 11:27).

Mwito atoke kwa familia - Mwa. 11:27-25:11

8. Vizazi vya Ishmaeli (Mwa. 25:12).

Mgawanyiko wa yale ya kiasili kutoka kwa yale ya kiroho - Mwa. 25:12-18

9. Vizazi vya Isaka (Mwa. 25:19).

Maendeleo ya Mbegu ya Agano - Mwa. 25:19-35:29

10. Vizazi vya Esau (Mwa. 36:1).

Maendeleo ya Mbegu ya Mtu wa Dhambi - Mwa. 36: 1-8

11. Vizazi vya Wana wa Esau (Mwa. 36:9).

Maendeleo ya Mbegu ya Nyoka - Mwa. 36:9-43

12. Vizazi vya Yakobo (Mwa. 37:2).

Maendeleo ya Israeli - Mwa. 37:1-50:26

 

Tena, zingatio la makini la migawanyiko hii litadhihirisha kuwa vinaoenyesha kikawaida dhamira ya Mungu, kutoka uumbaji hadi Israeli ya baadaye. Mataifa yakuzwa, watu wa taifa moja watenganishwa kwa Jina, halafu familia yaitwa kutoka kwa taifa, tenganisho la mambo ya kiroho na yale ya kiasili katika familia, na kadhalika. Hii ndio njia ambayo kusudi la Mungu limefanya kaazi miaka yote: hivi kwamba maelezo ya kihistoria ya Mwanzo yanajumuisha kielelezo ya maisha ya baadaye.

Ni la muhimu kujua kuwa kirai "vizazi vya ..." chatokea mara tatu katika Maandiko Matakatifu, nje ya Mwanzo, ikifanya jumla ya mara kumi na manne, ama saba mara mbili. Kunavyo " vizazi vya Haruni na Musa (Hes. 3:1); " vizazi vya Peresi" (Ruthu 4:18); na "Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo" (Matt. 1:1). Katika kila sehemu, kirai kinajulisha mtu mashuhuri katika jamii ya binadamu, na hatua zaidi ya mbele katika mpango mkubwa wa Yehova wa wokovu.

Matumizi ya mwisho ya kirai hiki ni muhimu. "Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo" ni tofauti mwafaka na " kitabu cha vizazi vya Adamu" (mahali pawili tu ambapo "kitabu" kinapotajwa katika muktadha huu). kirai cha kwanza kinazungumzia Kitabu cha Uzima; cha pili Kitabu cha Mauti. Sote tumeandikwa katika "Kitabu cha vizazi vya Adamu" kwa mujibu wa kuzaliwa kimwili; lakini tutaandikwa tu katika "Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo" tukipata uzazi wa kiroho uliozungumziwa na Yesu kwa Nikodemo.

 

Muhtasari

Genesis (Mwanzo) linatokana na neno la Kigiriki likimaanisha "generation" (kizazi), na ndilo jina lililopeanwa katika tafsiri ya Septuagint ya Biblia, kwa kitabu cha kwanza. Kwa Kiyahudi, kichwa chake ni bereshith,ikimaanisha "hapo mwanzo" (Mwa. 1:1).

Kitabu hiki kinaanza na asili ya mbingu na nchi, kinafuatilia nasaba ya watu wa Mungu kutoka nyakati za awali kabisa, ama "mwanzo" wa uumbaji. Kimegawanywa katika nasaba za mbingu na nchi (Sura 2-4); Adamu (5:1); Nuhu (6:9); Wana wa Nuhu (10:1); Shemu (11:10); Tera (11:27); Ishmaeli (25:12); Isaka (25:19); Esau (36:1); Wana wa Esau (36:9); na Yakobo (37:2)

Adamu, Nuhu, Ibrahimu, Isaka na Yakobo wanaashiria hatua tano kubwa za kuendelea, Yusufu akiwa na sehemu kubwa katika hadithi ya Yakobo. Kuna mwafaka wa umoja kwa ujumla, ikibainisha kwamba katika Mwanzo tuna hamasisho la historia takatifu, na wala sio mkusanyiko wa hadithi za kilimwengu na hekaya kama inavyodaiwa. Marejeo mengine ya Mwanzo katika Agano Jipya ni: Mat.5:48; 19:4-5; 23:35; Mk. 10:6-8; Lk. 11:51; 17:26, 28, 32; Mdo. 7:2-16 ; Rum. 4:3; 17-18; 9:7, 9, 12; 1 Kor. 6:16; 15:45; Gal. 3:6, 8; 4:30; Efe. 5:31; 1 Tim. 2:13-14; Ebr. 4:4; 6:14; 11:3-32; 13:2; Yak. 2:3; 1 Pet. 3:6, 20; 2 Pet. 2:6; 1 Yoh. 3:12; Yud. 11, 14.

Orodha hii haijakamilika kamwe na zoezi muhimu sana ni kukamilisha orodha hii kwa kusoma Agano la Kale ukiwa na hayo katika fikira.

 

Uchambuzi

MAONI YA KIDARUBINI

Itakuwa muhimu kuwa na maoni ya kidarubini na ya kimaikroskopu ya vitabu vya Biblia. Maoni ya kidarubini hutoa muhtasari wa kitabu kwa ujumla, yakiwezesha ujumbe uliyotolewa humo kuchukuliwa katika mtazamo mkubwa; maoni ya kimaikroskopu yataleta maana halisi ya maneno, virai na aya. Maoni ya kwanza yatatoa usuli na mazingira ya kweli; ya pili yanajaza kwa kina na undani.

Kwa hivyo, tutaanza na uchambuzi wa ujumla, halafu, kwa mazingira hayo, ufafanuzi wa kina.

Twachukua kitabu cha Mwanzo katika kwa muhtasari, hivi:

 

MWANZO: KITABU CHA MIANZO

1 — HISTORIA YA AWALI KABISA — Sura ya 1-11. Matukio Manne Muhimu:

(1) —UUMBAJI: Utukufu wa Uungu katika Uumbaji wa Kiasili - Sura ya 1:1-2:3

(2) — USHUKAJI: Mamlaka ya Uungu katika Kutoa Adhabu - Sura ya 2:4-5:32

(3) — GHARIKA: Hukumu ya Uungu Yaonyesha Wema na Ukali - Sura ya 6:1-9:28

(4) —CHAFUO LA USEMI: Hekima ya Uungu katika Utekelezaji wa Madhumuni ya Mungu - Sura ya 10:1-11:26

 

2 _ HISTORIA YA UBABA — Sura za 11:27-50:26 Sura za 11:27-50:26 Watu Wanne Mashuhuri:(1 )_ IBRAHAMU: Mwito wa Mungu

Sura 11:27-25:10

(2) — ISAKA: Uzazi wa Uungu

Sura 25:11-27:46

(3) —YAKOBO: Utunzaji wa Uungu

Sura 28:1-35:29

(4) _YUSUFU: Madaraka ya Uungu

Sura 37:1-50:26

 

Aidha katika uchambuzi wa hapo juu unaojenga kitabu hiki kuhusiana na matukio muhimu, na watu wanne muhimu, kuna mgawanyiko wa kitabu hiki katika sehemu kumi na mbili kama ifuatavyo:

 

MWANZO: KITABU CHA NASABA

1. Utangulizi - Sura 1:1-2:3

2. Vizazi vya Mbingu na Nchi (Sheria, Dhambi, Mauti na ahadi ya Ukombozi) Sura 2:4-26

3. . Kitabu cha Vizazi vya Adamu (Maendeleo ya ya jamii ya binadamu) Sura 5:1-6:8

4. Vizazi vya Noa, mtu wa haki (Hukumu ya ulimwengu wa zamani, na utunzaji wa mabaki) Sura 6:9-9:29

5. Vizazi vya wana wa Noa (Maendeleo ya mataifa) Sura 10:1-11:9

6. Vizazi vya Shemu (Utengano wa watu kwa ajili ya Jina) Sura 11:10-26

7. Vizazi vya Tera (Mwito kutoka kwa familia) Sura 11:27-25:11

8. Vizazi vya Ishmaeli (Utengano wa yale ya kiasili na yale ya kiroho) Sura 25:12-18

9. Vizazi vya Isaka (Maendeleo ya Mbegu ya Ahadi) Sura 25:19-35:29

10. Vizazi vya Esau (Maendeleo ya Mtu wa Dhambi) Sura 36:1-8

11. Vizazi vya wana wa Esau (Maendeleo ya Mbegu ya Nyoka) Sura 36:9-43

12. Vizazi vya Yakobo (Maendeleo ya Israeli) Sura 37:1-50:26

Katika mfumo wa chambuzi mbili zilizoainishwa hapo juu, twatoa muhtasari wa kina wa kitabu chote ambamo twaziunganisha zote mbili:

 

MWANZO: KITABU CHA MIANZO

SEHEMU YA KWANZA: HISTORIA YA AWALI KABISA — Sura za 1-11

 

1. UUMBAJI: Utufu wa Mungu katika Uumbaji wa Asili — S 1:1-2:3 (Utangulizi wa Vizazi Kumi na Kimoja)Dunia wakati wa mwanzo

Sura 1:1-2

Kazi ya siku sita za kwanza

aya za 3-25

Kuumbwa kwa mtu na Agano la Mungu

aya za 26-28

Muhtasari wa Uumbaji — vyote " ni vyema sana "

aya za 29-31

Pumziko la siku ya saba

Sura 2:1-3

 

2. USHUKAJI: Mamlaka ya Mungu katika Kutoa Adhabu— Sura 2:4-5:31 Vizazi vya Mbingu na Nchi

(Sheria, Dhambi, Mauti na Ahadi ya Ukombozi) — Sura 2:4-4:26(a) Binadamu Chini ya SheriaBinadamu kabla ya Ushukaji

aya za 4-7

Bustani yaanzishwa Edeni

aya za 8-14

Binadamu aletwa chini ya Sheria

aya za 15-17

Ndoa ya kwanza

aya za 18-25

(b) Ushukaji Na Matumaini Ya UkomboziMajaribu na dhambi

Sura 3:1-7

Uchunguzi wa chanzo

aya za 8-13

Hukumu, adhabu, na matumaini

aya za 14-19

Matumaini ya ukombozi yaonyeshwa

aya za 20-24

Ibada yaa Kaini na Habili

Sura 4:1-4

Mauaji ya kwanza

aya za 5-8

Adhabu ya Kaini

aya za 9-12

Ulinzi wa Kaini

aya za 13-15

Maendeleo ya ukoo wa Kaini

aya za 16-24

Uteuzi wa Sethi mahali pa Habili

aya za 25-26

 

Kitabu Cha Vizazi Vya Adamu

(Maendeleo ya ukoo wa binadamu: ushindi wa dhambi na mauti) — Sura 5:1-6:8)

Binadamu hufa na hatima yake ni kaburi - aya 1-32

 

3. GHARIKA: Adhabu ya Mungu katika dhihirisho la uzuri na ukali— Sura 6:1-9:28 Uasi wa Kabla ya Gharika - Sura 6:1-8

 

Vizazi Vya Noa Mtu wa Haki (Hukumu ya ulimwengu na utunzaji wa waliobaki — Sura 6:9-9:29)

(a) Kizazi Chaangamizwa Na Gharika — Ch. 6:9-9:17.Noa na familia yake

aya 9-10

Walioishi wakati mmoja na Noa

aya 11-13

Noa aamurishwa kujenga safina

aya 14-22

Aliyebaki duniani kuokolewa

Sura 7:1-9

Shughuli za Noa wakati wa Gharika

aya 10-24

Mafuriko yapungua

Sura 8:1-5

Ujumbe wa ndege

aya 6-12

Ulimwengu uliosafishwa

aya 13-19

Ahadi ya Mungu

aya 20-22

Utaratibu mpya

Sura 9:1-7

Agano na viumbe vyote

aya 8-17

 

(b) Dhambi katika Mwili Yasalia — Sura 9:18-29Dhambi ya Hamu

aya 18-27

Kifo cha Noa

aya 28-29

 

4. CHAFUO LA USEMI:

Hekima Ya Uungu Katika Utekelezaji Wa Madhumuni ya Mungu — Sura 10:1-11:26

Vizazi Vya Wana Wa Noa (Maendeleo ya mataifa) — Sura 10:1-11:9 Wazawa wa Yafethi - Sura 10:1-5Wazawa wa Hamu (Nimrodi Mjenzi wa Kwanza wa Falme)

aya 6-20

Wazawa wa Shemu

aya 21-32

Babeli na utawanyikaji wa watu

Sura 11:1-9

 

Vizaai vya Shemu (Mwito wa kuacha ukoo kwa ajili ya Jina) — Sura 11:10-26. Wazawa wa Abramu - aya 10-26

 

SEHEMU YA PILI: HISTORIA YA UBABA — Sura 11:27-50:26 - Watu Wanne Mashuhuri

 

1: MAISHA NA NYAKATI ZA IBRAHIMU — Mwito wa Mungu — Sura 11:27-25:10 Vizazi vya Tera (Mwito wa kuacha ukoo) — Sura 11:27-25:11.(a) Ibrahimu kama Mgeni na Msafiri — Sura 11:27-13:18Uzao wa Tera

aya 27-30

Mwito wa kwanza katika Uru

aya 31-32

Mwito wa pili katika Harani

Sura 12:1-3

Abramu na Lutu waingia Kanaani

aya 4-5

Ahadi yathibitishwa katika nchi

aya 6-9

Abramu katika nchi ya Misri

aya 10-20

Lutu amwacha Abramu

Sura 13:1-13

Abramu aahidiwa nchi milele

aya 14-18

 

(b) Har-Magedoni Yaashiriwa — Sura 14:1-24.Uvamizi wa muungano wa nchi za kaskazini

Sura 14:1-7

Lutu atwaliwa

aya 8-12

Abramu amwokoa Lutu

aya 13-16

Melkizedeki ambariki Abramu

aya 17-20

Wafuasi wa Abramu wagawana mali

aya 21-24

 

(c) Kuzaliwa kwa Ishmaeli: Mbegu ya Mwili — Sura15:1-16:16.6 6 Abramu aahidiwa mbegu ya halaiki

Sura 15:1-6

Abramu aahidiwa kizazi chake kitaiingia nchi

aya 7-16 6

Mipaka ya nchi ya ahadi yafafanuliwa

aya 17-21

Abramu amwoa Hajiri

Sura 16:1-3

Hajiri amdunisha Sarai

aya 4-6

Hajiri apata msaada wa Mungu uhamishoni

aya 7-14

Hajiri arejeshwa na kumzaa Ishmaeli

aya 15-16

 

(d) Ahadi ya Isaka: Mbegu ya Agano — Sura 17:1-18:15.Jina Abramu labadilishwa kuwa Ibrahimu

Sura 17:1-8

Tohara yateuliwa kuwa ishara ya Agano

aya 9-14

Jina Sarai labadilishaw kuwa Sara

aya 15-16

Kuzaliwa kwa Isaka kwaahidiwa

aya 17-22

Ibrahimu na wanaume wote wa nyumba yake watahiriwa

aya 23-27

Ibrahimu awakaribisha malaika bila ya kujua

aya 18:1-8

 

Kutoamini kwa Sara kwa ahadi ya mwana wa kiume - aya 9-15

(e) Usiku wa Mwisho wa Kutisha Katika Sodoma — Sura 18:16-19:38.Ibrahimu aambiwa juu ya hukumu inayokuja Sodoma

aya 16-21

Ibrahimu awatetea wenye haki Sodoma

aya 22-23

Malaika wazuru jioni

Sura 19:1-3

Uovu uliokithiri usiku unapopasha

aya 4-11

Woga usiku

aya 12-14

Kutoroka alfajiri

aya 15-22

Uharibifu asubuhi

aya 23-29

Wapata mimba ya Moabu na Benami kwa baba mzazi

aya 30-38

 

(f) Abraham awaombea watu wa mataifa mengine — Sura 20:1-18.Abimeleki amtwaa Sara

Sura 20:1-2

Abimeleki aonywa na Mungu asimguse Sara

aya 3-8

Abimeleki ajitetea

aya 9-13

Zawadi ya Abimeleki kwa Ibrahimu

aya 14-16

Marejesho ya Abimeleki

aya 17-18

 

(g) _ Kuzaliwa kwa Isaka — Sura 21:1-34.Furaha ya Sara kumzaa Isaka

Sura 21:1-7

Sara amwachisha Isaka kunyonya, amdhihaki Ishmaeli

aya 8-9

Hasira ya Sara baadaya kumdhihaki Ishmaeli

aya 10-11

Ishmaeli afukuzwa lakini alindwa na Mungu

aya 12-13

Dhiki ya kukata tamaa ya Ishmaeli

aya 14-16

Ishmaeli aokolewa na Mungu

aya 17-21

Ibrahimu na Isaka wanyanyaswa na Wafilisti

aya 22-26

Maridhiano katika Kisima cha Agano

aya 27-32

Ibrahimu Katika Beer-sheba

aya 33-34

 

(h) Isaka kama Sadaka — Sura 22:1-19Ibrahimu ajaribiwa na Mungu

Sura. 22:1-5

Isaka akubali kutolewa sadaka

aya 6-8

Imani yashinda

aya 9-14

Ahadi zadhibitishwa

aya 15-19

 

(i) Kifo na mazishi ya Sara — Sura 22:20-23:20.Uhusiano wa Ibrahimu na Harani

aya 20-24

Umri na kifo cha Sara

Sura 23:1-2

Ununuzi wa mahali pa kumzika Sara

aya 3-18

Mazishi ya Sara

aya 19-20

 

(j) Mke kwa Isaka — Sura 24:1-67.Tume

Sura 24:1-6

Imani katika mwongozo wa Mungu

aya 7-9

Sala kwa sababu ya mafanikio

aya 10-14

Haiba ya Rebeka ya sura na ya tabia

aya 15-16

Jibu la Rebeka kwa ombi

aya 17-21

Tuzo la Rebeka

aya 22-25

Asante kwa Mungu kwa baraka

aya 26-27

Jamaa wa Rebeka wafurahiwa

aya 28-31

Eliezeri anatangaza ujumbe wake

aya 32-49

Rebeka anunuliwa kwa bei

aya 50-53

Eliezeri ana wasiwasi wa kurudi

aya 54-56

Safari ya Rebaka nchini

aya 57-61

Rebeka akutana na Isaka

aya 62-65

Ndoa

aya 66-67

 

(k) Kifo cha Ibrahimu — Sura 25:1-11.Familia yake na Ketura

Sura 25:1-4

Upendeleo wake kwa Isaka

aya 5-6

Kifo na mazishi

aya 7-10

 

2. MAISHA NA NYAKATI ZA ISAKA: Uzazi wa Uungu — Sura 25:11-27:46.

Isaka mbarikiwa wa Mungu - Sura 25:11

 

Vizazi vya ishmaeli:

Kutenganisha mbegu ya asili na mbegu ya kiroho— Sura 25:12-18.

Uzao wa Ishmaeli, urithi na kifo - aya 12-18

 

Vizazi vya Isaka: Maendeleo ya mbegu ya ahadi — Sura 25:19-35:29.(a) Yakobo Apata baraka — Sura 25:19-27:46.Utabiri na uzazi wa Esau na Yakobo

aya 19-24

Sifa za Esau na Yakobo

aya 25-27

Mvurugano katika nyumba

aya 28

Esau auza haki yake ya kuzaliwa

aya 29-34

Matatizo ya Isaka katika nchi

Sura 26:1-5

Udanganyifu wa Isaka kuhusu mkewe

aya. 6-11

Mafanikio ya Isaka

aya 12-16

Isaka anyanyaswa na Wafilisti

aya 17-22

Isaka ahamasishwa na maono katika Beer-Sheba

aya. 23-25

Wafilisti wanyenyekea Isaka

aya 26-31

Uanzishaji wa Kisima cha Agano

aya 32-33

Ndoa za Esau zawahuzunisha wazazi wake

aya 34-35

Isaka aandaa kumbariki mzaliwa wake wa kwanza

Sura 27:1-4

Njama ya Rebeka

aya 5-10

Udanganyifu wa Yakobo

aya 11-25

Braraka yatolewa

aya 26-29

Udanganyifu wagunduliwa

aya 30-33

Manung'uniko ya Esau na tuzo

aya 34-40

Rebeka amhimiza Yakobo aitoroke chuki ya Esau

aya 41-46

 

3. MAISHA NA NYAKATI ZA YAKOBO: Utunzaji wa Mungu — Sura za 28:1-36:43. Vizazi vya Isaka

(b) — Familia ya Yakobo nchini Harani — Sura 28:1-30:43.Isaka amtuma Yakobo Padan-aramu

Sura 28:1-5

Esau amwoa binti ya Ishmaeli

aya 6-9

Maono yaYakobo katika Betheli

aya 10-15

Majibu ya Yakobo na nadhiri

aya 16-22

Yakobo katika kisima cha Harani

Sura 29:1-8

Yakobo akutana na Raheli na Labani

aya 9-14

Yakobo amtumikia Labani ili ampate Raheli

aya 15-20

Yakobo adanganywa na kuozwa Lea

aya 21-25

Yakobo amtumikia Labani tena ili ampate Raheli

aya 26-30

Kuzaliwa kwa Reubeni,Simeon, Lawi naYuda (Lea)

aya 31-35

Kuzaliwa kwa Dani na Naftali (Bilha — mjakazi wa Raheli)

Sura 30:1-8

Kuzaliwa kwa Gadi na Asheri (Zilpa — mjakazi wa Lea)

aya 9-13

Kuzaliwa kwa Isakari, Zabuloni na Dina (Lea)

aya 14-21

Kuzaliwa kwa Yusufu (Raheli)

aya 22-24

Yakobo ajadili mshara kwa mbuzi na kondoo

aya 25-36

Kuongezeka kwa ufanisi wa yakobo

aya 37-43

 

(c) Yakobo Arudi Kwa Nchi Ya Agano — Sura 31:1-33:20.Yakobo apanga kuondoka kisiri

Sura 31:1-18

Raheli aiba vinyago vya babake

aya 19-21

Labani awafuata

aya 22-24

Laban amkemea Yakobo lanini hakuvipata vinyago

aya 25-35

Yakobo amkashifu Labani kwa ukali wake

aya 36-42

Agano baina ya Yakobo na Labani

aya 43-55

Maono ya Yakobo Mahanaimu

Sura 32:1-2

Ujumbe wa Yakobo kwa Esau

aya 3-5

Uwoga wa Yakobo kwa Esau

aya 6-8

Ombi la Yakobo la msaada

aya 9-12

Tahadhari ya Yakobo

aya 13-23

Yakobo amenyana na malaika

aya 24-32

Yakobo na Esau wapatana

Sura 33:1-11

Yakobo hamwamini Esau

aya 12-16

Yakobo ajenga madhabahu Shekemu

aya 17-20

 

(d) Yakobo Kama Msafiri Katika Nchi — Sura 34:1-36:43.Dina abikiriwa

Sura 34:1-6

Shekemu apendekezewa amani kwa masharti

aya 7-19

Shekemu akubali masharti

aya 20-24

Udanganyifu wa Simeoni na Levi

aya 25-29

Karipio la Yakobo

aya 30-31

Mungu amtuma Yakobo Betheli

Sura 35:1-6

Kifo cha Debora, mlezi wa Rebeka

aya 7-8

Yakobo abarikiwa na Mungu

aya 9-15

Kuzaliwa kwa Benyamini; kifo cha Raheli

aya 16-20

Uovu wa Reubeni; Muhtasari wa familia Yakobo

aya 21-26

Kifo cha Isaka

aya 27-29

 

Vizazi vya Esau:

[1] Udhihirisho wa mtu wa Dhambi — Sura 36:1-8.Wake na familia za Esau

aya 1-5

Esau autawala Mlima Seiri

aya 6-8

 

[2] Uenezi wa mtu wa Dhambi (Baba wa Waedomu) — Sura 36:9-43.Wana wa kiume wa Esau

aya 9-14

Majumbe wao wana wa Esau

aya 15-19

Wana wa kiume na Majumbe wa Seiri Mhori

aya 20

Wafalme na Majumbe wa Edomu

aya 21-43

 

4. MAISHA NA NYAKATI ZA YUSUFU: Madaraka ya Uungu — Sura 37:1-50:26 Vizazi vya Yakobo —Uhifadhi na Maendeleo ya Israeli — Sura 37:1-50:26.(a) Ujana wa Yusufu — Sura 37:1-36.Yusufu alimpenda baba yake — aliwachukia nduguze

aya 1-4

Ndoto za Yusufu

aya 5-11

Yusufu awatafuta nduguze Shekemu

aya 12-14

Yusufu awapata nduguze Dothani

aya 15-17

Yusufu atupwa katika shimo

aya 18-24

Yusufu auzwa kwa Waishmaeli

aya 25-28

Huzuni ya Yakobo

aya 29-35

Yusufu auzwa kwa Potifa

aya 36

 

(b) Kuzaliwa Peresi: Mtangulizi wa Yesu — Sura 38:1-30.Yuda awazaa Eri, Onani na Shela

Sura 38:1-5

Eri amwoa Tamari

aya 6

Hukumu ya kifo kwa Eri ana Onani

aya 7

Yuda amwahidia Shela Tamari

aya 8-11

Mbinu za Tamari za kumpata mumewe

aya 12-23

Yuda amwondolea Tamari lawama

aya 24-26

Tamari awazaa Peresi na Zera

aya 27-30

 

(c) Madaraka ya Yusufu Misri — Sura 39:1-41:57Yusufu afanywa mwangalizi katika nyumba ya Potifa

Sura 39:1-6

Uadilifu wa Yusufu katika majaribu

aya 7-12

Mashtaka ya uongo ya uasherati dhidi ya Yusufu

aya 13-18

Yusufu afungwa jela

aya 19-20

Mungu Amfanikisha Yusufu gerezani

aya 21-23

Mnyweshaji na Mwokaji wa Farao wafungwa jela

Sura 40:1-4

Ndoto zao zatafsiriwa na Yusufu

aya 5-19

Tafsiri ya Yusufu yadhihirika

aya 20-22

Mnyweshaji wa Farao amsahau Yusufu

aya 23

Ndoto mbili za Farao

Sura 41:1-8

Mnyweshaji wa Farao ampendekeza Yusufu kwa Farao

aya 9-13

Yusufu mbele ya Farao

aya 14-24

Yusufu atafsiri ndoto

aya 25-32

Yusufu apendekeza sera ya kitaifa

aya 33-36

Yusufu afanya waziri mkuu

aya 37-40

Mamlaka ya Yusufu na ndoa

aya 41-45

Umri wa Yusufu, utawala na familia

aya 46-52

Miaka ya shibe yafuatwa na miaka ya njaa

aya 53-57

 

(d) Nduguze Yusufu Wanyenyekea Mbele Yake — Sura 42:1-45:15.Ndugu zake Yusufu watumwa kununua nafaka Misri

Sura 42:1-5

Watiwa gerezani eti ni wapelelezi

aya 6-17

Waachiliwa kwa masharti kuwa warudi na Benyamini

aya 18-28

Hofu kubwa ya Yakobo

aya 29-38

Yuda ajitolea kuwa mdhamana wa Benyamini

Sura 43:1-14

Uwoga wa ndugu za Yusufu kwake

aya 15-25

Yusufu awaburudisha nduguze

aya 26-34

Mpango wa Yusufu kuwachelewesha nduguze

Sura 44:1-13

Yuda amsihi Yusufu kumwachilia Benyamini

aya 14-34

Yusufu ajitambulisha kwa ndugu zake

Sura 45:1-15

 

(e) Siku Za Mwisho Za Yakobo — Sura 45:16-50:13.Mwaliko wa kuishi Misri

aya 16-24

Furaha ya Yakobo

aya 25-28

Kuhamia Misri

Sura 46:1-7

Uzao wa Yakobo

aya 8-27

Yakobo akutana na Yusufu

aya 28-34

Yakobo aletwa mbele ya Farao

Sura 47:1-10

Yakobo apewa ardhi ncini Misri

aya 11-12

Wamisri wafanywa watumwa wa Farao

aya 13-21

Mashamba ya makuhani hayakutwaliwa

aya 22-26

Uzao wa Israeli waongezeka Misri

aya 27-28

Amri ya Israeli kuhusu mazishi yake

aya 29-31

Yakobo akumbuka baraka za mungu kwake

Sura 48:1-4

Yakobo awatwaa wanawe Yusufu

aya 5-7

Efraimu apata haki ya kuzaliwa

aya 8-14

Baraka kwa Yusufu

aya 15-16

Hali ya Kuzaliwa yadhibitishwa

aya 17-22

Yakobo atoa baraka katka Siku za Mwisho

Sura. 49:1-28

Yakobo atoa amri kuhusu mazishi yake

aya 29-32

Kifo cha Yakobo

aya 33

Wamwomboleza Yakobo

Sura 50:1-6

Mazishi ya yakobo

aya 7-13

 

(f) Siku Za Mwisho Za Yusufu — Ch. 50:14-26.Yusufu awaliwaza ndugu zake

aya 14-21

Maisha marefu ya Yusufu

aya 22-23

Kifo na ujumbe wa mwisho wa Yusufu

aya 24-26

 

Riwaya juu ya Elohim

Neno la Kiyahudi la Mungu katika Mwanzo 1 ni Elohim. Linatokea mara nyingi kote katika Maandiko. Katika Phanerosis , Ndugu Thomas asema: Wingi wa neno hili (yaani Eloahh) ni Elohim, na lapatikana mara 2,470 katika Agano La Kale. Katika Sura za kwanza na ya pili za Mwanzo, limewakilishwa katika Biblia ya Kiingereza na neno 'God' (Mungu); lakini katika Sura ya 3:5, limetafsiriwa kama 'gods' (miungu). Katika Sura ya 23:6 limetolewa kama 'mighty' (-enye nguvu) lakini kimakosa kabisa. Katika Sura ya 30:8 limeandikwa 'great' (-kubwa). Katika 31:30,32: 35:2,4, na kwingineko kwingi, sanamu zimeitwa elohim, sio kwa kuwa zilikuwa na nguvu yoyote, bali kwa sababu ziliheshimiwa na waabudu sanamu walioziita vile. Katika Kutoka 21:6; 22:8-9 linaitwa 'judges' (majaji). Katika 1Sam. 2:25, ni 'judge' (jaji). Katika 1 Wafalme 11:5, limetafsiriwa kama 'goddess' (mungu wa kike). Katika Jona 3:3, limetolewa kama 'exceeding' (kupita kiasi); na katika Mal. 2:15, limetafsiriwa kama 'godly' ( - ki-mungu). (Phanerosis uk. 51,52).

Katika Elpis Israel (p. 181-183), vipengele vifuatavyo vyasisitizwa: "Kanuni za sarufi zilizokubaliwa zahitaji kwa ujumla kuwa 'kitenzi kikubaliane na uhusiano usiobadilika (nominative) katika nambari na nafsi; mfano, roho hutembea, maji hunguruma. Hapa, roho ni nambari ya umoja, na nafsi ya tatu; na kitenzi hutembea pia; hivyo zakubaliana na nambari na nafsi; 'maji' (waters) ni ya nafsi ya tatu wingi, na 'hunguruma' pia; kwa hivyo zakubaliana. Lakini katika katika Sura ya kwanza ya Mwanzo, kanuni hii haizingatiwi na Roho, ambye alimwongoza Musa kuandika. Katika aya ya kwanza inasema, Berayshith bara Elohim; hivyo ni Hapo mwanzo Elohim aliumba. Katika sentensi hii bora ni kitenzi katika nafsi ya tatu umoja, na Elohim ni nomino (jina) katika nafsi ya tatu wingi; hivi kwamba havikubaliani kama kulingana na kanuni. Kwa ukubaliano kupatikana, ama nomino yastahili kuwa Eloa, au El, katika umoja, ama ibaki kama ilivyo katika wingi na kitenzi kibadilike kuwa barau: kama barau ELOAHIM (wao) waliumba. lakini haisimami hivi: inasoma hivi: (yeye) Eloahim (yeye) aliumba.

"Akizungumzia Elohim, Dkt. Eilson anasema 'Nomino hii, ambayo bila kukusudia yaunganishwa na kitenzi cha umoja bora, hata hivyo ni wingi, yaonekana sio tu kwa kiambishi im lakini pia kwa kuunganishwa mara kwa mara na vivumishi, viwakilishi nomino, na vitenzi katika wingi. Vayyomer Elohim nashah adam betzalmainu, hiyo ni, Elohim akasema, 'Na tumfanye mtu kwa mfano wetu'."

Bwana Parkhurst, katika msamiati wake chini ya neno alah, anukuu vifungu vingi ambapo Eloahim linahusishwa na wingi (plurals) mara nyingi. Kwa uchunguzi wa kina haikutapatikana sababu nzuri kamili ya kupinga hitimisho kuwa Eloahim ni nomino ya wingi (noun plural) na yamaanisha 'miungu'.

" Kanuni ya kwanza yangu kwa malumbano yote ya jambo hili ni, kwamba 'Kuna Mungu Mmoja na Baba kwa wote, ambaye ni mkuu kwa wote, kupitia wote, na yote' familia Yake ya kiroho. Msemo mwingine ni, kwamba 'Yeye ni mbarikiwa na Mtawala pekee, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana; Ambaye peke yake huishi milele, akikaa katika nuru ambayo hakuna mtu anayeweza kuikaribia; AMBAYE HAKUNA MTU ALIYEMWONA, wala hakuna anayeweza kumwona" (1 Tim. 6:15; 1:17). Na tena, "Mungu ni roho" (Yn. 4:24); hana uharibifu (Rum 1:23). ROHO ASIYE MHARIBIFU ANAYEKAA KATIKA MWANGA ni ufunuo wa Kibiblia wa sifa zisizoelezeka za kuishi kibinafsi kwa Yule wa Milele, ambaye ametoka kwa Mungu anayeishi milele na milele. Vipengele vya sifa Zake, Hajafichua; Ametujulisha jina Lake, ama tabia, ambavyo ni muhimu kwa binadamu kujua; lakini kusema eti kwa kuwa Yeye ni roho, kwa hivyo "hafai", ni kuongea upuzi mtupu; kwa kuwa kisicho na umuhimu si kitu; sifa, kama twaweza sema, ambayo ni geni kwa ulimwengu wa Mungu.

"'Hakuna mtu,' asema Yesu, 'ashawahi muona Mungu wakati wowote'; lakini Adamu, Ibrahimu, Yakobo na Musa walimwona Elohim na Bwana wao; kwa hivyo, Elohim halimaanishi "Mungu wa Milele" Mwenyewe.

"Elohim ni jina lililopewa malaika na vikundi vya wanaume. Imeandikwa 'Msujuduni yeye, enyi nyote Elohim' (Zab. 97:7). Hii imenukuliwa na Paulo katika Sura ya kwanza ya Waebrania, kama amri ya Mungu wa Milele kwa malaika, kwamba sharti waonyeshe heshima kwa Bwana Yesu kama Mwana Wake, wakati atakapomtambulisha kwa dunia tena katika ufunguzi wa Nyakati za Baadaye. Imeandikwa pia kumhusu, ' Umemfanya mdogo punde kuliko Eloahim' (Zab. 8:5). Paulo atumia haya kumhusu Yesu akisema, ' Twamwona Yesu, aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika' (Ebr. 2:9). Aliendelea na hali hiyo duni hadi baada ya miaka thelathini, kutoka kuzaliwa kwa mwili hadi ufufuko wake; alipoenziwa juu zaidi yao katika cheo na hadhi, hata kwa 'madaraka ya mkono wa kuume', ambapo ni kuenziwa katika mwanga, anakoishi kwa Utukufu katika mbingu." Kutokana na hayo ya juu tunahitimisha ya kuwa jina Elohim latumika kumaanisha malaika; linaashiria "wenye nguvu" ambao kupitia kwao Mungu Alijidhihirisha.

Kulingana na Dkt. Strong, jina hili limetolewa kwa kina uwl maana yake "kusokota" (kama kuviringisha pamoja), kwa hivyo kuwa na nguvu. Ufafanuzi huu unapendekeza ya kwamba, Elohim ni wingi na pia umoja; wingi ikiashiria msururu wa viumbe; na umoja ikimaanisha kundi la viumbe wakiunganika kama kitu kimoja.

Davidson, katika Analytical Hebrew and Chaldee Lexicon alinganisha neno hili na neno Alah, la Kiarabu, ambalo mzizi wake ni alaha, "kuheshimu, kupenda, kuabudu, kuogopa."

Parkhurst alitoa katika mzizi wa Kiyahudi, alah, "aliapa, ama alijizingira na kiapo". Hii, tena, inapendekeza idadi fulani iliyounganika kuwa sehemu moja.

Neno hili laonekana mara 2,470, na linahusiana na El, nguvu, uwezo; lakini likiwa kwa wingi (ikiashiriwa na kiambishi im), linamaanisha "wenye nguvu".

Ni jina linapewa malaika ambao ni wenye nguvu wanayopewa na Yehova ili kuwa hivyo.

Linatumiwa kwa wanaume (Kut. 7:1; 15:11; 1 Sam. 28:13-14; Zab. 45:6-7; 82:1,6; 97:7,9; 136:2— taz. Yon. 10:33-35); limetafsiriwa "hakimu" (Kut. 21:6; 22:8-9; 1 Sam. 2:25); "miungu" (Mwa. 3:5; Kut. 32:8,23,31; Kum. 10:17); "malaika" (Zab. 8:5; taz. Amu. 13:21-22) nk. Kwa hivyo matumizi yake, kuhusiana na Bwana, hayakubaliani na mafunzo ya Utatu; kwani hata kama Yesu aliitwa "Mungu" (Yn. 20:28), hata na Musa pia (Kut. 7:1). Bwana mwenyewe alieleza kwa kina umuhimu wa neno hili, akiashiria kuwa Maandiko ya Agano la Kale yalimhusu binadamu (Yn. 10:33-35).

Ingawa Elohim li katika wingi na linaashiria "wenye nguvu", linatumika mara nyingi na kitenzi katika umoja kama ilivyo katika Mwanzo 1:1. Hii inamaanisha kuwa Eloahim, ingawa wanajumuisha idadi kubwa ya watu wasiokufa, wanapewa motisha nguvu moja, "Roho wa Mungu" (Mwa. 1:2). Eloakim, kwa hivyo, kundi kubwa lililounganika kama moja, na kutii kwa pamoja nguvu ya uhamasisho ya Mkuu Asiyeumbwa. Mwimbaji wa Zaburi alitangaza: "Yehova ameweka kiti Chake cha enzi mbinguni; Na ufalme Wake unavitawala vitu vyote. Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno Lake. Mhimidini Bwana, enyi majeshi yake yote, Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake. Mhimidini Bwana, enyi matendo yake yote, Mahali pote pa milki yake. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana." (Zab. 103:19-22).

Yehova ni Roho (John 4:24), na malaika Wake ni pepo (Zab. 104:4; Ebr. 1:7). Wao ni "familia Yake mbinguni" (Efe. 3:15), wakiwa walitoka Kwake, na kwa kufanya mapenzi Yake kupitia kwa Roho Wake aliye kila mahali. (Mwa. 1:2). Kwa hivyo wanafanya kazi kama kundi moja, ingawa idadi yao haihesabiki.

Katika sehemu nyingi, hata hivyo, Eloahim linatumika na kitenzi cha wingi (Mwa. 1:26; 3:22; 11:7; Isa. 6:8 —kulingana na Parkhurst, pia katika Mwa. 20:13; 31:7,53; 35:7; Kum. 4:7; Yos. 24:19; 2Sam. 7:23; Yer. 10:10; 23:36). Matumizi ya vitenzi vya umoja na vitenzi vya wingi kuhusiana na nomino hii ya wingi yaonyesha kuwa ingawa Eloahim ni wengi, na waliounganika kama kitu kimoja, wana uwezo pia wa kufanya uamuzi na kitendo huru.

Hata hivyo, nguvu wanayotumia, na utukufu wanaouonyesha, vyote vyatoka mahali pamoja: hata Yehova. Tazama Ayubu 38:7

 

FUNDISHO KWETU.

Wasomi wengi wamejaribu kukanusha uhalisi wa Mwanzo. Hili ni jaribio bure kama vile mageuzi kujaribu kuepuka wajibu kwa Mungu Mwenye nguvu, Mjua yote, ambaye Yuko kila mahali.

Twastahili kusoma Mwanzo katika maana yake halisi lakini pia twangalie matumizi ya sifa, mfano, istiara, mafumbo, methali, unabii na kadhalika. Mara kwa mara, maelezo ya Maandiko yana maana ya kawaida na pia umuhimu wake halisi, na hivi ndivyo Mwanzo kilivyo.

Mwanzo kinajumuisha kitalu ambamo Biblia nzima iliota. Yote yanayoelezwa katika vitabu vingine yana mwanzo wake kitabuni humu. Maswala mengi changamani yapatikana hapa katika hali ya kiinitete. Upatanisho waonekana kufichika katika sura za awali; Har-Magedoni imepigwa chapa katika uvamizi wa Kedorlaoma (sura ya 14); maendeleo ya baadaye ya historia na uhusiano wa Mungu na watu na mataifa yameelezwa kwa mfano (Wagalatia 4:24-31); mafunzo ya kimsingi ya Injili yameanikwa humo. Hakika ni salama kusema ya kuwa ni vigumu kung'amua vizuri makusudio ya Mungu pasipo kuelewa kiasi kitabu cha Mwanzo.

Unaanza kuelewa kitabu chochote kwa kuanza kwa jalada la mbele na kukichambua mpaka nyuma. Vivyo hivyo na Biblia. Kuelewa kwetu kunaanza na kusoma Mwanzo, na tutakuwa tumekomaa tunapoelewa vitabu vyote hadi kufikia Ufunuo.

Agano la Kale liliandikwa hasa kwa Kiyahudi, na mara nyingi ni muhimu kutambua neno halisi lililotumiwa mwanzo ili kuelewa fungu kikamilifu. Ni nadra kwa mwanafunzi kuelewa kiyahudi, kwa hivyo vifaa kama vile concordance na lexicon ni vya umuhimu si haba. Hata hivyo mwanfunzi wa Biblia mwenye bidii ataihakiki lugha angalau kidogo.

MAKTABA ZA MAREJEO

Genesis Expositor - HP Mansfield

Elpis Israel - John Thomas

Lexicon - Parkhurst

Concordance - Strong

 

MASWALI YA IBARA:

  1. Nini maana ya neno Pentateuch?

  2. Nani aliyeandika Mwanzo?

  3. Nani aliyeandika kuhusu kifo cha Musa?

  4. Nini umuhimu wa kiroho wa nambari tano katika Maandiko?

  5. Ibara ya mwisho ya kitabu cha Mwanzo ni ipi?

 

MASWALI MEPESI

  1. Andika muhtasari wa sehemu kuu za Mwanzo

  2. Mbona Mwanzo yaitwa kitalu?

  3. Eleza matumizi ya kibiblia ya neno Elohim

 

English files: