MWANZO - Sura ya Kwanza

 

2. MWANZO - Sura ya Kwanza.

"Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia."

 

MPANGILIO KUTOKA KWA ZAHAMA

(Sura ya 1:1-2:3)

Kwa ufupi na haiba ya utenzi, taarifa ya uumbaji ya Mwanzo haina kifani.Inaeleza kwa maneno machache ya kusisimua, matendo ya Mungu ya kuleta mpangilio kulikokuwa na zahama awali. Inasiszitiza funzo muhimu kuwa ilikuwa kwa "Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake" (Zaburi 33:6); kwa kuwa ni kwa neno hilo hilo ambapo "kiumbe kipya" kadhalika kilitiwa sura (Ufunuo 3:14). Hivyo kuzaliwa upya kimaumbile kwa dunia kumeelezwa katika maandiko kama mfano wa kuzaliwa upya kwa mtu kimaadili kwa nguvu za Injili.

Mungu Muumba atawala hapo ambapo dunia ya giza yaangazwa kwanza na hatimaye kujazwa uhai. Nguvu na utukufu zakita katika kila sentensi viumbe vya hali ya juu vinapojitokeza; hadi kilele kinapofikiwa na uumbaji wa mtu "kwa mfano na sura ya Mungu". Na basi hatima ya mtu ilinenwa katika tangazo: "Mkatawale..."

Iwapo swali lingeulizwa "Mungu aliumba lini?" jibu ni "Hapo mwanzo" (Mwa. 1:1); iwapo itaulizwa jinsi gani Aliumba? jibu ni kwa uwezo wa Roho Wake (Mwa. 1:2-3); ingeulizwa kwa sababu gani Aliumba? twaambiwa ya kuwa ilikuwa ni kujaza ulimwengu na uhai (Isa. 45:18), ambapo ingeonyesha kwa utukufu Wake."Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa" (Ufu. 4:11). Ingawa maneno haya yanahusu "uumbaji mpya" wa baadaye, kadhalika yanahusu uumbaji wa kimwili wa awali.

Kila kitu kilifanywa kwa hekima (Mit. 8:22-24; 3:19; Zab. 136:5); kwa utukufu wa Yehova (Hes. 14:21; Mit. 16:4); na akiwa na mtazamo wa kusudi lake halisi (Isa.45:18; Yoh. 1:1-3). Hekima na nguvu zinazoonekana katika uumbaji wa asili zadhihirisha uwezo Wake kuokoa. (Zab.147: 3-4).Utukufu unaodhirika hapo ulikuwa chanzo cha kumfurahia Elohimu (Ayubu 38:4-12); na tunapoyatafakari haya, sisi pia tunajumuika na mwimbaji wa Zaburi kufurahi: " Ee Bwana, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa mali zako"(Zaburi 104:24); "Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi, Zitafakarini ajabu zake zote" Zaburi 105:2).

 

SURA YA KWANZA

UUMBAJI:

UTUKUFU WA MUNGU KATIKA UUMBAJI WA ASILI

"Hapo mwanzo Mungu"––Mungu ndiye nguvu ya kale ya vyumbe vyote; vyote vyatoka Kwake. Paulo alitangaza: ex an tou kai di autou, kai eis autou ta panta, "Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake" (Rum. 11:36; 1 Kor. 8:6). Kwa msingi wa haya, taarifa ifuatayo imefanywa: "Kiini ama kisima cha nguvu katika dunia ni kimoja. Ni kitengo kimoja. Kwa hivyo chochote kiishicho ni ex autou, Kutoka kwake Mungu. Maadamu, Muumba 'hakutengeneza vitu vyote kutoka kwa utupu'. " Hili ni fundisho la theolojia, theolojia ya Kanisa la Asili, ya Bwana Mzee wa Kimwili; na ambayo inaongoza wengi wa watoto wake kuthibitisha kwamba 'kifaa ni Mungu,' ufahamu wa 'kifaa' kinachotambulika na hisia tano za mwili.Hivyo jua, mwezi na nyota na vitu vyote wanavyoweza kuona, onja, hisi, nukia, na kusikia duniani ni Mungu. Wanakanganya kile ambacho "ni Chake Mungu" na "Yeye Mungu" ambaye kutoka Kwake vitu vyote huendela. Kwa upande mwingine wana wengine wa Bwana Mzee wanadhibitisha kuwa " Mungu si kitu " kwa hii wakiashiria kuwa Mungu si kitu, wala jambo ama mwili; lakini ni kitu kisichoeleweka kinaochoitwa 'roho',  kisicho na mwili, duni,  roho bure, kisiyokuwa na maana kabisa kadiri maneno yanavyoweza kuelezea. Lakini Maandiko matakatifu yanatangaza kuwa pneuma ho Theos esti, maana halisi, 'Roho ndio Theos'.  Nasema Theos tu kwa sababu tutahakikisha ung'amuzi wa Agano Jipya wa Theos. 'Roho', kwa hivyo, ni Theos anayeitwa Mungu. Zaidi ya haya, huyu Roho ni Baba, yaani,  Yule Mmoja ex autou ambaye vitu vyote vyatoka kwake" (Phanerosis pp. 53-54).

Maandiko Matakatifu, kwa hivyo, yanafundisha kuwa  Roho wa Mungu ndiye kiini cha vitu vyote; ni nishati ya nyuklia kwa viumbe vyote (Mith. 8:22). Kwa hivyo, hayo yote yalifanyika kwa malengo yake katika fikira, na siyo kwa nguvu pofu ama kwa ajali.

Siku Ya Kwanza: Nuru Yaja — aya 1-5 Nchi ilikuwa giza tupu, na nuru ilikuwa muhimu ili kudhihirisha kiwango cha kazi iliyohitajika. Hii kwa hivyo ikawa ni kazi ya siku ya kwanza. Ilitendeka "kwa neno la Mungu". Udhihirisho wa mwanga pia ni tendo la kwanza muhimu ili kuleta uumbaji wa kiroho wa Yehova kuwepo. Yohana alikuwa akirejelea haya aliposema " Hapo mwanzo kulikuwako Neno" na neno hilo lilimaanisha "mwanga wa binadamu" (Yohana 1:1-5). Matendo kumi ya uumbaji, yaliyonakiliwa katika aya za kwanza za Mwanzo, si ukweli wa kihistoria tu, bali ni malengo halisi ya kusudi la Mungu kwa binadamu.

AYA YA 1

"Hapo mwanzo" — Kiebrania kina neno moja, bereshith, likimaanisha "hapo mwanzo." Linasawirisha kichwa cha Mwanzo, na limetoKana na kiambishi, rosh, kumaanisha "kichwa", "mwanzo" na kadhalika. Wakati "mwanzo" huu ulikuja kuwa hatujaambiwa. Lakini tunafunzwa kuwa hekima ilibainika katika matendo ya uumbaji kutoka mwanzo. Yohana anasema " hapo mwanzo" kulikuwako Neno ama Logos (Yohana 1:1). Logos linaashiria usemi wa nje wa mawazo ya ndani au sababu. Linawakilisha zaidi ya neno tu, kwa maana linashirikisha mawazo yaliyo chini ya neno lililonyeshwa. Kwingineko, twajifunza kuwa hekima ilikuwa na Mungu hapo mwanzo, na ilidhihirishwa na matendo Yake.

Kwa hivyo, hapo mwanzo kulikuwa Mungu, na ndani ya Mungu kukatoka viumbe vyote, kwa kuwa Roho Wake ni chanzo cha yote hayo. Na hapo mwisho kutakuwa Mungu, akidhihiriswa katika dunia iliyoafikiwa, na rundo la viumbe walioafikiwa. Hii inafafanuliwa na Paulo katika maneno "Mungu awe yote katika wote" (1 Kor. 15:28). Katika mwanzo Mungu alisimama na utukufu na umaarufu, na mwishoni Atafanya vivyo hivyo.

Ni jinsi gani gani dunia na sayari zingine zilikuja kuwa katika uwepo? Sayansi ya mageuzi inadokeza kitu kimoja, na Maandiko Matakatifu jingine. Kulingana na sayansi, kuna nadharia mbili kuu: (1) kukaribia jua kwa sayari nyingine, ikisababisha kusogea mbali kwa sayari chipukizi; (2) Muungano wa jua na sayari zake kutoka kwa mvurugo wa gesi na vumbi. Sayansi ya mageuzi ingependa kumwondoa Mungu katika uumbaji, na kwa hivyo inatoa nadharia zinazopendekeza kwamba uwepo wa mbingu na ardhi ilikuwa bahati na wala sio uumbwaji.

Kwa upande mwingine, Maandiko Matakatifu husema juu ya kutengenezwa kwa mbingu na dunia kama tendo maalum la uumbaji (Isa. 45:8). "...Kwa maana aliamuru, vikaumbwa" (Zab. 148:5). "...Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya..." (Isa 45:18). Pamoja na maazimio kama haya, kuna matatizo ya kimsingi ambayo bado hayajatatuliwa na wanasayansi wa mageuzi. Kama nadharia zao zingekuwa za kweli, sayari zote zingekuwa zikifuata kanuni sawa lakini hazizifuati. Wanasayansi wa mageuzi wameshindwa kueleza ni kwa nini sayari saba kati ya nane zilizounganika na mfumo wa jua zina mzunguko wa moja kwa moja ukizingatia mzunguko wazo kwa jua, lakini Venus huzunguka polepole nyuma, hali Uranus huzunguka nyuzi 98 kutoka kwa kina cha mzunguko, ingawa mzunguko huegemea nje kidogo kuliko sayari nyingine yoyote. Kadhalika hawana jibu kwa shida za sayari zinazozunguka kinyumenyume. Kwa miezi thelathini na miwili ya mfumo wetu wa jua, kumi na mmoja huzunguka kinyume na mzunguko wa sayari sa kiasili.

Mbingu na nchi ziliumbwa wakati wa kipindi cha siku sita halisi zilizotajwa katika Mwanzo 1? Hakuna sababu ya kusema hivyo. Ni kweli Kutoka 20:11 inasema: "...kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo..." lakini kitenzi "fanya" (Kiyahudi asah), chaweza maanisha "teua" kama inavyoashiriwa katika Zaburi 104:19, na inaweza husiana na kuamuru kwa dunia, ambayo ilikuwa ingaliko kwa muda mrefu wa nyakati.

"Mungu aliumba" — Kwa Kiebrania ni bara Elohim: kitenzi katika idadi ya umoja pamoja na nomino ya wingi inaonyesha uwahamasisho wa nguvu moja ikijijitokeza kupitia msururu wa mawakala. Nguvu moja ya uhamasisho katika uumbaji ni "Roho wa Mungu" (aya ya 2) ama Yehova aliyefanya kazi kupitia malaika kusababisha uumbaji kuwepo.

"Uhusiano huu wa karibu, wa karibu sana jinsi ya kuashiria uwepo wa Umoja katika wingi (lakini sio wingi katika nguvu kamili za kiasili, kiini cha vyote) unaelezwa katika kitabu cha Isaia 45:18, " Maana Yehova, aliyeziumba mbingu hu ha-Elohim, asema hivi; Yeye ni Elohim; yeye Elohim ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye Aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, Aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni Yehova, wala hapana mwingine." Katika haya maandishi, Yehova ametajwa nmara mbili. Hii inaashiria moja,  ikiwa ni tarakimu ya umoja; lakini Elohim ni wingi ikiashiria mbili ama halaiki; na nomino hii ya halaiki imepewa utangulizi, sio na wao kama wao Elohim; lakini na 'Yeye' (kiume - He), kama Yeye Elohim. Jambo hili la kipekee ni la mafundisho na si la kiajali, wala desturi holela ya lugha, bali ni jambo lililopangwa. Linafundisha ya kuwa uumbaji ulifanyika kutoka kwa nguvu moja ex ou, yaani kulikotoka, vitu vyote, na kwamba nguvu hii moja iliyatekeleza haya kupitia wingi wa mawakala, ama Elohim, ambao ni roho mawakala wa mionzi yake" (Phanerosis ukurasa 52).

"Mbingu na nchi" — "Mbingu" ni hashshamayim kwa Kiebrania, na iko kwa wingi (mbingu-heavens) kutoka kwa mzizi, 'kuwa juu'. Inahusiana na anga, sehemu kubwa ya nyota iliyo juu ya nchi, juu zaidi kutoka kwa ardhi. Mbingu yatajwa kabla ya dunia kwa sababu ndio mpangilio wa kweli na wa kawaida. Kuna wakati ambapo hakukuwa na dunia (Mithali 8:23); lakini hakukuwa na wakati ambapo mbingu haikuwepo, kwa maana ya kiwango cha juu ya kuashiria makao ya Mungu. Hata hivyo, mbingu, katika aya hii, inamaanisha kilichoumbwa halisi, na kwa hivyo, hasa kwa ulimwengu ambamo dunia ni mshirika mojawapo.

"Dunia" kwa Kiebrania ni ha eretz, na inamaanisha ardhi ikilinganishwa na mbingu juu yake.

 

AYA YA 2

"Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu. — Maneno haya bora yangekuwa "bure na tupu" . Maneno ya Kiebrania ni tohu na bohu. Maelezo hayo yapatikana pia katika Yeremiah 4: 23-26, lakini muktadha waonyesha kuwa Yeremia hakuwaza uumbaji wa kawaida katika fikira zake, lakini uumbaji wa Yehova wa kitaifa: taifa la Mungu la Israeli. Mashirika ya kisiasa ya taifa yalikuwa yaangushwe, na watu waondolewe nchini. Uporaji na uharibifu ambao ungetokana na uvamizi wa Wakaldayo, ungesababisha nchi ya Yuda kuwa "bure na tupu" kisiasa. Hali ya kale ya uumbaji ikawa aina ya uangushwaji wa nci ya Yuda. Yeremia hata aliona milima ikitetemeka kabla ya kujongea kwa vikosi vya Nebukadreza, kwani "milima", kama ishara, yaashiria falme za nguvu, na uzito na fanaka ya uvamizi wa Wakaldayo ilisababisha hata Misri na nguvu zake nyingi, kutetemeka kwa hofu.

Kuhusu uumbaji mwenyewe, maneno "ukiwa na utupu" yaashiria hali ya kuwa shaghalabaghala ambamo Mungu alileta mpangilio na maisha. Awali ukungu wa giza kisichopenyeka kilitanda ulimwengu uliozungukwa na maji, hivi kwamba inaelezwa kuwa "isiyokuwa na umbo" na tupu.

Dunia ilikuwa hivyo siku zote? Pendekezo la wakati kabla ya Adamu limefanywa katika Elpis Israel, na ingawa

hatukubaliani na mafunzo kuwa "malaika walioasi" ni wa wakati huo, kuna mapendekezo katika Maandiko Matakatifu yanayoashiria kuwa kulikuwa na viumbe kabla ya kuumbwa Adamu.

Kwa mfano, baada ya Adamu na Hawa kuasi, Elohim alitangaza kuwa Adamu na Hawa wamekuwa jinsi malaika walivyokuwa wakati fulani: "kujua mema na maovu" (Mwa. 3:22). Hii inadokeza kuwa malaika walikuwa wakati fulani wanakufa, na kwamba walipata hali zao kimalaika za kuishi milele kupitia majaribio katika hali ya uovu. Kwa upande mwingine Isaya 45:18 yaeleza juu ya uumbaji wa dunia; kulingana na Waebrania: "Aliiumba sio maganjo" (tohu). Hii inaashiria kwa dhati kuwa dunia haikuwa katika ile hali iliyoelezwa katika Mwanzo 1:2. Na hii inaungwa mkono na kitenzi kinachotumiwa hapo na kutafsiriwa "ilikuwa". Kitenzi hayah chaonyesha si hali "kuwa" bali "itakayokuwa", "itakayofanyika". Dkt. Strong anatoa kitenzi  hiki katika wakati ujao, na kwingineko katika Biblia inaonyeshwa vivyo hivyo. Kitenzi hicho hicho, katika muktadha huo huo, chapatikana katika Mwanzo 2:7: "mtu akawa nafsi hai. "

Kwa hivyo, twaweza eleza Mwanzo 1:2 "Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu." Hii inaonekana inaonyesha hukumu ya janga ya Mwenyezi Mungu kutumbukiza ardhi katika hali ambayo imeelezwa katika aya za mwanzo za kitabu cha Mwanzo.

Hakika matumizi ya Yeremia ya kirai ya "kuangusha Taifa la Wayahudi" yaonyesha kuwa ingekuwa hivyo.

 Ikiwa hivyo ndivyo, ni dhana duni eti kwa nini nchi kutumbukia katika hali hiyo, au hali ya hapo awali.

"Na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji" —Giza kisichopenyeka  ilitanda bahari za awali silizofunika dunia. "Kilindi" (t'hom) ni shimo la kina kirefu la maji ambalo wakati huo lilifunika ardhi. Maneno haya yametumika kuhusu bahari katika sehemu nyingi za Neno Takatifu. Giza ya dunia ya asili ni ya fumbo la giza ya akili ya kiasili ya mwanadamu  kabla mwanga wa ukweli kupenya. Hapo mwanzo kulikuwa giza na Mungu akasema, "Iwe nuru". Ombi kama hili limefanywa kwa wote watakaosikiliza. Matumizi ya Yohana ya kazi ya uumbaji katika aya za kwanza za Injili yake, yanaonyesha waziwazi kusudi la Mungu la baadaye kwa binadamu. Kwa njia hiyo, Mungu alisema "Iwe nuru" wakati "hapo mwanzo" Alitangaza mpango wake wa wokovu (Mwa. 3:15).

"Roho ya Mungu Mungu ikatulia juu ya uso wa maji." — Roho ya Mungu (Elohim) alikuwa Roho wa Yehova,

lakini kupitia Elohim (ama mawakala wa Mungu) kwa malengo ya uumbaji. Roho wa Mungu husambaa katika kila kiumbe  (Zab. 139:7-12), hata katika sehemu hizo ambamo mtu hawezi kupumua. Roho wa Mungu katika hali ya kuunganika, hata hivyo, hutumika kufanya  kazi za miujiza (Ayubu 26:13; 33: 4). Neno "tulia" ni rachaph, maanake - liangua, na limetafrsiriwa hivyo katika kuta za Revised Version. Kitenzi hiki kinaashiria mtetemo wa kuku anapoangua mayai yake, ama anapowalea vifaranga wake. Kuna mapendekezo ya utunzaji na uangalifu wa msisimko uliohusuriwa katika kirai hicho. Duniani-yai ilikuwa karibu kudhihirisha maisha, na kanuni muhimu kwa matokeo hayo ilikuwa ni Roho ya Mungu. Angalia Zaburi. 104: 30; 139: 7.

AYA YA 3

"Mungu akasema" — Mungu anapozungumza, mambo yanafanyika. Angalia Zaburi 33:6; 2 Petro 3:5. Kuna nguvu katika Neno Lake, kama ilivo dhahiri kwa watu wote wanaokuja chini ya ushawishi wake. Petro anatangaza kwamba dunia "hufumba macho yao wasione" ukweli huu. Wanaume ni wajinga wa

 nguvu za Neno la Mungu kuhusiana na uumbaji wa asili, na vilevile kuhusiana na viumbe vyake vya kiroho. Kama Neno la Mungu lilivyoleta mpangilio kutoka kwa zahama za awali, ndivyo Neno Lake linavyoweza kuleta mpangilio kutoka kwa zahama za akili za watu, na badala yake kuweka ukweli wa Mungu.

"Iwe nuru; ikawa nuru" — Nuru ni Mungu. Tunasoma kwingineko, kuwa si tu kwamba Mungu anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa na mtu (1 Tim 6:16.), Lakini pia kwamba "Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake" (1 Yohana 1: 5). Hivyo, harakati za kwanza za ubunifu wa Mungu katika kuleta mpangilio kutokana na zahama, ilikuwa kufanya mwanga uwepo dunia inakohusika. Huu mwanga ungeweza kutolewa na malaika kwa urahisi zaidi ya binadamu anavyoangaza chumba cha giza leo kwa kubonyeza swichi ya stima; ama ingekuwa mwanga wa jua, usioweza kuzimwa kama kifaa cha mbinguni kinachosababishwa kupenya giza kilichotanda kinachotokana na mivuke inayozunguka ardhi. Kwa hakika, hii ni njia inyowezekana zaidi ambayo kwayo mwanga ulitolewa, kwa kuwa maelezo yanaashiria kwamba mchana na usiku zilifuatana kwa mzunguko.

AYA YA 4

"Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza" — Faida ya mwanga kama ikilinganishwa na giza imeashiriwa na kauli hii. Hakika ni kweli kuhusiana na Ukweli, Kwa kuwa chochote kilicho kizuri na cha kifalme hutoka hapo (tazama Yohana 3: 19-21).

Kwa njia hiyo hiyo ambapo nuru ilikuwa muhimu kuleta mpangilio kutoka kwa zahama katika viumbe vya kimwili, hiyo ilikuwa hatua ya kwanza muhimu katika uundaji wa viumbe vya kiroho vya Yehova. Nuru ya kweli ya uungu sharti kwanza iingie  katika roho ya kiumbe binafsi kama kitaumbwa kuambatana na kanuni za Mungu (2 Kor. 4:6); na, kama katika mwanzo, haya yanafanyika kwa Neno la Mungu. Kwa jinsi hiyo, mtu anapita kutoka kwa giza hadi kwa "nuru yake ya ajabu" (1 Peter 2:9).

Kuna uwezekano mkubwa kuwa tendo la uumbaji lilifanyika kwa mzunguko wa ardhi;  jua likipenyeza mwangaza hafifu katika ukungu na mawingu yaliyotanda dunia. Vivyo hivyo, Ukweli ilikuwa tu wahisiwa mara ya kwanza (Rum. 16:25), mwangaza kamili wa umuhimu wake ukiwa wazi katika ufufuo na utukufu wa Bwana (Mat. 4:16).

AYA YA 5

"Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku " — Ni kwa nani Mungu "aliita" nuru na giza kwa majina haya? Bila shaka kwa Adamu na Hawa ambao walipewa maagizo katika njia za Mungu (ona Mwanzo 2:19). Hivyo kulikuwa na ufunuo wa makusudio ya Mungu kabla ya ule aliyopewa Musa (ona Mwanzo 18:19).

"Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja" — Jioni inaanza kwanza maana giza lilikuwa kabla ya mwanga. Kwa sababu hiyo, siku ya Wayahudi huanza thenashara jioni, kumkumbusha kila Mwisraeli kwamba giza ni urithi wake wa asili, lakini inapaswa kubadilishwa na mwanga. Siku hizi zilikuwa na urefu gani? Baadhi ya watu huamini kwamba zinaashiria vipindi virefu vya nyakati , ambapo michakato ya uumbaji tunavyoujua leo ulifanyika. Katika Elpis Israeli, Ndugu Thomas anatangaza hivi: "Siku sita za Mwanzo zilikuwa bila shaka sita za mchana za mizunguko ya dunia juu ya mhimili wake. Hii ni wazi kutokana na mujibu wa sheria ya Sabato. 'Siku sita fanya kazi (Enyi Israeli) utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako:  maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.' Je, ingekuwa sababu mwafaka kwamba, kwa sababu Bwana alifanya kazi vipindi sita vya miaka elfu moja au zaidi kila moja, na aliacha kama elfu mbili hadi utoaji wa Sheria, kwa hiyo Waisraeli wangefanya vipindi sita vya masaa kumi na mawili, na kutofanya kazi yoyote kwa kipindi cha saba au siku cha muda kama huo? Je, Mwisraeli yeyote au mtu wa Tataifa jingine, asiyeharibiwa na falsafa bure, aweza fanya hitimisho ya wanajiolojia kwa kusoma sheria ya Sabato? Tunaamini sivyo. Siku sita za urefu wa kawaida ulikuwa muda tosha kwa Muweza na nguvu zote za ulimwengu zikiwa kwa amri yake kufanya mageuzi duniani, na kuweka wanyama wachache juu yake wakiwa muhimu kwa ajili ya mwanzo wa utaratibu mpya wa mambo katika dunia "(uk. 11 , 12).

Companion Bible inatoa maoni haya: "Wakati neno 'siku' hutumika kwa tarakimu , inaainishwa, na kumaanisha siku ya masaa ishirini na manne." Hii ni lazima iwe hivyo hasa wakati mipaka ya siku inafafanuliwa, kama zilivyo katika maandishi mbele yetu, yaani jioni na asubuhi. Ni nini kingeshikamanisha jioni na asubuhi ya enzi ya wakati?

Lakini jambo hili limetatuliwa zaidi ya shaka na ukweli kwamba Adamu aliumbwa siku ya sita, na kuendelea kwa siku ya saba! Je, aliendelea na kipindi hiki kinachodaiwa cha miaka elfu na zaidi? Alikuwa na umri wa miaka elfu kabla ya wakati wa kujaribiwa kwake katika Edeni?

Taarifa ya Kutoka 20: 8-11 kwamba kama Bwana alivyofanya kazi kwa siku sita na kupumzika siku ya saba, wana wa Israeli wanapaswa kufanya vivyo hivyo, inafundisha wazi kuwa siku za Mwanzo1 zilitambuliwa kama siku za kawaida za masaa ishirini na manne; na kwa hakika, kama Ndugu Thomas anavyosema, huo ulikuwa muda tosha kwa Makadara kufanya upya uumbaji jinsi inavyoelezwa.

Katika fumbo la uumbaji, siku ya kwanza ilibashiri miaka  elfu ya kwanza ya historia ya mwanadamu. Enzi hii ilishuhudia mgawanyiko wa Wana wa Mungu kutoka kizazi cha Kaini. Iliona kifo cha Adamu, ikisisimua ufaji wa mwanadamu ambaye kitendo chake kiliuleta kwayo,  na tafsiri ya Henoko "asije akaona mauti" (Mwa 5:. 3-4; 23-24; Ebr 11 : 5), kana kwamba kumkumbusha mtu kuwa ingawa alikuwa na uhusiano na kifo anaweza kupata maisha kama akiyatafuta kwa mfano alioachiwa. Katika fumbo hili "siku ya kwanza" ya historia ya mwanadamu, kwa hivyo, kulisababika utengano kati ya wana wa mwanga na wana wa giza.

 

Siku ya Pili: Anga Lafanyizwa — aya za 6-8

Tendo cha pili katika kuumbwa upya dunia, lilikuwa ni kusababisha kutengana kati ya maji ya kidunia na maji ya kimbinguni. Hii ilifanyika kwa kuanzisha "anga '' baina yazo. Ilhali  hili lilitekelezwa katika siku ya pili, kimafumbo inatwelekeza mbele kwa enzi kubwa ya pili katika maendeleo ya madhumuni ya Mungu na mpango wa miaka 7,000, iliyoashiriwa katika vitendo saba vya uumbaji (linganisha 2 Pet 3: 8). Tendo la kwanza lilikuwa usambazaji wa mwanga duniani kote (ona Mwanzo 1:15; Yohana 1:1; 2 Kor 4:6; Zab 119:05,130; Isa 45: 7).Tendo la pili lilikuwa kugawanya binadamu katika makundi mawili:

wale waliovutwa kwa mwanga, na wale  walioukataa. Miaka elfu mbili baada ya kuumbwa, mgawanyiko  kama huo ulifanywa, kwa kuwa Abramu aliitwa kutoka kwa giza ya Uru, na akawa kama baba wa wale wote ambao wangetengwa. na watu wa mataifa mengine ya giza na kwenda kwenyemwanga wa ajabu wa kweli  (1 Petro 2: 9). Kama maji yalivyo kiashirio cha watu (Ufunuo 17:15) , mwanadamu halafu alitengwa katika maji ya kimbinguni na maji ya kidunia; wa kwanza akielekezwa kutawala katika siasa za mbinguni ya enzi ijayo,na wa mwisho akiwakilisha mataifa yalitotawaliwa na Ufalme.

AYA YA 6

" Mungu akasema, Na liwe anga" — Neno lililotafsiriwa "anga" ni rakia , kutoka kwa mzizi unaomaanisha " kupiga, kuponda, kutandaza, au kuunyosha ", na kwa hivyo anga (tazama Strong, A.V. mg.). Elihu alimwuliza Ayubu: "Je! Waweza kuzitandaza mbingu pamoja naye, Ambazo zina nguvu kama kioo cha kuyeyushwa?" (Ayubu 37:18). Katika swali hili, kitenzi kutandaza ni kutoka mzizi rakah. Elihu alikuwa akirejelea paa kubwa ya anga ya juu, akidokeza ukubwa na umilele; upinde mkubwa wa mbingu unaozunguka dunia. Anga imetumika kimafumbo katika Maandiko ya mahali pa mamlaka ya mataifa tawala ya dunia, na unabii unaangazia mbele kwa "mbingu mpya" ambazo Bwana anakusudia kuanzisha duniani (Isa 65: 17-18). Madhumuni ya Injili ni kutenganisha watu kutoka nje ya mataifa kuchukua anga ya kiashirio ya siku za usoni (Matendo 15:14; Danieli 12: 3).

"katikati ya maji" — Kabla ya kufanyizwa anga, au anga ya juu, ni  dhahiri mawingu yalitua juu ya bahari zilizofunika nchi na kujaza nafasi ya juu, na kufunika kabisa mwanga wa jua.

"Likayatenge maji na maji. " — Ufanywaji wa anga juu ya nchi kwa uhakika ulisababisha utengano uliosimuliwa. Kwa njia hiyo, maji yaliyokuwa baharini chini yalitenganishwa na yale ya mawinguni ambayo sasa yalipepea katika hewa nzito ya anga iliyo juu, iliyoundwa na mkono mbunifu wa Mungu.

 

AYA YA 7

" Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. " — Neno la Kizungu "firmament" latokana na la Kilatini firmamentum, ambalo pia laegemea la Kigiriki stereoma, yote yakiwa na rai ya umadhubuti. Hata hivyo mkazo katika neno la asili la Kiebrania, rakia si kwa kifaa chenyewe lakini kwa tendo la kunyosha, ama hali ya kunenepeshwa. Katika sehemu nyingi za Agano la Kale, tendo la kunyosha hadi mbinguni limepewa kipaumbele (angalia Ayubu 9:8; 26:7; Zab. 104:2; Isa. 45:12; 51:13; Yer. 51:15 Zak. 12:1). Maji yaliyo juu, yanaashiria mawingu na ukungu; yale ya chini, "kina" ambacho hatimaye kilisambaa dunia nzima.

AYA YA 8

"Mungu akaliita lile anga Mbingu " — Hii haikuwa mbinguni kama makao ya Mungu, lakini anga iliyo punde tu juu ya ardhi mawingu yanakotanda. Neno hili kwa Kiebrania ni shameh, na linamaanisha "kuinuliwa"

"Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili. " — Hii siku ya pili iliashiria mabadiliko yaliyofanyika katika miaka elfu ya pili ya historia kutoka kwa enzi ya uumbaji. Hii ilishuhudia mgawanyiko uliyosababika wakati wa Gharika Kuu na

kuendelea katika siku za Pelegi (Mwa 10:25), iliyofanyika kabisa kwa wito wa Abramu na jamaa yake kutoka nje ya Uru wa Wakaldayo (Mwa 11:31). Kwa mfano wa kibiblia, maji yanawakilisha binadamu (Ufu. 17:15), na katika milenia ya pili kulikuwa na utengano uliyosababika humo kugawa watu wa Mungu kutoka kwa wale wa mwili.

 

Siku Ya Tatu: Ukuaji Juu ya Ardhi — aya za  9-13

Kabla wakati huu, maji yalifunika nchi nzima; sasa mungu akafanya mabadiliko makuu duniani yaliyoimarisha vina vya bahari, na kufanya maji yakusanyike mahali pamoja, hivi kwamba mabara yakawepo.

Umeaji mimea ukafuata. Huu mkusanyiko wa mabara,na utokezo wa kwanza wa uhai, ni mfano wa ufufuko, na uliwakilisha sehemu ya kwanza ya utimilifu wa uumbaji. Kwa sababu hiyo, tarakimu tatu ina maana ya ya kimafumbo ya ufufuko, ama utimilifu. Utokezo wa kwanza wa nchi kavu pia ulikuwa wa umuhimu mkubwa katika lengo la maendeleo la Yehova. Katika Maandiko ya kinabii, milki za Mataifa mara nyingi huwakilishwa na "bahari" (Isa. 57:20; Ufu. 17:15), na Israeli na "nchi" iliyozungukwa na bahari (mf. Hag. 2:6). Kwa mujibu wa miaka elfu saba ya kujitokeza kwa kusudi la Mungu, Israeli, kama taifa, ilionekana katikati ya mataifa mengine wakati wa milenia ya tatu kutoka wakati wa uumbaji.

AYA YA 9

"Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo." — Katika Wimbo wa Uumbaji (Psa. 104), Daudi anarejelea tendo hili la uumbaji: " Uliifunika (nchi) kwa vilindi kama kwa vazi, Maji yalikuwa yakisimama juu ya milima. Kwa kukemea kwako yakakimbia, Kwa sauti ya radi yako yakaenda zake kasi, Yakapanda milima, yakatelemka mabondeni, Mpaka mahali ulipoyatengenezea. Umeweka mpaka yasiupite, Wala yasirudi kuifunikiza nchi" (Sura 6-9). Marejeo haya ya kuletwa kwa milima, utorokaji wa maji kwa kukemewa na Mungu, ukusanyikaji pamoja wa mabahari, na uanzishwaji wa mabara, watoa wazo juu ya jinsi na ukubwa wa kazi ya Mungu amri yake ilipotokea.

AYA YA 10

"Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema" — Neno nchi, (eretz), kulingana na Dkt. Strong, lina mzizi wake kwa Kiebrania likimaanisha kuwa imara; ambapo kiishara, neno nchi linaashiria Israeli ya kiasili (linganisha na Hag. 2:6 na Ebr. 12:26), na "bahari" likiashiria milki za Mataifa (Isa. 57:20; Ufu. 17:15). Katika ufafanuzi wa hili, angalia jinsi Paulo anavyoghairi marejeleo ya Hagai ya "bahari" wakati yeye anatumia kauli ya nabii huyo kwa Israeli (Ebr 12:26.).

AYA YA 11

"Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu" — Muumba aliweka ndani ya ardhi uwezo wote kwa ajili ya maisha ya mmea. Kimafumbo, nchi ni ishara ya moyo wa mwanadamu; ulio na uwezo wa kupandwa mbegu nzuri na kuzaa kwa wingi; au wa kuzalisha miiba (Mathayo 13: 3-9, 19-23; Ebr 6: 7).

Aina tatu za mimea zimetajwa katika aya hii. Wa kwanza ni nyasi. Deshe kwa Kiebrania, kutoka kwa mzizi wa neno likimaanisha kuchipua, linazotumika kwa kila aina ya majani ya kijani kibichi katika hali ya kuchipua. Nyasi ina maisha mafupi, na hunyauka katika hali ya joto kali ya jua. Katika suala hilo, linazungumzia hulka ya muda mfupi ya mwili (Isa 40: 6-8.). Aina ya pili ya mmea ni "mche utoao mbegu." Hapa neno ni eseb, na linaashiria hali ya juu ya mimea inayopandwa kutoka kwa mbegu. Aina hii ya mmea ni chakula, kwa maana ilikuwa baina ya mlo wa asili wa mtu (aya 29).

"Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo." — Miti ya aina nyingi ya kutoa matunda ilisababishwa kukua, kila mmoja ukizaa "matunda kwa jinsi yake."

AYA YA 12

"Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema" — Aina ya kwanza ya maisha ilitokea juu ya nchi, ikiletwa kwa amri ya Mungu. Neno la Mungu linaweza kusababisha watu wa dunia kuzaa matunda mema kwa maisha ya usalihina. Hiyo ni mtoto wa "mbegu...  isiyoharibika, kwa neno la Mungu, lenye uzima, lidumulo hata milele" (1 Pet. 1:23). Kwa kulinganisha, mwili ni "kama nyasi, na utukufu wake wote ni kama ua la majani. Nyasi hunyauka na maua huanguka Lakini neno la Bwana hudumu milele." yaani, neno kama lilivyotangaza kupitia Injili (1 Petro 1:. 24-25).

AYA YA 13

"Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu " — Uakisi wa hii siku ya tatu katika fumbo la Wiki ya Uumbaji unabashiri maendeleo ya milenia ya tatu baada ya uumbaji. Kipindi hicho kiliona mgawanyiko kamili wa Israeli kama taifa kutoka kwa mamlaka ya Mataifa (dunia kuonekana katikati ya bahari), na kilishuhudia maendeleo ya maisha ya kiroho kutoka ndani ya "ardhi" Israeli ilipopata agano huko Sinai, ikiafikia mazao na matunda ambayo mimea na miti ya siku ya tatu ilitoa. Msafara wa Kutoka Misri ulifanyika kama miaka 2500 baada ya uumbaji ili ifikapo mwishoni mwa milenia ya tatu, Israel kama taifa ilikuwa imara mbele ya mamlaka zingine zote.

Siku Ya Nne: Jua, Mwezi na Nyota aya ya 14-19 — Giza ya siku za giza ilikuwa imepenya kiasi mnamo siku ya kwanza; yamkini mawingu yaliyotanda siku ya pili (aya ya 6) yalikuwa yamegubika nchi na ukungu. Hayo yalikuwa sasa yamefukuzwa, na nchi ikawa chini ya ushawishi wa mionzi ya moja kwa moja ya jua na mwezi. Siku ya nne, kwa hivyo, ilikuwa na usambamba na siku ya kwanza. Siku hizo sita zinaweza kugawanywa katika sehemu mbili za siku tatu kila moja. Kila sehemu na mwanga kwanza, halafu na maji, na hatimaye kwa nchi kavu. Katika hitimisho la milenia ya nne kutoka Uumbaji, akiwa amefurahishwa na siku hii ya nne, Bwana Yesu alionekana kama "mwanga wa ulimwengu" (Yohana 1: 9; 8:12).

AYA YA 14

"And God said, Let there be lights in the firmament of the heaven" — Katika aya tangulizi (aya za 3-5), neno la "mwanga" ni owr, lakini hapa ni meourouth, na linaashiria kinachotoa mwangaza ama mchukuzi wa mwanga. Katika neno hilo hilo, japo katika wingi, kama ile inayozungumzia kinara cha taa katika hema ya kuabudu (Kut 25:6; 24 Law. 2: Hes 4: 9, 16). Hili ni la muhimu zaidi, kwa kuwa linaeleza Jua na Mwezi kama Vinara vikubwa vya mbinguni, vikionyesha mwanga wa Mungu. Jua ina mwanga wake mwenyewe, lakini Mwezi hauna; unaduta ule wa Jua. Katika ufumbo wa Maandiko, Jua inawakilisha Kristo (Mai 4: 2.), Na Mwezi, Iklezia, Bibi Harusi wa Kristo (Wimbo 6:10.) akiangazia mwanga wa Bwana wake.

Zimefalanuliwa katika aya hii, katika uhusiano wao na dunia. Vile mwanga wa Jua na ule wa mwezi ni kuangaza juu ya nchi, hivyo mwanga wa ukweli ulitawanywa, kwanza na Kristo, na baadaye na Iklezia. Katika utekelezaji wa huduma hii Iklezia huonyesha mwanga kutoka kwa Jua, ukiwa "barua ya Kristo ijulikane na kusomwa kwa watu wote - (2 Kor 3:18; 4: 4,6).

Kama mwanga wa Jua na mwanga wa Mwezi ulipoangaza kwa kila pembe siku hiyo ya nne, ndivyo mwangaza wa ukweli umetengwa mbele ya wanadamu wote tangu siku za Kristo kupitia kwa matangazo yaliyoenea ya Injili kumwacha "mtu asikiaye" (Ufu 22:17). Na, kwa kiasi kikubwa, Kristo alitokea katika milenia ya nne baada ya uumbaji.

"Kugawanya mchana kutoka kwa usiku" — Hii ingefaa iswemwa: "Kugawanya bain ya mchana na baina ya usiku." Tofauti bain ya utukufu wa sasa wa Yehova duniani katika kuhubiri kwa Injili, na ule ambao bado haujabainika duniani, unaweza kulinganishwa na tofauti bina ya mwanga wa mwezi na ule wa jua (Isa. 30:26) Kwa sasa mwanga duni wa mwezi wa Iklezia unaonekana; ilhali katika siku zijazo mwanga wa jua-Kristo litaangaza katika mbingu za kisiasa wakati a ukamilifu wa utukufu wa ahadi (Mal. 4:2).

"Nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka" — Taarifa hii, pia inaonyesha ukweli wa kawaida na wa kiroho. Kwanza, ni sahihi kwa jamii ya kijijini, kama vile Mungu alivyokusudia mtu kuwa (. Linganisha na Mwa 2:15; 3:19), kujali mpangilio wa viumbe vya mbinguni katika hali iliyopendekezwa. Neno owth, "ishara" ama "bendera" laashiria kutokea hali fulani ama kitu, bendera ikimaanisha uwepo wa kinachowakilishwa nayo. Katika muktadha wa kilimo, mpangilio wa jua na mwezi huashiria wakati murua wa kupanda  na wa kuvuna. Kiroho, zinafunza binadamu pia. Wakati ulioteuliwa ili kuadhimisha Pasaka ulimaiziwa na mwezi. Huangaza kikamilifu wakati huo, na kwa hivyo ni mwakilishi kamili wa Israeli kwa utukufu mzima wa mwanga wa kiroho. Aidha, jua na mwezi zimetumiwa kama kielelezo cha nguvu za Muumba na kusudi lake. Ni mfano wa mpango wake, ukibashiri utukufu wa enzi inayokuja (2 Sam. 23:4). Maandiko ya kinabii hutumia mbingu kwa jinsi hiyo (Zaburi 19:.. 1; Isa 30:26; Yer 31:35; 33:. 19-21).

Kuhusu Daudi imenakiliwa: "Wazao wake watadumu milele, Na kiti chake kitakuwa kama jua mbele zangu. Kitathibitika milele kama mwezi; Shahidi mwaminifu aliye mbinguni " (Zaburi. 89:36-37). Maneno haya yanafafanua "siku ya kuja kwa Kristo" wakati utukufu wake utamulika kutoka Yerusalemu ukiangaza watu wote kwa haki yake.

Tofauti na jua, mandhari ya mwezi si imara. Unang'ara na kufifia daima. Ishara hii katika mbingu ni muhimu kwa watu wa Yehova. Kung'ara huku na kufifia ni ishara ya mtetereko wa kiroho wa eklezia. Katika hili kuna kushajisha na kuonya. Wakati mwezi uko katika kilele cha mwanga, wakati yaelekea kwamba eklezia ina nguvu kiroho: jihadhari kwa maana unaweza kufifia; wakati uko katika hali ya kufifia kabisa, jipe faraja, kwa maana unaweza kupata nuru kubwa. Mwezi hauna udhabiti kamili; na Iklezia pia haina.Mwezi huu wa rangi ya fedha, ukitangaza ujumbe wake wa ukombozi wenye nuru katikati ya kuba la giza la mbinguni, ni ishara ya ajabu ya Injili. Sayari za ambinguni zilimsisimua mtu wa awali; ni dhahiri kuwa unajimu ni mada iliyokuwa imemchangamsha Ayubu (Ayubu 9: 9; 38: 31-32; angalia pia Amos 5: 8).

Gesenius anapendekeza kwamba neno Mazzaroth (Ayubu 38:32) linahusiana na unajimu, na hii inaungwa mkono na maelezo ya Toleo Lilizoidhinishwa (la Biblia). Ishara kumi na mbili za nyota, zikiashiria miezi kumi na miwili ya mwaka, zinahusiana na misimu tofauti, nazo, kwa upande wake, zaongea juu ya madhumuni ya Yehova. Kwa mfano, majira ya baridi mara nyingi yanahusishwa na kifo, na majira ya kuchipua na ufufuo.

Hata hivyo, kujifunza mambo mbingu bila ya uongozi wa ufunuo wa Mungu, kulisababisha wengi wa watu wa zamani kupotosha Ukweli. Hii ilisababisha ujenzi wa mnara wa Babeli, ambao kuba lake liliiga mbingu, kwa ajili huenda kuba lenyewe lilipambwa na ishara za Nyota. Mnara wa Babeli umeelezwa kama uliokusudiwa "kifikia mbinguni" ambayo pengine maana yake ni kwamba ulikuwa  ulijengwa na kupambwa ili uige na kuwakilisha mbingu. Hii tamaa ya uovu kwa upande wa mtu pengine inatokana na utafiti wa kupotosha wa nyota za mbinguni. Kuna njia sahihi na ya kupotosha ya kujifunza nyota za mbinguni kama ikielezea dalili za kusudi la Mungu, kama Jeremiah alivyoonya (tazama Yer 10: 2).

Misimu inahusiana na nyakati za miaka kama inavyoongozwa na uhusiano wa dunia kwa jua, ikitoa majira ya joto, ya vuli, ya baridi na ya chipuko. Neno ni mowada, na linaashiria "nyakati zilizowekwa". Neno hili hutumika kuhusiana na sherehe za Kiebrania, na limetafsiriwa sikukuu katika Law. 23: 2 na kwingineko. Nyingi za sherehe zile zilienda sambamba na msimu wa chipuko na mavuno, na zilibainishwa na nyakati hizo za mwaka. Kwa hivyo jua, mwezi na nyota, zikiangaa kama taa katika kuba la giza la mbinguni, zilianzishwa kwa ajili ya" ishara "na" misimu "na ni maelezo ya madhumuni ya Yehova" kwa wakati uliopangwa ".

AYA YA 15

"Tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo. " — Maelezo ya asili ni "dalili na majira" (aya ya 14).  Jua halisi na mwezi hutenda hivyo. Zote mbili pia kutumika kimfano kwa ajili ya Kristo na Iklezia. Kristo anaelezewa kama "jua la haki" (Malaki 4: 2.), na alipokuwa duniani alitangaza kwamba alikuwa "nuru ya ulimwengu" (Yohana 8:12). Wakati yeye hayupo, "usiku" unatawala duniani (Yohana 9: 4-5) Lakini kama mwezi unapotoa mwanga wa kifedha juu ya nchi iliyotanda giza, ndivyo Iklezia ilivyoinuliwa katika "ulimwengu wa roho katika Kristo" (Efe 1: 3.), Ili "kutoa mwanga juu ya nchi." Kwa hivyo Paulo anawahimiza hivi: " Mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, mkishika neno la uzima" (Flp. 2: 15-16).

Wa asili hufundisha wa kiroho katika uumbaji wa Mungu.

AYA YA 16

"Mungu akafanya mianga miwili mikubwa " — Wakosoaji wa Biblia husema kuna utata dhahiri hapa. Mungu Aliamuru nuru ing'ae siku ya kwanza; na ingawa alikuwa Amegawanya kila siku kuwa mchana na usiku (ikimaanisha duru ya dunia kuzunguka jua), ilhali, siku ya nne, "akafanya mianga miwili mikubwa ya kutawala mchana na usiku." Kwaweza kuwa mwanga bila ya jua? mwenye shaka huuliza. Kwa kweli kwaweza! Tunao leo tunapoasha umeme, na kugeuza usiku kuwa mchana. Chanzo cha mwanga kipo, hata kama hatujabofya kiwashio. Kile binadamu anaweza kufanya, Mungu anaweza kufanya kwa ukamilifu zaidi.

Je, kulikuwa na jua kabla ya siku ya nne? Tunaamini kuwa ilikuwa. Hatuoni sababu ya kutofautiana na ufafanuzi uliotolewa na Elpis Israel, ukurasa wa 12, 13:

"Siku ya kwanza, mwanga ulisababishwa kuangazia giza, na kufichua uso wa maji; siku ya pili, anga inayoitwa Mbingu iliundwa, ambayo kwayo ukungu uliwezeshwa kwa kuelea kwa wingi juu ya vilindi; siku ya tatu, maji yalikuwa yamekusanyika huko bahari, na nchi kavu, iitwayo Dunia ikatokezea. Ilikuwa imevikwa kijani, ikiwa na matunda, na na miti ya misitu, ikawa ni maandalizi ya kuanzishwa kwa viumbe vya kula nyasi kwa kukaa ndani yake. Siku ya nne, anga iliyopanuliwa ikawa na uwazi, na vizingo vya ulimwengu vingeweza kuonekana kutoka kwa uso wa dunia. Dunia yetu halafu ikawekwa katika uhusiano wa kifalaki nazo na kukabiliwa na mvuto wao wa mzunguko wa mchana na usiku, majira ya joto na baridi; na kwamba zingetumika kwa ishara, na kwa miaka. Kwa hivyo, jua, mwezi, na nyota ambazo Mungu alizifanya, kwa kuupa mhimili wa dunia mwelekeo fulani kwa ubapa wa mviringo wa anga, zilikuwa na mtawanyiko wa mvuto wa kufana mno juu ya nchi kavu na baharini. Pakawa sasa makaazi maridhawa na mwafaka kwa wanyama wa kila aina. Makao haya yakakamilishwa, yakawa na hewa nzuri, na kutukuzwa kwa mwanga wa taa za mbinguni; chakula kikatolewa kwa wingi; na mtaa huu wa kifahari ulingoja tu wapangaji wenye furaha ili kukamilika ". Ufafanuzi huu umeungwa mkono na hadithi katika Mwanzo ambayo haisemi kwamba Mungu "aliumba mianga miwili mikubwa" siku ya nne, lakini kwamba, siku hiyo, Yeye "aliifanya kutawala mchana na usiku." Kwa maneno mengine, Yeye aliteua msimamo wao na ushawishi katika mahusiano ya nchi.

Katika suala hilo, ni lazima ieleweke kwamba kitenzi kilichotumika katika aya ya 16 ni tofauti na kile kilichotumiwa katika aya ya1. Hapo neno ni bara, kuumba; hapa ni asah ambalo lina maana ya kuteua, na kuumba vilevile. Kitenzi hiki kinatokea katika Zaburi 104: 19:

"Yeye aliuteua (asah) mwezi kuwa wa misimu". Tukitumia maana sawa hapa, tunahitimisha: "Mungu aliziteua taa mbili kubwa, ile kubwa zaidi itawale mchana, na ile ya mwanga mchache itawale usiku." Tena, Ndugu Thomas ananena:

"Simulizi ya Musa sio ufunuo kwa wenyeji wa sayari ziyingine zilizo mbali na dunia, ya muumbo wa ulimwengu mkubwa kupita kiasi; bali ni kwa binadamu kama mwenyeji wa mfumo wa nchi kavu. Hii inaeleza ni kwa nini mwanga husemwa kuumbwa siku nne kabla ya jua, mwezi na nyota. Kwa mchunguzi wa dunia, huu ndio uliokuwa utaratibu wa kuonekana kwazo; na kwa uhusiano naye kiumbe msingi, ingawa kabisa alikuwepo kwa mamilioni ya miaka kabla ya zama za Adamu. Muda wa mizunguko ya dunia kwa jua wakati wa kabla ya siku ya kwanza si wazi; lakini ushahidi unaodhihirishwa na rusu za mawe ya dunia yetu zinaonyesha kuwa kipindi kilikuwa kimeendelea zaidi "(ELPIS Israeli, uk. 10).

Nadharia ya Mageuzi inachocheleza mafundisho ya Biblia juu ya Uumbaji, na ingawa bado inasalia nadharia na inakosa ushahidi, ni shauku iliyopitishwa na dunia ya kisasa ya ubahili ambayo inakataa kukiri wajibu wowote kwa Mungu. Kukubali simulizi ya Biblia, ni kuidhinisha ukweli wa Muumba; na wakati hayo yatajiri, kuna kukiri kimyakimya kuwa Yeye ni lazima Aheshimiwe, Alisikilizwe, na kutiiwa. Mwanadamu wa kisasa hataki kufanya hivyo, na kwa hivyo anajitihadi kueleza Uumbaji kwa jinsi ya kutomhusisha Mungu. Hii, tunaamini, ndio maana kuna wingi wa wanamageuzi katika taasisi za kisayansi na elimu, na ukiritimba mfanisi wa maoni ya mageuzi katika vitabu vya kisasa. Kwa upande mwingine, hii imesababisha nadharia ya kuwa na miungu ya mageuzi ambayo ni maarufu katika baadhi ya duru za kidini, na, kwa bahati mbaya, imepata tajamala miongoni mwa wachache wa Wakristadelfiani wa falsafa. Hakuna haja ya kuona aibu juu ya mafundisho ya Uumbaji. Ukitafakari, kuwepo kwa Muumba ni mantiki bora zaidi kuliko nadharia ya mageuzi. Tafakuri kwamba Kuumbwa kwetu kugumu na kwa ajabu kulifanyika kwa nasibu tu bila mpango ni kupendekeza  nadharia inayohitaji ushahidi mkubwa kuliko chochote kilichoendelezwa na Maandiko Matakatifu, ikiwa ni pamoja na miujiza ya ajabu. Kila nyanja ya biolojia (uwanja wa kisayansi ambao nadharia ya mageuzi inaendelezwa zaidi) inaweza kuelezwa katika suala la Uumbaji wa Biblia kwa urahisi zaidi kuliko katika zile za nadharia ya mageuzi ambazo bado "hazina viunganishi" vingi.

Kama  yeyote ana shaka kuhusu haya, twayaelekeza mawazo yake kwa kitabu cha kiada juu ya Biolojia, kilichooandikwa hasa kwa ajili ya shule na wanasayansi ambao wanaamini kuwa Mungu aliumba maisha duniani kwa siku sita za mchana miaka ipatayo 6,000 iliyopita. Kitabu hiki cha kurasa548, kinaitwa: Biolojia: Upekuzi wa Mpangilio katika Utata. Utangulizi wa vitabu hiki chaa kiada ni pamoja na maoni yafuatayo:

"Wengi wa wanabiolojia wa kisasa hupendelea falsafa ya mageuzi ya asili kama maelezo ya ukweli sahihi ya biolojia. Kwa kweli, wengi wamekuwa na ujasiri mwingi katika jambo hili hivi kwamba wao hata husisitiza kuwa mageuzi ni ukweli wa sayansi. Lakini madai haya hayajawahi dhihirishwa kamwe na kwa kweli, katika hali ya kawaida ya mambo, hayawezi hata kuthibitika."

Leo pia kuna kundi kubwa la wanabiolojia na wanasayansi wengine ambao wanaamini kwamba uumbaji maalum ni falsafa ya busara na inayoridhisha zaidi ya asili kuliko ile ya mageuzi. Wengi wa watu hawa ni wanachama wa Creation Research Society, shirika la takriban wanasayansi 350 (wa angalau Shahada ya MS, nawanaowakilisha taaluma nyingi katika sayansi za kifizikia na kibiolojia) waliojitolea kwa utafiti na uchapishaji katika kuunga mkono uumbaji dhidi ya mageuzi kama maelezo yaliyo ya uwezekano zaidi wa asili ".

"Ule mwanga mkubwa utawale mchana" — Kwa Kiebrania, meowr (umoja wa meourouth, sura ya 14) ni neno moja na lile lililotumika kwa taa ya kinara katika Hema — Kutoka 25: 6; Law. 24: 2; Hes. 4: 9, 16. Kazi ya mwanga huu mkuu, jua, ilikuwa kutawala kama Mfalme; kwa maana liliteuliwa "kutawala mchana." Mwandishi wa Zaburi anarejelea jua kama "bwana harusi" na "shujaa" anayejitokeza kutoka gizani na kutawala yote chini ya ushawishi wake (Zaburi 19: 5-6). Jua, kama mtawala mkubwa wa mbingu, kimfano linawakilisha Bwana (Zab. 84:11), na, Bwana Yesu Kristo kama mtawala mkubwa wa Mbingu ya Milenia. Kwa hivyo kiti cha enzi cha Daudi chasemwa kuwa kinachodudumu kama "jua mbele zangu" (Zab. 89:36). Daudi, akitarajia utawala wa Mwana wake mkubwa katika kiti chake cha enzi alisema: "Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua lichapo, Asubuhi isiyo na mawingu." (2 Sam 23: 4.); na Malaki alitabiri: "jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake" (Mal 4: 2). Yohana alitoa wasifu wa Bwana kama "mwanga wa ukweli" (Yohana 1: 9); na katika porojo na wanafunzi wake, Yesu alisema: "Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima" (Yohana 8:12). Tena, katika tukio jingine, akasema: "Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu." (Yohana 9: 4-5). Kimithali, usiku ulikuja wakati Bwana aliondoka kwenda juu mbinguni, na mchana utakucha atakaporudi kutoka humo. Kama jua linavyotawala mchana, na kuharibu giza, na kuleta mwanga, ndivyo Bwana atakavyofanya katika ujio wake siku zijazo. Atayaangamiza matendo ya giza, na atadhihirisha "nuru ya elimu ", na kuleta joto, furaha na maisha kwa watu wote.

Jua liliteuliwa katika sehemu hii siku ya nne, na wakati wa kuhitimisha milenia ya nne baada ya Uumbaji, Bwana Yesu, kama "mwanga wa ulimwengu" alijitokeza kati ya watu.

"Na ule mdogo utawale usiku" — Mwezi ni mfano wa Iklezia, bibi harusi wa Kristo, kama ilivyofafanuliwa kuwa "Mzuri kama mwezi" (Wim. 6:10). Ni ishara mwafaka ya ajabu kweli! Mwezi hauna mwanga wake binafsi, bali unautegemea mwanga wa jua, unaonurisha kutoka kwa giza za mbingu jirani. Ni kimwezi cha dunia, kipande kidogo cha sayari hiyo, iliyotengwa kutoka kwa ukubwa wake, na kuangaza kwa utukufu wa jua lisilokuwepo. Umeelezewa kama "Shahidi aliye mbinguni mwaminifu" (Zab. 89:37). Ni kwa njia gani ni vile? Ni mwanga msafi mweupe, unaong'aa vizuri kutoka mbingu zilizotiwa giza, yaonyesha kuwepo kwa jua wakati limetoweka. Ndivyo pia Iklezia katika ushahidi wake kuhusu kuja kwa Kristo akiwa hayupo. Mwezi huangaza subui moja tu ya utukufu kamili wa jua, kama malaika wanavyobeba sehemu kidogo tu ya ukamilifu wa utukufu wa Kristo. Hata na mwezi unapong'ara na kufifia daima una somo unalolifundisha. Unazungumzia hali ya kiroho ya Iklezia katka ongezeko au upungufu. Kuna onyo na matumaini katika haya. Mwezi katika mwanga wake kamili unazungumzia Iklezia katika utukufu kamili wa usitawi wa kiroho na mwanga. Lakini mwezi haudumu katika hali hiyo, unafifia hatimaye. Na imekuwa kumbukumbu isyoepukika ya Iklezia, hata kama imewakilishwa na Israeli kama taifa, au na jamii mbalimbali ambazo zimeasisiwa kutoka kwa mataifa mengine. Kwa hivyo, wakati mwingine, wakati Iklezia iko "katika hali yake ya ukamilifu," tukumbuke kwamba hakuna muda wa madaha, kwani mwanga waweza kufifia. Na wakati Iklezia ni dhaifu, na mwanga wake kufifia, tukumbuke kwamba mwezi haubaki katika hali hiyo, na hivyo inatupasa kutekeleza wajibu wetu katika kuendeleza Iklezia kikamilifu. Mwezi hutumika mara nyingi kama ishara katika Maandiko. Tafakari mfano mzuri wa Isaya 30:26: "Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile Bwana atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha yao." Siku hiyo, bibi harusi wa Kristo atang'aa katika utukufu kamili ya Mpenzi wake; hali utukufu wa bwana harusi utakuwa mkamilifu, kama "mara saba." Aya hii inaweza tu kutafsiriwa kimfano, kwa maana kama ikutumika kwa jua na mwezi halisi, na kufundishwa kwamba jua litakuwa na joto mara saba zaidi ya lilivyo leo, maisha yangeangamizwa kabisa kutoka uso wa dunia.

Wakati huo huo mwezi hutawala usiku. Unafanya hivyo kwa maana halisi: kwa maana hali ya maji kujaa na kupwa baharini hudhibitiwa na tendo la jua na mwezi kwa pamoja; na hali ya upwaji na mtiririko wa baharini ni muhimu kwa maisha ya duniani. Na umuhimu wa kiroho? Bahari huwakilisha mataifa na watu (Isa 57:20; Ufunuo17:15), na upwaji na mtiririko wa hayo (ona Matendo 17:26), ni "kwa ajili yenu" (wateule) (2Kor 4. : 15). Kuinuka na kuanguka kwa mataifa ni kuambatana na kusudi lake Yehova ukitangamanisha na watakatifu.

"Akafanya na nyota pia" —Musa hajadili tendo la uumbaji, lakini uteuzi wa vyombo hivi vya mbinguni kama "ishara" (aya ya 14) Nyota zimetumika katika Neno kuashiria wakuu. Kwa hivyo wale waongozao wengi kutenda haki, wanaahidiwa kuang'ara katika siasa za mbingu ya baadaye "kama nyota milele na milele" (Dan 12: 3.). Mzao wa Ibrahimu ni unatajwa kama "nyota kwa wingi," na, ingawa hakuna mtu anayeweza kuzihesabu nyota, tunaambiwa kwamba Yehova amefanya hivyo, akaziita zote kwa majina (Zaburi 147: 4). Yeye anajua idadi ya waliokombolewa; na anmjua kila mmoja kwa undani jinsi ya kuweza "kuwaita wote kwa majina." Paulo anatumia nyota kama mfano wa watakatifu, na kutangaza kwamba "maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota" (1 Kor. 15:41). Kwa hivyo, Kristo alieleza katika mfano wake jinsi tuzo kuu litapewa wale waliofanya kazi kwa bidii zaidi na kwa ufanisi katika utumishi wake (Luka 19: 16-26).

AYA YA 17

"Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi" — Aya hii inahusiana na "mianga miwili mikubwa" ya aya ya 16. Wao ni wabeba-taa walioainishwa kuiangaza nchi. Hiyo, pia, ni kazi ya Kristo na Iklezia kama jua na mwezi za kimithili. Wakati Iklezia inashindwa kutoa mwanga, inashindwa katika utenda kazi wake muhimu. Tungechukuaje iwapo jua na mwezi zingeshindwa kuangaza na kufichua uzuri wa viumbe?

AYA YA 18

"Na kuutawala mchana na usiku" — Jua na mwezi asili zina mamlaka juu ya mchana na usiku; na vivyo hivyo kwa jua na mwezi za kimithili. Angalia aya ya 16 hapo juu.

"Na kutenga nuru na giza " — Jua huangamiza giza kama Kristo atakavyoangamiza giza la ujinga na kosa katika kurudi kwake. Iklezia lazima ifanye hivyo sasa; ikibagua wazi kati ya ukweli na kosa, na njia ya haki na ya uovu. Paulo aliandika: "Bali ninyi, ndugu, hammo gizani...kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza." (1 The. 5: 4-5. ); "enendeni kama watoto wa nuru" (Efe 5: 8.).

"Mungu akaona ya kuwa ni vyema. " — Aliona kuwa ilikuwa vizuri kwamba mwanga wa jua ulidhibiti na kuangamiza giza, bila kujali kama ulichomoza moja kwa moja kutoka kwa sayari hiyo, au ulikuwa ukiduta kutoka kwa mwezi. Katika maombi ya kiroho ya ukweli huu, Yohana anasema: "Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza (maana halisi: "kushikilia"ili kuangamiza) halikuiweza" (Yohana 1: 5). Kazi ya mwanga ni kulitawala giza ili kuliangamiza, na hili ndilo Mungu Alilotangaza kuwa zuri. "mwezi" wa Iklezia lazima uone kwamba umeangaza mwanga wa kutosha wa jua ili kufanya hivyo; kwani vinginevyo si "vyema." "Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo!" (Mathayo. 6:23).

AYA YA 19

"Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne " — Ilhali Siku ya Tatu ilishuhudia utengano, Siku ya Nne iliona kutawanyika kwa mwanga uliotiririkakutoka kwa jua na mwezi kuangaza nchi. Katika mithili, hii ilitimia katika tangazo la Injili kwa ulimwengu wote (Matendo 28: 30-31; Kol 1:23). Kristo alionekana wakati wa kuhitimisha milenia ya nne kutoka Uumbaji, na kwa kutokea kwake duniani, mwanga wa ukweli uliangaza kwa nguvu zaidi kuliko ulivyoangaza awali.

Siku Ya Tano: Wanyama wa Majini na wa Angani — Aya za 20-23

Siku ya tano, kulikuwa na mwendelezo zaidi wa kazi ya Mungu: bahari ilianza kufurika na maisha, na nyimbo za ndege zilisikika katika anga ya juu. Mahali pengine katika Neno, wanyama wa majini na angani wametumiwa kimfano kuashiria watu wa mataifa. Kwa mujibu wa madhumuni ya Mungu yaliyoaguliwa katika siku sita za uumbaji, milenia ya tano iliona Injili ikizagaishwa kwa mataifa. Ni muhimu kuwa nambari tano daima huhusishwa na neema. Katika huruma ya Yehova, upeo wa wokovu wake ulipanuliwa wakati wa milenia ya tano kutoka uumbaji, ili kuhusisha mataifa mengine katika mpango wake wa ukombozi.

AYA YA 20

"Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai" — Tunasoma haya kana kwamba wakazi wa kina waliumbwa kutoka ndani ya maji! Hata hivyo, maneno "yajawe kwa wingi" yemetafsiriwa kutoka kwa neno moja, sheretz, likiashiria "kutanda". Biblia ya Darby yatafsiri hivi:

"Acha maji yatandwe". Pembe ya Biblia ya Revised Version inasema: "Acha maji yatandwe na utandu na viumbe vyenye uhai." Wanyama wa majini waliumbwa kutoka kwa "mavumbi ya ardhi" kwa pamoja na viumbe  wengine wote duniani, na marejeleo katika Mwanzo sio juu ya uumbwaji wao , lakini kwa nguvu zao za kiajabu za uzalishaji ziazozidi kustaajabisha katika maisha ya samaki tangu wakati huo. Bahari ni chanzo kikubwa cha chakula kwa binadamu; mamilioni ya samaki hutolewa humo kila mwaka, na bado bahari inaendelea kuzagaa na maisha, isipokuwa pale ambapo uchafuzi umeharibu uwezo wake. Katika kuwabariki Efraimu na Manase, Yakobo alisema, "Na wawe wingi wa watu kati ya nchi" (Mwa 48:16). Katika Kiebrania, kama ilivyoelezwa katika pembe ni, "Kama samaki wanavyoongezeka."

Neno "kusonga"  tena ni neno sherertz, likimaanisha "kutanda" au viumbe vinavyotanda.

"Kiumbe mwenye uhai" limetafsiriwa kutoka chayiah nephesh, nafsi zenye uhai. Kwa hivvo kirai

hicho chaweza kufasiriwa kiasili hivi: "Acha maji yatande na utando wa nafsi zilizo hai."

Katika Elpis Israeli, uk. 32, Ndugu Thomas anena juu ya ukanushaji wa nadharia ya maish ya roho wa milele . Anaandika:

"Mtu kwa hivyo ni mwili wa uhai katika maana ya kuwa mnyama, ama kiumbe mwenye uhai— nephesh chayiah adam. Kama mtu wa asili, hana ukuu mwingine juu ya viumbe Mungu aliowafanya zaidi ya mpangilio wake wa kipekee unayomtwika. Musa hatofautishi baina yake na wao; kwani anawatambua wote kama viumbe walio hai, wakipumua pumzi ya maisha. Kwa hivyo, ikitajwa kihalisi, anasema: "'Elohim alisema, maji yatazalisha kwa wingi sheretz chayiah nephesh, nafsi inayoishi ya watambaazi'; na tena, 'kal nephesh chayiah erameshat, viumbe vyote hai vitambaavyo.' Katika mstari mwingine duni na izae nephesh chayiah, nafsi hai kwa jinsi yake, na mifugo, nacho kitambaacho, na mnyama wa nchi, 'nk .; na 'lekol rumesh ol eretz Asheri bu nephesh chayiah, kwa kila kitambaacho juu ya nchi ambacho (kina) ndani yake pumzi inayoishi' (Mwa 1: 20,21,24,30), hiyo ni ni pumzi ya maisha. Na mwisho, 'Lolote Adam alichoita nephesh chayiah, hilo lilikuwa jina lake (Mwa 2:19). "

Juu ya ushahidi huu, samaki, ndege na wanyama wanamiliki "nafsi zilizo na uhai" kwa pamoja na binadamu, na kuonyesha kwamba nadharia ya kinachojulikana kama roho isiyokufa ni ubunifu wa mawazo, na haijulikani kwa Maandiko. Kwa ufafanuzi wa sauti kuhusu "nafsi" angalia Eureka, toleo la 2, uk. 246-253.

"Na ndege waruke juu ya nchi " — Angalia ufafanuzi wa pembeni: " Na ndege waruke juu ya nchi". Aya hii inaeleza nia ya Mungu, na si matendo yake ya ubunifu na ambayo kwayo walisababishwa kuwa. Malengo yake yalikuwa, kwamba bahari ziwe na wingi wa samaki; na kwamba ndege waruke juu. Toleo la A.V. lina maana kwamba maji yangezalisha samaki na ndege, lakini hilo limesahihishwa na maandishi ya Kiebrania, kama pembe inavyoonyesha.

"Katika anga la mbingu" — Kwa maana ya asili aya hii inasema: "Maji yatande (pamoja na) makundi ya nafsi hai, na ndege ambao wanaweza kuruka kote juu ya nchi, na juu ya anga la mbingu" (angalia Biblia ya Interlinear ya Kiebrania, Kigiriki na Kiingereza). Aya inaeleza kuzidisha kubwa ya maisha, hususan katika maeneo ambayo hapo awali hayakumilikiwa. Inabashiri ongezeko kubwa katika idadi ya watu duniani, na enzi ya ugunduzi na uenezi ambayo ilikuwa hulka ya maisha katika milenia ya tano ya historia ya dunia. Ujumbe wa Injili haukuwa tena kwa Wayahudi tu, bali ulienea kwa Mataifa mengine pande zote.

AYA YA 21

"And God created" — Kitenzi ni bara kama katika aya ya 1, na inaelezea jinsi Mungu Alivyofanyiza lengo lake kama ilivyoonyeshwa katika mstari wa 20.

"Nyangumi wakubwa" Tanninim, kutoka kwa mizizi, tan, likimaanisha kurefusha, au kunyoosha (Nguvu); na hivyo kuonyesha ukubwa wa kiumbe kilichotengenezwa. Toleo la R.V. linaelezea kuwa ni "madubwana ya bahari," na, kama neno lilivyotafsiriwa mara nyingi katika Biblia, ni neno la kawaida la viumbe wakubwa wa bahari ikiwa ni pamoja na nyangumi, mamba, na kadhalika. kiendacho

"Na kila kiumbe chenye uhai" — Maneno haya (nephesh chayiah) yanajumuisha viumbe wengine wote wa baharini.

"Kiendacho" — Hii ndio tofauti kati ya maisha ya mimea iliyoumbwa siku ya tatu, na maisha ya wanyama ambayo sasa yalikuwa yakisababishwa kuwa.

"Ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi" — Haya yaweza elezwa kwa njia halisi: "Ambavyo na maji vilitanda." Maji "hayakuvisababisha," kwa maana vilifanywa kwa "mavumbi ya nchi"; lakini maji yalisababishwa kutanda na kila aina ya maisha ya majini.

"Kwa jinsi zao " — Hii ni kauli muhimu sana, na inatupilia mbali mara moja nadharia zote za mageuzi. Hakukuwa na andao la mpito kutoka ukoo mmoja hadi mwingine, lakini viumbe vyote vilizaa "kwa jinsi zao." Kauli hii haitoi nafasi ya mkengeuko kama mageuzo kutoka kwa babu mmoja, lakini inaonyesha kuwa kila aina ya maisha ilikuwa imeumbwa kivyake. Hata hivyo kuna upeo wa maendeleo ndani ya jamii, hivi kwamba iwezekane, kwa uzalishaji, kuboresha ubora wa aina fulani mnyama, lakini farasi abaki farasi, kondoo awe kondoo, mbwa awe mbwa, hata licha ya kuzaana baina ya koo tofauti.

"Na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake" — Angalia aya  20. Na " na kila ndege wa angani" ya Sura ya 2:19.

"Mungu akaona ya kuwa ni vyema" — Mungu alipanga Uumbaji ili kwamba dunia iweze kumilikiwa; na tendo lake la asili liliafiki kuwa na usawa katika hulka ambayo mtu, kwa uchoyo wake na ujinga, ameangamiza. Kwa udhalimu wake mtu ameangamiza wanyama wengi walioumbwa mwanzo, na kuendelea kuwepo kwa baadhi ya wanyama hao kumebaki katika hatari kwa ajili ya uchoyo wa binadamu na kutojali.

AYA YA 22

" Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi" — Kuzidisha na mwendelezo kulianza katika siku hii ya tano. Angalia maelezo katika aya ya 20 hapo juu.

AYA YA 23

" Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano" — Katika uakisi, "siku" hii anatuelekeza enzi ya milenia ya kwanza baada ya kujulishwa kwa Kristo ulimwenguni. Ujumbe wa Injili ulisambaa zaidi. Pia kilikuwa ni kipindi cha kuongezeka kwa wakazi wa dunia pamoja na kuzidisha uvumbuzi  na ugunduzi.

Siku ya Sita: Wanyama wa Duniani — Aya za 24-27

Siku hii ya sita ilishuhudia uunmbwaji wa wanyama kuendelea hadi mtu. Kilele chake kilikuwa ni kutokea kwa mtu "katika sura na mfano wa Mungu," akifuatiwa na uumbwaji wa mwanamke, na amri: "Wakatawale". Hitimisho la siku ya sita lilishuhudia ndoa kati ya wawili walioumbwa, ili wapate kuwa na umoja kama mmoja, na zoezi la mamlaka juu ya viumbe vya chini. Tendo hili la mwisho la ubunifu lilibashiri nia ya Yehova katika kukamilisha milenia ya sita kutoka uumbaji, wakati, tena, kutakuwa na ndoa kati ya Kristo na Bibi Harusi wake, nao, wakiunganika kama mmoja, watatumia mamlaka juu ya wenyeji wa dunia ambao hufa. Tutaona kwamba tendo hili la mwisho la ubunifu, na tamko la Mungu lililoandamana nalo, ndio msingi wa kusudi la Mungu kama ilivyotangazwa katika Injili, na kwamba imeashiriwa mara nyingi katika Maandiko.

AYA YA 24

"Mungu akasema, Nchi na izae" — Kama mimea (mstari wa 12), wanasemekana kuzaliwa na nchi, miili yao ikiwa sehemu ya mali ya dunia; hii haingeweza kusemwa juu ya samaki katika mahusiano na maji, na hivyo maelezo tofauti yalibidi kutumiwa katika aya ya 20.

"Kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. " — Hii ni nephesh chayiah, kama katika aya ya 21 (angalia maelezo), na hapa ni jina pana la wanyama wa nchi, wakiwa wamebanwa na yaliyotangulia: "viumbe hai vinavyochipuka kutoka nchini" Makundi matatu  yametolewa katika aya ya 25.

AYA YA 25

" Mungu akafanya" — Kitenzi si bara, fanya, bali asah, tengeneza, tenda, ama teua. Hiai ni teuzi tatu katika aya hii. wanyama pori, wanyama wa kufugwa, na wanyama watambaao.

"Mnyama wa mwitu kwa jinsi zake" — Maana asili  ya "kiumbe hai" cha dunia (Kiebrania chayiah), na kwa ujumla linaloeleweka kumaanisha wanyama pori kinyume na waliofugwa, au wanyama wa nyumbani.

"Na mnyama wa kufugwa (ng'ombe) kwa jinsi zake" — Neno behemah lina maana pana zaidi ya neno letu ng'ombe, na bila shaka linahusu wanyama wakubwa, wa miguu minne. Linatokana na mzizi unaoashiria "kuwa bubu,"

hiyo ni kama wanyama bubu wa kufugwa ukilinganisha na mtu.

"Na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. " — Kiebrania remes, ni "kitu kitambaacho," ikimaanisha mtambaazi, nyoka, mijusi, minyoo, na kadhalika.

AYA YA 26

"Mungu akasema, Na tumfanye mtu" — Kama tulivyoona katika uk. 26-28, nomino ya ya wingi ya Elohim wakati mwingine hutumiwa na kitenzi cha umoja, na mara nyingine na kitenzi cha wingi. matumizi ya vitenzi vya umoja na wingi kwa uhusiano na nomino hii ya wingi ni muhimu.Inaonyesha  kuwa ingawa Elohim ni wengi, na wameunganika kama kitu kimoja, wao pia wana uwezo wa kufanya uamuzi wa kujitegemea na utekelezaji. Hata hivyo, mamlaka wanayotumia, na utukufu wanaoonyesha, ni kutoka kwa  Mmoja, hata Yehova. Katika aya iliyo mbele yetu, kitenzi hiki kiko katika wingi, kuonyesha wingi wa mawakala. Matumizi ya wingi ya kiwakilishi "sisi" huwakanganya Waamini wa Utatu wakiamini kuwa inaunga mkono mafundisho yao; lakini hakuna chochote katika matumizi yake kuashiria utatu wa mawakala kuliko matumizi mengine yoyote ya wingi. Marejeleo ya Uumbaji yanayopatikana katika Ayubu 38: 7 yaweza kupendekeza kwamba "sisi" inahusiana na "nyota za asubuhi" na "wana wa Mungu" waliopiga makelele kwa furaha kwa utukufu wa Uumbaji. Matumizi sawa ya lugha katika uhusiano na Elohim yanapatikana katika Mwanzo 03:22; 11: 7; Isa. 6: 8 na kwingineko. Katika Mwanzo 3:22 taarifa hii imerekodiwa: "Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya." Mtu hangeweza kuwa kama mmoja wa Utatu; lakini angeweza kuwa kama mmoja wa malaika, kwa kuwa ni wazi kwamba wao walipata hadhi yao ya sasa kwa kupitia majaribio. Kristo aliahidi kwamba walioidhinishwa watakuwa "sawasawa na malaika" katika Enzi ijayo (Luka 20:36).Katika Zaburi 8: 5, neno hilo hilo Elohim limetafsiriwa "malaika." Na linganisho na Hesabu 12: 8 na Matendo 7:38, au cha Mwanzo 32:30 na Hosea 12: 3-4, litaonyesha kwamba neno Elohim, lililotafsiriwa "Mungu" linahusiana na malaika, wawakilishi wa Muumba Mkubwa .

"Kwa mfano wetu" — Hiyo ni, katika mfano wa Eloahim ambao Baba aliwatumia katika kazi za uumbaji. Angalia kipengele katika  Elpis Israel kilich na kichwa: Man In the Image And Likeness Of The Elohim, uk. 37-41. Neno tselem lina maana ya kivuli, ama mfano, ufananishaji. Neno hili limekaririwa katika Danieli 2

likihusiana na mfano, na kwa hivyo linahusisha kusawiria utokeo. Mwanzo 5: 3 inasema "Adam akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake" ambamo matumizi yake yanadhibitika hapa. Mtu aliumbwa "kwa mfano" wa Eloahim, na walivyo "watoto wa Mungu," picha ni ya Mungu (ingawa hulka ya mwanadamu sio). Yakobo anafafanua kwamba

"sisi tumefanywa kwa mfano wa Mungu," "hata Baba" (Yakobo 3: 9). Juu ya Bwana Yesu Kristo pia, tunasoma kwamba yeye ni "chapa ya  nafsi yake (Mungu) mtu" (Ebr 1: 3). Yehova anaishi kwa mwili mbinguni.

Kwa mfano wetu" — Hii ni kauli muhimu sana inyofundisha kwamba mtu aliumbwa kwa mfano wa Mungu,

kutafakari tabia ya Mungu. Mfano ni demuth kwa Kiebrania kutoka mzizi damah, kuleta pamoja, kulinganisha. Limetafsiriwa "mfano" katika Ezekieli 1: 5, na hapo limetumika kuhusisha makerubi. Katika Isaya 40:18, 25; 46: 5, limetumika katika uhusiano na Yehova. Uzingatifu wa vifungu hivi utaonyesha kwamba damuth limefafanua uwezo, mamlaka na hadhi. Mtu aliumbwa kwa mfano wa Baba, akapewa hadhi sawa na Yake juu ya viumbe vyake an akapewa uwezo wa kutafakari tabia ya Mungu. Kwa hivyo, tabia ya mwanadamu lazima ilingane na sura yake iliyo kama ya Mungu, kama Yakobo anavyopendekeza (tazama Yakobo 3: 9). Ilhali Adamu aliumbwa kwa "sura na mfano wa Eloahim," kizazi cha Adam kinarithi matokeo ya Anguko. Seth alikuwa "katika sura yake na mfano wake" Adam (Mwa 5: 3), na siyo ile ya Mungu.

Kwa hivyo, tangu Anguko imekuwa vigumu kwa mtu kutafakari ubora wa Mungu katika ukamilifu wake, na hii imehitaji malezi ya Mtu Mpya ambaye atatoa picha na mfano halisi wa Mungu. Kristo aliyakamilisha haya kwa kuushinda mwili (Rum 1:. 3; Ebr 1: 3; Kol 1:15.). Ndugu Thomas anaandika: "Wakati picha, basi, inaashiria muundo au sura, 'mfano' unahusiana na mpangilio wa akili, au uwezo ... uwezo wa kiakili wa Adamu ulimwezesha kutafakari na kupokea mawazo ya kiroho, ambao ulimwelekeza kwenye heshima, matumaini, nidhamu, usemi wa maoni yake, upendo, na kadhalika. Sethi alikuwa na uwezo wa onyesho sawa la kiakili kwa matukio ya kimaadili; na uchukuaji wa tabia ya baba yake. Kw hivyo alichukua mfano na pia picha ya Adamu; na, kwa maana hiyo, wote wawili walikuwa 'katika mfano wa Elohim.'

"Lakini, ingawa Adamu 'alifanywa kwa mfano na sura' ya 'Watakatifu,'  Mfano huu umeharibiwa kiasi kikubwa hivi kwamba, vizazi vyake sasa vinawasilisha mfano hafifu wa yote mawili. Harakati endelevu ambayo karibu haidhibitiki ya 'sheria ya dhambi na kifo '(Rum. 7:23), iliyoundwa na wanafalsafa na kuitwa 'sheria ya hulka', ambayo uwepo wake umeunganika na uchumi wetu sasa, umepoozesha sana picha, na kufuta mfano wa Mungu, ambayo mtu wa awali aliionyesha. Ilihitaji, kwa hiyo, onekano la Mtu Mpya, ambaye kwake sura na mfano lazima zijitokeze upya, kama hapo mwanzo. Huyu alikuwa ni 'binadamu Kristo Yesu,' ambaye Paulo anamwita 'Adamu wa mwisho.' Yeye ni 'Sura ya Mungu Asiyeonekana' (Kol 1:15), 'ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake' (Ebr 1: 3.)" (Elpis Israeli, pp 39. 40).

"Wakatawale " — Ilikuwa nia ya Muumba kwamba mtu awe na mamlaka juu ya viumbe wengine wake, lakini dhambi ilichelewesha kufikia lengo hilo. Hata hivyo nia hiyo haikutupiliwa mbali. Amri hiyo ilinukuliwa na Daudi baada ya kumshinda Goliathi (Zaburi 8: 6), kufundisha kwamba nguvu iliyomwezesha kupata ushindi kwa jitu itaibuka mshindi juu ya dhambi, na kuleta utawala ulioahidiwa wakati wa mwisho. Ushindi huu uliwahiwa na Bwana Yesu (Ebr. 2:14), na kwa kuupata yeye aliweka msingi kwa zoezi la mamlaka juu ya ya viumbe wengine wote. Katika Waebrania 2: 8, Paulo ananukuu Zaburi 8: 6, na kusisitiza kwamba utimizaji huo haujatimizika. Amri hii ya kiiElohim, ilionyesha mapenzi na kusudi la Mungu katika uumbaji. Mungu alipanga kwamba mtu lazima atengenezwe katika sura na mfano wa Elohim, na kutumia mamlaka juu ya  viumbe wengine wa hali ya chini. Mamlaka haya yalitekelezwa kiasi kabla dhambi haijaingia ulimwenguni (Mwanzo 2:19); lakini matukio ya dhambi yalizuia udhihirisho wake kamili. Hata hivyo, Mungu hakutupilia mbali kusudi lake. Kutimizika kwa kina kutapatikana wakati ambapo Zaburi itatimizwa: "Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako." (Zab 2: 8); "Na awe na enzi toka bahari hata bahari, toka mto hata miisho ya dunia" (Zab 72: 8.).

Mamlaka kamili juu ya viumbe ina maana ya hali ya usawa na Elohim kwa upande wa wale wanaoyatumia. Hawa aliyashikilia halafu akayapoteza (Mwa 3:16).

Mtazamo wake umelinganishwa na Paulo na usikivu wa hiari wa Bwana Yesu, ambaye, kwa kutambua kwamba "usawa na Mungu" haukuwa "kitu cha kufumbata ," alijikabidhi kwa mapenzi ya Mungu, na kupokea jina na hadhi zaidi ya  wengine wote.

Katika amri hii: "Uwe na mamlaka," Injili ilihubiriwa kwa Adamu na Hawa kwa wazi kabisa, hivi kwamba azimio hilo ndilo msingi wa sehemu kubwa ya ufafanuzi wa Agano Jipya. Angalia Uwe Na Mamlaka.

"Wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. " — Ilhali Adamu na Hawa huwakilisha Adam wa Pili na bibi harusi wake wa kikwi; viumbe wa kiwango cha chini vinawakilisha viumbe hai ambao watamilikiwa  na kundi la kwanza. Matumizi ya ishara ya samaki, ndege, wanyama, nk, kuashiria watu, kwapatikana katika mara nyingi Maandiko. Yesu alimwambia Petro kuwa angemfanya mvuvi wa watu; na katika mfano wa mvuo wa samaki, madaraja mbalimbali ya watu ambao wanafuliwa katika wavu wa Injili wanawakilishwa na aina mbalimbali za samaki. Ni muhimu, kwamba katika agano Mungu alilofanya na Nuhu, linalofikia mbele kwa milenia, aliwajumuisha hasa waliokuwa katika Safina, wote wa familia ya Nuhu (mwakilishi wa familia ya Kristo), "na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili "(Mwa 9:15). Ni bayana kuwa, viumbe wa ngazi ya chini katika jahazi waliwakilisha viumbe hai katika milenia ambao Kristo na wafuasi wake waliosifika wangetekeleza mamlaka juu yao. Yaani Mungu hakufanya uhusiano wa agano na wanyama, lakini alifanya hivyo kwa misingi ya umuhimu wake. Hivyo, malezi ya Adamu na Hawa "kwa sura na mfano wa Eloahim," ndoa yao pamoja, na amri ya mamlaka waliopewa, zilitoa ubashiri wa kusudi la Mungu kwa mwanadamu. Katika hitimisho la milenia ya sita, kutakuwa na Mtu (Bwana Yesu) na Mwanamke (Bibi harusi wake wa kikwi) wakiunganishwa katika ndoa, na wao watapewa mamlaka juu ya viumbe wa kimithili wa Yehova wa mataifa (mfano angalia Dan 4.: 11-12, 20-22).

AYA YA 27

"Mungu akaumba" — Hii ni mara ya tatu na ya mwisho ambapo neno hili, bara, linajiri katika sura hii (angalia aya za 1,21). Katika kila tukio lina maana tofauti na ile iliyotangulia kutajwa, na kwa hakika halionyeshi mwendelezo na lile la awali kuwepo, kama wanafalsafa wa mageuzi wanavyopendekeza. Badala yake, mkazo wake ni juu ya mkondo mpya unaosababishwa na uumbaji. Katika Hesabu 16:30, maneno, "Akiumba kitu kipya" yanawakilisha katika Kiebrania asili, "Umba kiumbe." Hakuna nafasi ya maendeleo ya mageuzi kutoka kwa wanyama wa chini katika tamko la Mwanzo 1:27. Nadharia yoyote ile iwe ya miungu ama ya mageuzi ni kinyume na Neno la Mungu.

"Mtu kwa mfano wetu" — Ni muhimu kuona tofauti katika viwakilishi kwa aya hii. Cha binafsi, kiume "yeye" kinaashiria mume aliye mfano wa Mungu, wingi "wao" ni maendeleo kutoka kwa mume wa awali, kama nilivyoeleza katika sura ya 2. Ni mtu aliye katika sura ya Mungu, na anayestahili kutekeleza mamlaka juu mke. Hadhi yake katika familia yake ni ile ya Yehova katika familia ya Mungu. Paulo alifundisha kwamba pahala pa Mungu panapaswa kuwekwa wazi, hasa katika ibada, wakati ambapo hadhi ya mume lazima ikiriwe. Alisema: "Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa (yaani katika ibada), kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume." (l Kor 11: 7-9.).

Kazi ya siku ya sita ilibashiri utimilifu wa kazi ya Mungu wa viumbe vyake vipya. Katika uumbaji wa awali, mtu aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Katika uumbai mpya, utaona sura ya Kristo ikidhibitika kikamilifu  katika muumini: " yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake" (2 Thess. 1:10); " Atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo" (1 John 3:2). Kama Mchumba wa Kristo, waumini wamechaguliwa tangu asili wafananishwe na mfano wa mwana wa Mungu (Rum. 8:29), kwa kuwa yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana (Kol 1:15). Wakati huo huo, kwa nguvu ya Roho-neno (neno hilo hilo lililotokezea katika uumbaji), Kristo anaumbika ndani yetu (Gal. 4:19).

"Kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. " — Taaifa hii inatueleza jambo la pili ya mambo mawili ya msingi kuhusu mwanadamu. Kwanza ni kwamba mtu amefanywa kwa mfano wa Mungu; pili, alikuwa katika jinsia zote mbili. Mungu alikuwa na madhumuni mawili makuu katika umbo: kwanza, ni kwamba sharti lionyeshe utukufu wake; na pili, kwamba dunia nzima lazima kujazwa na utukufu huu. Uumbaji wa Adamu kwa sura na mfano wa Mungu uliwezesha jambo la kwanza kufanyika; na nguvu ya uzazi ilifanya la pili liwezekane. Hata hivyo, dhambi aliingilia kati kuchelewesha udhihirisho wa makusudi kamili ya Mungu.

Uumbaji wa mwanaume na mwanamke pia ulianzisha uhusiano kati ya wawili hawa katika ngazi ya juu zaidi kuliko ile iliyopo kati ya mwanamume na mwanamke wa viumbe wa chini, kama tutakavyoona tutakapojadili hili zaidi kwa kina katika sura ya 2. Mtume Paulo, katika kufafanua juu ya uhusiano huu wa mume na mke katika Efe. 5: 25-33, anaonyesha kwamba lazima uwazie upendo, mapenzi , kuheshimiana na imani na hadhi ya wenzao wa kiroho katika Kristo na Bibi Harusi wake.

Kristo alitoa mfano wa aya iliyo mbele yetu kama thibitisho la heshima ya ndoa (Mathayo 19: 4; Mk 10: 6). Kwa upande wake kauli hii iliashiria maisha ya muda mrefu, uhusiano wa kipekee na uaminifu wa kuheshimiana kati ya mume na mke katika ndoa.

AYA YA 28

"Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha" — Haikuwa nia ya Mungu ya kwamba mtu aishi peke yake, na ndio maan ya amri katika aya hii. Katika maana ya kiroho, Bibi Harusi wa Kristo vivyo hivyo aliamuru " Zaeni, mkaongezeke." " Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu "

Adamu na Hawa walihidiwa "mamlaka" juu ya viumbe ya chini, na hii ilitimizwa wakati aina mbalimbali za wanyama waliletwa mbele ya Adamu ili awaite majina (Mwa 2:19).

Lakini wanyama hao hao walitumika kimfano katika Biblia kwa ajili ya aina mbalimbali ya binadamu, na kwa hivyo amri hiyo kikawaida ililenga matarajio ya mbele wakati "Adamu wa pili" atatumia mamlaka juu watu hai wa Ulimwengu Ujao.

Kabla ya kuweza kushika mamlaka haya, watu hawa wawili walihitajika kuonyesha utii chini ya mapenzi ya Mungu. Badala yake, Hawa alijihisi kuwa sawa na Mungu na akaasi, na Adam akamfuata katika dhana yake (Mwanzo 3: 6); Matokeo yake yalikuwa ni adhabu ya kifo, na kucheleweswa kupata mamlaka ya ahadi. Kufikia utawala sasa ilibidi wasubiri ushindi wa dhambi na mauti. Na katika hili Bwana Yesu alikuwa mshindi katika mashindano yake na hayo (Ebr. 2:14).

Tofauti na hatua ya Adamu na Hawa, yeye kwa unyenyekevu na utiifu alikubaliana na mapenzi ya Baba yake, hata kwa mauti ya msalaba. Lakini huo pia ulikuwa wakati wa ushindi wake, na alimradi , akapewa "jina... lipitalo kila jina" (Flp 2: 5-9). Kwa kusudi gani? Ndiyo apate mamlaka yaliyoahidiwa tangu mwanzo. Paulo aliendelea hivi: "Ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni (Watakatifu wameshinda kifo na kuinuliwakwa mbingu katika Kristo duniani - ona Waefeso 1: 3.), Na vya duniani, na vya chini ya nchi (binaadamu, kimfano viumbe wa hali ya chini mkiwemo viongozi na wananchi wa kawaida), na kila ulimi ukiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba "(Flp 2:. 10-11). Ufufuo na utukufu wa Bwana Yesu ulijumuisha matunda ya kwanza ya utawala ulioahidiwa (Ebr 2: 8.). Amri ya Mwanzo 1:28, kwa hivyo, si suala la shauku ya mpito inayohusiana tu na Adamu na Hawa, lakini ni muhimu katika kusudi Mungu ambalo limeongewa katika Injili, la kutimizwa na Bwana Yesu kama "Adamu wa pili ", na Bibi Harusi wake aliyetukuzwa, kama Hawa wa pili (2 Kor 11: 1-3.), katika Enzi ijayo.

Amri hiyo kwa ujumla aghalabu ni elezo la kusudi la Mungu katika Injili:

1. "Zaeni, mkaongezeke" — Amri hii itatimizwa na Kristo wakati "ataona uzao wake," (Isa 53:10.) Akiwa na kundi kubwa la waliokombolewa (Ufunuo 7: 9-12), mahali pengine ikielezwa kama "watoto niliopewa na Mungu" (Ebr. 2:13). "Mama" ambaye kwa njia yake watoto hawa wamefanya kuzaliwa ni Iklezia ikielezwa kama Hawa wa pili (2 Kor 11: 2.), "mama yetu sisi." ( Gal 4:26). 1.

2. "mkaijaze nchi, na kuitiisha" — Kimfano, haya yatatimizwa baada ya mioto ya kusafisha ya Harmagedoni na hatima yake imesafisha dunia. Nchi itakuwa imefanywa upya na kuitiishwa wakati wa "zamani za kufanywa upya vitu vyote" (Matendo 3:21). 2.

3. "Mkatawale " — Mamlaka yatatekelezwa na Adamu wa pili na Bibi Harusi wake aliye na wingi na utukufu katika Ulimwengu Ujao: " Nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako" (Zab. 2:8).

4. "Mkatawale samaki,  ndege, wanyama " — Katika maandiko hawa wanatumiwa kimfano kuwakilisha mataifa yenye uhai na watu (linganisha na  Dan. 4:12). Kwa hivyo, katika kiashirio halisi cha Mwanzo, amri hii inayotangaza mamlaka juu yao inalenga mbele kwa kule kutiishwa mataifa katika Ulimwengu Ujao.

Matukio ya dhambi na mauti katika Edeni, hata hivyo, yalichelewesha kupatikana kwa mamlaka ya ahadi. Kuishiriki nguvu hii ilibidi wasubiri ushindi wa dhambi na mauti. Vita na ushindi viliigizwa kimfano katika ushindi wa Daudi katika vita vyake na Goliathi (1 Samweli 17). Alitambua hili kama mfano wa ushindi mkubwa utakaompata Mwanawe mkubwa, ambaye kwake mamlaka ya ahadi yangepatikana. Alitoa maelezo haya kwa maneno ya Zaburi 8: 5-7 mtulivu baada kumuua Goliathi na kuikomboa Israeli kutokana kwa ukandamizwaji na Wafilisti:

" Umemfanya (Mwana wa Adamu ) mdogo punde kuliko malaika; umemvika taji la utukufu na heshima. Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni..."

Maneno haya ni ya kinabii ya wakati ambapo Jina la Yehova ni "tukufu duniani mwote" (vv. 1,9). Ipasavyo, Paulo, katika kunukuu Zaburi, anasema: "Lakini sasa bado hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake. Ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji la utukufu na heshima" (Heb. 2:8,9).

Kutimizwa kwa Zaburi, kunangoja kurudi kwa Bwana na maanzilisho ya Ufalme wa Mungu. Ushindi wa Daudi kwa Goliathi ulikuwa ushindi wa imani. Alipotagaa kwa ujasiri uwanjani mwa Ela kupigana na jitu, alimwakilisha Daudi kimfano, Mchungaji Mwema, ilhali Goliathi aliakilisha dhambi katika mwili kwa madhihirisho yake mbalimbali ya kibinafsi na ya kisiasa. Maneno mapeketevu  Daudi aliyomtupia Goliathi walipokabiliana ni muhimu katika mtazamo wa amri ilyiotangazwa wakati wa uumbaji, na kazi ya ukombozi iliyofanywa na Kristo katika kutimiza hayo. Daudi alimwambia Goliathi: " Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli. Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu. " (1 Sam 17:46-47).

Goliathi, kama uzao wa nyoka, "alichubuliwa kichwani" na Daudi, mbegu ya mwanamke, na kwa kiasi kikubwa, baada ya vita, Daudi alichukua kichwa cha adui yake, na kukizika Yerusalemu, na kupelekea mchipuko wa jina Golgotha - "mahali pa fuvu".

Matumizi Ya Amri Hiyo Katika Agano Jipya

Amri ya Mwanzo 1:28, kwa hivyo, ni muhimu katika kusudi la Mungu duniani, na, alimradi, inakuwa mandhari husika katika Agano Jipya. Inaashiriwa, au kunukuliwa, katika vitabu vya Injili, Nyaraka na Ufunuo, zaidi ya maandiko mengine yoyote ya Agano la Kale. Bwana aliinukuu ili kueleza imani yake katika matokeo ya mashindano yake matarajiwa na Goliathi wa siku zake. Kwa Mitume alisema: "Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu." (Yohana 16:33).

Alikuwa akimaanisha kifo chake kilichokaribia na ufufuo: ushindi ambao kwao angeweza "kuushinda ulimwengu" na kushika mamlaka yaliyoahidiwa. Aliona hili kama timizo la amri ya Mwanzo 1:28. Muda mfupi baada ya yeye kusema maneno haya kwa Mitume, akaomba kwa Baba:

"Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele" (John 17:1-2).

Neno "nguvu" ni exousia, kwa Kigiriki na linaashiria mamlaka au utawala. "Mwili wote" ni Uebrania ambayo unajumuisha uumbaji wa hayawani (ona Mwanzo 6:12; 7:15, 16, 21; 8:17; 9:11, 15, 16, 17). Taarifa ya sala ya Kristo, ikitarajia ushindi unaokuja juu ya dhambi na mauti, inatambua "mamlaka" ambayo yangetolewa kwa "viumbe wa chini" tofauti na "uzima wa milele" ambao ungetolewa kwa "wengi jinsi Mungu alivyompa ", na ambao ungejumuisha Hawa wa kimfano aliyepewa Adamu. Alimradi sala ya Bwana inaonyesha shukrani zake kwa ajili ya timizo la mamlaka yaliyoahidiwa na amri ya Mwanzo 1:28.

Wakati Bwana alifufuka kwa ushindi kutoka kwa wafu na akatukuzwa, alirejelea amri hiyo. Aliwaambia mitume: "Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani." (Mathayo 28:18.).

Nguvu hii ni kionyeshi cha mamlaka yalioahidiwa katika enzi ya uumbaji.

Mauti yamebatilishwa - 1 Wakorintho 15:27

Amri ya Mwanzo 1:28 ni muhimu katika mafundisho ya Paulo katika Waraka wake kwa Wakorintho. Katika 1 Kor. 15:27, ananukuu Zaburi 8: 6 (maoni ya Daudi juu ya Mwa 1:28) kufundisha kwamba mamlaka yaliyoahidiwa ni pamoja na ushindi wa mauti yake, "sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. Kwa kuwa (halafu mtajo unafuata - tazama pembe) 'alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake'. Lakini atakaposema, 'vyote vimetiishwa', ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.  "(1Kor 15:. 25-27).

Ushindi wa Kristo Juu ya Mbinguni Mataifa — Waefeso 1: 9, 22 Amri ya uumbaji inaasisi mandhari ya msingi ya Waraka wa Paulo kwa Waefeso. Anainukuu kuonyesha kwamba Kristo ameahidiwa mamlaka juu ya Mataifa ya ulimwengu wa kiroho, na kwa kutarajia huko, amewainua wanafunzi wake katika "ulimwengu wa roho" alioufanya (Efe 1: 3; 2: 6). Kwa sasa huo "ulimwengu wa roho" unashiriki katika vita vya maneno, vya Injili dhidi ya falsafa ya dunia, ukitangaza kwa Mataifa ya "ulimwengu wa roho" "hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi" (Efe 3:10.). Anaongelea mashujaa wa imani waliojihami kwa silaha wakifanya vita " juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya" katika ulimwengu wa kiroho wa Mataifa (Efe 6:. 12-13). Lakini hii pia inatarajiwa wakati mamlaka kamili itakuwa ikitekelezwa na Kristo na wateule katika kutimiza amri ya Mwanzo. Kwa hivyo, katika Waefeso 1: 9,22, ananukuu Zaburi 8: 6 ambayo imejikita katika Mwanzo 1:28:  1:28: "Akiisha kutujulisha (siri) ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo: Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha 'vitu vyote' (akinukuu Zaburi 8: 6) katika Kristo, vitu vya mbinguni (ona mg.) na vitu vya duniani pia;  Naam, katika yeye huyo; na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi" "Akavitia vitu vyote chini ya miguu yake (akinukuu Zaburi 8: 6) akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote (hayo ni mamlaka) kwa ajili ya kanisa; ambalo" (Efe 1:. 9-11, 22). Waraka unahusu pande mbili pinzani za "ulimwengu wa roho" au mamlaka ya kisiasa: wale walio katika Kristo (ona Waefeso 1: 3; 2: 6, mg.), Na wale walio katika ulimwengu (Efe. 6:12.). Kuna hali ya mapambano kati ya mifumo hii miwili na kwa hivyo Paulo aliandika: "kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho" (Efe. 6:12, mg.). Kwa sasa, vita ni juu ya mafundisho (Efe 3:. 9), na kwa ajili hiyo, askari katika Kristo lazima awe amejihami vyema na silaha (. Efe 6: 13-18). Lakini Kristo akirudi, vita vitakuwa vimezidi, na matokeo yake ni kuwa ulimwengu wa roho wa Mataifa utakuwa umemezwa na ule ulio katika Kristo; wakati ambao, ule wa Kristo utakuwa umepata mamlaka juu wa ule wa Mataifa.

Nguvu Ya Kushinda Ni Kutoka Kwa Yehova— Wafilipi 3:21 Wafilipi 3: 20-21 inajumuisha kifungu muhimu cha Waraka. Inazungumzia uraia wa mbinguni, kurudi kwa Kristo, mabadiliko ya asili yatakayokabidhiwa watu wa haki na kwa sababu ya " kuvitiisha vitu yote" kwake Bwana Yesu.

Kirai "kuitiisha vitu vyote" ni marejeo kwa Zaburi 8: 6 iliyo na msingi wake kwa amri ya Mwanzo 1:28. Ushindi wa Kristo ni kubadilisha miili yetu unyonge ya waliokombolewa ikiwa ni pamoja na kusababisha "kila goti" kuinama chini mbele yake. Uwezo wa kufanya hivyo ukiwa umetoka kwa Bwana utamwezesha "kuvitiisha vitu yote" chini yake, ili kushughulika na utawala juu ya vyote. Alimradi, Waraka huu pia umejengwa juu ya amri ya Mwanzo 1:28.

Kwa nini Paulo ananukuu kubuniwa kwa amri kama ushahidi wa mambo haya? Ni kwa njia gani gani inaonyesha kwamba "mwili wetu wa unyonge" au "mwili wetu wa udhalilishaji" lazima ubadilishwe? Kwa sababu hali ya sasa ya asili ya binadamu ilikuwa na Anguko, na timizo la Amri hiyo lilichelewshwa na udhihirisho wa dhambi. Uasi wa Adamu wa Sheria ya bustani ya Edeni ulimbaini ykuwa asiyefaa katika hali hiyo, kushika utawala wa ahadi. Paulo alitangaza: "Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; (kando na Hawa Eve — on Mwa. 3:5-6) alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi (viumbe vya chini vikiwakilisha mataifa ya binadamu katika Alimwengu Ujao) "(Flp 2:. 5-11). Kuhusu Hawa wa kimfano, Bibi Harusi wa Kristo, aliandika: Kwa maana sisi (uraia — R.V.)  wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake. (Flp 3:. 20-21).

Njia Ya Ushindi: Utoaji Ya Mzaliwa Wa Kwanza — Kol 1: 15-23 Marejeo kwa amri ya uumbaji msingi pia kwa mandhari ya Waraka kwa Wakolosai. Katika sura 1: 15-23, Kristo wasifiwa  kama "mfano wa Mungu asiyeonekana" ikileta kukumbuka ya maelezo ya awali ya kuumbwa kwa Adam katika "sura na mfano wa Mungu". Maoni katika Elpis Israel ni kwa uhakiki:

"Sheria ya asili, 'ambalo ni jambo la uwepo na sehemu isiyoweza kutengwa na uchumi wetu wa sasa, imeduduisha pakubwa, na kufuta mfano wa Mungu, ambao mtu awali aliutoa. Illihitaji, kwa hiyo, muonekano wa Mtu Mpya, ambaye kwake sura na mfano zitaonekana tena, kama hapo mwanzo. Huyu alikuwa ni 'binadamu Kristo Yesu,' ambaye Paulo alimtaja 'Adamu wa mwisho.' Yeye ni 'Sura ya Mungu asiyeonekana' (Kol 1:15); 'kioo king'aacho sana cha utukufu, na chapa ya nafsi yake ' (Ebr 1: 3.)" (Uk 40). Paulo anaendelea kusema kwamba Kristo ni "mzaliwa wa kwanza wa kila kiumbe" (Kol 1:15), au wa "viumbe vyote" kama Kigiriki kinavyosema (tazama Diaglott). Iliwezekanaje kwa Bwana, ambaye hakuwa na uwepo wa mwili mpaka miaka ya 4000 baada ya Uumbaji, kuitwa "Mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote"? Kwa sababu ya hali ya mzaliwa wa kwanza kilikuwa ni cheo kisheria, na sio kile cha lazima cha ajali ya kuzaliwa. Mtoto yule mdogo anaweza kuinuliwa na kuwa mzaliwa wa kwanza kisheria juu ya kakake, kama kakake ameonyesha kutowajibika ipasavyo au hastahili heshima (linganisha Kutoka 13: 1-2; 22:29; Kumb 21: 15-17; 1 Nyakati 5: 1; 26:10). Adamu wa kwanza alionekana kutostahili madaraka yake na hatimaye alipokonywa mahali pake na Adamu wa pili, ambaye Yehova alikuwa amesema: " Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia" (Zab. 89:27).

Tafakari kunukuliwa kwa Kol. 1: 19-20 kakika uhusiano na amri ya Uumbaji: "Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae (kwa umbo na mfano wa Mungu) na kwa yeye kuvipatanisha 'vitu vyote' (Zab. 8:6) na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi (wanaokufa) au vilivyo mbinguni (watawala wasiokufa wa Ulimwengu Ujao)".

Katika marejeleo yake ya "vitu vyote", Paulo alikuwa akunukuu kwa ujumla kutoka kwa Zaburi 8:6 na mwanzo 1:28, akieleza jinsi mamlaka yatatekelezwa kwa vyote.

Mfiko kamili wa Enzi - 1 Petro 3:22 Katika fungu hili, Petro ananukuu maneno ya Kristo (Mathayo 28:18.) Ambayo yametolewa kutoka Zaburi 8: 6, ili kuonyesha kiasi kamili cha mamlaka leo yanayotekelezwa na Bwana, nguvu ambayo anaiutumia kuleta wengine kwa utukufu. Petro aliandika: " Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi... kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa (Mwa . 1:28) chini yake" (1 Pet 3:. 21-22). Amri ya Mwanzo 1:28 kwa hivyo inatekelezwa katika Kristo.

Sifa Kuhusishwa Na Adam Pili Ufu. 5:12 Kama mwendelezo wa sheria ya Mwanzo 1:28, na kwa kuzingatia historia yake (ushindi wa Daudi kwa Goliathi), Zaburi 8, inadhihirisha kuwa mamlaka yaliyoahidiwa yatatekelezwa tu kupitia vita vya kibinafsi na vya kisiasa. Itaasisiwa  wakati ambapo jina la Yehova litatukuzwa duniani (zaburi 8:1) na Mwana wa Adamu ("amevikwa taji la utukufu na heshima" (aya ya 5).  

Siku kabla ya kusulubiwa, Bwana alitangaza kwa Baba yake, " Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye" (Yohana 17:4). Hata hivyo, kama Paulo anavyosema, mahitaji ya kinabii ya Zaburi 8 hayajatimizwa kikamilifu (Ebr 2:. 8-9). Wakati huo utafika katika ujio wa pili wa Bwana, wakati utukufu na heshima zitahusishwa kwa Mwana wa Adamu na wote juu ya nchi, kama ilivyoainishwa katika Ufunuo 5: 9-14. Kunaonekana mwangwi wa maneno ya Zaburi 8 na ya Mwanzo 1:28 katika mnasaba wa "nguvu" na utukufu vilivyoonyeshwa katika Ufunuo 5: 11-13: "Nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu, wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka. Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele".

Katika picha hii ya kimfano ya utukufu ujao, Elohim wanajiunga na viumbe wa chini katika kushangilia mamlaka aliyopewa Mwana wa Adamu, na kumtunukia sifa kutokana na jina lake takatifu.

Nukuu za Zaburi 8 na Mwanzo 1:28 zanazopatikana katika Agano jipya zajumlisha taarifa ya Bwana aliyefufuka kwa wawili wale aliokutana nao juu njia ya kuelekea Emau: "Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?  "(Luka 24:26). , Akafungua kuelewa kwao juu ya mahitaji ya Maandiko upande huo, akigusia hasa juu ya Musa na Zaburi (Luka 24:27, 44). Hii ingehusisha ufafanuzi wa Mwanzo 1:28 na Zaburi 8.

Muhtasari

Marejeo yetu kwa Nukuu na vidokezo vya Mwanzo 1:28 na Zaburi 8 katika Agano Jipya hayanuiwi kuwa makakamilifu, na kutafuta kutaonyesha machimbuko mengine. Kila rejeleo kwayo limekwisha tumika kwa uhusiano maalum kama kuonyesha pembe fulani ya namna ambayo ushindi wa Mwana utadhibiika, na upeo wa mamlaka atakayotekeleza kwa ushirikiano na Bibi Harusi wake, Hawa pili. Marejeo ambayo tumenukuu yanaweza kuwekwa kimpango kama yayoeleza yafuatayo: Katika Waefeso: Changamoto; Katika Wafilipi: ushindi; Katika Wakolosai: mwinuko; Katika Waraka wa Petro: nguvu; Katika Ufunuo: utukufu; Katika 1 Wakorintho: matokeo ya mwisho: kifo kuangamizwa.

Muhtasri  wa Uumbaji —aya za. 29-31 Mungu anamkimu mwanadamu ili kumwendeleza, na anakusuru kazi ya uumbaji kuionyesha kuwa ni mfano wa kusudi lake kubwa na wanadamu.

AYA YA 29

"Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;" — Mungu kwa neema Huyajali mahitaji ya mwanadamu. Awali, mtu alipewa mboga kama chakula chake. Kilikuwa kimezuiliwa tu kwa "mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia," na matunda ya miti. Hii ilimpa mtu chakula cha kutosha kwa ajili ya mahitaji yake. Baada ya Mafuriko, Nuhu aliambiwa " Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu" (Mwa 9: 3). Kutokana na haya, inaweza fikiriwa kuwa watu wa wakati wa Nuhu walikuwa walaji mboga tu bila nyama, na kwamba kuongezwa kwa nyama katika mlo wao kulikuja tu baada ya Mafuriko. Lakini si lazima iwe hivyo. Nuhu alitambuliwa tofauti za wanyama safi na najisi alipoingia katika Safina, na alichukua wanyama safi zaidi kuliko najisi, bila shaka ili wampatie chakula. Aidha, sadaka ilitolewa kabla ya Mafuriko, na bila shaka waabudu walikula nyama ya matoleo kama ilivyokuwa kawaida chini ya sheria ya Musa. Ulaji wa mboga tu huenda ulikuwa kabla ya Kuanguka wala sio kabla ya Gharika. Kwa mpito, neno "nyama" kwa mandhari kama ya aya hii lilimaanisha "chakula" kwa Kiingereza cha zamani.

AYA YA 30

"Na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo" — Neno la Kiebrania la maisha ni nephesh, ama moyo, kama ilivyo katika pembe. Kwa hivyo aya hii intufundisha kuwa kiumbe wotw wanaotembea wana "mioyo" kama ya binadamu.

AYA YA 31

" Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita " —Neno tob lamaanisha "ch/ema" ili kuashiria sifa za kitu/mtu. Hiyo ilikuwa hali ya Uumbaji kabla ya Kuanguka, lakini sio baadaye, Mungu mwenyewe akiwa shahidi. Maelezo, "chema sana" hayajahusishwa na mwanadamu tena na Mungu. Badala yake, katika kutambua kwamba mtu aliamua apotee, Yehova alitangaza: "Mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake " (Mwa. 8:21). "Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu," alitangaza Sulemani (Mhubiri 7:29), "lakini wamebuni mavumbuzi mengi.

MAREJELEO YA MAKTABA

Genesis Expositor - HP Mansfield

Phanerosis - John Thomas

Elpis Israel - John Thomas

Concordance - Strong

Companion Bible

Lexican - Gesenius

Biology: A Search for Order in Complexity.

Eureka - John Thomas

MASWALI YA KIFUNNGU:

  1. Mungu aliumba nchi siku ipi?
  2. Ni siku gani ambapo Mungu alisema "ni vyema"?
  3. Mungu aliumba jua siku gani?
  4. Nyota ziliumbwa kwa sababu gani?
  5. Siku za uumbaji zilikuwa na maana ya kawaida?
  6. Eleza maana ya neno "anga" katika Kiebrania.

MASWALI YA INSHA

  1. Je, ni jinsi gani vitendo saba vya uumbaji vinatabiri lengo la Uungu ambalo Mungu analo na watu?
  2. Mungu alikuwa anaongea na nani katika aya ya 26?
  3. Malaika walitoka wapi?

 

 

 

 

Swahili Title: 
Mwanzo - Sura 1
English files: 
Status: 
Translator Identified
African text: 
Carl Hinton
Translator 1: 
Jonathan Nkombe
Translator 2: 
Martin Silwani
UK Owner: 
Carl Hinton