CSSA 1-1-02 - CREATION

2. UUMBAJI

“Mungu akaona kila alichokifanya na tazama ni chema sana”

Shabaha

Kuonyesha kwamba Mungu aliumba vitu vyote ili dunia ijawe na Utukufu wake.

Muhtasari

Biblia inaanza na kitabu cha Mwanzo. “Mwanzo” maana yake ni Hapo mwanzo, mstari wa kwanza katika Biblia unasema “Hapo mwanzo Mungu akiumba mbigu na nchi”. Hatuna uhakika kabisa ni wakati gani Mungu alipoumba mbigu na nchi, tunalolifahamu ni kwamba Mungu ambaye ni wa milele aliiumba nchi miaka mingi sana iliyopita. Mwanzo 1:2 husema kuwa “nayo nchi ilikuwa tupu tena ukiwa”. Hatuambiwi ni kwa nini lakini tunaambiwa katika Mwanzo Sura 1, kwamba Mungu alikusudia kufanya jambo duniani. Alikusudia kuitengeneza tena ili kusudi ikaliwe na watu iweze kuleta sifa na utukufu kwake. Alifanya hivi miaka 4000 KK (Hii yapata miaka 6000 iliyopita) Kutoka 1 hadi 2:7, 18, 25.

KUSUDI LA UUMBAJI

Sura ya kwanza ya Kitabu cha Mwanzo inatuambia kwamba Mungu alipoumba vitu vyote na kuviweka vyote duniani Alikuwa na makusudi tayari katika fikra zake. Tangu mwanzo lilikuwa kusudi la Mungu kwamba uumbaji wake wote ni lazima umpatia utukufu Yeye. “Hakika yake kama niishivyo mimi na dunia yote itakavyojawa na utukufu wa BWANA”. (Hesabu 14:21). Kwa kuijaza dunia na “Utukufu wake”, Mungu ana maana kuwa kila kitu kilichoumbwa kinapaswa kumwabudu na kumtii Yeye hakutakuwepo dhambi yoyote, magonjwa au kifo. Maana dunia itakuwa imejawa na watu ambao Mungu amewapatia uzima wa milele. Tunasoma hili katika badiliko lililo kuu katika ufunuo 21: 3-4.

SIKU SITA ZA KUFANYA KAZI: Mwanzo 1 hadi 2:3,7,18-25.

Dunia haikuwa nzuri kabisa wakati huo Mungu alipo kuwaanaiweka katika mpangilio. Ilikuwa nyeusi na Utupu. Haikuwa na uhai au nuru, au uzuri wa aina yoyote. Ndipo Mungu alipoamua kuibadilisha na kuifanya ikaliwe na watu. Akawaamuru malaika wafanye kazi hiyo. Katika Zaburi 103:20 tunasoma kuwa malaika zake ni wenye bidii. Ilikuwa ni kazi kubwa sana, Lakini kwa kuwa Mungundiye mwenye nguvu zote, Kazi ya uumbaji ilifanyika kwa muda wa siku sita.

Kila siku “ ikiwa ni jioni na asubuhi” zaidi ya masaa ishirini na nne. “Kwa siku sita BWANA akaifanya mbigu na nchi, bahari, na vyote vilivyomo ndani yake” (Kutoka 20:11) Kwa kila siku uumbaji ulifanyika kwa siku sita, jambo moja jema na la mhimu lililoongezwa duniani, mpaka hapo ilipo kuwa tayari kwa mtu kuweza kuishi, ambaye Mungu alimkusudia kumuumba mwisho wa viumbe vyote. Ndipo Mungu  “akapumzika” siku ya saba. Na tuangalie ni nini kilichofanyika katika juma hilo la uumbaji.

Siku ya kwanza (mistari 3-5) Kwanza Mungu akasema “Na iwe nuru”.  Mungu alisema nao Malaika wakafanya kama alivyoamuru). Dunia ilikuwa imefunikwa kabisa na giza, lakini sasa Mungu akatenganisha nuru (ambayo aliita “mchana”) na giza, ambalo aliliita “Usiku”).

Siku ya Pili (mistari ya 6-8) Inapozungumzia kuwa Mungu aliumba mbingu kati ya maji ya juu nay ale ya chini, inazungumzia kuhusu anga, hewa tunayovuta. Hii ilikuwa ni mhimu kabla ya miamba, au wanyama au mtu kuweza kuishi duniani. Hivyo Mungu aliumba hilo baadaye.

Siku ya Tatu (mistari ya 9-13) Siku hii Mungu alitenganisha maji kati ya nchi kavu, makusanyiko ya maji. Mungu aliyaita bahari na pakavu Mungu alipaita nchi. Wakati Mungu alipofanya hivi, aliiwekea mipaka bahari ili kwamba bahari isiipite hiyo. Kisha Mungu akaumba mimea miti na miti ya matunda ikaota katika ardhi, kila mmoja ukiwa na mbegu zake. Na hii ndiyo sababu tunapopanda mbegu za mahindi tunapata mahindi. Mbegu za machungwa hazibadiliki kuwa za mti wa limao au mahindi kuwa ngano.

Tunapaswa kutulia na kufikiria jinsi Mungu alivyopangilia vizuri kazi zake zote za uumbaji zilivyokuwa kwa kuwa “kwa hekima yake ameviumba vitu vyote” (Zaburi 104:24).

Siku ya nne (mistari ya 14-19) Jua, Mwezi na Nyota pia ziliwekwa mahali pake sahihi katika anga kuleta nuru usiku na mchana. Ziliumbwa ili ziwe kwa ajili ya dalili, majira, siku na miaka. Kwa hiyo tuna majira manne kwa mwaka, na masaa ishirini na nne kwa siku, Jua huchomoza na kuzama kila siku bila kushindwa na limeendelea kufanya hivyo tangu siku hii ya nne ya uumbaji, siku na miaka hakuna ambayo imekuwa mifupi au mirefu.

Siku ya Tano (mistari ya 20-23) Siku hii Mungu aliumba viumbe vyote viishivyo baharini, na aina ya ndege wote warukazo angani.

Siku ya Sita (mistari ya 24-31) Hatimaye, siku ya sita, Mungu aliviumba viumbe vyote viishivyo nchi kavu, wanyama wa kufugwa, kila kitambaacho na aina zote za wanyama mwitu. Kisha kabla ya siku ya sita kuisha Mungu aliumba Mtu. “Na BWANA, Mungu akafanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai” (Mwanzo 27)

Mungu akamweka mtu, Adamu, katika bustani nzuri sana ambayo aliipanda katika Edeni. Akawaleta wanyama wote kwa Adamu naye akawapatia majina yao. Lakini Mungu akaona si vyema Adamu awe peke yake. Alihitaji awe na msaidizi wa kufanana naye, ambaye angemsaidia kumsifu Mungu. Kwa hiyo Mungu akamuumba “msaidizi (anayemfaa) kumsaidia Adamu”. Mungu akamletea Adamu usingizi, aksinzia, na akachukua ubavu mmoja wa Adamu. Akamuumba mwanamke kutokana na huo ubavu (“Mwanamke” maana yake “aliyetwaliwa kutoka kwa mwanaume”). Kisha Mungu akampeleka huyu Mwanamke, Hawa, Kwa Adamu kuwa mkewe (Mwanzo 2:18-24). Yote hayo Mungu aliyafanya siku ya sita.

Siku ya saba (Mwanzo 2:1-3). Siku ya saba “Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya, Mungu akastarehe siku ya saba” (mstari 2). Neno “kustarehe” halina maana kuwa Mungu alikuwa amechoka akahitaji kupumzika, maana yeye ni mwenye nguvu zote na kamwe haja acha kufanya kazi. (Zaburi 12:4, John 5:17). Alistarehe kwa sababu alikuwa amemaliza kazi aliyokuwa ameazimia kuifanya. Mungu “aliacha kazi ya uumbaji”. Kwa muda wa siku sita aliumba nchi na akaweka mtu na viumbe vyote katika nchi.

FUNDISHO KWETU

Kuna mambo mawili tunayotakiwa kujifunza kufanya – kumsifu Mungu na kumshukuru yeye kwa wema wake. Mfalme Daudi alisema: “Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu na nafsi yangu yajua sana”.

Kwa hiyo kila tutazamapo juu mbinguni au tunapoona wadudu wadogo sana; wameumbwa kwa ajabu mno, au kuvuta harufu nzuri sana ya maua, au tunapotazama mawimbi yanavyovyuma yakiishia ufukweni, na tumshukuru Mungu, Muumbaji Mkuu wa vitu hivi vyote. Tunaweza kumshukuru kwa haya yote aliyotutendea sisi?—kwa kuliamini Neno lake na kutii amri zake, “Ee BWANA, jinsi yalivyo matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia” (Zaburi 104:24).

MAELEZO YA NYONGEZA

Ni watu wachache sana siku hizi wanaoamini kwamba Mungu ndiye aliyeumba vitu vyote. Watoto wetu katika Shule na Vyuo Vikuu badala yake wanafundishwa nadharia ya mabadiliko ya maumbile ya vitu (hasa ni wazo lililopendekezwa) linalokubaliwa na wanasayansi wengi kueleza jinsi Mwanadamu alivyokuja kutofautiana na wanyama wengine. Wansema ati maisha katika dunia yanabadilika badilika (hasa yanaendelezwa au yalibadilika) zaidi ya miaka ina milioni iliyopita yalifanyika. Haya yote yalianza kwa bahati tu lakini si kwa mpango maalumu wa Mungu, wanasema.

Watu wengi wanapenda kumwamini Mungu na kumtii yeye. Hata hivyo nadharia hiyo haiwezi kuthibitishwa. Biblia ni ya kweli ma ni rahisi kuweza kuonyesha ukweli. (Soma somo la 1, Maelezo ya nyongeza). Bwana Yesu Kristo yeye mwenyewe aliamini na akafundisha kwamba Mungu pekee ni Mwumbaji mwenye hekima wa vitu vyote (Soma Marko 10:6). Mitume pia walifundisha kwamba “Mungu ndiye aliye ulimwengu na vitu vyote vilivyomo” (Matendo ya Mitume 17:24-26, pia linganisha na 1 Petro 4:19).

MASWALI

Majibu Marefu

 1. Ni nani aliyeumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo?
 2. Ni nani aliyemsaidia Mungu wakati alipoweka dunia katika utaratibu maalumu?
 3. Majina ya mtu wa kwanza na mwanamke wa kwanza ambao Mungu aliowaumba ni?
 4. Neno “mwanamke” maana yake nini?
 5. Mtu wa kwanza na Mwanamke waliishi wapi?
 6. Mungu aliumba vitu vyote kwa muda wa siku ngapi?
 7. Mungu “akastarehe”. Hii ina maana gani?

Majibu ya Kina

Hapo mwanzo Mungu aliumba vitu vyote

 1. Eleza nini Mungu aliumba:-
  1. Siku ya kwanza na
  2. Siku ya nne.
 2. Ni jinsi gani Mungu alivyomwumba mtu wa kwanza?
 3. Ni jinsi gani Mungu alivyomwumba Mwanamke?

Majibu ya Nyongeza

Hapo mwanzo Mungu aliweka utaratibu wa kuumba vitu vyote duniani

11. Eleza yote unayofahamu kuhusu siku sita za uumbaji

 

Swahili Title: 
UUMBAJI
English files: 
Swahili Word file: 
PDF file: 
Macedonian file: