CSSA 2-1-21 - THE GOLDEN CALF

146. NDAMA YA DHAHABU

Kusudi la Mungu kwa watu wake lilikuwa kuwafanya “Ufalme wa makuhani na taifa takatifu”. Ilikuwa shughuli ngumu kwa sababu asili ya ubinadamu (utu) haupokei kwa rahisi sheria za Mungu – inabidi ifunzwe kabla hatujafunga masomo yetu juu ya ibada ya Israeli na huduma katika Hema, tunahitaji kutafakari onyo la namna kwa haraka Israeli walisahau kumluhusu Yahwe. Katika somo hili tutaona jinsi wana wa Israeli walirudi nyuma kwenye njia za kimwili walizojifunza huko Misri.

 

Musa anadhihirishwa kuwa mpatanishi kwa ajili ya watu wake na mapenzi ya Yahwe yanaonekana wakati anapowasahihisha na kuwaadabisha watu wake.

 

Kutoka 32

 

Israeli Katika Sinai:

Katika mwezi wa tatu baada ya kuondoka Misri Israeli walifika Sinai na huko wakapokea zile amri kumi na sheria nyingine nyingi na kanuni. Pale Mungu akafanya agano nao. Kama wangemtii, Angewafanya Ufalme wa makuhani na taifa takatifu (Kut. 19:5-6). Watu walikubali toleo la Mungu wakilipokea na kulifanya lenye kudumu kati yao. Sasa walikuwa watu wa agano, waliotengwa kutokana na mataifa mengine yote kwa sababu walimwabudu Mungu wa kweli badala ya vinyago. Walikuwa ndiyo watu pekee kupata sheria zilizotolewa na Mungu. Sura za 25 mpaka 31 za Kutoka zinaainisha jinsi Musa alivyopokea sheria na mchoro wa Hema. Sura ya 32 inaainisha matukio ndani ya kambi ya Israeli wakati huo huo.

 

MUSA MLIMANI –ISRAELI WANAANZA KUKOSA SUBIRA

Wakati Musa alipokuwa mlimani siku 40, Haruni aliachiwa uongozi juu ya watu pamoja na wazee. Hakuwa na nguvu za kutosha kuzuia nia yao kuvunja sheria ya Mungu. Akaafikiana na nia ya Israeli kwa ajili ya “Mungu itakayokwenda mbele yetu”, akiwaogopa hao watu. Akichukuwa pete za dhahabu masikioni mwao akaziyeyusha na kuunda ndama (ng’ombe) na dhahabu ambaye walimwabudu. Wakisema, “hawa ndiyo miungu wenu, o Israeli, waliokutoa kutoka nchi ya Misri (mst. 4). Jinsi alivyokuwa tusi kwa Yahwe, mkombozi wao!

 

Siku iliyofuata iliamrishwa na Haruni kuwa ni sherehe kwa Yahwe. Wakiondoka (wakiamka) asubuhi na mapema, watu wakaja na kutoa kafara za kuteketezwa na dhabihu za amani katika madhabahu iliyojengwa mbele ya yule ndama. Haruni huenda alitumaini wangalimwabudu Yahwe lakini Paulo anasema walikuwa wanaabudu –sanamu na wapenda anasa ambao “walikaa chini kula na kunywa, na kusimama kucheza” (1 Wakor. 10:7). Jinsi watu walivyofanyika waovu kiongozi wao alipoondoka! Katika kumwabudu yule ndama walikuwa:

  1. Wamevunja amri ya kwanza nay a pili (Kut. 20:22-26);

  2. Wamemtukana Yahwe;

  3. Wameonyesha jinsi walivyokuwa watovu wa uaminifu kabisa kwa kurejea njia za kuabudu sanamu za misri katika fulsa ya kwanza kabisa.

 

MUSA AWAOMBEA WATU WAKE (Kutoka 32:7-18

Katika hali ile ya kuabudu sanamu iliyoendelea kati ya watu wake, wivu wa Yahwe ukapaa katika hasira ya kutisha. Mungu akamwambia Musa yaliyokuwa yakitokea kambini. Alikuwa amekasirika mno hivi kwamba alikuwa ameamua kuwateketeza Israeli na kuunda (kuanzisha) taifa jipya kutokana na Musa. Musa akawaombea watu wake ambao aliwajuwa kuwa watovu wa uaminifu. Aliwaokoa kutokana na kuangamizwa hivyo kwa kumsihi Mungu kukumbuka utukufu, heshima ya Jina Lake kati ya mataifa. Mungu angeacha wapotee baada ya kuwaokoa kutoka Misri. Musa pia alimwomba Mungu kukumbuka agano lake kwa Abrahamu, Isaka na Yakobo kuwapa uzao wao (Israeli) urithi katika Nchi ya Ahadi.

 

Tabia ya ajabu ya Musa akiwa mpatanishi inabainika wakati huu. Badala ya kukamata heshima ya kuwa mwasisi wa taifa kutokana naye, akamsihi kwa nguvu kwa ajili ya msamaha. Alikuwa tayari kuacha jina lake lifutwe kutoka kwenye kitabu cha uhai, iwapo tu Mungu angewasamehe (Kut. 32:32). Walakini, Mungu alimwonyesha ya kuwa yeyote atakayetenda dhambi ni lazima aadhibiwe kama vile katika Wakolosai 3:23-25 “yule anayefaifanya dhambi atapata, kwa kosa alilofanya, na hakuna kuheshimu uso wa watu”. Dhambi zaweza kusamehewa lakini mkosaji mwenyewe yampasa atubu na kutaka msamaha (1Yoh. 1:9).

 

MUSA ANARUDI (Kutoka 32:15-24)

Musa akashuka kutoka mlimani huku anabeba mbao mbili za mawe zilimoandikwa sheria. Alikuwa pamoja na Yoshua. Walipokuwa wakikaribia kambi waliweza kusikia watu wakipiga kelele kuzunguka vinyago alivyounda Haruni. Yoshua alidhani zilikuwa kelele za vita (mst. 7) lakini Musa alijuwa kuwa haikuwa hivyo.

 

MUSA ANASHUGHULIKIA TATIZO (Kut. 32:25-35)

Musa alipoona upeo wa dhambi ya Israeli, alikasirika mno hivi kwamba akavunja zile mbao ambamo sheria ya Mungu iliandikwa na ambazo alipewa (mst. 19). Akigeukia kile kinyago (cha) ndama wa dhahabu alikichoma kwa moto na kukisaga saga kuwa unga, akauchanganya na maji na kuwanywesha waisraeli. Musa alimlaumu Haruni akawageukia kuwalaumu watu (mst. 24).

 

Musa akawaomba wale waliokuwa tayari kusimama kwa ajili ya mambo ya Mungu, kusimama pamoja naya. Kabila lake mwenyewe la Walawi likafanya hivyo, wakishika mapanga mkononi wakapita kati ya makabila ya Israeli kwa hukumu, wakiwaua waabudu sanamu 3000.

Hasira ya Mungu haikuliwazwa naye akapeleka tauni juu ya watu. Ilichukuwa juhudi isiyokoma ya maombi ya Musa ambapo hatimaye aliwasamehe hao watu na kuahidi ya kwamba angempeleka malaika wake kuwaongoza kuelekea kwenye urithi wao.

 

Musa akaambiwa kwenda tena mlimani pamoja na mbao mbili mpya, ambazo Mungu angeziandika zile amri kumi kama vile mwanzo.

 

DHAMBI YA ISRAELI NI ONYO KWETU

Katika vitu vyote vilivyotokea kwa Israeli maandiko yanatuonyesha sisi kwamba kuna maonyo ya nguvu kwetu (1 Wakor. 10:6-14). Paulo anatuambia kwamba vitu hivi viliandikwa kama dalili au mfano, habari zilizo na onyo kwa ajili yetu tunaoishi miaka hii mingi baadaye. Walitamani vitu viovu nao walikuwa waabudu vinyago, lakini inatupasa tujichunge ili kamwe tusitelezee kwenye njia ya uovu. Walipata dalili nyingi za Yahwe aliyekuwa nao, lakini wakatenda kana kwamba hawakujali au kumuamini. Tunazungukwa na jamii iliyo ovu, hivyo na tuchukuwe tahadhali maalumu kuwa waaminifu kwa Mungu.

 

Kama Musa alivyopanda kwenda mlimani, vivyo hivyo Yesu Kristo amepaa mbinguni ambako anafanya upatanisho kwa ajili ya wale wanaomsogelea Mungu kupitia kwake. Inawezekana kwetu sisi kuchoka juu ya kutokuwepo kwake (2 Pet. 3:4). Yawezekana tukawa na mashaka, kama wao walivyofanya, iwapo atakuja tena. Waisraeli walivunja ahadi zao kumpenda na kumtumikia Yahwe pekee. Hatutengenezi sanamu (vinyago) kama ndama, lakini tunaweza kumsahau Mungu na kuabudu vitu vingine, kama vile fedha, raha au cheo kikubwa duniani, na huenda tusiwe tayari kwa ajili ya kurudi kwake Kristo sawa na Israeli walivyokuwa juu ya kurejea kwa Musa. Ndipo, badala ya kupata baraka yake na kibali (upendeleo), tutashuhudia hasira yake tu na kupata adhabu yake. Inatupasa kungoja kwa imani, tukisoma Neno Lake, tukiwazia juu ya kweli yake na kuwa tayari kwa ajili ya kurudi kwake, tukifanya mapenzi yake Bwana wetu.

 

VITABU REJEA:

The Story of the Bible” (H.P. Mansfield) pp. 313-327

The Visible Hand of God” (R. Roberts) – chapter 17

 

MASWALI YA FUNGU

  1. Kwa nini lilikuwa kosa kwa watu kuunda yule ndama wa adhabu?

  2. Ni kwa jinsi gani Musa alifahamu uabudu-vinyago wa Israeli na alifanya nini?

  3. Musa alilishughulikia vipi tatizo la ndama wa dhahabu aliporejea?

  4. Ni sehemu gani kabila la Walawi lilichukuwa kulikabili (kulimaliza) tatizo la ndama wa dhahabu?

 

 

 

MASWALI YA INSHA

  1. Ni mafunzo gani tunajifunza kutokana na dhambi ya Israeli katika kumtengeneza ndama wa dhahabu?

  2. Eleza ni nini Musa alitenda wakati akishuka kutoka mlimani Sinai na kuona kwamba watu waligeukia kuabudu vinyago. Jinsi gani tukio hili lilivyo sambamba sawa na yale atakayotenda Yesu Kristo atakaporudi?

 

 

Swahili Title: 
NDAMA YA DHAHABU
English files: 
Swahili Word file: