CSSA 2-1-22 - THE TABERNACLE: GOD'S MEETING PLACE WITH ISRAEL

147. HEMA YA KUKUTANIA: MAHALI PAKUKUTANA MUNGU NA ISRAELI

Wana wa Israeli walihitaji sehemu muhimu sana ya kwa ajili ya kuabudu katika maisha yao. Walihitaji wakati wote kukumbushwa juu ya utakatifu wa Yahwe na njia sahihi ya ibada. Hema ya kukutania iliwafundisha yote haya pamoja na kuwapatia maelekezo ya thamani kuhusu udhihirisho wa utakaoonekana wa utukufu wa Mungu wakati ujao. Kila dokezo la hema na samani zake linajaa maana. Katika kugundua maana hizi kuna hazina ya maelekezo kwa ajili yetu katika kumsogelea Mungu katika ibada (linganisha Waebr. 9:1-10)

 

Kutoka 25

 

MAMBO YA KAWAIDA KWA KINA

Wakati Musa akipokea sheria kule mlimani, Mungu aliamuru kwamba mahali maalumu pajengwe ambapo angeonana na Israeli. Pale wangekusanyika kumwabudu Mungu na kumkumbuka. Hili lilikuwa muhimu kwa ajili yao ya elimu yao ya kiroho. Hapa kunadhihirika kujali kwa Mungu kwa watu wake na vipaji vyake kwao “wanijengee mimi mahali patakatifu ili niweze kukaa kati yao” (Kut. 25:8; 29:43-46). Mahali patakatifu inamaanisha “mahali palipotengwa”. Ingawa Yahwe anakaa (yuko) Mbinguni, alipendezwa kudhihirisha uwepo wake ndani ya Hema katikati ya Taifa Lake. Kwa kuwa Israeli haikuwa bado na mahali pa kudumu pa kuishi nyumba (jengo) la kudumu halikuwezekana lijengwe. Kwa hiyo Mungu alitayarisha hema ya kuhamishika au mahali patakatifu. Ingaliweza kubebwa katika sehemu sehemu na kujengwa bila matumizi ya nyundo na misumari.

 

Mungu Mpangaji (Kut. 25:8-9)

Katika kujenga nyumba yoyote, fundi –michoro, mpango, makisio, vifaa na wafanyakazi ni lazima, Mungu alimpa Musa chapa yenye kina ya Hema ya kukutania.

 

Vifaa (Kut. 25:1-7). Musa aliomba zawadi (matoleo) nao watu kwa hiari wakaleta vitu vya thamani walivyochukuwa kutoka kwa Wamisri. Ni vifaa vyema sana peke yake vilitolewa. Dhahabu, fedha, na shaba vilikuwa ndivyo vito vya thamani vilivyohitajiwa kwa ajili ya vyombo; nyuzi za rangi ya samani, na rangi ya zambarau, kwa ajili ya mapazia; na singa za mbuzi, na ngozi za kondoo waume na ngozi za Pomboo kwa ajili ya kufunika paa la nje la Hema. Mbao zilizotumiwa ilikuwa ya miti ya Mshita inayoota jangwani. Ni mti wa kupendeza sana, mgumu sana na uwezao kudumu sana.

 

Watenda kazi (Kut. 35:30-35). Wahunzi wenya ujuzi waliteuliwa kwa amri ya Mungu. Mungu akawapa hekima na ufahamu (uelewa) wa jinsi ya kutenda (kutumia) vifaa. Miti iliandaliwa na kuwekwa sawa. Vifaa vya thamani viliyeyushwa na kutengenezwa. Nyuzi za mapazia zilisukwa na kuwekwa nakshi (mapambo). Wanawake wenye vidole hodari walifanya hilo, wakifahamu kwamba kazi hiyo ilikuwa kwa ajili yake Mungu. Walitenda kazi kama mzinga wa nyuki kwa jinsi watu wengi wenye hiari ya moyo na mioyo ya hekima waume kwa wake, walivyofanya kazi kwa kujituma kwa ajili ya Yahwe. Nasi tujitume kama hivyo kuhusu shughuli zetu katika shule ya Jumapili tukitenda kazi kwa furaha pamoja na wengine walio na imani ya thamani sawa nasi.

 

Mahali pa Hema ya kukutania (Hes. 2:17-34)

Hema iliwekwa kwenye nafasi yenye uzingo wa mita 46 urefu kwa mita 23 upana, mbali na kufikiwa na watu ikiwa imewekewa ukuta wa pazia. Hema na uzio wake, wenye kiingilio upande wa mashariki, iliwekwa katikati ya kambi ya Israeli (Hes. 2:17). Kambi ya Israeli ilijengwa kwa kona nne. Mashariki walikuweko (kabila la) Yuda, Issakari, na Zehuluni; Kusini Rubeni, Simeoni na Gadi; Magaribi Efraimu, Manase na Benyamini, Kaskazini Dani, Asheri na Naftari. Ndani ya mzunguko huu kulikuwemo mzunguko huu kulikuwemo mzunguko mwingine uliofanyizwa na mahema ya Walawi. Kabila la Lawi pia liligawanywa katika sehemu nne (Hes. 3). Kisha ndani ya mzunguko huu wa makuhani kulikuwepo Hema yenye (ya kukutania).

 

Hivyo Israeli walikusanywa kuizunguka Hema, alama ya kile ambacho kila mwisraeli wa kweli ilimbidi kufanya. Lakini hawakuruhusiwa kuikaribia Hema kwa sababu walawi makuhani walisimama katikati yao na Hema. Mungu alikuwa akiwaonyesha watu wake kwamba yeye ni mtakatifu (yaani mtengwa) na angalao walikuwa wamechaguliwa kuwa juu zaidi ya mataifa mengine yote ikiwapasa kumheshimu yeye.

 

BARAZA YA HEMA – UWA ULIOZUNGUKA HEMA

Kutoka 40:29-33 (Angalia mchoro wa ramani). Baraza lilikuwa eneo la mita 46 urefu na mita 23 upana, likiwa limezungukwa (limezingirwa) kwa pazoi za kitani safi kilichosokotwa kufikia kimo cha mita 21/2 . Ilikuwa ikisimamishwa na mihimili ya shaba vilivyowekewa vishikio vya fedha na shaba. Lango lililotengenezwa na nguzo (mihimili) mine na mapazia ya rangi ya buluu, huzurungi na samawati ya kitani safi iliyosokotwa, ndilo lilikuwa la kuingilia ndani ya baraza. Vikiwekwa ndani ya baraza hili lilikuwa:-

 

 • Madhabahu ya Shaba ya sadaka za kuteketezwa;

 • Birika (la maji ya kutakasia)

 • Hema yenyewe, yenye kugawanywa katika Patakatifu, na patakatifu pa patakatifu.

 

Tuangalie sasa jinsi maelezo haya ya kina yanavyoelekeza mbele kwa kristo:

 

Mapazia: yalizingira baraza ya Hema. Ni waisraeli tu waliomtumikia Mungu, waliingia barazani. Kristo ndiye njia yetu ya pekee ya kusogea kwa Mungu. Kristo ndiye mlango (Yoh. 10:9) “Hakuna mtu ajaye kwa Baba ila kwa mimi” (Yoh. 14:6). Kabla hatujaweza kuja kwa Mungu katika kweli, inatupasa kuelewa na kukubali kazi ya Mungu katika Kristo (Matendo 4:12). Baraza la nje linawakilisha ujulisho (ujilio) wa mtu katika kweli; hivyo vishikizo vyake vilikuwa vya shaba.

 

Madhabahu ya shaba: ilikuwa ya mbao (mti) iliyofunikwa kwa shaba ikiwa karibu mita 21/4 mzunguko kwa mita 11/2 kimo. Katikakati yake palikuwa na chuma bapa ambapo juu yake wanyama walioletwa kwa ajili ya kafara waliunguzwa (waliteketezwa). Moto kamwe haukuruhusiwa kuzimika (Walawi 6:12). Waisraeli walikuwa wamejifunza kwamba kitu cha kwanza katika ibada iliyokubalika kwa Mungu ilikuwa kafara (dhabihu). Damu ya kafara ilimwagika “kuleta upatanisho” kwa Mungu (Walawi 8:15).

 

Madhabahu hii ilikuwa mfano wa kuelekea kwa Kristo. Kupitia kwake tunasogea karibu na mungu (Waebr. 13:10). Zaidi, damu ya utakaso ya Kristo inapata msamaha na ukombozi kwa ajili yetu.

 

Birika: lilikuwa barazani kwa ajili ya makuhani kuoga kabla ya kuhudumia ndani ya Hema (Kut. 30:20-21). Ilikuwa kufundisha heshima kwa ajili ya utakatifu wake Mungu. Ni wale tu wenye mikono safi na moyo mweupe watasimama mbele ya Mungu (Zab. 24:3-4). Kuoga penye birika ni mfano wa sisi kuwa karibu na neno la Mungu kila siku; “kusafika kwa neno” (Waef. 5:26 linganisha Yoh. 15:3). Kupitia Neno tunaweza kutakaswa na kuepukana na uchafuzi wa dunia iliyotuzunguka.

 

HEMA NA VITU VILIVYOMO (Kut. 40:1-28)

Rejea pia sura zilizotangulia za kutoka kwa ajili ya mambo ya kina ya Hema.

 

Ujenzi: Hema lilikuwa jengo la mbao lililozungushiwa dhahabu ya kupigwa ikawa bapa (kama shuka vile). Mbao ziliunganishwa kwa vyuma kwenye pande zake na kusimikwa kwenye msingi wake ndani ya vishikizo (viguu) vya fedha. Hema haikuwa kubwa sana-kiasi cha mita 14 urefu na mita 4.6 upana na mita 4.6 kina. Ikiwa Hema kuta (pande) zake na paa zilifunikwa na mapazia, manne kwa hesabu yake, kuvihifadhi (kuvilinda) vyombo ndani yake. Ingeweza kuingiwa kutokea upande mmoja tu.

 

Mifuniko: pazia la kwanza lilikuwa la kitani safi iliyosukwa na kurembwa (kupambwa) katika rangi za buluu, huzurungi na samawati. Pazia ya pili ilikuwa nywele za mbuzi zilizosokotwa- kuhifadhi kitani safi. Pazia ya tatu ilikuwa ngozi za kondoo (dume) zilizoshonwa pamoja, na kupakwa rangi nyekundu. Pazia ya nne ilikuwa ngozi ya samaki wan chi-baridi-ngumu sana kuvaa.

 

Patakatifu: Hema ilijengwa katika sehemu mbili ya kwanza ilijulikana kama patakatifu yenye urefu wa mita 9, na mita 41/4 upana na mita 41/4 kimo upande ule mwingine, ukigawanywa kutoka patakatifu kwa pazia au ushungi ulikuwa ndiyo Patakatifu pa Patakatifu (au Patakatifu zaidi), ambapo patashughulikiwa kwa kina katika somo lifuatalo. Makuhani walihudhuria kwenye kazi zao za kila siku pale patakatifu.

Vyombo ndani ya Patakatifu na Patakatifu zaidi vilikuwa vya dhahabu ambalo linamaanisha imani iliyokamilika (1 Pet. 1:7). Kwa hiyo Hema inawakilisha kazi ya muumini kwa Mungu baada ya ubatizo (yaani kutembea katika imani). Sehemu ya Patakatifu palikuwa na:-

 

 • Meza ya mkate wa wonyesho;

 • Kinara cha kushikia taa chenye matawi saba;

 • Mimbara ya dhahabu ya kufukizia uvumba

 

Meza ya mikate ya wonyesho; iliwekewa juu yake mikate kumi na mbili ambayo iliwakilisha makabila kumi na mbili ya Israeli. Mikate ilibadilishwa kila siku ya sabato (Wal. 24:8). Mikate ya zamani ilikuwa ya makuhani tu, na kila wakati katika mahali patakatifu. Muda wa maisha ya kazi tukiwa ndugu na dada tunamshiriki kristo ambaye mikate ya wonyesho ilimwakilisha kama “mkate wa uhai” (Yoh. 6:53 na 38). Hivyo kumshiriki, tunatoa kwa Mungu matunda ya shughuli zetu, ikiwa toleo la kujihusisha kwake maishani mwetu.

 

Kinara cha dhahabu kwa ajili ya Taa: kilichukuwa taa saba zilizowaka bila kukoma, na kiliwakilisha taa ya kweli (2 Peter 1:19). inatupasa tutembee tukiongozwa na nuru hii, inayokuja kwa kusoma na kulielewa Neno la Mungu (Zab. 119:105) kwa njia hii mawazo yetu yanaongozwa kuelekea kwa Mungu.

 

Madhabahu ya Uvumba: Asubuhi na jioni uvumba ulichomwa juu yake. Uvumba ni unga wa manukato yatokanayo na miti ya ubani nao ni wenye harufu tamu inayoburudisha. Daudi alisema, “Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba” (Zab. 141:2). Kupitia madhabahu hii, uvumba ulipaa kwa Mungu. Vivyo hivyo sala hupaa kwa Mungu katika yesu Kristo aliye madhabahu ya kweli. Maombi (sala) kwa Mungu hueleza tama ya urafiki (ushirikiano) naye, na siku wakati wema wake utashinda ulimwengu. Sala za ndugu na dada waaminifu katika kristo hupaa kwa Mungu mithili ya “harufu njema” inayompendeza Mungu.

 

WINGU JUU YA HEMA (Kut. 40: 34-38)

Ndipo wingu likaifunika hema ya jumuia” (mst. 34). Kwa nje likaonekana kwa watu, wingu na nguzo zilikaa. Maadamu wingu kwa mchana na mwonekano wa moto saa za usiku vilikaa pale mahali wasifanye safari; wakati wingu lilipoondolewa kutoka juu ya Hema, watu walikwenda mbele na kufuata lilikoongozwa.

 

Wakati tunatafakari umbo la ajabu laHema pamoja na sehemu zake mbalimbali zenye msingi wa maana vile, tunaweza kuthamini ukuu wake Mungu na wema wake. Kambi ya Israeli ilikaa katika pembe nne na Hema iliwekwa katikati ya kambi. Humo ndani ya Hema, utukufu wa Mungu uling’aa kama tutakavyoona katika somo litakalofuata. Watu walikumbushwa daima kumsifu na kumheshimu Yeye.

 

VITABU REJEA:

The Visible Hand of God” (R. Roberts) – chapter 16

The Story of the Bible” (H.P. Mansfield) pp. 307-312

Law of Moses” (R.Roberts) – chapts. 14,15,16.

 

MASWALI YA FUNGU

 1. Nani alifanya mpango wa hema na kwa nini Israeli walihitaji?

 2. Taja madini aina mbili zilizotumiwa katika kujenga Hema na useme zinawakilisha nini?

 3. eleza maana ya:-

(a) Kinara cha kuwekea taa; (b) Birika; (c) Lango

 

MASWALI YA INSHA

 1. Ainisha sababu za sehemu ya Hema kuwa katikati ya Israeli?

 2. Kuna masomo gani kwa ajili yetu kwenye Baraza la nje na Patakatifu, katika Hema? Hakikisha unarejea kwenye madhabahu ya sadaka za kuteketezwa.

 3. Fafanua meza ya mikate ya wonyesho, kinara cha taa, madhabahu ya uvumba ndani ya Patakatifu na ueleze vinamaanisha nini kwetu leo.

 

SAMANI ZA HEMAYA KUKUTANIA

(Mchoro wake ukurasa 53 na ukurasa 54)

 

Swahili Title: 
HEMA YA KUKUTANIA: MAHALI PAKUKUTANA MUNGU NA ISRAELI
English files: 
Swahili Word file: