CSSA 2-1-23 - THE MOST SACRED PLACE IN ISRAEL

148. MAHALI PATAKATIFU PA PATAKATIFU KATIKA ISRAELI

Mahali Patakatifu zaidi palikuwa mahali nyeti kuliko pengine popote, kama jina lake linavyoonyesha. Ni kuhani mkuu peke yake aliruhusiwa ndani yake, na hata hivyo mara moja tu kwa mwaka baada ya “utakaso mahususi”. Kwa njia hii Israeli walitambua utakatifu wa Yahwe, Mungu wao. Ni mtengwa kutoka kiumbe wote, na mtu inampasa ajishushe mbele yake kama anataka kukubaliwa na Mungu.

 

Kutoka 25:10-22; 37:1-9

 

MAHALI PATAKATIFU ZAIDI

Upande wa mwisho wa Hema uligawanywa kwa pazia au ushungi kama uliopo mlangoni. Pazia lilitenga sehemu ya Patakatifu Pa Patakatifu kutoka sehemu ya Patakatifu na ilikuwa kupitia hapo ya kwamba Kuhani Mkuu aliingia mara moja tu kwa mwaka katika siku ya utakaso (Kut. 30:10). Ni yeye peke yake aliyekubaliwa kuingia ndani ya Patakatifu pa Patakatifu. Israeli walifunzwa kwamba Yahwe alikuwa mtengwa kutoka viumbe vyote vya mwili na kwamba mtu anahitaji mpatanishi aliyeteuliwa na Mungu kati yake na Mungu.

 

 

 

PAZIA

Pazia ilikuwa kazi ya kusukwa na kunakshiwa na nyuzi za rangi ya Bluu, huzurungi na nyekundu na makerubi wa dhahabu ilitundikwa kwenye nguzo nne zilizopakwa dhahabu. Ilitenganisha mahali Patakatifu na Patakatifu zaidi. Rangi za nyuzi za Pazia zinatumika kumaanisha yafuatayo ki-maandiko:-

 

Kitani safi – huwakilisha haki (Uf. 19:8)

 

Nyekundu – huonyesha dhambi (Isa. 1:18) Kristo ndiye mbebaji wa dhambi ambaye damu yake ilimwagika kwa ajili yetu (1 Pet. 2:24).

 

Hudhurungi – ni alama ya makuhani wakipatanisha kati ya wanadamu na Mungu (1 Tim. 2:5)

 

Bluu – ni mfano wa utakatifu kwa Mungu (Hes. 15:38-40)

 

SAMANI KATIKA PATAKATIFU PA PATAKATIFU

Samani ya pekee katika Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa ni SANDUKU la Agano. Lilikuwa sanduku lililotengenezwa kwa mti wa mshiti uliofunikwa kwa dhahabu pamoja na pete (bangili) za dhahabu kwenye kila kona na mishikio ya mbao zenye kupakwa dhahabu. Mfuniko ulioitwa “kiti cha Rehema”, ulikuwa na kipande bapa cha dhahabu pamoja na picha (mfano) wa makerubi wawili –moja kwenye mwisho huu na mwisho ule (kwenye kingo zake), kutokana na kipande kile kile cha dhahabu iliyopigwa. Makerubi wale wawili walikuwa na mbawa zilizoinamia juu ya kiti cha rehema. Nyuso zao zilitazamana kuelekea juu ya kiti cha rehema. Ndani ya sanduku mlikuwa na mbao zile za mawe, ambazo ziliandikwa sheria, kile chungu kilimowekwa manna, na fimbo ya Haruni iliyo chipuka.

 

MAKERUBI NA KITI CHA REHEMA

Kiti cha rehema kilielekeza mbele kwa Yesu Kristo, ambaye ni kiti chetu cha Rehema (Rum. 3:25). Kupitia kwake ndugu na dada zake humsogelea Mungu na katika yeye hupata msamaha wa dhambi zao. Makerubi ni umoja na kiti ya Enzi, kwa kutengenezwa kutokana na kipande kimoja cha dhahabu (Kut. 25:18-20). Kwa njia hiyo hiyo, waumini wa kweli inawapasa kuwa umoja na Yesu Kristo (Yoh. 17:20-21). Angalia kwamba nyuso za Makerubi zinaelekea kwenye kiti cha Rehema (Kut. 25:20), kama nyuso za waumini wa kweli inabidi kila wakati zigeukie kumwelekea Bwana wao (Waebrania 12:2).

 

DAMU NDANI YA PATAKATIFU ZAIDI

Mara moja kila mwaka katika siku ya utakaso, kuhani Mkuu aliingia kupitia PAZIA katika Patakatifu pa Patakatifu. Aliamrishwa na Mungu kunyunyizia kiti cha Rehema kwa damu (Walawi 16:14). Kama angejaribu kwenda ndani ya Patakatifu Pa Patakatifu bila kufanya hivyo, angeadhibiwa kwa kifo. Kiti cha Rehema kilinyunyiziwa kwa damu ya mafahali na mbuzi (Wal. 16:14-15). Kama Makerubi walivyoangalia chini, nyuso zao zilielekea kwenye kiti cha Rehema kilichonyunyiziwa damu. Kama macho yetu yanavyogeukia kwa Bwana Yesu Kristo “tunaona” dhabihu yake kuu kwa ajili yetu, na tunatambua kwamba bila kumwagika damu hakuna ondoleo la dhambi. Tunafahamu kwamba katika yeye imo sheria ya kweli, maana ya kweli aumkate wa uzima (uhai) Yoh. 6:48-51), na ufufo wa hakika ambao fimbo iliyokufa ya Haruni ambayo ilichipuka ni mfano.

 

UTUKUFU WA YAHWE

Patakatifu sana hapakuhitaji mwanga wa kutengenezwa kwa muda kwa kuwa palimulikwa na nuru ya utukufu wa Yahwe, iliyoangaza katikati ya makerubi na juu ya kiti cha Rehema (Kut. 29:43-46; 25:22).

 

Yesu alipotokea miaka 1960 iliyopita, alifananishwa na nuru au utukufu wa Yahwe ukiangaza mahali pa giza (Yoh. 1:5). Alidhihirisha utukufu wa Baba kwa watu katika yote aliyosema, na kutenda, na hata katika tabia ya ajabu aliyokuwa nayo, kulionekana mwangwi wa Utukufu wa kimungu. Hili lilifanyika kumulika zaidi alipofufuka kutoka kwa wafu na kufanywa asiyekufa (wa milele).

 

Sasa akiwa na hali asili ya Mungu na tabia yake, amekuwa, kwa kweli, ndiye wonyesho wa Utukufu wa kimungu.

 

Kama vile Kuhani Mkuu alivyouona utukufu wa Mungu juu ya kiti cha Enzi, tunaweza kuona ukifunuliwa na Bwana Yesu. Yohana anasema kwamba wanafunzi waliuona ndani yake “utukufu wa Baba” (Yoh.1:14). Huu ulikuwa ni utukufu wa adili yake Baba. Paulo baadaye alimwona katika utukufu wake kimwili (Matendo ya Mitume 9:3; 22:6), nao ulimwengu wote utauona utukufu wa Kristo wakati wa kurudi kwake. Utukufu wa Yahwe haukuangaza juu ya kiti cha Rehema tu peke yake, ila katikati ya Makerubi pia. Somo lililofundishwa kwa Israeli (na sisi) ni Israeli wa kweli inatupasa kudihirisha utukufu uleule kama wa kiti cha Enzi. Hivi ndivyo Yesu alimaanisha aliposema “Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu, aliye mbinguni” (Mathayo. 5:16). Tunaweza kudhihirisha au kuonyesha utukufu ulio wa Bwana Yesu sasa. Tutapata hali yake ya kutokuwa na dhambi na kuvaa umilele, na kuchangia utukufu wa Bwana sasa hivi, Kristo akikaa ndani ya mioyo yetu kwa imani (Waef. 3:17). Kama hiyo ndiyo sehemu (msimamo) wetu, mwishowe tutajipatia utukufu ulio wa Bwana Yesu sasa. Tutapata hali yake ya kutokuwa na dhambi na kuvaa umilele, na kuchangia utukufu wake. Ndipo Paulo alisema tunaishi “katika tumaini la utukufu wa Mungu” (Rum. 5:2). Alituambia pia ya kwamba Yesu wakati wa kurudi kwake atabadilisha miili yetu “ili ifanane na mwili wake wa utukufu” (Wafilipi 3:21). Kisha watu wataona ndani yetu, kama ndani ya Bwana wetu, utukufu wa Yahwe uliofunuliwa (Rum. 8:18). Jinsi gani tuwe na shukrani kupewa tumaini la utukufu namna hii ya kushiriki katika kueneza utukufu wa Mungu katika kizazi cha Ufalme. Ni heshima ya jinsi gani sisi tumepewa!

 

MAANA YA HEMA KWETU

Katika Waebrania 9:1-10, mtume anaonyesha jinsi kanuni, kafara na thamani za Hema zilikuwa mfano wa kristo na kazi yake. Baadaye anatamka kuwa Kristo ndiye kuhani Mkuu wetu aliyeingia mbinguni (mist. 11-12). Yeye ndiye mpatanishi ambaye kupitia kwake tunaweza kusogea na kumwabudu Mungu (Waebr. 10:19-24).

 

Hema ilikuwa mahali pa kukaa Mungu na mule alikutana na Israeli. Wakati kazi ya kristo imekamilika na ulimwengu umeokoka kutokana na dhambi, Mungu atakaa na watu kwa hakika kama tukistahili na kuzawadiwa uzima wa milele Mungu ataketi nasi daima.

 

UFUPISHO WA MAFUNDISHO YANATOKANA NA HEMA YA KUKUTANIA

Sehemu tatu za Hema ni kama hatua tatu ambazo kwazo tunaweza kushiriki utukufu wa Mungu katika Ufalme unaokuja.

 

 1. Baraza la nje – matayarisho

Wote inawapasa kuingia langoni (kupitia kwa kristo). Inawapasa wanawe penye birika kwa kusikia maelekezo ya Neno. Halafu inabidi wapitie madhabahu ya kafara kupitia ubatizo. Ni hapo tu wawezapo kuingia mahali Patakatifu.

 

 1. Patakatifu – kutembea katika Nuru

Mtu anafanya hili anapomkubali kristo kwa njia iliyowekwa. Inampasa kushiriki mkate wa uzima na kuzaa matunda kwa Mungu (mkate wa wonyesho). Inampasa aendelee kusali (uvumba).

 

 1. Patakatifu Pa Patakatifu – Kushiriki utukufu

Mtume anasema kwamba Pazia ni mfano wa mwili (Waeb. 10:20). Hivyo kwenda “nyuma ya pazia” nikufanyika asiyeweza kufa. Katika utukufu wa nuru inayoangaza inaonekana utukufu wa umalizio wa yule aliyempokea Kristo na ametembea bila kukoma kwenye nuru ya kweli yake.

 

Patakatifu zaidi paliposogelewa, wachache zaidi katika Israeli waliruhusiwa kuingia kama waabuduo. Hivyo:-

  1. Nje, ya Baraza walikuwepo maelfu ya Israeli

  2. Ndani ya Baraza Walawi na makuhani waliweza kuja

  3. Ndani ya Patakatifu ni Makuhani tu walioruhusiwa

  4. Katika Patakatifu Sana ni kuhani Mkuu pekee angeweza kuingia mara moja kwa mwaka.

 

Yesu ametuambia kwamba wengi wameitwa lakini ni wachache wamechaguliwa (wameteuliwa). Wataingia katika hali ya kutoweza kufa, hali ya ki-mungu, inayowakilishwa na mahali Patakatifu pa Patakatifu. Tusikilize wito ule na kwa shangwe tutafute kuijiwa kweli ili kwamba tuhukumiwe kuwa kwenye kustahili kuingia ufalme wake Mungu.

 

VITABU REJEA:

The Visible Hand of God” (R. Roberts) – chapter 17

Law of Moses” (R.Roberts) – chapts. 13.

Law and Grace” (W.F. Barling) pp 63-66

The Tebetuacle” (H.C. Gates)

 

MASWALI YA FUNGU

 1. (a) Mara ngapi Kuhani Mkuu aliruhusiwa ndani ya patakatifu pa Patakatifu?

(b) Ni vifaa na nyuzi za rangi gani zilitumiwa katika kutengeneza pazia na ni vipi hizi zilielekeza mbele kwa kristo?

 1. (a) Ni samani gani zilitumika katika Patakatifu sana?

(b) Nini kiliwekwa ndani ya sanduku la Agano?

 1. (a) Ni kwa nani kiti cha Rehema na Makerubi walielekeza?

(b) Ni nani alifananishwa na nuru au utukufu wa Yahwe?

 1. Kwa vipi Hema inakuwa sawa na ngazi tatu za wito wetu?

 

MASWALI YA INSHA

 1. Vilivyomo ndani ya Patakatifu sana vina maanisha nini kwetu?

 2. Kwa njia zipi Hema inaonyesha jinsi tunavyoweza kuingia ufalme wa Mungu?

 

Swahili Title: 
MAHALI PATAKATIFU PA PATAKATIFU KATIKA ISRAELI
English files: 
Swahili Word file: