CSSA 2-1-24 - TEACHERS FOR ISRAEL

149. WALIMU KWA AJILI YA ISRAELI

Makuhani na Walawi waliteuliwa ili kuwafundisha wana wa Israeli kuhusu sheria ya Mungu na kusudi lake kwao. Dhabihu zilikuwa zikionyesha mbele kwa Bwana Yesu Kristo nasi tunatakiwa kufahamu zina maana gani na zinatufundisha nini.

 

Hesabu 18; Kutoka 40:13-16.

 

KUTEULIWA KWA MAKUHANI (Hesabu. 18:1-7)

Hesabu 18; Kutoka 40:13-16.

 

Hema ilipomalizika kuwa mahali pa kukutanikia kati ya Mungu na Israeli, Musa alielezwa na Mungu kuteua makuhani.

 

Haruni akateuliwa kuwa kuhani Mkuu wanawe waliteuliwa kuwa makuhani. Mwisho wa utumishi wake Kuhani Mkuu alimrithisha wadhifa wake mwanawe mkubwa. Musa alipokea maelekezo ya kina kuhusu kuwekewa mikono (kutengwa) kwao katika ukuhani. Walitengwa kwa ajili ya kazi hii maalumu ya Mungu. Hata nguo zao ziliasisiwa nay eye (Kut. 28:1-4; 40:13-16)

 

Ilikuwasaidia familia ya Haruni katika wadhifa wao, kabila lote la Lawi walisaidia kazi yao. Waliwekewa mipaka katika kazi mahususi ambayo Mungu aliwapa ruhusa kufanya. Walawi waliruhusiwa katika baraza ya Hema, lakini hawakuruhusiwa ndani ya patakatifu sana, katika siku ya utakaso, ambayo ilikuwa mara moja kwa mwaka. Kazi ya makuhani na Walawi ilikuwa pamoja na:-

 

Hema ilipomalizika kuwa mahali pa kukutanikia kati ya Mungu na Israeli, Musa alielezwa na Mungu kuteua makuhani.

 

Haruni akateuliwa kuwa kuhani Mkuu wanawe waliteuliwa kuwa makuhani. Mwisho wa utumishi wake Kuhani Mkuu alimrithisha wadhifa wake mwanawe mkubwa. Musa alipokea maelekezo ya kina kuhusu kuwekewa mikono (kutengwa) kwao katika ukuhani. Walitengwa kwa ajili ya kazi hii maalumu ya Mungu. Hata nguo zao ziliasisiwa na Mungu Mwenyewe (Kut. 28:1-4; 40:13-16).

 

Ili kuwasaidia familia ya Haruni katika wadhifa wao, kabila lote la Lawi walisaidia kazi yao. Waliwekewa mipaka katika kazi mahususi ambayo Mungu aliwapa ruhusa kufanya. Walawi waliruhusiwa katika baraza ya Hema, lakini hawakuruhusiwa ndani ya patakatifu sana, katika siku ya utakaso, ambayo ilikuwa mara moja kwa mwaka. Kazi ya Makuhani na Walawi ilikuwa pamoja na:-

 

 • Katika Hema ya kukutania mojawapo ya majukumu ya makuhani ilikuwa kulinda moto wa madhabahuni kwa ajili ya kafara kuhakikisha unawake kila wakati.

 • Walitoa kondoo kwa ajili ya taifa, kafara ya kila jioni na asubuhi

 • Walipokea na kutoa kafara zilizoletwa na waabuduo.

 • Walitunza na kuhakikisha kuwa mafuta yamo katika kinara cha zile taa saba

 • Walibadilisha mkate wa wonyesho kila juma.

 • Walifundisha Israeli katika sheria za Mungu

 

MAISHA YAO: (Hes. 18:8-32)

Makuhani na Walawi hawakupewa urithi katika nchi (mist20-23). Hili liliwandisha kumtegemea kabisa Mungu kwa riziki zao. Watu wa nchi walitoa sehemu ya kumi katika mapato yao ili kuwatunza kwa kuwapatia Walawi fungu la kumi(moja ya kumi) iliyotokana na ongezeko la mapato yao (Hes. 18:24). Walifanya hivi kwa kila miaka mitatu (Kumb. 14:28-29). Kwa upande wao, Walawi waliwapatia Makuhani sehemu ya kumi ya sadaka walizopata kutoka kwa watu. “Sadaka” hii iliitwa“sadaka ya kuinuliwa”. Neno “inua” linamaana “kilichohuishwa” au “kilichotozwa” kama kodi. Kwa kweli kilikuwa ni cha Mungu.

 

Kwa maana hiyo kitu chochote kilichotolewa na watu, ikiwa ni pamoja na chochote walichowaptia Walawi kwa sehemu ya kwanza kabisa kilikuwa ni cha Mungu. Walikuwa wakirejesha kwa Mungu, sehemu ya mibaraka aliyowabarikia Mungu. Walipoacha kutoa fungu la kumi (kama walivyowahi kuacha kutoa wakati fulani) ilikuwa sawa na kumwibia Mungu ambacho kilikuwa haki yake (Malaki 3:8)

 

Hivyo Mungu aliwafundisha watu kwamba kitu chochote walichopata kilitoka kwake, na kilikuwa mali ya Mungu. Na ili kuthibitiha ukweli huu, aliagiza wampatie “fungu la kumi” kama sehemu yake, ambayo walipewa Makuhani wakiwa ndiyo wawakilishi wake katika Israeli.

 

Kwa nyongeza, Makuhani walipewa baadhi ya sehemu za dhabihu ambazo walikula pia kama haki yao.

 

Makuhani na Walawi walitazamiwa, kwa upande wao, kuyatoa maisha yao kumtumikia Mungu. Walijifunza na kuwafundisha wana wa Israeli Torati (Walawi 10:11; Kumb. 24:8); walihudumu kama waamuzi wake (Kumb. 17:9), na Israeli walipositawi juu ya nchi, walipewa miji katika taifa lote (miji 48-Hes. 35:2-8). Kwa hiyo kila wakati walikuwa tayari kufundisha na kuwaelekeza watu (Mal. 2:7).

 

DHABIHU:

Sehemu kubwa ya kazi ya Makuhani, na ibada ya Israeli ilihusu utoaji wa dhabihu. Sadaka hizi walizotoa ilibidi zisiwe na kilema wala dosari (kanuni hii ya kawaida kuhusu sadaka imetajwa katika Mambo wa Walawi 1:2;3 kuhusu dhabihu za kuteketezwa).

 

Dhabihu zilikuwa ziligawanywa katika makundi ya aina mbili kuu:-

 

Dhabihu za watu binafsi: Hizi zilitolewa na watu binafsi nazo zilikuwa sadaka sadaka za dhambi na hatia, sadaka za kuteketezwa, sadaka za unga, sadaka za amani.

 

Dhabihu za Taifa: Hizi zilitolewa kila siku asubuhi na jioni kwa ajili ya taifa, na pia katika matukio mengine, kwa mfano, katika siku ya Upatanisho.

 

Dhabihu za watu binafsi kwa ajili ya dhambi zilifanyika mara kwa mara lakini hizi hazikutosha. Mungu aliweka Siku maalumu ya Upatanisho kwa ajili ya Taifa la Israeli, walipokiri na kutubu kwa mbele ya Kuhani Mkuu na kusamehewa na Mungu. Wote wawili aa.

 

Anayetubu na Makuhani walijiandaa hasa kwa unyenyekevu kwa ajili ya siku ile muhimu.

Taifa dhabihu:

Sadaka ya mtu binafsi kwa ajili ya dhambi yalifanywa mara nyingi lakini haya hayakuwa kutosha. Mungu alipanga Siku maalum ya upatanisho kwa ajili ya dhambi ya yote ya Israeli, baada ya hao watu kukiri na Kuhani Mkuu na yafuta na Mungu. Wote wawili na makuhani alikwenda kwa juhudi kubwa ili kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo muhimu na kubwa.

SADAKA YA MTU BINAFSI:

Sadaka za kuteketezwa (Walawi 1:1-3)

Sadaka hizi ni mnyama au ndege iliteketezwa kabisa na moto juu ya madhabahu. Kwa hili, watoaji wa dhabihu walionyesha kuwa wanataka kujitoa wenyewe kwa ajili ya kumtumikia Mungu kwa kujiweka wakfu kwa ukamilifu.

Sadaka za vyakula (Mambo ya Walawi 2:1-2)

Hizi hazikuwa nyama bali unga wa nafaka uliochanganywa na mafuta na kuokwa bila ya kuweka chachu.

Sadaka za amani (Walawi 3:1-5)

Hizi zilikuwa sadaka za hiari wakati watu walipopenda kumtolea Mungu, kwa mfano wakati walipokuwa wamepokea baraka kutoka kwa Mungu nao wakapenda kumshukuru.

Sadaka za dhambi (Walawi 4:22-35)

Wakati mtu akitenda dhambi pasipo kukusudia, alitakiwa kutoa sadaka ya dhambi. Angeleta mnyama mchanga na kumchinja na damu yake ingemwagwa chini ya madhabahu kwa ajili ya sadaka kwa Mungu. Damu ilikubaliwa na Mungu kama kifuniko kwa ajili ya dhambi, kwa kuwa iliwakilisha uhai. Mungu alisamehe dhambi za waliotoa sadaka kama walikuwa kweli na moyo wa toba.

SADAKA KWA AJILI YA TAIFA-SIKU YA UPATANISHO (Mambo ya Walawi 16)

Siku ya Upatanisho ilikuwa ni siku ya muhimu sana katika siku za mwaka wote kwa wana wa Israeli. Iliitwa hivyo kwa kuwa katika siku hiyo katika siku hiyo upatanisho ulifanyika kwa ajili ya dhambi za nchi. Haruni alitakiwa kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe na kwa ajili ya nyumba yake na kwa ajili ya (mkutano wote wa Israeli) taifa. “Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa ; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za YAHWE” (mstari 30).

Upatanisho ni kifuniko cha dhambi, ni tendo llinalomrudisha mtu karibu na Mungu. Wakati wana wa Israeli walipomtolea sadaka za dhambi Mungu, damu ya wanyama ilikubaliwa na Mungu kama kifuniko au upatanisho kwa ajili ya dhambi. Toba ilikuwa ni ya muhimu sana mbele za Mungu ili aweze kusamehe dhambi na kupokea uhai(damu) ya sadaka badala ya uhai wa mtenda dhambi.

Kuhani Mkuu alitakiwa kuoga na kuvaa mavazi meupe yalitengenezwa kwa kitani safi. Mavazi yake ya gharama au thamani aliyaweka kando kwa sababu siku hiyo ilikuwa ni siku maalumu ka ajili ya kufunga na kuomba msamaha. Siku hii ilikuwa ni kwa ajili ya maandalizi kwa jili ya yeye kuingia ndani ya Patakatifu pa Patakatifu na katika uwepo wa Mungu. Ilikuwa ndiyo siku peke ya mwaka ya kuingia ndani ya Patakatifu pa Patakatifu ambapo Kuhani Mkuu na ni yeye peke yake tu aliyepewa heshima hiyo. Sadaka za dhambi na sherehe za siku hiyo ilikuwa ni kivuli cha Kristo kwa njia zote.The sacrifices and the ceremonies of this day were a type of Christ in a very special way. Sadaka na sherhe zote za siku hiyo zilielekeza mbele kwenye kazi kubwa mno ambayo Kristo angeifanya ya upatanisho kwa ajili ya dhambi za watu wanaomwenda Mungu kupitia Yesu Kristo (Yohana 3:16).

Mavazi matakatifu yalivaliwa siku ya tendo hiliyaliwakilisha haki kamilifu ya Kristo asiye kuwa na kasoro (Zab. 132:9, 16; Ufu. 19:8).

Damu ya wanyama ilikuwa ni kivuli cha damu ya Kristo iliyomwagika kwa ajili ya ondoleo la dhambi, kadhalika Kristo ndiye sadaka kwa ajili ya dhambi zetu (Waeb. 9:28). Yeye ndiye Mwanakondoo wa Mungu, mkamilifu, mtiifu asiye na doa lolote (Yohana 1:29).

Kuhani Mkuu alikuwa mfano wa Kristo na kazi kubwa ambayo sasa anafanya ni ya kutuombea. Kristo anatuombe sisi kwa Mungu na kwa njia yake,wale waliobatizwa katika Kristo humwomba Mungu msamaha kwa ajili ya dhambi zao.

Siyo kama sadaka ya dhambi wana wa Israeli ambao iliwapasa kutoa sadaka za dhambi kila mara, kila mwaka, hakuna dhabihu tena inayotakiwa kwa ajili ya dhambi baada ya Kristo kumwaga damu yake. Kristo alikuwa ni sadaka kamilifu kwa ajili ya dhambi na dhabihu ambaye aliyatoa maisha yake mara moja tu kwa ajili ya wote. Kwa njia ya dhabihu ya Kristo, tunasamehewa dhambi zetu kama tutatubu na kuomba msamaha( Matendo ya Mitume 2:38;Warumi 6:3-4). Ipo tofautitena kati ya wanyama waliotolewa kuwa sadaka za dhambi na dhabihu ya dhambi aliyoitoa Kristo. Dhabihu za dhambi walizotoa Israeli, walipomchinja mnyama kwa ajili ya dhambi, mnyama yule alikufa moja kwa moja. Lakini, Kristo alipokufa, alifufuka kutoka kwa wafu na kupewa uzima wa milele. Na kwa hiyo amefanyika kielelezo cha tumaini letu (Warumi. 4:25).

DHABIHU ZETU

Tunatakiwa tumtolee Mungu dhabihu za aina tofauti. Hatutarajii tutoe sadaka za dhambi au sadaka za kuteketezwa pamoja damu ya wanyama. Mungu anatuhitaji tujitoe wenyewe kwa utii wa mawazo yetu na kwa mioyo yetu tumtumikie (Warumi 12:1-2). Tendo la kwanza la utii ni tendo moja kati ya yote yaliyo ya muhimu la ubatizo linalofuata baada ya kuamini na maungamo mazuri ya imani. Na ndipo tunapokuwa katika nafasi nzuri sana ya kusamehewa dhambi zetu na kuoshwa , tukijiandaa kumtumikia Mungu katika maisha yetu yote. Ni lazima tutoe tamaa zetu mbaya, nia zetu, mawazo yetu mabaya, matamanio yetu, muda wetu. Lililo jema pekee ni kumpendeza Mungu, na ni lazima tujiandae kumtumikia kwa kuwa hakuna kitu chochote tunachoweza kumpatia Mungu.

VITABU REJEA:

"The Law Of Moses" (R. Roberts)—Chapters 24 and 25

"Law And Grace" (WF Barling)—Ch.8, pp. 94-101; ch.9, pp.114-121

 

MASWALI YA VIFUNGU:

 1. a) Je, Kuhani Mkuu na Makuhani walitoka kabila lipi?

b) Ni kabila lipi ambalo Mungu alimpatia Musa ili lisaidie kazi ya kufundisha?

 1. a) Ni kwanini Makuhani na Walawi hawakupewa urithi katika nchi Israeli?

b) Je, ni sehemu gani watu waliwapatia Walawi?

 1. a) Upatanisho ni nini?

b) Je, tunatakiwa tutakiwa tutoe aina gani ya dhabihu?

 1. Mambo gani yaliyofanyika "Siku ya Upatanisho" ambayo yalitimizwa katika Yesu Kristo?

 2. Ni jinsi gani Kuhani Mkuu anavyomwakilisha Bwana Yesu Kristo?

MASWALI YA INSHA:

 1. Eleza majukumu muhimu waliyofanya Makuhani katika Israeli?

 2. Orodhesha aina tofauti ya sadaka zilitolewa na ntu binafsi wakati wa Sheria ya Musa na eleza kwa ufupi mafundisho tunayofundishwa.

 3. Eleza Kuhani Mkuu alifanya nini Siku ta Upatanisho.

Picha (mchoro wote kamili) ukurasa mzima

 

 

Swahili Title: 
WALIMU KWA AJILI YA ISRAELI
English files: 
Swahili Word file: