CSSA 2-1-25 - FEASTS FOR YAHWEH

150. SIKUKUU ZA YAHWE
Tufikirie Sikukuu za Kukumbukwa na Israeli na mafundisho yake kwetu.
Mambo ya Walawi 23
SIKUKUU ZA BWANA
Wana wa Israeli walitakiwa wakusanyike pamoja nyakati fulani za mwaka ili kuzitunza sikukuu hizi. Sikukuu hizi hazikuwa kwa ajili ya kula na kunywa. Watu walikusanyika pamoja kumsifu Mungu na kukumbuka matendo makuu ambayo Mungu aliwatendea. Zilikuwa ni Sikukuu za Kukumbukwa. Zilitunzwa kwa umakini sana sawa na nyakati za furaha (Kumbukumbu la Torati 16:14). Walimtolea Mungu kafara.
 
Zilikuwepo sikukuu saba, ikiwemo na Siku ya Upatanisho.Tafadhari angalia kwenye kalenda
Orodha ya sikukuu:-
Sikukuu za tatu za kwanza: Pasaka, Sikukuu ya Mkate usiotiwa Chachu na Malimbiko ya mavuno, hizi zilifanyika mwezi wa kwanza na zote zilijumuishwa katika Sikukuu ya Mkate usiotiwa Chachu.
Sikukuu ya Nne: Sikukuuu ya Pentekoste au Sikukuu ya Majuma ilifanyika mwezi wa tatu.
Sikukuu tatu za mwisho: Sikukuu ya kuzipiga Baragumu, Siku ya Upatanisho, na Sikukuu ya Vibanda hizi zote zilifanyika mwezi wa saba.
PASAKA (Mambo ya Walawi. 23)
Sikukuu hii iliwakumbusha wana wa Israeli tukio kuu katika maisha yao. Kutoka. 12:1-13 ina elezea kila kitu kuhusu Pasaka ya kwanza kabisa ambayo ilifanyika katika nchi ya Misri. Tunaweza kukumbuka jinsi wa Misri walivyokuwa wamefanya watumwa wana wa Isreali, na ingawa Mungu aliawaagiza wawape ruhusu. Musa aliagiza kila familia ya wana wa Israeli wachague mwanakondoo siku ya kumi ya mwezi wa kwanza. Na siku ya 14 wamchinje na kupaka damu yake kwenye miimo ya mlango na kizingiti cha juu. Usiku huo Malaika wa Mauti akapita katika nchi. Akapita juu ya nyumba za wana wa Israeli ambazo tayari zilikuwa zimelindwa na damu, lakini yule Malaika akaingia ndani ya nyumba za Wamisri na kumwua kila mzaliwa wa kwanza katika kila nyumba. Kwa hiyo kukawa na kilio kikuu katika Misri na wakawafukuza wana wa Israeli ili watoke katika nchi yao. Wana wa Isareli walitakiwa kutunza na kukumbuka tukio hili kila mwaka. Siku ya 14 ya mwezi wao wa kwanza wa Abib, walifanya ukumbusho kwa kula mwanakondoo asiyekuwa na kasoro.
Sikukuu hi ingewakumbusha kwamba—
Walikuwa wameokolewa na damu ya mwanakondoo;
Mwanakondoo alikuwa hana ila. Alichinjwa na damu yake ilitumika kuwaokoa wana wa Israeli kama Mungu alivyokuwa ameagiza.
Walikuwa wameokolewa na nguvu za Mungu. Mungu alikuwa amewaokoa kutoka katika jeshi la Misri lenye nguvu, na allikuwa amewaleta katika nchi ya Kanaani (Kutoka. 12:37-51; 14).
Yahwe(BWANA) alitukuzwa na kutakaswa mbele ya macho ya Wamisri
Kristo ndiye Pasaka wetu (1 Wakorintho. 5:7)
Kristo alikuwa "mwana kondoo" asiye na ila. Tunaweza kuokolewa na damu yake ya thamani (1 Petro. 1:19). Yesu Kristo aliyefufuka anaweza kutuokoa kutoka katika utumwa wa dhambi na kutuleta kwa Mungu (1 Petro. 3:18).
SIKUKUU YA MKATE USIOTIWA CHACHU (Mambo ya Walawi. 23:6-8)
Sikukuu hii ilikuwa ikifanyika muda wa siku saba baada tu ya Pasaka, kuanzia siku ya 14 mpaka siku ya 21 ya mwezi wa Abib. Watu walikusanyika pamoja,na walimtolea Mungu sadaka. Wakati huo walikula mikate isiyotiwa chachu. Mikate isiyotiwa chachu ni Mikate ambayo ilitengenezwa pasipo kuweka chachu(hamira). Haichachushwi kama vile ilivyo mikate ilio na chachu. Mtume Paulo anatuambia kuwa chachu huwakilisha uovu, kwa hiyo mkate usiotiwa chachu huwakilisha maisha huru ya kutokuwa na ubaya na uovu (1 Wakorintho. 5:6-8; 2 Wakorintho 7:1). Kwa hiyo Juma hili la Mikate isiyotiwa chachu iliwakumbusha wana wa Israeli kuwa walikombolewa ili watu waliojitenga kabisa na waliopaswa kuishi maisha ya utakatifu. Kwanza ukombozi na kisha waishi maisha ya utakatifu. Matumizi ya sikukuu hii katika maisha ya wafuasi wa Kristo yanaonekana katika jitihada ya maisha yao jinsi wanavyoenenda kama Mungu anavyowataka wafanye.
 
SIKUKUU YA MALIMBUKO YA MAVUNO (Mambo ya Walawi. 23:10-14).
Katika juma lile la mikate isiyotiwa chachu pia ilikuwemo Sikukuu ya Malimbuko ya mavuno. Mazao yaliyokuwa ya kwanza kukomaa ilikuwa shayiri. Masuke ya shayiri yale ya kwanza kukomaa yalikusanywa pamoja na kufungwa mganda na kupekwa kwa kuhani kama sadaka kwa Mungu. Watu hawakula mkate au masuke machanga ya nafaka mpaka yale ya kwanza kukomaa wawe wamepeleka sadaka kwa Mungu.
Hili, pia lilikuwa ni tendo la shukurani kwa kuwakumbusha watukuhusu wema wa Mungu kwao wa kuwapatia mahitaji yao muhimu ya maisha. This, too, was an act of thanksgiving to remind the people of God's goodness to them in providing them with the necessities of life. Kuleta malimbiko ya kwanza ya mavuno iliashiria mambo mema yanayokuja , baraka ya mavuno mengi ambayo wanapewa na Mungu
Kwa namna moja ya mfano, sikukuu hii inatukumbusha ufufuo. Yesu ndiye mtu wa kwanza kufufuka katika wafu, na kwa sababu hiyo anajulikana kuwa "mzaliwa wa kwanza" wa wao waliokufa. Na baadaye, wakati ufufuo utakapotokea kutakuwa na "mavuno" mengi, na wengi wa hao walalao katika mavumbi wataamka. Wengi watapata uzima wa milele (1 Wakorintho. 15:20-23).
SIKUKUU YA PENTEKOSTE (Mambo ya Walawi. 23:15-22)
Hii sikukuu ilifanyika siku 50 baada ya siku ya kwanza ya Mikate isiyotiwa Chachu. Na mara nyingi iliitwa Sikukuu ya Majuma kwa sababu yalihesabiwa majuma 7 kuanzia Sikukuu ya Malimbuko ya Mavuno. Wakati wa majuma haya ngano ilikuwa imekomaa tayari kwa mavuno, na ni katika Sikukuu hii watu walipomshukuru Mungu kwa mavuno ya nafaka. Mikate miwili ya iliyotengenezwa kutokana na unga mwembamba(laini sana) ililetwa kwa kuhani kama sadaka kwa Mungu. Katika sadaka hii iliruhusiwa kuweka chachu. Ilikuwa inakumbusha kuwa ndani ya kila mtu kuna uovu, na inatupasa kila wakati tujitahidi kupambana na udhaifu wetu ili tuwe kama Kristo. Na kama Israeli walivyofurahi mbele ya Yahwe (BWANA), pia na sisi, tunapaswa kufurahi kwa sababu ya wema wa Mungu kwetu (Kumbukumbu 16:11). Siku ya kwanza ya Pentekoste baada ya Kristo kupaa , Roho Mtakatifu aliwashukia Mitume (Matendo ya Mitume sura ya 2). Wakati huo waumini walikusanyika pamoja na kuunda ekklesia ya kwanza. Mikate iliyotolewa kuwa sadaka siku ya Pentekoste inatukumbusha ekklesia iliyoundwa Siku ya Pentekoste. Kama vile mikate ilivyotengenezwa kutokana na chembe chembe nyingi za unga na kuunda umbo la kitu kimoja au mkate, kadhalika na ekklesia imeundwa kutokana na wanafunzi mbalimbali kwa njia ya umoja katika imani (l Wakorintho 12:12, 20; 1 Wakorintho. 10:17).
Na pia kwa ajili ya tendo la shukurani ili kumpendeza Mungu , hawakutakiwa kuvuna mavuno yote ya kila shamba lao, bali walipaswa kuacha kabisa kila pembe ya shamba lao na masazo ya mavuno kwa ajili yao maskini. Masazo yalikuwa ni masuke ya nafaka ambayo wavunaji hawakuwa wameyaona mara ya kwanza walipokuwa wanavuna mavuno.
SIKUKUU YA KUZIPIGA BARAGUMU (Mambo ya Walawi. 23:23-25)
Sikukuu hii na sikukuu mbili zinazofuata zilifanyika mwezi wa saba.Sikukuu hii ilifanyika siku ya mwezi wa saba . Ilikuwa ni siku ya kuzipiga baragumu ili kuutangaza mwezi mpya na kuikaribia Siku iliyo kuu ya Sikukuu ya Upatanisho. Ni siku inayotuelekeza siku ya kurudi kwa Kristo na kukusanyika pamoja kwa Israeli waliotanyika katika nchi yao. Na tumaini letu ni Tumaini la Israeli. Tunasubiri muda wakati wa " parapanda ya Mungu" italia kuwakusanya wateule wake au waaminifu wake waende kwa Mungu (1 Thess. 4:16-17). Kwa tendo hili, Israeli wote watarejeshwa katika nchi yao na watamwamini Kristo kuwa Masihi wao.
SIKUKUU YA UPATANISHO (Mambo ya Walawi. 23:26-32)
Hii "sikukuu", ilifanyika siku ya kumi ya mwezi wa saba, kwa asili ilikuwa ni “kufunga” siku ya pekee ya kufunga ambayo Israeli walipaswa kuiadhimisha. Siku hii Israeli wote hawakufanya kazi na “walizitesa nafsi zao”, maana yake, wawe wanyenyekevube na kujutia dhambi zao nyingi walizokuwa wamezitenda. Ilikuwa ishara ya wakati unaokuja wa toba ya kweli ya Israeli, msamaha na upatanisho na Mungu. Siku ya Upatanisho ndiyo siku ya pekee ya mwaka ambayo Kuhani Mkuu angeingia Patakatifu pa Patakatifu katika Hema la Kukutania (angalia somo lililotangulia).
 
SIKUKUU YA VIBANDA (Mambo ya Walawi. 23:34-44)
Sikukuu hii pia inaitwa Sikukuu ya Kukusanyika kwa kuwa ilikuwa ikifanyika majira ya kupukutika majani wakati wa mavuno mengi ya nafaka, divai na mafuta vilikuwa vimekusanywa. Iliadhimishwa kuanzia siku ya 15 mpaka siku ya 22 ya mwezi wa Saba. Ilikuwa siku ya kufurahi na kumpashukurani wakati Israeli walipoonyesha furaha zao mbele za Mungu.
 
Walikumbuka kuwa Mungu aliwakomboa kutoka katika utumwa wa Misri na kuwaleta katika nchi yenye kujaa mambo mema. Wakati wa siku saba Israeli walikaa katika vibanda au mahema (ndiyo asili ya hema ya kukutania) iliyotengenezwa kutokana na matawi ya miti. Sikukuu hii , inatupeleka kwenye wakati wa mavuno mengi, ambayo ni matokeo ya kazi ya Kristo wakati wa utawala wa millennia(miaka elfu moja). Tukitazimia siku ambapo mataifa yote watafurahi pamoja katika Sikukuu hii wakati wa utawala wake (Zekaria. 14:6-9).
MAMBO YA KUZINGATI KUTOKANA NA SIKUKUU
Huu hapa ni muhitasari wa maana ya sikukuu kwa Israeli:
Sikukuu ya Pasaka: Kumega Mkate na kunywa Divai inatukumbusha ukombozi unaopatikana kwa njia ya damu ya Christo (1 Petro. 1:19), na uzima wa milele tunaoupata kupitia nguvu ya Kristo aliyefufuka (Wafilipi. 3:10, 21).
Sikukuu ya Mikate isyotiwa Chachu: Tunatambua majukumu yetu na ni lazima tujitahidi kuishi maisha matakatifu mbele za Mungu (Tusiweke "chachu" katika maisha yetu).
Sikukuu ya malimbuko ya mavuno: Tunakumbushwa tena kwamba Kristo ni mzaliwa wa kwanza katika wao waliolala. Ndiye pekee yake aliyefufuka kutoka katika wafu, na hafi tena
Sikukuu ya Pentekoste: Tunashauku kama nini kuwemo katika ufufuo, mavuno kwa wale walio katika Kristo siku atakayorudi.
Sikukuu ya Baragumu: Tunafaha kuwa tuna miili ya kufa, na ya kuwa uhai wetu ni wa muda mfupi. Wakati utafika ambapo parapanda (baragumu) italia nasi tutahukumiwa na Kristo. Tunatakiwa tujiandae tuwe tayari.
Sikukuu ya Upatanisho: Toba, na kumwoma Mungu ili atusamehe ni kupitia Kuhani Mkuu.
Sikukuu ya Vibanda: Nasi tunatazamia wakati tutapofurahi pamoja na Kristo katika Ufalme wake.
MAKTABA YA KUREJEA:
"The Law of Moses" (R. Roberts)—Chapter 21
"Law and Grace" (WF Barling)—Pages 133-150
MASWALI YA AYA:
1 a. Ni nani Pasaka wetu?
Mikate ambayo haikutiwa chachu ni nini na ilimaanisha nini kwa wana wa Israeli?
Ni nani anayefahamika kuwa "mzaliwa wa kwanza" katika wafu?
2 .a Sikukuu ya Pentekoste iliwakumbusha Israeli mambo mengi.Ni mambo gani hayo?
Ni kwanini wana wa Israeli walifunga siku ya Upatanisho?
Sikukuu ya Vibanda ilimaanisha nini?
MASWALI YA INSHA:
Fafanua kwa kina Sikukuu za Kukumbukwa na Israeli.
Eleza Sikukuu ya Pasaka na ina maana gani kwa wafuasi wa Kristo

 
Wasomi wanaweza kunakiri mchoro huu wa Kalenda na kuweka ndani ya Biblia zao na kuipaka rangi kutegemeana na shughuli za wakati huo kama vile mvuno an kulima .
UHALISIA UNAOONESHA NADHARIA YA MAGEUZI KUWA SIYO SAHIHI
MIANYA ILIYOPO KATI YA VIUMBE ANWAI
Mwanzo sura 1 inahusu aina “mbalimbali” za viumbe hai, kama vile, kila ndege arukaye kwa jins yake(mstari 21) na kila “wanyama wa mwitu kwa jinsi zake” (mstari 24).Elimu ya viumbe hai(Bailojia) inaainisha mianya iliyopo kati ya kiumbe na kiumbe. Muingiliano katika kuzaliana kati ya viumbe tofauti haiwezekani katika hali yoyote ya kawaida. Unapotokea mwingiliano upo kufuatana na mazingira ya aina fulani kibinadamu,kiumbe kitakacho tokea hakiwezi kuzaliana isipokuwa kwa kutumia njia hii hii iliyotumika- matokeo hayo yaliyo pelekea kuzaliwa kitu tofauti yanasababisha ubunifu wa kiumbe hicho — hiki ni kikwazo asili cha kuendeleza aina ile ile ya viumbe.
Hiki ni kikwazo asili cha kuendeleza aina ile ile ya viumbe.
Mtazamo huu si ule ambao nadharia ya mageuzi inaweza kuutolea maelezo. Kama mageuzi yanatokea , pangekuwa na ushahidi wa mtambuka wa asili jinsi aina fulani ya kiumbe inavyogeuka kuwa aina nyingine ya kiumbe. Lakini mianya iliyopo ni mikubwa wanavyoweza kudai wana mageuzi. Hata pale ambapo binadamu amekusudia kwa makusudi kuendeleza viumbe vipya bado hajafanikiwa. Wanaofunga mbwa wanapojaribu kuzalisha aina nyingine ya kiumbe bado wanapata mbwa na ndivyo inavyotokea kwa wakulima wa maua ya waridi wanapata maua ya waridi. Hata watu waliojaribu kwa muda mrefu kumbadilisha inzi anayeharibu matunda ili awe mdudu mwingine asiye na madhara lakini wameshindwa.
Mwaya uliopo kati ya mtu na jamii ya nyani ni jambo la kutaharisha sana kiasi cha kuhuzuisha wale wanoamini mageuzi. Ikiwa mtu ni jamii ya nyani, aliwezaje kuwa na ubongo, ijapokuwa mdogo kidogo kuliko wa nyani, ukaweza kufikia uwezo mkubwa mara milioni moja? Ni kitu gani kilichomwezesha huyu mtu kuweza kuwa mbunifu ,kuwa mwanahisabati, mwanafalsafa,mfizikia au mshairi? Ni kwa nini ni yeye peke yake mwenye uwezo wa kuwasiliana kwa kutumia lugha na kurithisha maarifa kutoka kizazi hadi kizazi kingine? Je ni jinsi gani alivyoweza kukuza mikono maalum inayomwezesha kufanikisha akili kufanya kazi kwa ufanisi? Ni mchakato gani uliotumika "kustahimili maafa yatokanayo na mazingira awe na tabia ya utu, juhudi ya kuwa mbunifu, kupenda muziki, kupenda utanashati, na kupenda maadili.
Nadhari ya mageuzi imeachwa kupapasa pasa juu ya maswali hayo, lakini Biblia imeeleza waziwazi kuwa mtu aliumbwa kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba mtu (Mwanzo 1:27).
2. KUSHINDWA KUPATA UTHIBITISHO WA VISIKUKU (FOSILI).
Darwini na wenzake walikuwa na matumaini kwamba utafiti wa kijiologia ungeweza kuonyesha visikuku vinavyoonyesha mabadiliko ya hatua kwa hatua kutoka aina ya kiumbe kimoja na kingine. Baada ya miaka 100 ya utafiti na ugunduzi wa visikuku mamilioni, miaya kati viumbe vya aina moja bado upo palepale. Zaidi ya hapo kumbukumbu zilizopo zinaoanishwa na mianya iliyopo katika viumbe vinavyoishi katika ulimwengu huu.
Hakuna uwezekano wa kujaziliza mianya kati ya:
Samaki na jamii ya vyura
Jamii ya vyura na jamii ya mijusi
Jamii ya mijusi na jamii ya ndege
Jamii ya mijusi na jamii ya wanyama.
Wana wanadharia ya mageuzi wameshindwa kabisa kuoesha ushahidi wa (fosili) kisikuku kuhusu nadharia ya mageuzi ya mtu, lakini visikuku vya watu wa zamani vilivyopatikana vinaonesha bado ni Homo sapiens wakitembea wima na kuwa na ubongo mkubwa sawa na mtu wa siku hizi. Madai ya kudhania kuwa visikuku vya kabla ya mtu kuwepo yamejikita katika ushahidi nadra unaopelekea wana nadharia ya mageuzi kutoaminika.
Kama mtu alitokana na kiumbe duni, basi pangelitokea viumbe maelfu maelfu ya jamii ya mtu wa kale (hominoids) kuhifadhiwa kikamilifu na kuwekwa kwenye tabaka linaloeleka. Huxley, mwana nadharia ya mageuzi maarufu aliwahi kusema kwamba utetezi wa mageuzi ungeweza kuthibitika au kushindwa kutokana na kumbukumbu ya kisikuku. Alikuwa sahihi. Imeshindikana!
3. UTATA WA UASILIA WA UHAI
Nadharia ya mageuzi inadai mabadiliko yalitokea hatua kwa hatua kwa kipindi cha miaka mingi. Lakini mionekano mbalimbali iliyopataikana katika asilia inaweza kupangwa makundi yote au bila kuwepo kitufosili (kikukuu)
Pamoja na jicho kuwa na uwezo mkubwa haliwezi kuona kila kitu mpaka liwe limezwa kikamilifu. Hata sikio haliwezi kusikia mpaka viungo vyote viwepo na viwe vishirikiane. Ni kwa jinsi gani nadharia ya mageuzi inavyoweza kueleza namna viungo hivi vilivyotokea hatua kwa hatua?
Ndege huruka kwa sababu: (1) manyonya yake (ni ngumu kuelezea jinsi manyoya yanavyofanya kazi), (2) mwili mwepesi, (3) mabawa yenye misuli ya nguvu. Je mambo haya yaonekane kuwa yalitokea kiupofu kwa bahati kuwepo kwa wakati huo huo , inaonekana kwamba mambo yote hayo matatu ili yafanye kazi kwa ukamilifu kabla ya ndege kujiandaa na kuruka na hivyo kufaidika zaidi kuliko viumbe vingine? Zaidi ya hayo,je , hiyo nafasi ya upofu ilitokea siyo mara moja, lakini mara tatu, uwezo wa kuruka ungetenganisha jinsi ya kuruka ya ndege,popo na wadudu?
Nyoka ana kiungo maalumu cha kuhifadhi sumu ambacho kinahitaji:(1) kiungo maalumu cha kutengeneza sumu, (2) kiungo malumu cha kuhifadhia, (3) mfumo salama wa kuisafirisha(meno), (4) silika ya matumizi ya sumu ili kuleta athari, (5) uhakika wa nyoka kutoathiriwa na sumu yake. Ni jinsi gani viungo hivi viliweza kujengeka hatua kwa hatua?
Ulimwengu umejawa na ugumu ambao nadharia ya mageuzi haiwezi kuelezea. Jawabu la uadilifu ni hili: "Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia" (Zaburi. 104:24).
4. TATIZO LA MWANZO WA UHAI
Ilidhaniwa kwamba uhai ulitokana na mageuzi ya chembe "ndogo sana". Hata hivyo, uhai mdogo sana upo mbali sana na ule udogo.
Viumbe vidogo sana vinavyo hai ni virusi ambavyo vinaundwa na kiini kikubwa cha nyukileiki asidi yenye kuzungukwa na moleku ya protini. Je, kuna uwezekano kuwa kirusi kilipitia mageuzi ya hatua kwa hatua? Jambo la kwanza, nyukileiki asidi ni kimikali yenye utata mkubwa imegumbikwa na makumi elfu ya makumi elfu ya atomu zilizopangilika kwa ustadi mkubwa. Jambo la pili, protini zenyewe pia ni kubwa mno na zenye moleku tata. Jambo la tatu, asidi ya nyukileiki haiwezi kustawi na kuongezeka pasipo moleku zake za protini. Jambo la nne, na linalokanganya sana, kirusi ni kimelea ambacho kinaweza kukua na kuzaliana kikiwa kinaishi ndani ya mwili wa kiumbe kingine kinachoishi kilicho kikubwa zaidi ya kimelea hicho.
Nadhari ya mageuzi kwanza ingehitaji fursa ya kizazi cha mbali, kiumbe chenye seli moja tata, kama vile bakteria. Jambo la kushangaza katika nadhari hii ya mageuzi ni kama kichekesho tu.
5. NADHARIA YA MAGEUZI BILA KUFIKRIA UWEPO WA MUNGU
Mara ya kwanza nadharia ya mageuzi ilifikiriwa kwamba mabadiliko yalitokana na mwenendo, matumizi, kutokutumia, au mabadiliko yaliyotokana na mazingira ya kurithiwa. Lakini baada ya miaka mingi ya utafiti usio na matokea tarajiwa, nadharia hii iliachwa kabisa.
Baada ya hapo ilikuja nadharia ya "Darwini- mambo leo" iliyoeleza mabadiliko katika msingi wa kubahatisha ikijumlisha na viumbe kuishi kwa kadri ya uwezo wa kila kiumbe. Mabadiliko yanatokana na kubadilika kwa vizazi kutokana na miali kuharibu vinasaba vya ukoo. Lakini mabadiliko mara nyingi siyo matukio ya kuyatarajia na mengi ya matukio hayo, kama siyo, mabadiliko yana madhara. Njia bandia ya kuleta mabadiliko kwa inzi wa matunda matekeo yake kuwa na mabawa yaliyodhoofika ,mabawa mafupi, mabawa yaliyopinda, mabawa kigutu — mabawa yote hayo hayafai kwa kuruka. Mabadiliko huleta machafuko,kuharibika kwa umbile na kukosa uwezo ambao wanyama halisi wanao kuwa nao.
Kukosekana dhamira ya dhati kuhusu nadharia ya mageuzi kumesababisha baadhi ya wana mageuzi kupendekeza kwamba mageuzi yalitokea hatua kwa hatua— kwa mfano unyoya ungelitokea ghafla kwenye kizazi cha jamii ya mijusi. Watu wataweza kufanya lolote, lakini wamgeukie na wamheshimu Yeye aliyeviumba vitu vyote!
 

Swahili Title: 
SIKUKUU ZA YAHWE
English files: 
Swahili Word file: