CSSA 2-3-03 - THE MESSIAH IN DAVID'S PSALMS

178. MASIHI KATIKA ZABURI YA DAUDI

“Ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa mimi katika Zaburi”

ZABURI  2, 22. 69, 110
 
Je, ulikuwa unafahamu kwamba kitabu cha Zaburi ndicho kitabu kikubwa kuliko vyote katika Biblia? Kimeundwa kwa jumla ya Zaburi 150 za aina mbalimbali. Zaburi moja ni wimbo au sala, ambapo Zaburi nyingi zimewekwa katika muziki. Zaburi nyingi zilitungwa na Daudi. Kumbuka Daudi alipopakwa mafuta jinsi “Roho ya BWANA ikamjilia juu yake” (1 Sam. 16: 13)? Hii ilikuwa na maana kwamba Mungu ndiye angemfundisha katika njia zake hata ikawa kwamba Daudi alipoandika aliweza kutamka, “Roho ya BWANA ilinena ndani ya yangu, Na Neno lake likawa ulimini mwangu” (2 Sam. 23: 2).

Hivi ndivyo alivyomaanisha Paulo aliposema, “kila andiko (na zaburi zikiwa ni sehemu ya maandiko) zimeletwa kwa pumzi ya Mungu” (2 Tim. 3: 16). Siyo tu kwamba Daudi aliziandika Zaburi lakini pia aliziandika kwa njia maalumu. Alikuwa na taaluma (ujuzi) katika kucheza na kuandika muziki (1 Sam 16 : 16 -23 ), Daudi alitumia uwezo huo kuandika Zaburi hizi katika aina ya njia inayoziwezesha kuimbwa ili nao Waisraeli waweze kuimba, na hivyo kumsifu BWANA na kujifunza juu ya njia za BWANA.
 
BAADHI YA ZABURI ZILIANDIKWA KUTOKANA NA MATUKIO MAALUMU
Kadiri tunavyosoma Zaburi tunaona kwamba baadhi ya Zaburi zina maelezo mwanzo mwa Zaburi, yanayoitwa maelezo ya ziada. Ni maelezo maalumu ili utambue sababu ambayo imesababishwa kwa nini Zaburi fulani ziliandikwa. Kwa mfano, angalia Zaburi 34, na mwanzoni mwake tunasoma, “Zaburi ya Daudi alipobadilisha mwelekeo mbele ya Abimeleki, aliyemfukuza naye akaondoka.” Tunaweza kusonma 1 Sam.21:10-15 na kupata tukio hili, na hivyo twaweza kuona akili ya Daudi wakati ule Zaburi hii ilipoandikwa. Unaweza kuangalia Zaburi nyingine, kwa mfano. Zaburi 52, na wewe ulinganishe na 1 Samweli 22:9. Angalia kama unaweza kupata Zaburi zingine zaidi na uwe unalinganisha na maandiko yaliyo katika vitabu vingine.
 
ZABURI NA MASIHI:
Katika Agano Jipya tunapata nukuu nyingi kutoka kwenye Zaburi kuhusu kazi ambazo Bwana Yesu Kristo alizitenda, na kwa kweli Yesu mwenyewe alisema kwamba maneno yote alikuwa ameshaandikwa “katika Zaburi kunihusu mimi” (Luka 24:44-46) “ni lazima yote yatimie”. Tunaweza kuelewa ya kwamba iwapo Mungu alimvuvia Daudi kuziandika Zaburi basi katika Zaburi hizo aliweza kutabiri mambo mengi kumhusu Masihi. Hebu sasa na tuangalie kwa ufupi Zaburi hizi chache.

MAISHA NA KIFO CHA MASIHI. Zaburi 69,22.

Zaburi 69:4 -“Wanaonichukia bure ni wengi, kuliko nywele za kichwa changu.”
Maneno haya yalinukuliwa na Kristo wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi wake (Yoh.15:25). Alikuwa akiwaeleza kwamba, walimchukia kwa sababu alikuwa amedhihirisha dhambi za adui zake; lakini hawakuwa na haki ya kumchukia. Tunaweza kuona watu wakituchukia kwa sababu tunasema na kutenda yaliyo sahihi machoni pa Mungu.
Zaburi 69:9 - “Maana wivu wa nyumba yako umenila.”
Maneno haya yalikumbukwa na wanafunzi wakati Kristo alipowafukuza kutoka Hekaluni wale waliokuwa wakibadilisha fedha na kuuza njiwa, kondoo na ng’ombe – dume (Yohana 2: 14 -17).

Zaburi 69: 21 - “Wakanipa uchungu kuwa chakula changu; Nami nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki”.
Daudi aliweza kuyaona haya mapito hata ndiyo yaliyosababisha yeye kuandika hivi na yanakwenda sambasmba na mateso yale ambayo Wayahudi waliyomtendea Yesu alipokuwa msalabani (Mathayo 27: 34).

Zaburi 22 - Inatupeleka kwenye mateso na kusulubiwa kwa Masihi.

Zaburi 22:1- “Mungu wangu,Mungu wangu,Mbona umeniacha?”
Maneno haya yalimesemwa na Yesu alipokuwa msalabani (Mathayo 27:46).

Zaburi 22:8 - Husema,Umtegemee BWANA;na amponye; na amwokoe sasa,maana alipendezwa naye”.
Maneno haya yalitamkwa na kundi la wauaji waliokuwa karibu na msalaba (Mathayo 27:43)

Zaburi 22:16 - “Wamenizuia mikono na miguu.”
Maneno haya yanaelezea kikamilifu jinsi Yesu alivyosulubiwa (Luka 24:40; Yohana 20:27).

Zaburi 22:18 -Wanagawana nguo zangu, Na vazi langu wanalipigia kura.”
Maneno haya yalitimizwa kabisa na askari wa Rumi wakati wa kusulubiwa kwake Kristo (Mathayo 27:35; linganisha Yohana 19:23-24).

KUFUFUKA KWA MASIHI: Zaburi 16.
Ahadi zilizotolewa kwa Daudi zinahitaji kwamba mwanaye awe mtu aliyefufuliwa. Daudi aliambiwa kabisa ya kwamba “mzao wa kutoka mwilini (viunoni) mwake mwenyewe” Mungu angemfufua huyo mmoja ambaye ndiye wa kuketi katika kiti chake cha enzi cha Daudi: Aliambiwa pia kwamba ufalme wake “ungeimarishwa milele”. Swali ambalo lilijitokeza akilini mwa Daudi – Ni kwa jinsi gani mmojawapo kati ya wazao wake wa mwili aweze kuishi milele? Daudi alitatua tatizo na kuelewa kwamba mzao wake ingempasa afufuliwe kutoka kwa wafu. Mtume petro anatueleza kuhusu jambo hili katika Matendo ya Mitume 2:25-31. Baada ya kunukuu Zaburi 16, iliyoandikwa na Daudi, ndipo aliendelea kufafanua – maana yake.Maneno ya maana yalipatikana katika Zaburi hii ambayo yasingemhusu mtu yeyote aliyeishi zamani. “Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu” Ingawaje yaliandikwa na Daudi, hayangeweza kumhusu yeye kwa maana ya kwamba Daudi “aliona uhalibifu.” (mstari 29).
 
Petro anasema kwamba Daudi alikuwa anatabiri wakati alipokuwa anaandika Zaburi ya 16, kwani alifahamu mambo yaliyotakiwa ili kuikamilisha ahadi – kwamba mwanawe wa mwili ata weza kuishi milele (mstari 30). Akiona kwamba kaburi la Kristo lilikuwa wazi nao walikuwa wamemwona na kumsikia Bwana aliyefufuka, matukio haya ya karibuni na unabii yalikubaliana na (mstari 32). Mungu alikuwa amemfufua mwanaye kutoka kwa wafu kulingana na maandiko yalivyonena.

Hakuna shaka kwamba Zaburi hii ilikuwa ni mwaongoza uliothibitisha katika mahubiri ya Mitume, ya kuwa ilimpasa Masihi awe mtu aliyefufuliwa. Na ndipo Bwana alikuwa “amewafungulia ufahamu wao.” Baadaye Mtume Paulo anaitumia Zaburi hii vile vile kwa njia hiyo hiyo ya uthibitisho wa kufufuka kwake Kristo (Matendo ya Mitume 13: 34-36).

MASIHI ANAPAA MBINGUNI NA KUJA MARA YA PILI. Zab 110
Iwapo Bwana alikuwa amefufuka alikuwa wapi? Hili ni swali ambalo liliwakabili Mitume katika mahubili yao. Lilijibiwa kikamilifu kwa kunukuu Zaburi 110: 1 “BWANA, alimwambia Bwana wangu, uketi mkono wangu wa kuume, hata niwafanyapo adui zako kuwa chini ya miguu yako”. Kupaa kwa Bwana kwenda mbinguni kulitabiliwa hapa (Linganisha na Matendo Mitume 2: 33- 35).

Zaburi 110 haiishia tu wakati wa kupaa kwake. Inautaja hata wakati wake wa kukaa huko mbinguni. Atakuwa huko “HATA adui zake watakapofanywa kuwa chini ya miguu yake”. Zaburi hii inaelezea juu ya Masihi kuingilia kati katika vita vya Har-magedoni na inaelezea pia kuhusu ushindi wake katika vita hiyo (mstari 2,5-7 ).

WATAWALA WA ULIMWENGU NA UFALME WA MASIHI Zaburi 2
Katika Zaburi hii unaonekana upinzani utakaomkabili Bwana Yesu wakati wa kurudi kwake na kuanzisha Ufalme wake katika Sayuni. Mataifa wataghadhabika na kujikusanya pamoja ili kumwondoa mpakwa mafuta wa BWANA (mstari 1-3). Lakini ghadhabu ya mwanadam ni kitu kidogo sana katika njia ya hukumu zake Mungu naye atawacheka na kuwafanyia dhihaka (mstari 4 – 5). Kwa sababu yeye ni Mwana wa Mungu na analo “jina lililo bora” naye atarithi “miisho ya dunia.” Atatumia nguvu za Mungu kuyapiga mataifa (mstari 8, 9 ).

Inanukuliwa katika ufunuo 2: 27. Hapa Bwana anaahidi nguvu hizo hizo kuwapatia watakatifu. “yeye ashindaye na kuyatunza matendo yangu hadi mwisho, kwake huyo nitampa nguvu juu ya mataifa, naye atawatawala kwa fimbo ya chuma”. Na sisi, pia twaweza kufanyika wana wa Mungu kupitia ubatizo katika jina la Mwana na “tukiwa wana” ndipo tutakuwa warithi wa Mungu pia (Warumi 8: 17).

Zaburi hii inamalizia kwa kuwapatia ushauri mwema watawala wakati Kristo atakaporudi. Wanahitakiwa kujisalimisha (kusalimu amri) au la sivyo wangamizwe (mstari 10 – 12). Kutokana na vifungu vifuatazo tunajua ya kwamba wengine watajisalimisha na wengine hawatajisalimisha (Mika 4: 2, 3; Zaburi 72: 9 – 11).

FUNDISHO KWETU
Tunapoelewa kwamba mambo aliyoyaandika Daudi katika Zaburi hizi ambayo tumejifunza, yaliandikwa miaka 1,000 kabla ya Yesu kuzaliwa, tumeona wazi kwamba Mungu ndiye aliyevuvia uandikaji wa Biblia. Mtu yeyote pasipo msaada wa Mungu asingebashiri mambo yote hayo. Ikiwa unabii katika Zaburi hizi umetimia kwa usahihi kabisa kuhusu kusulubiwa na kufufuliwa kwa Yesu Kristo, ndipo tunaweza kuamini kwa dhati kwamba unabii wa Mungu kuhusu kurudi kwake kuanzisha Ufalme nao utatimia hakika.

Kwa ushahidi wa aina hii tuliouona katika somo hili hatuna shaka lolote kuwa Biblia iliandikwa kwa pumzi ya Mungu, na kwa hiyo ni uwepo wa BWANA mwenyewe. Basi, kwa hiyo, tuithamini Biblia kwa kuwa ni Neno lake nasi tujifunze mafundisho ambayo aliyoandika humo kwa ajili yetu.
 
MASWALI YA VIFUNGU:
1. Zaburini nini na ni kwa nini ziliandikwa?
2. Kwa kutumia Zaburi mbili tofauti eleza jinsi mataifa yatakavyompinga Bwana Yesu Kristo wakati wa kurudi kwake na jinsi atakavyoyafanya mataifa hayo?

MASWALI YA INSHA:
1. Onyesha kutoka kwenye Zaburi jinsi unabii ulivyoelezea kuhusu maisha na kifo cha Masihi.
 
MFANO WA UTAWALA WA SULEMANI:
Jedwali lifuatalo limeorodhesha namna ambavyo Sulemani alivyotawala inavyoashiria utawala ule wa Bwana Yesu Kristo. Kwa ajili ya zoezi weka alama katika Biblia yako.
 

 ZAMANI

SIKU ZIJAZO

Wakati wa amani ulitanguliwa na vita vikuu 1 Wafalme 5:4

Zaburi 110:2; Isaya 9:6-7.

Yerusalemu, kiti cha enzi cha BWANA - 1 Mambo ya Nyakati 29:23;28:5.

Yeremia 3:17.

Mfalme mmoja juu ya Israeli iliyoungana- 1Wafalme 4:20.

Ezekieli 37:22.

Israeli, watu wengi sana na taifa lenye nguvu nyingi – 1 Wafalme 4:20.

Mika 4:7.

Israeli, salama na yenye amani 1 Wafalme 4:25.

Mika 4:4;Sefania 3:19-20

Israeli, mfalme mkuu wa mataifa yote-1 Wafalme 4:21.

Mika 4:8.

Israeli, mfalme mkuu wa nchi tatu Misri na Assyiria

(Wafalme wa kusini na kaskazini-Danieli 11:40)- 2 Mambo ya Nyakati 9:26; 1Wafalme10:29

Isaya 19:25.

Israeli, kitovu cha biashara cha mataifa- 2 Mambo ya Nyakati 1:17

Isaya 23:18.

Utajiri wa mataifa (Wapagani) ukafurika kwa wingi sana Yerusalema 1Wafalme 4:21; 2Mambo ya Nyakati 9:23-24

Isaya 60:11

Wafalme wa mataifa walikubali kutawaliwa na ufakme wa Israeli 1Wafalme 4:21

Zaburi 72:10.

Utajiri mwingi waajabu huko Yerusalemu -2Mambo ya Nyakati 1:15

Isaya 60:17.

Wakati wa rutuba sana katika nchi-1Waf;4:22-28;5:11

Isaya 35:1-2.

Kipindi cha shughuli kuu za ujenzi- 1Wafalme 9:10-20

Isaya 65:21-22.

Watu wa mataifawalisaidia katika kuijenga Israeli- 2Mambo ya Nyakati 2:2,17

Isaya 60:10,13.

Hekalu tukufu lilijengwa huko Yerusalemu –Wafalme 6

Isaya 56: 7-8.

Hekalu lilijengwa kutokana na mpango ambao Mungu aliutoa

1Mambo ya Nyakati 28: 11-19

Ezekieli .Sura 40 -48.

Hekalu lilijengwa na mfalme wa amani – 1Wafalme 6

Zekaria 6: 12.

Sulemani alijulikana kuwa ni mfalme wa amani – 1Wafalme 5: 12

Isaya 9:6

Mfalme akatambuliwa kwa ajili ya hekima, akili-1Wafalme 4: 29-34

Isaya 32: 4,33: 6

Mfalme alijulikana kwa hukumu inayoponya ,isiyokosea -

1Wafalme. 4: 29- 34

Isaya 11: 1-3.

Yerusalemu makao makuu ya hija ya ulimwengu mzima kuisikia hekima ya mfalme wake – 2 Mambo ya Nyakati 9: 23, 1 Wafalme 4: 34

Isaya 2:2-4;

Zakaria 14:16

Tiro ( Tarshishi ) rafiki mkuu wa Israeli – 1Wafalme 5: 1

Zaburi 45: 12, Isaya 60: 9 .

Sadoki, Kuhani mkuu 1Wafalme 1: 24,2: 26

Waebrania 7: 11-12, Ezekieli 40: 46.

Makuhani walihudumu Hekaluni mchana na usiku ( Zaburi134)hivyo kuwa mfano kwa wale watakaokuwa na uzima wa milele ( Isaya 40: 28-31)

Waebrania 7: 15-16,Ufunuo 4: 8, Ufunuo 5: 9-10.

 

Utaratibu kamili wa Ibada ya Mungu ulianzishwa kwa

mara ya kwanza-1Wafalme 9: 25,2Mambo ya Nyakati 8: 12 -16

Kumbukumbu la torati 30: 6-8, Isaya 42: 21.

Shetani anafungwa 1Wafalme 5: 4

Ufunuo 20: 2

Shetani anafunguliwa utawala unapokwisha

1Wafalme 11: 14

Ufunuo 20: 7

 

Swahili Title: 
MASIHI KATIKA ZABURI YA DAUDI
English files: 
Swahili Word file: