CSSA 2-3-04 - SOLOMON SUCCEEDS DAVID

179. SULEMANI ANAMRITHI DAUDI

“Ndipo Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha BWANA, awe mfalme badala ya Daudi babaye, akafanikiwa;nao Israeli wote wakamtii”

Daudi sasa alikuwa mzee na“mkongwe katika siku zake” (mstari 1) na ilionekana wazi kwamba siku ya kufa kwake ilikuwa imekaribia. Tokea dhambi aliyoitenda na Bath-sheba, nyumba ya Daudi ilikuwa imepata matatizo mengi –Absalomu, mwanaye alijaribu kuupindua ufalme wake, lakini alikuwa ameuawa, na sasa Daudi akiwa mzee sana na dhaifu wa kushinda kitandani, akiwa karibu ya kufa, mwanaye mwingine, Adonia akachukua hatua ya kumwasi baba yake .

1 Wafalme 1; 2:1-12; 1 Mambo ya Nyakati 28, 29.

UASI WA ADONIA – 1 Wafalme 1: 1-31
 Adonia aritayarisha magari ya vita na wapanda farasi, naye akakusanya watu wengi upande wake, kama vile Yoabu mkuu wa Jeshi la Daudi na Abiathari kuhani kumsaidia kuchukua kiti cha Enzi, Adonia akaandaa sherehe na watu wakapiga kelele “Mungu, na aishi mfalme Adoniya” (mstari 25).

Habari ya kwamba Adonia alikuwa katika maandalizi ya kuchukua kiti cha Enzi ilienea haraka. Nabii Nathani alitambua kuwa ni lazima jambo fulani lifanyike kumzuia Adonia kwani Mungu alikuwa ameahidi kumpaatia Sulemani kiti cha Enzi (1 Mambo ya Nyakati 22: 9) Akaenda kwa Bath-sheba, mamaye Sulemani na kumweleza kuhusu uasi wa Adonia. Nathani akatayarisha mbinu kumfanya Daudi amtie mafuta Sulemani kuwa mfalme. Ndipo Bath-sheba akaenda kwa Daudi, ambaye alikuwa hatoki kitandani, na kumweleza yaliyokuwa yakitokea Akasema,“Bwana wangu, uliniapia mimi mjakazi wako kwa BWANA, Mungu wako, ya kwamba, bila shaka Sulemani mwanao atamiliki baada yangu, yeye ndiye atakayeketi katika kiti changu cha enzi, na sasa, angalia, Adonia anamiliki” (mstari 17,18).

Bath-sheba alifahamu kwamba uhai wake na uhai wa Sulemani utakuwa hatarini iwapo Adonia ndiye angekuwa mfalme. Na Bath-sheba alipokuwa akiongea wakati huo huo Nathani, nabii akaingia naye akayathibitisha maneno ya Bath-sheba, na Nathani akamsihi amtie mafuta haraka. Daudi akamwambia Bath-sheba kwamba Sulemani inampasa kuwa mfalme.

SULEMANI ANATIWA MAFUTA KUWA MFALME – 1 Wafalme 1:32-40

Daudi akamwita Nabii Nathani, kuhani Sadokia na Benaya mmoja wa watu mashujaa wa Daudi na kuwaeleza la kufanya”: “Twaeni pamoja na watumishi wa bwana wenu, mkampandishe Sulemani mwanangu juu ya nyumbu wangu mimi, mkamtelemshe mpaka Gihoni; kisha Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, na wamtie maafuta huko, awe mfalme, kapigeni panda, mkaseme, Mfalme Selemani na aishi Kisha pandeni juu ya nyuma yake, naye atakuja kuwa ili aketi katika kiti cha enzi; kwa maana atakuwa mfalme badala yangu; ndiye niliyemweka awamiliki Israeli na Yuda” (mstari 33- 35). Mapendekezo ya Daudi yalitekelezwa ipasavyo kukawa na furaha kubwa mno huko Yerusalemu. Watu wengi sana wakampokea Sulemani kwa furaha kwani watu wote walikuja na “wakafurahi furaha kubwa mno, hata nchi ikapasuka kwa sauti zao” (mstari 40).
 
SHEREHE YA ADONIA ILIGEUKA KUWA HOFU – 1 Wafalme 1:41-53
Vigelegele vya shangwe vilivuma katika Bonde la Kidroni na kufika masikioni mwa wageni waalikwa wa Adonia. Kisha habari ikafika kutoka Yerusalemu “kwa hakika bwana wetu mfalme Daudi amemfanya Sulemani kuwa mfalme….” (mstari 43-48). Adonia na wageni wake wakashikwa na hofu. Kuwapo kwao pale kulionekana kuwa ujanja na uasi kwa Daudi na kwa BWANA. Hawakupoteza muda wa kamwacha Adonia na “kwenda kila mtu njia yake.” Adonia alitetemeka na kuelewa kuwa uhai wake ulikuwa hatarini. Akaenda katika hema na kuzishika nguzo za madhabahu katika tumaini la kupata rehema. Akaomba kiapo kutoka kwa Sulemani amhakikishie kuwa hatauawa. Kwa hekima Sulemani akamkubalia kwa masharti ya kuwa uovu usionekane ndani katika siku zijazo.

SULEMANI ANASIMIKWA RASMI KUWA MFALME – 1 Mambo ya Nyakati 28,29   
Hatimaye Israeli wote walikusanyika kumshuhudia Sulemani akisimikwa rasmi kuwa mfalme. Daudi alikuwa mzee na dhaifu, lakini kwenye tukio hili “Alisimama kwa miguu yake” (1 Mambo ya Nyakati 28:2) kuwahutubia watu. Akawaambia watu ya kwamba Mungu alikuwa amemchaguwa Sulemani kati ya wanawe wote kukalia kiti cha enzi. Akamhimiza (akamtia moyo) Sulemani “kumjua Mungu na kumtumikia kwa mkamilifu na kwa moyo wa kupenda” (1 Mambo ya Nyakati 28:9).

Sulemani alikuwa amechaguliwa na Mungu kujenga Hekalu. Daudi alikuwa ametaka kujenga nyumba hii kwa ajili ya Mungu, lakini kwa sababu alikuwa mtu wa vita Mungu alisema kwamba mwanawe Sulemani ndiye atakayejenga. Daudi alikuwa amekusanya akiba kubwa ya fedha na vifaa kwa ajili ya kulijenga Hekalu hilo. Akasema, “sasa nimeandaa kwa uwezo wangu wote kwa ajili ya nyumba ya Mungu, dhahabu, fedha, shaba, chuma, miti, madini ya vito vya thamani na marumaru kwa wingi” (Mambo ya Nyakati 29:2). Daudi alikuwa amempatia sulemani plani (michoro) kwa ujenzi wa Hekalu. Daudi alikuwa amepata michoro hii kutoka kwa Mungu (1 Mambo ya Nyakati 28:11-19).

Daudi akatoa mwito kwa watu kuchangia kwa hiari ujenzi wa Hekalu - nao kwa hiari wakafanya hivyo. “Watu wakafurahi, kwa kuwa walichangia kwa hiari, kwani kwa moyo mkamilifu walijitolea kwa BWANA naye Daudi mfalme akafurahi pia kwa shangwe kuu” (1 Mambo ya Nyakati 29:9).
 
Moyo wa Daudi ukajaa shukurani kwa BWANA nao watu wakatoa dhabihu na kufurahi wakati sulemani akitawazwa “kwa mara ya pili” kuwa mfalme “katika kiti cha enzi cha BWANA baada ya Daudi baba yake.” (Nyakati.29:20-23).

MWITIKIO WA MUNGU KWA OMBI LISILO LA UBINAFSI LA SULEMANI – 1 Wafalme 3:1-15
“Sulemani alimpenda BWANA, akaenda katika amri za Daudi baba yake” (1 Wafalme 3:3). Hivyo, punde baada ya kifo cha Daudi sulemani aliwakusanya viongozi wote wa Israeli Hemani huko Gibea kumwabudu Mungu na kutoa dhabihu (2 Mambo ya Nyakati 1:2-6). Hapa tunaona uaminifu wa Sulemani katika kujaribu kuwaunganisha Israeli katika msingi wa kumtumikia BWANA. Wakati Sulemani alipokuwa Gibea, BWANA akamtokea katika ndoto akamwambia, “Omba utakalo nikupe” (mstari 5). Jinsi swali lilivyo la kushangaza Mungu kumwuliza mwanadamu, Hata BWANA aliufahamu moyo wa Sulemani. Alifahamu kuwa Sulemani alikuwa amewakusanya viongozi ili kuwaunganisha kama taifa linalomtii Mungu. Moyo wake Sulemani ulijaa majukumu makubwa ya kazi ambayo sasa alibebeshwa mabegani mwake, kwani ilimbidi kuwa mwamuzi wa taifa lote. Alitakiwa kutawala kwa haki mbele ya BWANA. Kazi ilikuwa bayana, lakini namana ya kuifanya kwa utukufu wa BWANA ilionekana kuwa mbali ya upeo wake, hivyo wakati BWANA alipomwambia aseme alichokitaka, hakujifikiria mwenyewe bali aliifikiria ile kazi ambayo angeitenda mbele za Mungu. Akasema, “Kwa hiyo nipe mimi mtumishi wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua jema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi” (mstari 9). Shauku ya moyo wa Sulemani ilipodhihirika na ikaonekana kwamba hakujifikiria yeye binafsi, bali jinsi ambavyo angemtumikia BWANA,Mungu alipendezwa naye. Kwa hiyo Mungu akampatia Sulemani “moyo wa hekima na akili” (mstari 12) lakini juu ya hili Mungu akampatia utajiri na heshima na ahadi ya maisha marefu kama angeendelea kutembea katika njia za Mungu (mstari 11-13).

SULEMANI MWAMUZI MWENYE HEKIMA – 1 Wafalme 3: 16 -28
Hekima ambayo Mungu alikuwa amempatia Sulemani ilikuwa ikipimwa wakati wote, kuna tukio ambapo walifika mbele ya Sulemani wanawake wawili wakiwa na mtoto mmoja. Wote hawa wanawake wawili waliishi katika nyumba moja na kila mmoja wao alikuwa amezaa mtoto, lakini mmoja wa watoto alikuwa amefariki kitandani wakati mama yake alipomlalia kwa bahati mbaya. Sasa wote wawili waligombea kila mmoja akisema mtoto aliye hai ni mtoto wake. Mmoja alieleza kuwa yule mwingine aliamka usiku na kuwabadilisha naye yule mwingine akakataa kuwa siyo kweli.Lakini ni yupi alikuwa akisema ukweli? Tatizo hili lilikuwa kubwa sana kutatua – lakini Sulemani kwa hekima aliyopewa na Mungu alijuwa asili ya mwanadamu. Watu waliokuwepo walishituka kumsikia akisema, “Nileteeni upanga – mkate mtoto aliye hai vipande viwili, kampe huyu nusu, na huyu nusu.” Lakini sasa mama halisi alibainika kwani hakuwa mama aliyetayari kuona mtoto wake akiuawa, bali aliona ni afadhari amwache mtoto achukuliwe kuliko kuona akiuawa.

Hivyo akasema “Ee bwana wangu, mpe huyu mtoto aliye hai, wala usimwue kamwe” lakini yule mwanamke mwingine akasema, “na akatwe” (mstari 26). Hivyo Sulemani akaamuru yule mwanamke wa kwanza apewe mtoto mtoto aliye hai, na wakati habari ya hukumu hii ilipoenea katika Israeli watu wote wakamwogopa mfalme kwani waliona kwamba hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake (mstari 28).

FUNDISHO KWETU:
Kama vile Sulemani alivyomwomba Mungu ampatie hekima hivyo hivyo nasi tunapaswa kumwomba Mungu atupatie hekima. Hekima ya kweli ni kufahamu namna ya kuyatendea kazi tunayojifunza kutoka kwenye maneno tunayojifunza kutoka kwa Mungu katika maisha yetu. Sulemani aliandika: “Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; na kumjua Mtakatifu ni ufahamu” (Mithali 9:10). Pia aliandika, “Hata ukatege sikio lako kusikia hekima, na ukauelekeze moyo wako upate ufahamu BWANA” (Mithali 2:2) na “hekima hutoka kwa Mungu” (Mithali 2:6), na ndipo Yakobo akaandika, “Lakini mtu wa kwenu akipugukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa” (Yakobo1: 5). Na tufuate maneno ambayo Daudi alimwmbia Sulemani (1 Mambo ya Nyakati 28: 9). “Kumjua” Mungu – ni kusoma na kujifunza kuhusu Mungu na njia zote za hukumu ya Mungu na rehema: “Kumtumikia”. Mungu ni kutii yale yote yanayompendeza Mungu, na kufanya mapenzi yake wakati wote, “kwa moyo mkamilifu na kwa moyo wa kupenda”. Na tufanye mambo yanayompendeza Mungu kwa mwenendo safi, na kwa hiari, pasipo huzuni wala kwa kutokuridhika. Na tuwe na juhudi ya kufanya mambo ya Mungu huku tukimwomba Mungu hekima ili tuweze kutenda yote kwa ajili ya kumsifu na kumtukuza Mungu.

REJEA KATIKA MAKTABA:
 “Historia ya Biblia” ( H .P. Manofrield ) – Kitabu cha 4, No. 7 .
 “Mtu yule Daudi” ( N . Tennant ) – ukurasa 207 – 215 .

MASWALI YA FUNGU
1. Fafanua kutiwa mafuta kwa Sulemani kuwa Mfalme
2. Sulemani aliomba nini wakati Mungu alipomwambia “Omba utakalo nikupe?”
3. Kwa kutumia tukio la wale wanawake wawili na mtoto mchanga, onyesha nguvu ya hekima za Mungu aliyopewa Sulemani

MASWALI YA INSHA
1. Adonia yeye mwenyewe alijifanya mfalme, lakini Mungu alikuwa amemwahidi Sulemani kiti cha enzi kwa – eleza matukio na jinsi Daudi alivyofanya kumweka Sulemani katika kiti cha enzi.
2. Kwa kumtumia Sulemani kama mfano, eleza jinsi tunavyoweza kupata hekima ya kweli ili kwamba tuweze “kumjua” na “kumtumikia” Mungu

HEKALU LA SULEMANI
Katika mwaka wa nne wa utawala wake, Suleamani alijenga “nyumba ya BWANA”. Kama lilivyokuwa Hema la kukutania kabla yake, muundo wake, vifaa vya samani na utumishi wa makuhani yalikuwa mfano wa kazi ya ukombozi ya Kristo ambayo ilikuwa haijafunuliwa bado – “kivuli cha mambo ya mbinguni” (Kutoka 25: 40, Waebrania 8: 5 ; 9:9, 23, 24). Lilikuwa jengo la kupendeza kuzidi kiasi na likafanyika roho na kiini cha mapenzi ya taifa (1 Mambo ya Nyakati 22: 5, 1 Wafalme 10: 5, Isaya 64: 11). Maelezo ya kina ya muundo wake na uzinduzi wa kuliweka wakfu yameandikwa mara mbili (1 Wafalme 5 hadi 8, 2 Mambo ya Nyakati 2-7). Utawala wa Sulemani uliashiria utawala wa Masihi nalo Hekalu lilikuwa mfano wa “nyumba ya sala kwa mataifa yote” ambayo itakayojengwa na mzao mkuu wa Daudi na mrithi (Isaya 56: 7; 2 Samweli 7: 13; Zekaria 6: 12, 13 ).

ENEO: Mlima Moria, ambapo zammapema zaidi Ibrahimu “alimtoa” Isaka, naye Daudi alitoa sadaka ili kwamba tauni iweze kuzuiliwa (linganisha 2 Mambo ya Nyakati 3: 1; 1 Mambo ya Nyakati 21: 22-30, 22: 1. Mwanzo 22: 2, 14, Kumbukumbu la Torati 12: 11).

MUDA WA UJENZI: Miaka 7½. ulianzishwa katika mwezi wa pili wa mwaka wa nne (4) na kumalizika katika mwezi wa 8 wa mwaka wake wa 11 (1 Wafalme 6: 1, 37,38; 2 Mambo ya Nyakati 3: 2).

NGUVU KAZI: Mafundi mbao, maseremala, wabeba mizigo na wachonga mawe walichukuliwa kutoka Israeli na Tiro, ambapo viongozi wakuu walikuwa watumishi wa Sulemani (1 Wafalme 5: 6, 13 -18; 2 Mambo ya Nyakati 2: 17, linganisha na Isaya 60: 10 -13).
 
MPANGO KAMILI: Ulilingana na Hema ya Kukutania, lakini vipimo vyote viliongezwa mara mbili na mapambo ya uzuri ajabu. Vipimo kwa ndani: urefu ulikuwa ni mikono 60, upana mikono 20, kwenda juu mikono 30. Ilikuwa imegawanywa katika sehemu 3, zilizoitwa, patakatifu patakatifu (au patakatifu sana) mahali patakatifu, na Behewa.
 
Kuta zilikuwa zimejengwa kwa mawe yaliyochimbuliwa na kuchongwa chimboni kabla ya ujenzi, na akazifunika kuta kwa mbao za mshita, zilizonakshiwa kwa mapambo ya makerubi, na mitende na maua yaliyofunika wazi, na akaifunuka kwa dhhabu (1 Wafalme 6:7,15,18,21,29).
 Sakafu zake zilikuwa za maboriti na mbao za mwerezi ziilizofunikwa ndani kwa dhahabu (1 Wafalme 6: 15, 30).
Dari ilikuwa ya boriti na mbao za mti wa mwerezi na akazifunika kwa dhahabu (1 Wafalme 6:9, 22).
Milango ya Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa ya miti ya mizeituni iliyopambwa kwa naksi (mapambo) ya makerubi, mitende, maua yaliyofunuka wazi na akaifunika mitende kwa dhahabu na makerubi nayo yalifunikwa kwa dhahabu (1 Wafalme 6:31- 32).
 Milango ya Mahali Patakatifu ilikuwa 2 na kila mmoja ulikuwa na mikunjo ilikuwa ya (miti ya) mberoshi na kunakishiwa vile vile kwa makerubi na kufunikwa kwa dhahabu (1 Wafalme 6 : 33- 35).

VIFAA – NA MAANA YAKE KATIKA ROHO
1) JIWE. Mawe hayo yalichukuliwa kutoka ardhini na kuchongwa katika umbo kufuatana na maelekezo ya Mungu. Kwa njia inayofanana na hiyo Watakatifu yaani “mawe yaliyo hai” ya nyumba ya kiroho ya Mungu, wanaoitwa kutoka katika (wanachukuliwa) kutoka kati ya watu wa mataifa (wapagani) na waliotayarishwa kuwa mahali pa kukaa Mungu (1 Wafalme 6: 7; 1 Petro 2: 5; Yohana 14: 23).
2) MBAO.
a) Mwerezi – mti imara (unaodumu sana = Usioharibika (Zaburi 92: 12; 1 Wakorintho 15: 53)
b) Mberoshi – mti mgumu sana = Nguvu za Mungu (Waefeso 6: 10; Habakuki 3: 19)
c) Mzeituni - ulizaa mafuta ambayo yalitia nuru katika Mahali patakatifu = ufahamu wa Neno la Roho (Kutoka 27:20; Zab.119: 130; Nehemia 9: 20, 30; Zekaria 4: 14; Matendo ya Mitume 10: 38; Ufunuo 1:20).
3) MADINI. Dhahabu ndiyo madini pekee yaliyotumika ndani katika mahali Patakatifu na ndiyo yaliyotumika ndani ya Patakatifu pa Patakatifu (angalia maelezo kuhusu maana halisi ya vifaa vilivyotumika katika Patakatifu pa Patakatifu) ambapo shaba ilitumika kwa ajili ya Baraza (angalia maelezo kuhusu maana ya Madhabahu ya Shaba).

BEHEWA LA NJE
Mahali ambapo ibada inayokubalika ilipoanzia =UTAKASO NA USAFI WA AKILI Vidokezo maalumu
MADHABAHU YA SHABA (2 Mambo ya Nyakati 4: 1) Palikuwa “Patakatifu pa patakatifu (Kutoka 29: 37) = Kristo (Waebrania 13: 10). “Ilimfanya mtakatifu” kila mtu aliyeigusa (Waebrania 2: 10). Hiki kilikuwa ndicho kifaa cha kwanza ambacho kilionyesha kikwazo cha kuingia moja kwa moja katika Patakatifu pa Patakatifu na inasema kuhusu umhimu wa uhitaji wa kutangulia kwanza kwa dhabihu pale kwenye madhabahu ya Kristo (Warumi 12: 1, 2). Shaba = Dhambi za mwili (Hesabu 16: 38-39,31: 22- 23,21: 8; Kutoka 38: 8; Waebrania 2: 14; Warumi 8: 3).


BAHARI YA KUSUBU (2 Mambo ya Nyakati 4: 2-5; 1 Wafalme 7: 23-26) Ilikuwa ni sawasawa na Chetezo cha uvumba. Mikono na miguu (=matendo na mwenendo) ilipaswa kusafishwa kwa maji  (= Neno la Mungu. Waefeso 5 : 26; Matendo ya Mitume 26: 16). Iliwezekana kuikaribia madhabahu ya shaba (Zaburi 26: 6; Kutoka 30: 18-21). Ilisimamishwa juu ya ng’ombe maksai (madume) 12 = makabila 26 ya Israeli, na maksai = huduma au utumishi. Kabla hatujatoa ibada inayokubalika inatupasa kuoshwa na kulifahamu Neno la Mungu (Yohana 15: 3; 17: 7).
 
BIRIKA KUMI ZA SHABA na vinara vyake (1 Wafalme 7: 27 -39). Yalikuwa 5 katika kila (Nyumba) Behewa, nayo yalitumika kuoshea dhabihu za kuteketezwa (2 Mambo ya Nyakati 4: 6; Mambo ya Walawi 1: 9)

NGUZO MBILI za Shaba zlikuwa mbele ya mahali patakatifu (1Wafalme 7 : 15-22) ziliitwa Yakini (maana yake Mungu Atathibitisha) na Boazi (maana yake imo Nguvu). Zinawakilisha “mwili” uliosafishwa, kuimarishwa na kuwezshwa kusimama kwa ajili ya ukombozi wa Mungu (Ufunuo 3: 12; Danieli 10: 18 -19, 12: 13).

DARAJA LA KUPANDIA (Wafalme 10: 5). Kiebrania “Ola” neno kwa kawaida limetafsiriwa “dhabihu za kuteketezwa” (Linganisha na Ezekieli 40: 26) maana yake kujiweka wakfu kwa kazi ya kumtukuza BWANA na hivyo kufanyika kuwa harufu ya manukato katika pua za Mungu (Efeso 5: 2).

MAHALI PATAKATIFU Palikuwa ni katikati, hatua ya pili, na panawakilisha KUOSHWA DHAMIRI kulitakiwa sana kwa ajili ya mtu anayekwenda kuingia kwenye Ufalme wa Mungu (1 Yohana 3: 3). Ni mfano wa taifa la Israeli kiroho katika hali ya uhusiano wa agano na Mungu Ile madhabahu ya shaba na Bahari ya kusubu ( birika ) vilikuwa nyuma na uwepo wa Mungu ulikuwa ndiyo uko mbele .

Vidokezo maalumu

1. VINARA VYA TAA KUMI vya dhahabu, 5 kila upande wa mahali patakatifu (2 Mambo ya Nyakati 4: 7; 1 Wafalme 7: 49) maana yake Yesu na Eklesia (kusanyiko) ambapo nuru ya ufahamu wa kuijua Kweli inang'aa katika dunia ya giza (2 Wakorintho. 4: 6; Yohana 1: 9; Wafilipi 2:15; Ufunuo 1:20; Mathayo 5:14-16; Kumbukumbu la Torati. 4:6; Zaburi 119:105; Mithali 6:23).

MAFUTA - Yaliletwa na wana wa Israeli wote, na kwa hiyo Vinara vya Taa viliwakilisha taifa (Kutoka. 27:20,21).

MATAWI SABA – 7 ilikuwa ndiyo namba (au hesabu) ya Agano la Musa na (kwa) hiyo yaliwakumbusha juu ya uhusiano wao na Mungu (Kumbukumbu la Torati 5:15; Kutoka 31:16-17; Mambo ya Walawi 26:15,18,21,24,34,35). Na pia iliwkilisha ukamilifu wa ujuzi na hekima kutoka kwa Mungu (Ufunuo 4:5; 5:6; Zekaria 4: 2, 3:9).

KUMI - Ukamilifu, mwisho (Luka 19: 13; Mwanzo 31:7; Hesabu 14: 22; Daniel 1: 20; Zekaria 8: 23; Mambo ya Walawi 26: 26; Ayubu 19: 3; 1 Samweli 1: 8). Kwa hiyo “kumi” inahusiana na mng'ao unaotoka kwa vile vinara vya taa, vinamwakilisha Kristo, ambaye hekima iliyo ndani yake ni mwisho na yenye utimilifu wote (Wakolosai 2:8-10; 1 Wakorintho 1:18-24, 30). Ni ya upeo wa mwisho na kamili

2. MEZA KUMI ZA MIKATE YA WONYESHO (2 Mambo ya Nyakati 4: 8, 19; 1 Wafalme 7: 48 ), na mikate 12 juu ya kila moja (Wafalme 24: 5-9). 12 = makabila 12 ya wana wa Israeli, mikate = matoleo ya chakula, matunda ya kazi zao, na Haruni na makuhani walimwakilisha Mungu. Wakati makuhani walipokula “chakula cha mkate Mungu” (Mambo ya Walawi 21: 6). Katika ulimwengu wa roho ilimaanisha kuwa ni Mungu alikubali kupokea matunda ya kazi zao. Ubani ulifukizwa juu ya mkate, ukatoa harufu nzuri sana ya kupendeza, ikimaanisha ikionyesha Mungu kupenda (Wal. 24: 7). Mikate ilibadilishwa “kila sabato” – siku ambayo ilikuwa ni “ishara ya agano”, “wakikumbuka ukombozi wao kutoka utumwani (Kumbukumbu la Torati. 5: 15; Kutoka 31: 16, 17).

3.  MADHABAHU YA KUFUKIZA UVUMBA madhabahu hii ilitengenezwa kutokana na mbao za mti wa mshita zilizofunikwa kwa dhahabu (1 Wafalme 6: 22). Kupaa kwa uvumba = maombi ya watakatifu katika madhabu ya Kristo (Zaburi 141: 2; Luka 1:7- 10; Ufunuo 5:8 angalia pia 8: 3, 4). Ilikuwa ndani ya patakatifu sana au mahali Patakatifu pa Patakatifu (1 Wafalme 6: 22). Kwa hiyo “sala” inaingia ndani mbinguni (Waebrania 6: 19, 9: 24). Ni moto utokao kwenye madhabahu ya shaba tu ulioweza kutumika, fundisho ni kwamba maombi yanakubaliwa tu kwa msingi wa upatanisho wa katika dhabihu ya dhambi kupitia kwake Kristo. Hakuna “uvumba mgeni” uliokubaliwa kufukizwa isipokuwa ule tu uliokuwa umeagizwa na Mungu kuwa ndiyo utumike (Kutoka. 30:9, 34, Mambo ya Walawi 16: 12; Matendo ya Mitume 4: 12; Yohana.15: 4-5).

4. 4 PAZIA (2 Mambo ya Nyakati 3:14). Kiebrania “paroketh” = “tenganisha”. Ilikuwa ni kizuizi kilichosababisha wana wa Israeli watengane na Mungu. Kwa namna hiyo ilikuwa ni alama nzuri ya udhaifu wa sheria za Musa ambazo zilisingeweza kuvuka mpaka kwa sababu ya mwili na kuutia uzima (Wagalatia 3: 21; Warumi 8: 3). Ndiyo kusema kwamba, iliuwakilisha “mwili” na Sheria ambayo iliwatenganisha watu na Mungu (Waebrania 10: 20). Ilitengenezwa kwa nguo ya kitani safi nyeupe = (matedo ya haki ya watakatifu, Ufunuo 19: 7-8) ambayo ilipamba kwa rangi ya Samawi (Bluu) (=Sheria ya Mungu, Hes.15: 38), Zambarau (= ukombozi, Yohana. 19: 2) na Nyekundu ( = mwanadamu na dhambi, Isaya. 1: 18; Mathayo 27:28; Mambo ya Walawi 14: 4,6). Misingi wa ukombozi kwanza ilisukwa katika mwili wa Kristo na kwa utiifu mkamilifu lile pazia lilipasuka, ikiifungua njia ya kuingia Patakatifu pa Patakatifu (Waebrania 2:10-14, 5:5-8, 10: 20; Mathayo 27:51).

“Nyumba ambayo BWANA atajengewa ni lazima itakuwa nzuri mno, yenye sifa na yenye utukufu katika nchi zote” – 1 Mambo ya Nyakati 22: 5.

PATAKATIFUPA PATAKATIFU
Hatua ya kumalizia, lengo la maisha ya kiroho ya wana wa Israeli, na kwa jinsi ilivyo wakilisha —
1) Uwepo wa Mungu au “mbingu yenyewe” (Kutoka 25:21- 22; Waebrania 6:18-20;9:24).
2) KUOSHA MWILI, kutokuharibika, uzima wa milele katika ufalme (Waebrania 10:34; Wakolosai 3:3-4; 1 Wakorintho 15:50-54).

Vidokezo Maalumu
(1) UMBO - Mviringo kamili (1 Wafalme 6:20) = Eklesia (Kusanyiko) kamilifu, ambalo ni moja pamoja na Mungu (Ufunuo.21:16,3).

(2) DHAHABU- ilifunika kila kitu. Ni yenye thamani na haiharibiki na kwa ajili hiyo inasimama badala ya “urithi usioharibika, wala usio na uchafu”- uzima wa (1 Petro 1: 4 -7; Ufunuo 21:18; Zaburi 45:9, 13), na pia inawakilisha imani iliyothibitishwa ambayo kwa hiyo uzima wa milele unapatikana (Ufunuo 3:18; Ayubu 23:10).
(3) MAKERUBI (1 Wafalme 6:23-28) = Eklesia kamilifu, kusanyiko kuu la mwili wa Kristo, sasa likiwa limekwisha pata lengo (Ezekieli 1, 43:1-3; Ufunuo 4:7; 5:9-14). Ndani ya Hema ya kukutania mabawa ya Makerubi yalikitia uvuli kiti cha rehema, lakini hapa pia mabawa yao yamekunjuliwa, yakiwa yanamaanisha heshima yamataifa yote dunia kwa dola ya ufalme wa Sulemani (1 Wafalme 4:21, 24,34).
(4) SANDUKU LA AGANO - ndani yake mlikuwemo mbao za agano (2 Mambo ya Nyakati 5:10) = Mahali pa takatifu alipokaa Mungu (Hesabu 7:89; Zaburi 80:1) 2 Wakorintho 5:21; Yohana.1:14, “alikaa” = “Hemani”).
(5) KITI CHA REHEMA JUU = Kristo, ambapo Mungu atakutana nasi (Kut. 25:22; Waru. 3:25 “ondoleo la dhambi” (au ghofira) = “Kiti cha enzi”) Mungu ni mwadilifu naye atakutana nasi kwa msingi wa Mapenzi yake tu kwani kuishi kitakatifu kama ilivyoainishwa katika zile Amri 10 zilizoandikwa katika mbao za mawe na zikawekwa chini ya kiti cha rehema.
(6) MITI MIWILI - Iliachwa ndani ya vikuku vya Sanduku na ncha za miti zilionekana ndani ya Mahali Patakatifu (1 Wafalme 8:8). Kwa kuwa lilikuwa tayari kwa usafiri na fundisho lilikaziwa ya kwamba Hekalu la Sulemani halikuwa sehemu yake ya pumziko la Mungu la kweli na la mwisho, bali, bali yeye hupumuzika katika mioyo ya watu walio maskini waliotubu wanaotetemeke kwa ajli ya Neno la BWANA (Matendo 7:47-49; Isaya 66:1-2; 2 Wakorintho 6:16). Kiti cha rehema kilinyunyiziwa damu mara moja kwa mwaka kwa damu ya utakaso ili kupata msamaha wadhambi (Walawi 16:14-15). Kwa hiyo isingewezekana kuwa na uhusiano na Mungu isipokuwa kwa msingi wa “kumwaga damu”. Mara tu ondoleo la dhambi lilipokwisha kukamilika, ndipo “uhusiano” na Mungu ulipopatikana, na tendo hili lilikuwa likimaanisha njia ya kuingia ndani ya Patakatifu pa Patakatifu.

FUNDISHO LA JUMLA
Linaelezwa katika Kutoka 25:8 “Nao wanifanyie makao ili niweze kukaa kati yao” Hekalu lilithibitisha jinsi mwanadamu anavyoweza kupatanishwa na Mungu. Kwenye behewa la nje, mwanadamu alikuja, na ndani ya Patakatifu pa Patakatifu, Mungu alikaa. Hatua zilifunua katikati namna mwanadamu, anavyotakiwa kuyafuata matakwa ya Mungu, na angeweza kupata ukombozi na hatimaye uzima wa milele. Na kwa hiyo Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa kielelezo kwa wana wa Israeli kuendelea mbele na kuwa kama ndilo lengo. Hapa palikuwa na kiini mahali Paatakatifu, uwepo wa BWANA mwenyewe, lile sharti la ukamilifu na ushirika wa kudumu wa Mungu aliyemkomboa Israeli hasa hasa kwa ajili kufunua utukufu wa Mungu ndani yao na kupitia kwao.

NYUMBA YA KWELI:
Wakati Hekalu la Sulemani lilikuwa la kutisha naye Mungu alionyesha utukufu wake ndani yake, halingeweza kumtosha. Hata wa mjenzi alitambua hili (1 Wafalme 8: 11, 27). Hakuna nyumba yenye kujengwa kwa mkono wa mwanadamu ambayo ingeweza kumtosha mahitaji yake, lakini Mungu mwenyewe ametamka kwamba yeye atakaa na “mtu mwenye roho iliyotubu na kunyenyekea” (Isa 57: 15, 66: 1-2). Kwa imani anaingia ndani ya mioyo ya wenye hali ya aina hii na kwa utiifu wao huonyesha kwamba Mungu yumo ndani yao (Waefeso 3: 16-19; 2: 21-22). “Mtu akinipenda, atalishika neno yangu; naye Baba atampenda nasi tutakuja kwa;na kufanya makao kwake” (Yohana 14: 23). Uovu ulisababisha utukufu wa Mungu kuondoka kutoka katika Hekalu la Sulemani, na Wababeli wakalinajisi. (Eze. 10: 4,18,19,11: 23; 2 Waf.25: 8-17). Badala yake Mungu ameweka jiwe la msingi la nyumba nyingine tofauti kabisa “Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, lililojaribiwa jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio; yeye aaminiye hafanya haraka au hatatahayarika (Isaya 28: 16; Warumi 9: 33, 10: 11-12; Waefeso 2: 19-22, 1 Petro 2: 4-7). “Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu …yeye aliye na sikio, na asikie”.

REJEA KATIKA MAKTABA:
 “Historia ya Biblia” (H,P, Mansfield) ukurasa 4,Namba .8
 “Sheria na Neema” W.F. Barling) Sura 5
“Sheria ya Musa” (R. Roberts) ukurasa 95-154.
 

Swahili Title: 
SULEMANI ANAMRITHI DAUDI
English files: 
Swahili Word file: