1 Peter Chapter 00

Swahili

1 Petro – Utangulizi – Sura ya 1586

WARAKA WA KWANZA YA PETRO

Hakuna mtu anayejua maisha ya Kristo anahitaji uanzisho wowote kwa Petro – Petro, aliyejaa matumaini na waraka huu inaelezea tabia yake. Neno ka huhimu ni matumaini (1 Petro 1: 3). Tukio la waraka ni kesi iliyotarajiwa; hivyo kutiwa faraja ilikuwa muhimu. Lakini Uhimizo mkuu ulitoka kubadilika kwa Petro mwenyewe. Katika Injili, Petro alimwona Bwana wake akiwa amebadili sura: na pia tunamwona Petro pia akiwa amebadilika kwa neema isiyo na mipaka ya Mungu.Neno muhimu ni "kuteseka" ambalo limetajwa mara ishirini na moja katika kitabu hiki kifupi, na katika kila sura mateso ya Kristo yanatajwa. Lakini maono ya Petro yanatuwezesha kutazama zaidi ya majaribu kwa utukufu utakao funuliwa hatimaye (1 Petro 1: 7).

MWANDISHI WA WARAKA
Waraka wa Kwanza ya Petro ina umuhimu sana kwa ajili ya mambo mawili: (a) kama utafiti wa tabia ya Mtume mkuu mwenyewe; na (b) kama mwongozo wa utukufu wa Mungu.

Waraka huu unathibitisha nguvu za kubadilisha za Mungu. Petro ni mtu aliyebadilika, ambaye hana kiburi, wala mwenye kujivunia, bali "mchungaji wa kondoo" (sura ya 5:1-4), mwenye hamu ya kutembea na kuongoza kwa uangalifu wale ambao wanapata matatizo kutembea katika njia ya maisha. Waraka unahusu makosa yake ya zamani na uzoefu anaoweza kuwasaidia.

Imeandikwa katika Matendo kwamba wakati watu waliona mabadiliko makubwa yaliyofanyika katika mitume wa Bwana baada ya kufufuka kwake na kupaa, "walishangaa"; nao wakatambua kwamba walikuwa pamoja na Yesu (Matendo 4:13). Tunaweza kushangazwa na mabadiliko yaliyofanyika kwa Petro kama inavyothibitishwa na waraka ulio mbele yetu, na kuona ndani yake matendo ya Kristo ndani ya mtu aliye tayari kupokea maelekezo yake. Ni muhimu kutambua sehemu za waraka ambayo imeandikwa kutokana na uzoefu wa maisha ya Petro mwenyewe. Jinsi mapungufu ya ya hapo zamani ya athari katika mawazo ya Mtume, akiwahimiza ndugu kuepuka mambo ambayo yeye mwenyewe alifanya. Alikuwa amekataa mara kwa mara akiwa kwa kiapo kwamba yeye alikuwa mfuasi wa Yesu, lakini sasa anaandika hivi:

"Kwa maana ni sifa gani kustahimili mtendapo dhambi na kupigwa makofi?" Lakini, kustahimili mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele ya Mungu "(Mst 2: 20).
Alikuwa shahidi wa karibu wa mateso ya Kristo, na anaweza kuandika kutoka kwa msimamo wa kibinafsi kwa maneno yafuatayo:
"Yeye hakufanya dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake, alipotukanwa hakujibu kwa matusi, alipoteswa hakuogofywa, bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki" (sura. 2: 22-23). ).

Tena: "Wazee ambao ni miongoni mwenu ninawasihi, mimi niliye mzee kama nyinyi, na shahidi wa mateso ya Kristo, na pia mshirika wa utukufu utakafunuliwa baadaye" (Mst 5: 1).

Tunasoma kwamba Petro baada ya kumkana Bwana wake, na wakati ukweli wa upungufu wake uliletwa nyumbani kwake, alienda usiku "akalia kwa uchungu." Inaweza kuwa ni kumbukumbu za maovu yake ilimfanya maneno makali ya sura 3: 10-13:

"Kwa maana yeye anayependa uhai na kuona siku njema, basi na azuie ulimi wake kusema uovu, na midomo yake isitoe matusi, na aache uovu, na afanye mema, na atafute amani. Kwani macho ya Bwana yako juu ya waadilifu (lig. Luka 22:61), na masikio yake yako wazi kwa sala zao, lakini uso wa Bwana umewapindukia wale wanaotenda dhambi. Na wale watakao wadhuru ninyi mkiwa wafuasi yale yaliyo mema. "

Petro ndiye alikuwa amelala wakati Bwana alimwita kuangalia Gethsemane wakati alienda kujitia nguvu kwa sala; lakini sasa Mtume anaandika:
" Lakini mwisho wa vitu vyote umekaribia, basi kuweni na akili na busara, na mkeshe kwa sala" (sura. 4: 7).

Kulikuwa, na majadiliano ya kina yaliyoandikwa katika Yohana sura. 21, ambapo Bwana alimwuliza Petro; "Simoni, mwana wa Yona, unanipenda kuliko hawa?" Petro akamjibu: "Naam, Bwana, unajua ya kuwa nakupenda" (ms.15). Swali hili liliulizwa mara tatu, na mara tatu jibu lilikuwa lile lile. Toleo Maalum, halielezei kwa kikamilifu tukio hilo. Tunaona kwamba neno "upendo" linalotumiwa na Bwana katika maswali mawili ya kwanza ni, katika Agapao ya Kigiriki, linamaanisha upendo wa kujitolea ambao ni huduma kwa wengine. Petro katika majibu yake alitumia neno tofauti kabisa, fileo, ambalo linahusiana na upendo wa kibinadamu. Upendo ambao Petro alikuwa nao kwa Bwana wakati wote, hata wakati wa udhaifu alipomkanusha. Sasa akifahamu udhaifu wake, na kukumbuka mapungufu yake ya zamani, alikuwa makini kutokadiria zaidi hisia zake na uwezo wake, na hakuhisi kustahili upendo mkubwa ambao Bwana aliuliza kwa swali lake. Kwa hivyo, alikubali tu upendo wa Fileo kwa Bwana wake.

Wakati, katika tukio la tatu, Yesu alibadilisha neno ambalo Petro alikuwa ametumia hapo awali na akauliza: "Unanipenda (fileo) mimi?" Petro alihuzunika. Ilikuwa kama Bwana alikuwa anauliza hasa upeno ambao Petro alidai kuwa nao kwake. Lakini, Bwana alionyesha kwamba upendo huu lazima ufunuliwe kwa vitendo: "Lisha kondoo wangu."
Kama matokeo ya mazungumzo haya ya moyo, Bwana mwenye neema alimpa Petro uhakikisho kwamba atakomaa mpaka kufikia mahali ambapo angeonyesha kuonyesha kwa kikamilifu upendo wa agapao:


 

"Amini amini nawaambieni, ulipokuwa mdogo, ulikuwa ukijifunga mwenyewe, na kwenda mahali utakako, lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga, na kukupeleka usikotaka. "(Yoh 21: 18-19.) Yeye alisema hivi, akiashiria kwa mauti gani atamtukuza Mungu ..." (Yoh 21: 18-19.)


Hivyo, kubadilika kwa Petro, ambao Bwana alikuwa ameomba hapo mapema (Luka 22: 31-32) ungetimia kwa kamilifu.

Waraka ulio mbele yetu unatoa uthibitisho wa utimilifu wa utabiri wa Bwana. Inatufunulia tabia iliyobadilishwa, tulivu na iliy komaa ya Petro aliye tofauti na yule tuliyeelezewa kumhusu na rekodi za Injili. Lakini tizama jinsi Petro mwenyewe anarejelea tukio hili , kwa kuwatia moyo ndugu zake. Kwa kweli, anaonyesha kwamba wanapaswa kujifunza kwa uzoefu wake. Kama vile anandika hivi katika waraka:


"Kwa kuwa mmeitakasa nafsi zenu na kutii ukweli kwa upendo wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidi kupendana kwa moyo safi kwa bidii" (Mst 1:22).

Maneno mawili yaliyotafsiriwa "upendo" katika tamko hili ni tofauti kabisa na maandishi ya awali ya Kiyunani. Petro anawahisi ndugu kwa maneno sawa kama Bwana alivyomsihi; anawaita ili kuona kwamba upendo wao wa fileo unakuja kuwa upendo wa kujitolea kama ule Kristo alioonyesha wakati "alitoa maisha yake kwa ajili ya kondoo."


Hivyo kuna maelekezo mengi yanayofanana ya kusihi katika waraka huu ambayo yanatokana na matukio ya maisha Petro. Ni faida sana kutambua pointi hizi, na kuchunguza mabadiliko makubwa katika mtazamo na tabia iliyoonyeshwa na Mtume.


 

HIVYO TUNAJIFUNZA KUHUSU NGUVU ZA KUBADILISHWA NA NGUVU ZA KRISTO KATIKA MAISHA YA MTUME WAKE.
Maoni yetu ya mstari kwa mstari yameundwa ili kusisitiza kipengele muhimu cha waraka, pamoja na kuelezea umuhimu wa ujumbe wa Mtume.

MFANO WA MHUSIKA
Simoni Petro, mwana wa Yona (au Mwamba wa kusikia uliojaa Njiwa-ishara ya Kristo-Mathayo 12:39), alikuwa mvuvi wa Bethsaida (Nyumba ya Samaki) aliyekuwa "mvuvi wa wanadamu" (Mt. 4:19). Alikuwa akishirikiana na ndugu yake na Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo (Luka 5:10). Ingawa haijaelezewa waziwazi, labda alikuwa mwanafunzi wa Yohana Mbatizaji, lakini alitambulishwa na Yesu na Andrea ndugu yake (Yohana 1: 35-41), na kupewa jina la Petro (Mwamba au Jiwe) na Bwana ( Mst.42).

Hakumfuata Bwana mara moja, lakini alipewa wito mara tatu: Kwanza, kama mwanafunzi (Yohana Ch.1); pili, kama mshiriki (Mathayo 4:19); na, tatu, kama Mtume (Mk 3: 14-16; Luka 6: 13-14).

Pia alikiri kwa Kristo mara tatu (Mathayo 14:33, 16:16; Yohana 6: 68-69), kila mmoja zaidi kuliko ya awali, na pia kumkana Bwana mara tatu kwa, hata hivyo, alitubu haya kwa kuonyesha upendo mara tatu (Yohana 21: 15-17).

Nguvu zake, bidii, ujasiri, na msukumo wa tabia ulimfanya kufanya makosa, lakini pia ukamleta mbele ya wanafunzi (Mathayo 10: 2, Mk 3:16, Luka 6:14; Matendo 1: 13-alitaja kwanza). Ushawishi wake ulimfanya awe wa kwanza kumkiri Yesu kama Mwana wa Mungu (Mathayo 16:16), lakini, punde tu, akawa wa kumzuia Bwana kupita njia yake ya kuchaguliwa ya mateso (Mathayo 16:22). Kwa njia hizi mbili tofauti alipendwa na kulaumiwa.


 

Maisha yake yanaonyesha kuwa alikuwa mtu mwenye msukumo (Mathayo 14:28, 17: 4, Yohana 21: 7), mwenye huruma na upendo (Mathayo 26:75; Yohana 13: 9; 21: 15-17), wenye ujuzi wa kiroho ( Yohana 6:68), na wakati mwingine kutoelewa ukweli wa kina kwa haraka (Mathayo 15: 15-16). Kwa hivyo alikuwa na ujasiri wa ushuhuda, lakini mwenye woga (Mathayo 16:16, Yohana 18:10, Marko 14: 67-71), mwenye kujitolea, lakini mara nyingi kuwa mbinafsi (Mathayo 19:27), na hata wa kujisifu (Mathayo 16:22; Yohana 13: 8; 18:10). Lakini pale anapoamua, alikuwa hatikisiki kwa imani (Matendo 4: 19-20; 5: 28-29, 40-42).


Biblia inarekodi hatua tatu za maendeleo ya kiroho katika maisha yake:


Mafunzo Yake: Hii ilihusu ushirikiano na Bwana katika huduma yake ya umma, na alihitimisha kwa ushahidi wa Kristo kumwamini (Yohana 21: 18-19).

Uongozi Wake: Alionyesha uongozi ujasiri katika Kanisa ya kwanza, kuanzisha uteuzi wa Mathia kuchukua nafasi ya Yuda (Matendo 1:15); kutangaza Injili waziwazi siku ya Pentekoste (Matendo 2:14); kuponya, kuhubiri, na kutetea imani (Matendo 3: 4, 12; 4: 8); kumkemea na kumhukumu Anania na Safira (Matendo 5: 3, 8); akihubiri ukweli kwa Kornelio na kuwabatiza watu wa mataifa (Matendo ya Ch.10); na kuongea wazi wazi neno katika mkutano Yerusalemu (Matendo ya Ch.15). Lakini licha ya uongozi wake jasiri, ambao ulihitajika na Kanisa, tabia ya Petro haikuwa kamili. Paulo aligundua jambo hili, wakati alipinga na kumkemea kule Antiokia, "kwa sababu alikuwa wa kulaumiwa" (Wagalatia 2: 11-14).


Mchungaji Wake: Baada ya misingi ya Kanisa kuwekwa, Petro alianza kujiondoa kwenye umma, na kuchukua nafasi ya mfuasi mnyenyekevu. Yakobo alitawala Yerusalemu (Matendo 12:17, 15:13, 21:18, Wagalatia 2: 9, 12), na Paulo alifanya hivyo kati ya Wayahudi. Petro alijulikana kama Mtume wa waliotahiriwa (Wagalatia 2: 8), na alionekana kupunguza shughuli zake kwa wale walio nje ya Yerusalemu: Antiokia (Wagalatia 2:11); Korintho (1 Wakorintho 1:12); Babiloni (1 Petro 5:13), ambako, pamoja na mkewe, akawa mtu wa kawaida (1 Wakorintho 9: 5).

Kwa kutii amri ya Kristo, alichukua jukumu la kuongoza na kulisha kondoo (1 Petro 5: 1-4), na wakati huu haikuwa na hali kibinafsi kama hapo awali (cp 2 Pet 3: 15-16). na Wagalatia 2: 11-14). Hivyo hatimaye anaonekana katika rekodi za Biblia kama mtu aliyebadilika kabisa, mwenye nguvu zaidi za unyenyekevu wake kuliko wakati wa ubinafsi.

KILA SURA YA MAISHA YA PETRO INATOA USHUHUDA WA NGUVU ZA KUBADILISHA KUPITIA MIFANO YA KRISTO ( Matendo 4:13).
Daimam mwenye shauku, msukumo, na mtu wa vitendo, alionyesha kasoro pamoja na sifa za tabia. Uzuri na upngufu wake ulikuwa na msingi katika shauku yake kuu. Lakini ni sifa ya kuwa na msukumo ambayo ilibandilishwa na ukweli, na bidii yake ya kufuata Bwana. Alipewa usisitizo wa kipekee na Kristo, akipewa usisitizo wa kipekee hata wakati wa maumivu zaidi wa huduma ya Bwana (Luka 22:31) na baadaye (Yohana 21:15), na kupewa heshima ya kuwa na Kristo baada ya ufufuo wake (1 Wakorintho 15: 5).

Uzoefu wa Petro unatoa maelekezo, onyo, na faraja. Nyaraka zake mbili zinafafanua kina cha uzoefu wake katika Kristo, na kuongeza matumaini yake anapoangalia wakati ujao.


Desturi zinaonyesha kwamba alitembea Roma wakati wa utawala wa Nero, na miaka michache baadaye akauawa kwa kusulubiwa, kama vile Kristo alivyotabiri (Yohana 21:19). Simulizi zinasema kwamba Petro hakuona kuwa anastahili kufa kwa njia sawa na Bwana wake, kwa hivyo aiwasihi wauaji wake kumtia msalaba akiwa kichwa chini, na ilifanyika hivyo.

NYARAKA KAMA FUNGUO ZA UFALME
Akiwa Kaisaria Filipi, Petro alikiri jambo muhimu sana: "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai," kwa kumjibu Bwana alisema hivi:
"Heri wewe, Simoni Bar-yona, kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni." Nami nakwambia wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitajenga Kanisa langu na wala milango ya kuzimu haitalishinda, nami nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni ... "(Mathayo 16: 17-18).

Kuna mambo muhimu katika maneno haya yanayohitaji umakini wetu. Kwanza, kuna kucheza kwa maneno ya Petro na Mwamba, maana jina Petro linamaanisha mwamba. Lakini pia kuna tofauti kubwa katika maneno yaliyotumika katika muktadha. Neno Petro ni Petros kwa Kigiriki, na linaashiria jiwe lililo lengea; ambapo neno Mwamba ni Petra, na linaashiria mwamba ulio imara. Petro, kama jiwe lililolengea, linaweza kufanywa imara na kuwa hekalu la kiroho juu ya msingi wa Kristo. Hivyo Petro alifujindisha mwenyewe (1 Pet: 2: 4-5). Lakini Petra, mwamba imara, hakutaja mtu, bali jinsi ALIVYOKIRI Alifanya: "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai."
Ni juu ya msingi wa tamko hili lililo-ongozwa na Mungu ambapo Kanisa inaanzishwa.


Ni muhimu kutambua kwamba kukuri huku kunatambua kwamba Yesu ni Masihi wa Israeli, na Mwana wa Mungu. Lakini kile watu wanafurahi kuita "kanisa" haijakubali kukiri huku. "Kanisa" la wakati huu halijui matumaini ya kweli ya Israeli, na kwa hivyo halitambui nafasi ya kweli ya Kristo kama Masihi. kwani linakiri kwamba yeye ni Mungu, sio MWANA WA MUNGU.

Ni wale tu wanaojitambulisha na kukiri kwa awali kwa Petro wanathibitishwa na maneno ya Kristo kama Kanisa la kweli.


Bwana, anampa Petro "funguo za Ufalme", pia anawaambia wanafunzi haya:
"na lo lote utakalo funga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalofungua duniani litafuguliwa mbinguni."

Sentensi pengine imetafsiriwa vizuri katika tafsiriwa wa C.B Williams wa Biblia:
"Chochote utakachokikaza hapa duniani kitakuwa tayari kimekatazwa mbinguni, na chochote unachoruhusu duniani kitakuwa tayari kimeruhusiwa mbinguni."

Kukubali tafsiri hii, Yesu alikuwa anawaambia wanafunzi wake kwamba Kanisa, iliyoanzishwa juu ya kukiri kwa Petro, inapaswa kufuata kwa kikamilifu mapenzi ya Mungu. Yote ambayo Yamekataza, na yote ambayo yameruhusiwa, lazima yawe kwa mujibu wa mapenzi ya Baba, na ni lazima yote yawe katika misingi ya jina lake.

Petro, basi, alikabidhiwa funguo za Ufalme, na alianza kwa kuzitumia, kufungua siri za Ufalme wa Mungu kwa jina la Yesu Kristo kwa Wayahudi siku ya Pentekoste, na baadaye, kama ilivyoandikwa katika Matendo Ch. 10, kwa Kornelio, mtu wa Mataifa.

Ni kitu gani Petro aliweza kufungua kwa Wayahudi na Watu wa mataifa katika kutumia funguo hizo? funguo mbili ni muhimu katika kufungua mlango ambao utafunua Ufalme! Na funguo hizi ni zipi? Ukweli kuhusu MAUMIVU ya Kristo, na UTUKUFU ambayo utafuata. Kristo ndiye mlango (Yohana 10: 9), na ndani yake tunaona mateso msalabani yalikuja kabla ya kuvikwa taji.

Mambo haya mawili ya madhumuni ya Mungu yalitambulishwa kwa Mitume mara moja baada ya Bwana kutangaza kuwa atawakabidhi funguo za ufalme. "Alianza kuwaonya wanafunzi wake jinsi atakavyoteswa" (Mathayo 16:21). Huu ukawa "ufunguo wa kwanza". Ukawa ufungua ambao wanafunzi hawakuujali wakati huo (Mst 22-23). Kisha Yesu akawapa kionjo cha "ufunguo wa pili" : utukufu utakaofuata. "Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, Yakobo, na Yohana nduguye, na kuwapeleka juu ya mlima mrefu faraghani, akageuka sura mbele yao" (Mathayo 17: 1-2) - na hivyo waliona utukufu wake. Ilikuwa maono ya ufalme, na ingawa hawakutambua wakati huo, Yesu alikuwa anawakabidhi ufunguo mwingine, ambapo wangeweza kufungua "mlango" na tazama wakati ujao.

Ni muhimu, kutokana na yale yalitokea hapo awali, ikawa muhimu kwa Petro kuandika nyaraka mbili ambazo zinafunua sehemu mbili za Ufalme na Jina. Katika 1 Petro 1:11 anarejelea "mateso ya Kristo, na utukufu ambao utafuata," na anarejelea utukufu uliofunuliwa kwao katika Mlima wa Kubadilika Uso. Mfano wa mateso na utukufu wa Yesu Kristo ni mfano wa funguo mbili za Ufalme, na Petro anazitumia, kwanza wakati wa Pentekoste, na baadaye katika kubadilishwa kwa Kornelio.

Funguo hizi mbili zinawasilishwa katika nyaraka mbili za Petro.
FUNGUO YA KWANZA: inaonyesha wazi wazi mateso ya Kristo (1 Pet 1:11, 2:21; 3: 17-18; 4: 1, 13).
FUNGUO YA PILI: inatuonyesha utukufu (2 Pet 1: 4, 17; 3: 9-13).


 

Kwa hiyo Petro anatutendea yale Bwana aliyotenda kwenye barabara ya Ernmaus, alipowaonyesha wanafunzi wawili jinsi ya kutumia funguo hizi mbili (angalia Luka 24: 25-27).

Kwa aina ya Israeli, Sehemu ya Pili, Sura ya Kwanza, Ndugu Tomasi anaonyesha jinsi "funguo za Ufalme" zilikabidhiwa Petro ili awaze kufungua siri za Injili na kufunua njia ya uzima wa milele kwa "Yeyote aliye na masikio ya kusikia" . Alifanya hivyo, kwanza kwa Wayahudi katika siku ya Pentekoste, na, pili kwa watu wa mataifa katika kuhubiri Kweli kwa Kornelio. Kwa njia hii, njia ya Ufalme ilifunguliwa hadharani kwa Wayahudi na kwa Watu wa mataifa (kwa hivyo haja ya funguo mbili). Ndungu Thomas anafupisha sehemu hii ya ufafanuzi kwa njia ifuatayo:

"Baada hii Petro alitumia funguo za ufalme wa mbinguni alizokabidhiwa na Bwana Yesu Kristo. Na alipo kamilisha kazi hii, hakuwa na nguvu za funguo tena. Kwani zilikabidhiwa umati wa Wayahudi na watu wa Mataifa walioamini, Roho alifunua siri ya ufalme, na ushirikiano wa ajabu, kwa kinywa cha Petro wakati wa Pentekoste na Kaisarea, ili funguo ziwe mali ya umma kwa waumini wote. Bwana aliye na ufunguo wa Daudi, Yeye mwenye kufungua na wala anayeweza kuifunga "(Ufunuo 3: 7-8). Ameweka mlango wazi mbele ya Wayahudi, na hakuna mtu anayeweza kuifunga, wakati maandiko yamo mikononi mwa ya watu. Nabii wa uongo wanajifanya kuwa na funguo za kuathiri uwezo wa Mwana wa Mungu, lakini kama "SHERIA NA USHUHUDA" zinapatikana 'kila mtu mwenye kiu anaweza kuja; na yeyote atakaye kunywa maji ya uzima kwa uhuru. Maandiko yana funguo. Mapapa, makuhani, na waalimu wa dini wanaweza kuponda na kuharibu ukweli, na kuweka vikwazo njiani; lakini mtu anayekataa mamlaka haya, na kufikiria mwenyewe, anapata kuwa na hekima kwa wokovu wa imani iliyo katika Yesu Kristo. Basi wacha watu wajisaidie wenyewe, ikiwa naye Mungu atawapa msaada. "

KUANDIKWA KWA BARUA

Barua za Petro zilikuwa zimeelekezwa kwa watu sawa na wale Yakobo aliandikia. Kusudi lao kuu lilikuwa kuwatia ndugu waliokuwa wakipitia wakati wa mateso yaliyokithiri. Petro, kwa hiyo, aliongeza kwa wazo kuu la Yakobo. Ingawa Yakobo alisisitiza kwamba imani lazima ionyeshwe kwa matendo, Petro alisisitiza kwamba ni jaribio la imani ambalo litakamilisha kazi.


Petro alikuwa amegundua ukweli wa maisha yake mwenyewe. Katika siku ambazo Kristo alitabiri kuanguka na kuinuka kwa Petro, alisema: "Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi (yaani Mitume), ili awapepete kama ngano; lakini nimekuombea wewe, ili imani yako (Petro) isitingike na wakati utakapoongoka, uwaimarishe ndugu zako "(Luka 22: 31-32). Katika barua zake zote mtume alifanya hiyvo.


Barua hiyo inahusiana na maisha yake mwenyewe. Anaonyesha kusudi la kuandika kwake kama "kuhimiza na kushuhudia" (1 Petro 5:12). Anawahimiza ndugu zake kwa msingi wa uzoefu wake mwenyewe, na anatoa ushahidi, au kushuhudia, kwa kweli katika Kristo Yesu, akiwa na ushahidi binafsi wa yote aliyoyasimamia. Uchunguzi ufuatao wa barua hii unaonyesha Injili kama njia ya maisha; wakati yaliyomo yaliyashuhudia nguvu ya kubadilisha Kristo katika uzoefu wa mwandishi binafsi.

Barua inaonya juu ya mateso yaliyotarajiwa ambayo waumini watakumbana nayo, na ambayo ingewajaribu kabisa (tizama sura 4: 12-5: 11). Hii ni dhahiri na ile iliyoanzishwa na Nero dhidi ya Wakristo, kufuatia kuungua kwa Roma. Nero alitawala kutoka A.D. 54-68. Ana sifa ya kuwa mmoja wa watawala katili katika historia. Alikuwa na umri wa miaka 16 tu alipoanza kutawala. Seneka, mwanafalsafa mkuu wa Kirumi, alikuwa mwalimu wake na mshauri katika miaka ya mwanzo ya utawala wake. Pamoja na msaada wa Seneka Nero alikolezwa na nguvu. Aliwaua mkewe na mama yake, na aliamuru Seneka na mshairi Lukan kujiua.

Mwaka AD 64, moto mkali ulichoma Roma. Wanahistoria wanadai kwamba Nero aliwasha huu moto. Na inasemekana kwamba alishangilia moto huu huku akiimba kuhusu moto wa Troy. Ili kujiondolea lawama, alidai kwamba Wakristo walikuwa na hatia ya uhalifu, na kwa adhabu, alianzisha mateso ya kutisha dhidi ya Wakrsito. Kwa miezi kadhaa Wakristo wasiokuwa na hatia waliteswa kwa ukatili. Wanaume, wanawake na watoto waliwekwa katika uwanja wa kukabiliana na wanyama wa mwitu ambao kwa ukatili waliwararua vipande vipande, wakati umati mkubwa ulikuwa ukiangalia na kushangilia. Wakati wa jioni Nero alifanya "burudani" ambalo Wakristo walikuwa wametumbuizwa kwenye mafuta, kufungwa kwa miti mirefu, na kisha kuchomwa moto ili kutoa mwangaza. Mraba hiyo iliwashwa na taa za kuchomwa moto za miili inayoungua ya wanaume na wanawake ambao makosa yao tu yalikuwa uamuzi wao wa kumtumikia Mungu wao kulingana na dhamiri zao.


Ingawa mateso haya yalikuwa yakitendeka Roma pekee, matokeo yalifikia mahali kwengine. Wakati mateso yalienea katika ufalme, sheria zilipitishwa na ikawa makosa kuwa Mkristo. Kwa hiyo, ibada ilikuwa ifanyike kwa siri.


Katika mwaka A. D. 66 Uasi wa Kiyahudi ulianza, na Nero akamtuma Vespasiani kuukomesha. Hii ilianzisha vita vya Kiyahudi ambavyo vilipelekea uharibifu wa Hekalu katika AD 70. Upinzani wa Wayahudi ulienea katika Ufalme wa Roma na ulisikia na Wakristo.

Kwa mtazamo wa unabii wa Petro wa mateso yatakayotokea (ona sura. 4:12), barua hii, iliyoandikiwa Babiloni (sura 5:13), iliandikwa katika mwaka wa AD 60. Inatoal mafunzo jinsi Waumini walipaswa kuishi kwa sababu ya shida na majaribu yaliyokuwa yanajaribu imani yao.

UCHAMBUZI
Kuna njia mbili za kujifunza Biblia: kwa umbali na kwa kina. Ya kwanza inaangazia mtazamo wa jumla wa barua; wa pili unahusisha uchambuzi wa mstari kwa mstari. Mifumo yote ni muhimu kuelewa kikamilifu masuala ya Ufunuo wa Kimungu.


Tunapopata utambuzi wa umbali wa Biblia, tunaweza kutambua maana ya mstari kwa mstari au maneno fulani, na kwa hiyo tunaweza kuelewa kwa undani maana ya mstari huo au taarifa.


Hivyo basi tunaanza uchambuzi wa waraka huo, na tunashauri kwamba mwanafunzi asome kwa wakati mmoja barua nzima na muhtasari wake.

BARUA YA KWANZA YA PETRO YA USHINDI KATIKA MAJARIBIO
Funguo Ya kwanza kati ya mbili zilizokabdhiwa Petro, zilionyesha mateso ya Kristo kabla ya utukufu wake (sura.11:11) kwa njia ambayo milango ya Ufalme itafunguliwa.


 

1. UTANGULIZI — Sura. 1:1-2

Ufafanuzi wa Mkristo Sura. 1: 1- 2;

2. MWITO NA KILE UNAHUSHISHA —Sura. 1:3-2:10

Tumaini letu la Kuishi — Sura. 1: 3-12;

Njia ya Uhai — Sura. 1:13-16;

Sadaka ya Kuishi — Sura. 1:17-21;

Neno la Kuishi — Sura. 1:22-25;

Nguvu za kuishi — Sura. 2: 1- 3;

Mawe ya Kuishi — Sura. 2: 4- 8;

Ukuhani wa Kuishi — Sura. 2: 9-10;

3. MAISHA YA HIJA NA JINSI YA KUISHI — Sura. 2:11-4:11

Kwa ulimwengu — Sura.2:11-17;

Kwa Wakuu — Sura. 2:18-25;

Kwa Waume —Sura. 3:1-6;

Kwa Wake — Sura. 3:7;

Kwa Wakristo — Sura. 3: 8-9;

Kwa watu wa mataifa — Sura.3:10-13;

Kwa wanyanyasaji — Sura 3:14-17;

Kufanana na Kristo, Mfano — Sura.3:18-22;

Silaha za Ushindi —Sura. 4:1-11;

4. MAJARIBIO MAGUMU NA JINSI YA KUYAHMILI — sura. 4:12-5:11

Kama washiriki wa mateso ya Kristo — Sura.4:12-19;

Kama Wakuu wakitoa mfano — Sura.5: 1-4;

Kama Kondoo wakitii kwa uvumilifu — Sura.5: 5-11;

5. MANENO YA MWISHO — sura. 5:12-14

YALE TUNAYO JIFUNZA

 

Maisha katika Kweli haipaswi kuwa rahisi, hivi ndivyo tunafundishwa na Mungu

 

MAKTABA YA KUREJELEA

 

HP Mansfield – 1 Petro

 

MASWALI YA AYA:

Ni sifa gani za Petro katika hadithi za Injili

Ni sifa gani za Petro tunazopata katika Maandiko

 

MASWALI YA INSHA:

Mambo gani tunaweza kujifunza kutokana na mabadiliko ya Petro

 

MASWALI YA MAJADILIANO:

Tunawezaje kuendeleza mabadiliko kwa kila mmoja kwa ajili ya bora ndani ya Ekklesia?

 

Literature type