The Bible

Swahili

Utume wa Biblia ya Ndugu katika Kristo

KWELI ZA MSINGI ZA BIBLIA

Biblia

Kipeperushi hiki kinatoa majibu kwa maswali haya:

  1. Biblia ni nini?
  2. Je, tunaweza kuiamini Biblia?
  3. Kwanini tusome Biblia?
  4. Namna gani Biblia inaweza kutusaidia?
  5. Biblia inasema nini kwa wakati ujao?

KITABU CHA  MWONGOZO WA MAISHA

HAKUNA kitabu chechopote kinachoweza kulinganishwa na Biblia. Waandishi arobaini tofauti walitumiwa – wegine walikua wafalme, manabii, makuhani, viongozi, madaktari, wavuvi au wachungaji. Waliandika kwa kipindi cha miaka 1,600.

Ni ya kipekee NI NENO LA MUNGU.

“Zaidi ya yote mnapaswa kufahamu ya kuwa hakuna unabii wowote katika maandiko uliokuja kwa kutafsiriwa kwake mwenyewe. Maana unabii haukuletwa kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu, bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa mungu wakiongozwa na roho mtakatifu” (2 Petro 1:19, 20)

kila andiko lenye pumzi ya Mungu  

                                                   (2 Timotheo 3 :16)

Biblia si kitabu cha kawaida; hakina mawazo ya mwanadamu. Ni Mungu anazungumza nasi. Anza kusoma biblia leo.

KWANINI USOME BIBLIA

Ni kutoka katika Biblia pekee ndipo tunaweza kujua jinsi mungu alivyo. Soma  mistari hii michache. Unamsikkiliza mungu akiongea nawe.

Wewe ni mwema na unasamehe, Ee Bwana mwingi wa upendo kwa wote wakuitao.”                                  

                                                             (Zaburi 86:5)

Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana.”             (Mwanzo 1:31)

Mbingu za juu ni za Bwana bali nchi amempa mwanadamu.”                              (Zaburi 115:16) 

Usiwe na miungu mingine ila mimi.”

 (Kutoka 20:3)

Uso wa BWANA ni juu ya watendao mabaya, aliondoa kumbukumbu lao Duniani.”

    (Zaburi 34:16)

Mungu amekuambia mambo mangapi kuhusu yeye mwenyewe katika mistari hii.

BIBLIA INATUPA KUSUDI LA MAISHA YETU Tunaposoma tunamsikiliza Mungu. tunajifunza kile ambacho Mungu anataka tufanye. Tunajifunza jinsi ya kufanya kila siku kuwa ya thamani.

 “Neno lako ni taa ya miguu yangu” (Zaburi 119:105)

“BWANA, Mungu wako anataka nini kwako, ila kumcha BWANA, Mungu wako, kuenenda katika njia zake zote za kumpenda na kumtumikia BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kushika  maagizo na sharia za BWANA….. kwa faida yako mwenyewe”

                   (Kumbukumbu la Torati 10:12,13)

Tunamwomba mungu atusaidie kila siku “… Usitutie majaribuni bali utuokoe na yule mwovu

          (Mathayo 6:13)

Scrolls

Agano la kale linaandikwa kwa mara ya kwanza kwa Kiebrania kwenye gombo.

BIBLIA HUTOA UJUMBE HUO DAIMA

Unaposoma kidogo Biblia kila siku utaona kwamba Mungu anataka tumtii.

Katika agano la kale tuna miongozo katika Kutokaa 20:1-7 mara nyingi huitwa amri kumi za mungu. miongozo kama hiyo inapatikana katika Agano jipya pia kwa mfano katika Mathayo 5:21-38.

Ili kumpendeza Mungu tunajaribu kuzingatia miongozo hii. Unaposoma Zaidi kuhusu maisha ya watu katika Biblia unaona kwamba  wanaona ni vigumu kumtii Mungu siku zote. Yesu mwana wa Mungu alikuwa mtu wa pekee  wa kumtii mungu kwa kila namna. Yesu alielewa ujumbe huo huo. Alikumbuka “Mwanadamu haishi kwa mkate tu bali  kila neno litokalo katika kinywa cha BWANA”

                               (Kumbukumbu la Torati 8:3)

mche BWANA Mungu wako umtumikie yeye peke yake (Kumbukumbu la Torati 6:13)

Soma Mathayo sura ya 4 ili uone jinsi Yesu alivyitii amri hizo.

HISTORIA YA NYUMA INAONYESHA KWAMBA BIBLIA INATEGEMIKA

Yesu alitazama nyuma katika unabii unaomhusu yeye mwenyewe

“na akianzia Musa na manabii wote akawaeleza yale yaliyonenwa katika maandiko yoto kumhusu yeye mwenyewe” (Luka 24:27).

Haya yote yalitimizwa. Hapa kuna mifano mkingine ya unabii wa Biblia ambao umethibitika kuwa wa kweli:

  • Angalia Yeremia 51:37 na Isaya sura ya 13 na 14. Nini kingetokea Babeli?.- ilitokea.
  • Soma Ezekieli 26:5, 5, 12, 14. Nini kingetokea kwa mji wa Tiro? Huu ni unabii mwingine ambao umetimia.
  • Kumbukumbu la Torati 28:64,65 inatuambia kuhusu watu wa Israeli. Wangetumwa kila sehemu ya Dunia. Kwa hakika watu wa Israeli Wayahudi wanapatikana kila mahali leo.
  • Mungu alisema kwamba angewarudisha wayahudi kwa Israeli “nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zaop waimiliki” (Yeremia 30:3). Leo tunaweza kuona wayahudi katika nchi yao wenyewe - unabii mwingine ukitimizwa

Biblia haituambii tu mambo ya zamani lakini pia inatuambia kuhusu wakati ujao. Tunajua kswamba , yale yaliyosemwa zamani yalitokeaa kweli kweli, unabii wa Biblia ulitimizwa kwahiyo tunaweza kwa uhakika. Amini yale ambayo Mungu anayasema kuhusu wakati ujao.

Mungu kamwe hasemi uwongo. Yeye hutuambia kuhusu maneno halisi ya watu  na mataifa ya leo. Biblia ni kweli!

BIBLIA INAELEZA MATUKIO YAJAYO

Mungu anatuambia kwamba mambo haya yatatokea.

  • Hataruhusu ulimwengo wenye uovu uendelee milele                     (2 Petro 3:10)
  • Atamtuma mwanawe Yesu Kristo tena Duniani kuhukumu wanadamu       (Matendo 17:31)
  • Mtamfanya Yesu kuwa Mfalme wa ulimwengu wote                           (Zaburi 2)
  • Wote wanaompinga Mfalme wataangamizwa        (2 Wathesalonike (1:8)
  • Wote wanakuwa wafuasi wa Yesu na kungojea kuja kwake wataokolewa na kupewa nafasi katika Ufalme wa Mungu             (Warumi 2:6)
  • Utakuwa ufalme wa Amani na furaha wenye wingi wa chakula kwa wote.               (Zaburi 72)

Ni Biblia pekee inayokuambia  juu ya mambo haya yote na kuhusu mpango mkuu wa Mungu.

Soma biblia Zaidi ili jupate kujua Zaidi juu ya maisha yako yajayo. Ndani yake unaweza kupata jinsi unavyoweza kushiriki katika Amani na Baraka za ufalme wa Mungu. Unaweza kuwa hapo. Omba Mungu akuongoze unaposoma na kujifunza.

Tafadhali tuambie kama ungependa kujua Zaidi kuhusu mafundisho ya Biblia na Imani za Ndugu katika Kristo. Ungependa:

  • Vipeperushi vingine katika mfululizo huu?
  • Kijitabu cha Ndugu katika Kristo?
  • Jarida la kila mwezi Habari njema?
  • Kozi ya uandishi wa posta?

Waulize wakristo walio karibu nawe au waandikie:

CHRISTADELPHIAN BIBLE MISSION c/o 404 SHAFTMOOR LANE BIRMINGHAM B28 8SZ, UK

Swahili Title
Biblia
Swahili file
Literature type