8. IBRAHIMU ANAMTOA ISAKA
“Kwa imani Ibrahimu alipopimwa alimtoa Isaka kuwa dhabihu”
Shabaha
Kuonyesha jinsi Mungu alivyompima Ibrahimu na kumwona kuwa ni mwaminifu.
Ibrahimu alikuwa na umri miaka 86, Ishmaeli alipozaliwa (Mwanzo 16:16). Lilikawa baada ya miaka 13 baadaye ndipo Mungu alimwambia Ibrahimu kwamba yeye na Sara wangepata mwana ambaye wanga mwita Isaka (Mwanzo 17:15-22). Na ilitimia kama Mungu alivyoahidi (Mwanzo 21:2-3)
Mwanzo 22:1-19
MUNGU ANAMPIMA IBRAHIMU IMANI: Mwanzo 22:1-8
Tunaweza kufikiria furaha kubwa ambayo Isaka aliyo waletea wazazi wake. Kwani walikuwa wamemngojea kwa muda mrefu, kadri walivyo mwangalia akikua, akipenda Neno la Mungu la Upendo na mtiifu wa Kweli yake, walimwona akiongezekea kukua katika utu uzima, akiwa tayari kupokea baraka za Mungu. Sisi pia tunaweza kuwa kama Isaka kwa kuamini na kumtegemea Mungu. Maana tunayo maagizo yake katika Maandiko Matakatifu yanayo tuelekeza jinsi tunavyo takiwa kuishi.
Mara nyingi, miaka ilipita na Isaka akakua na kuwa kijana, Hatimaye baada ya maisha ya Ibrahimu na Sara kufanywa yenye furaha na ukamilifu, kwa kuwepo kwa mwana wao mwadilifu na mwaminifu, Mungu alisema “umchukue mwanao, wa pekee, umpendaye, Isaka ukaenda zako mpaka nchi ya Moria ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.” (Mwanzo 22:2). Ni kipimo cha namna gani cha Imani! Hebu angalia jinsi Mungu alivyo tambua upendo wa Ibrahimu kwa Isaka anamwita “mwanao, wa pekee, umpendaye”. Jinsi gani uzito wa moyo wa Ibrahimu bila shaka alivyojisikia kufikiria kumchinja mwanaye mpendwa wa ahadi. Lakini pamoja na mapenzi makubwa kwa Isaka, mapenzi yake kwa Mungu yalikuwa ni zaidi. Alitambua ukweli Mkuu ambao sote tunapaswa kukumbuka kwamba upendo wetu kwa mtu usichukua nafasi ya kumpenda Mungu.
Hivyo Ibrahimu kwa hiari yake alitii amri ya Mungu na kwenda kumtoa mwanaye kuwa dhabihu. Alijiwa kuwa hata kama Isaka angekufa, Mungu angefufua tena kwa uzima na kwa hiyo kuitimiza ahadi ambayo ingekuja kupitia kwake kwani Mungu alikwisha sema “kwa maana katika Isaka, Uzao wako utaitwa” (Mwanzo 21:12).
Ibrahimu hakusita. Mapema asubuhi siku iliyofuata, aliamka na kufanya maandalizi yote muhimu na kuanza safari na Isaka na vijana wawili kwenda Moria umbali wa safari ya siku tatu. Walichukua kila kitu kwa ajili ya sadaka isipokuwa sadaka yenyewe. Hili ndilo lililoshangaza Isaka, aliuliza, “Baba yangu tazama moto upo na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?” (Mwanzo 22:7-8)
Kabla ya kuifikia sehemu ambayo Mungu aliiteua, Ibrahimu aliwaacha nyuma vijana hao akisema “mimi na kijana tutaenda mbele na kuabudu, kisha tutarudi tena kwenu”.
Ni dhahiri kuwa Ibrahimu alitarajia Isaka kurudi naye. Lakini je kama Isaka angefariki? Ukweli ni kuwa Ibrahimu aliamini kuwa Isaka atakufa, lakini aliona katika Isaka uzao wa ahadi na alijua kuwa Mungu angemfufua kutoka katika wafu (Waebrania 11:9) walipanda mlima pekee yao. Biblia inasema, “Walikwenda wote pamoja” Baba na mwanaye waliungana pamoja kwa nia moja.
MUNGU ANATOA SADAKA: Mwanzo 22:9-14
Madhabahu ilikuwa imetengenezwa tayari na kuni kuwekwa mahali pekee. Ibrahimu alimchukua Isaka akamfunga na kumnyanyua juu ya madhabahu. Kisha alinyoosha mkono wake na kuchukua kisu ili kumchinja mwanaye. Ghafla ukimya ukatoweka baada ya malaika wa Mungu kumwita jina lake “Ibrahimu, Ibrahimu” kwa haraka alijibu “Mimi hapa” na kuambiwa “usimnyoshee kijana, mkono wako, wala usimtendee neno, kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu” (mistari 9-12). Ibrahimu aliangalia huku na huko na alipogeuka aliona kondoo mume nyuma yake aliyefungwa katika kichaka. Mungu alileta mwenyewe sadaka, hivyo Ibrahimu alikwenda kumchukua kondoo mume na kumtoa sadaka badala ya mwanaye (mstari13).
MUNGU ANAMBARIKI IBRAHIMU MWENYE IMANI: Mwanzo 20:15-19
Malaika alimwita Ibrahimu kwa mara ya pili baada ya kumtoa sadaka mwanakondoo katika madhabahu. Alimwambia Ibrahimu kwa sababu ya Imani yako kubwa, Mungu alimwahidi:
- Kumbariki
- Atazidisha uzao wake kuwa kama mwingi kama nyota za mbinguni
- Atampatia uzao wake nguvu za kushinda na kutawala mlango wa maadui zake.
- Ataleta amani na furaha katika dunia tena “na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia”.
Ili kwamba, Abramu mtu mwaminifu na mwanaye ambaye alimpenda watakaporejea kwa wale vijana wawili walio waacha wakiwangojea na punda. Mungu alionyesha upendo wake kwao na walifurahia wote pamoja katika ahadi hizo alizoahidi. Basi ahadi hizi zote zitatimizwa wakati Yesu atakaporudi tena, maana yeye ni uzao wa Ibrahimu (Wagalatia3:16) pamoja na wale wanaofuata kielelezo chake (Wagalatia3:26-29) Abramu atafufuliwa kutoka katika wafu na atapokea baraka ya Mungu ya uzima wa milele pamoja na wale wote ambao ni waaminifu katika mambo ya Mungu (Wagalatia3:7-8)
FUNDISHO KWETU
Mungu alimpatia ahadi hizi za ajabu, Ibrahimu “kwa sababu” alisema, “Umetii sauti yangu” (22:18). Hali kadhalika tena tunajifunza somo rahisi kwamba Mungu anatutaka tumwamini na kumtii Yeye. Ni somo rahisi, lakini sisi sote tunajua ni jinsi gani ni vigumu kutii. Mambo mengine mara nyingi yanaonekana kutuvuta na hivyo kutotii. Uchaguzi unaonekana kuwa mgumu. Namna gani ilikuwa vigumu kwa Ibrahimu, kuamini kwamba ni hakika Mungu angemlinda Isaka; lakini aliamini na sisi ni lazima tuwe na imani hiyo hiyo.
Hebu natujaribu, katika mambo yote madogo tunayo ambiwa kuyafanya, tutii “Enyi watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hiyo ndiyo haki” (Waefeso 6:1). Ni kwa kuwa watiifu tunampendeza Mungu na atatukubali kuwa watoto wake.
Maelezo ya ziada
Tendo alilolifanya Ibrahimu la kumtoa sadaka Isaka lilikuwa linaelekeza kuwa baadaye Mungu angemtoa sadaka mwanae wa pekee ili kutuokoa kutoka katika dhambi na kifo. Alikufa nje kidogo ya Yerusalemu karibu na mahali palepale ambapo Isaka alilazwa katika madhabahu, Yesu alikufa lakini Mungu alimfufua kutoka katika wafu ili asife tena. (Warumi 6:9). Ufufuo wake ni dhamana ya kuwa Ibrahimu na Isaka pia watafufuliwa na Mungu atawapa yote yale aliyewaahidi.
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Jina la mwana wa Hajiri ni?
2. Je mwana wa Hajiri alikuwa ndiye uzao wa ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu?
3. Je namna gani Mungu aliipima Imani ya Ibrahimu?
4. Isaka na baba yake walisafiri kwenda wapi ili kutoa sadaka?
5. Safari ilikuwa ya umbali gani?
6. Ibrahimu alisema nini kwa wale vijana wawili waliongozana naye na Isaka?
7. Ibrahimu alitoa nini badala ya Isaka?
8. Ni nani aliyetoa sadaka hiyo?
9. Ni nani aliyekuwa uzao Mkuu ambaye katika yeye Mungu angebariki mataifa yote?
10. Ni mambo gani mawili aliyoyafanya Ibrahimu ambayo ni lazima na sisi tuyafanye?
Majibu ya Kina
1. Ibrahimu aliitwa “baba wa imani”. Elezea historia namna Mungu alivyojipima imani kuu ya Ibrahimu kwa kumwambia amweua Isaka mwanaye.
2. Kwa kuwa Ibrahimu kwa hiari yake mwenyewe angemtoa sadaka mwanaye wa pekee ampendaye, Mungu alimpatia Ibrahimu ahadi nzuri sana.
a. Ni ahadi gani hizo?
b. Ni lini Mungu atatimiza ahadi hizi kwa Ibrahimu?
Maswali ya Ziada
1. Isaka alikwenda kwa utiifu na baba yake Ibrahimu hadi Moria.
a. Ni nani aliyekuwa mkuu kuliko Isaka aliyemtii Baba yake na kwa hiari yake mwenyewe akakubali kuwa dhabihu?
b. Je Ibrahimu aliamini kuwa mwanaye Isaka angepata uhai wake tena kama angemtoa dhabihu?
c. Kwa nini alikuwa na uhakika hata kuamini ukweli huu?
