12. YUSUFU – MFUNGWA KATIKA NCHI YA KIGENI
“Yakobo akararua mavazi yake ... na akaomboleza siku nyingi kwa ajili ya mwanawe ... na akataa kutulizwa”
Shabaha
Kuonyesha jinsi Yusufu alivyouzwa katika utumwa nchini Misri Yakobo alikuwa na wana kumi na mbili, wawili kati yao walikuwa wa mke wake mpendwa,Raheli-Yusufu (likiwa na maana ya “Anayeongeza”) na Benyamini. Katika wana wake Yakobo alimpenda sana Yusufu kupita wote na alimtengenezea kanzu yenye rangi nyingi, kitendo hiki kiliwafanya ndugu zake kumwonea wivu kwani kanzu hiyo lilimfanya aonekane kutengwa na wao na kuwa kama mzaliwa wa kwanza katika familia yao. Matukio yaliyofuata baadaye yalithibitisha jambo hili, Yusufu alikuwa mcha Mungu na kijana mwaminifu, kinyume na ndugu zake ambao walikua wakiwa wanamchukia.
Mwanzo 37,39 – 40.
NDOTO ZA YUSUFU:Mwanzo 37:1-11
Siyo kwamba ni Yakobo pekee yake aliyemtenganisha Yusufu na ndugu zake, lakini pia Mungu alimchagua kumpatia ndoto maalumu. Ndugu zake wakubwa tayari walimwonea wivu, lakini yote haya yaliwafanya wasimkubali, Yusufu alieleza ndoto zake mbili kwa jamaa yake. “Tazama sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani kumbe mganda wangu ukaondoka ukasimama na tazama miganda yenu ikauzunguka mganda wangu,ikainama mbele ya mganda wangu ( mstari 7). Ndugu zake wakamdhihali na kumwambia, je, kweli wewe utatumiliki sisi” (mstari 8).Kisha tena Yusufu akawaambia ndoto yake ya pili, na tazama jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia (mstari 9).Wakati huo hata baba yake akamkemea, lakini kwa kujua kwamba alikuwa kijana mzuri na mwaminifu,Yakobo “akayatunza maneno haya”, na akayazingatia sana maneno hayo.Mungu alikuwa akiionyesha familia Yakobo kwamba Yusufu atachukua nafasi ya mzaliwa wa kwanza katika familia , lakini hakuna hata mmoja wao aliyejua namna matulio ya ajabu yatakavyotokea katika miaka ambayo ingefuaata.
YUSUFU ANAUZWA UTUMWANI KATIKA MISRI :Mwanzo 37: 12 – 28
Siku moja Yakobo alimwambia Yusufu kwenda Shekemu kuwangalia kama ndugu zake walikuwa salama.Ndugu zake walikuwa wamepeleka kondoo kungia kule.Yusufu alipofika Shekemu walikuwa wameondoka pale na hatimaye aliwakuta Dothani. Walipomwona alikiwafuata wakaanza kupanga njama dhidi yake.“Tazama yule bwana wa ndoto anakuja”,walisema, “na tumuue” Reubeni ambaye ndiye alikuwa mkubwa wao akasema “tusimwue, lakini tumweke katika shimo hili”(mistari 19-22).Akifikiria kurudi baadaye ili amwokoe Yusufu kwa ajili ya baba yake.
Ikawa Yusufu alipofika kwa nduguze wakamkata na kumvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu yenye rangi nyingi aliyoivaa wakamtwaa, wakamtupa katika shimo na shimo lilikuwa tupu na wala halikuwa na maji ndani yake (mistari 23 – 24). Baadaye, walipokuwa wanakula chakula, waliona kundi la Waishimaeli wanakuja kutoka Gileadi wakiwa na ngamia zao zilizobeba bidhaa za kuuza katika Misri. Yuda akasema, “hebu na tumwuze kwa Waishmaeli wala mikono yetu isimdhuru kwa kuwa yeye ni ndugu yetu na damu yetu”, Na kwa hiyo wakamwuza Yusufu kwa vipande vya fedha ishirini kwenda kuwa mtumwa katika nchi ya Misri. Wakati huo Yusufu alikuwa na umri yapata kama miaka 17.
YAKOBO ANASONONEKA KWA KUPOTELEWA NA YUSUFU:Mwanzo 27: 29 – 36
Reubeni aliporudi pale penye shimo Yusufu alikuwa amekwishaondoka. Mara moja alijua kwamba baba yake angefadhaika na ni Reubeni ambaye angelaumiwa na baba yake.Kwa hiyo ndugu zake walifikiria mpango mwingine.Wakachukua kanzu yenye rangi nyingi ya Yusufu na kisha wakamwua mwanakondoo na kuichovya kanzu katika damu ya mwanakondoo.Kisha wakampelekea baba yao ile kanzu, wakasema wameikuta kanzu na wakamwuliza kama ilikuwa kanzu ya Yusufu.Yakobo akaitambua kanzu mara moja kuwa ni kanzu aliyompatia mwana wake mpendwa.Kama nduguzake walivyokuwa wamepanga,Yakobo alidhani kwamba mbwa mwitu atakuwa amemwua na akaomboleza kwa siku nyingi na akakataa kutulizwa.
Wakati huo Waishimaeli walikuwa wamemwuza Yusufu kwa Potifa aliyekuwa mkuu wa jeshi la ulinzi la Misri.Katika kitambo kidogo Yusufu akawa mpendwa katika nyumba ya Potifa,akamwekwa kuwa mwangalizi wa nyumba na mali kwa sababu Potifa aliweza kutambua kuwa “BWANA alikuwa pamoja na Yusufu” (Mwanzo 39:3)
Ingawa ndugu zake walimtendea mambo ya kuchukiza,Yusufu hakuwa na mawazo mabaya katika moyo wake dhidi yao, alimwamini Mungu ingawa sasa alikuwa mtumwa katika nchi ya kigeni.
YUSUFU ANATUPWA GEREZANI:Mwanzo 30:19 – 23
Yusufu bado alikuwa na majaribu mengi ya kukabiliana nayo,hata hivyo wakat wote alitenda kwa hekima na Mungu alimbariki. Wakati mke wa Potifa alipomshitaki Yusufu kwa uongo kwa bwana wake,alitupwa gerezani.Hata hivyo,Mungu alikuwa pamoja naye na “alimwonea rehema” (mstari 21). Kama alivyopata kibali kwa Potifa, ndivyo vilevile alivyopata kibali kwa na mlinzi wa gereza ambaye alimfanya kuwa mwangalizi wa wafungwa wengine waliokuwa mle ndani. Pomoja na yote ngumu,baraka za Mungu zilimwezesha Yusufu kufanikiwa katika kila jambo alilofanya.
MNYWESHAJI NA MWOKAJI WANAOTA NDOTO: Mwanzo 40
Mmyweshaji mkuu na mwokaji mkuu wa mfalme wa Misri walimchukiza bwana wao.Farao (yaani mfalme) aliwatupa gerezani, na mle ndani walikuwa chini ya uangalizi wa Yusufu.Siku moja asubuhi Yusufu aliwaona kuwa na hali isiyo ya kawaida ya huzuni.Wakamweleza kwamba kila mmoja wao alikuwa ameota ndoto usiku ule, na hawakuelewa ilikuwa na maana gani. Yusufu akamwambia “kutafsiri si kazi ya Mungu?" Akawasihi wamwambie (mstari 8) hivyo mnyweshaji mkuu akamhadithia ndoto yake. Katika ndoto yangu nimeota niko na mzabibu mbele yangu na katika mzabibu mlikuwa na matawi matatu na kikombe cha Farao kilikuwa mikononi mwangu, nikazitwaa zabibu nikazikamulia katika kikombe cha Farao nikampa Farao mikononi mwake (v. 9 – 11)
Kisha Yusufu akamwambia maana ya hiyo ndoto, matawi matatu ni siku tatu na baada ya siku tatu Farao atakurudisha katika kazi yako kama mnyweshaji mkuu kwa Farao tena, ila unikumbuke mimi utakapopata mema,ukanifanyie fadhila, Yusufu alisema,ukanitaje kwa Farao na kunitoa katika nyumba hii (mstari14)
Mwokaji aliposikia usalama wa hatima ya mnyweshaji mkuu juu ya ndoto yake akamweleza Yusufu ndoto yake.“Na tazama ziko nyungo tatu za mikate myeupe juu ya kichwa changu na katika ungo wa juu mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao na ndege wakavila vikiwa katika ungo juu ya kichwa changu (mstari 16 – 17).Kwa hiyo Yusufu alitafsiri ndoto hiyo, nyungo tatu ni siku tatu baada ya siku tatu Farao ataamuru utundikwe juu ya mti unyongwe.
Ilikuja kutokea kama Yusufu alivyosema.Siku tatu baadaye ilikuwa siku ya kuzaliwa Farao na alimfungua na kumrejesha mnyweshaji mkuu kazi yake katika Ikulu na mwokaji alinyongwa kufanya mnyweshaji alisahau mambo aliyoambiwa na Yusufu kwa hiyo Yusufu alibakia katika gereza miaka miwili zaidi.
FUNDISHO KWETU SISI
Ni mfano gani wa ajabu wa kijanaYusufu.Kila wakati alimwamini Mungu, akistahimili mateso bila manung’uniko. Alirudisha mema kwa mabaya na kila wakati alitenda kwa busara akitambua kwamba Mungu angemwona siku nzima. Hata akiwa katika nchi ya kigeni alimkumbuka Mungu wa Israeli na aliendelea kuwa mwaminifu kwake, Kama tunaweza kuyapokea masomo haya na kuyaweka katika mioyo,Mungu atatubariki na kupatia rehema yake sasa na kutupatia urithi pamoja na Yusufu katika Ufalme
MAELEZO YA ZIADA
Yusufu ni mtu wa aina ya Bwana Yesu Kristo. Hii ina maana ya kwamba maisha ya Yusufu yalikuwa na yakituelekeza katika maisha ya Yesu Kristo katika njia nyingi za kupendeza. Hapa ni baadhi ya yale tuliyoyapata kutoka katika masomo ambayo tumekuwa tukiyafikiria.
|
1 |
Yakobo alimpenda Yusufu kuliko ndugu zake (Mwanzo 37:4) |
Mungu akasema “Huyu ni mwanangu mpendwa wangu niliyependezwa naye” (Mathayo 3:17) |
|
2. |
Ndugu zake Yusufu wakasema, “Je kweli wewe utatumili sisi” (Mwanzo 37;8) |
Wayahudi wakasema“Hatutaki huyu atutawale” (Luka 19:14) |
|
3. |
Walimchukia yeye (Mwanzo 37:87) |
Walimchukia Yesu (Yohana 15;25) |
|
4. |
Walifikiria mpango mbaya dhidi ya Yusufu (Mwanzo 37:18) |
Pia walifanya njama dhidi ya Yesu (Mathayo 24:4) |
|
5. |
Wakasema “Na tumuue” (Mwanzo 37:20) |
Walisema na tumsulubishe (Mwanzo 27;20) |
|
6. |
Yusufu alitupwa katika birika shimo na kisha akanyanyuliwa (Mwanzo 37:23 – 28) |
Yesu akafa msalabani kasha akafufuka (Mathayo 28:5-6) |
MASWALI
1. Yakobo alimpa Yusufu kanzu maalumu.
Kwa nini kitendo hiki kiliwafanya ndugu zake wamwonee wivu?
2. Ni sehemu gani Yusufu aliwakuta ndugu zake na kondoo?
3. Ni ndugu yupi aliyefanya mipango ya kumwokoa Yusufu kutoka katika shimo?
4. Ni kwa nani ndugu zake Yusufu walimwuza, na kwa kiasi gani?
5. Ni nani aliyemnunua Yusufu katika Misri?
6. Kwa nini Yusufu aliwekwa katika nafasi ya uangalizi katika nyumba ya Potifa?
7. Inakisiwa Yusufu alikuwa na umri gani alipouzwa kuwa mtumwa?
8. Ni nani aliyemtupa Yusufu kifungoni katika Misri?
9. Ni nani mwingine aliyekuwa kifungoni pamoja na Yusufu?
10. Yusufu aliwezaje kutafsiri ndoto?
11. Ni nini Yusufu alimwomba mnyweshaji mkuu kumkumbuka?
Majibu kwa Kirefu
1. Ni ndoto mbili zipi Yusufu alizoota na kwa nini ndugu zake walimchukia?
2. Eleza ndugu zake Yusufu wenye wivu walichomfanyia alipokuwa na umri upatao miaka 17
3. Mnyweshaji mkuu aliota ndoto gani na ilikuwa na maana gani?
4. Mwokaji alikuwa na ndoto gani na ilikuwa na maana gani?
Majibu ya Nyongeza
5.Kwa njia nyingi maisha ya awali ya Yusufu yalikuwa sawa na maisha ya Bwaba Yesu Kristo. Orodhesha baadhi ya njia hizo.