16. MUSA KATIKA KICHAKA KINA CHOUNGUA
“Nitakutuma sasa kwa Farao ili upate kuwatoa watu wangu hao wana wa Israeli katika nchi ya Misri"
Shabaha
Kuonyesha jinsi Mungu alivyofanya Musa amjue Jina lake kuu na kusudi lake Israeli.
Tulijifunza katika somo letu lililopita kwamba Musa alitoroka kutoka Misri akakimbilia Midiani ambako alimwoa mmoja wapo wa binti za Yethro na akatumikia miaka arobaini akiwa mchungaji akizilisha kondoo. Kwa kuwa nchi hii ilikuwa ya miinuko na vilima vya mawe,ilikuwa ni shida kwake kupata kpata chakula na maji ya kutosha kwa ajili ya kondoo wake.Kwa hiyo ingempasa kuzunguka muda mrefu akitafuta nyasi,angetumia muda mrefu sana kwa ajili ya kujali wito wake wa kusudi la Mungu na watu wake na akitafakari kwa kina kuhusu Mungu,ambaye alikuwa anamwabudu.
KICHAKA KINACHOUNGUA :Kutoka 3:1 – 6
Musa alikuwa amewapeleka kondoo wake katika mlima uitwao “Horebu” na akiwa amekaa akiwaangalia kondoo, jambo la ajabu lilitokea. Aliona kichaka kikiwaka moto lakini kilikuwa hakiteketei kwa ndimi za moto.Kichaka kilibakia na majani mabichi na kuwa kuwa kama kilivyokuwa bila ya kuonyesha tofauti ya aina yeyote ingawa kiliendelea kungu.Jambo hili kwa hakika hili lilikuwa ni la ajabu kuliona, na Musa akasonegea karibu kuona kwa nini kichaka kilikuwa hakiteketei.
Lakini kadri alivyosogea karibu, malaika alitokeza katikati ya kichaka kilichokuwa kinaungua na kumwita kwa jina lake, akasema; “Musa, Musa, usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapa unaposimama ni nchi takatifu (mstari 5).Hebu fikiria maajabu ambayo yangemfika Musa moyoni mwake! Kwa nini malaika wa Mungu aliye hai amtokee yeye? Alijificha uso wake kwa sababu aliogopa kumwangalia uso wa malaika. Hata hivyo Mungu alikuwa na kazi maalumu ambayo alitaka Musa aifanye.Utakumbuka jinsi alivyofundishwa alipokuwa Misri kuwa kiongozi wa watu.Na sasa Mungu alikuwa anakwenda kumtumia Musa kuongoza watu wake mwenyewe, taifa la Israeli kutoka katika Misri.
MALAIKA ANATOKEA NDANI YA KICHAKA KINACHOUNGUA:Kutoka 3:7-12
Malaika akaendelea kusema,“Mimi ni Mungu wa baba yako,Mungu wa Ibrahimu,Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo”(mstari 6).Na Mungu kamwe hawezi kuacha kiti chake cha enzi cha mbinguni aje aongee na mwanadamu,“kwa maana hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote”(Yohana 1:18). Mungu anapotaka kuongea na mwanadamu,anafanya hivyo kupitia malaika zake,na hili ndivyo ilivyotokea hapa (Soma Matendo ya Mtume 7:30)
Malaika aliendelea kumwambia Musa kuhusu mpango wa ajabu wa Mungu wa kuwakomboa watu wake kutoka katika utumwa katika nchi ya Misri. Akamwambia, Musa inakubidi urudi Misri na kumtaka Farao awaruhusu wana wa Israeli kuondoka.
Mapema katika miaka arobaini,Musa alijaribu kuwakomboa Waebrania kutoka katika Misri kwa njia yake mwenyewe. Na sasa anafikiria kuwa kazi ilikuwa ngumu zaidi kwake.Miaka ya katikati ilitumika vizuri.Sasa alikuwa na umri wa miaka themanini na alizidi kuwa na busara zaidi, akiwa na muda wa kufikiria udogo wake akilinganisha na ukuu wa Mungu. “Musa akamwambia Mungu, mimi ni nani hata niende kwa Farao nikawatoe wana wa IsraelI watoke Misri?” (mstari 11). Alikuwa amejifunza kuwa mnyenyekevu wa kweli.Lakini Mungu ambaye anaujua moyo ulivyo, alimtia moyo akamwambia,“Bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe; na dalili ya kuwa nimekutuma ndiyo hii” (mstari 12).Kichaka kilichokuwa kinaungua mbele ya macho yake ambacho ndimo alimokuwa malaika aliyezungumza naye ilikuwa ni dalili ya hakika kwa Musa kwamba Mungu alikuwa pamoja naye, na atawaongoza watu kutoka Misri mpaka kwenye mlima huu ili kumtumikia Mungu wao.
JINA NA SHABAHA YAKE MUNGU KUJULIKANA:Kutoka 3:13 – 15
Musa alimwuliza akitaka kujua jina lake Mungu ni nani. Katika siku zetu jina lina maana zaidi ya alama au cheo. Katika siku za kale ilikuwa tofauti.Wakati huo majina yalikuwa na maana na mara nyingi yalionyesha kazi au tabia ya mtu aliyepewa jina hilo.Kumbuka jinsi Mungu alivyobadilisha jina la Abramu (Baba mwenye kutukuka) na kuwa IbrahImu (Baba wa umati mkubwa sana)ili kusudi lake liweze kujulikana kupitia jina lake. Kwa njia hiyo hiyo jina la Yakobo lilibadilishwa na kuitwa Israeli (Mwana wa Mfalme pamoja na Mungu),kuonyesha Mungu alichokusudia kumfanyia yeye na vizazi vyake kwa siku za zijazo.
Ni sawa na Jina la Mungu ambalo ni YAHWEH. Ni neno la Kiebrania lenye maana kubwa na ya ajabu sana,katika Jina hilo tunaambiwa kusudi la Mungu kwa dunia hii na watu wanaokaa humo. (Popote tunaposoma neno BWANA limeandikwa kwa herufi kubwa katika Biblia zetu,ni hakika kwa Kiebrania ni Jina la Mungu,YAHWEH)
MAAGIZO ZAIDI KWA MUSA:Kutoka 3:16 – 22
Yahweh, Mungu wa Israeli baada ya kujitambulisha kwa Musa Jina lake kuu,alimwambia arudi Misri.Musa awakusanye pamoja wakuu wa wana wa Israeli awambie ukombozi wa ajabu unaokuja. Kisha aende kwa Farao na kumtaka awaachilie wana wa Israeli waende zao, ili waweze kumwabudu BWANA jangwani (mstari 18). Na wakati huo huo Mungu akamwambia Musa, “mfalme wa Misri hata waruhusu kuondoka nami nitanyoosha mkono wangu na kupiga Misri kwa ajabu zangu zote nitakazofanya kati yake, kisha baadaye atawapa ruhusa kwenda” (mistari19,20).
MUNGU ANAMPA MUSA ISHARA ZA AJABU:Kutoaka 4:1 – 9
Ingawa Mungu alikuwa amemwaidi Musa kuwa atakuwa pamoja naye, hata hivyo Musa bado alikuwa hana ujasiri wakwenda kwa mfalme akiwa peke yake. Tunakumbuka jinsi Musa alikimbia kutoka Misri kwa sababu ya woga. Musa aliposema hawatamwamini yeye na kwamba hakuwa msemaji mzuri kwa ajili ya kigugumizi, Mungu akasema “nami nitakuwa pamoja na kinywa chako na kukufundisha utakalolinena’’ . Haruni, ndugu yake naye aliteuliwa kwenda pamoja naye na kumsaidia kusema kwa Farao kumwambia nini ni BWANA, Mungu wao alikuwa ameagiza.
Kumsaidia Musa kuwathibitishia watu wa Israeli kwamba Mungu alikuwa amemtuma alipewa ishara tatu.
1. Fimbo ambayo iligeuka kuwa nyoka
2. Mkono ambao uligeuka kuwa na ukoma kisha ukapona.
3. Maji yaliyogeuka kuwa damu
Wakati Musa aliporudi Misri, aliwakusanya wakuu wa wana Israeli na kuwaambia mpango wa BWANA, Mungu wao. Na walipoona ishara alizompa,wakajua kuwa hakika Mungu alikuwa pamoja naye( mstari 27-31).
FUNDISHO KWETU
Musalipokikaribia kichaka kilichokuwa kinaungua,aliambiwa:“Vua viatu vyako miguuni,kwa kuwa mahali hapa usimamapo ni mahali patakatifu”.Musa alipaswa kujua kwamba ili kumkaribia Mungu ni lazima awe na utii wa hali ya juu.Mungu ni lazima atumikiwe kama anavyotuelekeza kuwa wanyenyekevu wa moyo,tukijuwa jinsi alivyo mkuu.
Ni bahati ya ajabu kuisikia sauti ya Mungu. Musa aliisikia sauti kutoka katika kichaka kilichokuwa kinaungua na hapo akasema na Mungu. Tunaweza kumsikia Mungu akizungumza nasi kila siku ikiwa tutafungua biblia yetu na kwa uangalifu na kusoma ujumbe wake, kwa njia hii tunaweza kujifunza kumjua yeye na kujua ni nini anachotaka tukifanye.
Na tusisahau kuwa Yeye ni Mungu na si mwanadamu (Hosea 11:9). Kwa hiyo masomo ya Biblia,mazungumzo kuhusu Neno la Mungu,nyimbo zetu tunazoimba pamoja na sala na zetu ni lazima vifanyike katika kicho na heshima,kwa kuwa Yeye ni Mungu mtakatifu.
MAELEZO YA NYONGEZA
Katika kitabu cha hesabu 14:21 Mungu alimwambia Musa,“Lakini hakika yangu, kama niishivyo tena kama dunia hii yote itakajazwa na utukufu wangu”. Hapo mwanzo Mungu alifanya kila kitu kizuri, lakini mwanadamu kutokana na dhambi aliviharibu vyote hivyo na katika miaka 6,000 iliyopita watu wabaya wameendelea kueneza ubaya katika dunia hii ambayo Mungu aliiumba.Wakati mmoja Mungu aliiharibu kwa gharika hata hivyo aliahidi kutoiharibu tena. Badala yake ataijaza na utukufu wake.Nahii imekuwa ndiyo shabaha ya Mungu siku zote.Kwanza ni lazima awe na watu wampendao wenye uzima wa milele na kisha ndipo atakapo ibariki dunia milele.
Mungu alipomwambia Musa kwamba Yeye jina lake ni Yahweh, Yeye alikuwa kwa neno lingine, alikuwa akielezea shabaha yake kubwa kuhusu dunia hii. Maana ya jina Yahweh ni “Yeye takayekuwako” ina maana kwamba Yeye, Mungu atajidhihirisha au kuonekana kwa watu wenye wenye imani na watiifu. Mungu aliwaita wana wa Israeli kutoka Misri ili kuwa watu wake maalumu kwa kusudi hii, lakini tutajifunza katika masomo yajayo jinsi walivyoshindwa kumpenda na kumtii Yeye. Bwana Yesu Kristo pekee, kati ya wana wote wa Mungu, ndiye aliyekuwa mkamilifu kwa utiifu kwa Baba yake, aliwaza na kutenda kama Mungu na kwa hiyo aliweza kusema,“aliyeniona mimi amemwona Baba” (Yohana 14:9).Mungu amempa yeye uzima wa milele na utukufu wake.
Ingawa wana wa Israeli walishindwa, lakini kusudi la Mungu halikushindwa. Walikuwepo wanaume na wanawake waaminifu zamani ambao katika maisha yao yote walijaribu kumpendeza Mungu.Watakawa miongoni mwa wale mwa wale watakaopata uzima wa milele na utukufu katika ufalme wa Mungu.Hata leo kupitia kwa Bwana Yesu Kristo, Mungu anaita watu kutoka katika ulimwengu kwa ajili ya Jina lake (Matendo ya Mitume 15:14). Sisi tunaolisoma neno lake kila siku na kutii wito wake tutapata thawabu ile ile Kristo atakaporudi. Hapo ndipo Mungu hakika ataonekana katika kusanyiko kuu la watakatifu na mwishowe nchi yote itajawa na utukufu wake.
Ni ahadi ya ajabu ilioje ailiyomo katika jina la Mungu! Hebu na tujitahidi kwa bidii kila siku kujifunza njia zake kwa ili tuweze kuhesabiwa kuwa kati ya kundi kuu la watakatifu wakati unaokuja karibuni
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Musa alikuwa anafanya nini karibu na mlima Horebu?
2. Musa aliona nini cha ajabu katika mlima Horebu?
3. Kadri Musa alivyokisogelea kichaka sauti ilisema nini kwa Musa?
4. Je malaika alimwambia Musa,Mungu angependa afanye nini?
5. Je malaika alisema jina la ajabu la Mungu nani?
6. Ni nani angefuatana na Musa kumsaidia kuongea?
7. Je ni ahadi gani kuu ya Mungu kwa wale wanaoonyesha katika maisha yao kwamba wao ni mali ya Mungu?.
Majibu kwa Kina
Baada ya Musa kukimbia kutoka Misri alikwenda Midiani.
1. Eleza nini kilichotokea siku moja wakati Musa alipokuwa akichunga kondoo katika mlima Horebu
2. Je ni ujumbe gani malaika wa Mungu aliompa Musa katika kichaka kilichokuwa kinaungua?
3. Ni ishara zipi Mungu alizompa Musa kuwaonyesha wana wa Israeli kule Misri kwamba Mungu mmoja wa kweli alimtuma kuwakomboa katika utumwa?
Majibu ya Nyongeza
4. Ni jina gani Mungu ambalo Musa alimwagizwa kuwambia wana wa Israeli na lina maana gani?
5. Je Mungu alitangaza nini kuwa ndiyo shabaha yake kwa dunia hii?
6. Iwapo tunataka kuwa wana wa Mungu wa frgkweli, na kuwa na utukufu wake wa asili na jina, inatupasa tuishi vipi sasa?