CSSA 1-1-17 - GOD SENDS PLAGUES ON EGYPT

Swahili

17. MUNGU ANATUMA MAPIGO YA TAUNI NDANI YA MISRI

"Na wa misri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA hapo nitakapounyosha mkono wangu juu Misri."

 

Shabaha:

Kuonyesha jinsi Mungu alivyotumia nguvu zake kuu kuwakomboa wateule wake, na hivyo kuonyesha kwamba yeye pekee ndiye wa kweli na Mungu aliye hai. Watu walihamasika sana na kufikiria kuwa si muda mrefu, wangekuwa huru.

 

Misri lilikuwa taifa kubwa na lenye nguvu, lakini miungu yao ilikuwa si kitu kabisa- miungu ya mbao na mawe haikuwa na uwezo! Kuna Mungu mmoja wa kweli na yeye alitaka wamjue nguvu zake na kutambua ukuu wake na hasira yake ya kutisha.

 

Kwa hiyo BWANA, Mungu wa waebrania ambaye alikuwa ameona jinsi wamisri walivyowatenda kwa ukatili watu wake angewatoa kutoka Misri na kwa hukumu kubwa (Kutoka 6:6).

 

Kutoka 5 hadi 10; Matendo ya Mitume 7:36; Zaburi 78:43 – 52.

 

MUSA NA HARUNI MBELE YA FARAO: Kutoka 5 na 6

Wakati ulikuwa umefika kwa Musa na Haruni kuzungumza neno la Mungu kwa Farao."BWANA, Mungu wa Israeli asema hivi, wape watu wangu ruhusa waende jangwani ili kunifanyia sikukuu ". Farao alishangazwa na ombi hili la ujasiri. Alisema, BWANA,ni nani,hata niitii i sauti yake na kuwaruhusu Israeli waende? Mimi simjui BWANA, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao (Kutoka 5:1 – 2).

 

Ilikuwa ni sawa alikuwa hamjui Mungu wa waisraeli, lakini si kitambo kirefu angemjua, na vile vile wamisri wote pia wangemjua. Musa na Haruni walifukuzwa kwa hasira na wamisri wakaongeza mzigo mzito kwa waisraeli, sasa walitakiwa kufyatua matofali idadi ile ile kila siku kama walivyokuwa wakifanya kabla na badala ya kuletewa nyasi za kufyatulia tofali kama walivyopewa mwanzo, iliwabidi waende wajitafutie nyasi wao wenyewe. Ilionekana sasa kwa waisraeli kwamba tangu Musa kuingilia ,mambo yalizidi kuwa magumu kuliko hapo mwanzo na kumlaumu (Musa). Lakini Mungu alisema na Musa kumtia moyo (Kutoka 6:1 – 9), Musa na Haruni walikwenda tena ka Farao(Kutoka 7:10 – 13) .Fimbo ilitupwa chini mbele yake na watu wake wenye hekima na wachawi wake, na mara ikawa nyoka, lakini fimbo ya Haruni ilizimeza fimbo nyingine zote. Pamoja na yote haya moyo wa Farao ukazidi kuwa mgumu kama Mungu alivyo kuwa anajua itakuwa. Muda ulikuwa umefika kwa BWANA kuonyesha uwezo wake mkuu kwa Wamisri na Musa aliagizwa kwenda kwa Farao siku iliyofuata asubuhi asubuhi.

 

MARADHI YA TAUNI :Kutoka 7 mpaka 10

Ukweli kulikuwa na mapigo makuu makubwa na ya kutisha kumi ya maradhi ya tauni ambayo Mungu aliyapeleka katika Misri. Hapa tutayataja tisa kati ya hayo.La kumi na la kutisha zaidi lilitokea usiku ambapo Mungu aliwatoa wana wa Israeli kutoka katika Misri, tutasoma habari yake katika somo linalofuata.

 

1. MAJI KUWA DAMU:Kutoka 7;14 – 25

Musa akasema tena na Farao; “BWANA, Mungu wa Waebrania amenituma nije kwako kusema, Wape watu ruhusa ili wapate kunitumikia jangwani nawe tazama hutasikia hata sasa”. Kisha Musa akayageuza maji mto Nile kuwa damu na hivyo samaki walikufa na kukatokea harufu ya kutisha hata madimbwi na mabwawa ya maji yakageuka kuwa damu, wachawi wakaigiza kama alivyofanya Musa hata kusababisha baadhi ya visima kuonekana kama damu, mara hii tena Farao akataa kumsikiliza Musa.

 

2. VYULA : Kutoka 8:1 – 15

Musa na Haruni walikwenda tena wakiwa na ombi lile lile, “Waruhusu watu wangu waondoke”.Wakati Farao anayapuuzia maneno ya Mungu, Haruni alinyoosha mara moja fimbo yake juu ya vijito na mito na kusababisha vyura kutokeza katika nchi ya Misri,walivamia katika nyumba zao na walikuwa kila mahali; katika vitanda vyao, katika majiko yao na mabeseni ya kunawia. Wachawi waliigiza tena yale yaliyotendeka- lakini hawakuweza kuvifanya vyura waondoke.

 

Kwa hiyo Farao, alimwagiza Musa ili kumwomba BWANA, Mungu awaondoe vyura “Nami nitawapa ruhusu watu waondoke” m 8) vyura walikufa siku iliyofuata, Farao alibadilisha mawazo yake na kufanya moyo wake kuwa mgumu zaidi.

 

3.MAKUNDI YA CHAWA (Kutoka 8:16 – 19)

Pigo hili la kutisha lilikuja katika Misri baada ya Musa kumwamwagiza Haruni kunyoosha fimbo yake na kuyapiga “mavumbi ya nchi”.Na alipofanya hivyo,wakatokea chawa. Na wachawi hawakuweza kuingiza muujiza huu na chawa waliweza kutambaa juu kwa kila mwanadamu na kila wanyama. Wachawi wakapiga kelele “jambo hili ni chanda cha Mungu” (mstari 19). Hawakuweza kudanganya tena, Hila zao hazikuweza kulingana na uwezo wa Mungu, hata hivyo moyo wake Farao ukawa mgumu asiwasikilize (yaani Musa na Haruni) vile vile kama BWANA alivyonena (mstari 19).

 

Kwa hiyo Mungu aliweza kutuma mapigo katika Misri yote, kwa wamisri wote hali kadhalika kwa wana wa Israeli pia. Hata haikuwahi kutokea wakati wowote kabla kwa wana wa Israeli kuona uwezo wa Mungu kwa njia kama hiyo na vile vile waliweza kujifunza ukuu wake na kuamini.

 

Na baada ya mapigo haya matatu, mda ukafika kwa wote kutambua kwamba Mungu ameweka tofauti kati ya wana wa Israeli na Wamisri. Kwa hiyo Musa alisema kamba siku inayofuata Mungu atatuma mainzi wengi kueneza maradhi katika Misri isipokuwa nchi ya Gosheni ambako wana wa Israel waliishi.

 

4. Mainzi (Kutoka 8:20 – 32)

Kundi kubwa la mainzi lilijaa nchi yote ya Misri. Mainzi yalikuwa katika nyumba zao na walitambaa katika watu wote na waliijaza nchi nzima, jinsi gani watu walivyochukia! Hatimaye, Farao alionekana kutubu.Alimwita Musa na kumwagiza , “Mimi nitawapa ruhusa ili mumchinjie dhabihu BWANA, Mungu wenu ndani ya nchi hii”. Musa alimkumbusha Farao kwamba Mungu alikuwa amesema ni lazima waondoke Misri.Kwa hiyo Farao akasema “nitawaruhusu mwondoke …lakini hamtakwenda mbali sana” (mstari.28). Kwa hiyo Musa alimwomba Mungu kuyaondoa mainzi na ikafanyika.“Na moyo wa Farao ukawa mgumu tena na hakuweza kuwaruhusu waondoke”.

 

MKONO WA BWANA JUU YA WANYAMA (Kutoka 9:1 – 7)

Huu ulikuwa ugonjwa ambao ungeambukiza kutoka kwa mnyama mmoja hadi mwingine. Wanyama walipata shida ya kupumua na kwa kawaida walikufa, wanayama wa wana wa Israeli katika nchi ya Gosheni hawakuugua ugonjwa huu wa kutisha - hii ilikuwa ni ishara ya Mungu ya kuwalinda wateule wake na mali zao. Farao aliwatuma watumishi wake kwenda Gosheni kuulizia, na hakukuwa na mnyama yeyote wa wana wa Israeli aliyekufa, “Lakini moyo wa Farao ulikuwa mzito, wala hakuwapa hao watu ruhusa waende zao” (mstari 7).

 

Majipu kwa Mwanadamu na Mnyama (Kutoka 9:8 – 12). Kisha Musa akamwagiza Haruni kuchukua majivu ya tanuru na kuyanyunyiza kuelekeza juu mbinguni mbele ya macho ya Farao , majivu yaligeuka kuwa mavumbi na yalipokuwa yanaanguka, yalisababisha majipu kutumbuka juu ya kila mwanadamu na mnyama.Hata wachawi hawakuweza kusimama mbele ya Musa kwa sababu ya pigo hili la majipu.Hata hivyo moyo wa Farao ulikuwa mzito na “asiwasikilize”(mstari 12).

 

Mvua ya Mawe (Kutoka 9:18 – 35). Musa aliamriwa kusimama mbele ya Farao na kumwambia kwamba siku inayofuata itatokea mvua kubwa ya mawe na kuharibu kila mwanadamu na mnyama ambaye hatakuwa ndani ya nyumba lililowazi.Kwa wakati huu baadhi ya Wamisri walikuwa wamejifunza kumwogopa Mungu wa Israeli kwa hiyo waliwaamru watumishi wao kubakia nyumbani. Musa aliponyoosha fimbo, Mungu alituma ngurumo,mvua ya mawena radi naikamwua kila mwanadamu na mnyama, kuharibu mazao na miti.Lakini hapakuwa na mvua ya mawe katika Gosheni. Farao akamwita Musa na kusema, “Nimetenda dhambi, BWANA ni mwenye haki (kwa kuwa inatosha)… nami nitawapa ruhusa mwende zenu” (Kutoka 9:27 – 28).Lakini Farao, mara baada ya kuona mvua za mawe zimekoma, moyo ukawa ni mgumu (mstari 35) naye hakuwapa wana wa Israeli ruhusa waende zao.

 

NZIGE (Kutoka 10:1 – 20)

Mara nyingine tena Musa alikwenda mbele ya Farao na kumwambia kwamba BWANA,atapeleka pigo lingine kama angeendelea kuwa na kiburi na udanganyifu. Farao alimwambia Musa na Haruni kwamba watu wangeweza kwenda kumwabudu Mungu wao jangwani, lakini watoto nilazima wabakie, Musa alikuwa imara, wote lazima waende ikiwa ni pamoja na watoto na wazee, la sivyo nchi itaenezwa na nzige ambao watakula kila kilichokuwa kimebaki chenye majani mabichi na mazao yaliyo kuwa yamebaki na miti. Farao alikasilika na kuwafukuza. Kisa Musa alinyoosha fimbo yake na upepo wa mashariki ukawaleta nzige ambao walikula vyote vilivyokuwa vimebakia baada ya mvua ya mawe. Kwa haraka Farao alimwita Musa “Nimemkosea BWANA, Mungu wenu na ninyi pia, basi sasa nawasihi nisameheni dhambi yangu mara hii moja tu, mkamwambie BWANA, Mungu wenu aniondolee kifo hiki tu” (mstari16 – 17) Mungu aliwaondoa nzige kwa upepo mkubwa kuelekea magharibi na nzige wote waliswagwa ndani ya bahari nyekundu. Bado tena moyo wa Farao ulikuwa mgumu na hakuweza kuwaruhusu watu hao kuondoka.

 

GIZA NENE (Kutoka 10:21 – 29)

Mungu alimwambia Musa kunyoosha mkono wake kuelekeza mbinguni ili giza zito lije liifunike nchi ya Misri yote, giza nene ambalo lingewafanya watu wa Misri wasiweze kuonana, giza nene ambalo watu watapapasa papasa gizani (mstari 21). Hata hivyo katika nchi ya Gosheni wana wa Israeli kulikuwa na nuru. Farao akamwita Musa na kumwambia, haya nendeni mkamtumikie BWANA, kondoo zenu na ng’ombe zenu tu na waachwe(mstari 24). Farao alikuwa amechukia na kumfukuza Musa atoke mbele yake akisema hatauona tena uso wake ,naye Musa akamjibu, “Umenena vema, mimi sitakuangali uso wako tena” (mstari 29)

 

Kwa hiyo Mungu alileta mapigo hayo makubwa na ya kutisha juu ya Misri kuonyesha nguvu zake juu ya miungu ya Misri- “na tena ya kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote” (Kutoka 9:16). Lilikuwepo pigo moja linalokuja baya kuliko yote, kwani Farao asingekuwa na njia nyingine isipokuwa kutubu.Kilichokuja kutokea baadaye kilifanya mataifa yote ya karibu kumwogopa BWANA na kutetemeka (soma Yoshua 2:9 – 11).

 

FUNDISHO KWETU

Katika habari hii tunajifunza masomo mawili muhimu: -

a. tunahitaji kujinyenyekeza mbele ya Mungu na

b. tunahitaji kujitenga na dunia

 

Katika Methali 6:17 tunaambiwa kuwa Mungu anachukia “macho ya kiburi na ulimi wa uongo” Ndivyo alivyokuwa Farao. Wana wa Israeli iliwapasa kujinyenyekeza na kumwamini Mungu ili kuwakomboa. Kwa hiyo inatupasa tumwamini Mungu wa kweli na kutii amri zake, tukifanya hayo ametuahidi kutuokoa hata katika mauti. Kwanza,inatupasa tuishi maisha ambayo ni tofauti na wale wale wanaotuzunguka wasiomjua Mungu na kuishi maisha ya imani na utiifu – kwani Mungu ataiadhibu dunia hii yenye maovu kama alivyowaadhibu Wamisri hapo zamani .Na kwa hiyo tunamngojea Bwana Yesu Kristo kurudi kuja kuyahukumu mataifa na kutuokoa kwa uweza wake mkuu

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Tabia ya Mungu mwenyewe, kama alivyojihirisha kwetu katika maandiko, inamwonyesha kuwa ni mwenye haki na mwenye huruma. Ni Mungu mwenye rehema kwa watakatifu wake lakini anatisha kwa wale wanaomcha Mungu ( soma Kutoka 34:6 – 7). Hukumu kuu ya Mungu ilikuja juu ya Misri, lakini Waebrania wakapata rehema ya Mungu. Hata hivyo baadhi ya Wamisri walipona wakaamini .Kwa hao Mungu aliwapa njia ya kujiokoa kwa mfano wakati wa mvua ya mawe na hata wengine walijiunga na wana wa Israeli na wakaondoka Misri, na hali kadhalika hata siku hizi “Yeye aminiye na kubatizwa ataokoka” (Marko 16;16) .Bwana Yesu Kristo ndiye mwokozi mkuu.

 

Ni kwa njia ya ubatizo kwa jina lake tu ndipo tutaweza kuokolewa, Mungu amekwisha kuuonya ulimwengu kuhusu hukumu atakazozileta juu ya mataifa, ataonyesha rehema kwa wale tu wanaosikia na kuamini neno lake.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

1. Kwa nini Musa na Haruni walikwenda kwa Farao?

2. Ni kwa jinsi gani fimbo ya Haruni ilionyesha kuwa na uwezo kuliko fimbo za wachawi?

3. Kwa nini Mungu aliwapiga kwa tauni wamisri?

4. Kwa nini waebrania pia walipigwa yale mapigo matatu ya kwanza?

5. Wakati wa pigo la mvua ya mawe,ni kwa jinsi gani baadhi ya Wamisri walionyesha kuamini neno la Mungu?

6. Farao alikuwa mtu wa namna gani?

 

Majibu ya Kina

1. Musa na Haruni walimwomba Farao awaruhusu wana wa Israeli waende jangwani kumtumikia Mungu wao

a. Kwa nini Mungu alitaka kuwatoa watu wake Misri?

b. Nini kilitokea baraza wakati Musa na Haruni walipokwenda kwa Farao na Haruni kutupa fimbo yake

2. Eleza unavyojua kuhusu mapigo ya tauni ambayo Mungu aliipiga Misri (ukiacha lile pigo la mwisho la kutisha)

3. Tunajifunza nini kutokana mapigo kwa Misri?

 

 

 

Swahili Title
017 MUNGU ANATUMA MAPIGO YA TAUNI NDANI YA MISRI
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type