18. WANA WAISRAELI WANAIKUMBUKA PASAKA NA KUVUKA BAHARI SHAMU
"BWANA akawapiga walizaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri ... ... lakini akawaongoza watu wake wakaondoke moja kwa moja kama kondoo"
Shabaha
Kuonyesha jinsi Mungu alivyowakomboa watu wake kutoka katika Misri. “Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu” (Kutoka 4;22,23).Haya yalikuwa ni maneno ya Mungu ambayo Musa aliamriwa kuyasema kwa Farao; na haya yalikuwa nyongeza ya maneno ya kutisha “Nawe umekataa kumpa ruhusa aende, angalia basi mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako! (Kutoka 4:22 – 23).Na ukuu wa BWANA, Mungu wa Musa ulionekana kwa kila mmoja baada mwingine na wale walioitwa miungu wa wamisri walishindwa katika matukio ya mapigo tisa. Lakini Farao alikuwa mwnye kiburi sana na hakukufanya kama Mungu alivyosema, moyo wake bado ulikuwo mgumu na kusema asingeweza kuonana na Musa uso kwa uso tena. Hata hivyo,kwa muda mfupi angeuona mkono wa BWANA kwa njia ya kutisha zaidi katika pigo la mwisho la kutisha, alikuwa amekaribia kumpoteza mwanawe mzaliwa wa kwanza, mrithi wa utawala wa Misri. Baada ya hayo kutokea, Farao angeamuru wana wa Israeli kuondoka. (Kutoka 11;1) kutoka 12:1 – 14, 29 – 39; 13:17 – 22; 14.
MAANDALIZI YA PASAKA: (Kutoka 12:1 – 14)
Muda wa kukombolewa kwa wana wa Israeli kutoka Misri ulikuwa umefika na Waebrania walikuwa wamepewa maagizo muhimu ya kuzingatia
1. Iliwapasa kudai kama neno azima linavyomaanisha, vyombo vya fedha na vya dhahabu, na nguo na chochote ambacho wangekihitaji kwa ajili ya safari.Wamisri walikubali kuwapa chochote walichokihitaji kwa kuwa walitamani kuwaona waebrania wakiondoka. Kwa njia hii wana wa Israeli walipata malipo kidogo kwa miaka mingi ya utumwa wao (mistari 35, 36).
2. Mwezi wa Abibu ulikuwa uwe ndiyo mwezi wa kwanza wa mwaka mpya kwa wana wa Israeli, kwa sababu ndipo walipokuwa wanaanza maisha mapya kabisa (Kutoka 12:2). Katika siku ya kumi ya mwezi huu, kila nyumba itenge mwanakondoo mmoja asiyekuwa na doa lolote wala kilema chochote. Alitengwa peke yake hadi siku ya kumi na nne atakapochinjwa, wakati wa jioni, au kwa maana ya kiebrania “kati ya jioni mbili kati ya 9 na 12 jioni (mistari 2 – 6)
3. Wala msivunje mfupa wake wowote wakati wa kumla.
4. Damu yake ikingwe kwenye bakuli na kisha damu hiyo wanyunyiziwe watu na miimo miwili ya mlango kwa kutumia tawi la mti wa hisopo(mstari 22).
5. Nyama hiyo kondoo aliyechinjwa ilichomwa yote katika moto (mstari 8).
6. Ilipofika jioni ambayo ilikuwa ndiyo mwanzo wa siku ya kumi na nne ya mwezi wa Abibu familia nzima ilibakia ndani ya nyumba ambayo mihili yake ya mlango ilikuwa imepakwa damu(mstari 7). Familia zilizokuwa na watu wachache walikusanyika katika nyumba moja.
7. Wakiwa wamevaa viatu vyao miguuni na fimbo mikononi mwao tayari kwa kuondoka wakati wowote, ilikuwa wamle kondoo kwa haraka pamoja na mkate usiotiwa chachu pamoja na mboga zenye uchungu (mistari 8,11).
8. Wasisaze nyama yoyote ya kondoo hadi asubuhi,na nyama yoyote iliyokuwa imebakia na chochote kilichomwa na kuteketezwa katika moto (mstari 10).
Kuendelea kutunza sikukuu hii kwa taratibu zake zote ilikuwa na maana ya ukombozi kutoka katika kifo ambacho kingesababishwa na malaika wa Mungu wa mauti, kwani katika usiku huu, malaika wa Mungu angepita katika nchi yote ya Misri kuua kila mzaliwa wa kwanza wa kila nyumba ambayo haikunyunyuziwa damu. Baadhi ya wamisri walijihifadhi katika nyumba zilizonyunyuziwa damu wakati malaika wa kifo walipopita, lakini nyama ile ilikuwa iliwe na waisraeli tu (Kutoka 12:43) .Pasaka ilikuwa ni jina lililopewa siku hii ya sikukuu muhimu ambayo Mungu aliamuru kwamba itunzwe kila mwaka kwa namna hiyo hiyo kama kumbukumbu au ukumbusho wa ukombozi wa wana wa Israeli kutoka Misri. (Kutoka 12;14)
USIKU MKUU WA PASAKA (Kutoka 12:29 – 39)
Maneno ya mwisho ya Musa kwa Farao yalitoka kwa Mungu- onyo la kutisha kutokana na pigo la mwisho la kutisha ambalo lingekuja kuipiga Misri (Kutoka 11:4 – 8). Kisha Musa alikwenda kwa Farao akiwa mwenye hasira kubwa. Usiku huu utakuwa ni usiku wa kutisha ambapo kila mzaliwa wa kwanza katika Misri atakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza kiume wa Farao hadi mzaliwa wa kwanza wa kila mtumishi au mfungwa, na hata kila mzaliwa wa kwanza wa kila mifugo. Isipokuwa tu katika nyumba ya wana wa Israeli hakuna ambaye angekufa,ili kwamba sasa Farao apate kujua “kwamba BWANA,amewatenganisha wamisri na wana wa Israeli” (Kutoka 11:7).
Usiku wa manane malaika akiwa na amri ya Mungu akaenda Misri na kukawa kilio kikuu katika nchi yote,kwa maana hakukuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu .Ndipo Farao na watumishi wake wakamwita Musa usiku huo wakamwambia, “Ondokeni,toleni katika watu wangu,ninyi na na wana wa Israeli wote enendeni,kamtumikieni BWANA kama mlivyosema” (Kutoka 12:31).Wamisri kwa haraka wakawahimiza wanawa Israeli kuondoka kwa kuwa waliogopa sana kuwa na wao wote wanaweza wakafa.Kwa hiyo Farao akatambua kuwa BWANA, Mungu wa wana wa Israeli ndiye Mungu wa kweli na wa pekee.(soma Kutoka 5:2)
WANA WA ISRAELI WANAONDOKA MISRI: Kutoka 13:17 – 19
Wana wa Israeli hawakuhitaji kuhimizwa, kwa haraka walikusanya mali zao chache na kuondoka. Umati mkubwa wa watu wapatao wanaume 600,000 bila ya wanawake na watoto kuhesabiwa na ng’ombe na mifugo walianza safari yao kwenda Nchi ya Ahadi. Baadhi ya wamisri ambao walikuwa wamejifunza kumwogopa Mungu wa Israeli waliondoka pamoja nao, kwani sasa walijua kwamba Mungu wa Israeli alikuwa ndigye Mungu wa kweli.
Musa alikuwa bado anayo kazi maalumu moja zaidi ya kufanya, Yusufu alikuwa amekwisha kuwapiza ndugu zake miaka mingi iliyopita waahidi kwamba mifupa yake wataichukua kutoka Misri, na kuipeleka wakati Mungu atakapowakomboa.Kwa hiyo Musa akaamuru jambo hili litekelezwe, hakika Mungu alitimiza ahadi yake kama vile Yusufu alivyokuwa amesema (Kutoka 13:19 (Angalia somo la 14)
WINGU LA KUWAONGOZA Kutoka 13:20 – 22, 14:1 – 10
Malaika wa Mungu akiwa ndani ya wingu alitangulia mbele ya umati mkubwa wa watu kuwaonyesha njia. Wakati wa usiku wingu moto mkubwa ulikuwemo ndani ya wingu wapate nuru ili waone njia yao, na ikawa wakati wa mchana wingu lile likawaangulia mbele yao na likawakinga joto la jua(Fuatilia safari yao katika ramani ya biblia).Kwanza waliweka kambi yao Sukothi, ambako walipumzika wakatengeneza kambi yao kwa matawi ya miti. Kambi yao iliyofuata ilikuwa Ethamu ambayo ilikuwa kando ya jangwa na kisha kuelekea hadi Pi – hairothi kilometa 24.Eneo hili lilikuwa pweke,likiwa limezungukwa na milima,Ilikuwa katika eneo hili ambapo walielewa kwamba Farao alikuwa amechagua magari ya farasi 600,magari yote ya farasi ya Misri yalikuwa nyuma yao.
ISRAELI WANAVUKA BAHARI YA SHAMU: Kutoka 14:1 – 31
Waliogopa sana,ndipo wana wa Israeli wakamgeukia Musa “Je kwa sababu hapakuwa na makaburi katika nchi ya Misri umetutoa huko ili tufe jangwani?” (mstari.11).Haikuwepo sehemu ya kukimbilia, walikuwa wamezingingirwhata isiwepo sehemu ya kukimbilia.Farao alikuwa nyuma yao milima ilikuwa imezunguka sehemu zote na bahari ya Shamu ilikuwa mbele yao.
Lakini Mungu alikuwa anajua nini kitatokea, alikuwa anawapima ili kuwafundisha waweze kumtumainia yeye, Musa akawaambia watu “Msiogope, simameni tu mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo…BWANA atawapigania,nanyi mtanyamaza kimya” (Kutoka14:13,14) Kisha nguzo ya wingu ikaondoka ikasimama nyuma wana wa Israeli na kusababisha giza nene kama usiku kwa upande wa wamisri, lakini kwa Israeli kulikuwa na mwanga. Wakati huo Musa akawa amenyosha fimbo yake juu ya bahari Mungu akatuma upepo wa nguvu kutoka mashariki usiku kucha ambao ulivuma juu ya maji ya bahari ya Shamu,upepo ukaigawa bahari na kufanya njia ya kuvuka upande wa pili pakiwa pakavu.Watu wa Mungu wakaweza kuvuka kwa usalama kwenda upande wa pili “nayo maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kuume na mkono wa kushoto” (mstari 22). Wamisri walipojaribu kuwafuata malaika wa Mungu waliyaondoa magurudumu ya magari! Wana wa Israeli, sasa walikuwa salama,tena mbali upande pili na Mungu akamwambia Musa kunyosha fimbo yake mara moja tena.Na aliponyosha fimbo yake,Mungu akayarudisha maji yakawafunika wamisri ambao wakati huo walikuwa wamefika katikati ya bahari na wote wakazama. Kwa kitendo hiki cha mwisho alichokifanya juu ya wamisri,nguvu zote za wamisri ziliangamizwa na wana wa Israeli wakawa washindi.Ndipo Musa na Miriamu na watu wote waliimba juu ya ushindi wa ajabu ambao Mungu aliwapatia siku ile na walimsifu Mungu kwa wema wake wote.
FUNDISHO KWETU
“BWANA, atawapigania ninyi na ninyi mtakuwa kimya katika amani”
Maneno haya ya Musa yanatupatia somo muhimu sana, Mungu huokoa.Ni wajibu wetu kuamini na kutii. Tunaona jinsi Mungu alivyomwezesha Musa kuwa mkombozi; jinsi Mungu alivyowapatia wana wa Israeli njia ya wokovu, wakati malaika wa mauti alipopita na tunaona jinsi Mungu alivyoifungua bahari ya Shamu ili kuwaokoa wana wa Israeli na wakati huo kuwaangamiza wamisri “Kwa imani wakapita kati ya bahari ya shamu kama katika nchi kavu” (Waebr 11:29)
Mungu anataka tujifunze katika maisha yetu ya kila siku kumwani yeye,kama jinsi wana wa Israeli walivyojifunza somo hilo.
MAELEZO YA NYONGEZA
Wana wa Israeli wakatoka Misri wakapitia katika Bahari ya Shamu kwenda kwenye maisha mapya ng’ambo ya pili wakaenda Nchi ya Ahadi. Kuvuka huku katika bahari ya Shamu Paulo anaita kuwa ni namna ya ubatizo “Baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari, wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari”. (1Wakorintho 10:1 – 2).
Kama ilivyo ubatizo kuwa ni “kuzika ndani ya maji” au kuficha kisionekane ndani ya wingu na kuficha kwakutumia ukuta wa maji pande zote.Hivyo wamisri walikuwa wakiwakilisha njia zao za za maisha ya kale, ambapo hawakumtumikia Mungu kwa usahihi kwa sababu ya kutokujua sheria za Mungu.Wakati Musa,mwokozi wao alipowaendea walijifunzaama mtu ambaye angewaongoza kwenye uhuru. Waliona uwezo wa nguvu za Mungu ukijionyesha katika maradhi ya tauni na kuamini katika yeye kwa hiyo walivuka Bahari ya shamu wakiamini (Waebrania 11:29)
Maelezo haya ni kama ubatizo; mtu anapomwamini Mungu na kumwamini yeye anabatizwa na kuweka kando namna ya maisha yake ya awali. Kama wana wa Israeli walipoanza maisha mapya ng’ambo ya bahari hivyo hivyo mtu aliyebatizwa “huenenda katika upya wa uzima” (Warumi 6:4).Anakuwa ndani ya Kristo na ni lazima atembee kulingana na jina la Kristo ambalo analichukua. Kila mwisraeli alipaswa kushiriki pasaka ya mwanakondoo katika Misri kabla ya kuwa huru kuondoka. Kristo ndiye “mwanakondoo wa pasaka yetu”(1Wakorintho 5:7). Njia pekee tunayoweza kuila pasaka hii ni kwa njia ya ubatizo katika jina lake.
MASWALI
Majibu mafupi
1. Je, pigo la kutisha la kumi lililoipiga Misri ni lipi?
2. Ni nini waisraeli walichotaka wapewe na Wamisri?
3. Ni katika mwezi upi pasaka ilifanyika?
4. Ni ni nini kingefanyika kupitia mwanakondoo wa pasaka ?
5. Walimla mwanakondoo wakiwa wapi?
6. Nini kilitokea usiku wa manane wa pasaka?
7. Farao alijifunza nini kuhusu BWANA?
8. Musa aliwaambia nini watu wakati walipokuwa wakifikiri kwamba Farao atawaua wote
9. Ni nani aliyekuwa mkombozi wa wana wa Israeli?
Majibu ya Kina.
1. Eleza yote kwa kadri unavyojua kuhusu maagizo walipewa wana wa Israeli ili waweze
kupona wakati wa malaika wa kifo atakapopita juu.
2. Namna gani mwishowe Mungu alimwangamiza Farao na kuwaokoa wana wa Israeli kutoka katika mikono
dhalimu ya Farao?
3. Namna gani Mungu alilivyoliongoza taifa la Israeli katika safari yao walipoondoka Misri?
4. Eleza unavyoelewa juu ya kuvuka kwa bahari ya Shamu.
Majibu ya Nyongeza
5. Mtume Paulo alisema kupita katika Bahari ya Shamu anafananisha na nini?