CSSA 1-1-20 - ISRAEL AT MT

Swahili

20. ISRAELI KATIKA MLIMA SINAI

"Wewe ukashuka mlima Sinai na ukawapa hukumu za haki na sheria za kweli, maagizo mema na amri"

 

Shabaha

Ni kuonyesha jinsi Mungu alivyowapatia sheria na amri zake wana wa Israeli, watu wake aliwachagua.Mungu akawa amewakomboa wana wa Israeli kutoka Misri na kuwaongoza kwa mud awa miezi mitatu katika jangwa hadi Mlima Sinai, kama alivyokuwa ameshamwahidi Musa mwanzo (Kutoka 12). Utakumbuka kwamba waisraeli walikuwa watumwa katika nchi ya Misri na karibu wengi wao yamkini walikuwa na ujuzi kidogo au hawakuwa nao kabisa kuhusu Mungu na jinsi gani ambavyo Mungu alitaka waishi. Ilikuwa ni mhimu kwa wateule kufahamu njia ya Mungu,maana Mungu alisema, “nanyi mtakuwa kwangu ufalme na makuhani na taifa takatifu”

(Kutoka 19:6)

 

Na ili wana wa Israeli waweze kustahili kuwa ufalme wa Mungu ilikuwa ni lazima wajue mema na mabaya.Kwa hiyo ilikuwa ni lazima kuwapatia sheria ili kuwaonyesha njia ya Mungu ili waweze kuzitii na kumpendeza.Na sheria hizi pia ziliwaelekeza namna kosa lilivyokuwa kwa kumtenda Mungu dhambi.

Kutoka 19 na 20

 

ISRAELI KATIKA MLIMA SINAI:Kutoka19:1-15

Ikawa watu walipofika Sinai,wakapanga kambi na Musa akapanda juu mlimani kusema na malaika wa Mungu.Ndipo akaambiwa ni kwa nini Mungu aliwaongoza waebrania kupita katika njia iliyo ngumu na kusudi lake kwa wana wa Israeli.Ujumbe wa mzuri sana kuhusu wakati wao ujao ukawa wazi pale Mungu aliposema,“Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa (yaani watu maalum) tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu, maana dunia yote pia ni mali yangu.”

 

Musa akashuka chini akaenda kwa wale watu akawapatia ahadi nzuri sana ajabu ambazo wakaitikia pamoja wakasema,watu wote. “Hayo yote aliyoyasema BWANA tutayatenda”. Kisha Mungu akamwambia Musa kwamba baada ya siku ya tatu atakutana na watu wote. Ni lazima wajitakase na wajitayarishe kwa ajili ya tukio hili kubwa sana la utakatifu. Na mipaka ikawekwa kwa kuwa sehemu hiyo ilikuwa ni takatifu.

 

Wakaonywa wasiuguse mlima la watakufa.

 

Mkono wa mtu awaye yote usimguse mtu huyo, ila hakika yake atapigwa kwa mawe… kwamba ni mnyama au kwamba ni mwanadamu” (Mstari 13)

 

NENO LA MUNGU – AMRI KUMI: Kutoka 19:16-25,20.

Na siku ya tatu, “palikuwa na ngurumo na umeme na wingu zito juu ya mlima, na sauti ya baragumu iliyolia sana, na kwa hiyo watu wote waliokuwapo kambini wakatetemeka” ( mstari 16). Musa akawatoa hao kambini akawaleta na kuwapeleka sehemu ya mwanzo wa mlima na ndipo Mungu akashuka na kuufunika mlima wote na moto na moshi na mlima wote ukatetemeka sana. Hebu fikiria mshangao uliowapata hao watu, wakitazama kwa ukimya.

 

Na hapo walikuwa wako mbele za Bwana kabisa. ingawaje wasingeweza kumwona. Na sauti ya baragumu ikazidi kulia sana na sauti yake ikazidi kuongezeka sana sana. Musa akapanda peke yake, akapanda mlimani na kule Mungu akampatia maagizo, ambayo aliyaleta kwa watu. Kisha kutoka katikati ya moto na wingu, watu wakaisikia sauti ya Mungu wazi wazi na ya kuogofya (kumbukumbu la torati 4:11-13 ) akawahubiria amri kumi.

 

  1. Usiwe na miungu mingine ila mimi

  2. Usijifanyie sanamu ya kuchonga

  3. Usilitaje bure jina la BWANA

  4. Ikumbuke siku ya sabato, uitakase

  5. Waheshimu baba yako na mama yako

  6. Usiue

  7. Usizini

  8. Usiibe

  9. Usimshuhudie jirani yako uongo

  10. Usitamani

 

Na ikawa Mungu alipomaliza kusema, Ngurumo na umeme na sauti ya baragumu vikaendelea na watu wakaogopa sana sana. Wakamwambia Musa, “Sema nasi wewe , nasi tutasikia bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa”

(kutoka 20:19).

 

Kwa hiyo Musa akarudi tena kwa Mungu, ambapo Mungu alimpatia sheria nyingine ambazo aliporudi aliwaambia watu. Na sheria hizi zote na amri ziliwasaidia kujifunza kuwa watu maalum kwa Mungu wao. Wangejua jinsi ya kutendeana wao kwa wao na jinsi ya kuyatendea mataifa ya jirani ambayo walikuwa wana kwenda kuishi karibu nayo. Na Mungu pia akawahidi kuwa atatuma malaika mbele yao atakaye waongoza salama kwenda nchi ya ahadi, lakini akawatahadharisha: “Jitunzeni mbele yake... kwa kuwa jina langu limo ndani yake” (kutoka 23:21)

 

Na Musa alipo maliza kuwasomea amri hizi, watu wote wakasema wanakubali na watatii. “Hayo yote aliyoyanena BWANA tutayatenda nasi tutayatatii.” (Kutoka 24:7) .Walifanya agano au kiapo cha ahadi ya kuwa watakukwa watu maalumu wa Mungu . Na kutoka pale Sinai walikuwa waendele na safari yao wakiwa ni taifa la Israeli kwenda kuirithi nchi aliyoahidiwa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo .

 

FUNDISHO KWETU

Mafundisho makubwa kupita yote yako wazi kabisa katika amri kumi. Ikiwa katika maisha yetu ya kila siku tutayaweka katika matendo, zitatuwezesha kuwa wana na mabinti wa Mungu kweli kweli.

 

Ni lazima tujifunze kumfikiria kwanza Mungu kuliko vitu vyote; na kumpenda jirani yetu kama tunavyojipenda. Kumpenda Mungu , Bwana Yesu Kristo, kwa mioyo yetu na kwa akili yetu na kwa nguvu zote hii ndiyo amri iliyo kuu tena ni ya Kwanza. Na amri ya pili yafanana na hiyo, ya kwamba umpende jirani yako kama nafsi yako. “Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.”

 

Soma mafundisho ya Bwana Yesu Kristo katika Mathayo 22;37-40.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Kusudi la Mungu la kuwapatia waisraeli sheria, ili kuwa kuwafundisha njia wanayopaswa kuifuata, maana ilikuwa ni lazima wazitii sheria zake.

 

Ilikuwa ni kuwafundiha Waisraeli kuju mema na mabaya na kuwa kumbusha pia kuwa wao walikuwa ni watakatifu au watu waliotengwa na kamwe wasimsahau Mungu wao. Kwa hiyo sheria ya Mungu iliwafanya wamkumbuke kwa kila njia; wakiwa nyumbani, wakiwa katika masomo na wakiwa katika kazi zao za kila siku.

 

Tunapozitazama amri kumi, tunaona kuwa zimetegawanyika katika makundi mawili, na kila kundi likiwa na amri tano. Amri nne za kwanza zinahusu jinsi waisraeli walivyopaswa kumwabudu Mungu na ile ya tano inahusu maisha ndani ya familia; na amri zinazobakia zinahusu jinsi walivyotakiwa kuwajali majirani zao.

 

Ingawa hatufungwi uzifuata sheria za Musa siku hizi, hata hivyo tunatakiwa kuzitii amri hizi, kwa kuwa Bwana wetu Yesu Kristo alitufundisha kwamba tuzitii pia (soma fundisho kwetu) .Kwa mfano, amri ya tisa zimerudiwa katika Agano Jipya, na amri ya nne.(inayohusu sabato), inatakiwa kuitii kwa maana ya kweli yaani tusijipende wenyewe bali kuyafanya mapenzi ya Mungu kila siku.(Isaya 58;13-14) Sheria za Musa zimeondolewa lakani Mungu anaendelea kuita wanaume na wanawake wenye imani kutoka mataifa yote. Wale wanaoikubali kweli kwa wakati uliokubalika ,kwa kuamini na kubatizwa katika Yesu Kristo wanahesabiwa kuwa ni mzao mteule ,ukuhani wa kifalme ,watu maalumu , kama vile Israeli walivyo kuwa wakati wa Musa (1.Petro2: 9 linganisha kutoka 19:5-6)

 

MASWALI

1.Jina la mlima ambapo Mungu aliwapatia Israeli sheria zake ?

2.Je,Mungu alitaka taifa la Israeli wawe watu wanamna gani?

3. Watu walitakiwa wajitayarishe vipi kabla ya kukutana na Mungu?

4. Ni kwanini Musa aliagiza kuweka mpaka kuzunguka mlima

5. Je, watu walizisiki amri kumi alizozisema Mungu ?

6. Je, watu walijibu nini baada ya Musa kuwasomea sheria za Mungu?

7.Je, Yesu alisema ni ipi iliyokuwa amri kuu na tena ni ya kwanza?.

8. Na ni amri ipi aliyoisema kuwa ni ya pili nayoyafanana na hiyo?

 

Majibu ya Kina

  1. Sema unayojua kuhusu amri kumi?

  2. Ni amri zipi ambazo Yesu alisema kuwa zilikuwa amri mbili kuu?

  3. Je, kusudi la Mungu la kuwapatia waisraeli amri ni lipi?

  4. Ni jinsi gani tunavyo zitii amri kumi siku hizi?

 

 

Swahili Title
020 ISRAELI KATIKA MLIMA SINAI
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type