CSSA 1-1-22 - THE TABERNACLE-GOD'S MEETING PLACE WITH ISRAEL

Swahili

22. MASKANI SEHEMU YA MUNGU YA KUKUTANA NA WANA WA ISRAELI

"Nao na wanifanyie Patakatifu ili nipate kukaa kati yao"

 

Shabaha.

 

Nikujifunza kuhusu Maskani ambayo Mungu alimwagiza Musa ajenge pawe mahali Mungu anapokaa katika Israeli. Wana wa Israeli waliweka kambi yao katika mahema kando ya Mlima Sinai na pale wakaandaa vifaa na thamani kwa miezi mingi kwa ajili ya Maskani nzuri sana.

 

Maana Musa alikuwa ameonyeshwa mfano wake na akapewa maelezo na Mungu alipokuwa amepanda mlimani. Mungu akamwelekeza Musa kutengeneza sawa sawa na vile alivyo kuwa amemwonyesha “sawa sawa na hayo nikuonyeshayo wewe, mfano wa Maskani, na mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo mtakavyovifanya” (Kut. 25:9). Palikuwa patakatifu au mahali Patakatifu, sehemu ambayo Mungu angekutana na wana wa Israeli na wao wangekuja kumwabudu Mungu hapo.

 

Kutoka 25:1-9; 26, 35, 36:8-19;Hesabu 1:49-54; 2

 

VIFAA VILIVYOTUMIKA KUKTENGENEZA MASKANI: Kuto. 25:1-9

Jengo kama hili lilihitaji vifaa maalumu. Watu wakaambiwa kuleta vifaa vifuatavyo vilivyoandikwa katika :

Kutoka 35:5-9

 

  • Dhahabu, fedha, shaba

  • Nyuzi za rangi ya Samawi na za rangi ya Zambarau na rangi nyekundu

  • Singa za Mbuzi, ngozi za Kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, ngozi za Pomboo

  • Mbao za mshita

  • Mafuta kwa ajili ya taa

  • Viungo vya manukato

  • Madini ya vito (vito vya shohamu)

  • Kitani nzuri kwa ajili ya Mapazia.

 

Mungu akamwambia Musa, “kwa kila mtu awaye yote ni yeye mwenye moyo wa kupenda mtatwaa kwake matoleo yangu” (mstari wa 2). Watu wote wakapenda sana hiyo kazi “ hata ikawa wakawa wameleta vingi sana zaidi ya hivyo vitoshavyo kazi” (Kuto 36:5) naye Mungu aka kazi furahi sana.

 

Mungu alikuwa makini kuhakikisha kuwa Musa anaelewa ili maskani hiyo itengenezwe sawa sawa na jinsi alivyokuwa amemwonyesha.

 

Wanaume wenye ujuzi na wanawake wenye ujuzi wa kusokota kwa mikono walihitajika nao wenye hekima ya kutosha kufuata maagizo ya Mungu walihitajika.

 

Mungu akawachagua wanaume wawili akawapatia hekima maalumu ili kwamba wajue kufanya kazi hiyo yote kwa urahisi kabisa na ubora kama ilivyotakiwa. Nao walikuwa ni Bezaleli na Ohaliabu (Kut. 35:30,34).

 

Na wanawake wenye moyo wa kupenda, wakaleta nguo za kitani nzuri wakatengeneza mapazia, vifuniko vya maskani, na wakaleta nguo nyingi zenye kufumwa kwa uzuri, ambayo yalikuwa ni mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe. Baadhi ya wanaume wakatengeneza vifaa naye Mungu akawajaza “akili za moyoni ili watumike katika kazi za kila aina” (Kutoka 35:35).

 

RAMANI YA JENGO: Kutoka 26

Maskani au sehemu ya kuishi, ili kuwa na kuta nne zilizotengenezwa kwa mbao za Mshita ambazo zilifunikwa kwa dhahabu. Pazia lililofumwa kwa uzuri likawekwa juu kutengeneza dari. Na kisha juu ya maskani yote ziliwekwa ngozi za wanyama.

 

Ilikuwa ni kubiti 30 urefu, na kubiti 10 upana na kubiti 5 kwenda juu. (zingatia: kubiti moja ni sm 50. Kwa hiyo jengo lote kipimo chake ilikuwa yapata kama m.15 kwa m.5). Mlango wa kuingia katika Maskani ulikuwa upande wa mwisho wa mashariki, kupitia pazia ya nguo ya kitani safi iliyokuwa imesokotwa tanzi za rangi ya samawi, rangi ya zambarau na rangi nyekundu. Kulikuwa na hema mbili, mahali patakatifu na patakatifu pa Patakatifu, hema hizi zilitenganishwa na pazia jingine, lililoitwa. Mahali Patakati urefu wake ilikuwa kubiti 20 urefu na kubiti 10 upana. Sehemu hii ilikuwa ni mara mbili ya eneo la Patakatifu pa Patakatifu ambapo vipimo vyake ilikuwa ni kubiti 10 kwa kubiti 10 (kama ilivyokuwa kubiti 10 pia kwenda juu, ilikuwa ni kubiti sawa).

 

Eneo lililozunguka maskani pake yeke lilikuwa na ukubwa wa eneo la kubiti 100 urefu na kubiti 50 upana. Eneo hili lilikuwa imezungukwa na pazia ya Kitani safi ing’arayo ikiwa imefungwa kwenye nguzo za mbao zilizokuwa zimefungwa katika shaba. Mlango wa kuingilia sehemu hii na ukuta ulikuwa pia upana wa mwisho wa Mashariki, nao pia ulitengenezwa kwa kitambaa cha Kitani safi, iliyosokotwa kwa nyuzi za rangi ya Samawi, rangi ya Zambarau na rangi Nyekundu.

 

SEHEMU YA MASKANI KATIKA KAMBI. Hesabu 1:49;2

Kazi yote ilipokuwa imekamilika, maskani ilisimikwa kati kati ya kambi ya wana wa Israeli. Na kila wakati Mungu alitakiwa awe katikati ya watu wake. Eneo kubwa liliachwa kuzunguka Maskani ili Waisraeli wakusanyikie hapo wanapitwa kusikia maneno ya Mungu.

 

Mahema ya wana wa Lawi yalipangwa pembe tatu za Maskani (hema ya kukutania), lakini yakielekee upande wa mashariki na mbele pazia la lango la kuingilia palikuwapo mahema ya Musa na Haruni. Na mahema ya wana wa Israeli wote yalipangwa kwa kufuata makabila yao, wakati wote yaliwekwa kwa mpangilio. Kambi yote ilipangwa kwa ukubwa wa eneo na Mungu akiwa kati kati yao na wingu likiwa kifuniko chao kwa joto la jua. Ilipokuwa wakati wa kuondoa kambi wingu liliinuliwa na kutangulia mbele ya wana wa Israeli na taifa hilo likaondoka kwa kufuata utaratibu wa makabila kama Mungu alivyokuwa amemwelekeza (Kutoka 40:34-38) wakati wote Kabila la Yuda ndilo lililotangulia taifa na kufatiwa na makabila zaidi ya matano. Kisha likafuata kabila la Efraimu na makabila yanayosalia, jumla yalikuwa yote ni makabila kumi na mbili. Katika Hesabu 10:14-28 tunaweza kusoma utaratibu wa mpangilio wa makabila jinsi waliyokuwa wakiondoka.

 

FUNDISHO KWETU

Tumeona jinsi Mungu aliyoweza kuzikubali sadaka kwa ajili ya Maskani kutoka kwa watu waliokuwa na moyo wa kupenda. Mtume Paulo anatuambia katika 2 Wakorintho 9:7 kwamba Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Hebu na tujifunze kutoa kwa moyo wa kupenda, tukishirikiana kwa kitu chochote tulichonacho na tukiutumia muda wetu na uwezo wetu pasipo kulalamika. Kama tukitoa kama tunavyoweza, haijalishi ni kiasi gani au kwamba ni kiasi gani tunachotoa ni kidogo, lakini itakuwa bora kwetu na ni lazima kitolewe kwa moyo wa kupenda.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Mungu aliwachagua wanaume maalumu kwa kazi wasimamie ujenzi wa Maskani. Na kwa nyogeza, Mungu alitaka “Na kila mtu mwenye hekima na aje na kuyafanya hayo yote ambayo BWANA ameagiza” (Kutoka 35:10;25-26). Na katika watu hawa wote wanaume na wanawake, Mungu aliwapatia hekima na akili ili wajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu kama hayo yote BWANA aliyoagiza (Kutoka 36:1)

 

Mungu ametupatia maandiko matakatifu ili tujifunze tuwe watenda kazi wa BWANA, Mungu (2Timotheo 3:15-12).

 

Na kwa kadri tunavyosoma zaidi neno lake ndivyo tunavyokamilishwa vema ili kumtumikia Mungu. Kama Mtume Paulo alivyo mhimiza Timotheo, kwa hiyo tunaweza kutiwa moyo na maneno hayo. “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukilitumia kwa halali neno la kweli” (2 Timotheo 2:15)

 

MASWALI

Majibu Mafupi

 

  1. Ni nani aliye mpatia Musa ramani ya Maskani?

  2. Ni nani waliochaguliwa na kuongozwa hasa kwa ajili ya kazi?

  3. Wanawake walifanya nini kuhusiana na kazi hiyo?

  4. Ni watu wa namna gani waliotaa vifa kwa ajili ya ujenzi wa Maskani?

  5. Maskani iligawanywa katika sehemu ngapi kuu?

  6. Ni aina gani ya rangi iliyotumika katika Maskani?

  7. Vifuniko vya maskani vilitengenezwa kwa?

  8. Katika Kambi ya wana wa Israeli sehemu ya Mungu ilikuwa wapi?

  9. Je, taifa lilijuaje wakati wa kuondoa kambi yao?

  10. Ni katika mpangili upi ambao makabila yaliondoka walipoondoa kambi yao?

 

MAJIBU YA KINA

 

  1. Kuna fundisho gani kwa ajili ya kujenga Maskani ya Mungu?

  2. Ni vifaa gani vilivyotumika kutengeneza maskani na ni nani aliyevitoa vifaa hivyo?

 

MAJIBU YA NYONGEZA

  1. Eleza kwa ufasaha ramani ya maskani kwa kutumia mchoro na maelezo.

  2. (a) Ni watu wa aina gani waliofanya kazi katika kujenga Maskani?

(b) Ni jinsi gani Mungu alivyowaandaa kwa kazi?

(c) Ni jinsi gani tunavyoweza kujiandaa kutenda kazi ya utumishi wa Mungu?

 

UTARATIBU WA KUONDOKA WA MAKABILA YA ISRAELI

  1. YUDA

  2. ISAKARI

  3. ZABRON

  4. WALAWI

 

(GERISHONI NA MERARI PAMOJA NA MASKANI)

  1. REUBENI

  2. SIMEONI

  3. GADI

  4. WALAWI

 

KOHATHI PAMOJA VIFAA, VYOMBO NA SANDUKU LA AGANO

  1. EFRAIMU

  2. MANASE

  3. BENJAMINI

  4. DANI

  5. ASHERI

  6. NAFTARI

Swahili Title
022 MASKANI SEHEMU YA MUNGU YA KUKUTANA NA WANA WA ISRAELI
English files
Swahili file
PDF file
African text
CSSA
Translator 1
AI
Literature type
Sub type
Sub sub type