CSSA 1-1-24 - TEACHERS FOR ISRAEL

Swahili

24. WALIMU WA ISRAELI

"Watafundisha Yakobo hukumu zako, na Israeli Torati yake"

 

Shabaha

Ni kuonyesha jinsi Makuhani na Walawi walivyofundisha wana wa Israeli kuishi kwa kufuata Sheria za Musa.

 

Mafundisho ya ibada ya pale penye Maskani na mafundisho ya Kiroho yalikuwa muhimu lakini Torati ya Musa ilikuwa ni muhimu zaidi. Ilikuwa ni muhimu sana kwa kila mtu, mtoto pia, afundishwe ajue na kufahamu Torati ambazo ndizo zilizowaongoza katika maisha yao ya kila siku, ikiwa ni pamoja na siku maalumu ambazo Mungu aliwataka kuzitunza kwa ajili ya mafundisho maalumu.

 

Ili kuweza kufanya kazi hii muhimu sana ya kufudisha wana wa Israeli, na kuzifanya, Mungu alichagua kabila moja.

 

Kutoka 28:1-5: 38-46, Hesabu 3:6-10

 

Walikuwa watu wa kanuni, wliothibitika kutunza njia za Mungu na kuwaadhibu wote waliomtenda dhambi Mungu.

 

WA WALAWI – WALIMU WALIOTEULIWA NA MUNGU.

Kwa asili kulikuwa na makabila kumi na mbili ya wana wa Israeli, na kila kabila lilikuwa ni uzao kutoka kwa kila mmoja wa wana kumi na mbili wa Yakobo. Wakati Yakobo alipowaita wanaye pamoja ili kuwabariki, mwana wake Yusufu alipata Baraka mara mbili. Hii inamaana kwamba kila mwana wa Yusufu; ambao ni Efraimu na Manase walipokea sehemu kamili ya urithi katika Israeli, kwa hiyo tangu wakati huo wakawa ni makabila kumi na tatu.

 

Katika fundisho linalohusu ndama ya dhahabu, tuliona kuwa wana wa Lawi walijitenga wenyewe na watu waliotenda maovu na wakajiunga upande wa Mungu, ambaye aliwaamuru kuwaangamiza wale waliotenda dhambi. Na jina “Lawi”,maana yake “ungana” na hivi ndivyo kabila lililovyofanya wao wenyewe kuungana na Mungu.Walikuwa ni watu wenye msingi wa imani ,imara katika njia za na kuwaadhibu watu wote waliomtenda Mungu dhambi, hata rafiki pia au watoto wake (jamaa zake) wa karibu pale ilipobidi (Kumb. 33-8-10).

 

Ni kanuni ya kweli kwamba Mungu ni lazima awe ni chaguo letu la kwanza katika maisha zaidi kuliko vyote tunavyo vipenda- kama Yesu mwenyewe alivyofundisha (Mathayo 10:37). Na kwa sababu ya tabia hii ya uminifu kwa Mungu wao. Mungu akachagua kabila la Lawi kuwa watendaji wake wa kazi muhimu, kufanya utumishi katika Hema ya kukutania na kuwafundisha wana wa Israeli njia za Mungu.

 

Nami nimempa Haruni hao Walawi wawe kipawa chake yeye wanawe ili watumike utumishi wa wana wa Israeli” (Hesabu 8:19). Wakati wana wa Israeli walipokuwa wanasafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, ulikuwa utumishiwa wa Walawi kuichukua Maskani(hema ya kukutania). Nao Makuhani walipomaliza kufunika samani zote kwa uangalifu, ilikuwa ni jukumu la Walawi kubeba katika Safari.

 

Kisha wao ndiyo walioisimaisha tena mahali ambapo Mungu amewaonyesha. Lilikuwa ni jukumu lao pia kujifunza Torati, ili kwamba waifahamu vizuri sana na waweze kuwafundisha wengine.

 

MAKUHANI

Katika baadhi ya Walawi, familia ya Haruni ilichaguliwa kumkaribia Mungu. Wakiwa makuhani, kazi yao ilikuwa ni muhimu sana, maana ni makuhani pekee yao walioruhusiwa kuingia ndani ya maskani (Hema ya kukutania). Kwa hiyo ulikuwa ni wajibu wao kuhakikisha kuwa mafuta yamo ndani ya kinara cha taa kila wakati na kubadili mikate ya Wonyesho kila juma. Kila asubuhi na jioni, walipaswa kutoa sadaka ya kuteketezwa kila siku. Na hapo ndipo walipochoma ubani juu ya madhabahu ya kuvukizia uvumba mahali patakatifu kwa niaba ya wana wa Israeli wote.Ulikuwa ni wajibu wa Makuhani kutunza moto wa madhabahu ya kuteketezea sadaka na ndiyo waliowahudumia watu wote waliokuja kutoa sadaka au dhabihu kwa Mungu pale penye maskani.Walawi pia walifundisha wana wa Israeli njia za Mungu (Malaki 2:7).

 

KUHANI MKUU

Kuhani Mkuu, Haruni,alikuwa mtu mhimu sana, kwa ajili ya watu wote, ni yeye pekee yake aliyeingia Patakatifu Pa Patakatifu na kuwa karibu sana na Mungu. Kuhani Mkuu alikuwa ni mtu mmoja kila wakati, na hata mavazi yake mazuri sana yalibuniwa na Mungu kwa “ajili ya utukufu au kwa uzuri” (Kutoka 28:2). Alivaa suruali ya kitani safi nyeupe na joho ya naivera na juu yake alivaa kanzu ya kitani ya bluu na mshipi. Kanzu hii ya blue ilizungukwa na Makomamanga ya rangi ya baharamani (bluu) na ya rangi ya zambarau, maua ya rangi nyekundu ambayo yalitiwa katika pindo za kanzu kotekote. Na kati ya komamanga na Komamanga kulikuwa na kengele ya dhahabu. Na rangi hizi zote za uzuri zilikuwepo kwenye mapazia matatu ya Maskani,na kila rangi inafundisho la muhimu sana. Kisha mavazi hayo yalifunikwa kwa naivera.

 

Juu ya kifua chake kulikuwa na Kitani safi kilichokuwa cha mraba na ambacho kiliwekwa madini ya vito vya thamani sana. Madini haya ya vito 12 ya thamani, kila moja liliwakilisha kabila moja la wana wa Israeli. Hiki kiliitwa kifuniko cha kifuani. Kuhani Mkuu alivaa kilemba cha kitani safi, bamba la dhahabu safi likawekwa kwenye kilemba upande wa mbele wa kilemba nacho kikawa katika kipaji cha uso na kikawa kimechorwa maandishi haya. “MTAKATIFU KWA BWANA”. Ni mng’ao wa ajabu sana wa rangi hizi na kwa uzuri wake wa jinsi Haruni aliovyoonekana alipovaa mavazi haya mazuri sana.

 

ULINZI WA MUNGU KWA WALAWI

Wakati wana wa Israeli walipokuwa ni watu wenye makazi katika Nchi ya Ahadi, Walawi, wakiwa tofauti na mkabila kumi na mbili, wao hawakupewa sehemu yoyote ya kupanda mazao na kutumia kwa ajili ya mahitaji yao ya kila siku. (Hesabu 18:20-23). Mungu akawaambia Walawi kuwa yeye atawatunza wao na kila baada ya miaka mitatu makabila mengine yote yaliwapa fungu la kumi ya mapato yao yote. Na matokeo yake Walawi nao walimpatia Haruni na wanawe; Makuhani fungu la kumi la vyote walivyopata. Mungu akasema “Mimi ni fungu lako na urithi wako” na Walawi walijua kuwa vitu vyote vyema hutoka kwa Mungu. Na ingawa kulikuwa na makabila kumi na tatu, lakini kabila la Lawi wakati wote lilitengwa kwa hiyo nchi wakati wote inanenwa kuwa inamilikiwa na makabila kumi na mbili.

 

FUNDISHO KWETU

Tangu Mungu alipomweka Adamu na Eva katika Bustani ya Edeni, Mungu aliwapatia watu wake sheria ya mambo waliyotakiwa kufanya, naya mambo wasiyotakiwa kuyafanya. Pia aliwachagua watu ambao wajibu wao ni kusaidia kufundisha sheria hizo kwa Wana wa Israeli, Mungu aliwachagua Walawi, kisha Manabii na na mwishowe Mungu akamtoa Mwanaye wa pekee Yesu Kristo, ambaye alikuwa ni mkubwa wa walimu wote ambao Mungu aliwachagua kufundisha (Waebrania 1:1-2). Mafundisho ya Bwana Yesu Kristo yameandikwa katika Biblia kwa ajili yetu tujifunze. Katika upendo wake wa ajabu na wema wake, Mungu ametupatia wazazi na Walimu watufundishe Neno lake. Wao ni wasaidizi wetu na wao wanatuonyesha katika Biblia yale tunayotakiwa kuyafanya. Na kwa hiyo tusikilize kwa makini yale wanayotuelekeza tunayoyapata kutoka kwao, ili Mungu aweze kutubariki sisi na uzima wa milele “Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, wala usiache sheria ya mama yako, yafunge hayo katika moyo wako daima, Jivike hayo shingoni mwako. Uendeakao yatakuongoza, ulalapo yatakulinda na uamkapo yatazungumza nawe. Maana maagizo hayo ni taa na sheria hiyo ni nuru” (Mithali 6:20-23).

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Kuhani Mkuu alivaa kibamba cha dhahabu, kilichokuwa upande wa mbele wa kilemba na akakiweka katika kipaji cha uso wake ambacho kiliandikwa “MTAKATIFU KWA BWANA”. Hili lilimfundisha kuhani Mkuu na watu wote wanaomwona kuwa akili (mawazo) yake ambayo yalikuwa nyuma ya kimbamba cha dhahabu kuwa zinapaswa kufikiria njia za Mungu tu kila siku. Na ili kufanya hivyo alitakiwa kulitafakari Neno la Mungu kila siku kuhusu.

 

Bwana Yesu hakuwahi kutenda dhambi katika maisha yake yote, kwa sababu alifikiria tu mawazo ambayo ni mawazo yale ya kumpendezaa Mungu. Alikuwa ni Mtakatifu kwa BWANA kwa mawazo na matendo. Na waumini wa siku hizi wanatakiwa wawe watakatifu pia. Petro anasema; vifungeni viuno vya nia zenu” (maana yake- uhakikishe kuwa nia yako imejiandaa kwa ajili ya Ujio wa pili wa Yesu Kristo) na kuwa mtakatifu katika mwenendo wenu wote, maana Mungu amesema “Iweni Watakatifu maana Mimi ni Mtakatifu” (1Petro 1:13-16).

 

Neno la Mungu lina uwezo wa kututakasa sisi (maana yake- linaweza kutusafisha tukawa safi na kuwa watakatifu) (Yohana 17:17), na kwa hiyo tunaweza kuangusha mawazo yote ili kutii mapenzi ya Mungu (2Wakorintho 10:5).

 

MASWALI

Majibu Mafupi

 

  1. Ni kabila lipi ambalo Mungu alimpatia Haruni limsaidie kuwafundisha wana wa Israeli?

  2. Ni jinsi gani Walawi walivyowezakusaidia katika maskani?

  3. Ni kwa nini Walawi wachaguliwa kama Watumishi maalumu wa Mungu?

  4. Ni nyumba ipi iliyochaguliwa kuwa ya Makuhani katika Israeli?

  5. Ni yapi yalikuwa ni majukumu ya Makuhani?

  6. Ni nani aliyechaguliwa kuwa Kuhani Mkuu kwanza?

  7. Ni maandishi gani yaliyoandikwa kwenye bamba la dhahabu alilolivaa Kuhani Mkuu mbele ya utosi?

 

Majibu ya Kina

 

  1. Mungu alichagua kabila moja wawe Walimu wa Torati katika Israeli. Ni kwa jinsi gani Mungu alivyo wapatia chakula Walawi, ambao hawakuwa na ardhi ya kwao wenyewe?

 

  1. Kazi ya Makuhani ilikuwa :-

  1. Katika Maskani.

  2. Katika kuwasaidia watu.

 

Majibu ya Nyongeza

  1. Elezea mavazi ya uzuri aliyovaa kuhani Mkuu.

  2. Ni nini lilikuwa fundisho la bamba la dhahabu katika kilemba cha Kuhani Mkuu?

 

 

Swahili Title
024 WALIMU WA ISRAELI
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type