29. WALIPOKARIBIA KUMALIZA SAFARI - NYOKA ZA MOTO.
"Alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi".
Shabaha:
Kuonyesha jinsi tunavyopaswa kumfuata Mungu sawa sawa na amri zake na daima tumpe Utukufu Mungu kwa wema wake kwetu.
Muhtasari:
Mkutano wa wana wa Israeli walizunguka zunguka miaka thelathini na nane katika hali ya taabu, wakawa katika nchi mbaya kwa sababu hawakuwa na Imani na hawakumtumaini Mungu wao. Safari yao ya kuhuzunisha ilipokaribia kuisha karibu wazee tayari walikuwawamefariki, wakiacha wale ambao wangeingia Nchi ya Ahadi hatua ya mwisho ya safari yao jangwani yalikuwpo bado majaribu ambayo lazima wangeyapata ,kizazi kipya walisafiri kuelekea Kaskazini na kusimama kwenye mipaka ya Kanaani. (Hesebu: 20:21:4-9: Kumb.8:15-16).
MUSA ANAPIGA MWAMBA : Hesabu 20:1-13
Wana wa Israeli walipofika Kadeshi tena na ilikuwa ni hapo Miriamu alipofia. Kwa hiyo Musa na Haruni walimzika dada yao penye ukingo wa Nchi ya Ahadi. Miriamu alikuwa ni msaada mkubwa sana kwa Musa katika miaka yote ya taabu na akalala mauti kusubiri mapambazuko ya ufufuo wenye Utukufu.
Kwa wale waliokufa wakiwa na imani watafufuka kwa uzima wakati Yesu Kristo atarudi kuwekaUfalme wake. (1Wathe. 4:16)
Karibu miaka yote ya kuzunguka zunguka jangani, wana wa Israeli walikuwa hawana maji na wakawa na kiu sana.
Hawakuwa wavumilivu, wakakata tamaa na wakahofu sana kuwa wangekufa jangwani. Imani yao ikatindika wakawa wakifikiria Misri. Musa na Haruni wakawakasirikia sana, walikumbuka jinsi baba zao walivyo watendea miaka thelathini iliyopita.
Hata hivyo, Mungu hakuwaacha. Mungu alijua kuwa watahitaji maji na yeye BWANA ndiye angewapatia mahitaji yao. Kwa hiyo Mungu akamwagiza Musa achukue fimbo ya Haruni na kumwambia. "Ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba". (Mst.8).
Lakini Musa akiwa na hasira zake aliichukua fimbo, badala ya kuwambia mwamba kama BWANA alivyomuamuru aliupiga mwamba marambili na kuwaambia "Sikia sasa,enyi waasi; je tuwatokezee maji katika mwamba huu?" (mst10). Akiwa ni mwenye hasira, Musa alisahau kutomtii Mungu sawasawa kama BWANA alivyokuwa amemwamuru.Musa alikosea kuupiga mwamba alipaswa kuuambia kama alivyokuwa ameagizwa.Hakuweza kumpa pia BWANA utukufu , alikuwa ni Mungu aliye sababisha maji yatiririke, Musa alitakiwa kuhakikisha wana wa Israeli wanajua kuwa Mungu ndiye awapaye ili waweze kumshukuru kwa msaada wake. Na kwa sababu ya kosa hili Musa hakuruhusiwa kuingia Nchi ya Ahadi BWANA akamwambia Musa na Haruni, " Ninyi hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi ." (mst 12).
Baada ya miaka hiyo yote ya uongozi wa uvumilivu kwa watu wenye shingo ngumu na waasi kwa Mungu, mtu huyu mkuu na nabii hakuruhusiwa kuwaingiza katika Nchi. Musa alitenda dhambi, ni lazima asubiri hadi Kristo atakaporudi na kisha ndipo ataweza kuingia nchi hiyo akiwa mwenye furaha na utukufu.
KIFO CHA HARUNI: (Hesabu 20:12-29).
Muda ukafika wa Haruni, kaka yake Musa, kufariki. Mungu akamwambia Musa awachukue Haruni na Eliazari mtoto wa Haruni ukawalete juu ya mlima Hori. Walipofika kule, Musa akamvua Haruni mavazi yake akamvika Eliazari mavazi, ambaye akawa Kuhani Mkuu baada ya kifo cha baba yake. Haruni akafa kule katika kilele cha mlima, ilikuwa siku ya kwanza ya mwezi wa tano katika mwaka wa arobaini baada ya wanawa Israeli kutoka katika Nchi ya Misri, akiwa mwenye miaka 123 (Hes. 33:38-39). Wana wa Israeli wakamwomboleza kifo chake muda wa siku thelathini. Haruni angali amelala kaburini akisubiri ufufuo na Ufalme wa Mungu utakaposimamishwa.
NYOKA ZA SUMU PIGO KWA WANA WA ISRAELI (Hes 21:4-9; kumb.8:15-16)
Musa alituma wajumbe kutoka Kadeshi kwenda ufalme wa Edomu awape ruhusa kupita katika nchi yake ili kwenda nchi ya Kaanani. Mfalme wa Edomu aliwakatalia, hivyo Waisraeli wakawa na safari ndefu sana na yenye kuchosha inayopita katika jangwa ili kuepuka wasipite Edomu. Maji yalikuwa ya shida na walikuwa wameishaikinai mana. Hivyo walifadhaika na kukosa imani.
Wakamnung’unukia Mungu na Musa, wakasema. "Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe Jangwani?." (mst 4,5). Zilitokea siku nyingi kama hii, wakati walipopata shida walilalamika na kumlaumu Mungu kwa ajili ya taabu zao.
Waisraeli waliadhibiwa mapigo ya "nyoka za moto", ambazo zilikuwa na sumu zilipouma, iliyo sababisha homa ya …. na kifo. Wana wa Israeli walipoona wengi kati yao wamekufa walimwendea Musa wakasema "Tumetenda dhambi…. Utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa". Musa akawaombea watu naye BWANA akamwambia Musa, Jifanyie nyoka wa shaba ukaiweke juu ya mti, hata "ikiwa nyoka amemuuma mtu, alipoitazama nyoka ya shaba, akaishi."
Mungu alikuwa mwenye rehema tena kwa watu wake. Wote walioitazama nyoka ya shaba katika Imani, waliamini neno la Mungu, waliponywa(mst8,9).
FUNDISHO KWETU.
Hata wakuu kama Musa na Haruni mara nyingi walimtenda BWANA dhambi. Katika Zaburi ya 106:22-33 tunasoma kwamba wana wa Israeli wakamgadhibikia Musa wakamkasirisha. Na matokeo yake, akasema yasiyofaa kwa midomo yake na hakumpa BWANA utukufu. Ni lazima tuwe waangalifu kwa yale tuyasemayo na hasira tusiipe nafasi. Ni vyema kufikiri kabla ya kusema na vilevile tunapokumbushwa hili na mtume Yakobo tunaposoma, "Basi kila mmoja na awe mwepesi wa kusikia, si mwepesi wa kusena wala kukasirika" (Yakobo 1:19)
MAELEZO YA NYONGEZA:
SOMO LA KIROHO KUHUSU NYOKA WA SHABA. (Yohana:3:14-15)
Kulikuwapo tofauti kati ya nyoka halisi na nyoka yule aliyewekwa juu ya mti. Nyoka wa moto walikuwa wenye sumu na mtu waliyemuuma alikufa. Lakini nyoka ya shaba iliyowekwa juu ya mti haikuwa na sumu na watu walipoitazama kwa imani nyoka ya shaba waliokoka na mauti. Kwa imani waliokoka na sumu walipokuwa wameumwa na nyoka wa moto. Katika Yohana 3:14-15 tunasoma, "na kama vile Musa alivyomuinua yule nyoka jangwani vile vile Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele".
Bwana Yesu Kristo alitumia tukio hili kuonyesha kuwa imani ndiyo iliyowaokoa wana wa israeli jangwani wasife walipoumwa na nyoka. Yesu kristo akifahamu kuwa mwisho angesulubishwa,Yesu alifundisha kuwa,kama vilenyoka alivyowekwa juu ya mti,naye vilevile angeinuliwa juu. Na wale wote wanaomtazama kwa imani wataona katika maisha yake,kifo, ufufuo na njia ya wokovu kupitia ubatizo katika jina lake Yesu Kristo (Rum 4:25; 6:3,4).
Rejea kitabu cha mwalimu wa shule ya Jumapili swali Na 54.
MASWALI MAJIBU MAFUPI.
-
Mungu alimwambia Musa afanye nini kuleta maji kutoka mwamba kule Kadeshi?
-
Musa alisema nini kabla maji hayajatoka katika mwamba?
-
Musa aliitumiaje fimbo yake?
-
Mungu aliwaambiaje Musa na Haruni baada ya maji kutoka?
-
Ilitokea nini Musa,Haruni na Eliazari walipokwea juu ya mlima Hori?
-
Ni kwa nini Mungu aliwatuma nyoka za moto kwa waisraeli?
-
Mungu alimwambia Musa afanyeje ili kuwaokoa wana wa israeli?
-
Waisraeli walipaswa wafanyeje ili kuokoka kutokana na kuumwa na nyoka?
Majibu ya Kina
(1) Musa hakutii kwa uangalifu maagizi yote mungu alipotoa maji kutoka katika mwamba kule kadeshi.
(a) Ni kwa nini Mungu aliwakasirikia Musa na Haruni?
(b) Mungu alimwambiaje kutokana kosa walilolifanya?
(2) Eleza jinsi Musa alivyoleta maji kutoka katika mwamba kule Kadeshi kabla wana wa israeli kuingia Nchi ya Ahadi?
(3)(a) kwa nini Mungu alituma nyoka za moto kwa wana wa israeli?
(b) Nikwa namna gani waisraeli wangeokolewa kutoka mauti walipokuwa wameumwa na nyoka?
Majibu ya nyongeza
4.Yesu Kristo alisema "Na kama vile Musa alivyomwinua nyoka jangwani,vivyo hivyo mwana wa adamu hana budi kuinuliwa". Alikuwa ana maana gani kusema hivi?