CSSA 1-2-06 - THE NEW LEADER

Swahili

31. KIONGOZI MPYA

"Uwe hodari na moyo wa ushujaa kama nilivyokuwa pamoja na Musa ndivyo

nitakavyokuwa pamoja nawe"

 

Shabaha:

Ni kuonyesha jinsi kazi ya Musa ilivyokwisha; na mwingine mwenye busara na mwaminifu,Yoshua alivyochaguliwa kuendeleza na kuongoza wana wa Israeli kuingia Nchi ya Ahadi.

 

Muhtasari:

Kule kuzungukazunguka Jangwani kwa wana wa Israeli kuliisha na walikuwa waingie katika nchi ya Kanaani mapema. Walifahamu kuwa nchi hiyo ilitunzwa kwa ajili yao, Mungu aliwapatia kiongozi mwenye sifa nzuri ili kuchukua nafasi ya Musa. Hes: 27:15-23, Joshua 1:1 - 11

 

KIONGOZI MPYA Hesabu: 27:15-23

Ilikuwa kabla hajafa Musa aliambiwa na Mungu kuwa Yoshua ndiye aliyekuwa ameteuliwa kuwaongoza wana wa Israeli kwenda Nchi ya Ahadi. Musa alimpeleka Yoshua mbele ya Eliazari, Kuhani Mkuu na kwa Waisraeli na akawaambia kuwa yeye ndiye atawaongoza wana wa Israeli kama Mungu alivyoagiza. Alikuwa ni Yoshua mwenyewe wa kuwafikisha katika Nchi ya Ahadi (Hes: 27:18-19; Kumb. 1:23) Yoshua alikuwa mtumishi wa Musa kwa miaka mingi (Kutoka 33:11). Alikuwa na sifa nzuri za kuwa kiongozi wa watu wa Mungu. Alikuwa mtu mwenye sifa bora.

 

Shujaa: alikuwa amewaongoza Waisraeli katika Vita walipopigana na Waamaleki

kutoka 17:10-13

Imani: alikuwa ni kati ya wapelelezi wawili waaminifu walioleta taarifa nzuri

kuhusu Nchi ya Ahadi (Hes: 14:6-9) (angalia somo la 2)

Hekima: alipata hekima hii kutoka kwa Mungu (kumb 34:9)

Mungu alimwambia kusoma kitabu cha Torati klia siku na ayatafakari

maneno yake (Josh 1:8).

Uzoefu: alijifunza kutoka kwa Musa namna ya kuongoza watu, alikwisha kuwa

msaidizi wa Musa kule Sinai na wakati wote wa safari ya kuzunguka

zunguka katika jangwa.

 

YOSHUA ANATIWA NGUVU NA MUNGU : Joshua 1:1-9

Kazi ya Joshua ilikuwa ngumu lakini Mungu alimuimarisha kwa ajili ya kazi hiyo: "Uwe hodari na moyo wa ushujaa, usiogope". (mist 6,9)

 

Waisraeli walikuwa wana wa Mungu. Ilikuwa kiongozi wao, Yoshua alipaswa kuwafundisha kumtii na kumpenda Mungu. Walipovuka mto Yordani walikuwa ni Jeshi la Mungu, walivamia nchi na kuwafukuza wenyeji wake. Kwa hiyo Yoshua alikuwa ni Jenerali mwenye akili pia. Kama vile Musa, nayeye alikuwa mpole. Alifahamu kuwa majukumu yake yalikuwa ni makubwa kwake "isipokuwa tu awe amepata msaada wa Mungu". Mungu aliahidi kumsaidia na kumthibitisha ikiwa tu Yoshua angedumu katika kumtegemea Mungu. Yoshua akiwa mwaminifu alikumbushwa kufikiria kitabu cha Torati mchana na usiku na kuyafanya yote yaliyoandikwa humo. Kama angeyafanya asingeshindwa.

 

"Hapatakuwa mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako, kama nilivyokuwa pamoja na Musa ndivyo nitakavyokuwa na wewe;sitakupungukia walakukuacha.Uwehodari na moyo wa ushujaa maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliwapia baba zao ya kwamba nitawapa".(mist 5,6)

 

WAISRAELI WALIJANDAA: Yoshua1:10-11

Mkutano wote wa Isaraeli walikuwa wameweka kambi yao huko Shitimu,Mashariki ya Mto Yordani.Yoshua aliwaambia waandae chakula,kwa maana baada ya siku tatu wangevuka mto Yordani"ili kuingia na kumiliki nchi".

 

FUNDISHO KWETU.

Yoshua aliagizwa na Mungu-"Kitabu hiki cha Torati kisiondoke kinywani mwako,bali yatafakari maneno yake mchana na usiku,upate kuangalia na kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo;maana ndipoutakapoifanikisha njia yako,kisha ndipo utakapostawi sana"(Yosh.1:8).Lazimahuu uwe ndiyo utaratibu wa maisha yetu.Na kamwe tusiache siku kupita bila kusoma Biblia zetu ya kuyafikiria kwa uangalifu maneno ya Mungu jinsi gani hasa yanavyotuhusu.

 

KWAUKUMBUSHO ZAIDI.

Daudialifahamu na alipenda sheria ya Mungu;aliitafakari na akapata mwongozo wa maisha yake."Heri waliokamilika njia zao,waendao katika njia za BWANA.Kwamausia yako najipatia ufahamu ndiyo maana naichuakia njia ya uongo.Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu"(Zab119:1,104,105).Kwa siku hizi ambazo ni rahisi kuongozwa na vibaya na ulimwengu unaotuzunguka,tunawezakupata msaada na kutiwa moyo na neno la Mungu,kma tuaruhusu neno lake lituongoze.Zaidi ya haya pia,Neno la Mungu,"linawezakutuhekimisha hata kupata wokovu kwa njia ya imani iliyo katika Kristo Yesu",kama mtume Paulo alivyomwambia Timotheo(2Tim3:15).Imani maana yake ni"kusadiki".Yoshua aliamini kuwa Mungu atawapeleka katika Nchi ta Ahadi.Alisadiki kuwa Mungu tawasaidia kuwafukuza wale wenyeji waovu wa nchi.Na ndiyo maana alikuwa mtu anayefaa.

 

MASWALI.

Majibu mafupi

1.Kiongozi mpya alichaguliwa baada ya Mungu kumwambia Musa kuwa hataingia pamoja nao. Ninani aliyekuwa kiongozi mpya?

2.Yoshua aliagizwa kuwa afanye nini kila siku?

3.Ni wapi kambi ya Waisraeli ilipokuwa kabla ya kuvuka kuingia Nchi ya Ahadi?

4.Ni siko ngapi Waisraeli waliagizwa kujiandaa kabla ya kuvuka na kuingia Nchi ya Ahadi?

 

Majibu ya Kina

1.Ni sifa zipi zilizomwezesha Yoshua kuwa mtu anayefaa kuwaongoza Israeli?(Zimetajwa nne katika somo hili)

2.Mungu alimtia nguvu Yoshua kwa ajili ya kazi.

a)Je,Mungu alimwambia nini katika kumtia nguvu?

b)Je,Mungu alimwambia afanye nini kila siku?

c)Je,Yoshua ni kwa jinsi gani alivyo kielelezo kwetu katika hili?

 

Majibu ya Nyongeza.

3.Ni kwa vipi kusoma Biblia kila kunaweza kutusaidia katika maisha yetu?

 

Swahili Title
031 KIONGOZI MPYA
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type