CSSA 1-2-12 - JOSHUA TURNS NORTHWARD

Swahili

37. YOSHUA ANAELEKEA KASKAZINI.

"Nayo nchi ikatulia isiwe  na vita tena.

 

Shabaha

       Kuonyesha kwamba tunapaswa kuwa na bidii katika kutii amri ya Mungu kama tunatamani kuingia katika ufalme .

Muhtasari

     Kama vile Mungu alivyowaongoza salama Waisraeli walipokuwa na Musa jangwani,na vivyo hivyo Mungu sasa alivyokuwaakiwaongoza  kwenda Nchi ya Ahadi wakiwa na kiongozi wao Yoshua.

 Ilikuwa ni lazima mataifa saba ya Kanaani yaangamizwe kabla Israeli hawajaanza kukaa katika nchi ambayo Mungu aliwapatia . Wakanaani walikuwa ni maadui wenye nguvu sana lakini baada ya miaka sita ya vita ,kampeni ya mwisho ya kutwaa nchi ilikuwa imekwisha fanyika na Yoshua “akaitwaa hiyo nchi yote sawasawa na hayo yote BWANA aliyokuwa amemwambia Musa” (Yoshua 11:14 na 18:1-10)

 

DALILI ZA KUTISHA KUTOKA KASKAZINI :Yoshua 11:1-5

 Yoshua alishafanikiwa kuangamiza miji ya kusini na ile ya Kanaani ya kati bado alikuwa amebakiza sehemu ya kaskazini ambayo alikuwa hajaishinda. Wakati Yabini mfalme wa Hazori alipopata habari, naye ndiye alikuwa kichwa cha hizo falme alituma ujumbe kwa wote ili wakusanyike pamoja kupigana na Israeli. Lilikuwa ni kusanyiko la jeshi kubwa mno kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi pamoja na farasi na magori mengi sana (msitari wa 4) wakapanga mahema yao pamoja hapo penye maji ya Meromu. Hili lilikuwa jeshi kubwa mno kuliko majeshi yote aliyowahi kupigana nayo Yoshua. Na siyo tu kwamba walikuwa jeshi  kubwa mno lakini pia walikuwa na farasi na magari wakati jeshi la Israeli walikuwa wote wanatembea kwa miguu. Bila msada wa Mungu, Waisraeli wasingethubutu kujongelea jeshi la namna hiyo .

MUNGU ANAMTIA NGUVU JOSHUA Joshua 11:6
Kabla hawajaingia Kanaani Musa aliwaambia Israeli wasiogope watakapo kuwa wanaenda vitani, hata kama maadui wataonekana wenye nguvu sana kuliko wao " kwakuwa bwana Mungu wako yu pamoja awe kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi (Kumb 20:21) Yoshua alifahamu kuwa Mungu yu pamoja na Israeli na imani yake ilitiwa nguvu na maneno ya Mungu yenye faraja. Usiwache wewe kwa ajili ya hao kwani kesho wakati kama huu nitawatoa hali wameua wote mbele ya Israeli (mst 6)

SHAMBULIZI LA KUSHTUKIZA LA JOSHUA: Joshua 11:7-9

Majeshi ya Yabini walipiga mahema yao karibu maji ya Maromu upande wa kaskazini. Nchi ilikuwa ya tambalare hivyo ilikuwa sehemu zuri kwa kutumia farasi na magari. Na wakati huo yamkini Yoshua alikuwa huko Gilgali umbali wa km 100 kutoka kusini. Aliamua kuwashtukiza maadui zake kama alivyofanya kule Gibeoni.     Na hivyo jeshi lake likaelekea upande wa  Kaskazini haraka sana na kuwafikia  Wakanaani,ambao hawakuwa wamejiweka tayari kukakabiri aina ya yoyote ya mashambuluzi kwa wakati huo.Hawakuwa na nafasi ya kukutumia magari yao wakiwa katika hali ya kuchanganyikiwa wakatawaanyika, “BWANA akawatia mkononi mwa Israeli ,nao wakawapiga na kuwafukuza hata na  hata wasiwasaze hata mtu mmoja aliyesalia”(mstari wa 8).Farasi wakaharibiwa na magari yakateketezwa kwa moto kama  Mungu alivyokuwa amewaagiza.Waisraeli hawakupaswa kuweka tumaini katika vitu hivyo,bali walipaswa kukumbuka  kuwa Mungu ndiye aliyewapatia ushindi(soma Zabri33:16-22)

 

WAKANAANI WANASHINDWA –KISHA  NCHI INATULIA:Yoshua 11:10-23

   Baada ya kushinda jeshi la Yabini,Yoshua aliitwaa miji ya wafalme hao waliokuwa wameungana jeshi la Yabini na kuwaangamiza wenyeji waovu wa miji hiyo,kama vile Mungu alivyomwamru Musa.Yoshua alikuwa amemshinda mfalme mwenye nguvu sanawa Wakanaani na hivyo nchi ikatulia “isiwe na Vita tena”(mstari wa 23)

 

KUGAWANYWA KWA NCHI:Yoshua 18

 Kabla ya kuingia nchi ya Kanaani makabila ya Rubeni,Gadi na nusu ya kabila la Manase walikuwa wamemwuliza Musa kuhusu nchi iliyokuwa upande wa Mashariki wa Yordani,maana ilikuwa nchi nzuri kwa ajili ya mifugo na sehemu hii walikuwa wamepewa(Yoshua12:6).Kwa sababu hiyo Mungu alimwgiza Yoshua kuigawa nchi ya Kanaani kwa njia ya kura kwa makabila tisa na nusu yaliyokuwa yamesalia.Kumbuka kuwa yalipatikana makabila mawili kwa Yusufu;Efraimu na Manase(Yoshua 14:4).

 Lakini Walawi hawakupewa fungu lolote katika nchi kuwa urithi wao,“kuwa huo ukuhani wa BWANA ndiyo urithi wao”(Yoshua 18:7) Walawi walipewa miji 48 katika nchi yote,kila kabilalilitoa miji kadhaa,kwa kuwa Mungu alikuwa ameamru kwamba wapewe miji wakae,ikwa ni pamoja na maeneo ya kuchungia mifugo yao(Yoshua 21:1-3).Walipaswa wakae katika ya watu ili kuwafundisha njia za Mungu na sheria zake.

 

FUNDISHO KWETU

Yoshua aliendelea kuwa mwaminifu katika hazi aliyopewa na Mungu aifanye. Hata pale alipokaliliwa na la Yabini alikuwa shujaa na mkweli. Alifahamu kuwa angetumainia Msaada wa Mungu. “Hawa wanataja magari na hawa wanataaja farasi; bali sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu” (Zab 20:7). Mungu aliyemsaidia Yoshua ,ndiye  Mungu  ambaye atatusaidia sisi katika taabu zetu leo. Tunayomatumaini ya kuishi katika Nchi hiyo milele, muda umekaribia. Kwa hiyo tumaini la Yoshua ndilo tumaini letu pia na anaweza kuwa mfano kwetu. Ilichukua miaka mingi kuweza kuiteka Nchi yote, hata hivyo hakusita wala hakupoteza tumaini lake kwa Mungu.

MAELEZO YA NYONGEZA.

KALEBU - MTU MWENYE IMANI: Yoshua 14.

Baada ya makabila kupewa  sehemu zao katika Nchi, waliambiwa waende wakae katika sehemu zao na kumiliki hiyo Nchi. Walipaswa kwenda na kuishi huko kabisa na Wakanaani. Wengi wao walikosa imani na ujasiri wa kufanya hivyo, bali alikuwepo mtu mmoja aliyeonyesha imani kubwa kabisa. Ilikuwa kama miaka 45 iliyopita, kalebu alikuwa kati ya wale wapelelezi wawili waaminifu waliorudi kwa Musa wakiwa na taarifa nzuri ya Nchi ile. Kwa sababu ya uaminifu wake, Mungu alimwahidi Kalebu kumpatia wake Urithi wa kwake katika Nchi ya Kanaani (Yosh 14:9 Kumb 1:1-36). Tunasoma kuwa  “Yoshua akambarikia, akampa Kalebu, huyo mwana wa Yefune, Hebroni kuwa urithi ”  (mstari wa 13).Akiwa na miaka 85,hakusita kwenda  kumilki urithi wake. Kazi ilikuwa ngumu bali alitegemea msaada wa Mungu na kufanikisha (mstari 12) “ Hata sasa mimi nina nguvu zangu hivi leo kama nilivyokuwa siku hiyo Musa aliyonituma; Kalebu alisema yumkini BWANA atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza watoke nje” (mstari (11,12).

MASWALI

Majibu Mafupi.

  1. Yabini mfalme wa Hazori alifanya nini aliposikia kuhusu ushindi wa Yoshua ?
  2. Jeshi la Yabini liliweka kambi wapi?
  3. Ni kwa jinsi gani jeshi la Yabini lilikuwa tofauti na jeshi la Israeli?
  4. Ni mbinu gani Yoshua aliyoitumia kushambulia jeshi la Yabini ?

 5.  Yoshua aliwatenda vipi farasi na magari ya Yabini?

6.Yoshua alipokwisha kuwashinda Wakanaani alifanya nini baadaye?

7.Ni makabila mangapi yaliyopata sehemu kuwa urithi wao katika Nchi ya Kanaani ? 8.Walawi walipewa nini badala ya sehemu ya Urithi wao katika Nchi?

 9.Ni fundisho gani tunalopata kutokana na habari ya Yoshua kulishinda jeshi kubwa mno la Yabini ?

Majibu ya Kina.

  1. Vita ya mwisho ya Yoshua ilipiganiwa eneo la Kanaani ya Kaskazini.

 a)Tofauti ilikuwa ipi kati jeshi la Yoshua na jeshi la Yabini mfalme Hazori?

 b) Ni nani aliyeshinda vita hiyo na kwa njia gani?.

2.Wakati Yoshua alipowashinda Wakanaani; kazi iliyofuata ilikuwa kuigawanya nchi. a)Ni makabila mangapi yaliyopata sehemu katika Kanaani? b)Ni jinsi gani Mungu alivyowatunza Walawi?

Majibu ya Nyongeza.

3. Kalebu alikuwa ni nani,na ni jinsi gani alivyoonyesha  imani yake na ushujaa wake ?

 

 

Swahili Title
037 YOSHUA ANAELEKEA KASKAZINI.
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type