CSSA 1-2-17 - RUTH

Swahili

42. RUTHU

“Watu wako watakuwa watu wangu na Mungu wako atakuwaMungu wangu.”

Shabaha

Kuonyesha kwamba Mungu atawabariki wanofanya kazi kwa uaminifu.

 

Muhtasari

Kitabu cha Ruthu ni cha nyakati ambapo waamuzi walitawala. Ulikuwa wakati ambapo Israeli hawakuwa na mfalme na kila mtu alifanya lililoonekana kuwa jema machoni pake mwenyewe. (Waamuzi 21:25) .Walakini tunafahamu kwamba wapo kila wakati watu wachache walio waaminifu kwa Mungu hata wakati ambapo wengine wote ni waovu.

 

Katika kitabu cha Ruthu tunajifunza juu ya baadhi ya watu waliomtumikia Mungu hata nyakati za Waamuzi  ambapo wengi sana waliacha njia yake. Kitabu hiki kinaonyesha jinsi mwanamke mpagani alivyofanyika kuwa mmojawapo wa watu wa Taifa la Israeli, na kushiriki katika baraka zao.

 

Ni jambo la kusisimua zaidi, kwa sababu Ruthu  alifanyika kilembwe (bibi wa bibi) wa mfalme Daudi  ni katika ukoo huu Yesu alizaliwa. Ruth 1:1-12; 4:9-22

 

RUTHU  MWAMAMKE MMOABU: Ruthu  1

Wakati wa njaa Elimeleki mtu wa Bethlehemu aliondoka nyumbani na kuvuka mto Yordani kwenda kuishi  Moabu. Alimchukua mke wake Naomi na watoto wao wa kiume wawili Maholoni na Kilioni.

 

Baada ya kukaa kwa muda fulani nchini Moabu, Elimeleki alifariki nao maholoni na Kilioni walioa  Ruth na Oripa, wanawake wawili wamoabu. Baada ya miaka kumi  wana wa Naomi wote wawili walikufa naye alibaki na wakwe wake wawili. Naomi aliposikia kwamba njaa iliisha katika nchi yake mwenyewe aliamua kurejea nyumbani kwake naye akaondoka na Ruthu na Oripa, ambao walimpenda sana. Walipoendelea kuelekea njia ya kwenda Yuda; Naomi aliwashauri wakwe zake kurudi kwa watu wao kwani hakuwa na chochote cha kuwapatia.Wote wawili walisema hawaangemuacha lakini baadaye Oripa alishaurika kurejea kwa jamii yake nchini Moabu.

   

Lakini Ruthu aliendelea kumsihi Naomi ,usinisihi nikuachea au nirejee nisifuatane nawe maana wewe uendako ndiko nitakwenda,na wewe ukaapo nitakaa;watu wako watakuwa watu wangu na Mungu wako atakuwa Mungu wagu .(mtari wa 16 na 17). Hivyo Naomi alirejea pamoja na Ruthu mwanamke mmoabu, mkwe wake pamoja naye walirudi kutoka nchi ya Moabu nao walifika hadi Bethlehemu  mwanzo wa mavuno ya shayiri (mstari wa 22).

 

MUNGU AMWONGOZA RUTHU: Ruthu 2:1-12

Ruthu alitambua kwamba watakaporudi Bethlehemu itamlazimu kumtunza Naomi kwa sababu walikuwa maskini sana. Mungu kwa wema wake alikuwa ametayarisha namna ya kutunza  katika sheria za Musa kuwa watu maskini wangekusanya chakula cha kuwatosha kutoka kwao walio na  vingi (Kumbukumbu la Torati 24:19-21).Wavunaji walipaswa kuacha vitoshavyo mashambani kwa ajili ya maskini kujikusanyia – “usivune kabisa pembe  za shamba  lako,wala usiyakusanye masazo ya mavuno yako...uyaache kwa ajili ya maskani na mgeni” (Walawi 19:9-10).

 

Ruthu alimwomba Naomi amruhusu kwenda kuokota mabaki ya masuke ya ngano Mashambani (“kuokota mabaki”maana yake ni kukusanya ngano au masazo yaliyoachwa na wavunaji). Sasa  ilimtokea yeye kwenda kwenye shamba lake Boazi, aliyekuwa tajiri,ndugu wa ukoo wa Elimeliki.Boazi alikuwa mtu mwema aliyempenda Mungu na kutoa sadaka ya shukrani kwa ajili ya mavuno yake makubwa. Aliwauliza wavunaji wake kuhusu mwanamke kijana aliyekuwa akiokota shambani mwake. Aliposikia ni nani, alisema naye kwa wema na kumweleza kuwa asiende mahali pengine popote kukusanya. Ruthu alikuwa na shukrani sana, naye hakuelewa yote haya akizingatia kuwa alikuwa mgeni. Boazi alieleza kwa upole kwamba alikuwa amesikia yote aliyomfanyia Naomi na kuhusu maisha mapya aliyoyachagua pamoja na watu asiowafahamu.

 

Kwa neema alisema “BWANA  na akujazi kwa kazi yako nawe upewe thawabu kamili upewe na BWANA ,Mungu wa Israeli ambaye umekuja kukimbilia   chini ya mabawa yake”(mstari 12). Baraka za Mungu wa Israeli zilimshukia Ruthu na kuongoza hatua zake kwenye shamba la Boazi.

 

MWISHO  FURAHA- BOAZI AMWOA RUTHU : Ruth 4:9-22

Habari hii ilikuwa na mwisho wa furaha katika ndoa ya Rutthu na Boazi. Muda ulipwadia mtoto wa kiume alizaliwa, naye walimwita Obedi. Obedi baadaye alikuja kuwa baba wa Yese; ambaye alikuwa baba yake Mfalme Daudi (mstari wa 22).Mlolongo mrefu wa ukoo (uzao) waweza kufuatwa kuanzia hapo, na miaka mamia  baadaye mwanadamu mkuu kulito wote waliowahi kuishi alizaliwa katika ukoo huu. Jina lake, bila shaka alikuwa Yesu Kristo.

 

FUNDISHO  KWETU:

Hii ni taarifa njema, ambayo inaonekana kung`ara mithili ya nuru katika siku za giza za Waamuzi. Imejaa upendo na wema . Upendo wa jinsi hii tunauona ndani ya Bwana Yesu Kristo, aliyezaliwa kutoka kwenye ukoo wa Ruthu na Boazi.Aliutoa uhai wake ili sisi tuwe na uzima. Paulo anasema  kuhusu huu upendo katika 1Wakorintho 13. Huvumilia yote na hufadhili, hauhusudu kwa walivyo navyo wengine, hautakabari nao huwatanguliza wengine. Sifa  hizi ndani ya Ruthu , ndizo zilizomvutia Boazi kwake. Upendo  wa jinsi hii kwa mtu kwa mwingine, huundeleza  tabia ambayo Bwana Yesu Kristo anapenda kuiona.

 

MAELEZO YA ZIADA

Kwa mara nyingine tena,  Maagizo kuhusu huruma  kwa maskini na wajane ilioonyeshwa katika sheria ambayo Mungu alimpatia Musa.Iwapo mtu alikufa naye hakuwa na watoto, ndugu yake au jamaa wa karibu (katika ukoo) alipaswa kumuoa mjane wa marehemu ili kwamba watoto wazaliwe kuendeleza jina lake na urithi .Kwa njia hii jina la mtu huyo halingeweza kusahauliwa naye mjane angetunzwa (Kumbukumbu 25:5-6). Mungu ni Baba yetu wa mbinguni na ndiye tunayemtegemea (zaidi ya baba zetu wa duniani) kwa ulinzi. Wana  wa Israeli walikuwa watoto wa Mungu. Hivyo sheria za Musa ziliwafundisha kuwa waangalifu na wema kila mmoja kwa mwenziwe.

 

Waliokuwa maskini wangeweza kila wakati kutazamia msaada kutoka kwa ndugu  zao wa karibu ( Mkombozi wao).Utakuwa umekisia kwa sasa kuwa Boazi angeitwa “mkombozi” wa Ruthu na Naomi. Alikuwa ndiye ndugu yao tajiri, ambaye angeweza kuwasaidia kwa shida yao.

 

Walakini, alikuwepo ndugu wa karibu ambaye alikuwa na haki  ya kumwoa Ruthu, lakini hakutaka kufanya hivyo. Hivyo haki ya kufanya hivyo alipewa Boazi. Alikuwa na uwezo mzuri wa kumwoa na kupata watoto ili kuwe na mtu mmoja  wa kuendeleza jina la ukoo. Katika Israeli, hii iliitwa sheria ya ukombozi. Boazi alizidi  kumpenda Ruthu nao wakaoana.

 

Hii ndiyo historia ya mwanamke  mmataifa,Ruthu ambaye alikuja kumpenda Mungu wa Israeli. Alitunzwa na kulindwa na mkombozi wake Boazi ambaye alikuja kuwa mume wake. Matokeo yake, walimtunza Naomi;ambaye alipata raha sana kwa mjukuu wake Obedi.

 

MASWALI.

Majibu   Mafupi

1. Kwa nini Elimeleki na familia  yake waliondoka Bethlehemu?

2 .Nini kiliwatokea Elimeleki na watoto wake katika nchi ya Moabu?

3. Nani alimbatana na Naomi aliposafiri kurudi nchini kwake?

4.  Ni wakati wa majira gani ya mwaka Naomi na Ruthu walirudi Bethlehemu?

5. Nani alikuwa mwenye shamba alikokwenda Ruthu kuokota masazo ya shayiri  iliyovunwa?

6. Nani aliyeongoza hatua za Ruthhu kwenye shamba lile?

7. Alifanya nini Ruthu shambani mwa Boazi?

8. Mtoto wa kiume  alizaliwa kwa Ruthu na Boazi  .Jina lake aliitwa nani?

9. Je unaweza kutaja  majina ya baadhi ya watu wakuu waliotokana na familia ya Ruthu na Boazi?

Majibu ya Kina

1.) a).Kwa nini Elimeleki na familia yake walikwenda  nchi ya Moabu?

    b).  Nini kiliwatukia walipokuwa kule?

   c). Kwa nini Naomi aliamua kurudi Israeli?

2). Ni maneno gani mazuri aliyoyasema Ruthu kwa Naomi baada ya Naomi kuwaambia Ruthu na Oripa kurejea kwao Moabu?

3) a). Ni jinsi gani Ruthu alimtunza Naomi walipowasili Bethlehemu?

b). Baozi alimfikiriaje Ruthu?

Majibu ya ziada

4 .Ni kwa jinsi gani sheria ya Mungu ili tosheleza mahitaji ya watu maskini kama Naomi na Ruthu?

  1. Ni jinsi gani Boazi alikuja kuwa Mkombozi wa Ruthu?

 

 

Swahili Title
042 RUTHU
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type