47. DAUDI NA GOLIATHI
“Vita ni ya Bwana”
Shabaha
Kuonyesha jinsi Daudi alivyopata nguvu kwan njia ya kumwamini Mungu.
Muhtasari
Maisha ya mchungaji wa kondoo, wakati wa Daudi yalikuwa ya upweke na mara nyingine talikuwa ya hatari. Ilimpasa kulinda makundi yake dhidi ya wanyama wa porini na wakati huo huo kuwaongoza kwenye malisho mazuri. Siku moja simba alikuja na kuchukua mwana kondoo kutoka kundini mwa Daudi; na wakati mwingine dubu naye alifanya hivyo hivyo( 1 Samweli 17:34,35).Lakini Daudi alimwamini Mungu aliyemsaidia kuwaua wale wanyama wa porini na kuokoa kondoo wake .Mungu alikuwa mchungaji wa Daudi, kama vile Daudi alivyokuwa mchungaji wa kondoo wake (Zaburi 23). Mungu alimfundisha Daudi kumtegemea yeye kwa ulinzi na ndiyo maana hakumuongopa hata Goliathi (1 Samweli 17)
CHANGAMOTO KALI KUTOKA KWA MFILISTI ALIYEKUWA JITU LA WAFILISTI: (1 Sam.17:1-11)
Wafilisti walikuwa adui wa muda mrefu wa Israeli katika siku ambazo Samweli alikuwa mwamuzi ,Mungu aliwasaidia Israeli dhidi yao nao walipigwa na kufukuzwa mbali na miji ya waisraeli .Muda fulani baada ya samweli kumpaka mafuta Daudi, hawa wafilisti waliivamiaIsraeli tena. Kwa hiyo, Mfalme sauli alikusanya jeshi lake kuwalinda watu wa Mungu dhidi ya adui zao. Jeshini walikuwamo wana watatu wakubwa wa Yese.
Majeshi hayo mawili yaliweka kambi kwenye mitelemko ya milima miwili yakikabiliana pembeni mwa bonde la Ela ambalo lilikuwa katiakati ya majeshi yote mawili. Mfilisti mkubwa sana kutoka kambi ya Wafilisti,Goliathiti alijitokeza mbele ya jeshi la wafilisti kuwatukana ,”Nayadharau majeshi ya Israeli leo” alipiga kelele. “Nipatieni mtu nitakayepigana naye" (mstani wa 10).Siku baada ya siku kwa siku arobaini alisemamaneneno yaleyale, lakini hakuwepo Mwisraeli aliye diriki kupokea changamoto yake kwa kukabiriana naye. Goliathi alikuwa jitu kubwa karibu mita tatu kwa urefu. Alikuwa askali mzoefu (mistali4,33) ambaye alifunikwa mavazi ya shaba tokea kichwani hadi vidole vya miguuni. Hata mfalme Sauli, aliyekuwa “kuanzia mabegani hadi kichwani alikuwa mrefu kuliko Waisraeli wote“ hakuwa jasiri kiasi cha kukubaliana naye.
Karibu muda huo Yese alimtuma Daudi kuona maendeleo ya kaka zake watatu na kuwapatia chakula. Mara baada ya kuwasili Daudi, Goliathi alijitokeza, akipiga kelele kwa maneno ya changamoto yake ( mstari wa 23 ). Wakati waisraeli walipomsikia walikimbia “kwa woga mkuu“ lakini Daudi alisikia maneno yake ya kujivuna, naye akawauliza askari kilichokuwa kinaendelea.
DAUDI AKUBALI KUKABILIANA NAYE: (Samweli 17: 32 – 40)
Daudi aliposikia maneno ya Goliathi, aliweza kuona mara moja jinsi yalivyokuwa ni matusi kwa Mungu wa Israeli. Anadiriki vipi huyu mfilisti “kuyadharau majeshi ya Mungu aliye hai!" (mstari wa 26 ).Goliathi hakumjua Mungu wa Israeli. Hakumbua kwamba ni “Mungu aliye hai,“ ambaye angewaokoa upesi sana waisraeli kutoka kwa maadui zao, iwapo wangekuwa na imani itoshayo kwake. Lakini hakuwepo hata mmoja ndani ya jeshi lote la Israeli, waliokuwa katika kambi ya jeshi katika bonde la Ela, aliyekuwa na imani ya kweli kwa Mungu, kwenda na kumkabili Goliathi. Hivyo Daudi, alikuwa amejaa imani, alimwendea mfalme Sauli na kusema, “Asizimie moyo mtu yeyote kwa ajili ya huyu; mtumishi wako atakwenda kupigana naye huyu mfilisti. ( mstari wa 32 ). Akamweleza Sauli jinsi Mungu alivyomsaidia na kuwaokoa kondoo wake mkononi mwa Simba na Dubu. Angemwua huyu shujaa wa Wamfilisti , kama alivyowauwa wale wanyama wa porini. “BWANA aliyeniokoa kwenye makucha ya Simba na makucha ya Dubu ataniokoa kutoka mikononi mwa mfilisti huyu,” ( mstari wa 37 ).
Sauli alikubali.alipoona imani kuu aliyokuwa nayo Daudi, Alishauri Daudi avae mavazi ya Sauli ya vita ili ajihami na Goliathi. Daudi hakuwa amezoea mavazi ya vita mazito. Alihitaji fimbo yake tu, kombeo na “mawe laini matano kutoka katika kijito“ ( mstari wa 40 ). Alimwamini Mungu ,kumlinda.
KUPIGANA VITA VYA MUNGU KWA IMANI: (1 Sam. 17: 41 – 52)
Daudi alikwenda moja kwa moja kukutana na Goiliathi ( mstari wa 40 ). Mfilisti alishangaa kwamba hatimaye mmoja alipata ujasiri kwenda kupigana naye, lakini alipomwona kijana mdogo tu akitokea kukabiliana naye, akiwa na fimbo na kombeo, alimdharau na kumkejeli Daudi “Je,mimi ni mbwa,” alinguruma,, “kwamba unanijia na fimbo?” “ Naye mfilisti huyo akamlaani Daudi kwa Miungu yake. “ (mstari wa 46 – 47).
Na vita sasa vilikuwa ni vita kati ya Mungu wa Israeli na miungu ya wafilisti. Hivi ndivyo alivyoona Daudi pia, kwani alisema , “wewe unanijia na Upanga, na mkuki, na ngao, lakini mimi nakujia katika jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli, uliowatukana. Leo hii "BWANA atakutia mkononi mwangu” (Mstari wa 45 ). Daudi alitaka kila mmoja kujua kwamba haikuwa kwa minajili ya heshima yake binafsi, bali kwa ajili ya heshima ya Mungu wa Israeli kwamba alikuwa anapigana “ ili kwamba dunia nzima wote upate kujua kwamba yuko Mungu katika Israeli. Na kusanyiko lote (yaani, watu wote wa Israeli) watajua kwamba BWANA haokoi kwa upanga wala kwa mkuki, kwani vita ni ya BWANA, naye atawatia mikononi mwetu. (Mstari wa 46 – 47).
Bila shaka maneno ya ujasili ya Daudi yalimkasirisha Goliathi. Alisimama na kukimbia kuvuka bonde ndani ya mavazi mazito ya vita kuelekea kwa Daudi. Naye Daudi akakimbilia kuelekea kwa adui yake, akiweka jiwe ndani ya kombeo lake wakati anakwenda. Akalizungusha zungusha na kuliachia akimwamini Mungu kuliongoza. Na ndivyo Mungu alivyofanya, kuonyesha kwamba imani ya Daudi ilikuwa tegemeo bora zaidi kuliko kutumainia upanga na mkuki. (Mstari wa 47). Jiwe likavuma na kumpiga shujaa katika kipaji cha uso,naye akaanguka chini kwa kishindo.
Kisha, kwa upanga wake Goliathi mwenyewe,Daudi akamkata kichwa yule jitu. Wafilisti walipoona kwamba shujaa wao amekufa walikimbia kwa hofu. Waisraeli waliruka, wakipiga kelele za shangwe. Daudi alikuwa ameshinda kwa imani na hili liliwapa moyo wote. Wakiwa wenye mori na hakika ya ushindi, waliwafuatia wafilisti mpaka kwenye malango ya Ekroni, huku wafilisti wengi walikuwawameuawa njiani. Ushindi wa Mungu ulikuwa umekamilika. Sasa wote wakajua kwamba “yumo Mungu katika Israeli”. (Mstari wa 46).
Daudi alitukuzwa sana na mfalme Sauli ambaye alimweka jeshini mwake. Miaka mingi baadae, baada ya kufa Sauli, Daudi alifanyika mfalme wa Israeli.
FUNZO KWETU.
Ushindi wa Daudi juu ya Goliathi unatufundisha moja ya masomo muhimu sana yayopatikana ndani ya Biblia :- Imani kwa Mungu wa kweli ina nguvu halisi. Mungu hatuelekezi sisi kumwua jitu, lakini anatutaka sisi kuonyesha imani sawa na Daudi. Daudi hakika alimwamini “Mungu aliye hai“ naye aliweza kuonyesha hilo kwa ujasiri katika kupigana vita na adui za Mungu. Sisi tunaweza kuonyesha imani kwa Mungu aliye hai katika yale tunayo yatenda na kusema kila siku. Kila wakati tukiamua kufanya linalompendeza Mungu, hapo tumeshinda vita – kwa kuwa tunapomwasi Mungu, tunakuwa adui zake. Hebu na tumtii Mungu na kujifunza kuwa na imani kwake sawa na alivyofanya Daudi.
MAELEZO YA ZIADA
Tunaweza kwa urahisi kabisa kuwa adui za Mungu sisi wenyewe, kama vile Goliathi. Siyo wazo zuri, au sivyo, kwa sababu ni kweli tunahitaji kumpenda Mungu. Amefanya mengi kwa ajili yetu. Lakini, tukiwa wakweli katika nafsi zetu, tutakubali kwamba mara nyingi tunafikiri mawazo yasiyo mema, tunafanya upumbavu au hatuwatii wazazi au walimu wetu. Nyakati zingine tunasahau kufanya mambo mema, ambalo hili ni baya vile vile. Kwa njia hizi tunafanyika adui za Mungu. Njia moja tu ya kuwa mwaminifu, kama Daudi , ni kujaza akili zetu na mawazo ya Mungu kutoka Biblia na kujifunza masomo kutokana na mifano ya wanaume na wanawake waaminifu, ambao tunawasoma humo. Hivyo ndivyo hasa hata Bwana Yesu Kristo alifanya wakati wote.Kamwe,hata mara moja hakuteleza na kumtenda dhambi Mungu. Hakuwahi kuwa na ubongo kimwili, akitaka kujipendeza mwenyewe; alikuwa na ubongo wa kiroho – mawazo yake wakati wake yalikuwa mawazo ya Mungu. Ilikuwa vita maisha yake yote, na kwa msaada wa Mungu, alishinda vita hiyo, naye sasa anaishi milele katika mkono wa kuume wa Mungu.
Inatupasa tuyaone maisha yetu sawa na hivyo kabisa – vita ndani ya akili zetu kuhusu mawazo ya Mungu dhidi mawazo ya ubinafsi.
Mtume Paulo katika waraka wake kwa Timotheo alibainisha vitu vingi viovu alivyowahi kuviona watu wakivifanya na kumwambia Timotheo: “Lakini wewe, mtu wa Mungu, yakimbie mambo haya; nawe fuata haki, utawa, imani, upendo, saburi, na upole, pigana vita vile vizuri vya imani; shika uzima wa milele, ulioitiwa ( 1Timothy 6: 11 – 12 ). Kama tunaendelea kujaribu, Mungu atatusasidia na sisi pia tutapewa ile zawadi yenye utukufu ya uzima wa milele wakati Bwana Yesu Kristi atakaporudi.
MASWALI:
Majibu mafupi:
1.Ni namna gani Daudi aliwalinda kondoo wa Baba yake ili wasishambuliwe na wanyama wa porini?
2. Ni nani waliokabiliana kwenye bonde la Ela?
3.Je,Waisraeli walifanya nini walipomwona Goliathi?
4.Je, Goliathi alionekanaje?
5.Ni silaha gani Goliathi alikuwa nazo?
6.Ni silaha gani Daudi alichagua?
7.Ni jinsi gani Daudi aliweza kumwua Goliathi?
8.Wafilisti walifanya nini walipomwona shujaa wao amekufa?
Majibu ya kina:
1. (a) Daudi alijihisi vipi aliposikia maneno ya Goliathi?
(b) Daudi alifahamu vipi kwamba angeweza kumshinda Goliathi?
2. (a) Goliathi alisema nini alipomwona Daudi?
(b) Je, vita hii ilikuwa kati ya Daudi na yule yule jitu?
3. Malizia nukuu ifuatayo: “Wewe wanijia na upanga ………” ( 1Samweli 17: 45 )
4. Je, Daudi alitaka nini?
(a)“ Dunia yote ijue”?
(b)“ Watu wote wa Israeli wajue”?
Majibu ya nyongeza:
5. Eleza tukio la vita kati ya Daudi na Goliathi. (Anzia na kufika kwa Daudi katika kambi ya Israeli kuwaona kaka zake).
6.Tuna vita akilini mwetu kila siku.
(a)Tunawezaje kuwa waaminifu, kama Daudi?
(b)Ni nini Mungu atatupatia iwapo tutaendelea kujaribu kumpendeza?