50. AHADI YA MUNGU KWA DAUDI
“Ufalme wako utaimarishwa milele mbele yako”
Shabaha
Kuonyesha kwamba ahadi alizopewa Daudi zitatimizwa na Bwana Yesu Kristo.
Muhtasari
Zamani za kale, Mungu alimwambia Musa nia yake kwa dunia "Kama niishivyo,tena kama dunia hii nzima itakayojawa na utukufu wa BWANA" (Hesabu 14:21). Mungu atatimiza haya atakapomtuma Bwana Yesu Kristo, kurudi tena ulimwenguni kutawala kama Mfalme katika kiti cha enzi cha Daudi. 2 Sam. 7: 1-17.
MAPENZI YAKE DAUDI YANAKATALIWA: 2 Samweli 7:1-7
Sasa, akiwa mfalme wa Israeli na Mungu akiwa amemstarehesha asiudhiwe na maadui zake, Daudi alitambua jinsi Mungu alivyo wa ajabu alivyombariki. Alitaka kufanya kitu fulani kumwonesha Mungu jinsi alinavyomshukuru.
Ilimhuzunisha Daudi, kufikiri kwamba yeye hali anaishi ndani ya Ikulu nzuri; iliyojenga kwa mbao safi za mielezi bali sanduku la Mungu lilikaa ndani ya hema ambayo aliitengeneza juu ya mlima Sayuni.
Daudi alitamani kujenga hekalu kuu na nzuri ambamo angeliweka sanduku la “Mungu aliye hai” ambaye Daudi alimwabudu.
Alimwambia Nathani Nabii, mapenzi yake. Nathani aliwaza kuwa lilikuwa jambo zuri na kumwambia Daudi aendelee,"Fanya yote yaliyomo moyoni mwako",Nathani alimwambia maana BWANA yuko pamoja nawe (mstari wa 3). Lakini Nathani alikuwa amekosea.Ikawa usiku uo huo Mungu alisema na Nathani,na alimwambia kwamba Daudi hatamjengea Bwana hekalu.Daudi alikuwa mpiganaji na aliua watu wengi katika vita vyake.Haikustahili kwamba mtu wa vita wa aina hiyo ajenge nyumba ya kumwabudu Mungu. Badala yake Mungu aliahidi kumpatia Daudi mtoto,ambaye atakuwa mtu wa amani na huyu mtoto atajenga nyumba ya Mungu(I Nyakati22:7-9).Lakini Mungu si kana kwamba hakupendezwa na Daudi,katika kutaka kumjengea Mungu hekalu ,hata hivyo alionyesha tena kwamba alikuwa "mtu aupendezaye moyo wa Mungu".Kwa jambo hili Mungu alimpenda(hata hivyo ,jina "Daudi linamaanisha mpendwa") na kumheshimu kwa kumpatia ahadi iliyo sisimua inayopatikana katika 2 Samweli 7.
MWANA WA DAUDI AMBAYE NI MWANA WA MUNGU: 2 Samweli 7:12-17
Kwa kuwa lengo la Mungu ni kuweka Ufalme,hakika anahitaji Mfalme.Kwa kuwa utakuwa ufalme wa Mungu,mfalme wake ni lazima awe safi na mwenye haki.Kwa hiyo;katika ahadi hiyo kwa Daudi,Mungu alizungumzia kuhusu mtu huyo ambaye angeweza kutawala katika Ufalme Wake.Ahadi kwamba mfalme atakuwa wa uzao wa Daudi moja kwa moja.
Mamia ya miaka ingepita, kabla ya Mfalme wa haki kuzaliwa; na Daudi kwa wakati huo angekuwa amekwisha fariki (mstari wa 12). Kitu kinachosisimua kuhusu ahadi hii ni kwamba hiki kizazi cha Daudi, pia atakuwa mwana wa Mungu. Hataweza kutenda dhambi lakini atateswa na kufa kwa ajili ya kuwaokoa wengine ambao wanafanya dhambi (mstari 2wa 14). Mungu aliahidi kumfanya huyu mfalme wa ajabu milele ili aweze kutawala katika ufalme wa Mungu milele (mistari ya 13, 16) itakuwa ni kazi ya huyu mfalme kujenga hekalu la Mungu pia.
Haya mambo yote yatatimizwa katika Bwana Yesu Kristo. Malaika Gabrieli alimwambia hivi Maria, Mama wa Yesu kabla hajazaliwa,kuwa Yesu ni mwana wa Daudi aliyeahidiwa na pia ni mwana wa Mungu (Luka 1:32:35).
Ni mfalme Mkuu wa Israeli atakayetawala ufalme wa Mungu milele (Luka 1:33).
Hata hivyo yesu bado hajatawala kama mfalme wa Israeli, na bado hajakaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi(Matendo 2:31). Na sasa amefufuliwa ,kutoka kwa wafu na kupaa, atakaa mbinguni mpaka muda utakapoamriwa wa kurudi kwake hapa duniani (matendo 3:20-21). Ni wakati huo tu atakapo kaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala katika ufalme wa Mungu duniani. Mungu alisema ,"Uketi mkono wangu wa kuume,hata nitakapowaweka adui zako kuwa kiti cha kuwekea miguu yako" (Zab. 110:1). Kwa namna hiyo hiyo, Daudi naye alisubiri kwa muda mrefu katika nchi ya wafalisti kabla ya kuwa mfalme mpaka Sauli alipofariki.
Ni muda mrefu tangu Bwana Yesu Kristo aende mbinguni, lakini muda wa kurudi kwake umekaribia (Zab. 102:13-18). Kama tulivyosoma katika somo la 24 (Maelezo ya Nyongeza) kurudi kwa Wayahudi katika nchi ya Israeli, ni ishara ya hakika kwetu kwamba kurudi kwake kumekaribia (Mungu aliwaondoa watu wake kutoka kwenye nchi ile zaidi ya muda wa miaka 1900 iliyopita kwa sababu walimuua Mwana wake. Ni katika muda wa maisha ya wazazi wako na mababu zako, ambapo Wayahudi wameanza kurudi katika nchi ile na sasa Israeli ni Taifa tena).
Yesu atakaporudi ,kuwa mfalme wa Israeli; na kujenga hekalu la Mungu, Daudi baba yake mtangulizi utafufuliwa kutoka kwa wafu. Hii ni sehemu ya maana ya ahadi kwa kuwa 2Samweli 7:12 inaahidi kwamba ufalme wa Mungu, utawekwa baada ya kifo cha Daudi, mstari wa 17,unasema ufalme ulioahidiwa utawekwa milele daima mbele ya Daudi.
Neno “mbele” lina maanisha mbele ya macho yake Daudi hasa.
Ili hili litokee hivyo ni lazima Daudi afufuliwe kutoka kaburini (Zaburi 71:20).
Natuchunguze mambo muhimu katika ahadi hii ambayo Mungu alimwahidi Daudi.
- Baada ya kifo cha Daudi mmoja kati ya wana wake (wazao) atakuwa mfalme kwenye kiti chake cha enzi.
- Atajenga nyumba kwa jina la Mungu, ambayo ni hekalu.
- Huyu mwana maalumu wa Daudi atakuwa mwana wa Mungu,Bwana Yesu Kristo.
- Hatafanya dhambi lakini atateswa na kufa kwa ajli ya kuwaokoa wengine.
- Daudi atafufuliwa kutoka kwa wafu na kumwona Kristo aliyethibitishwa kuwa mfalme mteule kwenye kiti cha enzi katika Yerusalemu.
Fundisho Kwetu.
Mungu alifanya ahadi za ajabu kwa Abrahamu, Isaka na Yakobo na pia kwa Daudi. Ahadi hizi zinaitwa "Tumaini la Israeli" (Matendo 28:20) na“ahadi baba zetu waliyopewa na Mungu”(Matendo 26:6). Ni tumaini la wayahudi kwa kuwa hawa watu wote walikuwa Wayahudi, lakini hata hivyo tunaweza kuwa watu wa mataifa Mungu amefanya hili liwezekane kwetu tushiriki katika tumaini hili, kwa njia ya ubatizo katika Kristo.Kwa yeyote anayeamini katika ahadi hizi (zilizoitwa katika Wagalatia 3:8"Injili") na akiwa amebatizwa anaweza kushiriki furaha ya uzima wa milele katika ufalme wa Mungu (Wagalatia 3:26-29).
Ni huruma ya ajabu ambayo Mungu ametuonyesha kwa kutupatia ahadi kuu na za thamani sana. Anatupa tumaini lile lile ambalo alimpatia Daudi – tumaini la uzima wa milele katika ufalme wake wa ajabu (2 Petro 1:2-4 Yohanne 3:16).
Ni lazima tujaribu kumpendeza Mungu, kwa mawazo yetu, kwa maneno yetu na kwa vitendo ; kama Daudi alivyofanya ili Mungu atufikirie sisi kama alivyomfikiria Daudi, kuwa "mtu anayeupendeza moyo wangu" Alitenda maovu hata fadhili za Mungu zikamwondokea(1Wafalme 11:9).Katika mambo haya yote,Sulemani hakutimiza ahadi za Mungu huu ni uthibitisho kwamba utimilifu kamili utatimizwa na Bwana Yesu Kristo.
MAELEZO YA NYONGEZA
Sehemu ya ahadi zilizotekelezwa na Selemani, mwana wa Daudi, lakini zitaweza kutimizwa kwa ukamilifu na Kristo tu. Ingawaje,Selemani aliyetawala baada ya Daudi, alijenga Hekalu la Mungu ;hakuwa ndiye Mwana wa Mungu wa ahadi. Maana alikuwa mfalme wakati Daudi alipokuwa hai (1 Nyakati 29 :20-24). Na ufalme wake haukudumu milele (1 Wafalme 11:11). Alitenda dhambi na Bwana akomwondelea fadhali zake(1Wafalme11 :9).Ni katika mambo haya yote,Selemani hakuweza kutimiza ahadi,ni uthibitisho kwamba utimilifu wake kamili utaweza kutimizwa na Bwana Yesu Kristo.
MASWALI
Majibu Mafupi
- Mungu alimwambia Musa kusudi lake kuu kuhusu dunia. Alimwambi nini ?`
- Daudi alitaka amfanyie nini Mungu?
- Ni kwa nini Daudi litaka kujenga Hekalu?
- Ni kwa nini Mungu hakumruhusu Daudi kumjengea hekalu?
- Je Mungu alifurahishwa na tendo la Daudi kutaka kujenga hekalu?
- Ni nani anayenenwa katika ahadi za Mungu kwa Daudi ambaye ni anatimiza yote kuwa Mwana wa Daudi na Mwana wa Mungu?
- Ni lini Yesu ataanza kutawala akiwa kwenye kiti cha enzi cha Daudi?
- Itatokea nini kwa Daudi Yesu atakaporudi?
- Kama tunaziamini ahadi za Mungu kwa Daudi, ni mambo gani mengine tunayopaswa kufanya ili tushiriki katika tumaini lake?
Majibu ya kina.
- Eleza mambo matano muhimu Mungu aliyomwahidi Daudi kuhusu uzao wake Mkuu.
2
(a) Daudi alikufa na akazikwa. Ni jinsi gani "ahadi zitafanywa imara milele mbele zake ?"
(b) Kwa sasa Kristo yuko wapi?
(c) Ni lini Kristo ataketi katika kiti cha enzi cha Daudi?
3
(a) Tumaini la Israeli ni lipi ?
(b) Ni jinsi gani tunavyoweza kushiriki katika tumaini la Israeli ?
MAJIBU YA NYONGEZA
4)Ahadi za Mungu kwa Daudi katika 2 Samweli 7 hazikumhusu kabisa Sulemani.
Toa sababu tatu kwa nini Sulemani siyo mwana wa Ahadi.
© CBM Publishing
32 Blenheim Road
Far Cotton
Northampton
United Kingdom
Email: Carl@CBM-tz.org
NGO Uk: 448979/1020558 Tz: 7328
Mtafsiri: Jonathan Nkombe
Mwandishi: Carl Hinton