54. UTUKUFU WA SULEMANI:
“Sulemani aliwazidi wafalme wote duniani kwa utajiri na hekima”
Shabaha
Kunyesha jinsi umaarufu wa Sulemani ulivyoenea katika nchi zote za Mungu kusifika. Sulemani alipomwomba Mungu kwa ajili ya hekima ,Mungu alimwahidia siyo hekima pekee bali hata utajiri na heshima pia, “ hivi kwamba hakutakuwepo yoyote kati ya wafalme kama wewe, katika siku zako zote” (1Wafalme 3:13).
Mungu hakuchelewa katika kutimiza ahadi yake na kabla ya muda mrefu dunia nzima ilifahamu umaarufu wa Sulemani (4:20-34; 10)
MUNGU ANAIBARAIKI ISRAELI CHINI YA SULEMANI:
1Wafalme4:20-28;10:16-20
Wakati Sulemani alipokuwa mfalme wa Israeli, Taifa lilipumzika kama Mungu alivyoahidi (1 Wafalme 5:4) Yuda na Israeli wakakaa salama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake” (1Wafalme 4:25). Watu walikuwa wameongezeka (wakazaliana) “kama mchanga wa ukingoni mwa bahari kwa wingi” (mstari 20). Walifurahi na kuridhika, kwani aliwatawala kwa hekima. Utawala wa enzi ya Sulemani ilipanuka hadi mto Frati kwa upande wa kaskazini na kufikia hadi mpaka wa Misri kwa upande wa kusini. Mataifa yaliyowazunguka yalikuwa na imani naye na umaarufu wake ulienea karibu mbali, kwa kuwa Israel lilikuwa taifa lenye nguvu.
Wafame wa nchi nyingine walimpelekea zawadi za dhahabu na fedha, na mavazi ya kupendeza,na viungo vya manukato na farasi (1 Wafalme 10:25) Watu wa Israeli nao walikuwa na shughuli, wakijenga majumba mazuri kufuatana na mpango wake. Alijenga hata bandari kubwa na kupeleka meli kwenda nchi za mbali, na kutoka huko walileta nyumbani dhahabu, fedha, pembe za ndovu, nyani na tausi (ndege wazuri sana) (1 Wafalme10:22). Akajenga ngome nyingi sana za kutunzia farasi wengi na magari mengi ya vita yaliyonunuliwa kutoka Misri (1 Wafalme10:26-29).
Na Israeli ikawa tajiri sana na kuwa mashuhuri na kuwa na utukufu zaidi kuliko taifa yote yaliyoizunguka.
HEKIMA YA SULEMANI: 1Wafamle 10:1-3
Huko Gibea Mungu alikuwa amemwahidi kumpa Sulemani hekima, utajiri na heshima. Kila mmoja haraka akaja kusikia juu ya hekima yake, kwani hekima yake “ilizidi hekima ya wana wote wa nchi za mashariki, na hekima yote ya Misri. Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote” (mstari 30-31). Mungu alimpatia ufahamu mpana wa vitu alivyoviumba. Alizungumzia juu ya miti ya mwerezi ulioko Lebanoni na hisopo zinazoota ukutani: akazungumzia pia juu ya wanyama, na juu ya ndege na juu ya vitambaavyo na samaki (mstari 33)
Sulemani alikuwa mchunguzi na akawa mwangalifu kwa kila kitu alichokiona. Alikuwa na maneno ya busara kueleza yote aliyoyachunguza na maelezo yote haya yalikusanywa pamoja na kuandika katika kitabu. 'Tunaambiwa kwamba alisema Methali elfu tatu na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano' (mstari 32) Alikuwa Mungu aliyempatia hekima hii naye Mungu amehifadhi misemo mingi sana kwa kumbukumbu ajili yetu ambayo ilikusanywa pamoja na kuandikwa katika kitabu, yaani Biblia.
Tunaweza kusoma maneno haya katika Mithali, Mhubiri na Wimbo Ulio Bora wa Sulemani kwani yamehifadhiwa humo ili na sisi tuwe na hekima.
Hekima ya ajabu na maarifa aliyopewa na Mungu ilikuwa ya kushangaza hata ikawa kwamba walikuja watu wa kutoka sehemu zote kusikia hekima ya Sulemani, kutoka wafalme wote wa dunia ambao walisikia juu yake (mstari 34).
MALKIA WA SHEBA ANAKWENDA YERUSALEMU: 1 Wafalme 10:1-13
Yapata kama umbali wa kilomita 2,000 kusini ulikuwapo ufalme wa Sheba, nchi ambayo ilikuwa tajiri na yenye mafanikio sana, na maarufu kwa ajiri ya mimea ya manukato ambayo iliyooteshwa humo. Manukato hayo yalipelekwa katika nchi za mbali kwa njia ya misururu ya ngamia ambayo ilipitia Israeli. Ndipo ikawa kwamba Malkia wa Sheba akawa amesikia taarifa ya utukufu wa wa Israeli na hekima ya ajabu ya mfalme. Habari zilielezwa mara kwa mara kiasi kwamba hakuweza kujizuia kwenda kujionea mwenyewe kama ni kweli aliyoyasikia yalikuwa kweli. Alifikiri angemjaribu Sulemani kwa maswali magumu. Hivyo aliondoka kwa safari hiyo ndefu kuelekea huko Yerusalemu akiwa na wafuasi wengi sana wa ngamia uliobeba zawadi zilizofaa kwa mfalme, zawadi za “manukato, na dhahabu nyingi sana na mawe ya thamani” (mstari 2).
Kwa hakiki alipenda sana hasa habari aliyokuwa ameisikia “kuhusu jina la BWANA” (mstari 1) kwa maana alikuwa amesikia kuhusiana na habari iliyokuwa imeenea wazi wazi kwamba hekima ya namna hiyo ilitoka kwa Mungu. Wakati Malkia wa Sheba alipotoa maswali magumu aliyoyatayarisha, ili kumjaribu Sulemani kama atayajibu, aliweza kuyajibu waziwazi na kwa hekima maswali yote.
Wala hakukuwa na jambo lolote ambalo Mungu alikuwa amemficha mfalme, kwa kuwa aliweza kumweleza yote aliyotamani kuyajua. Kisha akaongozwa kuutembelea mnara wa mji wa Yerusalemu; kuona utukufu wa hekalu alilomjengea BWANA na Ikulu yake; iliyokuwa na kiti cha enzi kizuri sana cha pembe za ndovu ambacho kilifunikwa dhahabu iliyo safi (mstari 18), na majengo mengine yote aliyoyajenga.
Akaona jinsi watu walivyoridhika na namna watumishi wake walivyomtumikia kwa furaha, akapendezewa namna maafisa wake walivyovalia na akashangazwa na wingi wa chakula mezani pa mfalme.
Ndipo alipokuwa ameyaona mambo haya yote, tunaambiwa ya kuwa “roho yake ilizimia” (mstari 5) haya yote yaliitoa pumzi yake! Akaona ni kweli kabisa kuwa habari alizozisikia hazingaliweza kwa vyovyote vile kuelezea utukufu wa uzuri wa yote hayo.
“Akamwambia mfalme, Ndizo kweli habari zile nilizozisikia katika nchi yangu za mambo yako na za hekima yako. Lakini mimi sikuzisadiki habari hizo, hata nilipokuja na kuona kwa macho yangu; tena, tazama, sikuambiwa nusu; wewe umezidi kwa hekima na kufanikiwa kuliko habari nilizozisikia. Heri watu wako, na watumishi hawa wako, wasimamao mbele yako siku zote, wakisikia hekima yako” (mstari 6-8).
Lakini katika haya yote aliweza kueleza kwamba utukufu huu umekuja kutoka kwa Mungu naye akamtukuza Mungu wa Israeli.
“Na ahimidiwe, BWANA, Mungu wako aliyependezwa nawe, ili akuweka juu ya kiti cha enzi cha Israeli: kwa kuwa BWANA amewapenda Israeli milele, na kwa hiyo amekufanya kuwa mfalme, ufanye hukumu na haki ” (mstari 9)
Aliporudi katika nchi yake, Sulemani alimruhusu kuchukua kama zawadi ya kuagana “kila alilolitaka”, (mstari 13).
Hivyo umaarufu wake na umaarufu wa BWANA, Mungu wa Israeli, ukaenea katika miisho ya yote ya dunia.
FUNDISHO KWETU
Mungu alikuwa amembarikia Sulemani mali, heshima na hekima kwa kadiri alivyoendelea kumtii Mungu na kutembea katika njia zake (1wafalme 9:4).
Alikuwa ameahidi pia kuwabariki wale wote wanaomwamini na kuzitii amri zake. Kwa watu wa namna hiyo wanaompenda, Mungu aliwaahidi “utukufu, heshima na amani, kwa kila mtu atendaye mema” (Warumi 2:10).
Siyo vigumu kufikiria kuwa kwa namna nyingi ambazo Mungu ametubarikia sisi. Ametupatia chakula chetu cha kila siku na nguo, nyumba nzuri sana,afya na nguvu na marafiki kwenye kusanyiko (eklesia), Lakini zaidi ya haya yote, ametubarika na ufahamu wa kuijua Kweli.
Na ikiwa tutaendelea kumtumikia Mungu kwa bidii hadi wakati wa kurudi kwa Kristo, ndipo atatubariki na “uzima wa milele” (Warumi 2:7). Hiyo ndiyo baraka kuu kuliko zote tunayoweza kuitumainia.
MAELEZO YA NYONGEZA
Siyo vigumu kuona katika somo hili kwa namna nyingi utawala wa Sulemani ulikuwa ni mfano wa utawala utakaokuwepo wa Bwana Yesu Kristo.
Tunaweza kuongezea vidokezo vifuatavyo katika orodha yetu
|
SULEMANI |
KRISTO |
|
Akaketi katika kiti cha enzi cha BWANA,Mungu huko Yerusalemu. (1 Mambo ya Nyakati 29:23) |
Kristo atatawala Yerusalemu (Yeremia 3:17) |
|
Alijenga hekalu takatifu huko Yerusalemu. (1Wafalme 6)
|
Atajenga nyumba ya sala kwa mataifa yote (Isaya 56:7) |
|
Mataifa mengine yalimsaidia Sulemani kwa kumpatia watumishi na mbao(1Wafalme 5:8 -10,18) |
Wapagani watasaidia kujenga upya Yerusalemu (Isaya 69:10,13) |
|
Ufalme wake ulikuwa tajiri sana (1Wafalme 10:21,27 |
Mataifa wataleta utajiri wao kwa Kristo (Isaya60:11,17) |
|
Watu walikuja kutoka mbali sana kusikia hekima yake (1Wafalme 4:34) |
Watu kutoka mataifa yote watakwenda hadi Yerusalemu kusikia hekima ya Kristo(Isaya 2:2 – 4) |
MSWALI
Majibu Mafupi
- Kinamaanisha nini kifungu hiki “Yuda wa Israeli wakakaa salama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake?”
- Ufalme wa Sulemani ulienea umbali gani kwa upande wa kaskazini na kusini?
- Sulemani alinunua nini kutoka Misri?
- Ni zawadi gani ambazo wafalme kutoka nchi nyingine walimpelekea?
- Ni wapi tunaweza kusoma baadhi ya misemo ya hekima ya Sulemani?
- Ni nani alikuja kujaribu hekima ya Sulemani kwa maswali magumu?
- Ni nini alifikiri Malkia wa Sheba alipoona mwenyewe utukufu wa ufalme wa Sulemani?
- Malkia aliwaona watu katika hali gani?
- Ni nani Malkia wa Sheba aliyemtukuza baada ya kusikia hekima ya Sulemani na kuuona utukufu wake?
- Sulemani alimpatia nini Malkia wa Sheba kama zawadi ya kuagana?
Majibu ya Kina
- Eleza jinsi Israeli ilivyokuwa wakati Sulemani alipokuwa mfalme.
- a) Kwa nini Malkia wa Sheba alikuja kumtembelea Sulemani?
b) Alisemaje alipokuwa amesikia hekima yake na kuona utukufu wake?
Majibu ya Nyongeza
- Eleza njia tano ambazo utawala wa Sulemani ni mfano wa utawala wa Kristo