CSSA 1-3-06 - ELIJAH THE PROPHET

Swahili

56. NABII ELIYA

“Hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, mpaka kwa neno langu”

 

Shabaha

Kuonyesha jinsi Mungu alivyoleta ukame juu ya nchi lakini akamtunza Eliya na kumbariki mwanamke mjane wa Sarepta kwa ajili ya wema wake kwa Eliya. Ufamle wa kaskazini wa Israeli ulianza vibaya sana. Kama tulivyoona, kitu cha kwanza ambacho Yeroboamu alifanya kilikuwa kubadili ibada ya kweli ya Mungu kwa kuabudu miungu (sanamu). Alipoondoka Mfalme mwovu mwingine Mfalme mwovu aliifuata.

 

Kabla ya muda mrefu kupita kukawa na mfalme ambaye alitawala wakati huo aliyeitwa Ahabu, ambaye “alifanya mabaya machoni pa BWANA kuliko wote waliomtangulia” (Wafalme 16:30). Ahabu alimkasirisha Mungu zaidi kuliko mfalme mwingine yeyote, siyo tu alifuata katika dhambi za Yeroboamu lakini alioa mwanamke mwovu sana Yezebeli, binti mfalme wa Wasidoni.

1. Wafalme 17

 

MUNGU ANAMTUMA ELIYA KUMWONYA AHABU:

1 Wafalme 16;31-33,17:1

Israeli walikuwa wamemsahau BWANA Mungu wao. Walikuwa wamesahau amri zake, ambayo ilisema; “usijifanyie sanamu yeyote ya kuchoga” (Kumbukumbu la Torati 5:7-8). Mke wa Ahabu, yule mwanamke mwovu Yezebeli, alikuwa ameweka madhabahu kwa ajili ya mungu wake, Baali, akaweka katika nchi yote ya BWANA na kuwashirikisha watu kuzisujudia sanamu na kuzitumikia. Mfalme Ahabu pia alijenga hekalu kwa ajili ya Baali katika Samaria, ambako alitawala juu ya zile kabila kumi na kuabudu sanamu yake ya kuchonga.

 

Siyo ajabu Mungu alikasirika sana, akamtuma nabii wake Eliya kumtangazia mfalme kwamba kungekuwa na njaa juu ya nchi, hiyo Eliya alikuja mbele ya Mfalme, akiwa amevaa nguo zake isiyopendeza ya ngozi ya kondoo aliyoivaa kwa mkanda wa ngozi kiunoni (1 Wafalme 1:8), naye alipaza sauti kubwa ili watu wote waweze kusikia. “Kama BWANA, Mungu wa Israeli aishivyo, ambaye nasimama mbele yake:Hakutawa na umande wala mvua miaka hii, mpaka kwa neno langu” (17:1). Mungu angewaadhibu watu kwa ajili ya dhambi zao, na kuwapa muda wa kumkumbuka Mungu wao, na kujutia uovu wao.

 

MUNGU ANAMLISHA ELIYA: 1 Wafalme 17:2-9

Ahabu alishitushwa na habari hizi naye Yezebeli alikasirika wakamtafuta Eliya kila mahali (18:10) lakini Mungu alikuwa ameshamtuma kwenye kijito cha Kerithi ngambo ya pili ya Yordani kujificha. Mungu akamwambia Eliya, “itakuwa ya kwamba utakunywa maji ya kile kijito nami nimewaamru kunguru wakulishe kule” (mstari 4). Kila asubuhi na kila jioni kunguru walikuja, wakileta mkate na nyama ili kumlisha yule nabii mwaminifu. Kwa hiyo Mungu akamtunza Eliya wakati Israeli wakiteseka kwa ukame. Punde si punde, hata hivyo hata kile kijito cha Kerithi kilikauka, kwa sababu hapakuwa na mvua iliyonyesha Mungu akasema tena na Eliya akamwambia, “ondoka uende Sarepta, iliyoko Sidoni nawe ukae huko tazama nimemwamrisha mwanamke mjane akulishea” (mistari 9)

 

ELIYA NA MWANAMKE WA SAREPTA: 1 Wafalme 17:10 -16

Sarepta ilikuwa Sidoni na hata Yezebeli mwenyewe alikuwa ametokea huko lakini Mungu alikuwa amemtuma Eliya huko ili amtunze. Eliya alipofika penye lango la mjii akamwona yule mwanamke mjane akiokota kuni. Akamwita “Akamwambia; Niletee, nakuomba, maji kidogo katika chombo ili nipate kunywa” (mstari 10). Alipokwenda kuchukua maji akasema, “Niletee, nakuomba, kipande cha mkate cha mkate mkononi mwako” (mstari 11). Na katika nyakati hizo za ukame maji na chakula vilikuwa havipatikana sana, na Eliya alijua hilo. Yule mwanamke mjane ni hakika kuwa alimtambua Eliya, kwani aligeuka na kusema, “kama BWANA Mungu wako aishivyo sina mkate ila konzi ya unga katika pipa na mafuta kidogo katika chupa; nami naokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule itukafe” (mstari 12)

 

Ni kwa jinsi gani huyu mjane maskini angemsaidia Eliya wakati alikuwa na kile kidogo tu kwa mlo mmoja wa mwisho kwa ajili yake na mwana wake na kisha wafe? Lakini Eliya alimpa tumaini na kumpa moyo mjane ili amwamini BWANA Mungu wa Israeli ambaye alimtuma Eliya kwake.

 

Eliya akamwambia, “Usiogope”; “enenda na ukafanye kama ulivyosema lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee, na kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao” (mstari13). “Kwa kuwa BWANA Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka wala ile chupa ya mafuta haitaisha hata siku ile ambayo BWANA atakayoleta mvua juu ya nchi” (mstari 14).

 

Yule mjane akamwamini Eliya na kumtegemea Mungu wa Israeli. Akaenda na kufanya kama Eliya alivyosema, na tangu wakati ule na kuendelea unga wake na mafuta hayakupungua hata angetumia mara ngapi kumpikia Eliya na yeye mwenyewe na mwanawe.

 

MWANA WA MJANE WA SAREPTA:1 WAFALME 17:17-24

Na ikawa, baada ya siku kadhaa, jambo la huzuni likatokea. Ikawa mwana wa yule mjane akaugua na kufariki. Ndipo yule mama maskini alishikwa na huzuni kubwa. Akawaza kuwa Mungu alikuwa akimwadhibu kwa ajili ya dhambi zake. Eliya akamchukua mwanawe kutoka katika mikono ya mjane yule na kumbeba na kupanda naye hadi chumba alichokuwa akikaa ndani ya nyumba ya yule mjane. Akamlaza juu ya kitanda chake mwenyewe na kumlilia Mungu kwa ajili ya msaada. Kisha akajinyoosha juu ya yule mtoto mara tatu na kumwomba Mungu “Ee BWANA Mungu wangu, nakusihi, roho ya mtoto huyu imrudie ndani yake tena” (mstari 21). Mungu akasikia maombi ya Eliya, roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka.

 

Jinsi Eliya kwa furaha alivyomchukua mvulana mpaka chini na kumrudisha mikononi mwa mamaye tena. Eliya akamwambia, “Tazama mwanao, yu hai” (mstari 23). Yule mwanamke mjane kwa moyo uliojaa shangwe na shukrani akamwambia Eliya, “Kwa ajili hii sasa ninajua kuwa wewe ni mtu wa Mungu na kwamba neno la BWANA kinywani mwako ni kweli” (mstari 24).

 

FUNDISHO KWETU

Israeli ambao ni watu wa Mungu walikuwa wamemsahau BWANA, lakini mwanamke maskini ambaye ni (mpagani) mmataifa aliyeishi katika nchi nyingine alikuwa amesikia kuhusu Mungu wa Israeli na kumwamini.

 

Sisi sote tu wa mataifa kwa kuzaliwa lakini tumesikia habari kuhusu BWANA Mungu wa Israeli. Tunasoma juu ya matendo yake makuu kila siku katika Biblia zetu. Iwapo tuna imani kama yule mjane wa Sarepta Mungu kila wakati atatupatia riziki kwa mahitaji yetu kama alivyofanya kwa yule mama na mwana wake. Matatizo yaliyokuja juu yake, kama vile yatakavyokuja juu yetu, kwa hakika lakini Mungu alimpatia shangwe na furaha mwishowe kwa sababu alimwamini Mungu. Na sisi pia tumwamini Mungu pia, Mungu atupatia furaha ya milele katika ufalme wake.

 

MAELEZO YA ZIADA

Mojawapo ya masomo muhimu ambayo Mungu alitaka watu wake wajifunze ni kwmba “mwanadamu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha BWANA (Kumbukumbu la Torati 8:3). Katika siku za Ahabu watu wa Israeli walikuwa wameziba masikio yao wasitake kusikia neno la Mungu.

 

Hawakutaka kusikia, walikuwa wamejazwa na ibada ya kumwabudu-Baali hata hawakuwa na muda wa ziada ya kumtafarikari BWANA ili kuwafundisha somo Mungu alipeleka njaa ambayo ilimaanisha kwamba mkate wao wa kila siku ungeisha haraka. Na kama wasingeisikia sauti yake basi asingewapatia (mikate) chakula cha kila siku.

 

Mungu alimwona kwamba yule mjane wa Sarepta alikuwa mtu wa tofauti kabisa katika wote. Yeye alimwamini Mungu wa Israeli, alimwamini nabii wake Eliya na kusikia neno la Mungu ambalo Eliya alisema. Na kwa sababu ya imani kubwa aliyoionyesha, Mungu alimpatia mkate wake wa kila siku kwa muda wote wa ukame. Kadiri imani yake ilivyoendelea kamwe hakukosa chakula na mafuta ya kutengenezea mkate wake.

 

Bwana Yesu alimtaja mjane huyu maskini aliyekuwa tajiri katika imani wakati alipojaribu kuwafundisha neno la Mungu watu wa mji wa kwao Nazareti mioyo yao ilkuwa migumu na hawakumwamini (Mathayo 13:58) hivyo aliwaambia kwamba walikuwepo wajane wengi katika siku za Eliya,lakini Eliya hakutumwa kwa mjane yeyote katika Israeli. Eliya alitumwa kwa mjane wa Sarepta kwa kuwa Mungu alijua kwamba yule mjane alikuwa anamwamini Mungu (Luka 4:24-28).

 

MASWALI

Majibu Mafupi

  1. Ni nani alikuwa mke wa Ahabu?
  2. Ahabu na Yezebeli walimwabudu mungu yupi?
  3. Ni amri ambayo Israeli walikuwa wameisahau?
  4. Ni onyo lipi ambalo Eliya alimpa Ahabu?
  5. Ni wapi Mungu alimpeleka Eliya kujificha?
  6. Kwa jinsi gani Mungu alimtunza Eliya wakati wa ukame huko Keriti?
  7. Ni wakati gani Eliya aliomba apewe “kipande cha mkate”ni kiasi gani kilikuwa kimebaki kwa yule mjane wa Sarepta?
  8. Ni kwa namna gani Mungu alimsaidia mjane wa Sarepta kwa kumlisha chakula Eliya?
  9. Ni jambo gani la huzuni lilimtokea mtoto wa mjane wa Sarepta?
  10. Jinsi gani Eliya alimsaidia yule mjane wa Serapta wakati mwanawe alipofariki?

 

Majibu ya Kina

 

  1. Eleza namna Mungu alivyo mlisha Eliya wakati wa ukame:
    1. Huko Keriti
    2. Huko Sarepta

 

Majibu ya Ziada

  1. Ndani ya maandiko mafuta yanatumika kama alama ya kuwakilisha neno la Mungu. Ni fundisho gani tunalojifunza kutokana na chupa ya mafuta ya mjane?

 

 

Swahili Title
056 NABII ELIYA
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type