CSSA 1-3-07 - THE CONTEST ON MOUNT CARMEL

Swahili

57. MASHINDANO KATIKA MLIMA KARMELI

“BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni mungu, mfuateni yeye”

 

Shabaha

Kuonyesha namna Mungu alivyothibitisha kwa watu mlimani Karmeli kwamba yeye ndiye alikuwa Mungu wa kweli na aliye hai. Ukame uliendelea katika Israeli kwa muda wa miaka mitatu na nusu (Luka 4:25) Nchi ilikuwa kame na ilikuwa imekauka kabisa.

 

Visima na vijito vilikuwa vimekauka na chakula kilikuwa adimu au kiliadimika. Katika mwaka wa nne wa ukame Mungu akamwambia Eliya: “Enenda ukajionyeshe kwa Ahabu; nami nitaleta mvua juu ya nchi (mstari 1).

 

Hivyo Eliya alijiandaa kuwangazia Israeli habari njema ya kunyesha kwa mvua lakini kwanza lazima watu waongozwe kuona kwamba BWANA ndiye aliyekuwa wa kweli na Mungu aliye hai.

 

1 Wafalme 18

 

ELIYA ANARUDI :1 Wafalme 18:1-24

Wakati Eliya alipokuwa njiani ili kukutana na Ahabu, Mfalme mwenyewe alikuwa nje na mkuu wa mtumishi wake, Obadia, wakitafuta nyasi na maji kwa ajili ya farasi na nyumbu wa mfalme. Ahabu akaenda njia moja na Obadia akaenda njia nyingine.Ghafla Obadia, mtu aliye mwogopa sana BWANA alishtushwa kuonana uso kwa uso na Eliya Nabii, ambaye alikuwa hajaonana naye tokea siku ile aliyotangaza kuja kwa ukame huu wa kutisha. Eliya sasa akamwomba aende kumwambia mkuu wake kwamba alikuja kuzungumza naye.

 

Ahabu alipomkaribia nabii Eliya akamwambia Eliya, “Je! Ni wewe, Ewe mtaabishaji wa Israeli?”(mstari 17).

 

Naye Eliya akajibu, “Si mimi niliyewataabisha Israeli; bali ni wewe na nyumba ya baba yako, kwa kuwa mmeziacha amri za BWANA; nawe umewafuata mabaali” (mst.18). Ahabu alikuwa hajajifunza jambo lolote katika miaka mitatu iliyopita ya ukame. Bado Ahabu alimwona Eliya kuwa ndiye aliyekuwa chanzo cha matatizo yake yote.

 

Ndipo Eliya akamwambia mfalme, “Unikusanyie jamii ya Israeli katika mlima wa Karmeli na wale manabii wa Baali” (mstari 19). Kwa hiyo Eliya akasimama mbele yao katika mlima.

 

Akawaambia wote, “Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini? “BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! mfuateni yeye” (mstari 21).

 

Alishauri mashindano halisi yafanyikie palepale mlimani kuonyesha wazi ni yupi alikuwa ni Mungu wa kweli.Manabii wa Baali wangetoa ng’ombe dume kama sadaka kwa Baali kuita miungu yao kuleta moto ushuke kutoka mbinguni kuteketeza dhabihu yao. Ndivyo hivyo Eliya angetayarisha dhabihu na kuliitia jina la BWANA. Mungu yule ajibuye kwa moto na awe ndiye Mungu. Watu wote wakajibu, wakasema, Maneno haya ni mazuri (mstari 24).

 

MASHINDANO KATIKA MLIMA KARMELI:1 Wafalme 18:25-29.

Hivyo mashindano yakaanza. Eliya aliwaambia wale manabii mia nne na hamsini wa Baali Jichagulieni ng’ombe mmoja, mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini (mstari 25). Na wale manabii wakamtwaa yule ngo'mbe wakamtengeneza walipokwisha kumtayarisha wakaliitia jina la mungu wao ili aleta moto, tokea asubuhi hadi adhuhuri wakamwomba mungu wao “Ewe Baali tusikie” (mst 26). Kisha tena na tena wakalia wakaruka ruka juu ya madhabahu yao, “lakini hapakuwa na sauti wala aliyejibu.”

 

Eliya alikuwa na subira sana. Maana alijua kuwa kelele zao hazisaidii kitu kwani mungu wa mataifa ni sanamu ambazo hazisemi tu (Zaburi.135:15-18). Eliya sasa akaanza kuwakejeli na kuwadhihaki labda wapige kelele nyingi zaidi mungu wao huenda amesafiri au pengine amelala mchana kutwa wakalia kwa nguvu wakajikata kwa visu bado hapakuwa na jibu lililopatikana.

 

BWANA ANAJIBU KWA MOTO: 1 Wafalme 18:30-40

Sasa ukafika muda wa kutoa dhabihu ya jioni wale manabii wa Baali wakawa wamechoka. Eliya akawaita watu wote, “Nikaribieni mimi” akaanza kukarabati madhabahu ya Mungu ambayo kwa muda mrefu ilikuwa haitumiki, akachukua mawe yasiyochongwa kumi na mbili, jiwe moja kwa ajili ya kabila moja la Israeli, na kuyaweka moja juu ya jingine. Kisha akachimba mfereji kuizunguka madhabahu akaweka kuni mahali pake na kumkata ng’ombe dume vipande vipande na kuviweka juu ya kuni halafu akaita walete maji mapipa manne na kuyamwaga juu ya sadaka na kuni na kujaza mfereji. Hilo lilifanyika mara tatu mpaka na kuni na madhahu vyote vikalowa maji kabisa.

 

Kila kitu sasa kikawa tayari, mbele ya watu wote Eliya akaanza kuomba. “Ee BWANA Mungu wa Ibrahamu, na wa Isaka na wa Israeli na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli na ya kwamba mimi ni mtumishi wako na kwamba nimefanya mambo haya yote kwa neno lako” (mstari 36). Mara moja moto wa BWANA ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, na kulamba maji ambayo yalikuwa mferejini (mstari 38). Ikawa watu wote walipoona hilo wakaanguka kifudifudi na wakasema “BWANA, ndiye Mungu; BWANA, ndiye Mungu” (mstari 39).

 

Jambo moja likawa limebakiakufanyika. Eliya akasema, Wakamateni hao manabii wa Baali asiokoke hata mmoja. Hivyo wakawakamata manabii walipojaribu kukimbia kuokoa uhai wao nao wakawauwa.

 

MUNGU ANALETA MVUA: 1 Wafalme 18:41-46

Eliya alikuwa anajua kuwa mvua ilikuwa karibu kunyesha akapanda hadi kilele cha mlima Karmeli na akainama kifudifudi akainama hadi nchi akmwomba Mungu. Akamtuma mtumishi wake kuangalia upande wa bahari, mtumishi wake akatazama hakuona kitu. Mara saba Eliya alimtuma wakati yeye akiendelea na maombi. Hatimaye yule mtumishi akarudi na kumwambia kwamba aliona wingu dogo likiinuka kutokea baharini kama mkono wa mtu. Na hiyo ndiyo ilikuwa ishara ambayo Eliya alikuwa anangojea. Eliya akamtuma mtumishi wake amtafute mfalme Ahabu, na ampelekee ujumbe kwamba atandike gari lake la farasi ondoke haraka mlimani atayarishe gari lake haraka ili mvua isimzuie.

 

Mawingu meusi yenye upepo yalikuwa yakitanda haraka mbinguni na mvua nzito ikaja tokea upande wa bahari. Mfalme akaharakisha garini mwake akijua kwamba mara mvua ikinyesha angekwama bondeni.

 

Lakini ingawa Ahabu aliendesha gari lake kwa kasi sana, Mungu alimpa Eliya nguvu siku ile hadi akakimbia haraka hata akampita mfalme mpaka akaingia lango la Yezreeli.

 

FUNDISHO KWETU

Israeli waliteseka sana katika ule ukame wa muda mrefu, kwa sababu walikuwa wamegeukia kuabudu (vinyago) sanamu. Katika Kumbukumbu la Torati 11:16-17, Mungu aliwaonya Israeli kwamba asingeleta mvua iwapo wangegeuka na kumwacha na kuabudu miungu mingine. Watu walipoona kwamba Baali hakuwa na nguvu na walipaza sauti kwa kelele wakasema “BWANA ndiye Mungu” na Kuwaua manabii wa Baali ndipo Mungu alipoleta mvua. Ni fundisho zuri ajabu kwetu sisi, kamwe tusigeuke tukaacha kumwabudu Mungu wa kweli  “Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watendamabaya.” (1 Petro.3:12)

 

MASWALI

Majibu Mafupi

  1. Ukame ulidumu kwa mda gani katika Israeli?
  2. Eliya alisema ni nani aliyekuwa amewataabisha Israeli?
  3. Ni akina nani waliokusanyika pamoja katika mlima Karmeli?
  4. Ni jinsi gani wangemtambua Mungu wa kweli?
  5. Nini kilitokea wakati manabii wa Baali walipomwita mungu wao kushusha moto?
  6. Ni madhabahu gani Eliya alitumia kwa dhabihu yake?
  7. Ni jinsi gani Eliya alitayarisha dhabihu yake?
  8. Waisraeli walisemaje wakati Mungu alipojibu kwa moto?
  9. Eliya aliwaambia watu wawafanye nini hao manabii wa Baali?
  10.  Mtumishi wa Eliya aliona nini kilichomwonyesha kuwa mvua ilikuwa inakuja mwishowe?
  11. Ni nguvu gani ya pekee Mungu aliyompatia Eliya siku ile?

 

Majibu ya Kina

 

  1. Katika Mlima Karmeli ilikuwa rahisi kumfahamu ni nani alikuwa Mungu wa kweli.
    1. Eleza jinsi manabii wa Baali walivyomwita Baali kwa ajibu
    2. Eleza namna Eliya alivyotayarisha sadaka na jinsi Mungu alivyojibu maombi yake.
  2. (a) Eleza kwa nini Mungu alizuia kuleta mvua juu ya Israeli.

        (b) Eleza namna Eliya alivyongojea na kungalia dalili ya mvua tena.

 

   

Swahili Title
057 MASHINDANO KATIKA MLIMA KARMELI
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type