61. NAAMANI MTU MWENYE UKOMA
''Na sasa ninajua kwamba hapana Mungu duniani, ila Mungu wa Israeli''
Shabaha
Kuonyesha jinsi Elisha alivyompanya Naamani mtu wa Shamu, ugonjwa wa ukoma, na ni kwa nini Gehazi, mtumishi wa Elisha alipigwa kwa ukoma.
Basi Elisha nabii akajulikana sana na akaheshimika katika Israeli yote. Ni kwamba yeye alikuwa mtu aliyetofauti na Elisha wa kawaida, kwa sababu ya Roho wa Mungu alikuwa juu yake kwa ajili hiyo, kwa ajili ya kufundisha neno la Mungu na kutenda miujiza ya kushangaza sana.
Katika maisht yake Elisha alikaribishwa katika ikulu ya wafalme wa Israeli, na hata wafalme wa Shamu walimheshimu Elisha pia. Elisha alitabiri wakati wa utawala wa wafalme wengine wanne ambao walifuata, kwa karibu miaka 60. Kama kweli wafalme wa Israeli wangemwamini Mungu na kumtumikia kama vile Elisha alivyofanya, Israeli wangekuwa na ufalme wenye furaha.
2 Wafalme 5
NAAMANI MTU WA SHAMU ANATAFUTA MSAADA:2 Wafalme 5:1-7
Basi ufalme wa Shamu ulikuwa upande wa kaskazini wa Israeli na watu wa Shamu walikuwa wapenda vita.Ingawaje kwa wakati huu hapakuwa na vita kati ya Israeli na Shamu,vikosi vya jeshi la Shamu walikuwa wanashuka na kuvuka miji ya mpakani,wanateka nakuharibu vijiji na kuchukua vitu vyote walivyovitaka.
Katika moja ya tukio kama hilo walimteka kijana msichana wa Israeli kumpeleka Shamu. Msichana huyu akawa mtumishi katika nyumba ya jemadari wa jeshi la Shamu, ambaye jina lake ni Naamani. Naamani alikuwa askari hodari sana, “alikuwa ni mtu hodari wa vita”. Lakini jambo la kusikitisha, ni kwamba Naamani alikuwa na ugonjwa wa kutishwa ukoma. Hakuna dawa yoyote ambayo angepewa kwa sababu ukoma ulikuwa hauna dawa ya kuuponya.
Mfalme wa Shamu alifikiria sana kuhusu tatizo la jemadari wake Naamani, isisitoshe alikuwa yuko tayari kumsaidia kwa namna yoyote kwa ajili ya tatizo lake. Lakini asingefanya lolote kwa maana haikuwapo dawa ya kuuponya ukoma.
Yule msichana aliyechukuliwa mateka kutoka Israeli alikuwa akitendewa mema katika nyumba ya Naamani lakinii msichana huyu alisikitishwa kumwona bwana wake akiwa na ugonjwa wa ukoma. Huyu msichna alikumbuka miujiza ambayo Elisha nabii aliitenda katika nchi yao. Akamwambia mke wa Naamani, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria / maana angemponya ukoma wake”. Msichana huyu aliongea kwa uhakika kabisa kuhusu uwezo wa Elisha wa kuweza kumponya ukoma bwana wake maelezo haya yakamfikia mfalme. Mfalme alifurahi sana kujaribu wazo la kumponya Naamani na akaamua kuandika waraka haraka kwenda kwa mfalme wa Israeli. Naamani akaichukua barua hiyo mwenyewe, pamoja na zawadi za upendo za dhahabu, fedha na mavazi kumi na Naamani akaenda mwenyewe na kusimama mbele ya mfalme wa Israeli. Waraka huo ulisema hivi: “Nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, ili upate kumponya ukoma wake” (mstari 6). Mfalme Yoramu alikasirika sana na kufadhaika mno aliposoma waraka huu. Akararua mavazi yake, akasema, “Je! mimi ni Mungu, niue na kuhuisha, hata mtu huyu akanipelekea mtu ni mponye ukoma wake” (mstari 7). Mfalme wa Israeli aliona ombi hilo haliwezekani kabisa. Alifikiria kuwa mfalme wa Shamu anataka kugombana naye. Kwa huyu mfalme mwovu, Mungu alionekana kama hawezi kusaidia. Yule msichana aliyekuwa mateka na kupelekwa Shamu alikuwa na imani kubwa kuliko mfalme wa Israeli.
KIBURI CHA NAAMANI KINAJARIBIWA:2 Wafalme 5:8-12
Taarifa za mfalme Yoramu ambazo ni za kuaibisha zikamfikia haraka nabii Elisha.Elisha alituma mjumbe kwa mfalme, kusema, Mbona umeyararua mavazi yako? Na aje sasa kwangu mimi, naye atajua ya kuwa yuko Nabii katika Israeli” (mstari 8).
Bila shaka mfalme alikuwa tayari kumfukuza Naamani aondoke. Kwa hiyo Naamani akafika nyumbani kwa Elisha na farasi wake na magari yake na watumishi wake.
Naamani kwa mshangao, Elisha nabii hakutokea kumkaribisha Naamani.Badala yake, Elisha alimtuma mjumbe ambaye alimwagiza: “Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, nawe utakuwa safi” (mstari 10). Naamani alifikiri kuwa amedharauliwa na akaondoka kwa hasira. Naamani alikuwa akifikiria kuwa nabii mwenyewe angetoka na kuomba kwa jina la BWANA, Mungu wake na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi ukoma. Lakini kwa kuoga maji ya tope, na maji yenye harufu mbaya ya Yordani. Alisema kwa dharau! Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira (mstari 12)
NAAMANI ANANYENYEKEA NA ANAPONYWA: 2 Wafalme 5:13-16
Watumishi wa Naamani walitamani sana kuona bwana wao amepona. Kwa hiyo walimfuatana kumwambia afikirie makini sana.
Wakamwambia, “Baba yangu, kama yule nabii angalikuambia kutenda jambo kubwa, usingalilitenda?.Je! si zaidi basi, akikuambia, jioshe, uwe safi? (mstsari 13). Huu ulikuwa ni ushauri mzuri Kiburi cha Naamani kilisababisha hata asifikirie kwa busara. Lakini sasa aliweza kuwasikiliza watumishi wake. Ushauri wao ulimfanya Naamani kunyenyekea, akashuka katika mto Yordani na akajichovya mara saba, kama Elisha alivyomwagiza. Hata ikawa, alipojichovya mara saba, “Nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikiwa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi!” (mstari 14). Ni mwujiza wa ajabu jinsi gani!
Kwa hiyo Naamani, alinyenyekea, mwishowe akawa safi, na akashukuru, akarudi nyumbani kwa Elisha. Wakati huu Elisha alikuwa ni mwenye furaha alipokuwa akiongea naye uso kwa uso,kwa maana Naamani alikuwa ni mtu aliyebadilika.Basi kwa shukrani jemadari akakiri, “Sasa tazama, najua kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli. Alijua kuwa ugonjwa wake ulikuwa hauna dawa-lakini sasa Mungu wa Israeli kwa mwujiza alimponya! Ili kuonyesha shukrani yake Naamani alimpatia Elisha zawadi, lakini Elisha hakuzipokea, Alisema, “Kama BWANA aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu (mstari 16). Na ingawa Naamani alimsihi sana, lakini Elisha alikataa. Maana Elisha lijua nguvu zile za kuponya siyo za kwake; siyo yeye aliyekuwa amemponya Naamani; bali zilikuwa ni nguvu za BWANA, Mungu wa Israeli ambaye amemponya huyu mtu.
GEHAZI ANADANGANYA NA ANAADHIBIWA: 2 Wafalme 5:20-27
Gehazi, alikuwa ni mtumishi wa Elisha ambaye ndiye aliyechukua maagizo ya Elisha na kumwambia Naamani na alikuwa ameshuhudia kabisa kuponywa kwa ukoma wa Naamani,jemadari wa jeshi wa mfalme wa Shamu. Na ingwaje alifahamu kuwa zilikuwa ni nguvu za Mungu, na siyo nguvu za Elisha ambazo zimemponya Naamani, alifikiria kuwa mtu huyo ambaye ni mkuu sana anapaswa kulipia huduma hiyo nabii. Naamani alikuwa ni mtu wa Shamu-wala hakuwa Myahudi-na Elisha hakuwa amemwambia kulipa gharama yoyote! Wakati Gehazi alifahamu jinsi Naamani alivyokuwa tajiri, akatamani-akataka baadhi ya utajiri huo uwe ni zawadi kwake.Kwa hiyo Gehazi akamkimbilia Naamani.
Wakati Naamani alipomwona akimkimbilia, aliweza kumtambua kuwa ni mtumishi wa Elisha, akasimamisha gari lake na akashuka na kwenda ili kukutana naye. Akamwambia, Je! ni amani? Gehazi alimhakikishia kuwa ni amani, lakini akasema kuwa bwana wake ndiye amemtuma ili amfuate.Alisema, Vijana wawili wa wana wa manabii wamekuja kumwona bwana wangu, na labda jemadari utawapa mavazi mawili na talanta ya fedha.
Furaha ya Naamani ilikuwa kupata nafasi yakusaidia, Naamani akamsihi Gehazi ili achukue talanta mbili. Ndipo watumishi wa Naamani wakazibeba zawadi na kuzifikisha mahali pa siri alipoandaa Gehazi ili kuzificha zawadi hizo. Naamani n watumishi wake wakaendeleana safari yao hadi Shamu, naye Gehazi akaingia na kusimama mbele ya Elisha. Elisha akamwuliza, Watoka wapi Gehazi?
Gehazi akajibu, “Mtumishi wako hakwenda mahali”
Uchoyo wa Gehazi ulisababisha aseme uongo, uongo wa kwanza hukuongoza kusema uongo mwingine.
Elisha alikuwa ameshampatia Mungu utukufu kwa ajili ya mwujiza huo wa kumponya Naamani ukoma. Lakini dhambi ya Naamani ilimdhalilisha Mungu. Na Elisha lijua kuwa mtumishi wake alikuwa amedang'nya. Elisha akasema, “Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele.” Gehazi akatoka mle chumbani mwenye ukoma kama theruji (mstari 27).
Kwa hiyo nguvu za Mungu zikaonyeshwa katika mambo mawili kwa kumponya mtu aliyenyenyekea na kwa kumwadhibu mtu yule aliyetenda dhambi.
FUNDISHO KWETU
Naamani aliponywa baada ya kujisafisha sawasawa katika Yordani mara saba. Alitakiwa asahau kiburi chake na yeye mwenyewe amtii Mungu. Na kama angejisafisha mara sita, angeendelea kuwa mwenye ukoma. Uponyaji wake haukuwa katika maji ya Yordani, bali uponyaji wake ulikwa katika kutii kwake agizo la nabii.
Kwa hiyo Mungu anategemea sisi tuliamini yote ambayo aliyasema katika Biblia ambayo aliyasema kupitia watumishi wake manabii na mitume, kuyafanya yote aliyotagiza sisi katika Biblia tuyatende.
Na ni kwa njia hiyo ndipo tupona kifo cha milele. Hata hivyo, kwa wale wanaomtumikia Mungu kwa kujionyesha, mfano kama Gehazi, ni wapumbavu. Mungu anajua mioyo ya wanadamu wote, na Mungu anataka sisi tumtumikie kwa moyo wote.
MAELEZO YA NYONGEZA
Ukoma ni ugonjwa wa kutisha sana. Husababisha baadhi ya sehemu za mwili kuoza na kufa pole pole. Ni mfano wa dhambi. Dhambi huleta kifo. “Basi roho itendayo dhambi itakufa” (Ezekieli 18:4)
Sisi sote tumetenda dhambi na sisi sote tunakufa. Ni sawasawa na ugonjwa usiotibika. Ni mwujiza peke yake unaoweza uponya ukoma. Wakati Naamani aliponyenyekea mwenyewe na kuliamini neno la Elisha, alishuka katika maji ya mto Yordani na kujichovya yeye mwenyewe mara saba. Kitendo hiki ni sawa kabisa na ubatizo-alizama kabisa ndani ya maji, na akainuka kutoka majini akiwa ni mtu mpya kabisa. Mwili wake haukuwa na ukoma tena, na Naamani akamsifu na kumshukuru Mungu.
Na kwa kadiri tunavyokua, tunajitambua ni jinsi gani tulivyowatenda dhambi. Tunapojifunza Neno la Mungu, ndipo tunapofahamu kuwa Mungu anatutaka sisi tuache dhambi na tumtii yeye.Kitendo cha kwanza cha kutii Mungu ni ubatizo (Marko 16:16).
Dhambi zetu za kale zinsafishwa kabisa na kisha tunakuwa na tumaini la uzima wa milele,ikiwa tutaendelea kumsifu na kumshukuru Mungu.Na kwa hiyo kutakaswa kwa Naamani ni fundisho kwetu sisi ya kwamba sisi sote tunahitaji kutakaswa kutokana na dhambi zetu.
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Naamani alikuwa na ugonjwa gani?
2. Ni nani alimwambia Naamani mahali ambapo anaweza kupata uponyaji?
3. Mfalme wa Shamu aliandika maneno gani katika waraka wake aliomwandikia Mfalme wa Israeli?
4. Mfalme Yoramu alifanya nini na alisema nini aliposoma waraka wa Mfalme wa Shamu?
5. Elisha alimwambia Naamani afanye nini?
6. Je! Naamani aliufikiriaje mto Yordani?
7. Ni ushauri gani mzuri ambao watumishi wa Naamani walimpatia?
8. Palitokea nini baada ya Naamani kumtii Elisha?
9. Naamani alisema nini baada ya kupona?
10. Ni kwa nini Gehazi alimkimbilia Naamani?
11. Gehazi alifanya ini alipopata vitu kutoka kwa Naamani?
12. Ilimtokea nini Gehazi?
Majibu ya Kina
13. Yule msichana aliyetekwa alikuwa na imani kuliko Mfalme wa Israeli.
(a)Elezea kuhusu imani yake na wema wake
(b) Mflme Yoramu alisema nini aliposoma waraka kutoka kwa Mfalme wa Shamu?
14. Simulia kulitokea nini wakati Naamani alipofika nyumbani kwa Elisha, na jinsi Alivyoponywa.
15. Eleza habari kuhusu upumbavu wa Gehazi, na namna alivyoadhibiwa
Maelezo ya Nyongeza
16.Kutakaswa kwa Naamani ukoma wake.
Eleza
(a) Ni kwa vipi ukoma ni sawasawa na ugonjwa
(b) Ni jinsi gani dhambi ni sawasawa na ukoma
(c) Ubatizo unatutendea nini sisi