62. HUKUMU KATIKA NYUMBA YA AHABU
''Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu, ambaye Yezebeli mkewe alimchochea''
Shabaha
Ni kuonyesha jinsi Mungu alivyomwinua Yehu ili kuingamiza nyumba ya Ahabu ikiwa ni pamoja na kuwaangamiza watu wote waliokuwa wakimwabudu Baali. Wakati Eliya alipokimbilia katika Mlima Horebu, Mungu alimrudisha tena Israeli ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ya ziada. Mojawapo ya jukumu lake ni kumtia mafuta Yehu ili awe mfalme wa Israeli.Mungu alimchagua Yehu ili aiangamize kabisa nyumba ya uovu ya Ahabu.
Ahabu na Yezebeli walikuwa wametenda maovu mengi katika Israeli na njia pekee ya kuepukana na ushawishi wa matendo yao maovu-ni familia yote kuangamizwa.Eliya alikuwa amekwisha tabiri kuhusu kifo chao cha kutisha, lakini hili lilibakia kwa Elisha kumpaka mafuta Yehu awe mfalme.
2 Wafalme 9;10:18-28
YEHU ANATIWA: 2 Wafalme 9:1-15
Mfalme Ahabu aliuawa na Mfalme wa Shamu vitani, na mwana wake mwovu, Yoramu akatawala juu ya Israeli. Hata hivyo, Yezebeli bado alikuwa hai, na akiwa na uovu wake kama kawaida, na aliendelea kugeuza mioyo ya watu wngi katika Israeli kuacha kumwabudu BWANA na kumwabudu Baali.
Elisha nabii akamwita mmojawapo wa wana wa manabii, akampatia ujumbe. Alitakiwa achukue chupa ya mafuta ambayo Elisha angempa, na kwenda kumtafuta Yehu mwana wa Nimshi, mmoja wapo kati ya majemadari wa Israeli. Alitakiwa amwite Yehu na awe peke yake na yeye waingie ndani ya chumba, na kisha achukue chupa ya mafuta na kuyamimina juu ya kichwa cha Yehu na amwambie, “BWANA asema hivi, Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli. Kisha ufungue mlango, ukakimbie, wala usikawie” (mstari 3). Kwa kufanya kitendo hicho cha kumtia mafuta awe mfalme wakati mfalme Yoramu ikiwa bado anatawala, ingeweza kuleta taabu moja kwa moja katika Israeli. Nabii kijana alikwenda na kufanya kama alivyoambiwa, na alipokwisha kumimina mafuta juu ya kichwa Yehu, alitabiri kazi ambazo Mungu alimchagua ili azitende. “Nawe utawapiga nyumba ya Ahabu, bwana wako, ili nijilipize kisasi cha damu ya watumishi wangu manabii, na damu ya watumishi wote wa BWANA, mkononi mwa Yezebeli. Kwa maana nyumba yote ya Ahabu wataangamia; nami nitamkatilia mbali kila mwanaume wa nyumba ya Ahabu, yeye aliyefungwa, na yeye asiyefungwa, katika Israeli” (mstari 7,8). Na kisha mjumbe alikimbia.
Jemadari wengine walikuwa wakimsubiri Yehu arudi, wakati anaporudi wangeweza kueleza kwamba Yehu alikuwa amesikia ujumbe wa kushangaza, walikuwa wanauliza, “Je! ni amani?” Yehu alipowafahamu kuhusu ujumbe wa yule nabii kijana, wakamtangaza haraka kuwa ni mfalme.Kila mmoja akalitwaa vazi lake na kulitia chini ya miguu yake juu ya madaraja na wakazipiga baragumu zao, wakasema, “Yehu ni mfalme” (mstari 13)
NYUMBA YA AHABU INAANGAMIZWA: 2 Wafalme 9:16-29
Yehu alikuwa tayari amejiandaa kulifanya jukumu ambalo Mungu amempatia.Aliwaambia majemadari wasimwache hata mmoja atoke mjini kwenda kupeleka ujumbe, ambapo yeye alitaka kwenda haraka Yezreeli, ambapo Yehu alifahamu kuwa atamkuta Mfalme Yoramu.
Yoramu alikuwa Yezreeli apate kupona majeraha aliyoyapata kutokana kwa washami katika vita alipokuwa akipigana na washami. Ahazia, mfalme wa Yuda alikuwa amekuja kumtazama.
Wafalme wote hawa wawili walikuwa na uhusino, maana wote wawili walikuwa wanatoka katika nyumba ya Ahabu (Yoramu alikuwa ni baba mdogo wa Ahazia).
Katika mnara wa mlinzi wa Yezreeli, mlinzi akaliona kundi la wanaume ambao wlikuwa wanakimbia wakivuka bonde kwelkea mji wa Yezreeli. Ndipo mfalme Yoramu akaagiza atumwe mpanda farasi ili aende kujua kama wanakuja kwa amani. Mjumbe alikimbia ili kukutana na wapanda farasi lakini hakurudi na jibu.Mjumbe wa pili akatumwa, na yeye pia hakurudi. Matokeo yake,kikosi cha wanaume hao wakaukaribia mji. Mlinzi aliweza kumtambua mtu aliyekuwa mbele ya kikosi cha wanaume hao, hakuwapo mwingine anayeendesha kwa kasi kama Yehu.
Yoramu alianza kuhisi ishara ya vita. Gari lake liliwekwa tayari na yeye na Ahazia wakatoka ili kumlaki Yehu. Na alipomkaribia, alimwuliza jemadari wa jeshi lake, “Je! ni amani?” Yehu akajibu, “Amani gani, maadamu uzinzi wa mama yako Yezebeli na uchawi wake ni mwingi?” (mstari 22)
Ghafla, alielewa kusudi la Yehu kufika hapo, ndipo Yoramu akageuka na kukimbia, akamwambia Ahazia, “Ni uhaini, Ahazia”. (mstari 23)
Yesu akauvuta upinde wake kwa nguvu zake zote, akampiga Yoramu kati ya mikono yake, akaanguka katika gari lake, akafa. Ahazia akakimbia ili kuokoa maisha yake, lakini Yehu akampata na kumwua pia.
YEZEBELI ANAUAWA: 2 Wafalme 9:30-37
Basi Yehu akaingia Yezreeli. Sasa Yehu alikuwa mfalme na habari ikamfikia Yezebeli. Yezebeli hakuwa ni mtu ambaye ungeweza kumkimbia. Badala yake alivalia nguo nzuri za mapambo, “akatia wanja machoni pake” (mstari 30) na akachungulia dirishani.Yehu alipofika penye lango la mji, Yezebeli alimpatia changamoto. Yehu akainua kichwa chake kutazama dirishani akamwona Yezebeli pale, akawaita wale waliokuwa ndani ya nyumba ya mfalme, akasema, “Aliye upande wangu ni nani?” (mstari 32).
Watu wawili au watatu wakachungulia dirishani, Yehu akawambia, “Mtupeni chini” (mstari 33). Kwa hiyo wakamtupa chini akafa na akamkanyagakanyaga na farasi wake. Na mwishowe, akawaita watu waliokuwa karibu akawaambia wamzike, Akasema, “kwa-maana ni binti mfalme” (mstari 34). Na walipokwenda kumzika mbwa wa mji walitngulia kwanza. Hawakuona kitu ila fuvu pekee yake la kichwa chake na vitanga vya mikono yake.
Wale watu walipomwambia Yehu alisema, “Hili ndilo neno la BWANA, alilolinena kwa kinywa cha mtumishi wake Eliya, kusema katika kiwanja cha Yezreeli mbwa wataila nyama ya Yezebeli” (mstari 36)
YEHU NA MANABII WA BAALI: 2 Wafalme 10:18-28
Yehu aliendelea kuwaangamiza wana wote sabini wa Ahabu na Yezebeli.Na kisha akapanga mpango wa kuwaangamiza manabii wa Baali, ambao walikuwa wanamtumikia Yezebeli, pamoja na wale wote waliokuwa wanamwabudu Baali. Aliwadanganya kuwa amekuja ili kuungana na wao kuwa anayo dhabihu kubwa ya kumtolea Baali wao. Yehu akasema, “Ahabu alimtumikia Baali kidogo, bali Yehu atamtumikia sana” (mstari 18). Aliwaambia wote wamwabuduo Baali wafike; na asiyekuwapo basi auawe. Kwa Yehu alituma wajumbe katika Israeli yote na ndipo wote waliomwabudu Baali wakaja. Walikusanyika wote pamoja katika nyumba ya Baali, ambayo Yezebeli alijenga. Nyumba ya Baali ikajaa “tangu mlango hata mlango” (mstari 21). Yehu akaagiza wapewe kila mmoja vazi jeusi ili wavae kwa kuwa ndilo vazi lililovaliwa na watu wamwabuduo Baali. Yehu akaagiza, “Tafuteni mkaangalieni, asiwepo hapa pamoja nanyi mtu amtumikiaye BWANA, ila wamwabuduo Baali peke yao” (mstari 23).
Wakati huu alikuwa ameshajiwekea maaskari themanini kuizunguka nyumba ya Baali, ili asiokoke hata mmoja kati yao wamwabuduo Baali. Ndipo watu waliokuwa ndani walipokuwa wakimtoa dhabihu Baali, Yehu akawapatia ishara wale watu aliowaweka. “Ingieni mwapige, mtu awaye yote asitoke” (mstari 25). Kwa hiyo wote wamwabuduo Baali na pamoja na manabii wa uongo wakauawa siku moja. Wakazitoa sanamu zilizokuwamo ndani wakaziteketza kwa moto; wakazivunja madhabahu na kuiangusha nyumba ya Baali pia. “Ndivyo Yehu alivyomharibu Baali katika Israeli” (mstari 28).
FUNDISHO KWETU
Katika Torati, wana wa Israeli waliambiwa wampende BWANA, Mungu wao kwa moyo wao wote, na kwa nguvu zao zote, na kwa akili yao yote. Wasingeweza kumwabudu BWANA na Baali. Katika Mlima Karmeli walifundishwa kwamba BWANA ndiye aliye Mungu wa kweli, lakini Ahabu na Yezebeli walikuwa wakiendelea kuwafundisha watu amwabudu Baali. Kwa hiyo walisthili kuuawa.Kama tunampenda Mungu na njia zake, tutayachukia mambo yote ambayo Mungu anayachukia.Mwandishi wa Zaburi aliandika: “Sheria yako naipenda mno ajabu, ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa” (Zaburi 119:97). Na wakati alipozifikiria jinsi sheria za Mungu zilivyo nzuri na za haki aliiandika: “Kila njia ya uongo naichukia” (mstari 128).
Na kuhusu Bwana Yesu Kristo, ambaye alimpenda Baba yake kwa ukamilifu, imesemwa hivi, “Umeipenda haki; Umeichukia dhuruma.” (Zaburi 45:7). Na hili ni fundisho kwetu sisi.Ni lazima tumpende Mungu kwa moyo wote na ni lazima tuchukie kila njia za uovu. Mungu atawaangamiza watenda maovu wakati atakapomtuma Bwana Yesu Kristo kuja hapa duniani ili kutawala milele.
MASWALI
Majibu ya Kina
1. Ni jinsi gani Ahabu alivyokufa?
2. Mungu alimwinua nani kuiharibu nyumba ya Ahabu?
3. Yehu ni nani?
4. Ninani aliyemmpaka mafuta ehu?
5. Nikwa nini Yehu alikwenda Yezreeli?
6. Ni jinsi gani mfalme Yoramu alivyokufa?
7. Je, Yezebeli alifanya nini aliposikia kuwa Yehu anakuja?
8. Yehu aliwaambiwa watu waliokuwapo pale ikulu wamtendeje Yezebeli?
9. Ni nani aliyekuwa ametabiri kuwaYezebeli atakufa kifo cha namna hii?
10. Yehu aliwaalika nani waje wakati anapomtolea dhabihu kubwa Baali?
11. Ni fundisho gani tunalojifunza kutokana na mbinu aliyoitumia Yehu kuiangamiza nyumba yote ya Baali?
Majibu ya Kina
12. Eleza jinsi Yehu alivyopakwa mafuta?
13. Eleza jinsi Yehu alivyomwua mfalme wa Israeli?
14. Eleza jinsi Yehu alivyowadanganya wamwabuduo Baali na akawaangamiza wote ?