CSSA 1-3-14 - HEZEKIAH - JUDAH'S GREATEST KING

Swahili

64. HEZEKIA-MFALME MKUU WA YUDA

 

''Enyi wana wa Israeli,mrudieni BWANA''

 

Shabaha

Ni kuonyesha jinsi Hezekia alivyogeuza mioyo ya watu kumwelekea Mungu. Kati ya wafalme wote wa ufalme wa kaskazini wa Israeli, hakuna hata mmoja aliyempenda BWANA, Mungu wao.Miongoni mwa wafalme wa Yuda uliokuwa ufalme wa kusini baadhi yao walizidi sana katika uovu, lakini wachache walifuata mfano wa Daudi.Kati ya hao waliokuwa mfano aliyewazidi wote ni Hezekia. Baba yake, Ahazi, alikuwa ni mtu mwovu, “akaziendea njia za wafalme wa Israeli” (2 Mambo ya Nyakati 28:2). Alimfukizia Baali uvumba, na akaufunga mlango wa Hekalu la Mungu katika Yerusalemu. Na kwa sababu ya Ahazi, “BWANA akawainamisha Yuda” (mstari 19). Ni jambo la kushangaza kuwa mwana wake alithibitisha kuwa mfalme mkuu wa wafalme wa Yuda. “Alimtumaini BWANA Mungu wa Israeli; hata baada yake hapakuwa na mfano wake katika wafalme wote wa Yuda, wala katika hao waliomtangulia” (2 Wafalme18:5)

2 Mambo ya Nyakati 29 na 30

 

KAZI YA KWANZA YA HEZEKIA: 2 Mambo ya Nyakati 29:1-9

Hezekia alikuwa na umri wa miaka 25 alipoanza kutawala.Jambo la kwanza alilolifanya katika mwezi wa kwanza wa kutawala kwake, ilikuwa ni kuufungua milango ya Hekelu na kuanza kuifanyia ukarabati.Alitambua umhimu wa kuigeuza mioyo ya watu imwelekee Mungu. Watu walipaswa ajifunze tenajinsi ya kumwabudu katika roho na kweli.

 

Milango ilikuwa imefungwa kwa muda wa miaka mingi, kinara cha taa cha dhahabu ambayo ilitakiwa kuwaka milele ilikuwa imesha zimika, na ubani ulikuwa haufukizwi tena, sadaka zakuteketezwa na dhabihu zilikuwa hazitolewi tena katika madhabahu muda wote. Bila hata kujali ingawa Mungu alikuwa ameleta taabu nyingi juu yao.

 

Kwanza kabisa ni lazima Walawi na makuhani wajitakase na walitakasa Hekalu. Aliwakusanya pamoja wote na akawatia moyo ili waifanye kazi ya Mungu kwa uaminifu, akawaambia, “kwa maana BWANA amewachagua ninyi ili msimame mbele yake; mmtumikie” (mstari 11). Kwa hiyo makuhani n Walawi walitakiwa waweke kando mambo yote na kuindaa mioyo yao na akili yao kwa ajili ya kazi kubwa ambayo Mfalme Hezekia alikuwa ameikusudia. Walipokuwa tayari makuhani waliingia ndani ya patakatifu katika Hekalu na wakavioa nje vyombe vyote vilivyokuwa vichafu walivyovikuta kule, na kila kimoja ambacho hakikuwa mali ya Hekalu viliwekwa kando ya katika hema ya nje. Walawi wakavibeba kutoka hapo wakavipeleka katika mto wa kidroni na wakaviteketeza huko. Na kila mmoja alipokuwa amejitakasa tena na kuweka kila kitu kwenye utaratibu wake kwa ajili ya kuabudu, walikuja na kumwambia mfalme.

 

HEZEKIA ALITOA DHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI YA TAIFA:

2 Mambo ya Nyakati 29:20-36

Asubuhi ya siku iliyofuata, mfalme Hezekia aliamka mapema sana, maana aliazimia kufungua sherehe. Aliwaita wakuu wa Yerusalemu wakakusanyika wote pamoja na wakafuatana naye kwenda katika Hekalu. Walipeleka ng'ombe saba dume, kondoo dume saba, wana-kondoo saba, na mabeberu saba kwa ajili ya sadaka ya dhambi.

 

Makuhani walikuwa tayari wako huko wakisubiri ili watoe sadaka hizo juu ya madhabahu ya kuteketezea. Kwa njia hii, wakuu wote na mfalme waliungauma dhambi na kukubali kuwa wametenda dhambi, kwa kuwa walidharau kumwabudu Mungu kama alivyoagiza katika Torati. Wakati makuhani walipokuwa wakitoa sadaka, walawi walikuwa wakicheza na kuimba wakipiga vyombo vya muziki kama alivyoamuru Daudi miaka mingi iliyokuwa imepita.

 

Ndipo makuhani wakapiga vinubi na mapanda.Haukuwa wimbo wenye sauti ya kuufurahisha moyo, bali wimbo wa huzuni unaowakumbusha kuwa wanatakiwa kumwinulia Mungu wa mbinguni mioyo yao na kumwomba Mungu msamaha. Wakati dhabihu ilipokuwa imetolewa walawi walimwimbia BWANA wimbo wa sifa kwa maneno ya Daudi.

 

Kisha mfalme na wote waliokuwa naye katika kuabudu akainamish vichwa na wakaabudu kwa saa ya shukrani na kumsifu Mungu.Na walipokwisha kuziungama dhambi zao na kujiweka wakfu ili wamtumikie Mungu katika njia iliyosahihi, Hezekia akaamuru kuwa kila anayependa alete dhabihu na matoleo ya shukrani nyumbani mwa BWANA. Ikawa siku ambayo ilikuwa imeanza kwa huzuni sana ikaisha kwa furaha na shukrani.

 

Akafurahia sana Hezekia. Siku yote nzima Hezekia alikuwa amepanga kwa uangalifu mkubwa, alipanga utaratibu vizuri sawa sawa na jinsi Daudi alivyokuwa ameigiza kabla ya kufa kwake. Ulikuwa ni mwanzo mzuri wa kuanza utawala wake.

 

HEZEKIA ANAWAKARIBISHA ISRAELI WOTE KUISHIKA PASAKA:

2 Mambo ya Nyakati 30:1-9

Mfalme Hezekia aliweza kuona wazi wazi kuwa watu wa Mungu walikuwa wameiacha njia sahihi ya ibada ya kweli.Ilikuwa ni mhimu kuwarudisha katika njia ya zamani.

 

Jambo la kwanza ambalo Mungu alikuwa amewagiza katika sheria, ilikuwa ni kwenda Yerusalemu kuzitunza sikukuu. Na sikukuu ya kwanza kila mwak ilikuwa ni Pasaka, ambayo ilikuwa inasherehekewa katika mwezi wa kwanza, lakini muda huo ukawa umepita maana walikuwa wakilitakasa Hekalu. Hata hivyo, katika Torati Mungu aliwaruhusu wale ambao watashindwa kusherehekea mwezi wa kwanza washerehekea mwezi wa pili (Hesabu 9:10-11). Kwahiyo, Hezekia akaagiza kuwaita Israeli wote na Yuda kuja Yerusalemu kwa ajili ya pasaka mwezi wa pili.

 

 Aliagiza nyaraka kwa Israeli wote kutoka Beer-sheba kwa upande wa kusini mpaka Dani kwa upande wa nchi kaskazini.

 

Ulikuwa ni waraka mzuri sana.Hezekia aliandika katika waraka; “Enyi wana wa Israeli, mrudieni BWANA, Mungu wa Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, apate kuwarudia waliosalia wenu waliookoka mikononi mwa mfalme wa Ashuru” (mstari 6). Aliwakumbusha kwa njia hii kuhusu ahadi nzuri sana ambazo Mungu aliwaahidi baba zao miaka mingi iliyokuwa imepita.Aliwasihi wanyenyekee waje Yerusalemu katika Hekalu la Mungu. Katika siku za Selemani wote walikuja kuzishika sikukuu, lakini ikawa baada ya ufalme kugawanyika; ufalme wa kaskazini hawakuja tena Yerusalemu kuzishika sikukuu.

 

Hezekia, kwa moyo wa upendo anawakaribisha kwa wema ili wote waje kwa pamoja kumwabudu Mungu. Hezekia alifahamu kabisa kuwa wafalme wa Ashuru waliokuwa wamewateka baadhi ya watu wa Israeli, watarudishwa haraka ikiwa tu watu watageuza mioyo yao kumwelekea Mungu na wamwombe Mungu msaada. “Kwa kwa BWANA Mungu wenu ndiye mwenye neema, na mwenye rehema, wala hatawageuzia mbali uso wake, mkimrudia” (mstari 9).

 

WANAISHIKA PASAKA: 2 Mambo ya Nyakati 30 :10-22

Wajumbe waliotumwa nyaraka walipowafikia watu wa makabila ya kaskazini wengi “wakawacheka na kuwadhihaki” (mstari 10), lakini baadhi yao walinyenyekea na kwa hiari yao walikuja Yerusalemu. Hata hivyo katika Yuda watu wote wakakubaliana kwa furaha kuitimiza amri ya mfalme. Kwa hiyo siku ilipokaribia, kulikuwa na kusanyiko kubwa sana, walikuwepo Yerusalemu watu wengi sana. Na madhabahu yoyote aliyoifany mfalme Ahazi ilipoonekana ziliondolewa na kuzitupa nje ya mji katika mto kidroni. Watu walijionyesha kuwa amejiandaa kuishika Pasaka, lakini miaka mingi ilikuwa imepita tangu waliposhika pasaka hii, na sasa watu wengi hata walikuwa hawajui Mungu aliwaagiza wafanye nini. Hezekia akawaombea, “BWANA mwema na amsamehe kila mtu, aukazaye moyo wake kumtafuta Mungu” (mstari 18-19).

 

Mungu akamsikia Hezekia maombi yake, akazikubali dhabihu zao. Kwa hiyo wakafanya sikukuu siku saba kwa furaha kubwa. Na Walawi na makuhani wakamsifu Mungu kila siku, wakiimba na kucheza kwa nguvu zote kwa vyombo vyenye sauti kuu.Mfalme akawafurahisha na kuwahimiza Walawi kuingia katika kusanyiko ili kuwafundisha watu, “maarifa mema ya BWANA” (mstari 22).

 

WATU WAKABAKIA SIKU SABA NYINGINE:2 Mambo ya Nyakati 30:23-27

Kila mtu alifurahi sana ikawa ilipofika mwisho wa sikukuu wote wakakubliana wafanye sikukuu siku saba nyingine. Hezekia na wakuu wakawapatia watu hao maelfu ya ngo'ombe na maelfu ya kondoo ili waendelee na sikukuu wamtolee Mungu dhabihu maana walimwabudu Mungu na Walawi walikuwa wamewafundisha Sheria ya BWANA.

 

“Ikawa furha kuu katika Yerusalemu; kwa sababu tangu siku za Selemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, hayajakuwako mambo kama hayo huko Yerusalemu” (mstari 26)

 

Makuhani wakakawabariki watu naye Mungu akasikia maombi yao “Sala yao ikafika hata makao yake mataktifu, yaani mbinguni” (mstari 27)

 

FUNDISHO KWETU

Na tunasoma kwamba, “katika kila kazi aliyoanza kwa utumishi wa nyumba ya Mungu, n kwa torati, na kwa amri, ili kumtafuta Mungu, aliifanya kwa moyo wake wote, akafanikiwa” (2 Mambo ya Nyakati 31:21).

 

Hatuna mfano mzuri wa kufuata kuliko huu – “kwa moyo wake wote”. Mungu hana kitu kingine cha kumridhisha. Israeli walifikiri kuwa wangeabudu sanamu na bado wakaendelea kusema katika mioyo kuwa BWANA ni Mungu wao. Hezekia alijua kuwa ni lazima warudi watembee katika njia za zamani ndivyo hata sisi tunavyopaswa kutembea katika kli yote ya Mungu.Alitafuta katika Torati ya Musa na aksoma habari ya mfalme Daudi na ndipo alipojua Mungu anataka yeye afanye nini. Na sisi pia tunatakiwa tusome Biblia kwa uangalifu sana, na kila siku, na tutapata, kama Hezekia alivyopata, na hii itatupatia furaha kubwa ya kumtumikia Mungu kwa moyo wetu wote.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Walawi walipowabariki watu, waliyasema maneno ambayo Haruni aliagizwa na Mungu jinsi ya kuwabarikia wana wa Israeli.

 

''Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabarikia watu wa Isareli; mtawaambia; BWANA akubarikie, na kukulinda; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukuhifadhi; BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani” (Hesabu 6:23-26)

 

Kwa maneno haya yenye uzuri mno Kuhani Mkuu alimwomba Mungu awapatie neema wale wote walioitwa kwa jina lake.Kwa hiyo Hezekia akawaagiza makuhani wwabariki watu wote waliomtumikia Mungu kwa furaha kwa muda wa majuma mawili katika Yerusalemu.

 

Maneno haya ya baraka yanatumika katika Eklesia hata leo, wakati mtu anapobatizwa katika Kristo nakupokelewa na ndugu (yaani kaka na dada) katika ushirika.Ni tukio la furaha na tunafahamu kuwa hata Mungu hufurahi pia.

 

Ikiwa tutamwabudu Mungu kwa moyo wote kana vile Israeli walivyofanya wakati wa Hezekia, sisi pia tutapokea baraka za Mungu. Atatubariki wakati huu na kutubariki kwa kutupatia uzima wa milele katika ufalme wake.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

1. Baba yake Hezekia alikuwa ni mtu wa tabia gani?

2. Ni jambo gani la kwanza alilolifanya Hezekia alipoanza Kutawala?

3. Hezekia aliwapatia makuhani na Walawi kazi gani Waifanye?

4. Ni sadaka gani ambazo Hezekia na wakuu walitoa kwa ajili ya dhambi zao?

5. Ni sikukuu ipi ambayo Hezekia aliishika kule Yerusalemu ?

6. Ni watu gani ambao Hezekia aliwakaribisha kuja kwenye sikukuu?

7. Watu walifiriaje waraka ule wa Hezekia?

8. Watu walizifanya nini sanamu walizozikuta katika mji?

9. Sikukuu ilichukua muda gani kuisha?

10. Kila siku ya sikukuu Walawi walifanya nini?

11. Katika kila alilofanya, Hezekia alilitenda vipi?

 

Majibu ya Kina

12. Ni jambo gani alilolifanya kwanza Hezekia na ni jinsi gani makuhani na Walawi  walivyomsaidia?

13. Eleze jinsi Pasaka ilivyotunza katika siku za Hezekia?

 

ajibu ya Nyongeza.

14. Ni maneno gani ya baraka ambayo Haruni aliyatumia alipowabariki Israeli?

 

Swahili Title
064 HEZEKIA-MFALME MKUU WA YUDA
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type