CSSA 1-3-19 - IN THE FIERY FURNACE

Swahili

69. NDANI YA TANURU LA MOTO

“Uendapo katika moto hutateketea”

 

Shabha

Kuonyesha jinsi imani ya vijana watatu Wayahudi ilivyowaokoa kutoka katika kifo ndani ya tanuru la moto. Wakati Nebukadreza alipomsikia Danieli akimfunulia ndoto yake,alifahamu kabisa kuwa alikuwa amesema kweli na akamsifu Mungu wa Danieli.Alimpandisha cheo na rafiki zake watatu katika vyeo vya heshima katika uflme wake, na akamweka Danieli kuwa mkuu wa wenye hekima. Lakina pamoja na yote haya hakuweza kujinyenyekeza mwenyewe mbele za Mungu wa mbinguni.Na yeye kama wafalme wengine wa waliomtangilia, hakuweza kutambua kuwa ufalme wake unakwenda kufikia mwisho wake. Alipenda kutembea ndani ya jumba lake la kifalme, akiutazama utukufu wa mji mkuu wa Babeli, “mji wa dhahabu” na alifikiria nguvu zake na sifa yake. Kil wakati alikuwa akifikiria jinsi ya kuongeza utukufu wake, ili kwambs ufalme wake uwe wa milele.Moja ya mpango wake ulikuwa ni kuisimamisha sanamu ya dhahabu, kubwa sana,ili wote anaowatawala waisujudu

 

Danieli 3

 

SANAMU YA NEBUKADREZA YA DHAHABU: Danieli 3 :1-7

Nebukadreza alisimamisha sanamu yake ya dhahabu katika uwanda wa Dura ambapo wote wangeweza kuiona. Ilikuw dhiraa sitini urefu wake na upana wake dhiraa sita (yapata kama meta 27 urefu na meta 3 upana). Alipanga kuwa na sherehe maalumu na aliwaalika maliwali na wakuu wa wilaya ambao walikuwa wakitawa katika nchi alizokuwa ameziteka wafike kwa ajili ya kuzindua sanamu. Miongoni mwa watu waliopata mwaliko ni rafiki wa Danieli, Hanania, Mishaeli, Azaria, (lakini mwenyewe Danieli hakuwepo). Tena mfalme alikuwa amewabadilisha majina yao kuwa Shadraka, Meshaki na Abednego (Danieli 1:7), maana majina haya ni ya kuheshimu miungu ya Babeli.

 

Hatimaye mtangazaji wa Ikulu akafika na akawatangazia watu wote waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya amri ya mfalme. Mfalme aliamuru kwamba watu wote ni lazima wasujudie na kuiabudu sanamu mara wanaposikia sauti za vyombo. “Na kila mtu asiyeanguka chini na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto Uwakao” (mstari 6).

 

Katika muda ambao ulikuwa umeamliwa vyombo vya muziki, panda, zeze na namna zote za ngoma, tarumbeta, filimbi na kini kinumbi vikapigwa na watu wote waliokuwa wamekusanyika wakaanguka na kuabudu sanamu kubwa ya sanamu aliyo Nebukadreza alikuwa ameisimamisha. Walikuwapo wanaume watatu, ambao hawakuanguka chini. Shadraka, Meshaki na Abednego waliikumbuka amri ya BWANA, Mungu wao, inayosema, “Usiwe na miungu mingine ila mimi...usivisujudie wala kuviumikia” (Kumbu kumbu la Torati 5:7-9).

 

WAYAHUDI WANASHITAKIWA KWA MFALME: Danieli 3:8-18

Wenye hekima na washauri wa Babeli hawakupendezwa na Nebukadreza kuwapatia Danieli na rafiki zake watatu vyeo vya heshima katika utawala wake. Walitafuta sababu za kuwashitaki, lakini vijana hawa walitenda mambo kwa busara sana na walitenda kwa uaminifu, na wala halikuonekana kosa. Kwa kuwa dini yao ilikuwa ni tofauti na dini ya Wakaldayo jinsi walivyoabudu na hii ndiyo iliyoonekana kuwa ya kuweza kupata sababu ya kuwashitaki. Na hii ilikuwa ndiyo sababu Wakaldayo ilisababisha Shadraka, Meshaki na Abednego kukataa kuanguka chini na kusujudia sanamu ya dhahabu licha ya amri iliyokuwa imewekwa na mfalme. Kwa hiyo hawakuchelewa hata kidogo kupeleka taarifa kwa mfalme kuhusu habari ya wao ya kutoitii amri ya mfalme. “Wako wayahudi kadha wa kadha waliowekwa juu ya mambo ya wilaya ya Babeli, yaani Shadraka, Meshaki na Abednego; watu hawa, Ee mfalme, hawakujli wewe, hawaitumikii miungu yao, wala kuiabudu ile sanamu yako ya dhahabu uliyoisimamisha” (mstari 12).

 

Nebukadreza alighabika sana na kwa hasira akaagiza watu hao waletwe kwake. Walikuwa wakifanya majukumu yao kwa uaminifu kabisa, hivyo akaona basi kulikuwa na jambo.

 

Angewapatia nafasi nyingine ili waamue. Mfalme akawatahadharisha, “bali, msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani atakaye waoko ninyi na mikono yangu?” (mstari15).

 

Nebukadreza alifahamu kuwa Mungu wao alikuwa ni mfumbuaji wa siri, lakini hakuamini kuwa Mungu huyu alikuwa na nguvu juu ya moto, kwa kuwa Wakaldayo wenyewe walikuwa wakiabudu mungu wa moto. Vijana hawa hawakutikisika katika imani yao. Ufahamu wao wa imani ulikuwa umekomaa. Wale vijana wakasema, “Mungu wetu tunayemtumikia anaweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto”. Walikuwa na imani kamili kwa BWANA, maana walimjua Mungu angeweza kufanya mambo yote, hata kuwaokoa katika hiyo tanuru ya moto, ikiwa ni mapenzi yake. “Basi kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha” (mstari 18).

 

IMANI INAUZIMA MOTO: Danieli 3:19-30

Mfalme aligadhabika sana kwa hasira.Ni kwa jinsi gani hawa Wayahudi walivyomtukana! Mfalme asingeweza kuvumilia ukosefu wa utii wa aina hiyo hivyo akaamuru tanuru lichochewe moto mara saba moto wake uwe mkali kuliko mwanzo.Akawaita askari wake wenye nguvu wawafunge kamba Shadraka, Meshaki na Abednego na kisha wawatupe ndani ya tanuru la moto. Na ndipo hawa vijana watatu wakafungwa kamba sawasawa hali wakiwa wameva suluali, kanzu, joho kofia zao katikati ya tanuru la moto. Mwako wa moto ukawaunguza na kuwaua wale waliowatupa Shadraka, Meshaki na Abednego katikati ya tanuru lililokuwa na moto mkali sana. Kwa hiyo hasira ya mfalme ikatulia kwa wa aliwaona wale waliompinga wakiwa wameadhibiwa.

 

Ghafla mfalme aliinuka haraka akatazama kwa mshangao. Akawauliza washauri wake, Je! hatukutupa watu watat katikati ya moto? Wakamjibu mfalme, Kweli, Ee mfalme. Na maajabu hakuwaona watu watatu, bali watu wanne, waliokuwa wakitembea katikati moto bila kuwa na madhara yoyote na mwonekano wa yule mtu wa nne alionekana kama “Mwana wa Mungu” (mstari 25). Yule wa nne hakika alikuwa ni malaika wa Mungu, aliyetumwa na Mungu kulinda watumishi wake

 

Kisha Nebukadreza mwenyewe akakaribia mdomo wa tanuru akasema, “Enyi Shadraka, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu aliye jui tokeni, mje huku” (mstari 26). Ndipo Wayahudi waaminifu wakatoka katika ule moto.

 

Ndipo wale maamiri waliokusanyika pale kwa mshanga sana wakawatazama kwa kuwakazia macho wale watu, “ambao moto haukuwa na nguvu ya miili yao, wala nyele za vichwa vyao hazikuteketea, wala suruali zao hazikubadilika, hawa harufu ya moto hikuwapata hata kidogo” (mstari 27). Ulikuwa ni mmwujiza ambao waliuona kwa macho yao. Mfalme angefanya nini, isipokuwa ilikuwa ni kumsifu Mungu wao. Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme nakujitoe miil yao ili wasimtumikie mungumwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe (mstari 28).

 

Basi Nebukadreza akaweka amri kwamba mtu yeyote katika ufalme wake, kutoka taifa lolote, kutoka kila lugha yoyote atakayeneno lisilofaa juu ya huyu Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abednego, watakatwa vipande vipande na nyumba Mungu zao zifanywa jaa; “kwa kuwa hakuna Mungu mwingine aokoaye namna hii” (mstari 29)

 

FUNDISHO KWETU

Hawa vijana watatu Wayahudi katika Babeli wanasimama wakiwa ni kielelezo cha imani, kwa maana “kwa imani walizima nguvu za moto” (Waebrania 11:33-34).

 

Katika mioyo yao waliahidi kutii amri za Mungu, siyo kwa wakati mambo ylipokuwa ni mazuri, ambapo kwa kawaida ni rahisi, bali hata wakati wa shida na taabu na majaribu pia.Wlifahamu kuwa Mungu anaweza kuwaokoa, lakinihata kama asingewaokoa bado wan gezitii amri zake.

 

Tunaweza tusitupwe katika tanuru la moto, lakini jaribu ni la aina moja. Imani yetu ni lazima ionkane katika vitendo vyetu.Wao walikuwa wakiwa wanamwamini na kumpenda Mungu.

 

Kwa hiyo walikuwa wameandaliwa kukabiliana na kujaribiwa kwa imani yao majaribu yatakapowafikia. Mungu hupima imani za wale awapendao. Ni lazima tuandae mioyo yetu sasa tujifunze njia yake ili majaribu yatakapotupata tuweze kusimama imara kama wao walivyoweza kukabiriana nalo la walipotupwa ndani ya tanuru la moto.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

1. Nebukadreza alisimamisha nini katika uwanda wa Dura?

2. Kila mtu alitakiwa afanye nini asikiapo sauti ya vyombo vya muziki, na ngoma za kila

    aina?

3. Ni nani waliokataa kuanguka chini na kusujudu sanamu ya dhahabu?

4. Ni adhabu gani aliyopewa mtu asiyeanguka chini na kusujudu sanamu ya dhahabu?

5. Ni jibu gani Wayahudi wale watatu walimpatia Nebukadreza alipokuwa amewapatia nafasi  

    nyingine?

6. Ni agizo gani Nebukadreza aliloliweka Wayahudi watatu walipokataa kumtii yake?

7. Ni watu wangapi ambao Nebukadreza aliaona ndani ya tanuru la moto?

8. Ni aliyekuwa wa nne ndani ya tanuru?

9. Nebukadreza aliwaita jina gani Wayahudi watatu alipoona kuwa moto hauna nguvu ya miili yao?

10. Ni amri gani aliyoiweka Nebukadreza baada ya Wayahudi watatu kutoka katika moto bila

      madhara yoyote?

11. (a) Ni amri gani aliyoiweka Nebukadreza aliiweka kwa ajili ya sanamu ya dhahabu?

      (b) Ni kwa nini Shadraka, Meshaki na Abednego walikataa kuanguka na kusujudia sanamu

            ya dhahabu?

      (c) Tunajifunza somo gani kutokana na hili?

12. (a) Eleza kilichotokea wakati Wakaldayo walipokwenda kumlalamikia Nebukadreza kuhusu

           Shadraka, Meshaki na Abednego kuwa walikataa kuanguka nakusujudia sanamu ya

           dhahabu

      (b) Eleza jinsi Mungu alivyowaokoa Wayahudi watatu?

 

 

 

Swahili Title
069 NDANI YA TANURU LA MOTO
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type