CSSA 1-3-23 - NEHEMIAH BUILDS THE WALLS OF JERUSALEM

Swahili

73. NEHEMIA ANAJENGA KUTA ZA YERUSALEMU

“Haya! na tuondoke tukajenge”

 

Shabaha

Kuonyesha namna Nehemia aliporudi Yerusalemu alivyowaandaa watu kujenga tena kuta zake na milango. Mungu hakuwasahau watu wake kamwe. Hata ingawaje wana wa Israeli mara nyingi walimsahau yeye, bali Mungu kamwe hakusahau Israeli, kwamba ni wakati walikupotwaliwa mateka katika nchi ya mbali; au wapo katika kona nne za dunia walikotawanyikia kama ilivyo leo. Katika utawala wa Ahasuero, wakati Esta alipokuwa malkia, Mungu alikomboa watu wake na maadui zao na kuwalinda wale waliorudi Israeli kulijenga tena Hekalu. Na sasa katika mwaka wa ishirini wa utawala wake Ahasuero, mawazo ya mbeba kikombe cha mfalme yalikuwa mbali sana upande wa magharibi akiwaza nchi ya baba zake. Mtu huyu mwaminifu, alikuwa Nehemia; ambaye moyo wake ulitamani sana arudi mji wa Yerusalemu. Ndugu yake Hanani, alikuwa amerudi kutoka Yuda akiwa na taarifa ya kusikitisha sana wa hali aliyoiona kule Yerusalemu. Taarifa hii ya kusikitisha ndiyo iliyobadilisha maisha yote ya Nehemia.

 

Nehemia 1; 2; 4 na 6

 

TAARIFA YA HUZUNI KUTOKA YERUSALEMU: Nehemia 1

Hanani alisema kuwa Wayahudi waliokuwa wamerudi kutoka utumwani walikuwa katika dhiki kubwa.Na maadui walikuwapo pande zote wakiwashambulia. Watu walikuwa ni maskini sana. Nazo kuta za Yerusalemu zilikuwa zimebomolewa na milango ilikuwa imeteketezwa kwa moto. Hakuna jambo lililokuwa likifanyika vizuri kule. Ilikuwa ni taarifa iliyoonyesha kuwa hali ilikuwa ni mbaya kule hakika.

 

Nehemia aliposikia habari hizi alifadhaika sana. Aliketi, akalia, na akaomboleza, na akafunga, na akamwomba Mungu wa mbinguni. Nehemia aliomba usiku na mchana kwa ajili ya ndugu zake waliokuwa Yuda. Nehemia alifahamu kuwa walikuwa katika mateso kwa sababu walitenda dhambi, maana aliyakumbuka maneno yaliyoandikwa katika torati ya Musa, mtumishi wa Mungu (Kumbu kumbu la torati 4:25-30). Kama wasingemtii, Mungu angewatawanyia katika mataifa, na hakika ndivyo alikuwa amefanya.

 

Pamoja na hayo yote, Nehemia aljua kuwa kama wakiziungama dhambi zao na kutubu na wakimgeukia tena Mungu, Mungu alikuwa tayari kuwasamehe na kuweza kuwarudisha katika nchi yao tena. Hili lilikuwa ni tumaimani la Nehemia, maana alimpenda Mungu na akawapenda watu wake, Wayahudi. Kwa hiyo alikusudia kurudi katika ile nchi ili kuona jinsi ambavyo angeweza kuwasaidia, kwa kuwa iliwapasa watu wajifunze namna ya kufanya kazi za Mungu kwa furaha na kutafuta msamaha wa Mungu. Ni kwanjia hiyo tu wangeweza kufanikiwa. Ilikuwa yapata kama miezi minne tangu Hanani alete taarifa hiyo, Nehemia alipomwomba Mungu ampe kibali mbele ya Mfalme Ahasuero. “Nakuomba sana, unifanikishe, mimi mtumishi wako, leo, ukanijalie rehema mbele ya mtu huyu” (mstari 11)

 

NEHEMIA ANAMWAM IA MFALME: Nehemia 2:1-8

Kwa muda ambao Nehemia alikuwa akimpatia mfalme divai, hakuwa akisaidia bali uso wake ulionyesha masikitiko yaliyokuwa yameujaa moyo wake. Mfalme aliyaona masikitiko hayo haraka akamwuliza “Mbona umesikitika uso, nawe huna ugonjwa? Nini hii, isipokuwa ni huzuni ya moyo?”

 

Nehemia aliogopa sana, maana alifahamu kuwa kwenda mbele ya mfalme ukiwa na huzuni inamaanisha uuawe. Kwa hiyo alimwambia sababu ya huzuni yake: “Kwani uso wangu usiwe na huzuni, iwapo mji, uli mahali pa makaburi ya baba zangu, unakaa ukiwa, namalango yake yameteketezwa kwa moto?” (mstari 3). Mfalme aliweza kuona jinsi Nehemia alivyokuwa amefadhaika sana akamwambia, “Una haja gani unayotaka kuniomba?” (mstari 4). Ndipo Nehemia akatambua kuwa kweli mfalme alidhamiria moyoni mwake kumsaidia, na hapa ilikuwa ndiyo nafasi yake kuomb ruhusa ili arudi Yerusalemu. Muda ule ule alimwomba Mungu ambariki ili maombi yake yapate kibali kwa Ahasuero. Ndipo alilomwomba mfalme ampe ruhusa aende Yerusalemu kuujenga mji. Mfalme alimwuliza aseme atakaa kule muda gani na atarudi lini na tena mfalme alimwahidi kuwa atampatia nyaraka za kifalme azipeleke Nehemia kwa maliwali wa majimbo kote ambako angepita. Nehemia aliomba pia waraka kwa mtunza msitu wa mfalme ili akate miti ya kufanyia boriti kwa ajili ya malango ya ukuta wa mji, kwa maana shauku yake kubwa ilikuwa ni kujenga kuta na malango ya Yerusalemu tena.

 

NEHEMIA ANAWATIA MOYO WATU: Nehemia 2:9-20

Kwa hiyo Nehemia alirudi Yerusalemu, akifuatana na maakida wa jeshi na wapanda farasi wa jeshi la mfalme wa Uajemi. Na majirani zao Wasamaria na Waamoni waliposikia habari hizi walihuzunika sana walifahamu “kwa kuwa amekuja mtu kuwatakia heri wana wa Israeli” (mstari 10). Nehemia alingoja kwa muda wa siku tatu Yerusalemu. Ilipokuwa ni usiku alitoka akiwa na watu wachache tu akichunguza kwa siri uharibifu uliofanyika kwenye kuta na malango. Hata hivyo, hakumwambia mtu yeyote kuhusu mpango wa ajabu ambao alikuwa amemwomba Mungu. Kikundi cha watu wachache kwa siri walizunguka eneo lote la mji lililokuwa limeharibiwa na Nehemia akatambua kuwa kweli Hanani alisema ukweli. Na hatimaye aliwaita Wayahudi wote kawaambia mpango aliokuwa nao. “Mnaona hali hii dhaifu tuliyo nayo, jinsi Yerusalemu ulivyo hali ya ukiwa, na malango yake yalivyoteketezwa kwa moto; haya / na tuujenge tena ukuta wa Yerusalemu, ili tusiwe shutumu tena” (mstari 17). Aliwaambia jinsi Mungu alivyombariki, na majibu ambayo mfalme alimweleza kuhusu ombi lake la kurudi. Alikuwa na juhudi sana na shauku ya kujenga, na watu kwa furaha wakakubali kushirikiana naye, Nao wakasema, “Haya / na tuondoke tukajenge”, na haraka wakapnga jinsi ya kuanza kumsaidia kujenga. Ndipo Sanbalati, Tobia walikuwa hawaishi mbali waliposikia habari hizi na ndiyo waliohuzunika Nehemia aliporudi, waliwacheka na kuwadharau. Walimshitaki Nehemia kwa kumwasi mfalme, naye Nehemia alikuwa yuko tayari kukabiliana na upinzani huo alisema: “Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondoka na kujenga; lakini ninyi hmna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu” (mstari 20)

 

Na familia nyingi za Wayahudi walikuja wakaanza kujenga tena baadhi ya maeneo ya ukuta, hata ikawa kazi inafanyika mji mzima.

 

KUTA ZINAJENGWA: Nehemia 4

Familia zilizokuwa zinajenga ukuta zilikuwa na bidii sana. Walifurahia kumpata kiongozi wao Nehemia. Wakati Sanbalati na Tobia walipojaribu kuizuia kazi, Nehemia alimwelekea Mungu na wala kamwe hakuwaacha watu kuvunjika moyo. Sanbalati kwaa huzuni alisema, “Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! watajifanyizi boma? watatoa dhabihu? au watamaliza katika siku moja? Je! watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto” Tobia akawadhihaki, akasema, “Hata hiki wanachokijenga,angekipanda mbeha, angeubomoa ukuta wao na mawe” (mstari 3). Nehemia aliendelea kuwatia watu nguvu na akayapuuza maneno ya maadui wao. Lakini majirani wa Wanyahudi waichukia sana kuona ukuta ukizidi kujengwa, wakapanga njama ya kuungana ili kuishambulia Yerusalemu, “Bali sisi tulimwomba dua Mungu wetu, tena tukaweka walinzi mchana na usiku, kwa sababu yao” (mstari 9). Nehemia akawaweka tayari watu waliokuwa na panga, mikuki na mishale na akawaambia wasiogope, bali wamkumbuke Mungu wao, aliye mkuu mwenye kuogofya, ambaye angewasaidia kupigania nyumba zao. Kuanzia wakati huu na kuendelea nusu ya watumishi wakachukua siraha na kulinda na nusu ya watumishi waliobakia waliendelea na kazi ya kujenga. Hata ikawa waliokuwa wanajenga wakajenga kwa mkono mmoja na mkono mwingine ukashika upanga walikuwa tayari kwa yote mwili.Mtu mwenye kupiga baragumu alikuwa na Nehemia wakati wote,ambaye angeipinga ikiwa angeona hatari.Na kama baragumu ingepigwa watu wote wangekusnyikia mahali alipokuwa Nehemia.Kwa hiyo kazi iliendelea na watu wakatoka vijijini kwao na kwenda kuishi ndani ya mji.Walilinda wakati wa usiku na mchana wakaendelea na kazi ya kujenga.Sasa kila mmoja aliweza kuona kuwa hakuna tena ambacho kingewazuia wasimalize kuzijenga kuta.

 

KUTA ZIKAMALIZIKA:Nehemia 6

Pia Nehemia alikuwa shupavu,slifakuwa Mungu alikuwa upande wake kwa kuwa kuna wakati Sanbalati alijaribu kumdanganya ili ashuke wakutane nje ya eneo kuta walizokuwa wanajenga. Akaona kuwa ulikuwa ni mpango wa uovu wa kumkamata au kumwua Nehemia,Nehemia akajibu, “Hii ni kazi kubwa ninayoifanya mimi, hata nisiweze kushuka; mbona kazi ikome hapo ninapoiacha,niwashukie?”(mstari 3). Walijaribu mbinu hii ya kudanganya mara nne, lakini Nehemia hakudanganyika. Na wakati mwingine walisambaza waraka kwa kila mmoja ndani ya mji wakimtuhumu Nehemia kuwa anataka awe mfalme. Nehemia akasema, “Hakukufanyika mambo kama hayo uyasemayo” kwa maana Nehemia alijua kuwa ni wao wenyewe wameyabuni (mstari 8).

Bado waliendelea kujaribu kumdanganya Nehemia kwa kumwogopesha wakamshauri aende kujificha ndani ya Hekalu. Nehemia aliwajibu, “Je! mtu kama mimi nikimbie? Sitaingia” (mstari 11)

 

Kwa hiyo kwa ajili ya kudumu katika kumwomba Mungu, Nehemia alitiwa nguvu za kuendelea kuwashinda maadui wake waliokuwa wanajaribu kudhoofisha mikono yao na kutaka kuizuia kazi. Katika siku ya hamsini na mbili ukuta ukamalizika.

 

FUNDISHO KWETU

Nehemia alikuwa ni mtu wa maombi na matendo. Katika kila alilolifanya alimwomba Mungu amsaidie na amwongoze, na kwa hili anakuwa ni mfano mzuri sana kwetu. Hakuyavamia mambo, bali aliweka utaratibu mzuri na kisha, baada ya kuomba baraka za Mungu, aliwajulisha na wengine kuhusu mpango wake. Hii ilikuwa ni busara, kwa kuwa ni rahisi sana kuongea mambo mengi tunayotaka kufanya kabla hatujayawapatia mawazo yetu makini.Hata wakati alipokuwa amesimama mbele ya mfalme, alimwomba Mungu kimya kimya na kwa haraka. Hata mfalme asingeweza kuelewa kuwa alikuwa anaomba, lakini maombi ilikuwa ni sehemu ya maisha yake hata mawazo yalikuwa tayari wakati wote kumgeukia Mungu. Hii ni hali ya utaratibu wa akili tunaotakiwa kuuanza tunapokua-kila mara kumweka Mungu karibu na mawazo yetu.

 

Nehemia pia alikuwa ni mtu wa juhudi sana. Maadui zake walibuni sana jinsi ya kumdanganya, lakini alifahamu jambo sahihi na akalishikiria hilo. Na kamwe tusichukuliwe na watu wanaojaribu kutuzuia kumtumikia Mungu. Tunayo kazi ya kufanya-katika kusoma masomo yetu ya Biblia kila siku, katika kusoma Biblia na hata katika mambo mengine tunayoweza kuyafanya kwa kuwaonyesha watu wengine wema wa Mungu. Ni lazima tufanye kazi hiyo, kuacha na kutowasikiliza watu wa dunia. Na tushirikiane na familia zile zinazoipenda Kweli, na Mungu atatufanikisha, kama vile alivyozifanikisha familia katika Yerusalemu siku za Nehemia.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Ezra, mwandishi, alikuwa amesharudi Yerusalemu katika mwaka wa saba wa utawala wa Ahasuero (aliyeitwa “Artashasta” katika kitabu cha Ezra, lenye maana ndogo ya, “mfalme mkuu”). Ilikuwa ni katika mwaka wa ishirini wa kutawa kwa mfalme ndipo Nehemia aliporudi. Wakiwa wote pamoja walijaribu kugeuza mioyo ya watu wamwelekee Mungu kwa kuwaonyesha katika torati ya Musa, mambo ambayo Mungu aliwaagiza wayafanye.

 

Katika tukio mojawapo (Nehemia 8), watu walimwomba Ezra awasomee kitabu cha torati na awafafanulie. Walikusanyikia pamoja katika mtaa wa lango la maji na Ezra alisimama juu ya mimbari ya mti ili kila mmoja aweze kumwona na kumsikia. Alikuwa amesha kuwa mzee sasa na watu walimfahamu kuwa alikuwa anaifahamu vizuri torati ya Mungu. Wakati aliposimama na kukifungua kitabu, watu wote walisimama wakaomba. Makuhani kumi na tatu na Walawi walimsaidia Ezra, yawezekana maneno ya Ezra yalikuwa yanarudiwa na kila kundi la watu ili kuhakikisha kuwa kila mmoja alielewa torati ya Mungu. “Nao wakasoma katika kitabu, katika torati ya Mungu, kwa sauti ya kusikilika; akaeleza maana yake, hata wakayafahamu yaliyosomwa” (mstari 8). Ikawa watu waliposikia wakahuzunika, kwa kuwa walitambua jinsi walivyokuwa wamemwasi Mungu, wakalia na kuomboleza. Lakini Ezra na Nehemia wakawaambia watu wasiomboleze wala kulia, bali wafurahie maana hatimaye wamejua na sasa wataanza kufanya yaliyo haki. Walawi wakawatuliza watu kwa kusema, “Nyamazeni, kwa maana siku hii ni takatifu kwa BWANA; wala msihuzunike” (mstari 11). Walisimama kuanzia asubuhi na mapema hadi mchana, wakisikiliza kwa makini yote yaliyosomwa. Na sasa walipata raha moyoni na wakafurahi. Na kila mtu alikwenda nyumbani wakala chakula kitamu pamoja na nyumba yake na waliwapelekea zawadi wale ambao hawakunacho. Siku iliyofuata mkuu wa mbali za mababa za watu wote, alikwenda tena kwa Ezra. Wakati huu wakajua kuwa ulikuwa ni muda wa kuishika Sikukuu ya vibanda. Kwa hiyo wakatuma ujumbe kwa watu wote miji yao yote na katika vijiji, wakiwaambia enendeni milimani, “mkalete matawi ya mzeituni, na matawi ya mzeituni mwitu, na matawi ya mihadasi, matawi ya mitende na matawi ya miti minene ili kufanya vibanda kama ilivyoandikwa” (mstari 15). Kila mmoja kwa furaha akatengeneza kibanda katika dari ya nyumba zao na katika mitaa ya Yerusalemu na katika nyua za nyumba ya Mungu. Waliishika Sikukuu kwa muda wa siku saba sawasawa na sheria. Kila siku, Ezra  “akaisoma torati ya Mungu” (mstari 18). Haikuwa ushikwa sikukuu kwa furaha kama hiyo tangu siku za Yoshua.

 

Kwa hiyo Ezra na Nehemia wakaiimarisha mikono ya watu wakawaonyesha jinsi ya kumtumikia Mungu kwa furaha.

 

MASWALI

Majibu ya Mafupi

1. Ni nani aliyekuwa mnyweshaji wa mfalme wa Uajemi?

2. Ni ujumbe gani ambao Hanani aliupeleka kutoka Yerusalemu?

3. Ni kwa nini Mungu aliwatanya Israeli katika mataifa?

4. Watu wa Mungu walipaswa wafanye nini ili warudi katika nchi yao?

5. Ni nani aliyemwona Nehemia kuwa alikuwa mwenye huzuni?

6. Nehemia alikuwa anafanya nini mbele ya mfalme kabla hajaruhusiwa kurudi Yerusalemu?

7. Nehemia alitaka kufanya nini aliporudi Yerusalemu?

8. Nehemia alifanya nini usiku mmoja baada ya kurudi?

9. Watu walisemaje Nehemia alipowaambia mpango wake?

10. Ni nani aliyejaribu kusimamisha kazi ya kujenga?

11. Ilichukua miaka mingapi kujenga tena kuta zaYerusalemu?

12. Nehemia alisema nini wakati Sanbalati alipotaka wakutane mbali na ukuta?

13. Nehemia alikuwa ni mtu wa aina gani?

14. (a) Eleza Nehemia alifanya nini aliposikia taarifa ya Hanani kuhusu Yerusalemu

      (b) Eleza kilichotokea wakati alipokuwa akimhudumia mfalme mvinyo

15. (a) Eleza Sanbalati na Tobia walisema nini walipowaona watu wakijenga?

      (b) Eleza jinsi Nehemia alivyotia nguvu watu kuendelea na kazi ya ujenzi?

16. Ni jinsi Sanbalati walivyojaribu kumdanganya Nehemia mara nyingi na ni majibu gani ambayo

      Nehemia alijibu?

17. Nehemia na familia za Yerusalemu walijenga tena kuta. Ni kazi gani ya Mungu  

      tunayowezakufanya?

 

Majibu ya Nyongeza

 

18. (a) Wakati Ezra aliposoma kitabu cha torati ni jambo gani lililokuwa la mhimu?

      (b) Watu waliposikia maneno yaliyosemwa na Ezra aliposoma torati walijisikiaje?

      (c) Walifanya nini?

 

Swahili Title
073 NEHEMIA ANAJENGA KUTA ZA YERUSALEMU
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type