75. MASIHI ANAZALIWA
“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume”
Shabaha
Kuonyesha jinsi Mungu alivyofanya kuzaliwa kwa Mwana wake kuwekwa mhimu sana na watuwengi wakafurahi wakati alipozaliwa, ingawa maadui zake walitaka kumwua.
Ikawa baada ya malaika Gabrieli alipokwisha kumtokea Zakaria katika nyumba ya Mungu, alitumwa na Mungu akiwa na ujumbe mwingine, wakati huu alitumwa kwa bikira aliyekuwa anaishi Nazareti. Ujumbe huu ulikuwa ni wa mhimu sana kuliko ule ujumbe wa kwanza, maana ulihusu kuzaliwa kwa Masihi-ambaye Yohana angemtangaza baadaye. Muda ulikuwa umefika wa Mungu kuitimiza ahadi yake kuhusu 'mzao' au mwana ambaye angekuwa Mwokozi wa ulimwengu. Mwana wa Mungu alikuwa karibu kuzaliwa, na kwa neema kubwa ya kuwa mama wa huyo mwana wa thamani sana. Alimchagua Mariamu, bikira aliyekuwa wa ukoo wa Daudi.
Luka 1:26-38,2
MALAIKA ANASEMA NA MARIAMU: Luka 1:26-38
Mariamu alishitushwa na kutokea ghafla kwa malaika, aliyemsalimia kwa kusema, “uliyepewa neema” (mstari 28). Mariamu alishangazwa na mwonekano wa yule malaika na saalamu ya maneno ya neema. Mariamu alipokuwa kitafakari, malaika alimwondolea hofu kwa kusema, “Usiogope, Mariamu; kwa maana umepata neema kwa Mungu” (mstari 30). Katika mwenendo wake Mungu alimwona kuwa Mariamu ni mwenye huruma na mwelekevu,hata akamjalia neema hii kubwa. “Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyu atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na BWANA Mungu atampatia kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho” (mstari 31-33). Maneno haya mazuri mara moja yatakuwa yalimkumbusha unabii mwingi sana ambao alikuwa anaufahamu kuhusu Masihi. Israeli wote walijua kuwa Masihi atazaliwa katika ukoo wa Daudi na ataketi katika kiti cha enzi cha Daudi; na kwamba atakuwa mfalme juu ya Israeli, ambayo ni “nyumba ya Yakobo”, na ufalme wake utakuwa ni ufalme usiokuwa na mwisho. Huu wote ulikuwa unabii uliojulikana sana, uliosemwa mara nyingi na kurudiwa na manabii wa Agano la Kale. Ingawaje Mariamu alikuwa anafahamu maneno haya ya unabii, ni jinsi gani angezaa mtoto hali alikuwa hajaolewa.
Mariamu alikuwa ameposwa na Yusufu, mtu wa haki wa ukoo wa Daudi pia, na walitarajia kuoana baadaye ili wapate familia yao wenyewe. Lakini malaika anamwambia Mariamu kuwa kwanza ni lazima azae huyu mtoto ambaye ni wa muhimu sana.
Kwa hiyo malaika akamwambia: “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu” (mstari 35). Mungu ndiye baba wa mtoto huyu. Kwa hiyo Roho ya Mungu itamfunika Mariamu kabla ya kuolewa na Yusufu. Wakati mtoto atakapozaliwa hataitwa mwana wa Yusufu, bali ataitwa na mwana wa Mungu mwenyewe.
Hakuwa kama watu wengi ambao mara nyingi Mungu aliwaambia ahadi nzuri ajabu, Mariamu yeye hakusita wakati aliposikia ujumbe wa malaika. Mariamu kwa unyenyekevu na upole aliyakubali maneno ya malaika na kwa kule kuchaguliwa na Mungu, alisema, “Tazama mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyonena” (mstari 38).
KUZALIWA KWA YESU KRISTO: Luka 2:1-7
Nabii Mika aliandika kwamba Yesu atazaliwa sehemu inayoitwa Bethlehemu (Mika 5:2), lakini Mariamu na Yusufu waliishi Nazareti. Neno la Mungu kamwe halishindwi, hata hivyo, wakati huu lilitimizwa kwa njia ya ajabu sana.
Mtawala wa Rumi aliweka amri kwamba kila mtu aende mjini kwake kuandikwa kwa ajili ya kodi. Mariamu na Yusufu wote wawili walikuwa ni wakutoka katika nyumba au ukoo wa Daudi. Hivyo walitakiwa wasafiri kutoka Nazareti kwenda Bethlehemu, mji wa Daudi ili kuandikwa kule.
Safari ilikuwa ndefu na ya shida tena ulikuwa ni wakati ambao siku za kujifungua zilikuwea zimekaribia sana. Na kwa kuwa watu wengi walikwenda kujiandikisha Bethlehemu, nyumba ya wageni ilikuwa imejaa, Mariamu na Yusufu kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni. Na sehemu pekee walipoweza kupata kwa ajili ya kupumzika ilikuwa ni katika hori ya kulia ng'ombe na hapo ndipo mtoto alipozaliwa. “Akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe” (mstari 7).
Katika mzingira haya ya unyenyekevu, katika mji ambao mchungaji kijana Daudi alipakwa mafuta kuwa mfalme, mwana mkuu wa Daudi alizaliwa. Hakuna mtu mwingine katika mji usiku huo aliyefahamu kuhusu tukio hilo la muhimu sana ajabu katika historia ya binadamu kuwa limetokea.
WACHUNGAJI WANAAMBIWA HABARI NJEMA: Luka 2:8-20
Katika mabonde ya Bethlehemu,usiku huo huo malaika wa Mungu wakawatangazia habari njema ya ajabu sana wachungaji waliokuwa wakilinda kwa zamu wanyama wao. Ilikuwa ni wakati wa usiku wa manane, walishtukia wamezungukwa na utukukufu, ambayo kwao hawakutarajia hali hiyo, hivyo mioyo yao ikajawa na hofu kuu. Malika wa Bwana akawatokea, akawaambia, “Msiogope; kwa maana mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi ndiye Kristo Bwana. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe” (mstari 10-12), na ikawa malaika alipokwisha sema, waliona kundi kubwa la malaika wengi sana pamoja naye, wakimsifu Mungu na kusema “Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia” (mstari 14). Wachungaji hawa waaminifu walikuwa na furaha kubwa sana kwa yale waliyoyasikia na kuyaona, wakafanya haraka kwenda mjini. Walipofika na kumwona Mariamu na Yusufu na yule mtoto mchanga kama vilevile walivyokuwa wameambiwa, ndipo wakamwambia kila mtu waliyekutana naye kwamba Kristo amezaliwa katika Bethelehemu. Na watu wote waliowsikia wakashangazwa na ujumbe wao huo.Mariamu aliposikia akayatunza maneno yao hayo moyoni mwake Kisha wale wachungaji wakarudi kuchunga mifugo yao, “huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyoyasikia na kuyaona, kama walivyoambiwa” (mstari 20)
MTOTO YESU ANAPELEKWA HEKALUNI: Luka 2:21-38
Alipotimiza siku nane, mtoto litahiriwa kwa kuwa kila mtoto wa kiume alitahiriwa siku ya nane kama Mungu alivyokuwa amemwamuru Ibrahimu (Mwanzo 17:12). Siku hiyo ndipo aliitwa Yesu, kama malaika alivyomwambia Mariamu. Na siku ya arobsini Mariamu na Yusufu walikwenda Yerusalemu kutoa sadaka ya kutakasika kwao, kama ilivyoandikwa katika torati ya Musa na wamweke kwa Mungu mtoto wao mwanamume wa kwanza kuzaliwa.
Na katika Yerusalemu alikuwapo mzee jina lake Simeoni, Mungu alikuwaamwahidi kuwa hatakufa mpaka atakapomona Kristo wa Bwana. Siku hiyo Mungh akamwongoza Simeoni hekaluni, na alipomwona mtoto Yesu, alimchukua mikononi mwake akamshukuru Mungu. Akiongozwa na Roho Mtakatifu, akasema, “Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako” (mstari 29-30).
Na saa hiyo hiyo nabii mke, jina lake Ana, aliingia hekaluni. Alipokwisha kumtambua mtoto alikuwa ni nani, alimshukuru Mungu, na kisha alikwenda na kuwaambia watu wote waliokuwa wakitarajia kuja kwa Masihi.
WALIKUJA WATU WENYE HEKIMA KUTOKA MASHARIKI: Mathayo 2:1-12
Mariamu na Yusufu walirudi Bethelehemu, walikokuwa wanaishi kwa wakati huo. Na wakati huo huo, kulikuwa na nchi ya mbali upande wa mashariki, wenye hekima walitafuta ishara itakayowafahamisha alipozaliwa Masihi, mfalme wa Wayahudi. Walipoiona nyota mpya mbinguni, walijua kuwa muda ulikuwa umetimia. Walisafiri haraka safari ndefu kwenda Yerusalemu, wakiwa na zawadi (tunu) za thamani. Walipofika Yerusalemu kwa furaha na shauku walianza kuuliza, “Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudiu” (mstari 2)
Wakati habari hizi zilipomfikia mfalme mwovu Herode, kwanza aliwaita kwake makuhani wote na waandishi na akawauliza Kristo atakuwa amezaliwa wapi. Nao wakamwambia atakuwa amezaliwa katika Bethelehemu kama ilivyotabiri nabii Mika (Mika5:2). Herode akawaita wale wenye hekima akawauliza vizuri tangu wakati walipoiona ile nyota. Na kisha Herode akawapeleka Bethelehemu, akawaagiza waende huko waulize habari za huyo mtoto, ili na yeye pia kwamba atakwenda kumsujudia. Hata hivyo, Herode, alikuwa anataka ampate mtoto ili amwue mtoto huyu. Ikawa hao wenye hekima walipoondoka, “tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda kusimama juu ya mahali alipokuwapo motto” (mstari 9). Na sasa walitambua kwamba kutafuta kwao na kusafiri safari ndefu hakukuwa kwa bure. Walifurahi sana, wakaenda, wakaingia ndani ya nyumba aliyokuwamo Yusufu na Mariamu, walimwona Mariamu na mtoto mchanga pamoja Mariamu wakaanguka na kumsujudi. Wakafungua hazina zao ambazo walitoka nazo nchi yao ya mbali wakampatia zawadi; dhahabu, uvumba na manemane.
Usiku huo huo, Mungu aliwaonya katika ndoto hao wenye hekima wasirudi tena kwa Herode, wakaenda kwao kwa njia nyingine.
AMRI YA KUTISHA YA HERODE: Mathayo 2:16-18
Wakati watu wenye hekima walipokwishaondoka, malaika alimtokea Yusufu katika ndoto, akamwambia aondoke, amchukue Mariamu na mtoto akimbilie Misri, na akae huko mpaka Mungu atakapomjulisha tena, “kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize” (mstri 13).
Mara moja Herode akatambua kwamba watu wenye hekima walifahamu mpango wake mbaya. Alighadhabika sana akawa kama kichaa akapeleka amri ya kutisha, kwamba watoto wote waliokuwa katika Bethelehemu na katika wilaya zake kuwa watoto wa miaka miwili na walipungua miaka hiyo, ni lazima wauawe.
Yesu akawa salama kule Misri, wanawake wa Bethelehemu wakaomboleza kwa ajili ya watoto wao kwa kuwa watu waovu wliitimiza amri ile wakawaua watoto.
Haikuchukua muda mrefu Herode akafariki, na malaika wa Mungu alimtokea tena Yusufu katika ndoto. Sasa ilikuwa ni salama kwao wakati huu kurudi Israeli. Hawakurudi Bethelehemu, lakini wakarudi Nazareti, mahali Yesu alikokulia. “Yule mtoto akakua, akaongozeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake” (Luka 2:40)
FUNDISHO KWETU
Hebu na tuwafikirie imani ya watu walioishi Israeli wakati huo. Walikuwa wamekwisha soma vitabu vya manabii kwa makini na walikuwa wakitazamia kuja kwa Masihi. Walikuwa wakisubiri kwa bidii sana, na alipozaliwa, walikuwa na furaha kubwa sana na walitangaza habari njema ya kuzaliwa kwa Masihi kwa marafiki zao. Ulikuwa ni wakati wa furaha kuu.
Kurudi mara ya pili kwa Kristo, kutasababisha furaha kuu zaidi, siyo tu kwa Israeli bali pia kwa dunia yote. Tunaweza kujua kurudi kwake kwa njia ya kusoma vitabu vya manabii, kama wao walivyofanya. Kwa kadiri tunavyoogea kuhusu habari hizi ndivyo tunavyopata msisimko zaidi ili kujua habari hizi sana.
Hivyo inatupasa kuoma Biblia zetu kila siku ili kuyafahamu yote yanayohusu kurudi kwake mara pili, na kuzungumza na wazazi wetu nini itatokea wakati Yesu atakaporuudi. Ndipo tunapoweza kujiandaa kwa ajili yake na kufurahia kushiriki katika ufalme wake wenye utukufu.
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Ni jina gani la mtoto ambaye Mariamu aliahidiwa?
2. Baba wa mtoto atakuwa ni nani?
3. Yesu alizaliwa wapi?
4. Ni kwanini Mariamu naYusufu walikwenda Bethelehemu?
5. Haikuwepo nafasi katika nyumba ya wageni; kwa hiyo Yesu alizaliwa wapi?
6. Ni nani aliyeambiwa habari njema ajabu ya kuzaliwa kwa Yesu?
7. Mungu alikuwa amwesha mwambia nini Simeone?
8. Nabii mke, Ana, alifanya nini alipomwona mtoto Yesu?
9. Ni kwanini watu wa hekima kutoka mashariki walikuja Yerusalemu?
10. Ni kwa nini Herodi aliwapeleka watu wa hekima Bethelehemu?
11. Ni aina gani ya zawadi (tunu)ambayo watu wa hekima walimpelekea Yesu?
12. Ni amri gani ya kutisha ambayo Herode aliweka?
13. Je malaika alimwambia Yusufu akimbilie wapi?
Majibu ya Kina
14. Eleza unavyofahamu kuhusu maneno ambayo malaika Gabrieli alimwambia Mariamu?
15. Eleza kulitokea nini wakati wa usiku katika makode ya Bethelemu wakati Yesu alipozaliwa?
16. Eleza kuhusu kufika kwa watu wa hekima Yerusalemu,na jinsi walivyofuata nyota hadi
Bethelehemu?