84. YESU ANAFUNDISHA WANAFUNZI WAKE
“Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake”
Shabaha
Kuonyesha namna Yesu alivyowafundisha wanafunzi wake waonyeshe kwa matendo yao kwamba wanampenda Mungu. “Yesu akazunguka Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu” (Mathayo 4:23). Habari za mambo haya zikaenea haraka katika nchi yote na makundi mengi ya watu wakamfuata, wakiwa ni ya dhati kusikia maneno yake ya neema na kuona miiujiza ya ajabu aliyoitenda. Wakati huu Yesu alipowaona watu wengi wakimfuata alipanda mlimani akifuatiwa na wanafunzi wake.Na Yesu alipoona watu wengi wamemzunguka pale mlimani, aliwafundisha mambo mengi na kuwaonyesha baraka kubwa watakazopata wale wote wanaomfuata.
Mathayo 5,6, na 7.
NINYI NI NURU YA ULIMWENGU: Mathayo 5:14.
Yesu kwanza aliwaambia jinsi walivyobarikiwa wanafunzi wote wa kweli kwa sababu furaha inayokuja kutokana na kuufahamu ukweli. Ni tumaini la utukufu zuri ajabu lililoje tulilonalo kuwemo katika ufalme wa Mungu (mstari 2 – 12). Si kitu kwamba ni matatizo gani yatakayoweza kuja juu yetu, Mungu huko mbinguni ametuwekea zawadi kuu kama tunabaki waaminifu kwake; “Furahini na kushangilia;” Yesu akasema, “kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni” (mstari12).
Ukweli ni kama taa inaangaza nuru sehemu ya giza. Inatuonyesha njia iliyo salama kwa ajili ya miguu yetu kuweza kutembea katika njia hiyo. Katika zaburii 119:105 tunasoma “Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu” Wafuasi wote wa Kristo wanaofahamu hiyo kweli, inawapasa wao wenyewe kuangaza kama nuru katika ulimwengu huu wa giza na uovu. Hivi ndivyo Yesu alivyowaambia wanafunzi wake; “Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, na wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni” (mstari 16). Watu wengine ni lazima watuone kwamba tunamjua na kumpenda Mungu. Kwa maneno yetu na matendo, inatupasa kuionyesha nuru ya Kweli kwa dunia yote, kwani Yesu aliwambia wanafunzi wake kuwa, “Ninyi ni nuru ya ulimwengu” (mstari 14).
LAKINI NAWAAMBIA NINYI…”
Yesu alitumia muda mwingi akiwaonyesha wanafunzi wake jinsi inavyowapasa kutenda iwapo walitaka kumpendeza Mungu. Akawakumbusha kuhusu amri kumi ambazo Mungu aliwapatia wana wa Israeli kabla miaka mingi iliyopita katika mlima Sinai. Amri zile zilikuja kujulikana kama sheria za Musa, kwa kuwa ni Musa aliyewafundisha watu, kwa Waisraeli wengi sheria ya Musa ilionekana kuwa ni orodha ndefu ya vitu vilivyotakiwa kufanyika na vitu visivyotakiwa kufanyika. Mungu kwa hakika alikusudia kwamba watii amri zake, lakini kila amri ilikuwa na fundisho lake ambayo Mungu litaka wajifunze mafundisho hayo. Bwana Yesu Kristo ndiye aliyekuwa mwalimu mkuu ambaye alitakiwa kuwaonyesha kwa usahihi hasa yale mbayo Mungu alitazamia wayafanye. Alipowambia kuhusu sheria aliwaambia “msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au Manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza” (mstari 17). Hakuwa anawafundisha jambo tofauti na jinsi Mungu alivyokuwa kila wakati akiwafundisha kupitia Musa na Manabii. Kwa kweli, yeye mwenyewe alitii sheria kwa ukamilifu kila siku ya uhai wake. Tofauti na watu wengine, hakuwahi kumtenda Mungu dhambi,au kuvunja amri. Walikuwa na mwalimu mzuri ajabu kiasi gani.
HAKI YA WAANDISHI NA MAFARISAYO: Mathayo. 5:19 – 20.
Watawala wa Israeli, waandishi na mafarisayo, walikuwa wamewaongoza vibaya watu kuwatoa kwenye ukweli wa Mungu. Walikuwa na shauku sana kuhakikisha kwamba watu wawatambue jinsi wao walivyokuwa wenye haki,hata ikawa kwamba walisahau yote kumhusu Mungu. Walitenda ili watu wawaone na kuwasifia. Yesu akasema, “wamekwisha kupata thawabu yao” (Mathayo 6:2). Walijionyesha kwa sura ya nje, lakini mioyo yao ilikuwa mbali na Mungu, hivyo Yesu akawatumia kama kielelezo cha onyo kwa wanafunzi wake. Akawaambia kuwa haki yao isipozidi ile haki ya mafarisayo, hawataingia katika ufalme wa Mungu (mstari 20).
Jinsi linavyotisha onyo hilo! Wangejuaje njia sahihi ya kutenda? Yesu aliwaonyesha njia hiyo Aliwakumbusha kwamba kile Mungu alichotaka kukiona ni mioyo yenye utiifu. Iwapo mioyo yetu I safi mbele za Mungu, hatutavunja amri zake ila kuzitii ni kwa hiari.
MSIKASIRIKE: Mathayo 5:21 – 22.
Katika sheria ya Musa amri ya sita ilisema ”Usiue” (Kutoka 20:13). Uuaji ni uovu mkubwa machoni pa Mungu, chini ya sheria ya Musa muuaji yeye mwenyewe aliuawa. Yesu alipokuwa akisema kuhusu hili kwa wanafunzi wake, aliendelea kusema, “Bali mimi nawaambieni, kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu” (mstari 22). Hata hivyo, mtu anaweza asiue , kwa kuwa anaogopa hukumu hiyo, lakini moyoni mwake anafikiria maovu na hasira dhidi ya ndugu yake. Hayo mawazo maovu ya chuki na hisia (mbaya) ni mabaya vilevile machoni pa Mungu. Mtu wa aina hiyo, Bwana Yesu alisema, hafai kwa ufalme wa Mungu.
Na kwa hiyo Yesu alikuwa akiwaonyesha wanafunzi wake namna ya kuzielewa Amri za Mungu. Siyo tu tendo la kuua peke yake kuwa ndilo lililokosa ila mawazo yote yanayomfanya mtu ajisikie ya kuua.
WAPENDENI ADUI ZENU: Mathayo 5:43 – 48.
Kwa mara nyingine tana, Yesu alionyesha kwamba ilikuwa imesenenwa katika sheria, “Umpende jirani yako na umchukie adui yako” (mstari 43, soma Walawi 19:18). Ni rahisi kuwapenda wanaotupenda na walio wema kwetu, lakini tunaona ni rahisi kuwachukia wasio wema kwetu. Yesu akasema kwamba mwanafunzi wa kweli inampasa kuwa tofauti. “Lakini mimi nawaambia” Yesu akasema, “Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi” (mstari 44). Hili ni gumu zaidi, lakini ikiwa tunampenda Mungu tutajitahidi kuwa kama yeye kwani yupo tayari kuonyesha wema kwa watu wote. “Huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki ” (mstari 45).
JIWEKEENI HAZINA MBINGUNI: Mathayo 6:19 – 21
Kila mmoja anataka kuwa tajiri. Ilikuwa hivyohivyo katika siku za Yesu, aliwaambia wanafunzi wake kuweka hazina mbinguni badala yake “Jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu; wala wevi kuwavunji, wala hawaibi” (mstari 20).
Hazina ya dunia ni fedha zetu, mali zetu na vitu tunavyowezatumia muda mwingi kuviwekea akiba vinaweza kuibiwa au kuharibiwa mara moja. Hazina ya mbinguni kwa upande mwingine, inapatikana katika ghala ya neno la Mungu, yaani Biblia. Katika ghala ile tunapata hekima, ambayo ni ya thamani kuliko vito vya thamani mafunzo na ujuzi wa kweli ambavyo ni vyenye thamani kuliko fedha na dhahabu (soma Mithali 8:10 – 11). Hazina hii itadumu milele na kamwe haitaharibiwa na nondo au kutu. Hakuna yeyote atakayeweza kutuondolea sisi hazina hii. Mungu amechagua kwa ajili ya ufalme wake wale walio masikini humu duniani, lakini tajiri katika imani (Yakobo 2:5). Yesu akasema “Kwa kuwa hazina yakoilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako” (mstari 21)
HAKUNA MTU AWEZAYE KUWATUMIKIA MABWANA WAWILI:
Mathayo 6:24
Mwanafunzi inampasa kumfuata Bwana wake. Wakati Yesu aliposema, “Nifuate”, wanafunzi wake waliacha vyote na kumfuata (Mathayo 4:18 – 22: 9:9). Yesu aliwakumbusha juu ya hili alipokuwa akifundisha mlimani. “hamwezi kumtumikia Mungu na “mammon” (“mammon” ni neno lenye maana ya utajiri wa dunia). Mwanafunzi hawezi kumpenda Mungu na dunia, akiweka tumaini lake katika fedha au vitu vya dunia hii atakuwa anaonyesha kuwa hamwamini Mungu kuwa anamtunza yeye. Na kama anamwamini Mungu, Mungu atampatia kila kitu anachokihitaji na mengine zaidi.
MUNGU ANAJUA MAHITAJI YETU: Mathayo 6:25 – 34
Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kwa mifano rahisi ajabu jinsi Mungu anavyotunza viumbe vyake vyote. Hebu fikiri jinsi anavyowajali ndege,Yesu alisema; “Je, ninyi siyo bora zaidi kuliko hao?” (mstari 26). Jinsi anavyoyapamba maua ya kondeni, na “je hataweza kuwavika vyema zaidi, enyi wenye imani haba?” (mstari 30). Watu hutumia muda mwingi mno kufikiri juu ya chakula na mavazi Yesu akasema “Kwa maana hayo yote mataifa huyatafuta”; kwa sababu “Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote” (mstari 32)
Jinsi Yesu alivyokuwa mwalimu wa ajabu! Ujumbe wake ulikuwa rahisi na mwepesi kuuelewa “Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa” (mstari 33).
MUWE WATENDAJI WA NENO WALA MSIWE WASIKILIZAJI TU: Mathayo 7:24 – 27
Yesu alimalizia kwa mfano ambao uliwafundisha alichotaka wakifanye sasa ikiwa walisikia na kuelewa maneno yake. Baadhi yao waliomsikia wangekuwa na hekima. Wangesikia maneno yake na kuyatenda kama vile mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. “Mvua ikanyesha, mafurikoyakaja, pepo zikavuma zikaipiga nyumba ile; isianguke; kwaana misingi yake imewekwa juu ya mwamba (mstari 25).
Na wengine ni wale waliomsikia wakaenda zao na kutofanya chochote juu yake kama vile mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. “Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile; ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa (mstari27).
Maneno ya Bwana Yesu ni sawa na msingi imara. Inatupasa kuyasikiliza kwa uangalifu na kujenga maisha yetu juu yake. Ndipo matatizo yanapokuja, kama yafanyavyo mara kwa mara hatutaondolewa kutoka kwenye Kweli, tutaona kwamba Mungu bado yu pamoja nasi, akituongoza kupita nyakati za matatizo hayo. Na baada ya mvua na mafuriko na mawimbi, jua linawaka tena likitupatia tumaini jipya. Hivyo Neno la Mungu, linatusaidia katika matatizo yetu, linatuongoza salama katika maisha yetu yote hadi tupatapo upata ufalme.
FUNZO KWETU
Mfano wa mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba unatupatia fundisho muhimu sana inatupasa kulisikia Neno la Mungu na kulitenda. Neno lake laweza kutubadilisha kwani hakuna anayestahili kuuingia ufalme kama tulivyo. Ni lazima sote tubadili njia zetu, huo ndio uliokuwa ujumbe wa Yohana mbatizaji na ujumbe wa Yesu mwenyewe. Tusiwaangalie wengine kuona makosa yao, lakini tuangalie katika mwenendo wake Yesu na kujaribu kuwa kama yeye.
MASWALI
Majibu Mafupi
- Ni nini kinawafanya wanafunzi wa Mungu kufurahi?
- Je, Yesu alitunza sheria za Musa?
- Ni thawabu gani waliyoipata waandishi na mafarisayo?
- Ni nini ambacho machoni pa Mungu ni kibaya sawasawa na uuaji?
- Ni kwa namna gani Mungu anaonyesha upendo wake kwa watu waovu na wasio na
haki?
- Ni aina gani ya hazinaambayo Yesu alituambia tuweke ghalani?
- “Mammon” ni kitu gani?
- Kwa nini tusijali sana kuhusu vyakula na mavazi?
- Yesu alituambia nikiti gani “tukitafute kwanza?”
- Ni watu gani ambao ni sawa na mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake juu ya
mwamba?
Majibu ya Kina
- Yesu alimaanisha nini alipowaambia wanafunzi wake, “Ninyi ni nuru ya
ulimwengu?”
- Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kwamba inawapasa kuwa na mioyo yenye utiifu
- Mafarisayo walikuwa na mwenendo gani?
- Tuwatendee nini adui zetu?
13. Yesu alisema jiwekeeni hazina zenu mbinguni”
- Ni hazina gani hii?
- Ni watu wa ina gani ambao Mungu huwachagua kwa ajili ya ufalme wake?
14. Ni fundisho gani muhimu tunalojifunza kutokana na habari hii?