95. CHAKULA CHA MWISHO CHA USIKU
“Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu”
Shabaha
Ni kuonyesha jinsi alivyotumia usiko wake wa mwisho akiwa na wanafunzi wake. Ilikuwa ni siku kabla ya Pasaka na Yesu hali akijua kuwa siku yake imekaribia, kwa kuwa katika mwaka huu alikuwa auawe kama mwanakondoo wa Pasaka.Kumbuka jinsi Yohana Mbatizaji alivyomtambulisha Yesu miaka mitatu na nusu iliyokuwa imepita, aliposema, “Tazama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29). Na sasa muda wake ulikuwa umefika wa Yesu kutolewa kuwa dhabihu. Hivyo ilikuwa ni lazimaawaonyeshe jinsi watakavyo mkumbuka.
Mathayo24:14-30, Yohana 13:4-17; Mrko14:10-26; Luka22:1-20
YUDA ANAKUBALI KUMSALITI YESU
Wakuu wa makuhani walikuwa wamepatana kumwua Yesu. Tatizo peke lilikuwa-ni jinsi gani wafanye wasihesabike kama wauaji? Katika mawazo ya mioyo yao Mungu hakuwemo. Na bado Yesu hakuwa amefanya kosa lolote.Kwa kweli, ingawa walijitahidi sana ili wampate na kosa, watu walimfuata wakisikiliza maneno yake na kuona miujiza yake. Walitakiwa wamtafutie tuhuma ambayo hukumu yake ilikuwa ni ya kifo.Na kama wangepanga jambo hilo likawa kabla ya pasaka lingefanikiwa, kwa kuwa kila mtu ambaye angerudi nyumbani akitokea Yerusalemu baada ya sikukuu wangesafiri na ujumbe kuwa Yesu siyo Masihi.
Jambo la kuhuzunisha ni kwamba, alikuwa ni mmoja kati ya wale rafiki zake wa karibu kumi na mbili wapendwa wa Yesu ambaye aliwarahisishia makuhani mawazo yao. Alikuwa ni Yuda Iskariote, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wale kumi na mbili, ambaye alikubali kumsaliti Yesu. Alikwenda kwao na kuwaambia; “Ninini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu” (Mathayo 26:15). Wakamwambia kuwa watampatia vipande thelathini vya fedha. Na Yuda akakubali vipande thelathini vya fedha, ili kuangalia muda mwafaka, wakati ambako watu wengi hawatakuwa wamemzunguka Yesu, ili aweze kumsaliti Yesu kwao.
NENDANI NA MKAANDAE
Ilikuwa ni muda mfupi tu, wanafunzi wengine walipoanza kuhangaika ni wapi waweze kula Pasaka pamoja na Yesu. Kwa hiyo akawatuma Petro na Yohana kufanya maandalizi yaliyo ya lazima. Yesu akawaambia “Nendeni zenu mjini, atakutana nanyi mwanamume amechukua mtungi wa maji; mfuateni” (Marko 14:13-15). Walipaswa wamfuate hadi nyumbani na wamwambie mwenye nyumba, “Mwalimu, asema hivi, kiwapi chumba changu cha wageni, niile pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu?”
Nao wangeonyeshwa chumba kikubwa ghorofani, kilichokuwa kimeshaandaliwa tayari ambapo wao wangeweka chakula tu (Marko14:13-15).
WANAKULA CHAKULA CHA MWISHO PAMOJA
Usiku huo, wanafunzi wote kumi na mbili walikuwa pamoja na Yesu katika chumba cha juu ka ajili ya chakula cha usiku. Ilikuwa ni nafasi ya Bwana muhimu sana kuongea nao wote pamoja. Na muda mfupi ambao ungefuata angeondolewa kwao. Alijua kuwa wangekuwa na mshituko sana na hatimaye wangeogopa. Hata hivyo, walionekana kutokuelewa ingawa aliwaambia waziwazi kabisa (Luka9:22).
Ni tukio la siku chache zilipita lilwapatia matumaini ya kuweza kujisema mwenywe kuwa ni mfalme. Na walipokuwa wakifikilia kuhusu ufalme, kukatokea mabishano kati yao ni nani atakaye kuwa mkubwa. Yesu akawaahidi kuwa watakaa katika viti wakiyahukumu makabila kumi na mbili ya Israli (Luka 22:30), kwa kuwa walikuwa wameendelea kuwa waaminifu wakiwa pamoja naye kwa miaka yote mitatu nusu. Lakini hilo lingefanyika baadaye kuliko kama walivyokuwa wanatarajia. Na sasa ilikuwa wajifunze kuwa watumishi, kumtumikia yeye na kuhudumiana wao kwa wao. Hii ilikuwa ni njia nzuri sana ya kuwaandaa wao kuwa wafalme na kuwa waamuzi katika ufalme wa Mungu.
NIMEWAPATIA MFANO: Yohana13:4-15
Kiburi kilisababisha wabishane wenyewe kuhusu nani atakaye kuwa mkubwa. Walipashwa kujifunza kunyenyekea kama Yesu mwenyewe alivyokuwa mnyenyekevu. Akiyajua mawazo yao yalivyo. Yesu akainuka pale mezani, akavua nguo yake akajifunga taulo kama watumwa wafanyavyo. Na kisha akayamimina maji ndani ya kalai na akaanza kusafisha miguu ya wanafunzi wake na akawafuta miguu kwa taulo alilokuwa amejifunga kiunoni. Kitendo hiki kilikuwa kinafanywa na mtumwa kuosha miguu ya wageni wa bwana wake na hapa sasa alikuwa Bwana mwenyewe anaosha miguu ya wanafunzi wake. Watakuwa waliaibika. Yesu alijua kuwa hawakuelewa kwa nini alifanya hivyo. Hata hivyo, wangeweza kukumbuka baadaye na kisha wangejua kwa nini alifanya hivyo. Na ilipofika zau ya Petro aliona aibu na akasema, “Wewe hutanitawadha miguu kamwe”. Yesu akamwambia, “Kama niposikutawadha mimi huna shirika nami” (mstari 8). Kitendo kilikuwa ni cha thamani sana kwa Petro. Kama Bwana alikuwa amekusudia kumwosha, ndipo akamwambia asafishe mikono yake na kichwa chake pia, kwa maana alimpenda sana Bwana. Kisha ndipo Yesu akafafanua, “Basi ikiwa mimi niliye Bwana na mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi” (mstari 14). Na hivyo ndivyo walivyotakiwa kuonyesha upendo wao kwake, kwa kunyenyekea.
CHAKULA CHA BWANA: Mathayo 26:26-29
Pale penye meza ya chakula walipokuwa wanakula, Yesu alichukua mkate na kuuweka mikononi mwake na kumshukuru Mungu. Na kisha akaumega na akampatia kila mwanafunzi kipande cha mkate huo. “Twaeni, mle, huu ndiyo mwili wangu”, ndivyo Yesu alivyosema (mstari 26). Na kisha akachukua kikombe cha divai na akashukuru. Kilipitishwa kwa kila mwanafunzi, ili wanafunzi wote waweze kunywa divai. Yesu akasema, “Hii ni damu yangu” (mstari 28).
Ilikuwa ni sikukuu ya kukumbuka, lakini bado hawakufahamu kwamba baada ya muda mfupi angeutoa mwili wake kuwa dhabihu, na kwamb damu yake ingemwagika kwa ajili ya msamaha wa dhambi. Mkate na divai vinawakilisha mwili wake na damu yake.
Ni kwa ajili ya tukio hili hata siku hizi, ndugu wanaume na wanawake waKristo duniani kote wanakusanyika pamoja, siku ya kwanza ya juma, kula mkate na kunywa divai kwa ajili ya kumkumbuka Yesu. Mtume Paulo aliwaambia wafuasi wa Kristo katika Korintho kwamba “Maana, kila mwulapo mkate na kukinywea kikombe hiki; mwaitangaza mauti ya Bwana mpaka ajabu” (1 Wakorintho 11:26).
PENYE MLIMA WA MIZEITUNI: Mathayo 26:30-36
Wakati chakula cha usiku kilipoisha, waliimba wimbo na wakaondoka nje ya mji kwenda hadi Mlima wa Mizeituni. Yuda alikuwa amekisha ondoka kuwaambia wakuu wa makuhani mahali ambapo Yesu angeweza kupatikana.
Moyo wa Bwana ulikuwa mzito sana wakati alipopita bonde la Kidroni kwenda Mlima wa Mizeituni. Alifahamu kuwa itakuwa ni wakati wa usiku wa manane wakati rafiki zake, waliompenda Yesu sana, wangekimbia kwa ajili ya maisha yao na angeachwa peke yake. Kwa kutambua jinsi huzuni ya bwana wake ilivyokuwa, Petro aligoma: “Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi nitayari kwenda gerezani au hata kifoni” (Luka 22:33).
Ndipo Yesu akamjibu, “Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hunijui” (mstari 34). Petro alishituka kwamba Bwana aliweza kuyajua hata mawazo yaliyokuwa moyoni mwake. Petro akasema, “Ijaponipasa kufa nawe, sitakukana kamwe na wanafunzi wote wekasema vivyo hivyo” (mstari 35). Ilikuwa ni hapa, katika bustani ya Gethsemane.
FUNDISHO KWETU
Wakati wa chakula cha mwisho cha usiku Yesu akasema, “Amri mpya nawapa, mpendane, kama vile nilivyowapenda ninyi” (Yohana 13:34). Upendo huu ambao Yesu alituonyesha sisi ulikuwa ni mkubwa sana kwa kuutoa uhai wake kuwa dhabihu kwa ajili ya wote wanao mwamini yeye.
Tunatakiwa tupendane sisi kwa sisi kwa namna moja. Kama vile Yesu alivyoosha miguu ya wanafunzi wake, kwa hiyo ni lazima tujifunze kuhudumiana sisi kwa sisi.Hii ina maana kwamba wakati wote tuwafikirie wengine na kuwasaidia na wakati mwingine kuwapatia raha zetu ili kuwapatia furaha wrngine.Kama tutawathamin rafiki zetu katika Kweli,siku zote tutafurahi kuwa dhabihu kwa ajili yao.Mungu hatuambii sisi tufe kama vile Yesu alivyokufa,bali tuonyeshe vitendo vyetu kuwa tuwanafunzi wake.
MASWALI
Maswali Mafupi
1. Ni nani aliyekubali kumsaliti Yesu?
2. N'i kiasi gani wakuu wa makuhani walikubali kumlipa kiasi gani?
3. Wanafunzi waliwezaje kupata nyumba ambayo Yesu alitaka waandae chakula cha
mwisho cha usiku?
4. Wanafunzi walibisha kuhusu nini?
5. Yesu alifanyaniniili kuwathibitishia ili kwamba waweze kuhudumiana wao kwa wao?
6. Yesu alikula mkate pamoja na wanafunzi wake.Mkate unawakilisha nini?
7. Ni kwa nini wafuasi wa Yesu siku hizi wanakusanyika kula mkate na kinywa divai?
8. Baada ya chakula cha usiku Yesu na wanafunzi wake walikwenda wapi?
9. Ni mwanafunzi yupi aliyekuwa tayari kufingwa au kufa na bwana wake?
10. Yuda alimkuta Yesu wapi?
11. Ni mri ipi mpya ambayo Yesu aliwafundisha wanafunzi wake?
Majibu ya Kina
12. Usiku kabla ya Yesu kufa, alikuta na na wanafunzi wake katika chumba cha juu?
a. Wanafunzi walianza kubishana kuhusu nini?
b. Ni thawabu gani Yesu aliyowaahidi?
c. Eleza ni jinsi gani Yesu alivyowa fundisha kunyenyekea?
13. Katika chumbacha juu, Yesu alikuwa na chakula maalumu cha jioni kilichoitwa
“Chakula cha Bwana cha usiku”,
a. Yesu alifanya nini?
b. Wanafunzi hawakuelewa, lakini, Yesu alikuwa anamaanisha nini?
c. Je, ndugu wanaume na wanawake katika Kristo wanafanya nini siku hizi kwa ajili
ya kukumbuka kifo chake?