CSSA 1-4-24 - THE RESURRECTION

Swahili

99. UFUFUO

"Kwanini mnamtafuta aliye hai katika wafu. Hayupo hapa, lakini amefufuka”

 

Shabaha

Kuonyesha jinsi Yesu alivyofufuka siku ya tatu na akajidhihirisha mwenyewe ka wanafunzi waake wengi. Wayahudi na watu wa mataifa wakaungana kumwua Yesu, mikono ya waovu ikmchukua na kumpigilia misumari juu ya mti hadi akafa, lakini mikono mizuri ikamzika. Baba wa mbinguni akayatazama mambo yote haya. Aalimpenda Mwanaye kwa sababu aliyatenda yote ambayo alitakiwa kuyafanya. Na sasa kaburi lisingeweza kumshika na ikawa siku ya tatu akafufuka. Aliwaotokea rafiki zake wengi na mitume, ambao hapo mwanzo walishinda huzuni kutokaa ne kifo, hata hawwakuweza kuamini kwamba ndiye.

 

Luka 24:1-48 Soma Mathayo28:1-15 Marko 16:1-14 Yohana 20:1-29

 

KABURI LIKATIWA MUHURI NA KULINDWA

Viongozi wa Wayahudi walipata walichokuwa wanakitaka. Na sasa Yesu alikuwa amekufa na kuzikwa, lakini hawakuwa na raha. Kwa kadiri walivyokuwa wakiyafikiria matukio ya kushagaza yaliyokuwa yametokea siku iliyokuwa imepita-giza zito lililokuwa limeifunika nchi yote kwa masaa matatu, tetemeko la ardhi na kuchanika kwa pazia la hekalu-walikuwa na hofu kiasi. Miujiza ya Yesu na maonyo yake yalikuwa bado ni ujumbe mzito katika fahamu zao. Lakini lililokuwa likiwasumbua sana yalikuwa ni maneno ya Yesu, ya kwamba siku ya tatu atafufuka (Marko 8:31-32; Mathayo 27:63). Walifikiria kuwa inawezekana wanafunzi wake wangeweza kwenda kuiba mwili wake na kisha kueneza habari kuwa amefufuka. Kwa hiyo wakamwomba Pilato aweke maaskari wa kulinda kaburi lake kwa sikutatu. Pilato akawaambia, “Nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyo” (mstari 65). “Kwa hiyo wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari kulilinda” (mstari 66). Ingawaje maadui wa Yesu alikumbuka maneno yake kuwa atafufuka siku ya tatu, wanafunzi wake walisahau. Walikuwa na majonzi mzito ya kusulubiwa kwa mpendwa wao. Walikuwa wanaamini alikuwa aanze kuweka ufalme wa Mungu na sasa matumaini yao yote yalikuwa yamepotea. Walikuwa na huzuni nyingi na kukata tamaa. Wakati Yesu alipokuwa nao, onyo lake kuhusu kifo ilionekana kuwa halikuwa halisi. Aliwaimarisha na kuwaongoza na kuwafariji. Na sasa alikuwa ameondoka, na walibakia dhaifu na wasio na matumaini, bila kufahamu la kufanya baadaye. Walikuwa hawafahamu kuwa manabii waliandika yaliyokuwa yanamhusu Masihi, ya kwamba atateswa kwanza na kisha kufufuka kwa utukufu.

 

WANAWAKE WANAKWENDA KABURINI

Kikundi kidogo cha wanawake, waliomfuata kutoka Galilaya hadi Yerusalemu waliokuwa wanashughulikia mahitaji yake njiani, walimfuata hadi Golgota na walisimama “kwa mbali kushuhudia kusulibiwa kwake” (Mathyo 27:55). Wanawake wawili kati yao, kwa ajili ya imani na upendo wao ndiyo uliowafanya wamfuate Yesu, walikuwa wakitazama wakati Yusufu wa Arimataya na Nikodemu walipouweka mwili wa Yesu kwa uangalifu kaburini. Nao “wakaliona kaburi, na jinsi mwili wake ulivyowekwa” (Luka 23:55). Walikuwa wamekusudia kufanya jambo la mwisho ili kuonyesha upendo wao. Siku iliyokuwa inafuata ilikuwa ni sikukuu, sabato, lakini wangekwenda kununua manukato ya thamani na marhamu baada ya sikukuu ili kuupaka mwili wa Yesu (Marko 16:1) Mapema asubuhi siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalena akiwa pamoja na wanawake wengine walikwenda kuliona kaburi.

 

JIWE LIKAONDOLEWA

Usiku huo, siku ya mwisho ya sabato, tetemeko kubwa lilitikisa mji. Mungu alimtuma malaika wake kuliondoa jiwe zito ambalo lilikuwa muhuri wa mlango wa kaburi ambalo Yesu alikuwa amezikwa kwa siku tatu mchana na usiku. Akakaa juu ya jiwe na walinzi waliokuwa wametumwa kulinda kaburi walitetemeka na kuogopa sana kwa ajili ya mwonekano wake. “Na sura yake ilikuwa kama umeme, mavazi yake meupe kama theruji” (Mathayo 28:3).

 

Wanawake walipokwenda kwenye kaburi walikuta jiwe limevingirishwa na kaburi lilikuwa wazi.Na ghafla waliona malaika waliokuwa wamevaa mavazi yanayometameta sana wakiwa wamesimama pale nao wakaogopa sana. Malaika wakasema: “Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu? Hayupo hapa, amefufuka”. Kisha wale wanawake wakakumbuka maneno ya Yesu kwamba “atafufuka siku ya tatu”, na wakaamini (Luka 24:5-8).

 

Kwa furaha kubwa wakaharakisha kwenda kuwaambia wanafunzi wake kwamba Bwana amefufuka kutoka wafu. Ingawa walikuwawameogopa kutokana mambo waliyokuwa wmeyaona, mioyo yao ilijaa furaha kwa ajili ya ujumbe huu waliopewa na wakakimbia kwenda kuwajulisha wanafunzi.

 

TAARIFA YA UONGO: Mathayo 28:11-15

Wakati wanawake walipokwenda mbio na habari ya furaha. Walinzi walitetemeka na kukimbia. Baadhi yao walikwenda moja kwa moja kwa wakuu wa makuhani na habari ya kutisha waliyoiona bustani. Wakiamini lile lililotokea ikiwa litajulikana, wakuu wa makuhani wakawaita wazee kwa pmoja ili kwa haraka waamue wafanye nini. Walinzi walikuwa wanatetemeka kabisa. Njia moja ya peke ya kuweza kuyabadilisha habari waliyoona ilikuwa ni kuwahonga kwa kuwapa kiasi kibwa cha pesa. Kwa hiyo wakuu wa makuhani na wazee waliwashauri walinzi waseme: “Walinzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala” (mstari 13). Kwa kweli, ikiwa mlinzi angekutwa amesinzia wakati wa zamu alipaswa kuuawa, lakini hawa Wayahudi waovu waliweza kudanganya hili nalo pia, ili habari ya kweli isimfikie gavana.

 

PETRO NA YOHANA WANAONA KABURI TUPU

Wakati wanawake wenye furaha walipofika na kuwaambia mitume habari ya kushangaza ya kukuta kaburi tupu na kuwaona malaika na kufufuka kwa Bwana Yesu, ambazo zilionekana kutokuaminika. “Maneno yao yakaonekana kama vile upuuzi mtupu kwao wala hawakuwasdiki” (Luka 24:11). Lakini Petro na Yohana wakaondoka mbio kwenda kuliona kaburi. Yohana alikuwa wa kwanza kufika pale, akainama na kuchungulia ndani ndani ya kaburi, akaiona vitambaa vya sanda vimelala pale.Kisha Petro akikimbia nyuma yake akafika na kuingia ndani ya kaburi. Pale aliviona vitambaa vya sanda na leso iliyokuwa inatumika kufinika kichwa chake, ilikuwa imezongwa mahali pa peke yake. Hatimaye Yohana akaingia ndani ya kaburi “akaona, nakuamini” (Yohana 20:3-8). Ni kweli Bwana hakuwepo pale, akiwemo Yohana na mitume wengine hawakuamini kwamba Yesu amefufuka na kuwa ataishi milele.

 

YESU ANAMTOKEA MARIAMU MAGDALENA: Yohana 20:11-18

Maskini Mariamu hakuwa na uhakika aamini nini. Alikwenda tena kaburini na kuona kwamba jiwe lilikuwa limeondolewa. Akasimama pale akilia, hakujua lililompata Bwana. Na akiwa anaendelea kulia, akainama na kuchungulia ndani ya kaburi. Malaika wawili wakiwa wamevaa nguo nyeupe walikuwa wamekaa pale, “mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wa Yesu.” Nao wakamwuliza, “mwanamke, unalilia nini?” Akawaambia, “Kwa sababu wamemwondoa Bwaa wangu, na wala mimi sijui walikomweka” (mstari 13). Akageuka nyuma akamwona mwanamme amesimama nyuma yake. Akafikiria kuwa ni mtunza bustani naye pia akamwuliza kwanini analia, akasema, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, niambie umemweka wapi, nami nitamchukua (mstari 15). Hakutambua, kutokana na machozi yake, kuwa aliyekuwa anaongea naye alikuwa Bwana mwenyewe aliyefufuka. Lakini Yesu akaongea neno moja, na mara moja Mariamu akamtambua. Yesu alisema, “Mariamu”. Alikuwa ameshaizoea sauti hii. Raboni, Mariamu kwa mshangao (maana yake “mwalimu wangu”) (mstari 16). Mariamu, sasa akawa na uhakika na anapaswa kufanya kama alivyomwambia kwenda na kuwaambia “ndugu wa Bwana” kwamba amefufuka.

 

MASHAHIDI WENGI WA KUFUFUKA KWAKE

Siku hiyo hiyo, siku ya kwanza ya juma, Yesu alijidhihirisha kwa wanafunzi walipokuwa wanakwenda Emau (Luka 24:13-35). Baadaye, wakati wa jioni, Yesu akaja na kuwakuta wanafunzi wakealiowachagua kuwa mitume na akawaambia, “amani na iwe kwenu”. Alipoona kuwa wanaogopa aliwaonyesha alama za mikono yake na alama ya ubavuni, kuwa hakikishia kuwa ni yeye mwenyewe Kristo aliyefufuka. Akasema,“Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe: nishikenishikeni, mwone”(Luka 24:39). Wakawa wenye kujaa furaha kuu, hata kutokuweza sana, kuamini kile macho yalichokiona. Na kisha Yesu akawauliza kama wana samaki na mkate na akala mbele yao. “Basi, wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana” (Yohana 20:19-20).

 

Tomaso hakuwepo wakati huo. Wenzakewalipomwambia hakuwaamini, Akasema, “Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari na kutia kidole changu katika mahali pa msumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo” (Yohana 20:25). Siku nane baadaye, Yesu kawatokea wote tena naye Tomaso alikuwepo. Yesu akamwonyesha makovu yake naye Tomaso akaamini mara moja. Yesu akamwambia, “Wewe kwa kuwa umeniona, umesadiki; waheri wale wasioniona wakasadiki” (mstri 29). Na mwisho akawatokea wanafunzi mia tano waliokuwa wamekusanyika pamoja (1Wakorintho 15:6). Walikuwepo mashahidi wengi walio ona na kuamini, na kuwa uongo ulikuwa ukienezwa na viongozi wa Wayahudi haukuweza kuzuia habari nzuri ya ajabu ya kufufuka kwa Kristo kweli kweli. Majuma machache baadaye, siku ya Pentekoste, Petro alitangaza ujumbe huo wa furaha kwa watu maelfu waliokuwakuwa wamekusanyika pale Yerusalemu kwenye sikukuu. Alisema, “Yesu huyu, Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake” na watu zaidi ya elfu tatu wakaamini siku ile (Matendo ya Mitume 2:32,41)

 

FUNDISHO KWETU

Ni kwanini ufufuo wa Yesu ni muhimu sana? Mtume Pulo anawaambia Wakorintho: “Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure” (1 Wakorintho 15:17). Mambo yote tunayoyaamini kuhusu kuja kwa ufalme wa Mungu hapa duniani, tumaini letu lote kuhusu mambo yajayo, yangekuwa hayana maana yoyote kama Kristo hakufufuka katika wafu. Na kama Kristo angekuwa hakufufuka basi sisi tungekuwa masikini kuliko watu wote. Na siyo hivyo tu bali hata wale walio mwamini Kristo zamani ambao sasa wamelala katika makaburi, wataendelea kuwa makaburini tu. Lakini, Mungu na ashukuriwe, tunalo jambo zuri sana tunalolitazamia kwa kuwa: “Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala” (1 Wakorintho 15:20). Yeye ni “limbuko”, wa kwanza kufufuka na kupewa uzima wa milele. Atakaporudi, wale waliolala “katika Kristo” pia watafufuka (1 Wathesalonike 4:16). Pamoja na sisi tutakaokuwa hai na tunaomwamini, tutabadilishwa na kupewa uzima wa milele pia. Kama wote tutakuwa tumeendelea kuwa waaminifu mpaka atakeporudi.

 

Na kwa kuwa tunaye Mwokozi aliye hai, ambaye hafi tena, hebu na tuwke tumaini letu kwake na kutegemea kuwa naye milele kama wanafunzi wake vilevile walivyotegemea.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Basi, tungalie kile kilichotokea katika barabara inayokwenda Emau siku ya wanza ya juma. Wanafunzi wawili walikuwa wakisafiri wakishuka kutoka Yerusalemu kwenda kijiji cha Emau, yapata kama umbali wa kilometa kumi na moja. Walikuwa na huzuni sana, watu hawa wawili, wakiwa wanatembea waliendelea kutafakari matukio yaliyotokea siku chache ambazo zilikuwa zimepita. Mtu ambaye ni mgeni akajiunga nao, hatimaye, kumbe hakuwa mgeni mgeni, bali Yesu mwenyewe, kwa kweli walikuwa na mawazo yao yalikuwa yahuzuni nyingi kiasi kwamba hawakuweza kumtambua kabisa. Huyu alikuwa ni mtu wa mwisho kukutana nao kwa jinsi walivyofikiria nao walikuwa katika mazungumzo mazito. Mara moja “yule mgeni” akawauliza, ni mambo gani haya mnayozungumza kwa makini sana na yanayosababisha ninyi mhuzunike sana. Wanafunzi wale wawili wakashangaa tena kwa hasira. Walimwona kama ni yeye peke yake katika Yerusalemu ambaye hakujua mambo yaliyotokea siku tatu zilizokuwa zimepita. Akawauliza “Mambo gani?". Wakasema, “Mambo ya Yesu Kristo wa Nazareti”, wakaendelea kuelezea kuhusu kifo chake cha ukatili. “Lakini sisi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakaye wakomboa Israeli: na zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu yalipotendeka mambo hayo”. Wakamweleza kuwa wanawake wamekuta kaburi tupu na wakasema kuwa wamewaona malaika, ambao wamewaambia kuwa Yesu amefufuka. Wakamwelezea pia kuhusu wanafunzi waliokwenda kaburini na hawakukuta mwili wake, na wala hawakumwona popote. Ikawa “yule mgeni” alipokwisha kusikiliza habari hiyo ya huzuni, akawaeleza wote wawili. “Enyi msiofahamu na wenye mioyo mizito ya kuamini mambo yote waliyoyasema manabii: Je, haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?” Maneno yake yatakuwa yaliwashangaza kwa furaha, lakini akaendelea kuwaambia maandiko, kuanzia Musa na akaendelea mpaka manabii wote, “mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe”. Ni jinsi gani watakuwa walisikiliza kwa makini, na wakaanza kuyaelewa yale ambayo Mungu aliyaandika katika Neno lake. Na hatimaye wakafika Emau. Ilionekana kana kwamba mwenzao alitaka kuendelea mbele, lakini wakamshawishi akae nao. Akaingia pamoja nao wakajumuika wote kula chakula. Kulikuwa na mkate mezani, akatwaa mkate akashukuru akaumega na akawapatia wale wanafunzi wawili. Ghafla wakamtambua. Alikuwa ni Yesu mwenyewe. Hakuna mtu mwingine anayetwaa mkate na kushukuru na akaumega jinsi ile. Alikuwa yu hai, kama wanawake walivyosema. Na bila neno lingine Yesu akatoweka mbele ya macho ya macho yao. Na sasa wakatambua ni kwa nini waliguswa sana mioyoni mwao wakati alipokuwa akiwaambia maandiko, walipokuwa njiani wakitembea. Walikuwa na furaha sana wakaharakisha kurudi Yerusalemu ili kuwaeleza wale wanafunzi kumi na moja.

 

MASWALI (Miaka 9-12)

Majibu Mfupi

1. Ni jambo gani lililosababisha Wayahudi wamwombe Pilato maaskari wa kulinda kaburi

2. Baadhi ya wanawake waliona sehemu Yesu aliyozikwa. Je, walikuwawamekusudia

    wafanye nini baadaye

3. Baada ya sabato Mungu aliwatuma malaika wafanye nini

4. Malaikawaliwambia nini wanawake waliokwenda kaburini

5. Wakuu wa makuhani waliwashauri walinzi waseme nini

6. Ni wanafunzi gani wawili waliekwe nda kaburini mbio na waliona nini

7. Mariamu Magdalena hakumtambua Yesu.Alifikiri kuwa ni nani

8. Yesu alisema nini hata Mariamu akaweza akamtambua

9. Yesualiwaonyesha nini mitume wake wateule alipowatokea

10. Je! Yesu alikula nini mbele yao

11. Ni mwanafunzi gani hakuamini

12. Ni nini kilisababisha hatimaye aamini

13. Yesu alikuwa wa kwanza kupewa uzima wa milele. Ni watu gani wengine

       watakaopewa

 

Majibu ya Kina

14. Wakuu wa makuhani walitaka  walinzi walinde kaburi la Yesu.

      a. Ni kwa nini walimwomba Pilato palindwe

      b. Kulitokea nini pale bustani siku ya mwisho ya sabato

      c. Walinzi walifanya nini

      d. Wakuu wa makuhani waliamua nini

15   a. Eleza palitokea nini wanawake walipokwenda kaburini

      b. ElezaPetronaYohana walifanya nini waliposikia habari

 

Majibu ya Nyongeza

 

 16. Eleza nini kilitokea katika barabara iendayo Emau.

 

 

Swahili Title
099 UFUFUO
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type