CSSA 1-5-02 - THE DAY OF PENTECOST

Swahili

102. SIKU YA PENTEKOSTE

“Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu”

 

Shabaha

Kuonyesha jinsi mitume walivyopokea nguvu za Roho Mtakatifu na wakatumia nguvu hii waliyopewa kuifundisha injili kwa wageni waliofika Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu. Ilikuwa ni wakati wa Pasaka wakati Yesu aliposulubiwa. Siku hamsini baadaye sikukuu nyingine ilisherekewa katika Yerusalemu. Sikukuu hii iliitwa Pentekoste (maana yake siku 50 kwa Kigriki). Wayahudi wageni kutoka duniani kote walifika kuishika sikukuuu hii, mitume walikuwepo pale pia, kwa maana Bwana alikuwa amewaambia siku chache kabla kuwa wasubiri katika Yerusalemu.

 

Matendo ya Mitume 2

 

KUMWAGWA KWA ROHO MTAKATIFU (mstari 1-4)

Mitume wote walikuwa pamoja siku ya sikukuu. Ghafla kukawa na sauti kama uvumi wa upepo ambao uliijaza nyumba yote waliyokuwemo wakiwa wamekaa katika chumba walichokuwepo, kukatokea ndimi kama za moto, ambazo ikimkalia kila mmoja. Hii ilikuwa ni ishara kuwa Mungu alikuwa amewapatia mitume nguvu ya Roho Mtakatifu. Kisha mitume wakaanza kunena katika lugha zingine au kunena kwa lugha.

 

ROHO MTAKATIFU NI NINI?

Neno “Mtakatifu” maana yake “weka kando” au “tenga” na “Roho” ni nguvu za Mungu. Wakati Mungu alipowapatia mitume Roho Mtakatifu, Mungu alikuwa anawapa nguvu ambayo “iliwaweka kando” na hasa kuwawezesha kuhubiri injili. Wakati Mitume kwa mara ya kwanza walipopokea Roho Mtakatifu walijikuta wakinena kwa lugha ambazo hawakuwa wamejifunza kamwe. Kwa hiyo waliweza kuhubiri watu wa mataifa tofauti katika lugha za watu hao wanaohubiriwa, pia waliweza kuwaponya wagonjwa, walemavu, vipofu na hata kufufua walikuwa wamekufa. Miujiza hii ilikuwa ni ishara kwa watu kwamba Mungu alikuwa pamoja na mitume.

 

MITUME WANENA KWA LUGHA MPYA (mstari 6-13)

Kwa sababu ya sikukuu Wayahudi wengi walitoka sehemu mbalimbali za dunia wakaja Yerusalemu. Na habari ya haya yaliyotokea yalienea kwa haraka na watu wengi walikusanyika eneo hili walipokuwapo mitume. Kila mmoja Walishangazwa kabisa,kila mmoja aliweza kuwasikia mitume wakisema kwa lugha na kila mmoja alielewa yale yaliyosemwa na mitume. Wakasemezana kila mmoja, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu kwa lugha yetu tuliyozaliwa nayo? Ingawaje watu wote walikuwa Wayahudi wengi wao katika kuishi nchi za kigeni walijifunza lugha za nchi hizo. Na orodha ya nchi ambazo watu waliokuja inapatikana katika ya mistari 9 -11. Angalia kama unaweza kuziona katika ramani. Kwa hakika kunenea kwa lugha ulikuwa ni muujiza uliotokea. Baadhi katika kundi waliuliza, “Hii ina maana gani?” Wengine walidhihaki wakasema hawa mitume watakuwa wamelewa! Lakini hawakuwa wamelewa: ulikuwa ni muujiza.

 

PETRO ANAFAFANUA( mstari 14-41)

Ndipo Petro akasimama akaanza kuwaambia watu wote.Akawaambia kuanzia kutoka Manabii ya kwamba Yesu wa Nazareti ambaye walimsulubisha alikuwa kweli ni Masihi (Maana yake Kristo, Mfalme). Hawakuwa na haja ya kufikiri mambo mengi ya miujiza aliyoifanya mbele ya macho yao, miujiza hiyo ilithibitisha kwamba Mungu alikuwa pamoja naye,na kwa ukaidi walikataa kumwamini yeye. Na badala yake wakawaruhusu watu waovu ambao walimwua kwa kifo cha kikatili wakitarajia kuwa wamemshinda. Petro sasa akawaambia kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Kitendo hiki kilikuwaa bado hakijatokea kamwe. Hata Mfalme mkuu Daudi, ambaye walimheshimu sana alikufa akazikwa na kaburi lake lipo pale Yerusalemu kuthibitisha hili. Daudi hakika alikufa akalala katika mavumbi ya nchi, Daudi hakika hakupaa mbinguni. Lakini mtu huyu Yesu, Mungu alimfufua kutoka kwa wafu kamwe hatakufa tena. Hakika kwa muujiza huu ambao Mitume wenyewe walidhibitisha (kwa maana walimwona Yesu akiwa hai na kuongea naye), hili liliwafanya waamini kwamba ni Masihi hakika. Petro alizungumza kwa muda mrefu na kuwathibitishia kwamba yote aliyoyasema ni ya ukweli, na wengi waliposikia habari hizi “walichomwa mioyoni mwao” na kumwuliza Petro na Mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? (mstari 37) Wakaaibika walipojitambua jinsi walivyokuwa wakosaji. Petro akawaambia “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, na ninyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu” (mstari 38)

 

Neno “kutubu” maana yake “kubadilisha mwenendo wako”. Siyo tu kujutia kwa yale tuliyoyafanya bali tubadilishe mwenendo na kuyafanya yanayompendeza Mungu. Watu walifurahishwa na maneno ya Petro na siku hiyo idadi ya watu wapatao kama elfu tatu kati yao walibatizwa. Mungu akawabariki mitume kwa nguvu ya “Roho Mtakatifu” ili kuthibitisha kuwa alikuwa pamoja nao na hii ilisababisha wengi walisikie neno la ujumbe wao. Ni kwa jinsi gani mwanzo wa kuhubiri injili ulivyokuwa mzuri sana.

 

FUNDISHO KWETU

Unajifunza Injili kwa kadiri unavyosoma Biblia katika shule ya masomo ya Jumapili. Kwa kadiri unavyojifunza utaona kuwa sisi sote tunahitaji kutubu na kumtii Mungu. Tunapokuwa tumeamini hili ni lazima tubatizwe na kuendelea katika njia za Mungu mpaka Bwana Yesu Kristo atakaporudi.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Siku hizi nguvu za Roho Mtakatifu kwa ajili ya kunena kwa lugha na kutenda miujiza haipo kwa watu. Mungu aliwapatia nguvu hii mitume na wafuasi wao wa kwanza ili kuweza kutenda ishara na miujiza kwa ajili ya kuwa thibitishia kwamba Mungu amewatuma. Ni Mitume pekee yao walioweza kuwapatia nguvu hii wanafunzi waliokuwa wanastahili, kwa hiyo wakati Mitume walipokufa uwezo huu wa kuwawekea mikono ili wapokee nguvu hii ulikoma. Siku hizi badala yake tuna Biblia, ambayo ni Neno la Mungu. Biblia iliandikwa na watu waliongozwa na Roho Mtakatifu (angalia Mwelekezaji wa maswali 6 na 7). Mungu anapenda tusome na kujifunza Neno lake ili tuweze kuelewa Injili na kuokolewa. Bwana Yesu Kristo aliwaambia wafuasi wake “enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili aaminiye na kubatizwa ataokoka” (Mark 16:16).

 

MASWALI

Majibu Mafupi

1.    Sikukuu ipi ambayo ilisherehekewa siku ya 50 baada ya sikukuu ya Pasaka?

2.    Ni jinsi gani mitume walivyopokea Roho Mtakatifu?

3.    Mitume walitakiwa kufanya nini baada ya kupokea Roho Mtakatifu kwa mara ya kwanza?

4.    Ni kwa nini Mitume walipewa Roho Mtakatifu?

5.    Je watu wengine walifikiria ni nini kilichowapata mitume?

6.    Je Yesu alifanya nini kilicho kuwakinadhihirisha kuwa ni Masihi?

7.    Walimsulubisha Yesu, lakini ni jambo gani la ajabu ambalo Mungu alilifanya?

8.    Mfalme Daudi yuko wapi sasa?

9.    Wakati Petro alipokwisha sema na watu, waliwauliza nini mitume?

10.  Je Petro aliwaambia watu wafanye nini?

11.  Je ni watu wangapi waliobatizwa siku ya Pentekoste?

 

Majibu ya Kina

12.  a) Ni mujiza gani uliotokea kwa Mitume kumi na mbili katika Yerusalemu siku ya Pentekoste?

      b) Kwanini wageni waliokuwa Yerusalemu kwenye sikuku ya Pentekoste walishangaa wakati

    Mitume waliponena nao?

13.  Kwa nini Mungu aliwapa Mitume nguvu ya Roho Mtakatifu?

14.  Watu wabaya walimsulubisha Yesu.

       a) Ni jambo gani la mwujiza ambalo Mungu alifanya?

       b) Watu walifikiriaje waliposikia habari ya mambo hayo?

       c) “Kutubu” maana yake ni nini?

 

Majibu ya Nyongeza

15.  Roho Mtakatifu ni nini?

16.  Kwa nini nguvu za Roho Mtakatifu hazipo siku hizi?

17.  Je Mungu ametupa nini siku hizi badala ya kipawa cha Roho Mtakatifu?

 

Swahili Title
102 SIKU YA PENTEKOSTE
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type