106. FILIPO NA TOWASHI WA KUSHI
“Wakatelemka wote wawili majini, Filipo na Yule Towashi, naye akambatiza”
Shabaha
Kuonyesha jinsi Mungu alivyomwongoza Filipo kumfundisha towashi wa Ethiopia njia ya wokovu kupitia Yesu Kristo.
TATIZO KWA WAUMINI
Wayahudi waliompiga mawe Stefano hadi kufa walisababisha matatizo katika eklesia ndani ya Yerusalemu. Wengi wa wafuasi wa Bwana Yesu Kristo waliteswa kwa sababu za imani zao. Waliondolewa katika makazi yao na kutupwa gerezani. Hii iliwafanya wengi kukimbia kwa hofu kutoka Yerusalemu kwenda sehemu za Yudea na Samaria. Na walipokwenda waliihubiri Injiri (Matendo ya Mitume.8:1; 11;19)
FILIPO ANAHUBIRI INJILI
Miongoni mwa wanafunzi waliotoka Yerusalemu alikuwa ni Filipo. Huyu alikuwa ni kati ya wanaume saba ambao walichaguliwa hasa kuwatumikia eklesia.Kama vile alivyokuwa Stefano hakuwa mwoga kuhubiri Injiri. Mungu alimpa Roho Mtakatifu kumfundusha Neno lake kwa ufasaha na kufanya miujiza kati ya watu.
Filipo alikwenda katika mji wa Samaria ambapo wengi waliamini mafundisho yake na kubatizwa “na kulikuwa na fuaha nyingi katika mji ule” (mstari 5-12). Eklesia mpya ilianzishwa wakati mitume waliokuwa Yerusalemu waliposikia habari hizi Petro na Yohana walikwenda Samaria walipoona kazi ya Filipo aliyoifanya na jinsi Mungu alivyo wabariki sana, waliwaita wanafunzi wote wakawapatia nguvu ya Roho Mtakatifu kwa kuwawekea mikono yao. Ni mitume kumi na mbili tu waliokuwa na uwezo wa kuwapatia Roho Mtakatifu kwa njia ya kuwawekea mikono hiyo. Filipo alifanya miujiza lakini hakuwa na uweza wa kuwapatia wengine kipawa cha Roho Mtakatifu (mstari 14-17). Petro na Yohana wakarudi Yerusalemu wakiwa njiani wakahubiri katika vijiji vingi vya Samaria (mstari 25).
MALAIKA ANAONGEA NA FILIPO (mstari 26-26)
Mara tu baada ya Malaika wa Bwana kumtokea Filipo, alimwambia “Ondoka ukaende upande wa kusini njia ile itelemkayo toka Yerusalemu kwenda Gaza; ambako ni jangwa” naye Filipo alitii haraka sana na haukuwa muda mrefu alielewa ni kwanini Mungu alimtuma huko. Mtu maarufu kutoka Ethiopia alisafiri njiani. Huyu alikuwa ni towashi aliyekuwa afisa na mkuu wa hazina ya Kandake Malkia wa Kushi. Ingawa mwethiopia huyu alimwamini BWANA Mungu wa Israeli na alikuwa Yerusalemu kuabudu na alipokuwa akirejea nyumbani akiwa ameketi garini, alikuwa akisoma chuo cha nabii Isaya. Mungu akamwambia Filipo “Sogea karibu na gari hili ukashikamane nalo”.
FILIPO ANAMFUNDISHA HABARI ZA YESU (mstari 30-35)
Filipo akaenda mbio kwa Yule towashi akamwuliza kama aliyaelewa hayo aliyokuwa akiyasoma. Na Yule Mwethiopia akamwambia Filipo apande ndani na kuketi pamoja nae. Wakiwa safarini alimskiliza kwa makini Filipo alipokuwa akimweleza kwa ufasaha. Jinsi alivyofurahi kufundishwa ukweli wa Neno la Mungu. Angalia Isaya 53:7-8 utaona maandiko ambayo Mwethiopia alikuwa akisoma. “Aliongozwa kwenda machinjioni kama Kongoo, Na kama mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, “vivyo hivyo yeye hafungui kinywa chake” (Mstari 7). Wakati Mwethiopia alipoyasoma maneno haya akamwambia Filipo “Nakuomba, Nabii huyu anasema maneno haya kwa habari ya nani ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine?” Filipo akafunua kinywa chake, naye akianza kwa andiko hilo hilo, akamhubiria habari njema za Yesu ambaye ni Masihi aliyeahidiwa. Isaya alikuwa akizungumza habari za Yesu.Ingawa Yesu hakufanya yale yanayostahili kufa. Yesu alikufa kwa kuuawa na watu waovu lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu na sasa yuko Mbinguni yu hai milele na milele. Mungu atamtuma tena kuja ulimwenguni kuwafufua wafu na kuwapatia uzima wa milele walioamini na kutii Neno la uzima.
TOWASHI MWETHIOPIA ANABATIZWA (mstari 36-40)
Ndipo Mwethiopia sasa akaelewa waziwazi yale aliyokuwa akiyasoma. Aliamini yale ambayo Filipo alikuwa akimfundisha kutoka katika maandiko, habari za Yesu Kristo na ufalme wake. Kwa moyo wake wote alipenda kuwa mfuasi wa kweli wa Bwana Yesu Kristo ili aweze kuokoka na kwa kuwa alikuwa amemwamini Yesu, lazima kwanza amtii Mungu na kubatizwa. Mara wakafika mahali penye maji mengi.Yule Mwethiopia akamwambia Filipo. “Tazama maji haya ni nini kinachonizuia nisibatizwe?” (mstari 36) Filipo akajibu akanena “Ukiamini kwa moyo wako wote inawezekana”. Akajibu akasema “Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu”. Akaamuru gari lisimame, na wote wawili wakatelemka majini na Filipo akambatiza Yule Towashi katika jina la Yesu liokoalo. Yule towashi Mwethiopia alizamishwa kabisa majini na alifunikwa na maji mwili wote na kisha akafufuka kutoka ndani ya maji hayo, akiwa kama vile mtu mpya kabisa mbele za Mungu na kasha walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, Yule towashi asimwone tena; bali alikwenda zake akifurahi. Roho wa Mungu akampeleka Filipo mpaka Azoto ambapo aliihubiri Injiri katika miji yote mpaka akafika kaisaria (mstari 40)
FUNDISHO KWETU
Huyu Mwethiopia alijaribu kumtumikia Mungu katika njia aliyoiona kuwa ndiyo iliyobora kabisa, lakini hakuifahamu njia ya kweli ambayo ndiyo Mungu anayowataka watumishi wake waifuate. Mungu akamtuma Filipo ili amfundishe towashi jinsi ya kuweza kuokolewa kwa njia ya Imani katika Kristo Yesu. Yule Mwethiopia aliamini na akaonyesha Imani yake kwa kukubali kubatizwa. Na sisi kama vile Yule Mwethiopia ni lazima tuwe na bidii tuifuate kweli ya Mungu katika Biblia. Na tunaifahamu na kuiamini kwa moyo wetu wote, ni lazima tubatizwe. Yesu alisema, “Aaminiye na kubatizwa ataokoka” (Marko 16:16).
MAELEZO YA NYONGEZA UBATIZO NI NINI
Tazama Maswalli kwa Mkufunzi 62 na 63.Hapa tuna maswali mawili na majibu kuhusu ubatizo.
1. Ubatizo ni nini Ni kuzika majini
2. Kwa kawaida ubatizo hutufanyia nini ni tendo la Mungu aliloagiza ili mwumini amvae Kristo na
kupokea ondoleo la dhambi zake.
Ni kwa mtu tu aliyeamini Injili au habari njema kuhusu Yesu Kristo na Ufalme wa Mungu ndiye anayebatizwa.Ndipo anapozamishwa ndani ya maji, kama vile anazikwa pamoja na Kristo (Warumi 6:4). Na anapotoka majini, anakuwa ni mtu mpya katika macho ya Mungu (mstari 4). Mungu anakuwa amemsamehe dhambi na katika maisha yake yote anatakiwa amtumikie Mungu. Ubatizo ni mwanzo wa kumtumikia Mungu, na atawpatia uzima wa milele wale wanaoendelea kumtumikia Mungu kwa uaminifu.
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Nini kilichosabbisha waumini wa eklesia kuondoka Yerusalemu?
2. Kutokana na mahubiri ya Filipo kulitokea nini Samaria?
3. Petrona Yohana walifanya nini walipokwenda Samaria?
4. Malaika wa Bwana alimwamuru Filipo afanye nini?
5. Filipo alikutana na mtu yupi?
6. Ni mtu yupi anayetajwa katika Isaya 53?
7. Towashi wa Ethiopia aliamini ujumbe alioambiwa na Filipo.Baada ya kuamini alitakiwa afanye
nini?
Majibu ya Kina
8. Elezea historia jinsi Filipo aivyombatiza towashi wa Ethiopia.
9. Somo hili linatufundisha umhimu wa ubatizo.
a) Ubatizo ni nini?
b) Ubatizo hutusaidia ni nini sisi?
Maswali ya Nyongeza
10. Towashi wa Ethiopia alimwamini Mungu
a) Alipaswa afanye nini zaidi ili aweze kuokoka?
b) Tunajifunza nini kutokana na somo hili?
11 a) Eleza kinachotokea wakati mtu anapobatizwa?
b) Mtu anatakiwa afanye nini baada ya kubatizwa?