CSSA 1-5-07 - HOW CHRIST CONVERTED SAUL

Swahili

107. JINSI KRISTO ALIVYOMBADILISHA SAULI

 

Amechaguliwa kuwa chombo, kwa ajili ya wasio wayahudi na kwa wana wa Israeli. “Nenda tu kwa maana huyu ni chombo kiteule changu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme na wana wa Israel. Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya jina langu”

 

Shabaha

Ni kuonyesha jinsi maisha ya Sauli wakati Bwana Yesu kristo alipomtokea njiani alipokuwa akienda Dameski. Kama tulivyo jifunza katika somo lililopita kumwua Stefano kwa mawe ulikuwa ndiyo mwanzo wa matatizo makubwa kwa ndugu wanaume na wanawake wa eklesi ya Yerusalemu. Mtesaji mkuu wa eklesi alikuwa ni kijana Myahudi, jina lake aliitwa sauli. Wale waliompiga mawe Stefano waliweka nguo zao miguuni pa Sauli (Matendo ya Mitume 8:1-4, 9:1-22; 26:4-20)

 

SAULI FARISAYO

Sauli alikuwa Myahudi aliyezaliwa Tarso, mji wa Rumi, jimbo la Kilikia. Alikuwa mfanya biashara ya Mahema, lakini baba yake alimtuma Yerusalemu kusoma chini ya miguu ya Gamalieli aliyekuwa mwalimu maarufu wakati huo. Sauli alikuwa mwelevu ambaye alijifunza maandishi ya Kiebrania kwa ufasaha, na akajifunza desturi zote za Wayahudi. Alikuwa ni mwenye bidii sana katika kutii sheria za Musa na kumtumikia Mungu kwa moyo wake wote. Hata hivyo ingawa alikuwa mnyenyekevu,kwa kweli Sauli alikuwa hafanyi yanayo mpendeza Mungu. Inawezekana Sauli alimwona Yesu na alikuwa Yerusalemu wakati akisurubiwa. Sauli alikuwa Farisayo na tunajua kwamba Farisayo ni moja kati ya wafuasi wa Kristo. Alishawishika kwamba wanafunzi walikuwa wakiwafundisha Wayahudi wasijali sheria za Musa, na alidhamiria kuwaangamiza wote.

 

BARUA KUTOKA KWA KUHANI MKUU (9:1-2)

Sauli alikuwa mkatili sana kwa jinsi alivyo watendea wafuasi wa Bwana Yesu Kristo, alifikiri kuwa ilikuwa sawa kumpiga mawe Stefano hadi kufa, na alitaka kuhakikisha kwamba waamini wote wanaadhibiwa pia. Alikwenda nyumba hadi nyumba kuwatoa nje waamini wote wanaume kwa wanawake na kuwatupa gerezani. Wengine walikimbia ili kuokoa maisha yao, lakini hata hivyo hawakuweza kuyaokoa maisha yao kutoka katika hasira na chuki ya Sauli. Hakuishia Yerusalemu bali alipanga kuwawinda popote hata katika nchi za kigeni. Alikwenda hadi kwa Kuhani Mkuu katika Yerusalemu kumwomba barua ya kumpatia nguvu na mamlaka ya kuwasaka Wayahudi katika Damaski kwa yeyote anayemwamini Yesu. Dameski ilikuwa yapata kilometa 240 kutoka Yerusalemu, lakini Sauli alipania kwenda kote huko kuwarudisha Yerusalemu ili awafunge gerezani. Sauli alifanya hivi kwa sababu alidhani kuwa anampendeza Mungu. Haikuchukua muda mrefu Mungu alimwonyesha kuwa alikuwa anafanya makosa.

 

SAFARI YA KWENDA DAMESKI (mstari 3-9)

Akiwa na barua ya Kuhani Mkuu, Sauli aliondoka akasafiri kwenda Dameski. Alikuwa radhi kuendeleza mpango wake, aliendelea na safari yake hata wakati wa joto kali mchana, wakati wasafiri wengine wakati kama huo hawakusafiri, ilibidi muda huo wapumzike. Na hata ikawa alipokaribia Dameski ilikuwa mchana,ghafla akaanguka nuru ikamwangazia pande zote, mwangaza ulikuwa mkali kuliko jua. Mwanga ulikuwa mkali mno hata sauli akaanguka chini akawa kipofu na akaogopa sana. Na kisha akasikia sauti kutoka Mbinguni ikamwambia “Sauli, Sauli, mbona waniudhi?”Sauli akajibu, “wewe ni nani Bwana?”. Naye akajibu mimi ndimi Yesu unayeniudhi. Ni vigumu kupinga mateke mchokoo.

 

Alikuwa ni Bwana Yesu Kristo aliyekuwa akizungumza na Sauli kutoka Mbinguni, Mungu likuwa akimwambia Sauli kwamba kwa kutesa eklesia alikuwa kama ng’ombe msumbufu ambaye anapiga teke zizi badala ya kwenda njia inayofaa kuingia zizini. Zizi lilikuwa linajengwa kwa nguzo ndefu zilizochongwa mwisho upande mmoja na zilitumiwa siku hizo na mwongozaji wa maksai kumtiisha kila mnyama msumbufu kuwaendesha wanyama wakorofi. Akitetemeka na kwa hofu Sauli akauliza “Bwana uatakanitafanye nini mimi?” Bwana akasema kwamba ni lazima aende hadi mjini na huko ataambiwa la kufanya (mstari 6). Na wale watu aliosafiri nao pamoja naye wakasimama wakishangaa. Walimwona Sauli akiwa kipofu, waliisikia sauti ikisema lakini wasimwone aliyekuwa akisema. Wakamshika mkono na kumsimamisha. Saulil sasa aliongozwa wakampeleka mpaka nyumbai kwa Yuda hapo akawa haoni, hali wala hanywi kwa muda wa siku tatu”. Jinsi gani ilivyokuwa tofauti kuingia Dameski ukilinganganisha na mipango yake aliyokuwa nayo ya kufika huko.

 

ANANIA ANAPELEKWA KWA SAULI

Wakati haya yakitokea mtu mwingine akapata ujumbe. Bwana Yesu Kristo alizungumza na Anania, mwanafunzi aliyekuwa Dameski na akamwambia enenda mpaka katika mtaa uitwao Mnyoofu ukaulize katika nyumba ya Yuda. Hapo uliza mtu aitwaye Sauli wa Tarso ambaye ameketi akisali na kungoja.Lakini Anania kwanza aliogopa kwa sababu alikuwa amesikia habari za Sauli na ukatili wake kwa eklesia lakini Bwana akamwambia “Nenda tu kwa maana huyu ni chombo kiteule changu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme na wana wa Israel. Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya jina langu” (mstari 15,16). Anania alitii akaenda na kumkuta Sauli katika nyumba ya Yuda. Alimwekea mikono juu ya Sauli na kusema, “Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu”. Mara macho ya Sauli yalifunguka na kuweza kuona tena.

 

SAULI ANABATIZWA.

Jambo la ajabu kilichomtokea Sauli katika siku hizo chache. Siku tatu za upofu zilimpa muda wa kufikiri na sasa alilitambua ambalo alilolichukia –Yesu wa Nazareti lilikuwa jina la Mwana wa Mungu, Masihi wa Israeli. Sauli alimsikiliza Yesu na aliongea naye na sasa nia yake ilibadilika kabisa na alitubu kwa moyo wake kwa yale mabaya na maovu aliyoyafanya. Sasa alikuwa tayari kubatizwa na Anania akambatiza (Mathayo 22:16). Sauli mpya na mnyenyekevu akakaa pamoja na wanafunzi huko Dameski kwa muda kadhaa. Jamo la ajabu lilimpata Sauli katika siku chache za mwisho. Upofu wake ulimpata kwa muda wa siku tatu ulimpatia muda wa kutafakari /kufikiri na akiwa huko alienda katika Sinagogi siyo tena kwa ajili ya kuwatafuta wale ambao kwa siri walimwamini Yesu, bali kumfundisha kila Myahudi ambaye angesikiliza kwamba yesu alikuwa Mwana wa Mungu. Wayahudi walipatwa na mshangao sana. “Huyu siye aliyeteketeza walilitaja jina hilo kule Yerusalemu?”. Hata wanafunzi pia walishangaa na walimwogopa mara ya kwanza, lakini baadaye walitambua kuwa kweli Sauli alikuwa mwanafunzi pia. Na sasa kweli alimtumikia Mungu kwa moyo wake na akawa amekuwa mtume maalumu kwa Bwana Yesu Kristo.

 

FUNDISHO KWETU

Kwa hakika sauli alifikiri anampendeza Mungu kwa kuwaadhibu wafuasi wa Yesu, lakini bidii yake ya kumtumikia haikuwa sahihi. Alitakiwa kubadilika ili kufanya kazi ya Mungu kwa njia sahihi. Alitubu na kubatizwa. Na ndipo Mungu alipopendezwa kwa yale yote ambayo Sauli aliyafanya kwa Jina Lake. Na sisi pia lazima tujifunze kuipenda kweli na hapo ndipo tutajua Mungu anataka sisi tufanye nini- tubatizwe na kumtumikia Mungu kwa moyo wote kama Sauli alivyoweza kufanya mwisho.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Baada ya muda huko Dameski, Sauli alikwenda peke yake Jangwani (Wagalatia 1:17), na aliporudi Dameski, aliwakuta Wayahudi wakipanga njama za kumwua. Walimngojea katika lango la mji mchana na usiku ili wamkamate. Sauli alijua mipango yao na usiku mmoja wanafunzi walimsaidia kutoroka kwa kumtolemsha chini ya ukuta ndani ya kikapu. Nae kasha alikwenda Yerusalemu lakini wanafunzi walikuwa wakimwogopa sauli wa Tarso na ndugu hawakumwamini kuwa nay eye ni mwanafunzi sasa. Lakini mmoja aliyeitwa Barnaba amchukua na akampeleka kwa mitume. Barnaba aliamini habari za Sauli na aliwaambia mitume yote yaliyomtokea Sauli alipokuwa njiani kwenda Damaski na ndipo akatokewa na Bwana. Ni kwa njia hii Barnaba akawa rafiki wa kazibua saulia na aliwasaidia ndugu waamini kule Yerusalemu wampokee kama walivyokuwa wakiwapokea wanafunzi wengine (mstari 23-28). Na mwisho katika masomo yetu tutaona jinsi Mungu alivyowachagua hawa ndugu wawili kusafiri nchi za mbali kwa ajili ya kuhubiri Injili.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

1.    Sauli alizaliwa wapi?

2.    Alifundishwa biashara gani?

3.    Kwa nini baba yake alimtuma kwenda Yerusalemu?

4.    Ni nani alikuwa mwalimu wake?

5.    Kwa nini Sauli aliwatesa wafuasi wa Yesu?

6.    Ni kwa nini Sauli alikwenda Damaski?

7.    Ni nani aliyeongea na Sauli alipokuwa njiani akienda Dameski?

8.    Jina la mwanafunzi aliyetumiwa kumbatiza sauli ni nani?

9.    Sauli alikuwa kipofu kwa siku ngapi?

 

Majibu ya Kina

10.  Lililompata Sauli njiani alipokuwa akienda Dameski.

11.  Bwana Yesu alisema na Anani.

       (a)  Alimwambia aende wapi?

       (b) Alimwambia afanye nini?

12.  Bwana alimwambia nini Anania kuhusu sauli na alimchagua afanye kazi gani?

 

Majibu ya Nyongeza

13.  (a) sauli alikwenda wapi baada ya kutoka Dameski mara ya kwanza?

       (b) Ni jinsi gani alivyo kubaliwa Yerusalemu?

 

 

Swahili Title
107 JINSI KRISTO ALIVYOMBADILISHA SAULI
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type