CSSA 1-5-09 - PETER BAPTISES CORNELIUS THE GENTILE

Swahili

109. PETRO ANAMBATIZA KORNELIO MTU ASIYEKUWA MYAHUDI

“Mungu amenionya, nisimwite mtu awaye yote mchafu wala wala najisi”

 

Shabaha

Ni kuonyesha jinsi Petro alivyojifunza kwamba watu wa Mataifa wanatakiwa wafundishwe Injili kama Wayahudi wanavyotakiwa kufundishwa wakati Mungu alipomtuma kumbatiza Kornelio. Baada ya Petro kumfufua Tabitha alikaa Yafa na aliishi na mtu aliyeitwa Simoni ambaye kazi yake ilikuwa ya kutengeneza ngozi za wanyama na kuifanya kuwa ngozi nzuri aliitwa fundi. Yafa ilikuwa bandari katika bahari ya Mediterania, na umbali kama km 48 kaskazini kulikuwa na mji mkubwa ulioitwa Kaisaria. Wakati Warumi walipoichukua Yudea walifanya mji wa Kaisaria kuwa makao makuu na ukawa makao makuu na ukawa makao makuu ya kikosi cha jeshi la Warumi kwa sehemu hiyo. Na sasa Petro alikuwa Myahudi na Wayahudi walikuwa hawana ushirikiano na watu wasio kuwa Wayahudi. Mungu aliandaa akili ya Petro kwa kazi atakayokwenda kuifanya kabla hajampeleka kwenda kuhubiri Injili kwa watu ambao siyo Wayahudi.

 

Matendo ya Mitume 10.

 

KORNELIO: ASKALI ALIYE MCHA MUNGU (mstari 1-2)

Katika kikosi kilichokuwa Kaisaria alikuwepo akida jina lake Kornelio. (Akida alikuwa mkuu wa kikosi cha maaskari mia moja). Kornelio alikuwa kiongozi,mtu muhimu katika jeshi lakini alikuwa amesikia mengi kuhusu Mungu wa kweli na akamwani Mungu.Alimcha Mungu yeye na nyumba yake(mstari 2).Nyumba yake na watumishi wake walimheshimu sana na wao walimwabudu Mungu wa Israeli kama vile Kornelio alivyofanya. Na siyo tu kwamba Kornelio alimwabudu Mungu bali aliwatendea matendo mema Wayahudi. Alimwabudu Mungu mara nyingi na akajitahidi kufanya yaliyompendeza Mungu kwa yote aliyokuwa akiyafanya. Maombi ya Kornelio yaka mpendeza Mungu, anayejua mioyo ya wanadamu wote, akayasikia maombi.

 

KORNELIO ANAPATA MAONO (mstari3-8)

Kornelio alikuwa akimomba Mungu kila wakati na siku moja mchana kama saa 9mchana wakati akisali malaika alimtokea waziwazi katika maono.Malaika akamwita, “Kornelio”. Aliogopa sana kusikia sauti ya malaika. Kornelio akamwuliza, “Kuna nini, Bwana?”. Malaika akamwambia kwamba Mungu ameyaona matendo yake mema na ameyasikia maombi yake na sasa alikuwa anamtuma mjumbe wake atayekayemwambia mambo ya kufanya. “Peleka watu Yafa, ukamwite Simoni, aitwaye Petro ... atakuambia yakupasayo kutenda”. Kornelio hakusita kumtii mjumbe wa mbinguni.Aliwata watumishi wake wawili pamoja na askari aliyemwaminifu akawajulisha mambo hayo yaliyotokea na jinsi alivyoambiwa. Kisha akatuma washuke hadi Yafa kwenda kumwita Petro.

 

MUNGU ANAIANDAA AKILI YA PETRO KWA MAONO (mstari 9-18)

Siku ya pili watumishi wa Kornelia walipokuwa wakikaribia Yafa, Petro alipanda juu darini kwenda kuomba. Ilipata kama saa sita mchana na akaumwa sana na njaa. Walipokuwa wakiandaa chakula roho yake ikazimia, alikuwa kama mtu aliyelala akiota ndoto. Petro akaona mbingu ikifunguka na chombo kikishuka kama nguo kubwa ikiwa imefungwa pembe zake nne ikashuka hata nchi, ndani yake kulikuwamo aina zote za wanyama najisi, yaani wanyama ambao Wayahudi hawakuruhusiwa kuwala kwa kadri ya sheria za Musa (soma Mambo ya Walawi 11:46-47). Na hapo Petro akasikia sauti ikimwambia “ondoka, Petro, uchinje ule”. Lakini Petro akaogopa sana maana Petro alikuwa hajawahi kula kamwe kitu najisi na aliamini kuwa ni kosa kula najisi. Sauti ikamwambia “kilichotakaswa na Mungu usikiite we najisi”. Jambo hiili likatendeka mara tatu kasha lile shuka likatwaliwa mbinguni. Petro alipatwa na mshangao sana. Alijua kuwa ni Mungu aliyezungumza naye lakini hakuelewa kwa nini Mungu amemwamuru kufanya jambo ambalo alifikiria kuwa ni kosa.

 

PETRO ANAKWENDA KWA KORNELIO (mstari 19-24)

Wakati Petro akitafakari ndoto hii ya ajabu, Mungu akamwambia, tazama wako watu watatu wanakutafua. Watumishi wa Kornelio walikuwa wamefika katika nyumba ya Simoni. “Nenda nao usihofu chochote ni mimi Bwana nimewatuma” (mstari 19-20). Petro akashuka ngazi akawakuta wale watu wakimwulizia, wakamwambia yale yote Kornelio aliyoyasikia katika maono yake. Na ndipo Petro akafahamu ndoto yake ilikuwa na maana gani. Mungu alikuwa akimwonyesha kuwa hata watu wa Mataifa ni sawa tu na Wayahudi mbele ya macho ya Mungu. Kama wanyama alivyowaona katika ndoto hawakuwa wanyama ambao ni najisi tena. Hikujalisha mtu huyu ni Myahudi au ni Mmataifa-watu wote wanapaswa kuja kwa Mungu kupitia Yesu Kristo. Usiku ule wale watu walikaa kwa Simoni na siku iliyofuata Petro aliondoka nao kwenda Kaisaria akaingia ndani ya nyumba ya Kornelio mtu wa Mataifa.

 

KORNELIO ANABATIZWA (mstari 25-48)

Katika siku hizo ilikuwa ni marufuku kwa Myahudi kuingia katika nyumba ya mtu wa Mataifa kama jinsi Petro alivyofanya. Lakini alitambua kuwa yalikuwa ni mapenzi ya Mungu (mstari 28). Kornelio alimlaki Petro kwa furaha kubwa na kumwangukia miguu, akamsujudia, lakini Petro akamwinua akasema “Simama, mimi nami ni mwanadamu” (mstari 25-26). Na akamwambia Kornelio na watu wote waliokusanyika mle ndani kumsikiliza. “Mungu amenionyesha mimi kwamba nisimwite mtu yeyote mchafu wala najisi” (mstari 28). Haijalishi, mtu awaye yeyote; awe Myahudi au mtu wa Mataifa ambaye anamcha na kumtii Mungu humkubali (mstari 34-35). Kornelio na wote waliokuwemo ndani ya nyumba yake wakamsikiliza Petro akiwafundisha Mwokozi mkuu, wa wanadamu wote ni Yesu Kristo Mwana wa Mungu (mstari 36-43). Na Petro alipokuwa akiendelea kuwafundisha nguvu ya Roho Mtakatifu iliwashukia watu wote waliokuwa wanamsikiliza. Walianza kunena kwa lugha mbalimbali na kumsifu Mungu. Mungu alikuwa akiwaonyesha waziwazi hawa watu (na Petro pia) ya kwamba katika tumaini la Israeli, Mungu anawapokea pia watu wa Mataifa “Ni nani awezaye kukataza maji, hawa wasibatizwe?” Mtume Petro kwa hofu aliamuru lazima watu wale wabatizwe. Ndipo Kornelio na familia yake walipo ingia na kuwa mojawapo ya familia ya Mungu wa kweli, akiwa yuko sawa mbele ya macho ya Mungu sawasawa na Wayahudi wote waaminifu waiaminio Injili.

 

FUNDISHO KWETU

Kuna watu wengi wanaoamini kuwa kama watafanya matendo mema haya yatampendeza Mungu, na kwamba Mungu atawaokoa haijalishi wanaamini nini. Hii siyo kweli kuna njia moja tu ambayo mtu anaweza kuokoka kwa kuiamini Injili na kubatizwa (angalia Somo la 1 Injili ni habari njema kuhusu ufalme wa Mungu na njia ya wokovu kwa kumwamini Yesu Kristo. Pia angalia swali la 72 la Swali la Mkufunzi) tusome Biblia ilituweze kufahamu Mungu anataka tujue na jinsi ambavyo Mungu ameagiza tumtumikie.

 

MAELEZO YA ZIADA

Katika Agano la kale tunasoma kuhusu watu wa mataifa waliounganika na Wayahudi na wakakubali na kutii amri za Musa na wakafuata desturi za Wayahudi. Miongoni mwao walikuwa wanaume na wanawake waaminifu kama Karebu na Rahabu na Lutu. Ilikuwa ni kusudi la Mungu siku zote awape Mataifa matumaini ya wokovu kama vile alivyowapatia Wayahudi tumaini la wokovu. Baada ya Yesu kufufuka mitume walifundisha kuwa ni lazima kuiamini Injili, kutubu na kubatizwa, (utakumbuka Petro alisema maneno haya siku ya Pentekoste angalia Somo la 2). Haikujulikana kabla hadi pale Petro alipotumwa kwa Kornelio ndipo Wayahudi walipotambua kuwa watu wa Mataifa pia wanaweza kuokoka kwa njia hii. Kuna njia moja ya wokovu kwa watu wote. Wakati Petro akizungumza habari za Kornelio kwa mitume huko Yerusalemu, alionyesha ni jinsi gani Mungu anawaita watu wa Mataifa kwa ajili ya jina lake (Matendo ya Mitume 15:14). Jifunze Wagalatia 3:26-29. Hapa Paulo anatuambia ninyi nyote ni wana wa Mungu kwa imani ya Yesu Kristo, kwa hiyo wengi wenu kama mlivyo batizwa kwa Kristo kuwafanya kuwa wakristo. Hivyo si kwa wayahudi wala wagiriki wote ni wamoja ndani ya Kristo. Ni furaha kubwa tuliyonayo. Mungu anatukubali sisi watu wa mataifa kama tukiamini (kuwa na Imani) katika Yesu Kristo na tukabatizwa.

 

MASWALI

Majibu mafupi

1.    Kornelio aliishi wapi?

2.    Kornelio alikuwa Mrumi alimwamini nani?

3.    Kornelio alikuwa anafanya nini kila siku?

4.    Malaika alimwambia Kornelio afanye nini?

5.    Maono ya Petro ni yapi?

6.    Mungu alikuwa anamwonyesha nini Petro?

7.    Petro alikwenda wapi baada ya maono?

8.    Petro alimtendea nini Kornelio na kwa watu wote waliokuwa nyumbani mwake?

 

Majibu ya Kina

9.    (a) Kornelio alikuwa mtu wa aina gani?

(b) Kornelio alitakiwa afanye nini zaidi?

10.  (a) Eleza Petro aliona nini katika maono?

(b) Petro alijifunza nini katika maono haya?

 

Majibu ya Nyongeza

11.  (a) Toa mifano ya watu wa Mataifa katika Agano la kale ambao walijiunga na kuwa

            Wayahudi.

      (b) Walikubali kufanya nini

12.  (a) Tunatakiwa tufanye nini ili tupate kuokoka?

(b) Je, hili ni la kweli kwa kila mtu?

(c) Taja kifungu cha Biblia kuthibitisha jibu lako.

 

Swahili Title
109 PETRO ANAMBATIZA KORNELIO MTU ASIYEKUWA MYAHUDI
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type