110. PETRO ANATOROKA KUTOKA GEREZANI
“Bwana amempeleka Malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode”
Shabaha
Kuonyesha jinsi Mungu alivyosikia maombi ya ndugu wanaume na wanawake na kumwacha huru Petro. Ilikuwa yapata miaka kumi na moja tangu Bwana Yesu Kristo alipopaa kwenda Mbinguni. Katika kipindi hiki maelfu ya Wayahudi waliongaka, wakaamini Injili na sasa kazi ilienea hata kwa watu wa Mataifa. Lakini hata hivyo Wayahudi wengi waliendelea kuwatesa waamini, wakijaribu kuizuia kazi ya mitume.
KIFO CHA YAKOBO (mstari 1-2)
Herode Agripa, ambaye alikuwa mjukuu wake Herode Mkuu, ilikuwa si muda mrefu tangu atoke Rumi na akitaka kujipatia umaarufu kwa Wayahudi. Aligundua chuki ya Wayahudi kwa wafuasi wa Yesu Kristo (nao sasa wanaitwa Wakristo Matendo ya Mitume 11:26) na akaamua kuwa njia ya haraka ni kuwaua viongozi wa kundi la waamini. Agripa alikuwa mkatili sana, alianza mpango wa ubaya wake kwa kumchukua Yakobo, kaka yake Yohana na kwa ukatili mkubwa alimchinja kwa kumkata kichwa hadharani. Ndugu, kaka na dada walipatwa na mshituko mkubwa, na woga uliwapata wote. Lakini hata hivyo Wayahudi walifurahi sana. Walitegemea kuwa iwapo Herode ataendelea hivyo wataweza kuutokomeza ukristo kabisa.
PETRO ANAFUNGWA (mstari 3-4)
Hata ikawa Herode aliona kuwa imewapendeza Wayahudi kutokana na kifo cha Yakobo, aliamua kumkamata Petro. Alitambua jinsi Petro alivyokuwa amekuwa maarufu na matokeo ya kufungwa na kifo chake kwa eklesia. Hata hivyo isingekuwa siku nzuri kumwua Petro kwani ilkuwa sikukuu ya Pasaka na Herode hakupenda kuona Wayahudi akivunja amri yao. Petro aliwekwa gerezani hadi mwisho wa siku ya saba “siku ya karamu ya mikate isiyotiwa chachu” ambao ndiyo ulikuwa unatumika wakati wa Pasaka. Na kila tahadhari ilichukuliwa, kulikuwa na ulinzi mkali kuhakikisha Petro hawezi kutoroka. Askari kumi na sita “Bataliani nne (four quaternions)” walipewa uangalizi wa juu.
SALA ZILIFANYIKA KWA AJILI YA PETRO (mstari 5,12)
Kifungo cha Petro kiliwafanya waumini wa eklesia kukutana pamoja.Usiku na mchana walikutana pamoja, wakisali sala mfululizo kwa ajili ya usalama wa mpendwa mtume wao. Siku saba za sikukuu zilikuwa zinakaribia kwisha, na mfalme alikuwa hajabadilisha uamuzi wake. Siku iliyokuwa inafuata ilikuwa Petro auwawe. Eklesia haikuwa na njia yeyote ya kufanya isipokuwa kumwomba Mungu ili Petro aachiliwe salama. Kundi lilikusanyika pamoja katika nyumba ya Mariamu mama wa Yohana Marko, ambako walipanga kukesha huko wakisali.
PETRO ANATOROKA GEREZANI (mstari 6:11)
Ingawa kanisa lilikuwa na mashaka, lakini Petro alikuwa mtulivu. Kipindi chote cha juma zima naye alikuwa akisali na sasa alikuwa tayari kuteseka mateso yoyote ambayo yangefanyika siku iliyofuata. Alikuwa amelala katikati ya Askari wawili amefungwa minyororo miwili, walinzi wawili walikuwa mbele ya mlango wakalilinda gereza. Mara nuru ikamulika mle ndani, Petro alimwona Malaika wa Mungu amesimama pale. Minyororo yake ikamwanguka mikononi na akasimama. “Jifunge kavae viatu vyako ukanifuate” Malaika alimwamru tena kutokana na nguvu za Mungu walipita bila kuonekana na walinzi sehemu zote mbili mpaka kwa walinzi wa nje ya gereza, hadi mwisho walilifikia lango zito la gereza ambao ulifunguka wenyewe walipoufikia. Hatimaye walifika nje ya gereza na Petro akawa huru. Na mara malaika akamwacha, na ndipo Petro alipojiona peke yake gizani katika eneo wazi la mtaa wa Yerusalemu, alitambua kwamba Mungu amemwokoa na mkono wa Herode. “Sasa nimejua ya kini kuwa Bwana, amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode”. Kazi ya Yakobo mwana wa Zebedayo ilikwisha lakini nguvu nyingi za Petro na uongozi bado ulihitajika kwa eklesia. Ilikuwa ni kwa sababu hii Mungu akamwokoa.
PETRO ANAFIKA NYUMBANI KWA MARIAMU (mstari 12-17)
Petro aliwafikiria wale wanaume kwa wanawake waliokusanyika nyumbani kwa Mariamu. Hara ingawa alikuwa amechelewa, alikwenda moja kwa moja na kugonga mlango wa nje.Mlango ulikuwa umefungwa kwa kuwa waliokuwa ndani walimwogopa sana Herode na Wayahudi. Dada mmoja jina lake Roda, alikwenda hadi mlangoni na kuuliza wewe ni nani? Aliposikia sauti ya Petro alipatwa na mshangao kwa furaha, hakulifungua lango alikwenda kuwaambia wenzake.Wale waliokuwa ndani hawakumwamini wakamwambia, “Una wazimu”. Lakini Roda aliendelea kusisitiza kwamba hana wazimu Petro hakika alikuwa pale. Nao wakasema “ni Malaika wake” hawakuamini kuwa alikuwa Petro mwenyewe. Huko nje Petro aliendelea kugonga hodi walipomfungulia mwisho kwa mshangao walimwona mtume mpendwa wao amesimama hapo. Aliwaeleza jinsi Mungu alivyo mtuma Malaika wake na kuachiliwa na kuwaambia wamjulishe Yakobo, kaka wa Yesu na mitume wengine. Na tena bila kuchelewa aliondoka na kwenda sehemu ya maficho ili Herode asimwone.
MUNGU AKAMWADHIBU HERODE MWOVU
Hata kulipo pambazuka “askari wakaingiwa na fadhaa nyingi”, amekuwaje Petro (mstari 18). Herode alipowatuma wampeleke Petro, waligundua kuwa Petro hakuwepo. Na hakuna mtu yeyote aliyeweza kueleza jinsi ilivyotokea, lakini Petro hakuwepo gerezani. Inaonekana kwa mawazo ya Herode kuwa wafungwa walimsaidia mtume kutoroka; na akaamuru wauawe. Inaonekana kwamba Herode alikata tamaa na mipango yake ya kumkamata mtume kwani kwa wakati ule aliondoka Yerusalemu na kwenda Kaisaria kuishi. Si muda mrefu kulikuwa na mkutano, Herode akihutubia watu walimpigia kelele “Ni chaguo la Mungu na si sauti ya wanadamu moyo wake ulitwaliwa na mfalme akakubali na Malaika wa Bwana akampiga” (mstari22). Kwa kiburi aliinua moyo wake, mfalme alikubaliana na sifa hiyo na mara moja malaika wa Bwana akampiga. “Aliliwa na chango akatokwa na roho” na akafa (Matendo ya Mitume 11:23).
SOMO KWETU
Mwanzo Yesu alifundisha ya kwamba “imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala wasikate tama”, kufa moyo (Luka 18:1). Mungu hujibu maombi yetu na huyafanya mengi zaidi ya tunavyoomba au kufikiri. Hata hivyo majibu yake si yale tunayoyategemea kupata wakati mwingine “ndiyo” na wakati mwingine “Hapana” na wakati mwingine “ngoja” wakati mwingine Mungu anapojibu maombi yetu (kama jinsi alivyomfanyia Petro usiku ule alipomwacha huru) tumekuwa kama hao ndugu ambao walikataa kuamini kwamba sala zao zilijibiwa, unakuwa kama wale watu waume kwa wake Tumwamini Mungu na tumwombe kila wakati. Na ndipo sasa haijalishi tutakuwa na ma tatizo ya namna gani, hatutakuwa na hofu, tukijua ya kwamba Mungu anatuangalia.
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Kwa nini Herode alimuua Yakobo, kaka yake Yohani?
2. Ni wakati wa sikukuu ipi ambapo Wayahudi walimweka Petro kifungoni?
3. Petro alilindwa vipi?
4. Herode alipanga amtende namna gani Petro?
5. Kanisa lilifanya nini Petro alipofungwa gerezani?
6. Taja jina la kijana aliyekwenda mlangoni wakati Petro alikuwa akigonga mlango?
7. Ni kwa nini hakumfungulia?
8. Ndugu walisemaje waliposikia habari aliyowaambia?
9. Mungu alimwadhibu namna gani Herode Agripa?
Majibu ya Kina
10. Ili kuwafurahisha Wayahudi wa Yerusalemu Herode Agripa alimfunga Petro jela.
(a) Kwanini wanaume kwa wanawake walikusanyika usiku sana katika nyumba ya Mariamu?
(b) Eleza palitokea nini wakati waliposikia mtu akigonga mlango?
11. Elezea jinsi Petro alivyookoka kutoka katika gereza.
12. Malengo ya uovu wa Herode yashindikana.
(a) Alifanya nini baada ya kujua kwamba Petro ametoroka?
(b) Mungu alimwadhibu Herode vipi ?
13. (a) Je, Mungu hujibu maombi yetu kila wakati?
(b) Je, Mungu hujibu maombi yetu kwa jinsi tunavyotegemea?