CSSA 1-5-14 - PAUL AND SILAS AT PHILIPPI

Swahili

114. PAULO NA SILA HUKO FILIPI

“Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae”

 

Shabaha

Kuonyesha jinsi Kweli ilivyohubiriwa huko Filipi ingawaje kulikuwa na mateso mengi waliyoyapata, nao wengi wakaongoka. Paulo alianza safari yake ya pili ya kuihubiri Injili na safari hii alimchukuwa Sila kusafiri pamoja naye. Wakitokea Antiokia ya Syria tena walipitia njia ya nchi kavu hadi miji ambayo tayari alikuwa amekwisha itembelea kabla, Derbe, Listra, Ikonio na Antiokia ya Pisidia. Ilikuwa ni katika safari hii ambapo Timotheo alijiunga nao.

 

Matendo ya Mitume 16: 9 -22

 

PAULO ANAONA MAONO YA MTU WA MAKENDONIA (mstari 9 – 12)

Hatimaye ndugu wakafika Trao, katika bahari ya Aegeni. Huko, usiku mmoja Paulo aliona maona ya mtu mmoja wa Makedonia amesimama, akimsihi na kumwomba msaada “vuka, uje Makedonia utusaidie”. Akitambua kwamba huu ulikuwa ni wito kutoka kwa Mungu ili kuieneza Injili katika eneo lile, Paulo hakupoteza muda ila akaanza safari katika bahari. Siku mbili baadaye wakafika Filipi, mji mkuu wa Makedonia.

 

UFANYA WANAFUNZI KATIKA FILIPI (mstari 13 -15)

Inaonekana kwamba sinagogi halikuweko huko Filipi kwa kuwa siku ya sabato watu walizoea kwenda kando ya mto kusali. Kati ya wanawake waliokusanyika pale alikuwepo Lidia,  “muuzaji wa rangi ya zambarau” ambayo ilikuwa ni rangi ya mavazi inayouzwa kwa thamani kubwa. Alikuwa tayari akimwabudu Mungu naye aliposikiliza kwa makini ujumbe wa Paulo, Lidia akamini ile kweli inayomhusu Bwana Yesu Kristo. Mungu alikuwa “amefungua moyo wake” ili kuisikia njia ya wokovui, yeye pamoja na nyumba yake wakaamini na kubatizwa. Lidia alikuwa na shukrani mno kwa Paulo na wale ndugu kwa tumaini ambalo sasa wanalishiriki, hata Lidia akawasihi, akiwaomba waomba waingie nyumbani kwake. “Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana ingieni nyumbani mwangu”. Kwa hiyo Lidia aliwahudumia chakula na kuwahudumia wakati walipokuwa wakiendelea kumtumikia Mungu huko Filipi.

 

MWUJIZA WA UPONYAJI (mstari 16 - 18)

Siku moja wakati Paulo, Sila na Timotheo walipokuwa wakienda kusali, walifuatwa na msichana mmoja mtumwa ambaye bila shaka alikuwa mgonjwa wa akili. Alijidhania kwamba angeweza kumtabiria watu bahati yake nzuri, au kwa maneno mengine, angewatabiria watu mambo ambayo yangewapata wakati ujao. Kwa hakika hakuna mtu anayeweza kufanya hivi, lakini baadhi watu waovu walimtumia mgonjwa huyo wa akilii kujitajirisha. Msichana huyu aliwafuata Paulo na wanafunzi hao kwa siku nyingi akipaza sauti na kusema: “Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu sana, wenye kuwahubiria njia ya wokovu”. Aliyokuwa akiyasema kwa sauti kuu yalikuwa ni ya kweli kabisa, lakini Paulo alisikitika sana kwa maana alikuwa haelewi alichokuwa akikisema. Paulo alipatwa na wasiwasi kwa sababu Kweli haienezwi kwa njia hii ya kupiga kelele. Kwa hiyo, siku moja, alipokuwa akiendelea kuwafuata, Paulo akageuka na kumwambia yule mwanamke. Mara moja akapona. Nguvu ya Roho Mtakatifu iliweza kumponya kupitia maneno ya mitume naye yule binti akawa mtu wa kawaida, msichana mwenye akili timamu, inaezakana kuwa ilikuwa mara ya kwanza katika maisha yake.

 

PAULO NA SILA WANAPIGWA (mstari 19-23)

Wakati matajiri wake walipoona kwamba hawangemtumia tena kujitajirisha, walikasirika sana. Hawakujali hata kidogo kwamba huyu msichana mdogo alikuwa amepona. Walijifikiria wao wenyewe. Wakawakamata Paulo na Sila, wakawaburuza kuelekea sokoni kwa watawala wa mji, ambao kwa upande wao wakawapeleka kwa makadhi. Wakasema kuwa “Watu hawa, wanachafua sana mji wetu; nao ni Wayahudi” (mstari 20). Na kwa kuwa Paulo na Sila walikuwa ni wageni katika Filipi, haikuwa vigumu kuwasingizia tuhuma ya uongo. Kwa hiyo wakatuhumiwa kwamba walikuwa wanafundisha mambo yanayopingana na sheria za Rumi. Kufumba na kufumbua kundi la watu wenye hasira lilikusanyika, wote walisisitiza kuona Paulo na Sila wanaadhibiwa. Hawakupewa hata muda wa kujibu tuhuma kwa makadhi na kabla hata ya kujibu makadhi wakawavua nguo kwa nguvu na waka toa amri kwamba wapigwe kwa bokora. Hao ndugu wasio na bahati wakapigwa mijeredi mingi, na huku migongo yao ikichuruzika damu na vidonda, wakatupwa gerezani. Mlinzi wa gereza ambaye aliamrishwa kuwatunza kwa usalama, akawafunga miguuni yao kwa mkatale.

 

FUNDISHO KWETU

Katika barua yake kwa Wathesalonike (1 Wathesalonike 2:2), Paulo akawakumbusha ndugu ya kwamba ingawaje walidhalilishwa kule Filipi, “twalithutu katika Mungu wetu, kuinena kwenu Injili ya Mungu wetu:” Hata aibu na jinsi walivyotendewa vibaya na maumivu makali sana waliyoyapata kutokana na mijeredi waliyopigwa haikuwabadili nia za akili yao kuhusu kuihubiri Injili. Walikuwa watiifu kabisa, wasio na ubinafsi, wakijua kwamba Bwana Yesu Kristo alikuwa ameteswa zaidi kuliko wao. Inatupasa kufikiria juu ya majaribu na matatizo yetu yanayofanana na hayo.Hii itatusaidia sisi kuwa watumishi bora zaidi wa Kristo na kuwa na shukrani zaidi kwa Mungu.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Ni jinsi gani ilivyo mfano kwetu sisi kuona unyenyekevu aliokuwa nao Lidia alipokuwa akisikiliza na kujifunza Kweli. Inaonekana kwamba hakuna wanaume katika Filipi waliokuwa na nia yoyote katika mambo ya Mungu wakati lakini hili halikumzuia Lidia kuwakusanya wanawake wenzake pamoja kando ya mto siku ya sabato kwa ajili ya sala na ibada. Siyo tu kwamba Lidia alichukua wajibu huu, lakini kazi yake “ya kuuza rangi ya zambarau” ingemfanya kukosa muda kwa sababu ya shughuli nyingi. Hakuweza kuruhusu mojawapo ya haya kumzuia Neno la Mungu. Kwa kuwa Baba huangalia moyo, Mungu alimfahamu jinsi Lidia alivyokuwa mwanamke mwaminifu, na alikuwa na bidii ya kumsikiliza Paulo, na Mungu “akaufungua moyo wake” na akamsaidia kuweza kuelewa. Hata tukiangalia nyakati za hema ya kukutania kule jangwani, Mungu aliwapatia hekima ya kipekee baadhi ya wote ambao mioyo yao ilipenda kwa hiari kutumika kwenye vipengere mbalimbali katika madhabahu ya Mungu (Kutoka 35:30-35; 36:1-2). Tutaweza kuona, kwamba Mungu anakuwa msaada wa karibu wakati tuapofungua moyo wetu kwa sala Neno lake na kuweza kulielewa.Kama iwapo mioyo yetu itakuwa na shauku ya kuitafuta kweli ya Mungu, kwa hakika tutaipata.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

  1. Mtu aliyeonekana katika maono kule Troa alimwambia nini Paulo?
  2. Lidia aliishi wapi?
  3. Lidia alikuwa ni nani?
  4. Mungu alimfanyia nini Lidia?
  5. Yule msichana mtumwa alipaza sauti akisema Paulo na Sila walikuwa watu wa namna?
  6. Ni kwa nini wale wanaume walikasirika wakati yule msichana mtumwa alipoponywa?
  7. Hawa watu walisema Paulo na Sila walikuwa wanafanya nini?
  8. Waliwatenda nini Paulo na Sila kabla ya kuwatupa gerezani?

 

Majibu ya Kina

  1. Eleza habari ya jinsi Paulo alivyomponya yule msichana mtumwa kule Filipi na nini

kiliwatokea Paulo na Sila kabla hawajatupwa gerezani?

Majibu ya Nyongeza

  1. Eleza jinsi Lidia alivyofika kuja kuisikia Kweli na tunajifunza nini kutokana na mfano wake

mzuri.

 

 

 

Swahili Title
114 PAULO NA SILA HUKO FILIPI
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type