CSSA 1-5-16 - PAUL AT ATHENS

Swahili

116. PAULO AKIWA ATHENE

“Kwa maana, Mungu ameiweka siku, ambayo atakayowahukumu walimwengu kwa haki”

 

Shabaha

Kuonyesha jinsi Paulo alivyowahubiri watu wenye hekima kule Athene ambao hawakuweza kuielewa hekima Mungu. Katika safari yake ya pili bila shaka Paulo alikuwa ni mwenye furaha kubwa kwa ajili ya wale alifuatana nao. Kwa kawaida wao hawakupata mateso mara nyingi, kama Paulo alivyokuwa akitendewa mikononi mwa Wayahudi, lakini hawakumwacha peke yake, nyakati za hatari. Wakati mwingine aliwaacha baadhi yao nyuma ili waweze kuziimarisha eklesia mpya, wakati yeye alipoku akisafiri kwenda mji mwingine. Kwa hiyo Luka na Timotheo wao walibakia Filipi, ambapo Paulo na Sila walikwenda hadi Thesalonike na Beroya. Baadaye Paulo alisafiri hadi Athene peke yake ambako alijihisi mpweke kati ya watu waliokuwa wamejaa mno hekima ya dunia hii, hata wasiweze kuelewa Injili kabisa.

 

Matendo ya Mitume 17: 16 – 34

 

 

WATU WA BEROYA WALIKUWA WAUNGWANA (mstari 10 – 15)

Huko Beroya, Paulo aliwakuta Wayahudi “walikuwa waungwana” kuliko wale wa Thesalonike. Hawakuyaziba masikio yao mara moja kwa kusikia jina la Yesu wa Nazareti, bali walikuwa tayari kumsikiliza Paulo na kuhojiana naye. “Walilipokea Neno kwa unyenyekevu wa moyo, wakayachunguza Maandiko kila siku, waone kama mambo hayo ndivyo yalivyo” (mstari 11). Kwa kuwa walikuwa tayari kusoma Biblia kwa uaminifu, wakagundua kwamba yale Paulo aliyowaambia yalikuwa ni ya kweli na kwa hiyo wakaamini. Paulo ilimpasa kuondoka Beroya kwa ghafla, kwa sababu Wayahudi waliotoka Thesalonike walimfuata kule ili kuchochea ghasia. Akaondoka, akaenda hadi Athene, akiwaacha Sila na Timotheo (ambao walikuwa wamewasili wakitokea Filipi) ili kuwatia moyo ndugu kwa siku chache zaidi.

 

PAULO AKIWA ATHENE (mstari 16 -18)

Wakati Paulo akiwangojea wale wengine ili wafike Athene, alizunguka kuuona mji na akaona kwamba mji ulikuwa umejaa vinyago. Ilimkasirisha sana kufikiri kwamba watu walikuwa wajinga kiasi hicho cha kuabudu miungu mingi namna hiyo. Hakupoteza muda, akaanza kuhubiri kwa yeyote aliyeweza kumsikiliza. Kwanza aliingia ndani ya sinagogi, lakini Wayahudi pale hawakuwa na nia. Kisha akaelekea sokoni, eneo lililowazi na kbwa ndani ya jiji, ambako watu wengi walikuja kufanya biashara au kuzungumza tu kila siku akazungumza na yeyote aliyepita hapo. Haikuchukuwa muda mrefu kabla ya Wayunani wenye falsafa kumsikiliza Paulo nao wakataka kujua zaidi juu ya mafundisho yake. Alionekana kwao kuwa ni “mwanzilishi wa kufundisha habari za miungu migeni” kwa sababu alihubiri kuhusu Yesu na ufufuo wa wafu. Neno mwanafalsafa linamaanisha ya “mpenda hekima” na watu hawa walipenda kutafakari kwa kina kuhusu vitu, kama vile wengi duniani wanavyofanya siku hizi. Lakini ilikuwa hekima ya watu tu, nayo hii ni tofauti kabisa na hekima ya Mungu. Hekima ya Mungu inaweza kufundishwa kutoka katika Biblia tu. Na iwapo watu hawataisoma Biblia , basi hapo haijarishi hata kama wangefikiri kwa nguvu kiasi gani, hawataweza kamwe kuwa na “hekima ya kuweza kupata wokovu”. Kwa maana wanapokufa na hekima yao huishia hapo. Wanafalsafa wakampeka Paulo sehemu yao maarufu sana katika mji, inayoitwa Areopago - “Kwa maana Wathene na wageni (yaani watu ambao wasio kuwa wenyeji wa mji ule) waliokaa huko hawakuwa nafasi kwa neno lokote ila kutoa habari na kusikiliza habari za jambo jipya” (mstari 21). Na sasa ilikuwa ni nafasi muhimu sana kwa Paulo ya kuwaambia kuhusu “mambo mapya” yaani alitakiwa awaambie Kweli kuhusu Mungu na Yesu Kristo.

 

PAULO AKIWA KATIKA KILIMA CHA MARS (mstari 22-31)

Paulo alipokuwa akizunguka katika mji, aliona baadhi ya madhabahu ya miungu yao, hiyo iliandikwa maneno haya “KWA MUNGU ASIYEJULIKANA” (mstari 23). Kwa sababu ya imani yao ya ushirikiana ndiyo maana waliitengeza madhabahu hii, wakihofu kwamba kama watamkosa mungu mmjawapo, mungu huyu ambaye hawajamweka hapo angewakasirikia na kuwaadhibu. Ndipo Paulo sasa akawaambia kuwa atawaeleza habari kuhusu huyu “MUNGU ASIYEJULIKANA”, ili waweze kumwabudu huyu Mungu. Kwa watu hawa Mungu aliyeumba mbingu na nchi alikuwa ni Mungu asiyejulikana-hawakuwahi kumfikiria,wla kumsikia habari zake na wala hawakumwamini Mungu huyu. Mji wa Athene ulikuwa na hekalu nyingi sana, lakini Mungu wa kweli hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono, (linganisha na Matendo ya Mitume 7:48, 17:24). Yeye ni mwumbaji wa mbingu na nchi. Mungu hutupatia pumzi na uhai na ndiye anatupatia mahitaji yetu. Hakuna sanamu ilitengenezwa kutoka na dhahabu au fedha au miti aliye kama huyu Mungu. Hapo mwanzo Paulo aliwaambia kuwa walikuwa hawamfahamu Mungh, lakini sasa wanapaswa kutubu na wamgeukie waache ujinga wao wamwelekee Mungu. Siyo kwamba Paulo aliwaambia watu maneno haya, bali pia aliwaonya kuhusu hukumu ya Mungu ambayo inaileta kwa watu wote wasiomcha Mungu. Akasema Mungu “ameweka siku ambayo atawahukumu wanadamu kwa haki kwa mtu Yule (Bwana Yesu Kristo) aliyemchagua”. Kufufuka kwa Yesu Kristo kutoka kwa wafu ni udhibitisho kwamba atawahukumu walimwengu. Paulo aliweza kuona kuwa watu hawa wasomi hawakuwa na nia ya ya kujifunza njia ya wokovu. Wao walifikiria kuwa mafundisho ya Paulo elikuwa ni elimu mpya na inayofurahisha sana, hata hivyo hawakuamini. Baadhi yao walicheka waliposikia habari ya kifo. Kwa hiyo Paulo akaondoka, baadhi ya watu wakafuatana naye na waliendelea kumsikiliza zaidi Paulo, wakaamini.

 

FUNDISHO KWETU

Watu wengi siku hizi ni sawa na Wayunani hawa wasomi wanafalsafa, ambao wanapenda kujifikiria kuwa ni wenye akili sana - lakini kwa huzuni hawajui chochote kuhusu mambo ambayo ni muhimu hasa kwa maana hekima ya dunia hii ni upumbavu kwa Mungu. Na tuiweke hazina ya hekima tunayoipata kutokana na Neno la Mungu, kuliko hekima yoyote ya dunia, ili kwamba katika “siku hiyo iliyowekwa” wakati Yesu Kristo atakaporudi, tuweze kukutwa tukimtumikia Mungu mmoja wa kweli.

 

MAELEZO YA ZIADA

 Katika Matendo ya Mitume 17:18 tuna ambiwa kuwa kulikuwa na matabaka mawili ya wanafalsafa ambayo Paulo alizungumza nao. Waliitwa Waepikureo na Wastoiko. Kwa muda mrefu walikuwa wametafakari sana kuhusu maana ya maisha na hatimaye wakafikia majibu yao wenyewe kuwa katika shabaha ya mtu ni ipi katika kuishi kwake.

 

(1) Waepikureo waliamini kuwa ulimwengu ulitokea kwa bahati tu. Walisema kwamba miungu walikuwa mbali mno kujihusisha na dunia au kujishughulisha na watu waliomo. Hii hakika ilimaanisha kwamba hawakumwamini Mungu. Kwa watu hawa Mungu anasema: “Mpumbavu amesema moyoni mwake, hakuna Mungu” (Zaburi 14:1). Waepikureo walifikira kwamba lengo bora kabisa maishani ni kuishi maisha ya anasa. Filosofia yao ilikuwa ni “na tule, tunywe na kujifurahisha kwa kuwa kesho tunakufa”

 

(2) Wastoiko waliamoni katika maisha ya kiasi. Ulikuwa ni udhaifu, walisema, kuonyesha hisia za furaha au huzuni au maumivu. Mwanadamu anapaswa kujitawala mwenyewe. Unaweza kutafakari jinsi walivyokuwa na kiburi. Hawakufikia kwamba wanamhitaji Mungu. Lakini Mungu anasema: “Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA” (Mithali 16:5).

 

Kitu kimoja ambacho wote hawa wanafalsafa walikiamini ilikuwa ni kwamba kila mtu alikuwa na sehemu ya mwili isiyokufa ndani yake na hata hata mtu anapokufa sehemu hiyo ya mwili huendelea kuishi milele. Hadi sasa, watu wengi bado wanaamini mafundisho haya. Hilo ni kosa (angalia Maswali ya Mkufunzi 31, 32, 34). Kwa kuwa waliamini fundisho hili, walidhihaki na kucheka fundisho hili la ufufuo, na wala hawakufikiria kwamba wanamhitaji Mwokozi. Hekima ya Mungu kwa kumleta Yesu Kristo ilionekana ni upuuzi kwao, lakini Mungu amesema. “nitaiharibu hekima yao wenye hekima” (1 Wakorintho. 1:19). Na kwa hiyo Paulo akamaliza hotuba yake juu ya Kima cha Marsi kwa kuwaambia kuhusu hukumu ya Mungu ambayo inakuja kwa wanadamu wote. Ni jinsi gani Paulo ilivyomhuzunisha kuona kwamba ingawa aliwajulisha hukumu ya Mungu inayokuja bado halikuweza kuamusha nia yao. Katika mawazo Walikuwa wamemwacha Mungu katika mawazo yao kabisa, kama watu wengi leo ambavyo wamemwacha Mungu katika mioyo yao. Tusiweke tumaini kamwe katika hekima na elima ya dunia, bali tulitegemee Neno la Mungu ili tupate hekima ya kweli ambayo inatuongoza katika uzima wa milele.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

  1. Mtume Paulo pale Athene aliokuwa akiwangojea akina nani?
  2. Paulo aliona nini kwa mara ya kwanza alipokuwa akizungumka mji wa Athene?
  3. Watu Waathene walipenda kusikia nini?
  4. Ni wapi Paulo aliposimama alipokuwa akisema na watu wa Athene?
  5. Ni maneno gani Paulo aliyoyaona kwenye madhabahu yao mojawapo?
  6. Je, kuna mtu yeyote aliyeamini maneno ambayo Paulo aliyowaambia?

 

Majibu ya Kina

  1. Je, Paulo aliwaambia nini watu wa Athene kuhusu Mungu?
  2. a) Malizia sentensi/nukuu hii: “Mungu ameiweka siku...”

       b) Watu wa Athene walifikiri nini walipoyasikia yale aliyoyasema Paulo?

 

Majibu ya Nyongeza

  1. a) Ni nini

(i)         Walichoamini Waepikureo?

                  (ii)         Wastoiko walichoamini nini?

b) Ni sehemu gani peke yake tunapoweza kupata hekima ya kweli?

 

Swahili Title
116 PAULO AKIWA ATHENE
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type