- KWEDA YERUSALEMU NA KUFUNGWA
“Nipo tayari, siyo kufungwa tu, bali hata kufa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu”
Shabaha
Kuonyesha jinsi maonyo ya Mungu kwa Paulo kuhusiana na kifungo katika Yerusalemu, yalivyotimia. Wakati wa safari yake ya tatu Paulo alihamasisha wana-eklesia kuchanga fedha kwa ajili ya ndugu maskini katika Yerusalemu. Na sasa wakati safari yake ilipokuwa ikimalizika, alielekeza uso wake kwenda Yerusalemu akazichukua na fedha ambazo zilichangwa (Matendo ya Mitume 24:17). Alifahamu kwamba matatizo na mateso yalikuwa yakimngojea huko Yerusalemu, kwa maana alikuwa amewambia watu wa Waefeso: “Nashika njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa rohoni, nisiyajue mambo yatakayonikuta huko; isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja. Lakini mambo yote hayo hayaniondoi katika imani kamwe...” (Matendo ya Mitume 20:22 – 24). Paulo hakusita kuhubiri Injili kwa watu wote ambao walipenda kusikiliza. Na sasa ilimpasa kuhu hubiri pale Yerusalemu - yamkini ilikuwa ni kazi ngumu kuliko zote katika shughuli yake.
Matendo 21
UNABII WA AGABO (mstari 8 – 14)
Wakati Paulo alipoondoka Troa alikuwa akilekea kwenda Yerusalemu. Alikuwa na shauku ya kufika kule kwa muda mwafaka ili kusherekea sikukuu ya pentekoste. Vituo vyake vikuo vilikuwa Mileto, Tiro na Kaisaria. Pale Mileto aliwaita ndugu wa Efeso waende kwake na akawafariji sana na kuwaonya. Walihuzunika sana kwa kumwona Paulo akienda hasa kwa sababu alisema, “hamtaniona uso wangu tena”. Pale Tiro, meli aliyokuwa amepanda Paulo ilitia nanga kwa muda wa siku saba ili kupakuwa shehena yake na Paulo alitumia wakati wake na wanafunzi wa huko. Hapa pia walimwonya Paulo, kwa njia ya Roho, kuhusu hatari itakayomkabiri katika Yerusalemu. Ndugu pamoja na wake zao na watoto wote walishuka hadi ufukweni mwa bahari kumwaga Paulo na wenzake aliokuwa nayo. Hapo walipiga magoti na kusali pamoja kabla Paulo hajapanda melini na kuondoka kuelekea kusini hadi Kaisaria. Kule Kaisaria Paulo alikaa katika nyumba ya Filipo (mstari 8 Matendo ya Mitume 6:5). Hapo nabii kutoka Yudea aliyeitwa Agabo, alichukua mkanda wa Paulo na kufunga mikono yake na miguu na kusema, “Roho Mtakatifu hivi, Hivyo ndivyo wasemavyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyo mfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya Mataifa” (mstari 11). Ndugu wakamwomba sana asiendelee mbele kwenda Yerusalemu. Na hata wenzake na Paulo aliokuwa akisafiri nao katika safari ambao kabla walikuwa wamesikia maonyo haya, na sasa walimsihi kabisa asiende Yerusalemu. Lakini Paulo akawajibu, “Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha yakufungwa; ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu” (mstari 13). Nao walipoana kwamba Paulo amekaza nia yake ya kuendelea na safari hadi Yerusalemu, wakasema: “Mapenzi ya Bwana na yatendeke” (mstari 14).
PAULO ANAFIKA YERUSALEMU (mstari 15 – 26)
Wakifunga mizigo yao pamoja (na sadaka ya thamani ya fedha zilizotokana na michango kutoka kwenye eklesia za watu wa Mataifa kwa ajili ya ndugu maskini wa Yerusalemu), Paulo na wenzake waliokuwa pamoja naye katika safari walianza safari yao ya siku tatu wakisindikizwa na baadhi ya wanafunzi waliotokea Kaisaria. Walipokelewa kwa moyo wa furaha huko Yerusalemu na siku iliyofuata Paulo alikwenda kumwona Yakobo na wazee wa ekelesia. Paulo aliwaeleza habari moja baada jingine ya mambo amabayo Mungu alikuwa amefanya kupitia kwake, nao waliposikia habari yote ya mambo hayo, walimtukuza Mungu. Lakini sasa Yakobo na wazee walikuwa na tatizo wakati kwa kuwa Paulo alikuwa Yerusalemu. Wayahudi maelfu ambao walikuwa wamebatizwa bado waliendeleza kufuata sheria ya Musa, nao walikuwa wameambiwa kuwa Paulo alikuwa akiwahamasisha Wayahudi hao kusahau sheria ya Musa. Na ukweli ni kwamba, walikuwa wakisema uongo. Paulo alifahamu kuwa haikutakiwa tena kuishika sheria ya Musa. Mungu huwakubali Wayahudi na watu wa Mataifa kwa sababu waliamini injili na kubatizwa. Mtume hakuwafundisha watu wa Mataifa kufuata sheria, na wala hakuwaagiza Wayahudi kutokuifuata sheria. Ilishauriwa kwamba Paulo aende hekaluni na kujiunga na Wayahudi wengine wanne, ambao walikuwa wakitimiza kiapo kwa Mungu. Hili lingeonyesha kwamba hakuanzisha mpango wa kuangamiza desturi za Wayahudi. Wakati alipokuwa hekaluni tuhuma nyingine ya uongo ilisemwa juu yake. Baadhi ya Wayahudi walipiga kelele wakisema alikuwa amemleta mtu wa Mataifa ndani ya hekalu, ambamo watu wa Mataifa hawakuwa wakiruhusiwa kuingia. Hili nalo halikuwa kweli.
PAULO ANAFUNGWA MINYORORO (mstari 27 - 37)
Kwa muda mfupi waliwahamasisha Wayahudi katika mji na ghasia ikatokea. Paulo aliburuzwa kutoka hekaluni na milango ikafungwa mara moja. Wayahudi wangemwua Paulo kama Lisia, aliyekuwa jemadari mkuu Rumi asingetokea ghafla na maaskari wake. Mara aliposikia makelele alichukua askari na walinzi na kukimbilia kundi lililokuwa karibu na hekalu. Wayahudi walipowaona Warumi hao wakifika waliacha kumpiga Paulo. Alikuwa amefungwa kwa minyororo miwili naye Lisia akamwuliza wewe ni na umefanya nini hata kuanzisha ghasia namna ile. Wayahudi wakapiga kelele huyu alisema hili na huyu alisema lingine kwa mvumo mmoja, naye hakuweza kuelewa walichokuwa wakisema. Hivyo akamchukua Paulo hadi kwenye ngome ya Warumi ya Antonia. Wayahudi walikuwa bado wana hasira, nao wakapiga mbio kuwafuata maaskari wakipiga kelele, “mwondoe huyo”. Askari walilazimika kumbeba kumpandisha ngazi mpaka kuingia ngomeni kwa sababu ya ukali wa watu. Na sasa alikuwa mfungwa, kama Mungu alivyokuwa amemwambia.
FUNDISHO KWETU
Kila mahali Paulo alipokwenda katika safari zake alipokelewa na waumini kwa furaha. Na hivi ndivyo inavyoendelea hata sasa kati ya ndugu wanaume na wanawake katika Bwana Yesu Kristo. Kila wakati na tuwe wakuwafikiria na kuwa wapole kwa rafiki zetu wanaoipenda kweli. Tunajifunza pia katika habari hii, kuwa kama Paulo, wenye hamasa ya kutenda mapenzi yake Mungu, bila kujali ni matatizo ya jinsi gani yaliyo mbele yetu. Kwa kweli ilihitaji ujasiri mkubwa kwenda Yerusalemu, wakati Mtume alikuwa anafahamu kwamba angefungwa huko. Na tuwe na ujasiri wa namna hii, wakati tunapopaswa kusimama kinyume cha wengine kwa ajili ya jina la Yesu Kristo.
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Kwa nini Paulo aliharakisha kurudi Yerusalemu?
2. Nabii Agabo alifanya nini na mshipi wa Paulo?
3. Agabo alimwambia nini Paulo?
4. Je, Paulo aliogopa kwenda Yerusalemu?
5. Je,Paulo alikutana na nani kule Yerusalemu?
6. Paulo aliwaambia nini wazee kule Yerusalemu?
7. Yakobo alimweleza Paulo ni kitu gani Wayahudi walikuwa wakisema kuhusu yeye?
8. Waliazimia Paulo afanye nini kuonyesha kuwa uvumi uliokuwepo ulikuwa uongo?
Majibu ya Kina
9. Paulo alikuwa safarini kuelekea Yerusalemu wakati alipoonana na Nabii Agabo kule Kaisaria.
a. Agabo alisema nini kitakachomtokea Paulo?
b. Ni jinsi gani alionyesha kuwa ndivyo itakavyotokea?
c. Paulo alisema alikuwa tayari kufanya nini kule Yerusalemu?
10. (a) Kwa nini Paulo alikwenda hekaluni pamoja na wengine wanne?
(b) Je, hili lilianzishaje uvumi?
(c) Eleza kuhusu ghasia iliyofuatwa na nini kilitokea kwa Paulo?