CSSA 1-5-22 - PAUL DEFENDS THE TRUTH BEFORE AGRIPPA

Swahili

122. PAULO ANAILINDA KWELI MBELE YA AGRIPA

“Na sasa ninasimama nihukumiwe kwa ajili ya tumaini la ahadi baba zetu waliyopewa na Mungu”

 

Shabaha

Kuonyesha jinsi Paulo alivyosimama imara katika kuihubiri Kweli na Mungu alivyotenda maishani mwake kumleta mtume huyo hadi Rumi ili aihubiri Injili kule pia.

 

Matendo ya Mitume 25:13 – 27; 26

 

MFALME AGRIPA NA BERNIKE WANAMTEMBELEA FESTO

(Matendo ya Mitume 25: 13 – 23)

Mara tu Festo alipokuwa mtawala alitembelewa na Mfalme Agripa na dada yake Bernike .Walikuwa ni mwana na binti yake Heredi Agripa yule mwovu ambaye alimwua Yakobo (12). Warumi walimfanya kuwa mfalme wa sehemu ndogo ya Palestina naye Agrippa alikuwa akimtembelea mtawala mpya wa Kaisaria. Kuja kwa wageni hawa kulimsaidia Festo, kwa sababu shauri la Paulo lilikuwa ni tatizo kwake. Mtume alikuwa amekata rufani kwa Kaisaria naye Festo ilibidi aandike barua Rumi kueleza tuhuma zilizowekwa dhidi yake. Lakini Festo hakujua aandike nini. Kwa kuwa Agrippa aliwaelewa Wayahudi, kwa hiyo Festo alitumaini kupata msaada ili ajue la kusema kumhusu Paulo. Wakati Agrippa aliposema kuwa yeye mwenyewe angependa kumsikiliza Paulo,Festo akatayarisha mkutano siku iliyofuata. Lilikuwa tukio lenye heshima kubwa sana, kwani Agrippa na Bernisi walipoingia wakiwa wamevaa majoho ya kifalme. Wakuu wa mji na maafisa wa jeshi la Warumi walikuwepo pia. Agrippa akakaa katika kiti cha hukumu na kila kitu kilipakuwa tayari Paulo aliletwa ndani na Festo akamtambulisha. Jinsi ulinganisho ulivyokuwa kati ya mfungwa Paulo na utukufu wa nguo zilizokuwa zimevaliwa na watu waliokuwa wamemzunguka.

 

PAULO ANAKARIBISHWA KUZUNGUMZA (Matendo ya Mitume 25: 24 -27; 26:1)

Watu wote mashuhuri waliokusanyika mle yakini walikuwa na shauku juu ya mtu huyu aliye mbele yao. Hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kusema kosa alilolitenda, ingawaje alikuwa gerezani kwa zaidi ya miaka miwili naye sasa alikuwa amekata rufani kwa Kaisaria huko Rumi. Hata Agrippa baadaye alisema. “Mtu huyu hatendi neno linalostahili kifo wala kufungwa” (Matendo ya Mitume 26:31). Lakini mkutano huu uliofanyika mbele ya Agrippa haukuwa wa kusikiliza kesi, hapakuwa na yeyote wa kumstaki siku ile. Agrippa alitaka tu kumsikiliza Paulo alitaka kusema nini. Akamgeukia mfungwa na kusema. “Una ruhusa kusema maneno yako” (Matendo ya Mitume 26:1). Paulo aliifurahia fursa hiyo ili ajitetee, kueleza kuhusu maisha yake yote na kazi yake.

 

ANAILINDA IMANI (Matendo ya Mitume 26: 2- 32)

Katika lugha rahisi inayoeleweka, Paulo alianza kueleza historia yake. Agripa alizifahamu imani na desturi za Wayahudi, kwa hiyo Paulo alikuwa na furaha kubwa kumweleza historia yake (mstari 2- 3). Wayahudi wote walifahamu matendo yake kuanzia miaka yake ya maisha yake. Walimfahamu vizuri kabisa kwamba aliitii sheria siku zote, akiwa Farisayo mwenye msimamo mkali. Aliamini yote ambayo Wayahudi wote waliyaamini - yaani kuhusu ahadi zilizotolewa na Mungu kwa mababa (mstari 4 – 7). Kuhusu ufufuo wa wafu, halikuwa jambo jipya. Kulikuwa na mifano mingi kuhusu ufufuo katika Maandiko. Lakini ufufuo wa Yesu wa Nazareti ndiyo ulioleta msisismko kwa Wayahudi (mstari 8). Paulo na mitume walikuwa wakihubiri kwamba Yesu yu hai na yuko mkono wa kuume wa Mungu. Ndipo Paulo akaendelea kueleza namna alivyowatesa wanafunzi wa Kristo na kuwatesa (mstari 9 – 11). Lakini aliamini akiwa barabarani kuelekea Dameski kwa kusikia sauti ya Yesu Kristo mwenyewe, ambaye Mungu alikuwa amemfufua kutoka kwa wafu (mstari 12 -15). Akapewa kazi aifanye ya kuhubiri Injili kwa Mataifa, ili wao pia na wao waweze kuwa na tumaini la ufufuo, kama vile Wayahudi walivyokuwa na tumaini, kwa imani iliyo katika Yesu Kristo (mstari 16 -20). Akamalizia hotuba yake kwa kurudia maneno aliyokuwa ameyaeleza mwanzo, ya kwamba mahubiri yake hayakuwa tofauti na yale ambayo manabii wote na Musa walikuwa wameyafundisha kuhusu Masihi (yaani, Kristo):

 

1)    “Kwamba Kristo angeteseka na kwamba

  1. Angekuwa wa kwanza kufufuliwa kutoka kwa wafu, na
  2. Atatangaza nuru kwa watu (Wayahudi) na
  3. Kwa watu wa Mataifa” (mstari 22 – 23).

 

Alipokwisha kuyasema maneno haya,Festo alipaza kwa sauti kuu “Paulo, unawazimu, kusoma kwako kwingi kumekugeuza akili”. (mstari 24). Lakini Paulo hakuwa kichaa hata kidogo. Maneno aliyoyasema yalikuwa ya kweli. Akimgeukia Agripa, Paulo alimwuliza, “Mfalme Agripa, je! wawaamini manabii? Najua ya kuwa waamini?” (mstari 27). Agripa ni dhahiri kuwa aliaibika Paulo alikuwa amesema vyema na Agrippa hakufahamu aseme nini, kwaa hiyo akamjibu, “kwa maneno machache wadhani kunifanya mimi kuwa Mkristo” (mstari 28). Jinsi gani Paulo angefurahi kama Agripa angemaanisha hivyo. Kifungo chake chote hiki kingekuwa chenye thamani sana. Baadaye Agrippa alimweleza Festo. “Mtu huyu angeweza kufunguliwa, kama asingalitaka rufani kwa Kaisari” (mstari 32).

 

FUNDISHO KWETU

Aliporudi gerezani Paulo aliyakumbuka maneno ya Bwana Yesu: “imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako” (Matendo ya Mitume 23:11). Kama tulivyokwisha kuona mwanzo, Paulo alikuwa akiteseka katika kazi ya kumtumikia Kristo, kama vile vile Kristo, naye alivyoseka. Paulo wakati wote alifahamu kuwa hatari ilikuwa ikimngoja mbele yake, lakini alikuwa tayari kujitolea kuacha raha yake au hata uhai wake, ili injili iweze kuhubiriwa. Kwa hiyo aliweza kuwaambia Wakorintho, “Mnifuate mimi kama mimi ninavyo mfuata Kristo” (1 Wakorintho 11:1). Nasi tutumie nguvu zetu zote na muda katika kumtumikia Mungu, kama vile Paulo alivyofanya.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

  1. Ni nani aliyekuja kumtembelea Festo?
  2. Ni kwa nini Festo alifurahi sana kutembelewa na wageni hao?
  3. Paulo alisema alitaka apelekwe wapi?
  4. Ni katika imani gani Paulo na Wayahudi wote walikubaliana?
  5. Paulo alisema ni nani aliyemsikia hata akaongoka ?
  6. Ni kazi gani ambayo Bwana Yesu Kristo alikuwa amempatia kutenda.
  7. Festo alisema nini Paulo alipomaliza kuzungumza?
  8. Agrippa alisema nini wakati Paulo aliposema: Ninaamini unawaamini manabii?
  9. Mkutano ulipokwisha Agrippa almwambia nini Festo?
  10. Ni mfano wa nani ambao Paulo alikuwa akimfuata?
  11. Ni mfano gani nani ambaloPaulo anatuambia tufuate?

 

Majibu ya Kina

  1. Paulo alikuwa amekata rufani kwa Kaisaria. Nitatizo gani ambalo lilisababisha Festo ashindwe kuamua?
  2. Ni mambo gani manne aliyosema Paulo kuwa yalifundishwa na manabii na Musa kuhusu Masihi? (yaani

      Kristo)?

  1. Paulo alipomaliza hotuba yake, alimgeukia Agrippa?
    1. Alimwambia nini?
    2. Agripa alijibu nini?
    3. Agripa alisema nini kumhusu Paulo baadaye?

 

 

 

Swahili Title
122 PAULO ANAILINDA KWELI MBELE YA AGRIPA
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type