CSSA 1-5-23 - SHIPWRECK ON THE WAY TO ROME

Swahili

123. KUHARIBIKA KWA MELI IKIWAINAKWENDA RUMI

“Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari”

 

Shabaha

Kuonyesha jinsi Mungu alivyomleta Paulo hadi Rumi na kamwe hakumwacha, ingawaje alikabiliwa na hatari nyingi. Paulo alikuwa gerezani kwa zaidi ya miaka miwili ingawaje alikuwa hana hatia kwa kosa lolote.Lakini hata hivyo alikata rufaa kwa Kaisari. Na kwa sababu hiyo Festo asingeweza kumwachia huru. Alitakiwa kumpeleka mtume huyo hadi Rumi. Bwana Yesu alikuwa amemwambia kuwa: “Mimi nitakutuma uende mbali kwa watu wa Mataifa” (Matendo ya Mitume 22-21), naye Paulo alikuwa amefanya safari ndefu katika nchi kavu na baharini, walakini, safari ya hatari kupita zote sasa ilikuwa mbele yake, na katikati ya hatari kuu Mungu, kwa kumtuma malaika wake, alimtia moyo mtume kwa mara nyingine tena.

 

Matendo ya Mitume 27: 1 – 38

 

SAFARI NDEFU INAANZA (mstari 1 - 12)

Paulo alichukuliwa pamoja na wafungwa wengine kwa meli iliyoelekea Italia. Rafiki zake, Luka na Aristarko walikuwa pamoja naye. Akida aliyeitwa Juliasi alikuwa amepewa jukumu la kumlinda Paulo, na ilimbidi amlinde mtume na ayalinde maisha yake mwenyewe. Juliasi alikuwa amepewa taarifa nzuri kuhusu taarifa ya Paulo kutoka kwa Festo yule mtawala wa Rumi, na bila shaka Paulo alikuwa ameonyesha dhamira yake kwamba ni ilimpasa kwenda Rumi kwa sababu alitaka kuihubiri Injili kule. Walipowasili Sidoni, mapema katika safari, kwa wema sana alimruhusu Paulo kushuka bandarini na kuwatembelea rafiki zake heshima ambayo hawakupewa wafungwa wengine. Walipofika Mira iliwapasa kubadilisha meli. Meli yao mpya ilikuwa ikibeba shehena ya ngano ikitokea Iskanderia (huko Misri) kuelekea Rumi, na walikuwemo watu 276 melini, kwa kuwahesabu mabaharia na abiria. Safari ilikuwa ya mwendo wa pole pole na ngumu. Walipoondoka Mira, walitaka kusafiri kuelekea Magharibi hadi Nido ambayo ilikuwa na Bandari Nzuri kwa kujilinda. (Fuatilia safari hii kwenye ramani). Lakini upepo ulivuma kwa nguvu sana dhidi yao, hata ikawaa kwamba walilazimika kuelekea Kusini mpaka kwenye Kisiwa cha Krete. Hatimaye walifika mbingu salama , bandari iliyo upande wa kusini wa Krete. Kipupwe kilikuwa kikielekea kwenye majira ya baridi kali, naye Paulo alimwonya nahodha kwamba dhoroba itawakuta baharini na ingekuwa hatari kuendelea na safari. Lakini nahodha hakuithamini sana mbingu salama, naye akafiri ingalikuwa vyema kwenda kwenye bandari bora zaidi umbali wa kama kilometa 65, mbele zaidi na kutia nanga pale wajihifadhi huko hadi majira ya baridi yaishe. Askari mlinzi alikubaliana na ushauri wa nahodha na kwa hiyo wakang'oa nanga na kuanza safari.

 

HATARI BAHARINI (mstari 13 - 20)

“Upepo mwanana unaovuma kutoka kusini” ulivuma mara tu walipoondoka (mstari 13), lakini haikuwa muda mrefu, ghafla upepo mkali uvumao kutoka kaskazini – mashariki ukawapiga, ambapo uliisukuma meli nje ya njia yake. Dhoruba kali ilisababisha mawimbi yenye nguvu ambayo yaliipiga meli, hata ikawa kwamba mabaharia walilazimika kutumia ujuzi wao wote kusaidia kuiweka meli katika usalama. Ilikuwa imebamizwa kwa nguvu mno na dhoruba ile, kiasi kwamba waliamua kupunguza shehena na kufunga kamba chini ya merikebu kuizunguka ili mbao zisivunjike. Hatari iliyofuata ni kwamba wangepelekwa kwenye mchanga sehemu ya pwani upande wa kaskazini ya Afrika. Mawingi mazito na mengi yaliwazuia kuona nyota wakati wa usiku na hata hawakuweza kuona jua wakati wa mchana, ambazo mahabaria walizitumia kuwaongoza ni wapi walikuwa wakielekea. Kwa hiyo hawakuelewa hata ni upande gani walikuwa wakielekea wakati wakisafiri. Siku iliyofuata wakatupa mizigo mizito zaidi kuiwezesha meli kuweza kuelea zaidi juu ya maji.

 

“WANAUME CHANGAMKENI” (mstari 21 -24)

 Ndani ya meli, abiria na watumishi wa meli walikuwa na huzuni sana. Walikuwa wamepoteza tumaini la kuweza kuokoka. Ni hapo ndipo Paulo aliposimama katikati yao na kusema. Alisema walipaswa kumsikiliza alipowaonya na kungoja katika bandari salama, lakini sana “wachangamke” kwa kuwa kila mmoja ataokoka. “Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu, amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe” (mstari 23 – 24). Kwa hakika watu hawa bila shaka walimfikiria kuwa huyu mtume Paulo ni mtu wa waajabu. Wakati huo hawakufahamu kuwa kupitia kwa mtu huyu wangeokoka kutokana na tatizo lililokuwepo. Kama tu wangesikiliza Injili aliyoihubiri, pia wangeweza kuokoka milele.

 

MELI INAPOTEA (mstari 25 – 44)

Paulo aliendelea kusema “kwa sababu namwamini Mungu ya kwamba yatakua vile vile kama nilivyoambiwa” (mstari 25). Mungu, ajuaye mambo yote, alikuwa amemwambia Paulo kuwa meli ingepotea, lakini kwamba wote waliomo melini wangetupwa kwenye kisiwa. Siku kumi na nne zilipita. Ilikuwa yapata kama usiku wa manane siku ile ya kumi na nne, mabaharia wa zamu wakatambua kwamba wanapwelea karibu na nchi kavu. Wakafurahia (yaani walipo pima kina cha maji) na kutambua kuwa bahari sasa ilizidi kuwa na kina kifupi. Kwa vile ilikuwa usiku bado, waliamua kutupa nanga mpaka asubuhi. Wakati wakingojea mabaharia walijaribu kuondoka. Paulo aling’amua walichokuwa wanataka kutenda, naye akasema wanaweza kupona ikiwa tu kila mmoja atabaki ndani ya merikebu; au vingenevyo wangekufa. Askari waliheshimu maneno ya Paulo nao wakabaki ndani. Wakiwa katika dukuduku la kumgojea asubuhi ifike, Paulo akawashauri wote wapate chakula. Walikuwa hawajala chakula chochote kwa siku kumi na nne nao walihitaji nguvu kwa ajili ya yale ambayo yangewakabili mbele. Wakati chakula kilipotayarishwa Paulo akamshukuru Mungu nao wote wakala kwa furaha, huku wakiwa wametiwa moyo na maneno ya Paulo: “kwa maana hapana hata unywele wa kichwa cha mmoja wenu utakaopotea” (mstari 34). Na ndipo walipoipunguza mizigo ili meli iwe nyepesi kwa kumwaga ngano baharini. Kulipopambazuka waliweza kuiona pwani ya kisiwa wakaamua kung'oa nanga wakitumaini kuileta mashua ukingoni. Lakini omo ikakwama ikakaa isitikisike, lakini tezi ilikuwa imefumuliwa kwa nguvu za mawimbi. Askari wa Warumi walitaka kuwaua wafungwa wote ikiwa yeyote angetoroka, lakini kwa sababu Juliasi alitaka kumwokoa Paulo, akawazuia wasitenda kama walivyokusudia. Akawaamrisha wote walioweza kuongelea kujitupa baharini na waogelea mpaka wafike nchi kavu. Wale wasioweza kuogelea walitumia mbao na vitu vingine vya merikebu iliyovunjika ili waweze kufika nchi kavu. Hivyo jumla ya abiria wote walikuwa abiria 270 wakafika ufukweni kama Paulo alivyosema na Mungu alivyokuwa ameahidi.

 

FUNDISHO KWETU

Paulo alionyesha imani kubwa akiwa uso kwa uso na hatari. Alijua kwamba Neno la Mungu ni la hakika na angefika Rumi bila shaka. Ilikuwa ni safari ya kutisha kwa wote walikuwa melini, lakini kwa sababu Paulo alimwamini Mungu, aliweza kuwaimarisha kwa kuwatia moyo wasafiri wengine waliokuwa wamekwisha kukata tamaa ya kuishi. Mungu hakuwamwacha Paulo, kama alivyoandika baadaye katika waraka wake kwa Waebrani. “Kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa” (Waebrania 13:5). Ni jinsi gani alivyo mfano mzuri wa ajabu wa utulivu na imani akiwa uso kwa uso na dhoruba na kuvunjika kwa meli. Tunaweza kupata nguvu na ujasiri kutokana na habari hii ya kweli, wakati wote matatizo yanapotokea.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

  1. Ni nani aliyeruhusiwa kufuatana na Paulo melini hadi Rumi?
  2. Walipofika bandari salama Paulo alishauri nini?
  3. Hali ya hewa ilikuwaje walipoondoka bandari salama?
  4. Ni aina gani ya upepo uliovuma muda mfupi tu baada ya kuondoka?
  5. Mabaharia walifanya nini ili kujaribu kuiokoa merikebu?
  6. Ni aina gani ya hatari nyingine ambayo wangekabiliana nayo?
  7. Kwa nini ilikuwa ni vigumu kwa mabaharia kujua ni upande upii walikuwa wakielekea?
  8. Ni nani aliyesema na Paulo ili kumtia moyo?
  9. Paulo alisema nini kingetokea kwa watu wale waliokuwa melini?
  10. Ni wakati gani tena waliona nchi kavu?
  11. Mabaharia walijaribu kufanya nini ili kuokoa uhai wao?
  12. Paulo alisema nini?
  13. Askari walitaka wawatendeje wafungwa wakati meli ilipokwama?
  14. Ni jinsi gani kila mmoja alifika nchi kavu?

 

Majibu ya Kina

  1. Eleza yote unayoyafahamu:
    1. Kuhusu dhoruba, baada ya merikebu kuondoka bandari salama
    2. Ni jinsi gani Paulo alivyomtia moyo kila mmoja aliyekuwa melini (mstari13 -26)
  2. Usiku wa kumi na nne wa dhoruba ya tufani mabaharia walijua kuwa walikuwa wakikaribia nchi kavu. Eleza

      ni nini kilitokea baada ya hapo. 

 

 

Swahili Title
123 KUHARIBIKA KWA MELI IKIWAINAKWENDA RUMI
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type