CSSA 1-5-24 - PAUL ON MELITA

Swahili

124. PAULO HUKO MELITA

“Watashika nyoka... wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.”

 

Shabaha

 Kuonyesha kwamba Paulo kamwe hakusahau kuwa Mungu alikuwa pamoja naye katika majaribu yake yote. Kundi lote la watu melini lilikuwa katika hatari ya kuzama ndani ya bahari, iliyochafuka na dhoruba, lakini sasa wote walisimama wakitetemeka ila wakiwa salama kwenye nchi kavu. Ni watu wachache tu kati yao walioweza kumshukuru Mungu aliyeumba mbingu na nchi, bahari na nchi kavu, kwa kuwaokoa kutokana na tukio la kutisha.

 

Matendo ya Matendo 28: 1- 15

 

PAULO ANAUMWA NA NYOKA (mstari 1 – 7)

Kisiwa cha Melita kilikuwa chini ya dola ya Rumi nacho kilikuwa kinatawaliwa na mtu aliyeitwa Publio. Wakati meli ilipovunjika abiria waliokoka na wakafika nchi kavu, wenyeji wa nchi kavu watu wake walikuwa wema sana kwao na waliwasaidia kukoka moto ili waweze kupata joto. Paulo alipokuwa akikusanya kuni kifutu mwenye sumu alijiviringisha mkononi mwake, lakini akamkungutia motoni. Wenyeji walikuwa washirikina sana, nao walidhania Paulo kuwa ni alikuwa mwuaji ambaye ingawa alikuwa ameokoka kuzama baharini, lakini ilikuwa lazima aadhibiwe. Kwa hiyo wakamwangalia kwa makini, walitazamia kuwa sehemu ya mwili iliyoumwa itavimba na halafu ataanguka chini na kufa. Kwa mshangao wao mkubwa Paulo hakupatwa na madhara yoyote kabisa. Ahadi ambayo Yesu alikuwa ameiahidi katika Marko 16:18 ya kwamba wanafunzi wake wangeshika nyoka bila madhara ilitimia hapa na uhai wa Paulo ulibakia salama. Watu wa kisiwa kile, hata hivyo, sasa wakabadili mawazo yao na kuamua kwamba Paulo yamkini ni mungu.

 

PAULO ANAMPONYA MGONJWA (mstari 8 – 10)

Mtawala wa kisiwa hicho, Publio, aliyewahurumia watu waliookoka kutoka katika merikebu, alikuwa mkarimu kiasi cha kumkaribisha Paulo na wenzeke nyumbani kwake ambako waliwahudumia kwa siku tatu. Baba yake Publio alikuwa mgonjwa sana kwa ugonjwa wa homa kali. Paulo akaja kumtazama, akamwombea na kuweka mikono yake juu yake, na kwa nguvu za Roho Mtakatifu aliweza kumponya. Hivyo Publo akapata thawabu kwa ajili ya wema wake. Habari za uponyaji huu wa kushangaza zilienea katika kisiwa chote, na wengine wenye kuugua magonjwa walikuja nao wakaponywa na Mtume. Matokeo ni kwamba Paulo na wote walikuwa pamoja naye wakaheshimiwa sana.

 

PAULO ANAONDOKA NA KWENDA RUMI (mstari 11 – 15)

Mwisho wa majira ya baridi, baada ya miezi mitatu Paulo na wenzake walipanda meli tena kuelekea Rumi. Wenyeji wa kisiwa hicho, wakiwa wenye shukrani kwa ajili ya yote ambayo Paulo alikuwa amewafanyia, waliwapatia kila kitu ambacho wangehitaji kwa sababu walikuwa wamepoteza kila kitu wakati meli ilipoharibika. Meli nyingine ya Iskanderia ilikuwa imetia nanga kutokana na hali mbaya ya hewa hapo kisiwani Melita. Waliweza kupanda meli na kuendelea na safari yao kwenda Rumi. Walipumzika kwa muda pale Sirakusa Regio na Puteoli ambayo ni bandari wangesafiri kwenda nchi kavu kuelekea Rumi. (Angalia sehemu hizi zote katika ramani zako). Jinsi ilivyokuwa furaha kwa Paulo na ndugu waliokuwa pamoja naye kupokelewa na kupewa mahitaji muhimu na ndugu wa Puteoli. Walikaa kwa siku saba na tunaweza kutafakari jinsi walivyozungumza kuhusu Kweli mmoja baada mwingine na hata kuhusiana na njia ya ajabu ambayo Mungu aliwatunza katika safari yao. Jinsi Paulo angalivyotiwa moyo na kuimarishwa. Wakati ndugu wa Rumi waliposikia habari ya furaha kwamba Paulo alikuwa anakuja, walikwenda kumlaki njiani. Walisafiri mpaka wakafika Soko la Apio na mikahawa mitatu umbali upatao kilometa 80, ili kumsalimia. Paulo alipokutana nao, “alimshukuru Mungu na kuchangamka” (mstari 15), na kwa hiyo wakasafiri pamoja naye mpaka Rumi.

 

FUNDISHO KWETU

Wakati Pailo, mfungwa aliposafiri kwenda Rumi hakufahmu mwisho wa safari yake ungekuwa wa namna gani. Lakini kwa vile alijua kuwa Mungu ndiye aliyetaka aende Rumi ili kuhubiri kule (Matendo ya Mitume 23:11), alielekeza uso wake kwa ujasiri upande huo. Kama vile Paulo, sisi pia inatupasa kwa ujasiri kutenda mapenzi ya Mungu na siyo kutafuta sababu zetu wenyewe wakati matatizo yanapotokea. Kama vile Paulo alivyotiwa nguvu na kuhamasishwa na ndugu waliokwenda kukutana naye na kuungana pamoja naye katika safari ya kwenda Rumi, ndivyo inavyotupasa kujifunza kuwafariji na kumsaidia kila mmoja katika kazi yake Mungu.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

  1. Jina la kisiwa ambapo Paulo na wafungwa wengine waliharibikiwa na meli ni?
  2. Ni jambo gani la kushangaza lilimpata Paulo wakati watu wa Melita walipokuwa wanaona?
  3. Publo alikuwa ni nani?
  4. Paulo alitendea nini Publo?
  5. Ni kwa muda gani wasafiri walipoharibikiwa na meli walikaa pale kisiwani?
  6. Ni kwa muda gani walikaa na ndugu kule Puteoli
  7. Ni nani waliokuja kukutana Paulo njiani kwenda Rumi?
  8. Paulo alijisikiaje alipokutana na ndugu hawa waliotoka Rumi?

 

Majibu ya Kina

  1. Paulo alikuwa njia kwenda Rumi wakati tufani iliposababisha meli ipotee. Eleza yaliyotokea wakati Paulo

      alipokaa katika kisiwa cha Melita.

  1. Eleza yote unayoyafahamu kuhusu hatua ya mwisho ya safari ya Paulo kuelekea Rumi, yaani tangu muda

walipoondoka Melita.

 

 

 

Swahili Title
124 PAULO HUKO MELITA
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type